HaMachiach
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 3,445
- 6,207
- Thread starter
- #221
SIRI
Episode 21
Mtunzi. Patrick CK
TANZANIA
Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania
alilazimika kukatisha ratiba ya
shughuli zake zote jijini Dar es
salaam baada ya kupata taarifa
za mlipuko uliotokea jijini
Dodoma na kumuua waziri
mkuu.Muda mfupi kabla ya
kupokea taarifa ile ya kuuawa
kwa waziri mkuu,rais alipokea
taarifa kutoka kwa mkuu wa
jeshi la polisi nchini akimjulisha
kuhusu mauaji ya mkubwa
Donald Nkebo aliyekutwa
ameuawa kwa kupigwa risasi
katika nyumba moja yeye
pamoja na watu wengine
watano.Taarifa ya kuuawa
Donald Nkebo ilimstua mno rais
kwani ni mtu aliyekuwa
anamtegemea sana katika
kufanikisha mipango ya
kuwamaliza wapinzani wake
kisiasa.Rais alimuagiza mkuu
wa jeshi la polisi nchini
kuhakikisha kwamba analiagiza
jeshi lake kufanya kila
linalowezekana kuwapata watu
waliofanya mauaji yale ya
Donald Nkebo na vijana wake.Akiwa bado katika
mstuko mkubwa wa kuuawa
Donald Nkebo rais alizidi
kutikiswa baada ya kupewa
taarifa ya waziri mkuu kuuawa
katika mlipuko.Ilikuwa ni
taarifa mbaya sana kuipokea
kwa siku ile.Mara tu baada ya
kupata taarifa zile alilazimika
kuitisha kwa haraka kikao cha
baraza kuu la usalama la
taifa.Kikao kile kiliwajumuisha
yeye rais,makamu wa rais,rais
wa Zanzibar ambaye alifika kwa
haraka baada ya kupewa mwito
wa kuwepo kwa kikao kile,alikuwepo pia makamu wa
rais wa Zanzibar vile vile
walikuwepo wakuu wote wa
vyombo vya ulinzi na usalama
wa nchi.
“Ndugu zangu
ninawashukuru sana kwa
kufika kwenu kwa haraka mara
tu baada ya kupokea
mwito.Kabla ya yote ninapenda
tusimame kwa dakika moja
tuwakumbuke wenzetu
waliopoteza maisha katika
mashambulio yaliyotokea leo
jijini Dodoma na katika mauaji
mengine yaliyotokea hapa Dar es salaam” akasema Dr Evans
kisha wote wakasimama
kuwaombea marehemu wote
waliofariki katika mashambulio
yale mawili.
“Ndugu viongozi wenzangu
sijui nianzie wapi,lakini naomba
nikiri kwamba nimetikiswa”
akasema rais na kunayamza
kidogo
“Nilipigiwa simu na mkuu
wa jeshi la polisi alfajiri ya leo
akanipa taarifa kwamba mmoja
wa wafanya biashara wakubwa
hapa nchini Donald Nkebo
amekutwa katika nyumba Fulani ameuawa pamoja na
watu wengine watano.Donald ni
mtu anayefahamika sana hapa
nchini ni mmoja wa wawekezaji
wakubwa ana viwanda vyake
kadhaa na biashara nyingine
kubwa kubwa na vile vile ni
mmoja kati ya wafadhili
wakubwa wa chama
chetu.Binafsi ni mtu ambaye
ninamfahamu na kumheshimu
sana hasa kutokana na mchango
wake mkubwa katika uchumi
wetu.Mazingira ya kifo chake
yalinistua sana na nikampa
maelekezo mkuu wa jeshi la polisi kuhakikisha watu
waliofanya mauaji hayo
wanapatikana.Mpaka sasa kuna
chochote ambacho
kimepatikana kuhusiana na
mauaji hayo?akauliza Dr Evans.
“Mkuu,mara tu baada ya
jeshi la polisi kupata taarifa za
mauaji yale na kuyathibitisha
nilikutaarifu na ukanipa
maelekezo,tayari tumekwisha
fungua jalada la uchunguzi na
vijana wako kazini wakiendelea
na kazi.Mimi mwenyewe baada
ya kupokea taarifa hiyo
niliondoka na kwenda eneo la tukio kuthibitisha kwani Donald
ni mtu niliyekuwa
nikifahamiana naye sana
tulikutana tukiwa chuo kikuu
cha Dar es salaam na toka hapo
tumeendelea kuwa marafiki
wakubwa.Mheshimiwa rais
tunaendelea kuchunguza
nyumba ile yalimofanyika
mauaji kujua shughuli gani
zilizokuwa zinaendelea kwani
kumekutwa vifaa mbali mbali
vya mawasiliano na inaonekana
kulikuwa na kompyuta kadhaa
lakini zote
zimeondolewa.Inaonekana baada ya kutekeleza mauaji yale
wauaji waliondoka na
kompyuta zote zipatazo
kumi.Tunahisi kuna kitu katika
hizo kompyuta ndiyo maana
zikachukuliwa na wauaji.Vile
vile wauaji walichukua simu
zote za watu waliowaua.Donald
amekutwa akiwa ameuawa
ndani ya gari akiwa amevaa
mavazi ya kulalia,inaonekana
aliondoka nyumbani kwake na
kwenda katika nyumba ile usiku
hivyo tunataka kujua
mahusiano yake na wale watu
waliouawa.Mheshimiwa rais timu maalum kutoka makao
makuu iko kazini hivi sasa na
nitakutaarifu kila pale
nitakapopata taarifa yoyote
kutoka kwao” akasema inspekta
jenerali wa polisi
“Kabla taarifa hiyo
niliyopokea kutoka kwa IGP
haijapoa nikapokea tena taarifa
nyingine ya kifo cha waziri
mkuu..” akasema Dr Evans na
kuinamisha kichwa
“I’m sorry,kifo cha waziri
mkuu kimeniumiza mno”
akasema Dr Evans naukimya
ukatawala ndani ya chumba kile.Kila mmoja alikuwa na uso
wenye simanzi.
