mm apa ibrah episode hii nimeiona fupi sana
naomba uwe unanitaggNITAKUPATA TU
SEHEMU YA 017
Alipambana akikataa giza kuuchukua mwanga wa mboni za macho yake, lakini haikusaidia kitu. Akakubali giza liyafunike macho yake. Na kweli ndivyo ilivyokuwa.
Alikuja kushtuka baada ya masaa mawili na kujikuta katika chumba kidogo. Chumba ambacho hakikuwa na kitanda isipokuwa maji tu. Tena maji ya baridi kupindukia. Mwanzo wakati anapatwa na fahamu alidhani labda alikuwa pembezoni mwa bahari ya hindi kutokana na maji yale. Akafumbua macho zaidi na zaidi, akayaona mazingira yale. Akahisi kukata tamaaa. Aliyajua matumizi ya chumba kile. Hakuna mtu ambaye aliwahi kutoka akiwa hai kati ya wote walioingizwa. Akainua kichwa chake na kuangalia juu, akakumbuka mengi aliowahi kulifanyia taifa lake, akakumbuka aliponusurika vifo mara kadhaa kwa sababu ya usalama wa taifa lake. Lakini yote yamesahaurika, lakini yote yalisahaulika kwa sababu ya watu wachache. Hata yeye alipelekwa ndani ya chumba kile ambacho hutambulika kama kuzimu. Alitakiwa naye afe, alitakiwa naye asirudi akiwa hai. Bado maji yaliendelea kumtesa na kumsulubu. Akainua macho na kutizama mwisho kabisa wa chumba kile. Aliamua kujaribu bahati yake, hakutaka kamwe kufa kikondoo, hakuamini kama angeshindwa kutoka pale. Aliamini atatoka tena atatoka akiwa salama. Akauvaa ujasiri na kuutoa uoga na ukataji tamaaa. Akainuka kutoka pale chini, akasimama kwa muda akiendelea kutupa macho yake kila pembe ya chumba kile. Akaunyoosha mwili wake kuupima kama una nguvu, aliporidhika akaanza sasa kutembea ndani ya kichumba kile. Kwa kuwa maji yalikuwa yamejaa mpaka kiunoni, hakuwa akiona chini alipokuwa akitembea. Alipokuwa akipiga hatua nyingine akajikuta akijikwaa kwenye kitu mfano wa mwili wa binadamu. Hilo likamfanya asite kuendelea kutembea, alikuwa amesimama akijishauri kitu. Alishaamua kufanya chochote, akili yake ikahitaji kufanyakazi mara mia zaidi ya kawaida yake. Hakutaka kushughulika na kitu mfano wa mwili wa binadamu aliyoukwaa. Alihitaji kufanya kitu kikubwa cha kumuondoa pale ndani. Akajaribu tena kutembea lakini safari bado alikikanyaga kile kitu mfano wa mwili wa binadamu. Kitu kama hisia kikamjia kichwani, hisia ya kwamba mtu huyu anaweza kumsaidia. Kwa kuwa siku zote aliziheshimu hisia zake, Masimba akainama na kuanza kutafuta chini ya maji. Kweli mikono yake ikagusa mwili wa binadamu. Baada ya kuugusa, akahakikisha mikono yake inaukamata ule mwili na kuanza kuusimamisha. Alipambana kwa muda na alipofanikiwa kuusimamisha akashangaa kumuona mtu anayemjua. Mwili wa mtu yule ulikuwa ni wa mmoja kati ya vijana ambao walikuwa wakimsaidia katika kazi yake.
Hilo hakulitegemea, kengele za hatari zikakigonga kichwa chake. Mmoja kati ya vijana waliokuwa wakimsaidia kazi kuuawa, alijua ilikuwa ni mbinu ya watu waliomfikisha pale. Alitambua vijana wote aliokuwa anasaidiana nao watauawa iwapo kama yeye ataendelea kuwepo pale mahabusu ya kuZimu. Akaendelea kuutizama wili wa kijana yule, hasira zikaonekana usoni. Kuuawa kwa maafisa usalama wa taifa kwa sababu ya manufaa ya watu wachache kulimpa sana hasira. Aliitambua hizi zilikuwa hila za Jimmy Lambert na maafisa waandamizi wa serikali. Alijua wote hawa walikuwa wakishinikizwa kusema wapi ulipo mzigo wa madawa ya kulevya aliouchukua nyumbani kwa Jimmy. Hilo likamfanya aihisi hatari hata kwa teddy, alihisi hata yeye ipo hatari atageukwa na kitakachofuatia ni yeye kupotezwa kama walivyofanya kwake. Kwa mara ya kwanza alitamani amuone teddy amwambie, kwa mara ya kwanza alitaka kumwambia teddy hatari iliombele yake. Alitaka kumwambia ukweli wa mambo. Lakini angetokaje wakati yupo kuzimu, alitokaje wakati muda mfupi ujao atakuwa maiti. Masimba akasonya huku akikifanya kitu ambacho hakuwa amekiwaza. Mikono yake ilizama kwenye mavazi ya marehemu yule. Akahisi kukigusa kitu katika mavazi ya marehemu yule. Akaongeza kasi ya mikono punde akakitoa kitu kile ambacho kilikuwa mfano wa golori. Tabasamu likachanua usoni mwake. Kilikuwa kitu maalum cha kufungulia sehemu zisizowezekana. Kitu ambacho hutumiwa sana na mashirika makubwa ya Kijasusi Hasa CIA na M15 pamoja na M16 ya Uingereza. Akakitizama kwa muda, harafu akakiwasha na kuanza kukizungusha kwa mikono yake akikielekeza kila upande. Sekunde kumi hazi kufika, maji yote yakapotea kisha chini kwa pembeni pakaachia. Mlango mkubwa ukaonekana mbele yake. Hakutaka kusubiri kwa kuwa alitambua huwa kuna muda maalumu. Sekunde ya kumi na mbili alikuwa nje ya chumba kile akitembea kuifuata korido ambayo ilikuwa akielekea kama Chini ya ardhi. Hakuwa na bastola, hakuwa na silaha ya aina yoyote, lakini alikuwa tayari kwa lolote. Jengo lillikuwa kimya kanakwamba hapakuwa na mtu ndani yake. Macho yalikuwa yakiangalia kila kona ya Jengo. Muda mfupi alikuwa ameibukia sehemu ambayo haikuwa kimya. Sauti za watu zilikuwa zikisikika kwa umbali mfupi kutoka mahala aliposimama. Wakati akifikiria nini afanye akavisikia vishindo vya mtu akisogea mahala pale. Akajiandaa kumkabili kwa mikono yake. Punde akamuona mtu akipita, alikuwa mwanamke. Alionekana na mlinzi wa Jengo lile. Alikuwa na Bunduki aina ya Oxcelf SG mkono. Alikuwa akitembea akiangalia huku na huko. Masimba akaona ulikuwa muda sahihi wa kufanya kitu. Alichokifanya ni kumtokea yule msichana kwa nyuma na kumpigia mluzi. Msichana yule akageuka akidhani aliitwa na mwenzake. Lakini alijikuta akikutana na flying kicks kutoka kwa masimba. Kwa kuwa hakutarajia kitendo kile, mwanamke yule akajikuta akishindwa kuzuia mapigo yale, na kuruhusu mateke yale kumtupa chini kama furushi.
Kuwa makin wakati wa copy unatesa wenginenaomba uwe unanitagg
usifanye hivyo siku nyinginenaomba uwe unanitagg