Riwaya: Siri

Riwaya: Siri

Basi ngoja tu nsubiri timu yangu ya simba inipe furaha ya leo naona watu wamekoo na adithi zao
 
Kulingana na ratiba yangu nitakuwa natupia usiku kuanzia saa nne
 
Kulingana na ratiba yangu nitakuwa natupia usiku kuanzia saa nne
sisi shifa yetu utupie hadithi mkuu na ahadi zitimie hata ukitupia saa saba za usiku tumeridhia ila tu usituchomeshe mahindi yakaungua
 
SIRI
episode 25
Mtunzi. Patrick CK

DAR ES SALAAM
Dr Olivia alirejea Dar es
salaam tayari kabisa kuanza
mchakato wa kuutafuta ukweli
kuhusu Edger Kaka ambaye kilamtu aliamini kwamba amefariki
dunia na kuzikwa
“Bado akili yangu
inanituma kuamini kwamba
yule tuliyemzika ni Edger Kaka
.Hata hivyo ngoja tufanya
uchunguzi ili tuubaini ukweli
kama kweli amekufa au yuko
hai kama mama yake
anavyohisi” akawaza Dr Olivia
akiwa ndani ya gari akielekea
nyumbani kwake baada ya
kushuka katika uwanja wa
ndege wa Julius Nyerere.Bila
kuchelewa alipofika nyumbani kwake akampigia simu rafiki
yake Walter kasuku.
“Dr Olivia” akasema Walter
“Walter ninahitaji kukuona
uko wapi?
“Niko katika mizunguko
yangu mjini”
“Unaweza ukaja nyumbani
kwangu mida hii?Niko hapa
ninakusubiri” akasema Dr
Olivia na Walter akamuahidi
kuwa angefika pale kwake
muda si mrefu.
“Ninajuta sana kuyaokoa
maisha ya Edger kwani msaada
wangu nilioutoa unanipeleka katika shimo la moto.Nimeingia
katika hatari kubwa sana bila
kutarajia. Hakuna anayeweza
kuhisi kama Edger kaka tumaini
la watu wengi si mtanzania na
vile vile ana mafungamano na
IS.Hii ni siri kubwa sana na
ninajuta kuifahamu.IS ni
kikundi hatari sana cha kigaidi
lakini siwezi kwenda kinyume
na maelekezo yao kwani
wamekwisa nilisha kiapo cha
kutunza siri hii niliyoifahamu
na nimewahakikishia kwamba
nitakwenda nayo
kaburini”akawaza Dr Olivia “Ninajiuliza ni vipi kama
nikigundulika kama
ninawasiliana na Habiba Jawad
ambaye ni mfadhili wa makundi
ya kigaidi? Ni vipi kama
ikigundulika kituo kile cha
utafiti wa magonjwa
kimejengwa kutokana na fedha
za watu ambao ni wafadhili wa
magaidi?Kuna wakati ninajiwa
na wazo la kutaka kukiwasha
moto kituo kile kiteketee kabisa
ili mimi na hawa jamaa tusiwe
na mawasiliano tena lakini
kituo kile ni muhimu na kina
msaada mkubwa sana” akawaza Dr Olivia na kuamua kunywa
mvinyo mkali ili kuondoa
mawazo yaliyojaa kichwani
Walter Kasuku aliwasili
katika makazi ya Dr Olivia na
kukaribishwa ndani.
“Walter karibu sana” Dr
Olivia akamkaribisha Walter
“Olivia are you
okay?akauliza walter mara tu
baada ya kumuona Dr Olivia
“I’m okay.Nina uchovu wa
safari nimerudi toka nje ya nchi
mchana huu” akasema Dr Olivia
“Pole na safari Dr
Olivia.Baada ya kupata mwito wako nimeachana na kila kitu
nimekuja kukusikiliza” akasema
Walter na Dr Olivia
akatabasamu
“Walter nimekuita
ninahitaji msaada”
“Sema Olivia unahitaji
msaada gani?
“Nina kazi muhimu sana
nataka unitafutie vijana majasiri
”akasema Dr Olivia.Walter
akatabasamu na kutoa pakiti ya
sigara
“Ni kazi gani hiyo Dr
Olivia?akauliza Walter huku
akiwasha sigara “Ni kazi ngumu kidogo na
inayohitaji usiri mkubwa”
akasema Dr Olivia
“Usiogope Dr Olivia
niambie ni kazi gani,hata kama
ni kuua mtu kwa ajiili yako
mimi niko tayari wewe ni mtu
wangu wa muhimu sana.Toka
uliponisaidia mwanangu
akafanyiwa upasuaji wa moyo
wakati ule nikiwa sina hata
shilingi kumi wewe si rafiki tu
bali ni ndugu yangu
kabisa.Niambie kazi gani
unayo? akasema Walter huku
akipuliza moshi wa sigara “Walter unanifurahisa sana
ndugu yangu sijawahi kuwa na
mawazo kama hayo ya kuua
mtu” akasema Dr Olivia huku
akicheka
“Hata mimi nilikuwa
nakutania Dr Olivia.Nieleze ni
kazi gani unayo?