“Wakuu wote wa vyombo
vya usalama mko hapa nataka
kujua nini kimetokea Dodoma
hadi bomu likategwa katika
ofisi ya waziri mkuu na
kumuua.Mmekwisha wajua
watu waliofanya tukio hilo ni
akina nani?akauliza Dr Evans na
kuwatazama wakuu wale wa
vyombo vya usalama
“Inspekta jenerali tuanze na
wewe.Jeshi la polisi ndio
wanaolinda ofisi zote kuu za
serikali.Imewezekanaje watu wakaingia na kutega bomu
wakati jengo lile lina ulinzi saa
ishirini na nne bila polisi
kugundua?Askari wako
walikuwa wapi?akauliza Dr
Evans kwa sauti kali kidogo
“Mheshimiwa rais ni kweli
jengo la ofisi ya waziri mkuu
linalindwa na askari polisi kwa
saa ishirini na nne na
kilichotokea kimetustua hata
sisi ngazi za juu na tumejiuliza
swali hilo hilo imewezekanaje
hawa watu wakapenya na
kutega mabomu katika geti la
ofisi ya waziri mkuu ambako kuna ulinzi wa saa ishirini na
nne?Askari wetu walikuwa
wapi? Mheshimiwa rais ni
mapema sana kupata majibu ya
maswali haya kwani uchunguzi
ndiyo kwanza umeanza,tayari
timu maalum ya makachero
mahiri kabisa ndani ya jeshi la
polisi wamekwisha tua jijini
Dodoma na tayari wameanza
uchunguzi kuhusiana na tukio
hili na mimi mwenyewe baada
ya kumalizika kwa kikao hiki
ninakwenda Dodoma kujua nini
hasa kilichotokea na
nitahakikisha ndani ya muda mfupi tunapata majibu”
akasema Inspekta jenerali wa
polisi.Ukimya ukapita tena
halafu Dr Evans akasema
“Idara ya kupambana na
ugaidi ni kazi yenu kudhibiti
matukio kama haya ya
ugaidi,mlikuwa wapi na kuacha
shambulio hili likatokea?
Shambulio kama hili si la
kupangwa kwa siku
moja,lazima limechukua muda
kuandaliwa.Ninyi kama idara
yenye jukumu la kuzuia mambo
kama haya yasitokee hamkuwa
na viashiria vyovyote vilivyowaonyesha kwamba
shambulio kama hili linaweza
kutokea?Mmeshindwaje
kubaini jambo kama hili
kutokea hasa katika sehemu
nyeti kama ofisi ya waziri
mkuu?akauliza Dr Evans kwa
ukali
“Mheshimiwa rais”
akasema Genevieve Nelson
mkuu wa idara ya kupambana
na ugaidi.
“Idara yangu haikuwa na
taarifa zozote za kuweza
kutokea kwa shambulio
lile.Tayari idara yangu imekwisha ingia kazini
kuwatafuta wale wote
waliofanya tukio hili
tukishirikiana na vyombo
vingine.Timu ya watu nane
tayari wamekwisha wasili jijini
Dodoma.Nina uhakika mkubwa
kwamba hadi kufika mchana wa
leo tutakuwa tumepata jibu zuri
la nani waliofanya shambulio
hilo”akasema Genevieve
“Kwa idara hii muhimu
sana kushindwa kubaini
kuwepo kwa shambulio hili ni
udhaifu mkubwa sana.Najiuliza
kama leo wameweza kutega bomu katika ofisi ya waziri
mkuu bila chombo chochote
kung’amua je watashindwa
kuingia na kutega bomu
ikulu?Kuna umuhimu gani wa
kuwa na idara ya kudhibiti
ugaidi ikiwa magaidi wanawza
kupenya hata katika ofisi nyeti
za serikali na kufanya
mashambulio?akauliza Dr
Evans kwa ukali akiwatazama
wakuu wale wa vyombo vya
usalama
“CDF kuna nini upande
wako? Akauliza Dr Evans
“Baada ya kupata taarifa za
tukio hilo nimeelekeza timu ya
wataalamu wa mabomu ifike
haraka sana eneo la tukio na
tayari wako eneo la tukio
wakisaidiana na wataalamu
kutoka jeshi la polisi kukusanya
kila kitu kwa ajili ya uchunguzi
kubaini ni bomu la aina gani
lililotumika na limetengenezwa
wapi.” akasema mkuu wa
majeshi.Ilimchukua Dr Evans
dakika chache za kutafakari
kisha akasema
“7 Agosti 1998 tulionja
adha ya mashambulio ya kigaidi baada ya ubalozi wa marekani
hapa nchini kulipuliwa.Watu 11
walipoteza maisha na wengine
85 walijeruhiwa.Leo kwa mara
ya pili tena magaidi
wanatushambulia na safari hii
wakimlenga kiongozi mkubwa
kabisa wa serikali ambaye ni
waziri mkuu wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania.Hili ni
jambo lisilokubalika na
linaumiza sana.Damu ya watu
hawa imepotea bila hatia
yoyote.Nataka vyombo vyote
vya ulinzi na usalama nchi hii
mshirikiane na muhakikishe kwamba watu hawa waliofanya
unyama wa namna hii
wanapatikana haraka sana na
watueleze nini sababu ya
kufanya hivi.Wametuchokoza
na hatuwezi kukaa
kimya.Yeyote aliyetuchokoza
lazima apate majibu yake.Awe
ni mtu,kikundi cha watu au taifa
lazima ajulikane na apate stahili
yake kwa unyama huu
waliotufanyia.Nataka tutume
ujumbe kwa dunia kwamba
Tanzania si sehemu salama kwa
magaidi na wale wote wenye
kufikiria kufanya mashambulio katika ardhi yetu wasithubutu
kufanya hivyo tena.Kwa kuwa
bado ni mapema sana na hatuna
taarifa zozote za nani
wamefanya shambuliohili
nataka tukutane tena hapa saa
kumi na moja jioni na mpaka
wakati huo kila mmoja aje hapa
akiwa na taarifa idara yake
imefikia wapi katika
kuwatambua magaidi
waliofanya unyama huu kwenye
ardhi yetu” akasema Dr Evans
na wajumbe wa kikao kile
wakatawanyika na kuwaacha
Dr Evans,makamu wa rais na rais wa Zanzibar katika
mazungumzo mazito
MAZISHI YA KITAIFA - BAADA
YA SIKU 3
Uwanja wa Uhuru jijini Dar
es salaam ulifurika pomoni
katika mazishi ya kitaifa ya
waziri mkuu wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania
aliyefariki katika mlipuko wa
bomu jijini Dodoma.Viongozi
kutoka nchi mbali mbali za
Afrika waliwasili kuhudhuria
mazishi yale ya kitaifa.Rais wa jamhuri ya muunganoi wa
Tanzania Dr Evans akiwa na
mke wake waliwasili katika
uwanja wa taifa tayari
kuwaongoza watanzania katika
shughuli ile.Dakika chache
baada ya rais kuwasili,mwili wa
waziri mkuu ukaingizwa
uwanjani kwa ajili ya kuagwa.
Viongozi wa dini
walifungua shughuli ile kwa
kusoma dua kisha zikafuata
salamu kutoka kwa wakuu
mbali mbali wa nchi
waliohudhuria mazishi yale na
hatimaye ukafika wakati ambao rais wa jamhuri ya muungano
wa Tanzania akapewa nafasi ya
kuhutubia hadhira ile kubwa ya
watanzania waliofika kumuaga
waziri mkuu.
“Ndugu watanzania na
wageni wetu mliotoka katika
mataifa jirani kuja kuungana
nasi katika mazishi haya ya
kitaifa,awali ya yote napenda
kumshukuru mwenyezi Mungu
mwingi wa rehema
kutukutanisha hapa sote siku ya
leo katika shughuli hii ya
kumuaga mpendwa wetu
mheshimiwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania” Dr Evansa
akanyamaza kidogo halafu
akaendelea
“Dakika thelathini kabla ya
uhai wake kukatishwa
kikatili,nilizungumza naye na
nikampa maelekezo katika
mambo kadhaa na nilimuahidi
kwamba mwisho wa wiki
tungekutana jijini Dodoma.Nusu
saa baada ya kuzungumza naye
nilipewa taarifa za kifo
chake,nilipatwa na mstuko
ambao siwezi kuuelezea.Kifo
hiki kimenigusa sana mimi binafsi,watanzania wote kwa
ujumla na wapenda amani kote
duniani.Nimepokea salamu za
rambi rambi kutoka kwa
mataifa mengi duniani wote
wakiguswa na msiba huu
mkubwa,nawashukuru sana
nyote mliotufariji katika wakati
huu mgumu” rais akanyamaza
tena kidogo na kuendelea
“Hakuna maneno mazuri ya
kumuelezea mpendwa wetu
huyu kwani hakuna
asiyefahamu utendaji wake wa
kazi.Binafsi amekuwa msaada
mkubwa sana kwangu na
serikali
ninayoiongoza.Amekuwa
msimamizi mzuri wa shughuli
zote za serikali kwa umakini na
weledi mkubwa sana.Muda
hautoshi kumuelezea mpendwa
wetu huyu itoshe tu kusema
kwamba utendaji wake wa kazi
ulitukuka na tumempoteza mtu
muhimu mno.