“Unamkumbuka Edger
Kaka?akauliza Dr Olivia
“Ndiyo ninamkumbuka.Si
yule mbunge aliyefariki katika
ajali ya gari?akauliza Walter
“Ndiyo”
“Ni miaka mitatu sasa
imepita toka alipofariki dunia.Ninataka kupata sampuli
ya mabaki yake kwa ajili ya
kufanya uchunguzi
Fulani.Ninahitaji unitafutie
vijana wanaoweza kuchimba
vizuri na kuingia ndani ya
kaburi kuchukua sampuli za
mabaki ninazohitaji.Ni kazi
ngumu na ya siri ila yenye
malipo manono” akasema Dr
Olivia.Walter akapuliza moshi
mwingi na kusema
“Olivia hiyo mbona ni kazi
ndogo tu.Kwa kuwa ni kazi
muhimu na ya siri nitaisimamia
mimi mwenyewe na sihitaji malipo yoyote.Vijana
watakaonisaidia nitawalipa
mimi mwenyewe”
“Walter hapana hupaswi
kufanya hivyo.Nitakulipa fedha
kama ambavyo ningemlipa mtu
yeyote ambaye angeifanya hii
kazi.Tafadhali naomba usiseme
hapana” akasema Dr Olivia
“Sawa Olivia wewe ni bosi
na mimi ninakusikiliza.Lini
unataka kazi hiyoifanyike?
“Nataka kazi hiyo ifanyike
usiku wa leo,ila na mimi
nitakuwepo eneo la tukio ili nichukue sampuli ninazohitaji”
akasema Dr Olivia
“Usihofu Dr Olivia kila kitu
kinawezekana.Mchana huu
mimi nitakwenda katika
makaburi ya midizini
alikozikwa Edger nitafanya
uchunguzi wa namna
tutakavyoweza kuendesha zoezi
hilo usiku wa le😵livia jambo
hili hesabu tayari limekwisha”
akasema Walter na kuagana na
Dr Olivia
“Bado akili yangu inakataa
kabisa kwamba Edger yuko
hai.Mimi ndiye niliyeutambua mwili wake hospitali.Japokuwa
Habiba amejaribu sana
kunielewesha kwa nini
wanaamini Edger yuko hai
lakini nikikumbuka namna
ilivyokuwa na namna
nilivyoweza kuutambua mwili
wa Edger siamini kama ni kweli
yuko hai.Lakini ukilichunguza
kwa undani zaidi suala hili lina
utata mwingi.Majibu yote
tutayapata baada ya kufanya
vipimo” akawaza Dr Olivia
baada ya Walter kuondoka “I’m so scared.Ni vipi kama
kweli mwili ule nilioutambua
haukuwa wa Edger? Akajiuliza
“Hili jambo linaniogopesha
sana.Lakini vipimo vitatupa
majibu” akaendelea kuwaza
****************
Saa mbili za usiku Walter
alikwenda kumchukua Olivia
kwa ajili ya kuelekea katika
zoezi la kwenda kuchukua
sampuli za mabaki ya Edger
Kaka. “Dr Olivia una hofu
yoyote?akauliza Walter baada
ya Dr Olivia kuingia garini
“Ninahofu lakini hakuna
tatizo lolote twendeni” akasema
Dr Olivia.Ndani ya gari
alikuwepo Walter na vijana
wengine watatu safari ikaanza
kuelekea makaburi ya Midizini
“Sijawahi kuingiwa na woga
wa namna hii katika maisha
yangu.Usiku huu ninakwenda
makaburini kufukua kaburi dah
! Nitaendelea kukijutia kitendo
cha kumuokoa Edger kwani
ndicho kimenifikisha hapa.Kama nisingemuokoa
Edger hivi sasa ningekuwa
naendelea na maisha yangu bila
matatizo lakini sasa maisha
yangu yamebadilika”
akaendelea kuwaza Dr Olivia
Walikaribia kufika katika
makaburi ya Midizini
ulikozikwa mwili wa Edger
Kaka.Ni makaburi yaliyoko nje
kidogo ya jiji na kulijengwa uzio
mkubwa kuzunguka makaburi
hayo na kulikuwa na ulinzi kwa
saa ishirini na nne.Toka mchana
Walter alifika eneo hilo na
kufanya uchunguzi namna atakavyoweza kuingia ndani ya
makaburi yale na akagundua
kwamba kuna mtaro mkubwa
wa maji ya mvua unaotoka
ndani ya makaburi yale.
Walisimamisha gari na
kuliacha umbali wa kilometa
mbili kutoka makaburi yale
wakachukua vifaa vyao na
kupita porini wakimuacha mtu
mmoja akilinda gari.Waliufikia
ukuta uliozunguka makaburi
yale.
“Kuna mageti matatu katika
makaburi haya na yote yana
walinzi hivyo tutaingia ndani kwa kupitia mtaro wa maji ya
mvua.Msiogope nimekwisha
fanya uchunguzi toka mchana
na ramani yote ya mahala hapa
ninayo.Nifuateni mimi
nitakavyosema” akasema
Walter wakaanza kuambaa na
ukuta akiwaongoza wenzake
hadi walipofika sehemu
ambako mtaro ule unatokea
ndani kulikuwa na wavu kwa
ajili ya kuzuia watu kupenya na
kuingia ndani.Walikuwa
wamekamilika kwa vifaa hivyo
likafanyika zoezi dogo la
kuung’oa wavu ule wakaingia ndani kisha walter
akawaongoza kuelekea katika
kaburi la Edger.lilikuwa ni
kaburi zuri lililopambwa kwa
vigae vyenye kung’aa na picha
ya Edger ikionekana katika
mojawapo ya kigae.
“Kaburi la Edger hili
hapa.Kazi ianze mara moja”
akasema Walter akiwaelekeza
vijana wake waanze kazi ya
kuchimba pembeni ya
kaburi.Kazi ilifanyika haraka
haraka na ndani ya saa moja
walikuwa wamekwisha chimba
shimo kubwa pembeni ya kaburi kisha wakatoboa tundu
katika ukuta wa
kaburi.Lilitobolewa tundu
kubwa ambalo mtu angeweza
kupenya na kuingia ndani ya
kaburi.Walter akakaingia
shimoni kuhakiki kazi
iliyofanyika halafu akatoka na
kumfuata Olivia
“Dr Olivia kazi tayari.Uko
tayari kuingia ndani ya kaburi
kuchukua sampuli
unazozihitaji? akauliza
Walter.Dr Olivia alikuwa
anaogopa sana “Dr Olivia kazi tayari.Ni
wakati wa kuchukua sampuli”
akasema Walter lakini bado
Olivia alionekana
kuogopa.Walter akamshika
mkono
“DrOlivia kila kitu tayari ni
wakati sasa wa kuchukua
sampuli unazozihitaji.Usiogope
nitaingia ndani ya kaburi
pamoja nawe”akasema Walter
na kumuinua Dr Olivia hadi
katika shimo lile akatangulia
kuingia ndani ya lile shimo
halafu akamshika Dr Olivia
akamshusha ndani ya lile shimo.Dr Olivia alikuwa
anatetemeka.Walter akawasha
kurunzi ndogo na kupenya
katika lile tundu akaingia ndani
ya kaburi.
“Olivia haraka ingia ndani
tumalize kazi”akasema Walter
na kumshika mkono Dr Olivia
akamvuta na kumuingiza ndani
ya kaburi lile alikuwa
anatetemeka kwa woga.Walter
akalifungua sanduku lile
ambalo bado lilikuwa linang’aa
kama limewekwa jana.Ndani ya
sanduku lile kulilala mifupa ya
mwanadamu. “Dr Olivia chukua
unachotaka kuchukua
tuondoke” akasema Walter.Dr
Olivia akaondoa woga na
kuchukua sehemu za mifupa
alizozihitaji akaziweka katika
mfuko maalum Walter
akalifunga lile sanudku kisha
wakatoka na kazi ya kulifukia
shimo lile walilochimba
ikaanza.Ilichukua nusu saa
kulifukia lile shimo kisha
wakaondoka hadi mahala
walikoacha gari wakaingia na
kuondoka.Dr Olivia alikuwa
kimya kabisa bado mwili ulikuwa unamtetemeka
hakuweza kuongea lolote hadi
walipofika nyumbani kwake
akaingia chumbani kwake na
kutoka na bahasha nzito
akamkabidhi Walter
akamshukuru kwa kazi ile
kubwa wakaagana
“Walter kumbuka hii ni siri
kubwa hapaswi mtu mwingine
kufahamu” Dr Olivia
akamsisitiza walter
Baada ya akina walter
kuondoka Dr Olivia akavua
mavazi yale aliyokuwa
ameyavaa na kuyatupia katika mashine ya kufulia akaingia
bafuni kuoga
“Mwili bado
unatetemeka.Eneo lile linatisha
mno usiku.Ahsante Mungu
ametusaidia tumetoka
salama.Nimeyaona tena masalia
ya Edger pamoja na ule mkufu
wake aliokuwa amevaa siku
alipofariki” akawaza Olivia
“Ninaamini si muda mrefu
ukweli utajulikana kama kweli
Edger yu hai au
amekufa”akaendelea kuwaza
akatoka mle bafuni nakuingia chumbani kwake akakaa
kitandani
“Siwezi kulala humu
chumbani leo peke
yangu.Jumba hili ni kubwa na
mambo niliyoyaona kule
makaburini yanatisha.Kila
nikifumba macho picha
inayonijia ni ile nikiwa ndani ya
kaburi.Ni vipi kama
tungekamatwa tukiwa ndani ya
lile kaburi? Ingekuwa ni aibu
isiyokuwa na kifani.Narudia
tena kujilaumu sana
kufahamiana na Edger kwani
amenisababisha nikafanya mambo ambayo sikuwahi hata
kuota kama nitayafanya”
akawaza Dr Olivia na
kukitazama tena chumba chake.