Kutokana na utendaji kazi
wake uliotukuka na uadilifu
usio na kifani,alitengeneza
maadui wengi wa ndani na nje
ya nchi hasa wafujaji wa fedha
za serikali,mafisadi na wahujumu uchumi.Hakusita
kukemea ubadhirifu na
kuchukua hatua stahiki kila pale
alipoubaini.Maadui hawa
aliowatengeneza hawakuona
namna nyingine ya kupambana
naye zaidi ya kuitoa roho
yake.Walichokifanya ni unyama
uliopitiliza na
haukubaliki.Ninatuma salamu
kwa wale wote waliofanya
kitendo hiki,awe ni mtu,kikundi
cha watu wa ndani au nje ya
nchi siku zenu
zinahesabika.Mmetuchokoza na
sasa ni wakati wetu wa kujibu mapigo na majibu yetu
hayatakuwa
madogo.Tutawasaka magaidi
hawa kila sehemu,iwe
ardhini,majini au hata
angani,hawana sehemu ya
kujificha.Hakuna jiwe libaki juu
ya lingine wote walioshiriki
uovu huu watapata stahili yao”
akasema Dr Evans kwa
msisitizo mkubwa
Wakati mazishi ya kitaifa
yakiendelea katika uwanja wa
uhuru jijini Dar es salaam,katika
uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere ndege ya shirika la ndege la Ethiopia ikitokea Tel
Aviv kupitia Addis Ababa ilitua
na abiria kuanza kushuka.Ndani
ya ndege hii walishuka majasusi
watano kutoka shirika la ujasusi
la Israel Mossad.Majasusi hawa
walikuja nchini kwa ajili ya
kutekeleza operesheni maalum
ya kumteka Edger kaka.Tayari
walikwishapata taarifa kwamba
Edger kaka alikuwa na mipango
ya kurejea nchini siku ya
mazishi ya waziri mkuu ili
aweze kuwahi mazishi hayo
kwani waziri mkuu alikuwa ni
mmoja wa watu aliowaheshimu sana.Waliwahi kufika nchini
kabla ya ndege aliyopanda
Edger Kaka na Olivia ambayo
ililazimika kuchelewa kuondoka
nchini Israel kwa sababu za
kiufundi.Ukweli ni kwamba
hakukuwa na hitilafu yoyote
katika ndege hiyo bali ulikuwa
ni mpango maalum wa Mossad
ili Edger achelewe kufika nchini
Tanzania na kufika Dar es
salaam usiku ili mpango wa
kumteka uweze kutekelezwa
kama ulivyopangwa.
Majasusi wale baada ya
kukamilisha taratibu za
uhamiaji na kuruhusiwa kuingia
nchini kila mmoja alipokelewa
na mtu maalum kutoka ubalozi
na kumpeleka katika nyumba
anakoishi afisa mmoja wa
ubalozi ambako ndiko mipango
yote ya operesheni ile ilikuwa
inafanyika.Siku mbili zilizopita
majasusi wengine watatu
waliwasili nchini kimya kimya
kwa ajili ya kuandaa operesheni
hiyo ya siri wakisaidiwa na
maafisa wa ubalozi wa Israel
nchini Tanzania.
Baada ya kuhakikisha kila
mmoja wao ameingia nchini salama na hakukuwa na tatizo
lolote bila kupoteza muda kikao
kikaanza
“Poleni kwa safari na
karibuni Tanzania” akasema
Gershom Rabin mkuu wa
operesheni ile.
“Kwa siku tatu tulizokaa
hapa tumekuwa na kazi kubwa
ya kuhakikisha tunaandaa
operesheni kubwa ya aina yake
ambayo itatuwezesha kumpata
Edger kaka na kuiacha serikali
ya Tanzania ikiamini kwamba
Edger kaka amefariki katika
ajali ya gari.Mpaka sasa mipango yote inakwenda
vyema.Nimekuwa na
mawasiliano na mawasiliano na
watu wetu Noam na Yosef
ambao wako ndani ya ndege
aliyopanda Edger na
wamenihakikishia kwamba
Edger bado yuko ndegeni
nimewasiliana pia na marubani
wa ndege hiyo
wamenihakikishia kwamba
ndege itaingia Dar es salaam saa
sita za usiku leo hivyo
operesheni yetu bado
inaendelea vizuri kama tulivyoipanga” akasema
Gershom
“Hapa mbele yetu kuna
ramani” akasema Gershon na
kuisogelea ramani ile.
“Hii ni barabara ambayo
inatoka uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere kuja
mjini.Shughuli yetu itafanyikia
eneo hili hapa lenye mduara
mwekundu.Ni kilometa kadhaa
kutoka uwanja wa ndege na
tumechagua eneo hili kwa kuwa
hatutaki tukio lifanyike kati kati
ya jiji ambako kwa nyakati hizo
bado linaweza kuvuta watu.Ilan na Moshe mtakuwa katika
uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere kumsubiri Edger kisha
mtawapokea Noam na Yosef
halafu mtalifuata kwa nyuma
gari atakalopanda Edger huku
mkiendeleza kuwasiliana
nasi.Sina haja ya
kuwakumbusha nini mnapaswa
kufanya kila mmoja anafahamu
sehemu yake ni ipi na
tumekwisha fanya mazoezi ya
kutosha hivyo kilichobaki ni
utekelezaji tu.Kikubwa
ninachowasisitiza ni umakini
mkubwa sana kwani operesheni hii ni ya siri na serikali ya
Tanzania haifahamu
chochote.Kosa moja hata dogo
linaweza kutuletea matatizo
makubwa hivyo epukeni
kufanya kosa.Mwisho kabisa
kumbukeni kunaweza kutokea
mabadiliko katika operesheni
hii hivyo kila mmoja awe
makini katika kumlinda
mwenzake” akasema Gershom
kisha wakaendelea na
majadiliano kuhusiana na
operesheni ile.