“I need to go out.Siwezi
kulala humu ndani peke yangu
leo” akawaza Dr Olivia na
kuchukua simu akampigia rafiki
yake Monica
“Olivia mbona umerudi
kimya kimya?akauliza Monica
rafiki wa Dr Olivia baada ya
kupokea simu
“Nimerudi mchana wa
leo.Uko wapi Monica? “Niko nyumbani
nimepumzika.Kuna nini Olivia?
“Monica nataka kutoka
nikapoteze mawazo.Una nafasi
tutoke wote?
“I’m sorry Olivia labda siku
nyingine leo Eddy amekuja niko
naye na siwezi kuondoka
nikamuacha peke
yake”akasema Monica
“Usijali Monica.Msalimu
sana Eddy” akasema Dr Olivia
na kukata simu
“Hata kama nimekosa mtu
wa kutoka naye nitatoka peke
yangu.Siwezi kulala mwenyewe humu ndani leo” akawaza Dr
Olivia na kufungua kabati lake
akachagua mavazi ambayo
yangemfaa kwa usiku
ule.Alichagua suruali ya jeans
ya bluu na blauzi
nyekundu.Nywele zake ndefu
akazifunga kwa nyuma
akajitazama na kutabasamu
“Nimependeza.Kinachonifu
rahisha kuhusu mimi nguo
yoyote ile inanipendeza”
akawaza na kuchukua pochi
yake akatoka akingia garini na
kuondoka. “Hakkas night club ni
sehemu nzuri na muafaka
kwenda kupoteza mawazo
usiku huu.Ni klabu bora kabisa
katika jiji hili kwani wateja
wake wengi ni watu wastaarabu
tena ni matajiri wenye hela zao
hakuna vitendo vya
vurugu.Hata ukienda
mwanamke peke yako hakuna
atakayekusumbua” akawaza Dr
Olivia akiwa garini.Bado picha
ya namna walivyoingia ndani ya
kaburi la Edger iliendelea
kumjia kichwani “Kila nikifikiria kitendo kile
mwili
unanitetemeka.Sikuitegemea
kama siku moja ningefikia
hatua kama hii ya kufukua
makaburi.” akawaza Dr Olivia
Alifika Hakkas night club
moja ya sehemu zenye burudani
ya kipekee kabisa jijini Dar es
salaam.Ni klabu yenye
kuheshimika kwani hata baadhi
ya viongozi wa serikali hufika
hapa kupumzisha akili baada ya
shughuli za kutwa
nzima.Kulikuwa na sehemu
maalum kwa ajili ya watu maalum matajiri na watu wenye
nyadhifa mbali mbali vile vile
kukawa na sehemu za kawaida
ambako mtu yeyote
anaruhusiwa.
Dr Olivia alishuka garini
akaelekea katika mlango wa
klabu ambako kulikuwa na
walinzi wawili waliovalia sare
maalum vile vile kukawa na
wahudumu watatu waliovaa
suti nyeusi wakamkaribisha
ndani ya klabu ile.Ni utaratibu
wa klabu hii wateja wote
wafikapo hukaribishwa kwa
furaha na wahudumu.Dr Olivia anaifahamu klabu hii amekuwa
akifika hapa mara kwa mara
kupata burudani hivyo
alipitiliza moja kwa moja hadi
katika upande wa watu maalum
au VIP.Hakukuwa na watu
wengi upande huu,akaketi
sofani muhudumu akafika
akamuhudumia kinywani kisha
akaendelea kupata burudani ya
mwnamuziki aliyekuwa akipiga
gitaa na kuimba.Makofi
yalikuwa mengi kila pale kijana
yule alipomaliza wimbo na
watu waliinuka kwenda
kumtunza.Kilikuwa ni kipaji kikubwa.Uso wa Dr Olivia
haukukauka tabasamu.
“Hello maam” sauti ya
kiume ilimstua Dr Olivia
ambaye mawazo yake yote
yalikuwa katika tumbuizo la
yule mwanamuziki.Akageza
shingo na kukutana na mtu
mtanasahati aliyevalia suruali
ya jeans iliyopauka kidogo
fulana na koti zuri.
“Hallo” akasema Dr Olivia
“Naweza kukaa
hapa?akauliza yule jamaa
ambaye alikuwa na glasi ya
kinywaji mkononi.Dr Olivi akamtazama kwa macho ya
kumsaili halafu akasema
“Hakuna tatizo”
Yule jamaa akaketi
pembeni ya Dr Olivia ambaye
macho yake aliyaelekeza kwa
yule mwanamuziki.Baada ya
wimbo kuisha akapiga makofi
ya furaha
“Oh my gosh ! what a talent
!Amenikosha sana yule kijana”
akasema Dr Olivia na kufungua
pochi yake akahesabu kitita cha
noti na kuinuka akaenda
kumtunza halafu akarejea
mahala pale “Kijana yule ana kipaji
kikubwa mno” akasema Dr
Olivia baada ya kurejea kutoka
kutunza.Yule jamaa aliyekuwa
pembeni yake hakujibu kitu
macho yake alikuwa
ameyaelekeza katika simu yake
ya mkononi na hakuonekana
kufurahishwa na burudani
iliyokuwa inatolewa.Dr Olivia
akageuza shingo akamtazama
kwa muda kisha akasema
“Unaonekana haufurahii
kabisa onyesho la yule kijana”
Yule jamaa akainua kichwa
na kusema “Mimi si mpenzi sana wa
miziki ya namna hii ndiyo
maana sijaguswa”
“Why are you here
then?akauliza Dr Olivia
akionekana kumshangaa yule
jamaa
“Nimekuja hapa na marafiki
zangu”
“Where are
they?Wameondoka na
kukuacha peke yako?akauliza
Dr Olivia
“Wapo lakini
wametawanyika kwenda
kutafuta wanawake” “What about you?Aren’t
you going to find one?akauliza
Dr Olivia
“I’m not interested” akajibu
yule jamaa aliyeonekana kuwa
na majibu mafupi.Dr Olivia
akanywa kinywaji halafu
akauliza
“What’s your interest? You
don’t like music,women,you are
not having fun what exactly do
you like?akauliza Dr Olivia yule
jamaa akageuza shingo
akamtazama na kuuliza
“Are you waiting for
someone? “Hapana sitegemei mtu
yeyote.Nimekuja hapa
mwenyewe”akajibu Dr Olivia
“Malaika kama wewe kwa
nini umekuja peke yako sehemu
kama hii?akauliza yule jamaa
“Nikusahihishe mimi si
malaika.Mimi ni
mwanadamu.Malaika wako
huko juu mbinguni”
akajibu Dr Olivia na yule jamaa
akatabasamu
“Finaly you are
smilling.Nini kimekufanya
utabasamu? “Hiyo kauli yako kwamba
wewe si malaika”
“Ni kweli mimi si malaika
mimi ni mwanadamu.Malaika
wanaishi na Mungu huko juu
mbinguni”
“Wanawake kama wewe
ambao muumba wa mbingu na
ardhi amewatunuku uzuri wa
kipekee tunawaita malaika”
akasema yule jamaa na Dr
Olivia akatabasamu
“Arlight Mr no interest I’m
not an angel.My name is
Olivia.Dr Olivia” “Wow! Are you a
doctor?akauliza yule jamaa
“Ndiyo mimi ni
daktari.Nilikuwa nafanya kazi
katika hospitali ya taifa ya moyo
lakini kwa sasa nimefungua
kituo changu cha utafiti wa
magonjwa ya binadamu na
wanyama”
“Ouh kile kituo kikubwa
kilichofunguliwa hivi karibuni
cha utafiti wa magonjwa wewe
ndiye mmiliki wake?akauliza
yule jamaa na Dr Olivia
akatikisa kichwa kukubaliana
naye “Hongera sana,wewe ni
mwanamke wa mfano
kabisa.Nimewahi kusikia sifa
zako namna unavyopambana
kuokoa maisha ya
watu.Nakupongeza kwa
kufungua kituo kile kikubwa
cha kisasa kabisa cha utafiti.By
the way I’m Mathew..Mathew
Mulumbi” akasema yule jamaa
“Nice to meet you mr
Mathew Mulumbi”akasema Dr
Olivia na kuinua glasi yake
iliyokuwa na kinywaji akanywa
kidogo na kuuliza “Mathew unajishughulisha
na nini?