Episode 21
Mtunzi. Patrick CK
TANZANIA
Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania
alilazimika kukatisha ratiba ya
shughuli zake zote jijini Dar es
salaam baada ya kupata taarifa
za mlipuko uliotokea jijini
Dodoma na kumuua waziri
mkuu.Muda mfupi kabla ya
kupokea taarifa ile ya kuuawa
kwa waziri mkuu,rais alipokea
taarifa kutoka kwa mkuu wa
jeshi la polisi nchini akimjulisha
kuhusu mauaji ya mkubwa
Donald Nkebo aliyekutwa
ameuawa kwa kupigwa risasi
katika nyumba moja yeye
pamoja na watu wengine
watano.Taarifa ya kuuawa
Donald Nkebo ilimstua mno rais
kwani ni mtu aliyekuwa
anamtegemea sana katika
kufanikisha mipango ya
kuwamaliza wapinzani wake
kisiasa.Rais alimuagiza mkuu
wa jeshi la polisi nchini
kuhakikisha kwamba analiagiza
jeshi lake kufanya kila
linalowezekana kuwapata watu
waliofanya mauaji yale ya
Donald Nkebo na vijana wake.Akiwa bado katika
mstuko mkubwa wa kuuawa
Donald Nkebo rais alizidi
kutikiswa baada ya kupewa
taarifa ya waziri mkuu kuuawa
katika mlipuko.Ilikuwa ni
taarifa mbaya sana kuipokea
kwa siku ile.Mara tu baada ya
kupata taarifa zile alilazimika
kuitisha kwa haraka kikao cha
baraza kuu la usalama la
taifa.Kikao kile kiliwajumuisha
yeye rais,makamu wa rais,rais
wa Zanzibar ambaye alifika kwa
haraka baada ya kupewa mwito
wa kuwepo kwa kikao kile,alikuwepo pia makamu wa
rais wa Zanzibar vile vile
walikuwepo wakuu wote wa
vyombo vya ulinzi na usalama
wa nchi.
“Ndugu zangu
ninawashukuru sana kwa
kufika kwenu kwa haraka mara
tu baada ya kupokea
mwito.Kabla ya yote ninapenda
tusimame kwa dakika moja
tuwakumbuke wenzetu
waliopoteza maisha katika
mashambulio yaliyotokea leo
jijini Dodoma na katika mauaji
mengine yaliyotokea hapa Dar es salaam” akasema Dr Evans
kisha wote wakasimama
kuwaombea marehemu wote
waliofariki katika mashambulio
yale mawili.
“Ndugu viongozi wenzangu
sijui nianzie wapi,lakini naomba
nikiri kwamba nimetikiswa”
akasema rais na kunayamza
kidogo
“Nilipigiwa simu na mkuu
wa jeshi la polisi alfajiri ya leo
akanipa taarifa kwamba mmoja
wa wafanya biashara wakubwa
hapa nchini Donald Nkebo
amekutwa katika nyumba Fulani ameuawa pamoja na
watu wengine watano.Donald ni
mtu anayefahamika sana hapa
nchini ni mmoja wa wawekezaji
wakubwa ana viwanda vyake
kadhaa na biashara nyingine
kubwa kubwa na vile vile ni
mmoja kati ya wafadhili
wakubwa wa chama
chetu.Binafsi ni mtu ambaye
ninamfahamu na kumheshimu
sana hasa kutokana na mchango
wake mkubwa katika uchumi
wetu.Mazingira ya kifo chake
yalinistua sana na nikampa
maelekezo mkuu wa jeshi la polisi kuhakikisha watu
waliofanya mauaji hayo
wanapatikana.Mpaka sasa kuna
chochote ambacho
kimepatikana kuhusiana na
mauaji hayo?akauliza Dr Evans.
“Mkuu,mara tu baada ya
jeshi la polisi kupata taarifa za
mauaji yale na kuyathibitisha
nilikutaarifu na ukanipa
maelekezo,tayari tumekwisha
fungua jalada la uchunguzi na
vijana wako kazini wakiendelea
na kazi.Mimi mwenyewe baada
ya kupokea taarifa hiyo
niliondoka na kwenda eneo la tukio kuthibitisha kwani Donald
ni mtu niliyekuwa
nikifahamiana naye sana
tulikutana tukiwa chuo kikuu
cha Dar es salaam na toka hapo
tumeendelea kuwa marafiki
wakubwa.Mheshimiwa rais
tunaendelea kuchunguza
nyumba ile yalimofanyika
mauaji kujua shughuli gani
zilizokuwa zinaendelea kwani
kumekutwa vifaa mbali mbali
vya mawasiliano na inaonekana
kulikuwa na kompyuta kadhaa
lakini zote
zimeondolewa.Inaonekana baada ya kutekeleza mauaji yale
wauaji waliondoka na
kompyuta zote zipatazo
kumi.Tunahisi kuna kitu katika
hizo kompyuta ndiyo maana
zikachukuliwa na wauaji.Vile
vile wauaji walichukua simu
zote za watu waliowaua.Donald
amekutwa akiwa ameuawa
ndani ya gari akiwa amevaa
mavazi ya kulalia,inaonekana
aliondoka nyumbani kwake na
kwenda katika nyumba ile usiku
hivyo tunataka kujua
mahusiano yake na wale watu
waliouawa.Mheshimiwa rais timu maalum kutoka makao
makuu iko kazini hivi sasa na
nitakutaarifu kila pale
nitakapopata taarifa yoyote
kutoka kwao” akasema inspekta
jenerali wa polisi
“Kabla taarifa hiyo
niliyopokea kutoka kwa IGP
haijapoa nikapokea tena taarifa
nyingine ya kifo cha waziri
mkuu..” akasema Dr Evans na
kuinamisha kichwa
“I’m sorry,kifo cha waziri
mkuu kimeniumiza mno”
akasema Dr Evans naukimya
ukatawala ndani ya chumba kile.Kila mmoja alikuwa na uso
wenye simanzi.
“Wakuu wote wa vyombo
vya usalama mko hapa nataka
kujua nini kimetokea Dodoma
hadi bomu likategwa katika
ofisi ya waziri mkuu na
kumuua.Mmekwisha wajua
watu waliofanya tukio hilo ni
akina nani?akauliza Dr Evans na
kuwatazama wakuu wale wa
vyombo vya usalama
“Inspekta jenerali tuanze na
wewe.Jeshi la polisi ndio
wanaolinda ofisi zote kuu za
serikali.Imewezekanaje watu wakaingia na kutega bomu
wakati jengo lile lina ulinzi saa
ishirini na nne bila polisi
kugundua?Askari wako
walikuwa wapi?akauliza Dr
Evans kwa sauti kali kidogo
“Mheshimiwa rais ni kweli
jengo la ofisi ya waziri mkuu
linalindwa na askari polisi kwa
saa ishirini na nne na
kilichotokea kimetustua hata
sisi ngazi za juu na tumejiuliza
swali hilo hilo imewezekanaje
hawa watu wakapenya na
kutega mabomu katika geti la
ofisi ya waziri mkuu ambako kuna ulinzi wa saa ishirini na
nne?Askari wetu walikuwa
wapi? Mheshimiwa rais ni
mapema sana kupata majibu ya
maswali haya kwani uchunguzi
ndiyo kwanza umeanza,tayari
timu maalum ya makachero
mahiri kabisa ndani ya jeshi la
polisi wamekwisha tua jijini
Dodoma na tayari wameanza
uchunguzi kuhusiana na tukio
hili na mimi mwenyewe baada
ya kumalizika kwa kikao hiki
ninakwenda Dodoma kujua nini
hasa kilichotokea na
nitahakikisha ndani ya muda mfupi tunapata majibu”
akasema Inspekta jenerali wa
polisi.Ukimya ukapita tena
halafu Dr Evans akasema
“Idara ya kupambana na
ugaidi ni kazi yenu kudhibiti
matukio kama haya ya
ugaidi,mlikuwa wapi na kuacha
shambulio hili likatokea?
Shambulio kama hili si la
kupangwa kwa siku
moja,lazima limechukua muda
kuandaliwa.Ninyi kama idara
yenye jukumu la kuzuia mambo
kama haya yasitokee hamkuwa
na viashiria vyovyote vilivyowaonyesha kwamba
shambulio kama hili linaweza
kutokea?Mmeshindwaje
kubaini jambo kama hili
kutokea hasa katika sehemu
nyeti kama ofisi ya waziri
mkuu?akauliza Dr Evans kwa
ukali
“Mheshimiwa rais”
akasema Genevieve Nelson
mkuu wa idara ya kupambana
na ugaidi.
“Idara yangu haikuwa na
taarifa zozote za kuweza
kutokea kwa shambulio
lile.Tayari idara yangu imekwisha ingia kazini
kuwatafuta wale wote
waliofanya tukio hili
tukishirikiana na vyombo
vingine.Timu ya watu nane
tayari wamekwisha wasili jijini
Dodoma.Nina uhakika mkubwa
kwamba hadi kufika mchana wa
leo tutakuwa tumepata jibu zuri
la nani waliofanya shambulio
hilo”akasema Genevieve
“Kwa idara hii muhimu
sana kushindwa kubaini
kuwepo kwa shambulio hili ni
udhaifu mkubwa sana.Najiuliza
kama leo wameweza kutega bomu katika ofisi ya waziri
mkuu bila chombo chochote
kung’amua je watashindwa
kuingia na kutega bomu
ikulu?Kuna umuhimu gani wa
kuwa na idara ya kudhibiti
ugaidi ikiwa magaidi wanawza
kupenya hata katika ofisi nyeti
za serikali na kufanya
mashambulio?akauliza Dr
Evans kwa ukali akiwatazama
wakuu wale wa vyombo vya
usalama
“CDF kuna nini upande
wako? Akauliza Dr Evans
“Baada ya kupata taarifa za
tukio hilo nimeelekeza timu ya
wataalamu wa mabomu ifike
haraka sana eneo la tukio na
tayari wako eneo la tukio
wakisaidiana na wataalamu
kutoka jeshi la polisi kukusanya
kila kitu kwa ajili ya uchunguzi
kubaini ni bomu la aina gani
lililotumika na limetengenezwa
wapi.” akasema mkuu wa
majeshi.Ilimchukua Dr Evans
dakika chache za kutafakari
kisha akasema
“7 Agosti 1998 tulionja
adha ya mashambulio ya kigaidi baada ya ubalozi wa marekani
hapa nchini kulipuliwa.Watu 11
walipoteza maisha na wengine
85 walijeruhiwa.Leo kwa mara
ya pili tena magaidi
wanatushambulia na safari hii
wakimlenga kiongozi mkubwa
kabisa wa serikali ambaye ni
waziri mkuu wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania.Hili ni
jambo lisilokubalika na
linaumiza sana.Damu ya watu
hawa imepotea bila hatia
yoyote.Nataka vyombo vyote
vya ulinzi na usalama nchi hii
mshirikiane na muhakikishe kwamba watu hawa waliofanya
unyama wa namna hii
wanapatikana haraka sana na
watueleze nini sababu ya
kufanya hivi.Wametuchokoza
na hatuwezi kukaa
kimya.Yeyote aliyetuchokoza
lazima apate majibu yake.Awe
ni mtu,kikundi cha watu au taifa
lazima ajulikane na apate stahili
yake kwa unyama huu
waliotufanyia.Nataka tutume
ujumbe kwa dunia kwamba
Tanzania si sehemu salama kwa
magaidi na wale wote wenye
kufikiria kufanya mashambulio katika ardhi yetu wasithubutu
kufanya hivyo tena.Kwa kuwa
bado ni mapema sana na hatuna
taarifa zozote za nani
wamefanya shambuliohili
nataka tukutane tena hapa saa
kumi na moja jioni na mpaka
wakati huo kila mmoja aje hapa
akiwa na taarifa idara yake
imefikia wapi katika
kuwatambua magaidi
waliofanya unyama huu kwenye
ardhi yetu” akasema Dr Evans
na wajumbe wa kikao kile
wakatawanyika na kuwaacha
Dr Evans,makamu wa rais na rais wa Zanzibar katika
mazungumzo mazito
MAZISHI YA KITAIFA - BAADA
YA SIKU 3
Uwanja wa Uhuru jijini Dar
es salaam ulifurika pomoni
katika mazishi ya kitaifa ya
waziri mkuu wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania
aliyefariki katika mlipuko wa
bomu jijini Dodoma.Viongozi
kutoka nchi mbali mbali za
Afrika waliwasili kuhudhuria
mazishi yale ya kitaifa.Rais wa jamhuri ya muunganoi wa
Tanzania Dr Evans akiwa na
mke wake waliwasili katika
uwanja wa taifa tayari
kuwaongoza watanzania katika
shughuli ile.Dakika chache
baada ya rais kuwasili,mwili wa
waziri mkuu ukaingizwa
uwanjani kwa ajili ya kuagwa.
Viongozi wa dini
walifungua shughuli ile kwa
kusoma dua kisha zikafuata
salamu kutoka kwa wakuu
mbali mbali wa nchi
waliohudhuria mazishi yale na
hatimaye ukafika wakati ambao rais wa jamhuri ya muungano
wa Tanzania akapewa nafasi ya
kuhutubia hadhira ile kubwa ya
watanzania waliofika kumuaga
waziri mkuu.
“Ndugu watanzania na
wageni wetu mliotoka katika
mataifa jirani kuja kuungana
nasi katika mazishi haya ya
kitaifa,awali ya yote napenda
kumshukuru mwenyezi Mungu
mwingi wa rehema
kutukutanisha hapa sote siku ya
leo katika shughuli hii ya
kumuaga mpendwa wetu
mheshimiwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania” Dr Evansa
akanyamaza kidogo halafu
akaendelea
“Dakika thelathini kabla ya
uhai wake kukatishwa
kikatili,nilizungumza naye na
nikampa maelekezo katika
mambo kadhaa na nilimuahidi
kwamba mwisho wa wiki
tungekutana jijini Dodoma.Nusu
saa baada ya kuzungumza naye
nilipewa taarifa za kifo
chake,nilipatwa na mstuko
ambao siwezi kuuelezea.Kifo
hiki kimenigusa sana mimi binafsi,watanzania wote kwa
ujumla na wapenda amani kote
duniani.Nimepokea salamu za
rambi rambi kutoka kwa
mataifa mengi duniani wote
wakiguswa na msiba huu
mkubwa,nawashukuru sana
nyote mliotufariji katika wakati
huu mgumu” rais akanyamaza
tena kidogo na kuendelea
“Hakuna maneno mazuri ya
kumuelezea mpendwa wetu
huyu kwani hakuna
asiyefahamu utendaji wake wa
kazi.Binafsi amekuwa msaada
mkubwa sana kwangu na
serikali
ninayoiongoza.Amekuwa
msimamizi mzuri wa shughuli
zote za serikali kwa umakini na
weledi mkubwa sana.Muda
hautoshi kumuelezea mpendwa
wetu huyu itoshe tu kusema
kwamba utendaji wake wa kazi
ulitukuka na tumempoteza mtu
muhimu mno.
Kutokana na utendaji kazi
wake uliotukuka na uadilifu
usio na kifani,alitengeneza
maadui wengi wa ndani na nje
ya nchi hasa wafujaji wa fedha
za serikali,mafisadi na wahujumu uchumi.Hakusita
kukemea ubadhirifu na
kuchukua hatua stahiki kila pale
alipoubaini.Maadui hawa
aliowatengeneza hawakuona
namna nyingine ya kupambana
naye zaidi ya kuitoa roho
yake.Walichokifanya ni unyama
uliopitiliza na
haukubaliki.Ninatuma salamu
kwa wale wote waliofanya
kitendo hiki,awe ni mtu,kikundi
cha watu wa ndani au nje ya
nchi siku zenu
zinahesabika.Mmetuchokoza na
sasa ni wakati wetu wa kujibu mapigo na majibu yetu
hayatakuwa
madogo.Tutawasaka magaidi
hawa kila sehemu,iwe
ardhini,majini au hata
angani,hawana sehemu ya
kujificha.Hakuna jiwe libaki juu
ya lingine wote walioshiriki
uovu huu watapata stahili yao”
akasema Dr Evans kwa
msisitizo mkubwa
Wakati mazishi ya kitaifa
yakiendelea katika uwanja wa
uhuru jijini Dar es salaam,katika
uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere ndege ya shirika la ndege la Ethiopia ikitokea Tel
Aviv kupitia Addis Ababa ilitua
na abiria kuanza kushuka.Ndani
ya ndege hii walishuka majasusi
watano kutoka shirika la ujasusi
la Israel Mossad.Majasusi hawa
walikuja nchini kwa ajili ya
kutekeleza operesheni maalum
ya kumteka Edger kaka.Tayari
walikwishapata taarifa kwamba
Edger kaka alikuwa na mipango
ya kurejea nchini siku ya
mazishi ya waziri mkuu ili
aweze kuwahi mazishi hayo
kwani waziri mkuu alikuwa ni
mmoja wa watu aliowaheshimu sana.Waliwahi kufika nchini
kabla ya ndege aliyopanda
Edger Kaka na Olivia ambayo
ililazimika kuchelewa kuondoka
nchini Israel kwa sababu za
kiufundi.Ukweli ni kwamba
hakukuwa na hitilafu yoyote
katika ndege hiyo bali ulikuwa
ni mpango maalum wa Mossad
ili Edger achelewe kufika nchini
Tanzania na kufika Dar es
salaam usiku ili mpango wa
kumteka uweze kutekelezwa
kama ulivyopangwa.
Majasusi wale baada ya
kukamilisha taratibu za
uhamiaji na kuruhusiwa kuingia
nchini kila mmoja alipokelewa
na mtu maalum kutoka ubalozi
na kumpeleka katika nyumba
anakoishi afisa mmoja wa
ubalozi ambako ndiko mipango
yote ya operesheni ile ilikuwa
inafanyika.Siku mbili zilizopita
majasusi wengine watatu
waliwasili nchini kimya kimya
kwa ajili ya kuandaa operesheni
hiyo ya siri wakisaidiwa na
maafisa wa ubalozi wa Israel
nchini Tanzania.
Baada ya kuhakikisha kila
mmoja wao ameingia nchini salama na hakukuwa na tatizo
lolote bila kupoteza muda kikao
kikaanza
“Poleni kwa safari na
karibuni Tanzania” akasema
Gershom Rabin mkuu wa
operesheni ile.
“Kwa siku tatu tulizokaa
hapa tumekuwa na kazi kubwa
ya kuhakikisha tunaandaa
operesheni kubwa ya aina yake
ambayo itatuwezesha kumpata
Edger kaka na kuiacha serikali
ya Tanzania ikiamini kwamba
Edger kaka amefariki katika
ajali ya gari.Mpaka sasa mipango yote inakwenda
vyema.Nimekuwa na
mawasiliano na mawasiliano na
watu wetu Noam na Yosef
ambao wako ndani ya ndege
aliyopanda Edger na
wamenihakikishia kwamba
Edger bado yuko ndegeni
nimewasiliana pia na marubani
wa ndege hiyo
wamenihakikishia kwamba
ndege itaingia Dar es salaam saa
sita za usiku leo hivyo
operesheni yetu bado
inaendelea vizuri kama tulivyoipanga” akasema
Gershom
“Hapa mbele yetu kuna
ramani” akasema Gershon na
kuisogelea ramani ile.
“Hii ni barabara ambayo
inatoka uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere kuja
mjini.Shughuli yetu itafanyikia
eneo hili hapa lenye mduara
mwekundu.Ni kilometa kadhaa
kutoka uwanja wa ndege na
tumechagua eneo hili kwa kuwa
hatutaki tukio lifanyike kati kati
ya jiji ambako kwa nyakati hizo
bado linaweza kuvuta watu.Ilan na Moshe mtakuwa katika
uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere kumsubiri Edger kisha
mtawapokea Noam na Yosef
halafu mtalifuata kwa nyuma
gari atakalopanda Edger huku
mkiendeleza kuwasiliana
nasi.Sina haja ya
kuwakumbusha nini mnapaswa
kufanya kila mmoja anafahamu
sehemu yake ni ipi na
tumekwisha fanya mazoezi ya
kutosha hivyo kilichobaki ni
utekelezaji tu.Kikubwa
ninachowasisitiza ni umakini
mkubwa sana kwani operesheni hii ni ya siri na serikali ya
Tanzania haifahamu
chochote.Kosa moja hata dogo
linaweza kutuletea matatizo
makubwa hivyo epukeni
kufanya kosa.Mwisho kabisa
kumbukeni kunaweza kutokea
mabadiliko katika operesheni
hii hivyo kila mmoja awe
makini katika kumlinda
mwenzake” akasema Gershom
kisha wakaendelea na
majadiliano kuhusiana na
operesheni ile.