“Mimi ni
mfanyabiashara.Nina kampuni
zangu kadhaa hapa nchini”
akasema Mathew na kumtajia
Dr Olivia kampuni zake
anazozimiliki
“Wow kumbe niko na
bilionea hapa.Ndiyo maana
mawazo yako hayakuwa hapa
kwani ninyi mabilionea muda
wote mawazo yenu yako
kwenye pesa” akasema Dr
Olivia na wote wakacheka “Baba yangu pia ni mfanya
biashara nadhani umewahi
kumsikia Agrey Themba”
“Bilionea Agrey Themba
nimewahi kumsikia japo
hatufahamiani” akasema
Mathew Mulumbi.
“Nitafurahi kama
mkikutana,mnaweza kuwa
marafiki wakubwa kwani tabia
zenu zinaendana”
“Dr Olivia hautajali
nikikuita Olivia?akauliza
Mathew
“Kuwa huru.Call me Olivia”
akasema Dr Olivia “Olivia si kwamba kila
wakati ninawaza pesa.Kuna
muda ambao unahitaji
kupumzisha akili na ndiyo
maana zikatengenezwa sehemu
kama hizi zenye burudani
ambako watu huja na
kupumzisha akili zao”akasema
Mathew
“Kama umekuja kuburudika
na kupumzisha akili kwa nini
hauonekani
kufurahi?Unaonekana kama
umelazimishwa kuja hapa.Let
me tell you one thing mr
Mathew Mulumbi,ukiingia ndani ya jengo hili kama
umekuja kufurahina kupoteza
mawazo matatizo yako yote
yaache getini utakutana nayo
wakati wa kutoka.Kama
unadaiwa na TRA,kama
umegombana na mke wako yote
hayo yaache getini.Ukiingia
humu dance like no body is
watching you,drink,have fun”
akasema Dr Olivia na kuinuka
akamuomba Mathew amsubiri
“Leo nimekutana na kiboko
yangu.Olivia ni muongeaji
hakuna mfano halafu pombe
imekwisha anza kumpanda kichwani” akawaza Mathew na
mara Olivia akarejea akiwa na
chupa ya whisky.
“Mr Mathew Mulumbi kwa
kuwa umekuja hapa kuburudika
naomba sasa tuanze
kuburudika.Usiniambie
kwamba hata mvinyo
hutumii.Tafadhali naomba
tunywe mvinyo huu hadi
tuumalize.Usihofu klabu hii
haifungwi hadi asubuhi”
akasema Olivia na kumimina
mvinyo katika glasi ya
Mathew.Wakagonganisha glasi na kila mmoja akaipeleka
kinywani
“Mhh ! so strong” akasema
Mathew na Dr Olivia akatoa
kicheko
“Usinitie aibu Mathew”
akasema Olivia na kumimina
tena mvinyo mwingine katika
glasi
“Olivia hautajali nikikuuliza
swali?akauliza Mathew
“Uliza usihofu mr Bilionea”
akasema Dr Olivia
“Kwa nini umekuja hapa
peke yako?Mwenzako yuko
wapi? “Mwenzangu yupi?
“Namaanisha mpenzi wako
yuko wapi?Tumezoea kuona
wanawake wengi wakija
sehemu kama hizi huwa
wanaambatana na waume au
wapenzi wao lakini wewe
umekuja mwenyewe yuko wapi
mpenzio? akauliza Mathew.
“Kwa nini unataka kujua
kuhusu mpenzi wangu? Dr
Olivia akauliza
“Ninataka kujihadhari pindi
akitokea hapa kwa sababu
wanaume wengine hawapenzi
kuwaona wapenzi wao wakiwa sehemu kama hizi na wanaume
wengine” akasema Mathew .Dr
Olivia akanywa kinywaji halafu
akaelekeza macho yake katika
glasi ile ya kinywaji akaitazama
kwa muda halafu akasema
“Sina mpenzi”
Mathew akamtazama Dr
Olivia kwa macho yenye
kuonyesha mshangao kidogo
“Vipi mbona umeshangaa?
Ni ajabu mimi kutokuwa na
mpenzi? akauliza
“Si ajabu kutokuwa na
mpenzi lakini nimewashangaa
wanaume kwa nini mpaka leo hii malaika kama wewe uko
mwenyewe?
“Mathew si kwamba
wanaume hawapo lakini ni
mimi mwenyewe ndiye
mwenye matatizo”
“Tatizo gani Olivia?
“Bado sijampata
mwanaume yule ambaye
naweza kusema ameuteka
moyo wangu”
“I see” akasema Mathew na
wote wakatazamana
“Vipi kuhusu wewe mbona
uko peke yako?Mwenzako yuko
wapi?akauliza Dr Olivia “Mimi nina mke na watoto
wawili”
“Hongera”
“Ahsante sana”
“Kama tayari unayo familia
unafanya nini muda huu mahala
hapa? Kwa nini usiende kukaa
na familia yako nyumbani?
“Familia yangu haiko hapa
Tanzania.Wanaishi nchini
Ufaransa”
“Mkeo ni mzungu?
“Hapana ni mtanzania
lakini amechagua kuishi
Ufaransa na tayari anao uraia
wa kule” “Wewe kwa nini uko
hapa?Kwa nini usiungane na
familia yako nchini
Ufaransa?akauliza Dr Olivia
“Hilo jambo limenishinda
kabisa.Siwezi kuukana utaifa
wangu.Mimi ni
mtanzania,nimekulia hapa na
nitazikwa hapa na ndiyo maana
nimechagua kuishi hapa”
“How do you guys manage?
Wewe uko hapa mkeo yuko
Ufaransa.Mnawezaje kuishi
kama mke na mume au
mmeachana tayari? “Hapana hatujaachana
tunaonana mara kwa
mara.Mahusiano ya mbali ni
magumu lakini tunajitahidi sana
kuendelea kulinda penzi letu na
familia yetu” akasema Mathew
“Wewe uko hapa klabu na
mwanamke mwingine
mnakunywa pombe, unaamini
huko aliko mke wako naye yuko
mwenyewe muda huu?akauliza
Dr Olivia
“Hizo ndizo changamoto
tunazokutana nazo lakini
inalazimu tuishi kwa imani” “Hujawahi kumsaliti mkeo
ukiwa huku?akauliza Dr Olivia
na Mathew akacheka
“Dr Olivia una maswali
magumu sana”
“Ugumu uko wapi Mathew
just answer me.Hujawahi
kumsaliti mkeo?Kuwa mkweli
usiogope.Haya ni maongezi tu
hakuna atakayejua” akasema Dr
Olivia
“Kusema ukweli nimewahi
japo ni mara chache.Unajua
kama mwanadamu kuna
nyakati mwili unahitaji
kutimiziwa mahitaji Fulani ya muhimu na kama mtu ambaye
anaweza kukutimizia mahitaji
hayo kwa muda huo hayupo
basi unatafuta namna mbadala
ya kuweza kutimiza haja zako
lakini si kwamba simpendi au
simheshimu yule niliyenaye ni
mazingira tu ndiyo
yanayopelekea hayo kutokea”
akasema Mathew
“Mr Bilionea unajua sana
kujitetea.Anyway siwezi
kukulaumu kwani umbali kati
yako na mkeo unachangia
mambo haya yote kutokea”
akasema Dr Olivia wakaendelea na mazungumzo huku wakipata
kinywaji.Ni Mathew aliyestuka
baada ya kutazama saa na
kukuta ni saa kumi kasoro za
alfajiri
“Olivia ni muda wa
kuondoka sasa.Mapambazuko
yanakaribia” akasema Mathew
na Dr Olivia alipotazama saa
yake akakubali waondoke
“Olivia huwezi kuendesha
gari ukiwa katika hali hiyo
umekunywa sana pombe”
akasema Mathew
“Usijali Mathew I can
Manage” “Hapana Olivia.Let me drive
you home” akasema Mathew na
kumpigia simu mmoja wa
madereva wa kampuni yake na
kumtaka aje kuchukua gari lake
pale klabuni halafu
atamuelekeza sehemu ya
kumfuata.Aliacha ufunguo
mapokezi ili apatiwe dereva
wake atakapofika.Mathew
akashika usukani wa gari la Dr
Olivia ambaye baada tu ya
kuingia garini akaegemeza
kichwa katika kiti na
kulala.Mathew akamuamsha na
kumtaka amuelekeze mahala anakoishi halafu akamuacha
alale.
“Such a beautiful lady”
akawaza Mathew huku
akimtazama Dr Olivia
aliyekuwa amezidiwa na
kinywaji
“Mwanamke mzuri kama
huyu,msomi na anatoka katika
familia yenye uwezo mkubwa
kwa nini hana mpenzi hadi
sasa?Alinieleza ukweli au
alikuwa
ananidanganya?Kingine
kinachonipa maswali kuhusu
mwanamama huyu ni namna alivyokuwa anakunywa
mvinyo.Ni nadra kumuona
mwanamke tena msomi kama
huyu anakunywa pombe kiasi
hiki.Kwa sisi ambao
tunafahamu kuwasoma watu
kwa kumtazama tu Olivia
anaonekana kama vile ana
tatizo Fulani anataka
kujishaulisha ndiyo maana
anakunywa pombe namna
ile.Wanawake kama hawa mara
nyingi tatizo lao huwa ni
masuala ya
mapenzi.Yawezekana
ameachana na mpenzi wake na ndiyo maana anakunywa
pombe kiasi hiki kujisahaulisha”
akawaza Mathew.
Kwa maelekezo aliyopewa
na Olivia walifika katika makazi
yake,mlinzi alipoliona gari la
Olivia hakuuliza chochote
akafungua mlango Mathew
akaingiza gari ndani hadi katika
kibaraza cha nyumba kubwa ya
Olivia akasimamisha gari kisha
akashuka garini akazunguka
upande aliokuwa amekaa Olivia
ambaye alikuwa
amelala.Mtumishi wa ndani wa
Olivia aliposikia gari limesimama mbele ya nyumba
akatoka haraka haraka ili
kumpokea Olivia na akapatwa
na mshangao kwa kukutana na
Mathew akamsalimu
“Naitwa Mathew ni rafiki
wa Olivia.Tulikuwa klabu lakini
Olivia anaonekana kuzidiwa na
kinywaji hivyo nimemrejesha
nyumbani”akasema Mathew na
kumshusha Olivia akambeba
hadi sebuleni akamlaza katika
sofa akamtaka yule mtumishi
aliyejitambulisha kwa jina la
Lucy akaandae kikombe cha
kahawa.Ndani ya muda mfupi kahawa ikaletwa na Mathew
akamuamsha Olivia akamsaidia
kunywa kahawa ile halafu
akamtaka mtumishi yule wa
ndani amuonyesjhe kilipo
chumba cha Olivia.Mathew
akambeba Olivia hadi chumbani
kwake akamlaza kitandani
halafu akampigia simu dereva
wake akamuelekeza mahala
alipo ili amfuate.Alimuacha
Olivia chumbani kwake amelala
akashuka chini kwenda
kumsubiri dereva wake ambaye
hakuchelewa sana akafika Mathew akaagana na Lucy
akaondoka.
*****************
Saa tatu za asubuhi Dr
Olivia akaamka.Kichwa chake
kilikuwa kinagonga kama
kinapigwa na jiwe gumu.
“Oh gosh ! I feel headache
like hell” akawaza na kuinuka
kitandani akatoka mle
chumbani akaenda jikoni
akanywa glasi mbili za maji
halafu akamtaka mtumishi
wake amuandalie supu “Jana nimekunywa pombe
nyingi kupita kawaida
yangu”akawaza Olivia wakati
akielekea chumbani kwake
kujiandaa kwa ajili ya shughuli
zake za siku
“Ni Mathew ndiye
aliyesababisha nikanywa
pombe nyingi kiasi
kile.Nilifurahi sana kukutana
naye” akawaza na kukumbuka
usiku wa jana kule klabu
akatabasamu
“Mathew ni mtu mcheshi
sana.Nilivyokuwa namchukulia
awali ni tofauti na alivyo baada ya kumzoea.Ni mtu ambaye
anafaa sana kuwa naye karibu
na kwa kiasi kikubwa naweza
kusema kwamba alinisaidia
sana kuupitisha usiku wangu
jana.Nilikuwa na mawazo na
woga mwingi na sikujua ni
namna gani ningeweza
kuumaliza usiku wa jana lakini
nilipokutana na Mathew
alinisaidia nikaweza kusahau
matatizo niliyokuwa
nayo.Natamani kama
ningeonana naye tena lakini
sijui nitaonana naye wapi na sikuchukua hata namba yake ya
simu” akawaza Dr Olivia
“It’s not a big deal sitakiwi
kuumiza kichwa sana kuhusu
Mathew kwanza ni mume wa
mtu ninachotakiwa kufanya ni
kujielekeza katika majukumu
yangu na hasa jukumu kubwa
nililo nalo la kufanya utafiti wa
kuhusiana na Edger kaka.Tayari
ninazo sampuli na kinachofuata
ni kuufahamu ukweli.Je Edger
ni mzima au amekufa na kama
ni mzima yuko wapi?Majibu ya
swali hilo yatategemea sana
matokeo ya uchunguzi nitakaoufanya” akawaza Dr
Olivia na kuingia bafuni kuoga
Japo alihisi maumivu
makali ya kichwa lakini
ilimlazimu kuelekea ofisini
kwake.
“I’m working with
terrorists.Hili jambo linanitesa
sana ni vipi kama
nikigundulika? akaongeza
mwendo wa gari huku mwili
wake ukihisi baridi
Dr Olivia alifika katika kituo
chake akaelekea moja kwa moja
katika ofisi yake.Katika kituo
kile kulikuwa na maabara ya siri ambayo aliyekuwa na
uwezo wa kuingia ni Dr Olivia
peke yake.Ilikuwa chini kabisa
ya jengo lile na ili kuingia katika
maabara hiyo inakulazimu
kupita katika ofisi ya Olivia.
Alipitia mafaili kadhaa
yaliyokuwa mezani kwake
halafu akafungua mkoba wake
na kuchukua bahasha ile yenye
sampuli za mifupa waliyoitoa
katika kaburi la Edger
akaitazama halafu akafunga
ofisi yake na kufungua mlango
uliokuwa ndani ya ofisi ile
akaingia katika chumba
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom