Riwaya: Mkoloni Mzawa

Riwaya: Mkoloni Mzawa

AFRIKA YANGU—10
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
MAWASILIANO: 0673056571

MATUTA YA HASIRA yalijijenga kwa haraka pajini kwa Brigedia Jenerali Buyoya pindi akipatiwa taarifa kutoka kwa Luteni Bazombanza kwenye lile jengo lao pale Buyenzi. Haikuwa taarifa yenye kufurahisha, wala kutengeneza kidogo msisimko nafsini mwake. Bali ilijikita kuzalisha utwetaji wa jazba na jasho jingi kumtiririka.

“Tumejaribu kumtafuta kila kona, lakini hatujabahatika kumwona,” Luteni Bazombanza alizidi kumfafanulia.

“Kwanza, waliwezaje kutoroka?” Brigedia Jenerali Buyoya aliuliza.

“Nasi tulishangazwa namna hiyohiyo. Maana ndiyo tuliwakuta wanatoka.”

“Shubamit!” Brigedia Jenerali Buyoya aliropoka huku akigonga meza kwa ngumi ya moja ya mkono wake. “Kwa hiyo mnataka kuniambia anaungulia kwenye huo moto?”

“Tunahisi hivyo. Hasa baada ya kumkosa.”

“Hainingii akilini. Na nashindwa kukubaliana kwa urahisi hivyo. Mtu mwenye mafunzo ya kijeshi ateketee kweli kwenye moto?” Brigedia Jenerali Buyoya alionyesha mashaka. Na kuwafanya wenzie watulie kumwangalia.

Baadaye Koplo Rumera akaingilia kati, “Mimi nina wazo afande.”

“La namna gani?”

“Kwa sababu tunakosa uhakika, ule moto ukishapoa turudi tukafanye uchunguzi wa kitaalamu kama majivu yatakayokuwepo, lipo litokanalo na binadamu. Lisipokuwepo, wewe una wadhfa mkubwa ndani ya nchi hii. Kuwa kamanda wa mafunzo na operesheni sio jambo dogo, hivyo nitapendekeza ifanyike operesheni kali ya halali kwa mwavuli wa takwa letu.”

“Ina maana kwamba tuandae operesheni halali ya kijeshi?” Brigedia Jenerali Buyoya aliuliza kwa udadisi. “Sasa akishapatikana itakuaje kwa upande wetu?”

“Tutamwondoa mikononi mwa jeshi kwa mtutu wa bunduki siku hiyohiyo watakayompta.”

“Ni idea nzuri lakini. Au Bazombanza unashaurije?”

“Namuunga mkono alichopendekeza. Haitotufanya tuumize sana kichwa.”

Kidogo, nuru ikajijenga wajihini kwa Brigedia Jenerali Buyoya.

Kama walivyoshauriana, Brigedia Jenerali Buyoya aliwatafuta wataalamu wa ki-sayansi. Moto ulivyohitimika wakaanza taratibu za kiuchunguzi wa chembechembe za hayo majivu yametokana na nini. Haikuchukua muda majibu kutolewa, na kubainika hamna jivu lolote la kibinadamu, jambo lililompelekea Brigedia Jenerali Buyoya na watu wake hasira ziwazidi. Kwani sasa walikuwa na uhakika, mtu wao bado anaishi. Na kama anaishi, basi waitumie mbinu nyingine waliyoipangilia.

Utekelezaji wa haraka ukafuatia, kwa Brigedia Jenerali Buyoya kusambaza hila kwa makamanda wa juu na kukubaliwa. Idhini ilivyopatikana, vikosi kutoka kambi mbalimbali za kijeshi vikaandaliwa, kisha mara baada ya hapo operesheni ikatangazwa. Operesheni waliyoiita safisha nchi. Operesheni iliyojaa kiapo cha damu.

Ndani ya dakika chache tu, zilitosheleza kuigeuza Bujumbura kuwa yenye hofu kwa namna wanajeshi walivyotanda mtaani kwa msako na ukaguzi.

***

Pindi gari linarushwa juu kwa ule mshindo wa shambulizi, Askofu Ponera na mama Ndinaa walijikuta wakitokea kioo cha mbele na kuangukia umbali wa mita kadhaa toka gari lilipotua. Askofu Ponera ndiyo aliangukia mbali zaidi ya mama Ndinaa. Na ndiye alikuwa na afuheni kidogo ya kiafya. Ambayo kwa namna fulani ilimwezesha kuwa mtambuzi wa vitu.

Hivyo Luteni Bazombanza na wenzie walivyoifikia ile gari aliwaona. Ijapokuwa ulikuwa muono wenye shida kidogo kutokana na vumbi lililotanda kopeni.

“Wajinga nyie, mlidhani mtanipata kirahisi rahisi?” Askofu Ponera alijisemeza,wakati huo akijitahidi kujiinua.

Pindi wanajigawa kuanza kumtafuta, tayari alikwisha inuka muda, na kujikongoja kwa mchechemeo uliomhimiza kupotelea msituni. Mwendo ukawa taratibu, huku akikata vichaka; vidogo kwa vikubwa mwisho alitokezea mjini na kuanza kuutafuta uelekeo aliodhamiria kuufikia. Ambako ni nyumbani kwa yule Afisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Burundi, Mandoo.

“Ndugu!” Mandoo alistaajabu.

“Nisaidie kwanza, hayo mengine tutayajadili baadaye,” Askofu Ponera alimsihi.

Mandoo akampisha.

Askofu Ponera alivyoingia ndani, Mandoo akaangaza angaza mazingira yazungukayo nyumba aishiyo kama kuna mtu yeyote aliyefuatilia matembezi ya Askofu Ponera. Alivyojihakikishia usalama naye aliingia ndani.

“Imekuaje?” Mandoo aliuliza, huku akichukua nafasi ya kuketi sofani.

“Ndiyo majukumu yaliyonileta huku. Nimeokoka kukiona kifo nitokako.”

“Aiseee,” Mandoo alizidi kustaajabu.

“Walifanikiwa kuniweka chini ya himaya yao wale jamaa.”

Mandoo akadakia, “Acha bhana.”

“Ndiyo hivyo. Lakini cha kushukuru nimefanikiwa kuwatoka.”

“Kuna ripoti yoyote ya kutuma...”

“Haina haja. Nahitaji niwe fit kwanza ili niwarudie wale wajinga.”

“Mbona mapema sana?”

“Ndivyo kazi itakavyo. Hivyo fanya jitihada afya yangu iwe vyema.”

Haikuchukua muda mrefu ombi la Askofu Ponera kutekelezeka. Mara baada ya Mandoo kupotelea chumbani kwake kwa dakika kadhaa, alivyorudi, alikuwa amebeba kisanduku kidogo chekundu kilicho na maandishi machache yatambulishayo ni mahususi kwa minajili ipi. First Aid.

Zoezi la ugangaji likaanza.

Kwa kuchua sehemu mbalimbali zilizovimba vimba na kufunga bandeji iliyochovywa dawa sehemu zenye majeraha.

“Kabla sijarudi rasmi mtanangeni...” Askofu Ponera akaacha kauli yake ikielea. Baada ya kubananisha meno kwa kusikilizia maumivu yapenyayo bandeji ilivyofungwa. “Nataka uniandalie usafiri utakaonifikisha mpakani siku hiyo.” Akampiga kidogo mbata Mandoo kwenye moja ya bega, kisha akaendelea, “Siku nitakayoenda kuwafundisha adabu inabidi uwe eneo la karibu, ili nikishahitimisha tu, uniondoe hapa jijini nitafute uelekeo wa kurejea Dar es salaam.”

“Hilo halina shaka. Maana nililetwa huku kwa ajili ya kazi za namna hii. Kikubwa...”

Askofu Ponera akadakia pasi na Mandoo kuhitimisha kauli yake, “Nitaongeza umakini, ili nisiangukie mikononi mwao kwa mara nyingine.”

“Swadakta.” Mandoo akaangua tabasamu.

Siku zilizofuata; siku za matazamio ya maendeleo ya afya yake, Askofu Ponera akatumia muda mwingi sana kufuatilia habari mbalimbali zinazoripotiwa na vyombo vya habari. Hasa mwenendo wa operesheni. Pasi na kusahau mazoezi madogomadogo kuurejesha mwili kwenye ukawaida.

Zoezi hili lilimchukua majuma mawili pekee, na kujiridhisha yuko ngangari, ijapokuwa Mandoo hakuacha kumsihi ajipe muda zaidi, angalau afikishe hata mwezi mmoja, lakini Askofu Ponera alikataa.

“Muda hauruhusu, wala haunisubiri. Hivyo kuna kila haja ya kufanya kazi hii kwa uharaka.”

Ndiyo ulikuwa utetezi wake.

***

Ilikuwa jumamosi, Askofu Ponera akiwa ndani ya teksi kulizunguka jiji la Bujumbura kutafuta uelekeo wa Buyenzi. Wakati huo operesheni ya jeshi ikiendelea kumtafuta, lakini katu, haikuwa sababu ya yeye kutofanya alichodhamiria. Dereva wa ile teksi alikuwa kijana wa makamo, hivyo ukiachilia uteja, alimmudu kila nyanja. Hasa kwenye suala la rika. Jambo lililomrahisishia kumwarumu kila ajisikiapo kuikwepa hatari.

Na hakika, walifanikiwa kuvuka vizuizi vingi hadi wakaikurubia Buyenzi. Hapo, Askofu Ponera akamwamuru dereva aegeshe gari kando apate kuteremka kwa sababu ameshafika. Dereva bila ajizi naye alitekeleza. Askofu Ponera alifanya malipo, kisha akateremka kwa uharaka na kuwa hima kupiga ndogondogo. Wa mbaruu.

Toka Askofu Ponera atoroke pamoja na mama Ndinaa ulinzi kwenye lile jengo alilodhamiria kulifikia uliimarishwa. Waliongezwa vijana wengine, na operesheni ilivyoanza ndiyo kuzidi, vikosi vya jeshi havikukatika kutembelea kila baada ya muda fulani. Ukiachilia mbali hilo, umbali wa mita mia moja toka lilipo kiliwekwa kituo cha ukaguzi. Lakini wao pindi wanawasili, walikikwepa kituo hicho pasi na kubainika. Ukijumlisha na ukwepaji wa vituo vingine walivyovipita huko nyuma, ikajenga walakani kwa dereva teksi.

Walakini ulikuja kuongezeka pale alipomwamuru amteremshe. Hakukuwa na makazi. Na kile kitendo cha kupiga ndogondogo kikapigilia msumari wa mwisho. Mteja aliyempakiza hakuwa mtu mwema. Fukuto la walakini hilo lilimsumbua hadi alipofikia kituo cha ukaguzi. Akasimamishwa, na kuamrishwa kuegesha gari kando ya barabara.

Kuepuka kusumbuliwa na wale askari wa jeshi la FDN, yule dereva teksi akawashirikisha ule walakini alionao.

“Nimemteremsha hapo mbele tu. Nimeshindwa kumwelewa kabisa kama ni mtu mwema. Amekaa kimachale machale sana,” dereva teksi aliwataarifu askari wawili waliokuwa wamesimama ubavuni mwa gari yake. Yeye hakuteremka.

“Ni muda mrefu sana?” askari mmoja wapo aliuliza.

“Hapana. Haichukui hata dakika tatu toka nilivyomteremsha.”

Taarifa hii ikawa kinga. Hawakumsumbua. Walimwacha aendelee na safari nao kujuzana waliyodokezewa. Sekunde kadhaa baadaye simu za upepo zikakesha kubadilisha taarifa kutoka kituo kimoja kwenda kingine. Wakati huohuo, magari kadhaa ya kijeshi yakiwa na askari wenye silaha yakafunga safari kuufuta uelekeo pasa. Ule aendao Askofu Ponera.

Dakika chache baadaye waliifikia ile nyumba, makazi ya siri ya genge la Brigedia Jenerali Buyoya. Hawakusubiri amri, wapiganaji wakateremka garini kwa kuchumpa kisha walilizingira jengo kwa ustadi.

***

Mandoo naye hakuwa mbali na lile jengo kama walivyokubaliana na Askofu Ponera. Ilikuwa siku mahususi ya Askofu Ponera kuliacha jiji la Bujumbura baada ya kufanikisha kuzifikia hatua zote alizotumwa kufuatilia. Hivyo pilikapilika zote ziendeleazo na wale askari alizishuhudia. Jambo lililompa hofu kwa wakati fulani kabla hajapotezea.

Kilichomfanya aondoe hofu mapema ni vile walivyokubaliana na Askofu Ponera. Kwamba awamu hii atakuwa makini. Hivyo imani hii ikamfanya awapimie kwa chati wale askari moyo ukijawa matumaini kuwa wanajisumbua. Hadi ikafikia wakati hakuwatilia maanani.

Pindi amepoteza umaanani kuna gari kadhaa za kijeshi na kiraia zilimpita pale alipoweka tuo pasi na kufahamu. Zote zikichukua uelekeo wa jengo lilipo. Miongoni mwa magari hayo, moja wapo lilikuwa Land cruiser Prado, ndanimwe waliketi Brigedia Jenerali Buyoya, Luteni Bazombanza na Koplo Rumera, ambaye alikamatia usukani, huku mwendo ukiwa wa wastani.

Walivyofikia umbali wa takribani mita tisa kutoka Mandoo alipoegesha gari, Brigedia Jenerali Buyoya alimwamuru Koplo Rumera asitishe mwendo, naye kutii.

“Nina mashaka na ile gari tuliyoipita pale. Gari ya Ubalozi wa Tanzania, inafanya nini usiku wote huu mahali pale?” Brigedia Jenerali Buyoya aliwaondolea fukuto la maswali ambalo angeulizwa kwa nini ameamuru kitu hicho. “Hebu rudi kwanza tukalikague.” Akakazia.

Koplo Rumera alitii amri kwa uharaka. Alirudisha gari nyuma, walivyoifikia, pasi na kuchelea, waliteremka garini na kuanza kuichunguza.

Wakati huo wote walishatawaliwa na mashaka ndani ya nyoyo zao juu ya uwepo wa gari hilo mahali hapo. Moja kwa moja wakalihusisha na tukio litendekalo upande wao.

“Yuleyule mlengwa wetu. Itakuwa amekuja na gari hii,” Luteni Bazombanza alitoa dukuduku lake, huku wakiimulika mulika kutazama ndani ya ile gari kwa kutumia tochi.

Hakukuwa na mtu ndanimwe.

“Hapana,” Brigedia Jenerali Buyoya alichangia. “Kwa mujibu wa maelezo, mlengwa wetu aliletwa na teksi. Hivyo hii ni mahususi kwa usafirishaji mara baada ya kufanikisha atakachokifanya pale kwetu.”

“Kwa hiyo amekuja nayo mtu mwingine tofauti na yule?”

“Ndivyo inavyoonekana.”

“Mmmh!”

“Tusisumbuke,” Brigedia Jenerali Buyoya aliwashauri, “Ninyi bakieni hapa, mimi nitaenda mjengoni kuangalia mazingira.”

“Hamna shida afande.”

Wakati Brigedia Jenerali Buyoya anaondoka, Mandoo ndiyo alikuwa anageuka arudi alipoiacha gari mara baada ya kuhitimisha kumwaga maji machafu nje kidogo ya barabara. Akastaajabu kuona gari yake imewekwa kati akisubiriwa mhusika arejee. Moja kwa moja akahisi watu hao ni wanajeshi, ukizingatia walikuwa wamevaa half combat.

“Bull-shit!” Mandoo alimaka. “Imekuaje? Na wameifikia muda gani gari yangu?” alijiuliza, huku akiwapimia kwa chati.

Ikambidi naye azidi kuwasubiri aone watafanya jambo gani. Ijapokuwa mapigo ya moyo hayakuacha kwenda kasi, wanaenda kuudhalilisha Ubalozi wao.

Luteni Bazombanza na Koplo Rumera nao hawakuonesha dalili za kuondoka kwa haraka mahali pale. Walichojiaminisha wamdhaniaye akitoroka kule, atakimbilia kwenye ile gari, hivyo wao watamdhibiti.

Mandoo kule alipojificha alifanya subira hadi akachoka. Baadaye akaamua kujirudisha mdogomdogo kwa uficho kuelekea gari lilipo. Sasa alishaamua, liwalo, na liwe afanye jambo kuziondoa hatua zenye mashaka nafsini mwake.

Kwa hatua ndogondogo zisizo na mshindo, alivizia kwa kuutafuta upande wa nyuma wa gari. Kwani Luteni Bazombanza na Koplo Rumera walikuwa wamesimama upande wa mbele. Alivyoifikia gari akachutama kwa muda kupunguza umbo. Ilikuwa gari ndogo, aina ya Audi.

Aliweka pozi kwa muda mchache pale kwenye mchutamo, viwambo vya masikio akiwa amevisimamisha vyema angalau anase watakayoyazungumza. Lakini hakukuwa na mazungumzo yoyote baina yao, zaidi ya sauti zilizosikika Redioni zikijumuisha call sign mbalimbali zikitoa mirejeo ya hali ya usalama wa vituo vyao na doria.

Alichukua takribani dakika mbili kwenye ule mchutamo, wakati wote huo akifikiria hila atakayotumia kuwagiliba. Akaipata. Na kufanya utekelezaji pasi na kuifikiria mara mbili. Aligonga kwa nguvu sehemu ya juu ya buti. Luteni Bazombanza na Koplo Rumera wakashtuka. Mshituko uliowageuza kwa pamoja wageuke kuangalia sauti itokeako.

“Unahisi ni kawaida?” Luteni Bazombanza aliuliza, huku akipiga hatua ndogondogo kuelekea kule nyuma.

Mandoo alivyosikia mshindo wa hatua, akatambaa taratibu kuelekea mbele. Alichokihitaji wale watu wasiwe pamoja. Lengo awatenganishe ili apate urahisi wa kukabiliana nao. Hivyo wakawa wanapishana na Luteni Bazombanza. Yeye alipita ubavu wa kulia wa gari, Luteni Bazombanza alipita ubavu wa kushoto.

Alivyokuwa karibu kuufikia upande wa mbele, mchakacho wa utambaaji ukamshtua Koplo Rumera. Akaondoka pale alipokuwa amesimama, na kupiga hatua chache kuchunguza mchakacho huo unasababishwa na nini.

Likawa kosa.

Kwani kabla hajavumbua ni nini, Mandoo alijiinua kwa haraka na kurusha ngumi za chapchap zilizoenda kukita tayani kwa Koplo Rumera na kumgongesha meno. Hali ya usalama mdomoni mwa Koplo Rumera ikabadilika. Ule mgongano wa meno ulimsababishia maumivu makali yaliyomfanya achanganyikiwe.

“Rumera, vipi?” Luteni Bazombanza aliuliza, akiwa amestopisha kuendelea na hatua, akageuka nyuma kuangalia kilichomsibu mwenzie.

Akastaajabu kuona kuna ongezeko la mtu mwingine. “Haaaa!”

Baada ya kuona mitupo ya ngumi aliyofanya imekuwa na manufaa kwake, alipiga hatua za harakaharaka kumsogelea Koplo Rumera ili asipate nafasi ya kujipanga. Alivyomfikia, alimkata shingo na kumtwika pigo la kichwa pajini kisha kushushia ngumi zingine za taya. Koplo Rumera akaula myumbo wa nguvu.

Wakati Koplo Rumera anahangaika kwa kupepesuka, Luteni Bazombanza tayari alishaanza kupiga hatua kurudi atokako. Na alivyomfikia Mandoo, alimvaa vaa kwa kumshika shati usawa wa mbavu kabla hawajapimana uzito kwa kila mmoja kutaka kumrudisha mwenzie nyuma. Kwani Mandoo naye alifanikiwa kukamata sehemu ya mwili wa Luteni Bazombanza.

Msukumano huo ulichukua takribani dakika mbili, baadaye Mandoo akaamua kujilegeza alivyohisi uhatari unaweza kumnyemelea akizidi kuweka kigingi. Alihofia atadhibitiwa na Koplo Rumera. Aliyekuwa anahangaika kujirudi mchezoni. Hivyo alikubali kurudishwa nyuma kwa kasi huku akijaribu kuwazua atakavyojinusuru.

Luteni Bazombanza naye pasi na kutumia maarifa kwa kina, akafurahishwa na kitendo hicho kiasi kwamba alipoteza umakini wa kinga dhidi ya shambulio lolote la dharura. Mandoo akaamua kuiachia mikono yake. Akaiacha ikielea elea kwa muda, baadaye aliivutia kasi na kuivuta kwa nguvu kuipangua ile mikono ya Luteni Bazombanza.

Kwa sababu Luteni Bazombanza hakujiandaa kwa hilo, alishtuka kuona mikono yake ikiondolewa kwenye ukamataji na kupata mpepesuko kuelekea mbele. Alivyotaka kuweka kituo ili ajipange upya, alijikuta akipokea ngumi kadhaa kifuani na iliyopigwa kwa mtindo wa chembe kidevu.

Akapata myumbo ulioenda kumtua chini pasi na mapendo.

Koplo Rumera akachukua nafasi yake, huku akiwa mwenye ghadhibiko lililomshinikiza ajitwalie ubingwa. Luteni Bazombanza naye hakuchukua muda mrefu pale chini. Aliinuka kwa haraka na kwenda kuungana na Koplo Rumera wachangie nguvu kumshinda adui yao.

Kosa ambalo walilifanya ni kujenga mihemko ya kiasi kikubwa pindi wanashambulia. Mandoo akatumia nafasi hiyo kuwachezea shere lililofanya mashambulizi mengi ya wapinzani wao kwenda kapa.

“Hata sik...hata siku moja hamtoweza kuzuia jitihada zetu,” Luteni Bazombanza alisema, akiwa anahema juujuu wakati huo mtupo wa ngumi ya aliyoidhamiria ikatue mbavuni ikizuiwa kwa mkono wa Mandoo.

“Nanyi mkae mtambue,” Mandoo alisema akiwa anarusha ngumi iliyompata Luteni Bazombanza usoni, usawa wa jicho la kushoto. “Tunaenda kuieneza amani ndani ya bara letu.” Akaishindilia ile ngumi. Luteni Bazombanza akayumba na kwenda kumsomba msomba Koplo Rumera.

Wakaanguka chini kwa pamoja.

Kabla hawajajiinua waendeleze pambano, Mandoo alipiga hatua moja ya nguvu kuwafuata pale alipoangukia. Hakuwakawiza, Luteni Bazombanza na Koplo Rumera walipokuwa wanafanya bidii ya kujiinua, alimchapa teke la shingo Koplo Rumera lililowafanya wakumbane kwa mara nyingine na kwenda chini.

Wakagugumia kwa maumivu. Awamu hii mgugumo ukiwa mkali zaidi. Walionekana kuzidiwa na maumivu.

Kwa namna walivyobananishwa nafasi ya kujitetea kwa upande wao ilikuwa ndoto. Hali ya mazingira haikuwaruhusu kufanikisha dhamira yao kwa mapigano ya kutumia viungo vya mwili. Walishazidiwa ujanja.

Matumizi ya manati ya mzungu ndiyo lilikuwa suluhisho kwa upande wao. Na walifanikiwa kuzitoa walipozihifadhi kwa msaada wa hila ya uviringikaji wa sekunde chache walioufanya. Walivyozimiliki vyema mikononi hawakuchelea kuruhusu mitupo ya risasi kumwelekezea Mandoo.

Lakini yeye alikuwa mjanja, kwa kuwahi mapema upande mwingine wa gari na kuchutama. Wakati huo ile kosakosa ya risasi ikimpa jambajamba lililoinua mapigo ya moyo na kumfanya atwete kwa wasiwasi.

“Pourquoi courez-vous?” Luteni Bazombanza aliuliza, akimaanisha kwa nini Mandoo amekimbia.“Enregistrez-le publiquement si vous êtes vraiment l'axe de la hache,” aliendelea kumchamba, akimtaka ajitokeze hadharani kama kweli yeye ni kidume wa shoka. Akafuatia kupiga risasi tairi za usawa ule aliopo. Gari likatitia.

Muda wote huo Mandoo alikuwa palepale alipojificha huku akifuatilia kwa ukaribu mwenendo wa miguu ya wapinzani wake. Kilichomtishisha kwa wakati huo hakuwa na silaha yoyote ambayo inaendana na zile za kina Luteni Bazombanza. Ambayo angeweza kujibiza mapigo pale atakaposhambuliwa.

“Lakini hamna...” Mandoo alijisemeza, na kugeuka nyuma kuangaza angaza mazingira ya karibu yamzungukayo. Kulikuwa na vi-mawe mawe na vi-miti yenye uzito wa wastani.
Akavisogeza karibu yake.

“Lazima niibuke kidedea kwa namna yoyote ile,” Mandoo alijisemeza akiwa amekamatia jiwe, huku akijiinua kidogo kwa kuibia kuwaangalia namna walivyosimama.

Walikuwa katika mkao wa windo. Uliombainisha wanateta namna watakavyomdhibiti.

Na kweli, ilikuwa hivyo.

Luteni Bazombanza alikuwa anampatia maelekezo Koplo Rumera namna gani wajipange kumfikia karibu ili wasije kujipiga wenyewe risasi.

“Utaambaa ambaa na huu uelekeo wa nyuma, kwa namna yoyote akishasikia atajiinua ili atoroke. Akishajiinua tu, mimi nitafanya...” Luteni Bazombanza alisema, kabla hajafika mwisho, kauli ikabaki kuelea baada ya kutua jiwe wajihini kwake.

Akapiga ukunga wa nguvu na kufumba macho. Jiwe lilitua usawa wa jicho la kuume.

Koplo Rumera akashawishika aampe msaada, lakini Luteni Bazombanza akakataa na kumhimiza afanye vile alivyomwambia.

Ilikuwa pindi Koplo Rumera anageuka nyuma aanze kupiga hatua amfuate Mandoo, pale alipojikuta akikumbana na ujiti uliokita wajihini kwa nguvu zaidi ya mara tatu na kumfanya aungane na Luteni Bazombanza kwenye uuguliaji maumivu.

Nguvu ya kuendelea kuishikilia bastola ikamtoka, hatimaye ikamdoka chini na kuleta faraja mtimani mwa Mandoo. Ilikuwa nafasi ya ufanikishaji kwa upande wake. Na aliitumia vyema, kwa kuwapatia kipigo cha nguvu kilichoshinikiza kukatisha fahamu zao kwa muda.

Pindi anahitimisha kumtuliza Koplo Rumera, Luteni Bazombanza akiwa amekumbwa na ile hali kwa muda mrefu, redio ya VHF ikasikika ikiunguruma. Mandoo akatega sikio, asikie kiongelewacho. Ijapokuwa lugha iliyotumika ni kifaransa, lakini aliielewa ile taarifa inahusu nini.

Hakuamini asikiacho, na kumfanya akatwe maini kwa unyong’onyo. Alinyong'onyea, kiasi cha kutaka kuanguka.

ITAENDELEA...
 
AFRIKA YANGU—11
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
MAWASILIANO: 0673056571

KILIKUWA KIKAO CHA DHARURA, asubuhi ya saa tatu ndani ya ofisi ya Fadhy kilichowakutanisha wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama Taifa, kuutafuta mustakabali wa ujumbe aliotumiwa Fadhy usiku wa siku iliyopita. Ujumbe uliotumwa kutoka ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi.

Hali ya hewa mle ukumbini ilitawaliwa na ubaridi. Uliohanikiza nyuso za wengi zikose uchangamfu. Ambao ni; Mkuu wa Majeshi, Jenerali Wilson Nyanda. Inspekta Jenerali wa Jeshi la polisi (IGP) Ally Kisogo. Mkurugenzi Idara ya Usalama wa Taifa, Benson Lau. Maafisa waandamizi wa mafunzo na operesheni kutoka vyombo husika, wakiongozwa na Fadhy. Mwisho, kamanda wa Intellijensia ndani ya jeshi la wananchi, Meja Jenerali Happy Kalachu. Kulikuwa jumla ya watu saba ndani ya ile ofisi. Jenerali Nyanda akikalia kiti cha uongozaji.

“Tuna kibarua cha kutuliza mioyo yetu kwa hii kadhia,” Jenerali Nyanda alifungua mazungumzo baada ya kitambo kidogo cha ukimya tangu walivyoingia mle ofisini na kutakiana hali. “Haipaswi ifahamike, kama Askofu Ponera ni mtoto wetu. Hivyo basi, narudisha hili jambo kwenu, fanyeni namna, mwanetu aokolewe kabla wale wajinga hawajatumia nafasi kutudhorotesha.”

IGP Kisogo aliingilia kati, “Hujakosea afande.” Akatulia kwa muda. Aliwasaili wenzie kisha, akaendelea, “Tusiruhusu kumporomoshea hadhi tuliyomjengea ndani ya jamii yetu. Nami nakazia, haipaswi kabisa kufahamika kama ni silaha yetu ya maangamizi. Ikija kufahamika, tunaweza hata tukawaondolea hadhi watu wetu waliopo ndani ya dini.”

“Nami naungana nanyi,” Lau alichangia hoja. “Cha kushauri, tujidhatiti vilivyo tunaenda kumwokoaje.”

“Kuna taarifa yoyote inayoonesha wapi amehifadhiwa?” Jenerali Nyanda aliingilia.

Fadhy akadakia, “Kwa taarifa za awali, punde baada ya kufahamishwa Chiwa (Askofu Ponera) amekamatwa iliambatana na eneo ambalo alikamatiwa kwa wakati huo. Lakini hiyo hatuwezi kuipa uhakika, kwa sababu wameshabainika. Hivyo wanaweza wakahama. Na ndilo tunalopaswa tulipe uhakika zaidi.

“Sasa nilichokitekeleza kwa haraka, nimezidi kumpa msisitizo kijana wetu wa Ubalozi azidi kufuatilia mienendo hadi afahamu wapi mlengwa wetu atakuwa amehifadhiwa.”

“Nini litakuwa wajibiko kwa kipindi chote hicho kwa huku kwetu?” IGP Kisogo aliuliza. “Maana tunaweza kujipa subira halafu wao wakatumia mwanya huo kufanya kile tusichokihitaji.”

“Hakika kwa hili tupo matatani. Tunatembelea kudra za Mwenyezi Mungu,” Fadhy alijibu. “Hivyo kwa kipindi ambacho tutakuwa tunasubiri taarifa kutoka Burundi, tutakuwa katika uteuzi wa vijana watakaounda timu ya kikosi kazi itakayoenda kufanya uokozi.”

“Kuna watu wowote uliowafikiria kwa harakaharaka watakaoweza kufanikisha hilo?” Jenerali Nyanda aliuliza.

“Ndiyo,” Fadhy alijibu kikakamavu. “Vijana kutoka CAT (Counter Assault Team) na CT & HR (Counter Terrorist and Human Rescuer)”
Wote wakasailiana, wamepokeaje maelezo ya Fadhy.

***

Kilikuwa chumba kikubwa, chenye giza totoro. Giza la kuogofya, kwa mtu mwenye rika lolote lile. Kwani hakukuwa hata na upenyo wa miali ya mwanga kupita na kuakisi mle ndani. Hiyo haikuzuia kumwezesha mtu apataye kuwemo kupumua. Kulikuwa na kaji-nafasi, kilichotengenezwa kwa mtindo wa wavuwavu usawa wa juu karibu na paa.

Kwa muda ule mle ndani alikuwemo Askofu Ponera. Akiwa dhoofu wa hali, hajiwezi kwa lolote. Maumivu yalimtawala karibia mwili mzima, kwani hakuna sehemu aliyoachwa kupigwa mara baada ya kukamatwa. Askofu Ponera, au Luteni Kanali John Chiwa, kama anavyotambulika na makamanda wa ngazi za juu za majeshi nchini alikamatwa na wapiganaji wa Red tabara hata kabla hajalifikia lile jengo.

Wao walivyomkamata wakaenda kumhifadhi sehemu nyingine tofauti na pale palipodhamiriwa na Askofu Ponera kwenda kufanya mambo yake. Walienda kumficha nyumba nyingine, lakini ni maeneo yaleyale ya Buyenzi. Vikosi vya jeshi walivyojaribu kufuatilia, kila sehemu waliambulia unyoya uliowapotezea uelekeo. Hivyo kazi ikawa nyepesi kwa Brigedia Jenerali Buyoya na timu yake kwa ujumla.

Iliwarahisishia walichokihitaji.

Toka alivyoingizwa mle chumbani kwa mara ya kwanza aliushuhudia mwanga alivyopelekewa maji na chakula. Ambavyo katu hakugusa hata kimoja mpaka mlango ulivyofunguliwa kwa mara ya pili. Kukiwa na utofauti wa masaa zaidi ya nane toka ulipofunguliwa hapo awali.

Ijapokuwa haukuwa mwanga toshelezi mle chumbani, lakini uliweza kumpatia faraja kwa kiasi kabla faraja hiyo haijawa dumishi pale ilipowashwa taa. Mwanga wa kutosha ukatamalaki, uliomwezesha angalau ajione mwenye nuru. Baada ya dakika kadhaa, wakaingia watu watatu mle ndani. Alivyowaona tu, akawakumbuka. Ni miongoni mwa wale aliowapiga picha ule usiku, siku ya mwanzo kabisa.

Walikuwa Brigedia Jenerali Buyoya, Wilhelmina na Clement.

Lakini katika hali ya kushangaza, mle chumbani hakuwa Askofu Ponera pekee. Walikuwepo watu wengine. Wawili; jinsia ya kike na kiume.

“Hee! Imekuaje nimekaa pasi na kufahamu kama kuna watu wengine humu ndani? Au wao wameshindwaje kufahamu uwepo wangu?” Askofu Ponera alijiuliza. Wakati huo akiwapiga jicho la udadisi wale watu wengine ambao aliokuwa nao muda wote mle ndani bila kutambua.

Matokeo aliyoyapata kwa tathmini ya harakaharaka ya udadisi wake alifahamu, wale watu ni wahanga kama ilivyokuwa kwake. Kuivilia kwa damu kwenye nguo na majeraha waliyonayo ilimbainishia hilo. Hawakuwa na afya iliyoimarika. Kiasi kwamba hawakuonyesha kutingishika kwa lolote juu ya ugeni ulioingia.

“Kuna lolote ulilofikiria kuliratibu?” Wilhelmina aliuliza. Muda wote akiangazia mboni zake kwa Askofu Ponera na wale wahanga wengine.

“Kuwahamisha hapa,” Brigedia Jenerali alijibu. “Nahitaji niwapeleke eneo la mbali ambalo hakuna mtu yeyote afuatiliaye nyendo zetu ataweza kulibaini,” alikazia.

“Wapi?” Clement alidakia.

“Nitaongea na Kinigi. Atutafutie eneo zuri. Eneo mujarabu pande zile za hifadhi ya msitu wa Nyungwe kule Rwanda.”

Ukapita ukimya mfupi, ulioonekana kuwatafakarisha Wilhelmina na Clement kuhusu lile jibu. Baadaye Wilhelmina aliufukuza, “Na vipi kuhusu serikali ya Tanzania?”

Brigedia Jenerali Buyoya alitabasamu kwanza. Akamwangalia Askofu Ponera kwa jicho kali, wakajikuta wanatazamana. Baadaye aligeuza mboni kuwaangalia wenzie. “Watasaga meno.”

Wilhelmina na Clement wakatabasamu.

Brigedia Jenerali Buyoya akaendelea kujitwalia hatamu ya ufafanuzi, “Nimepanga niwavumbulie huu uchafu wao. Jamii ya ki-Tanzania ielewe, viongozi wao wa kidini ni vibaraka wa serikali iliyopo madarakani.”

“Una uhakika jamii itashtuka?” Clement aliuliza.

“Sio jamii tu, ulimwengu kwa ujumla. Kiasi kwamba hata makao makuu ya dhehebu washangae na kujilaumu kuwapa wadhfa watu wasioeleweka.”

Wakaangua kicheko.

“Ni uratibu mzuri. Kikubwa, haya mambo yafanyike kwa uharaka,” Wilhelmina alishauri.

“Msihofu.”

Walivyohitimisha majadiliano ndiyo ukawa mwisho wa uwepo wao mle chumbani. Walizima taa na kuondoka. Huku wakiwaacha mateka wao katika hali ya hofu zaidi. Nini kitawapata huko watakakopelekwa?

Sambamba na hilo Askofu Ponera alikuwa na mshawasha wa kuwafahamu wale wahanga wengine. Ambao alijiaminisha wanaweza kuwa ni baba na mwana. Au, Richard Mugaza na Ndinaa. Lakini imani hii ilitoweka kwa haraka alivyopata kumbikizi awafikiriao wapo nchini Tanzania.

Kadri sekunde zilivyozidi kusonga mbele ndivyo mshawasha ulivyomwenea nafsini mwake. Liwalo na liwe, baadaye akaamua kuwasogelea, kwa mtambao.

Alivyowafikia, ikaibuka shauku nyingine, ya kutaka kuwasikia. Na wala hakuchelea, kuuhangaisha mdomo kuzungumza. Lakini kabla sauti haijamtoka, akapata kumbukizi nyingine. Mle walipo hakikosekani kitu kinachofuatilia nyendo zao. Hisia za harakaharaka zikamgotesha kwenye kinasa sauti. Kwa namna yoyote hakikosekani. Na kama kipo, atafanyaje kupata undani wa wale watu?

Hisia hii ikamkerehesha nafsi. Na kumfanya awazue kwa muda wa dakika kadhaa kabla hajakata shauri. Kwamba hata wakisia, poa tu!
“Je suis appelé ponera. Je peux savoir qui sont mes collègues?” Askofu Ponera alijitambulisha, na kuomba kama anaweza kuwafahamu wale watu ni kina nani.

Wale wahanga hawakujihangaisha kujibu. Kitendo kilichozalisha ukimya kwa sekunde kadhaa na hatamu ya uwazaji kwa Askofu Ponera awashawishi vipi wapate kukubaliana naye.

“C'est une bonne personne pour vous. Alors ne m'achetez pas,” Askofu Ponera alizidi kuwabembeleza. Awamu hii alitaka wasimhofie, kwa kuwa ni mtu mwema kwao. “Natokea Tanzania.” Alikazia.

Kidogo hili bembelezo liliwashawishi wale watu. Kwani lilimwibua yule mwenye jinsia ya kike, binti na kujenga ushirikiano wa maongezi.

“Je suis Ndinaa. Ici, il s'appelle Mugaza,” alisema yule binti. Akimaanisha yeye anaitwa Ndinaa. Na yule mwingine, mwenye jinsia ya kiume ni Mugaza.”

Askofu Ponera akashtuka. Moyo ukapiga kite kwa hofu. Wanavyo vile walivyokabidhiwa? Au vipo mikononi mwa watesi wao? Mshituko alioupata ulimpelekea hadi ahisi kijasho chepesi kinamtiririka.

“Imekuaje hadi mkakamatwa?” Askofu Ponera aliuliza, wakati huo ki-hasira kikimtukuta.

Mugaza akaingilia kati, “Kwani unatufahamu?”

Askofu Ponera hakujibu kwa haraka. Alifikiria kwanza, alipopata suluhisho ndipo alijibu, “Ndiyo. Nafahamu mengi kuhusu ninyi. Hivyo msisite kunieleza kwa sababu nipo kwa ajili ya kurejesha utulivu na usalama wa Burundi.”

“Nchi yetu imelaaniwa,” Ndinaa alidakia. Kwani tulikuwa na matumaini mengi yenye faraja dhidi ya serikali iliyopo madarakani lakini matokeo yake ni tofauti. Matokeo tuliyo, na tunayo-kumbana nayo kutoka kwa waandamizi wa Rais yamekuwa ya kifedhuli. Hayaishi kutunyanyasa, na kutuachia makovu yasiyomithilika.

“Awali tuliamini, serikali hii itatufuta machozi, na kutukaushia majeraha yetu, lakini imekuwa tofauti. Mpaka sasa tumekosa mfuta machozi. Na Afrika yote imekaa kimya, hakuna hata mmoja aliyejaribu kunyoosha kidole kukemea, na kulaani yaendeleayo. Sitaki kuamini.

“Sitaki kuamini Afrika yangu imekosa mfuta machozi!” Ndinaa alilalama. Sauti ikiwa nyongefu, hadi akamwambukiza Askofu Ponera.

ITAENDELEA...
 
AFRIKA YANGU—12
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
MAWASILIANO: 0673056571

ULIKUWA MCHANA WA JUA KALI, Mkuu wa Majeshi, Jenerali Nyanda, Mkurugenzi Idara ya usalama wa Taifa, Benson Lau na Fadhy walivyojumuika pamoja juu ya jukwaa kwenye uwanja wa mazoezi ndani ya Chuo cha Usalama wa Taifa, Mbweni. Wakati wote mboni zao walikuwa wamezielekezea chini ya uwanja kushuhudia vijana wanne waliokuwa wanakesha kutimua vumbi kwa mazoezi.

Yalikuwa mazoezi yaliyobeba ukali, uhitajika wa nguvu na matumizi ya akili kwa kiasi kikubwa. Kwani yalihusisha matumizi ya risasi na zana mbalimbali za kimapigano ya ki-vita. Wahusika wa mazoezi hayo walikuwa vijana wanne; watatu wa kiume, mmoja wa kike. Ambao ni Luteni Enos Ringo, aliyepambwa kwa umbo refu, mnene wastani, mweusi. Koplo Frederka Tarimo, yeye ni mrefu-kimo cha kati, mwembamba, mweupe. Private (PTE) Shaban Bayo, mfupi, mnene wastani, mweusi. Na Private (PTE) Mussa Pemba, mrefu, mwembamba, mweupe.

“Hawa ndiyo vijana niliowaandaa. Ni vijana makini, walio na weledi toshelevu katika nyanja za kimapigano. Nawakubali, nawaaminia, kiasi cha kujisikia fahari na hakika watakachoenda kukifanya hakitosita kutufurahisha kama nchi,” Fadhy aliwaeleza.

“Tunachohitaji ni ushindi. Wasisitizie hilo. Wasije kutuangusha, sote matumaini yetu yapo kwao,” Jenerali Nyanda alichangia hoja.

“Niwaondoe hofu kwa niaba yao, huu ni muunganiko wa washambuliaji hatari kutoka kwenye zile timu tulizokubaliana. Wawili wanatoka CAT, na hao wengine wanatoka CT&HR.”

“Waambie wafanye kweli, imani yetu isitetereke,” Jenerali Nyanda alikazia.

***

Mwili ulilowana kwa damu, wajihi ukamwonesha namna alivyozidiwa kwa maumivu na matokeo ya kipigo alichokipata dakika chache zilizopita. Alikuwa hajiwezi kwa lolote, kwani hata angalia yake haikuwa ya usahihi na ilionekana upeo wa mboni zake sio mbali. Macho hayakufunguka inavyotakikana. Na muda mwingi alikuwa wa kupepesa pepesa na kufumba.

Yale yote yalitokea kwenye chumba chenye ukubwa wa wastani, uliotamalaki vitu vingi vihusikavyo na utesi pekee. Kilikuwa chumba cha mateso, na ndimo Askofu Ponera alifikishwa punde tu walivyowasili eneo lao kusudiwa. Alivyowasilishwa hawakumpooza, walimpitisha moja kwa moja hadi chumba cha mateso kisha Brigedia Jenerali Buyoya na Meja Uwizeye wakachukua mamlaka ya kumsulubisha. Alisulubishwa huku akichukuliwa picha ya video.

“Bazombanza chukua nafasi,” Brigedia Jerenali Buyoya alisema, akiwa anautua mjeledi mezani. Aliokuwa anautumia kumshushia kipigo Askofu Ponera.

“Leo lazima uungame. La sivyo kifo chako kitakuwa cha uzalilishaji,” Luteni Bazombanza alijigamba pindi akichukua zana tendaji ya kusulubia. Aliuchukua uleule mjeledi uliokuwa unatumiwa na Brigedia Jenerali Buyoya. Alivyoumiliki vyema mkononi, alipiga hatua kadhaa hadi pale alipoketishwa Askofu Ponera.

Alifungwa kwenye kiti.

“Askofu, tunataka uhakika, kwa sababu tayari tumeshafahamu, serikali ya Tanzania ndiyo imekutuma ufanye haya?” Luteni Bazombanza aliuliza. Mboni amezitoa kama mdeni kwa mdaiwa.

Askofu Ponera hakujibu. Badala yake alitingisha kichwa ki-uvivu ishara ya kukataa. Kile kitendo cha kutotoa sauti, ikawa kama dharau kwa Luteni Bazombanza. Hakufurahika nalo, kiasi cha kuchipua na kusambaza ghadhibiko kwa kasi lililomshurutisha autumikishe ule mjeledi mwilini kwa Askofu Ponera pasi na kuangalia unatua wapi.

Askofu Ponera akagugumia kwa maumivu. Lakini hiyo haikuwa sababu iliyomshawishi Luteni Bazombanza asitishe kumpiga.

“Utaeleza ukweli? Eeh! Utatuambia kile tunachokitaka?” Luteni Bazombanza aliuliza akiwa amemwinamia kidogo huku akimtupia mboni kali za utisho.

“Niueni tu. Niuuu... Niueni tu,” Askofu Ponera alilalama kwa sauti ya unyonge.

“Na tutakuua kweli usipotueleza ukweli,” Meja Uwizeye alidakia.

“Mimi sina ukweli mnaoutaka. Sijui chochote kuhusu serikali ya Tanzania juu ya mambo yenu.”

“Sasa kwa nini ulikuwa unafuatilia nyendo zetu? Au umetumwa na viongozi wenye mamlaka ya juu ndani ya serikali ya Burundi?” Liteni Bazombanza aliuliza kwa mara nyingine.

Askofu Ponera akatingisha kichwa ishara ya kukubali.

“Pumbavuuu, Nyama ya mbavu!” Brigedia Jenerali Buyoya alifoka na kutua teke la nguvu kichwani kwa Askofu Ponera usawa wa sikio. “Unatuongopea sisi unadhani ni watoto wadogo?”

Mshindo wa teke ulimteteresha kwa kiasi kikubwa Askofu Ponera. Kwani lilikuwa teke la nguvu, ukizingatia Brigedia Jenerali Buyoya alivaa buti mguuni. Yenye makisio ya nusu kilo. Koplo Rumera akamrejesha kwenye ukawaida.

“Sasa sikia,” Brigedia Jenerali Buyoya aliiteka nafasi ya kuzungumza. “Kupitia wewe, tunaenda kumdhalilisha mtawala wa Burundi. Na tunaenda kuidhalilisha Tanzania utokako ili ikome kufuatilia mambo yasiyowahusu.” Akatulia kwa muda mfupi, wakati huo Askofu Ponera ametega viwambo vyake kwa umakini ijapokuwa maumivu yalimtatizisha. Brigedia Jenerali Buyoya akaendelea, “Iandaeni vizuri hiyo video, kisha tutaratibu siku ya kuisambaza mitandaoni kabla barua za kuomba ridhaa ya kuwarudisha wakimbizi haijapokelewa.”

“Sawa kamanda,” vijana walitii.

***

Mlango uligongwa kwa nguvu, kabla idhini haijatoka kwa mgongewa, ulifunguliwa na mgongaji kuingia ndani. Alikuwa binti wa makamo, akadiriaye miaka ishirini, akiwa kwenye mwonekano nadhifu wa kaunda suti rangi nyeusi.

“Huogopi kuingia bila idhini?” mgongewa aliuliza, Fadhy.

“Nilihisi utanikawiza, na ukizingatia nina ujumbe wa muhimu mno,” yule binti alijibu. Akiwa amepambwa kwa mwonekano mujarabu kabisa wenye kujaza mate. Alikuwa mrefu-kimo cha kati, mnene kiasi, mweupe. Kikubwa kilichokongesha watu wengi nyoyo, hasa wanaume, kuchomoza kwa ibio la kishundu.

Hakika, alistahili sifa. Mashaallah! Kwa kubarikiwa.

“Kutoka wapi?”

“Ofisi ya Ubalozi Burundi.”

Neno Burundi lilimwinua kwa haraka alipokuwa ameketi na kufanya mapokezi ya mzigo alioletewa. Ilikuwa karatasi rangi nyeupe, yenye ukubwa wa A4 ikiwa na maandishi machache.

Alivyokabidhiwa aliketi na kuzihimiza mboni kusafiri kwa haraka hadi kwenye yale maandishi. Yalisomeka,’Kitabi, Rwanda.’ Hakuyaelewa kwa haraka, kiasi kwamba alichukua takribani dakika mbili kuyasoma kwa mara nyingine na kuyafikiria.

Hata kabla hajafikia umfumbuzi, mlango ulifunguliwa tena. Akainingia yuleyule binti. Kwani awali alivyompatia ile karatasi aliondoka.

Awamu hii aliingia akiwa amekamatia karatasi pia, yenye muundo sawa na ile ya kwanza. Akamkabidhi Fadhy, kisha aliondoka.

“Ndiko alipohifadhiwa mlengwa wetu,” Yalisomeka maandishi yaliyopo kwenye karatasi ya pili. Hapo akapata ahueni ya utambuzi, kuwa Askofu Ponera amehifadhiwa Kitabi, nchini Rwanda.

Ilikuwa taarifa iliyoleta faraja. Na kumfanya awataarifu wakuu kwa uharaka ulioibua makutano.

Walikutana masaa mawili baadaye, palepale ofisini kwa Fadhy.

Kabla majadiliano hayajaanza, faili litumikalo kuhifadhi habari zihusuzo hiyo operesheni lilipitishwa kwa kila mmoja aangazie taarifa zote zilizokwishawahi kutumwa tangu mwanzo. Wote walivyomaliza, Fadhy akachukua hatamu ya ufafanuzi.

“Hizo ndizo taarifa zote za operesheni yetu kutoka Burundi. Ni chache, lakini zina usadifu wa mafanikio kwa kiasi kikubwa. Kabla Luteni Kanali John Chiwa (Askofu Ponera) hajakamatwa, alishapiga hatua kubwa mno ambayo ina uwezo wa kutuonyesha njia ya kufikia mafanikio.

“Kwanza, ni picha ya hao watu. Hao watu, ndiyo walengwa wa kiendeleacho Burundi. Ndiyo watu wasiohitaji nia ya Mhe. Rais Nibizi ikamilike. Baadhi ni makamanda wa jeshi, wengine, nadhani ni maafisa kutoka mashirika au idara fulani, aidha za ki-serikali, au zisizo za kiserikali,” akatulia kwa muda na kuwasaili wapokeaji wa maelezo yake.

Walikuwa wametulia, tuli.

Fadhy akaendelea, “Hayo majina mawili; ni watu wanaowindwa kwa udi na uvumba na hao waonekanao pichani. Mmoja, ambayo ni huyo Mugaza, ni afisa wa Usalama kule Burundi. Huyu mwingine sijapata undani wake. Lakini wote kwa pamoja wanaonekana kuwa ni mwiba.

“Hivyo basi, endapo tutafanikiwa kumwokoa Luteni Kanali John Chiwa salama, tutakuwa tumehitimisha jukumu letu la kupata undani wa taarifa za hawa wahusika. Na tukishapata undani huo, ndipo hatua za kuwaweka hatiani zitafuata. Naomba kuwasilisha kwenu kwa hatua zaidi.”

Akapongezwa kwa kupigiwa makofi kwa dakika chache, kisha Jenerali Nyanda akachukua nafasi.

“Nataka nizungumze kwa niaba ya wengine ili tusikawize haya mambo, peleka vijana. Vijana waende huko kitabi leo hii, na wakafanye kweli. Natoa muda, hadi panapo kesho asubuhi, wawe wameshakamilisha zoezi na kurejea nyumbani wakiwa na ushindi,” Jenerali Nyanda alichangia hoja.
“Hilo halina shaka,” Fadhy aliafiki.

***

Daima hakuacha kushurutishwa na ndoto aliyoijenga akilini mwake. Kuifanya Burundi kuwa kisiwa cha amani. Hili lilikuwa hitajio lake kwa muda mrefu tangu alivyoanza harakati za ki-siasa. Na kamwe, halikuwahi kumtoka. Kiasi kwamba mara kwa mara katika pilikapilika za kampeni miaka ya nyuma kabla hajautwaa urais, apatapo wasaa hakuacha kuzungumza hitajio hilo.

Juu ya malengo hayo mazuri lakini wananchi hawakumwelewa kiasi cha kumpatia mamlaka ya kuliongoza Taifa. Awamu nyingi alizogombea urais alipigwa chini. Ijapokuwa hakuwa na uhakika kama anaangushwa kiuhalali. Kukosekana sehemu yenye nguvu ya kupinga matokeo ikamfanya abaki kuugulia hisio lake moyoni.

Alifanikiwa kujitwalia kiti baada ya kupita awamu tatu toka alivyoanza kugombea. Na mara baada ya kuapishwa tu, akausisitizia mkakati wake wa kuifanya Burundi kuwa kisiwa cha amani kwa kuwarejesha wana-Burundi wote waliopo ukimbizini.

Cha kushangaza, wiki mbili baada ya kutangaza nia hiyo, lilijitokeza kundi la Red Tabara na kuanzisha machafuko yaliyopelekea kifo cha Jenerali Ndiyashena, na Richard Mugaza kukimbia kiti chake. Hiyo haikuwa ishara nzuri. Na aliigundua mapema, lakini kila alivyojitahidi kuwashirikiasha waandamizi wa serikali matokeo tarajiwa hayakuwa yale anayoyatamani.

Baadaye ikamlazimu kwenda kuomba msaada kwa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ili aitulize mioyo ya wengi iliyojaa masikitiko. Ombi likakubaliwa. Imani ikamjaa, wananchi wataendelea kumwaini. Tatizo likaja kwa kutopata mrejesho wa hatua zilizofikiwa kwenye msaada huo. Alitamani aachie ngazi. Lakini uvumilivu uliojengwa na mafunzo ya kijeshi kipindi cha nyuma ukamfanya avute subira.

“Hivi nitakiona kweli nikitarajiacho?” Rais Nibizi alijiuliza akiwa anaangalia habari za matukio mbalimbali ya machufuko yaendeleayo runingani.

“Kukiendelea kuwa hivi wale tuliowaandikia barua hawatoridhia kutukubalia,” aliendelea kujisemeza. “Na walikuwa wanahitaji hili. Wale watu wasirejee. Kwa nini lakini? Ilhali vikao vingi vya kimataifa vinahubiri amani kila uchao?”

Nafsi ilimuuma. Namna watu wengi wanavyoyaacha makazi yao na kwenda sehemu ambayo hawana uhakika nayo na maisha. Aliumia, kiasi cha chozi kumdondoka na kulifuta kwa haraka. Akafuatia kuizima ile runinga na kuinuka.

Hatua chache kutoka alipokuwa ameketi alisimama mkewe. Muda wote mboni kwa mumewe, huku akiwa amejawa huruma kumskitikia namna anavyonyanyasika na maamuzi ya watu wachache wenye nguvu wasiowatakia mema wananchi na taifa lao kwa ujumla.

Hivyo pindi Rais Nibizi anatokwa na chozi, naye aliguswa na ile hali. Moyo ukapiga kite kwa unyonge uliomsambaa kwa haraka na kumshinikiza naye aungane na mumewe kwenye udondoshaji wa machozi. Baadaye alimkimbilia pale aliposimama na kumkumbatia.

“Pole sana,” mke wa Rais Nibizi alisema, akiwa bado amemkumbatia, huku kiwango cha machozi kikiongezeka. “Ipo siku Mwenyezi Mungu atasimama kwenye hitajio lako. Ipo siku Mwenyezi Mungu hatokuangusha, atasimama nawe bega kwa bega na kuwaumbua wapinzani wako.”

Rais Nibizi alimtoa mkewe kutoka kumbationi na kumsimamisha vyema mbele yake.

“Uongozi jalala mke wangu. Lakini nataka nikutoe hofu, haya yataisha muda mfupi ujao.”

“Yataishaje ishaje? Wakati wenzio hawakuungi mkono?”

“Niamini. Wana muda mchache sana, baada ya hapo tutawatia nguvuni,” Rais Nibizi alimhakikishia mkewe, ijapokuwa nafsini kwake alifahamu azungumzacho hakina uhakika.

Lengo amtulize tu. Na kama kuumia, aumie yeye aliyeapa na sio kuiambukiza familia.

ITAENDELEA...
 
AFRIKA YANGU—13
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
MAWASILIANO: 0673056571

NI USIKU WA GIZA TOTORO. Usiku uliojaa hofu kwa wenye mioyo miepesi, pindi helikopta ya jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) ilivyokuwa inaacha anga taratibu na kutafuta uelekeo uliokusudiwa. Ndani ya helikopta mlikuwa na watu sita; marubani wawili, wengine ni wale vijana kutoka timu za CAT na CT&HR walioteuliwa kwenda kufanya uokozi wa Askofu Ponera.

Kwa mwonekano usiku ule wale vijana walikuwa ndani ya mavazi ya kijeshi, kombati. Pembeni yao kukiwa na mapeki ya kijeshi yaliyo na ujazo wa kutosha wa mavazi na zana zingine za kimapigano. Juu ya hilo wote walipakata bunduki mapajani, ukiachilia mbali bastola walizozihifadhi kwenye hostler zilizofungwa mapajani.

Haukuwa mwendo mdogo. Iliwachukua masaa kadhaa, yaliyozalisha mengi ambayo hayakutarajiwa. Kwani muda wote wa safari ni simulizi chache tu ndizo zilichukua nafasi. Muda mwingi ukimya ulitawala, huku asilimia kubwa wakiwa wamezama mawazoni yaliyowapeleka mbali kifikra. Kuna muda usingizi uliwapitia, lakini walivyokaribia eneo pasa waliamshwa. Wakajiweka sawa, mara baada ya hapo idhini ya uteremkaji ilifuatia. Idhini ilitoka kwa kiongozi wa timu (Team Leader) Luteni Enos Ringo.

Tukio hilo lilifanyika katikati ya msitu mkubwa, umbali wa takribani mita mia sita kutoka eneo wanalopaswa kulifikia. Kitabi.

Kamba maalum ikateremshwa kwa pande zote kisha taratibu vijana wakaanza kuteremka. Waliteremka wakiwa wameshajikoki. Vifaa vilivyopaswa kuvaliwa, vilivaliwa. Na vile vya kubebwa vikabebwa.

“Tunawatakia kila lenye heri,” mmoja wa wale marubani alisema.

“Amina,” vijana wa kikosi kazi waliitikia kwa pamoja. Baadaye ziliteremshwa kamba watakazotumia kuteremkia. Muda wote huo, helikopta ilikuwa imeganda angani.

Taratibu, pasi na papara, wakiwa wameshabeba mizigo yao vyema kabisa, mmojammoja alikamata kamba na kusererekea chini. Zoezi hilo lilichukua takribani dakika tatu kuhitimika. Walivyotua ardhini, mmoja wa marubani alizivuta zile kamba kisha helikopta ikachapa mwendo.

“Wote tupo vyema?” Luteni Ringo aliuliza, huku akijikagua kagua.

“Tupo shwari. Tupo timamu kwa kazi,” wenzie walijibu kwa pamoja.

“Basi haina kupoteza mu
da, uelekeo wetu ni huu,” Luteni Ringo aliwaelekeza kwa kuwaonyeshea mkono kule watakako kuelekea.

Hawakuchelea, Luteni Ringo alivyoteremsha tu mkono safari ikaanza. Pte Mussa Pemba ndiyo aliongoza timu. Mtu aliyekuwa na dira ya uelekeo wa safari yao. Alionekana imara hasa, kwa hatua kakamavu alizokuwa anapiga na namna alivyokamatia bunduki yake, AS 50. Ambayo ilibebwa na wote katika timu.

Kwa ujumla wote walikuwa kikamanda hasa. Kuanzia nyanja ya mawasiliano; kila mmoja alikuwa na redio-VHF iliyochomekwa earpiece kuwezesha mazungumzo yao kutosikika. Vilevile walivaa ballistic vest na ballistic helment kwa matumizi ya kuwa kinga dhidi ya mashambulizi ya adui. Pasi na kusahau tochi za kijasusi.

Mtu ambayo alibeba kitu cha ziada ni Pte Shaban Bayo. Kwenye peki alilolivaa mgongoni alihifadhi mtambo wa kuwezesha redio zipate uwezo wa kufanya mawasiliano. Sehemu ya mkonga wa ule mtambo ukawa umechomozewa kwa juu.

“Pana umbali gani kutoka hapa tufikie eneo husika?” Koplo Frederka aliuliza, taratibu wakizidi kuchanja mbuga, huku baadhi ya sehemu wakitumia kurunzi kuwasha iwaongoze kupita kwenye msitu huo salama.

“Mita mia tatu afande,” Pte Pemba alijibu.

“Oooh! Tumekaribia karibia.”

“Tutapafikia muda mfupi ujao. Kikubwa, kila mmoja aandae mwili na akili tayari kwa makabiliano,” Luteni Ringo aliwaasa.

***

Mshindo wa muungurumo wa helikopta uliosikika ukivuma sehemu moja uliwashtua wapiganaji wa Red Tabara waliopo zamu ya ulinzi kwenye lile jengo alilohifadhiwa Askofu Ponera. Ambalo lilikuwa kilomita kadhaa kutoka mkabala na kituo cha afya Kitabi. Lilijengwa katikati ya msitu wa wastani. Mshituko walioupata ukawajaza hofu iliyowahimiza kuchakarisha akili yao iwazue sababu ya tukio hilo.

“Hii sio kawaida aisee,” mmoja kati ya vijana wawili waliopo kwenye banda la ulinzi lililojengwa juu alimtaarifu mwenzie. “Au mwenzangu hujahisi kitu?” akamalizia kwa ulizo.

Yule muulizwa badala ya kujibu, alivuta darubini na kuangazia kule sauti isikikako. Ijapokuwa kulikuwa na giza, lakini alijitahidi kuhimiza mboni zake zishinde hali hiyo na kufanikiwa kuona baadhi ya vitu. Kwanza; taa nyekundu, iliyokuwa inawaka kila baada ya sekunde kadhaa na kuzima. Baadaye alishuhudia sehemu ndogo ya umbo lile la helikopta.

“Ni helikopta,” yule kijana mwingine alimhakikishia mwenzie pindi akiitua darubini. “Sasa sijui kwa nini imesimama pale msituni.”

“Hujaona pilikapilika za watu?”

“Sijaziona. Yumkini nimechelewa, au nimeharaka kuondoa darubini.”

“Angalia tena.”

Hakupingana naye, alivuta darubini kwa mara nyingine na kuitua usawa wa macho.

Isivyo bahati, awamu hii aliishuhudia ikijiondoa. Lakini lipo jema alilolibaini. Andiko la TANZANIA AIR FORCE kwenye moja ya kuta sehemu ya ile helikopta, usawa wa tail boom. Aina ya H 225.

“Helikopta ya jeshi la Tanzania.”

“Tutoe taarifa kwa wakuu. Kuna jambo lazima litakuwa limefanyika hapo sio bure.”

Dakika mbili baadaye waliwashirikisha wenzie ile hofu hadi ikafika ngazi za juu. Uzuri, jopo lote la viongozi lilikuwa jirani. Hivyo walivyofikishiwa tu taarifa, wakakutana kwa haraka.

“Sina haja ya kurudia kile tulichojuzwa,” Brigedia Jenerali Buyoya alisema. “Nahitaji mwongoze vijana sasa hivi kuelekea kule tukio lilipotokea. Naomba mkalizunguke hilo eneo usiku kucha hadi mpate kufahamu hiyo helikopta ilisimama kwa minajili ipi.”

“Hamna shida kamanda,” Meja Uwizeye aliitikia.

“Mbuzi yeyote mtakayokutana nayo msisite kumchukulia hatua katika kupata chochote kitu kitakachotusaidia,” Brigedia Jenerali Buyoya alikazia.

“Imeisha hiyo,” Luteni Bazombanza alijigamba.
Vijana wakajaa ari.

Mwisho wa mazungumzo hayo utekelezaji ulianza. Meja Uwizeye, Luteni Bazombanza na Koplo Rumera waliongoza timu ya vijana kadhaa-kila mmoja akiwa na bunduki ya kivita, Ak 47. Walivyoingia ndani ya magari madereva wakakanyaga moto wa kutosha wawahi kuwasili eneo husika.

Walipowasili karibu na kituo cha afya Kitabi madereva waliegesha gari kando ya barabara, kisha vijana wakachumpa kuingia mwituni. Kila kundi na uelekeo wao.

“Kwa lolote linalohitaji ushirikiano, tusisite kutoa ishara ya anga,” Meja Uwizeye aliwaasa, pindi wakichukua uelekeo.

“Imeisha hiyoooo,” vijana waliitikia kwa morali ya juu.

***

Miali ya mwanga itokayo kwenye kurunzi iliwashtua vijana walioambatana na Meja Uwizeye. Wakafahamu, mbele yao, kule waelekeako kuna watu wanakuja wakielekea watokako. Kitendo cha kuwasha na muda mwingine kuzima, kikawavumbua wahusika wafanyao hivyo sio wema. Wangelikuwa wema wasingesita kuacha mwanga uendelee kuwaongoza kutokana na giza lililotamalaki.

“Kama wanapita usawa huuhuu tuliopo haina haja ya kuzidi kuwasogelea, tutawashtua.” Meja Uwizeye aliwashauri, wakiwa wamepiga tuo. Ushauri ulioafikiwa kwa wote.

“Hivyo tutajigawa ili tuhakikishe jamaa wanapita katikati yetu. Wawe wahusika, wasiwe wahusika, yatupasa tuwaweke himayani,” Meja Uwizeye aliendelea kuwapatia utaratibu. Awamu hii aliongeza mkazo kidogo katika uzungumzaji.

Hawakuchelea, muda huohuo walijitawanya mboni wamezielekeza kule miali itokeako. Ilizidi kuwakaribia. Nao wakajipa utulivu uliosisimua mioyo yao iliyopo mbeleni sio ya kuwatoa jasho. Dakika tano baadaye wakaanza kusikia michakacho ya hatua, sambamba na sauti za maongezi kutoka kwa wale wasubiriwa wao.

Sauti zilizochanganyikana; baadhi walikuwa wanaimba, wengine wakiteta habari mbalimbali zilizowapa ujasiri. Kupitia lafudhi wakafahamu, pasi na shaka yoyote wakusudiwa wao ni wenyeji wa Tanzania. Walijithibitishia kutokana na ufasaha wa utamkaji wa lugha.

Meja Uwizeye akatuma taarifa kwa wenzie, “Tumewaona huku. Hivyo ambaeni kwa uharaka tulipotuwadhibiti kwa urahisi.”

“Hamna shida kamanda,” Luteni Bazombanza alijibu.

Ilikuwa vivyo hivyo kwa Koplo Rumera. Na kufanya waache mienendo ya uelekeo wao, waelekee Meja Uwizeye alipo.

Wakati Luteni Bazombanza na Koplo Rumera wanaongoza vijana kumfuata Meja Uwizeye, kwa upande wa Meja Uwizeye aliwasihi vijana wao wawaache wakusudiwa wapite kidogo ili wawavamie kwa nyuma. Na ikawa hivyo. Walivyoachwa umbali wa takribani mita nne, Meja Uwizeye alitoa amri kwa kupiga mbinja kisha vijana wakajichomoza kwa haraka mafichoni, mitutu ya bunduki ikielekezwa kwa wakusudiwa.

Na kwa utisho wa kwanza, walikoki bunduki zao pindi wanazitua kwenye nyama ya bega. Kabla hilo halijapoa, mmoja wao aliruhusu mtupo wa risasi mbili hewani.

Kikawa kimbembe kwa wale watu waliowalenga. Kikosi kazi, kilichotumwa kwenda kufanya uokoaji wa Askofu Ponera.

Hawakutarajia kama watabainika kiurahisi namna hiyo. Hata walivyojiuliza imekuaje wabainike? Hawakupata jibu la moja kwa moja lenye mafanikio.

Walivyojirudi ili wajipange kukabiliana na utisho, walistaajabu kuna watu wengine watokeako kule walikopangwa kueleakea. Wakajikuta wamewekwa kati.

“Jisalimisheni,” Meja Uwizeya aliamuru.

“Tunafanyaje hapa?” Koplo Frederka aliuliza, wakiwa wamejikumbata pamoja kwa kugusanishana migongo.

“Hatujaja huku kufeli,” Luteni Ringo alijibu. “Lazima tushinde kwa namna yoyote ile hata kama tutakutana na kizuizi ambacho hakipo kwenye njia ya misheni yetu.” Alizidi kuwapa hamasa.

Lakini katika hali wasiyoitarajia kwa mara nyingine, walijikuta wakimulikwa na miali ya mwanga kutoka kwenye kurunzi za kina Meja Uwizeye. Lile kundi litokalo mbele, liongozwalo na Luteni Bazombanza na Koplo Rumera likaweka kituo hatua chache toka wao waliposimama.

Meja Uwizeye alipaza sauti kwa mara nyingine, “Narudia kwa mara ya mwisho, wekeni silaha chini mjisalimishe.”

Luteni Ringo na wenzie wakaendelea kuwa wakaidi. Kwani hawakujishughulisha kwa lolote ambalo liliendana na amri wapatiwazo. Jambo lililokerehesha nafsi za wengi upande wa wapinzani wao.

“Kwa hiyo tunafanyaje?” Pte Bayo aliuliza.

“Tutawatoroka kupitia upande ambao hawajaudhibiti,” Luteni Ringo alijibu.

“Una uhakika tutafanikiwa kabla hawajatushambulia?” Koplo Frederka aliuliza. Maongezi yote yalikuwa katika mfumo wa unong'ozi.

“Ingelikuwa kutushambulia, wangelitushambulia toka awali. Wanahitaji watukamate tukiwa wazima.”

“Basi tuwagereshe kama tunatii matakwa yao kisha tuchukue hatua,” Koplo Frederka alishauri.

Kweli.

Walifanya hivyo. Walivua bunduki, kisha taratibu walijielekeza chini kwa kuinama kama wanazitua zile bunduki. Hawakufikisha chini, kila mmoja akafungua riadha kuelekea kumfaako.

Lilikuwa tukio la ghafla ambalo hata Meja Uwizeye na wenzie hawakulitarajia. Lakini hawakuupa nafasi mshangao utawale, wakaruhusu mitupo ya risasi kuelekeza walikopotelea walengwa wao. Mitupo ya risasi iliyoendana na tawanyiko la kuwazingira. Huku ile miali ya mwanga ikizidi kumulika pande mbalimbali.

Kwa upande wa kina Luteni Ringo kila mmoja alikimbilia upande wake. Hawakumbilia umbali mrefu, wakachukua maficho kwa kujibanza kwenye miti na kujibu mashambulizi. Ikawa piga, nikupige. Wakihisi kusogelewa, huama pointi na kwenda kujikita sehemu nyingine.

Ndani ya muda mfupi tu, harufu ya baruti ikahanikiza sehemu kubwa, pasi na kusahau damu iliyotoka kwenye miili ya wafu na waliojeruhiwa katika yale makundi ya kina Meja Uwizeye, Luteni Bazombanza na Koplo Rumera.

“Hatuwezi kushindwa na wale wachache, hivyo tuhakikishe tunawakamata,” Meja Uwizeye aliwaasa wenzie. Nao kujaa morali kama hakuna wenzao waliowapoteza.

Maneno hayo yalimtoka pindi akibadilisha kisanduku cha risasi; alitoa kilichomalizika, akaweka chenye ujazo toshelevu. Mara baada ya zoezi hilo alijiinua alipoketi na kupiga ndogondogo huku akijiibia kuwasha kurunzi. Kwani vijana wengi waliokata moto, waliponzwa na kurunzi. Kitendo cha kuwasha na kuzima kiliwarahisishia kina Luteni Ringo kuwabaini.

Ilikuwa ni mara ya tatu kuwasha, pale Meja Uwizeye alipombaini Pte Bayo akihama pointi akajifiche mbali zaidi, alipojihimiza kukiwahisha kidole cha shahada kwenye kifyatulio amshambulie. Pindi mtupo wa risasi unatoka, Pte Bayo akafanya hila ya kupunguza umbo ili aukwepe ule mwanga na apotee. Lakini hakuwahi.

Kwani shambulizi lilimfikia mgongoni na kumrusha umbali wa mita kadhaa huku akijipigiza pigiza kwenye miti kabla hajatua. Na alipotua hakutingishika, fahamu zilimtoka, kitendo kilichozalisha furaha kwa Meja Uwizeye.

“Mmoja wao nimeshamtuliza kule, tufanye hima tuwasake hao wengine kwa udi na uvumba walipo,” Meja Uwizeye aliwataarifu wenzie.

Yalikuwa maneno yaliyotoa hamasa ya hali ya juu wazidi kukata pori kuwatafuta.

Wakati huo Luteni Ringo alikuwa ameketi chini ya mti mkubwa akivuta pumzi baada ya zoezi la muda mrefu la kujibu mashambulizi. Jasho likawa linamtiririka kama maji, kofia ngumu ameivua na kuiweka kando ili kichwa kipate hewa kwanza kisha arejee zoezini kwa nguvu zote. Lakini alitatizika kwa kiasi kikubwa mno, imekuaje wamebainika mapema?

Kuna muda alihisi, taarifa zao zimevujishwa toka walivyotoka jijini Dar es salaam au wale marubani.

Ilikuwa vivyo hivyo kwa Koplo Frederka. Alijipumzisha chini ya shimo dogo baadhi ya zana amezitelekeza jirani; bunduki na kofia ngumu. Ballistic vest aliilegeza kidogo.

Mapumziko kwa upande wao lilikuwa jambo la msingi sana. Kwamba wakisharudi, warudi kwa ari kama ndiyo kwanza wanaanza.

Pte Pemba ndiye pekee aliyekuwa anashughulika nao wapinzani. Yeye hakupooza mashambulizi kule alipojificha. Aliliza shaba kama mwendawazimu anavyopoteza sifa ya uwendawazimu wakati avukapo barabara.

***

Zilipita dakika takribani thelathini, ndipo Pte Bayo alizunduka kutoka kwenye usingizi wa muda uliomchukua kwa lazima. Alivyojipa utulivu kusikilizia, viwambo vikanasa mirindimo ya risasi umbali mrefu toka alipo. Akafahamu, bado zoezi linaendelea. Hilo likamkumbusha kilichopelekea apoteze fahamu. Mshindo wa risasi alizoshambuliwa mgongoni.

Sasa kwa nini bado yu'hai?

Akajua kuna namna, iliyomfanya akasalimika.
Hiyo namna aliyoihisi ikamshinikiza avue peki na kuanza kulichunguza. Alilifungua, na kutoa vilivyomo kwa msaada wa mwanga wa kurunzi aliyoiwasha kiustadi wa hali ya juu, pasi na kuruhusu miali kusambaa eneo kubwa na kwa uwazi.

Alipigwa na butwaa, alipokuta mtambo uwezeshao mawasiliano ya redio zao umechakazwa vya kutosha kiasi cha kutotamanika. Akashawishika ajaribu kufanya mawasiliano, awasiliane na wenzie kabla hajajihakikishia ule mtambo umepotezewa nguvu. Isivyo bahati, redio iliishia kutoa mlio pasi na kusikika mrejesho kutoka upande wa pili. Mlio wa alamu tu.

“Ooooh! Shiiit,” Pte Bayo alimaka huku akiupiga piga chini ule mtambo.

Alihisi kuchanganyikiwa. Na kilichomchanganya, watawasilianaje waweze kukutana?

Hakutaka kuamini, kama ule unaweza kuwa mwisho wa wao kuonana. Kwani pasipo mawasiliano ingekuwa ngumu kufahamu wenzake walipo. Au kubashiri, uelekeo waliopita. Hali hiyo ilimchukua muda mrefu kuifanyia kazi pasi na mafanikio. Mwisho, alirudishia vitu alivyovitoa ndani ya peki, baada ya hapo alilirejesha mgongoni na kujiinua.

Wapi aelekee?

Ndilo swali la kwanza kujiuliza akiwa wima. Akafanya mafikirio kwa sekunde chache, moyo uliporidhia, hakuchelea, alipiga hatua kuelekea alipojiaminisha panamfaa kwenda.

ITAENDELEA...
 
MNYONGA TAI
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
MAWASILIANO: 0673056571

“Sihitaji uwepo wake. Amekuwa kichefuchefu sana kwa upande wangu,” m-baba aliyepambwa kwa umbo nene kiasi, mfupi-mweusi alisema. Akasogeza bahasha ndogo yenye rangi ya khaki iliyopo juu ya meza, msogezewa aliipokea na kuifungua.

Msogezewa alikuwa kijana, akadiriaye miaka thelathini na tano. Aliyepambwa kwa umbo jembamba, mrefu-mweusi.

Aliifungua ile bahasha, akatoa kilichohifadhiwa. Picha. Picha ya mnato.

“Nahitaji hili jambo litekelezwe kwa haraka sana. Ikibidi...” yule m-baba mnene alisema. Kauli iliyomvumbua kijana na kumfanya amtupie mboni za usikilizaji wa umakini. “Asifike wiki ijayo.”

Yule kijana akarudia kuisaili ile picha.

“Siku ipi utapenda kusikia taarifa za kifo chake?” yule kijana aliuliza.

“Mmmmh, jumatano.”

“Okay, tarajia hilo.” Akairudisha picha bahashani na kuihifadhi kwenye mfuko wa koti alilovaa.

***

Alijibweteka kwa nguvu sofani, mkewe na mwanae wakamtumbulia mboni zilizojaa ulizo kutaka kufahamu mafanikio ya mienendo aliyotoka kuifanya. Anafahamika kwa jina la Cheyaya, mmoja wa matajiri wakubwa mjini Mangaka.

“Pole sana,” mkewe alimliwaza.

“Stella, kaniletee maji kwanza,” Cheyaya alisema. Kisha akautua mhemo wa pumzi kwa nguvu.

Mwanae, afahamikaye kwa jina la Stella, binti akadiriaye miaka ishirini na saba akainuka sofani na kwenda kutii agizo la babaye.

“Ndiyo umetoka huko Halmashauri?” mkewe aliuliza.

“Ndiyo.”

“Umefanikiwa?”

Cheyaya kabla hajajibu, tayari alikwishaletewa maji na mwanae. Akayafakamia kwa haraka, alivyoyamaliza, alimkabidhi Stella glasi.

“Bado sijafanikiwa mke wangu. Wameniambia nirudi kesho kutwa, mara baada ya kufanyika kikao cha baraza la madiwani kesho.”

“Hilo baraza la madiwani ndilo litakaloamua maombi yako?”

“Nafikiri.”

“Tuombe Mungu lifanikiwe. Na kama watazidi kukuzungusha, wiki ijayo anakuja Mheshimiwa Waziri Mkuu, atakuwa na kikao cha hadhara hapahapa mjini, andaa jitihada zitakazokuwezesha unapata nafasi ya kuonwa uelezee lengo lako.”

“Nilivyopata taarifa za ujio wa ugeni huo nilifikiria hiki ulichonishauri.”

Mkewe akatabasamu. Mwanamke aliyepambwa kwa umbo jembamba, mrefu kiasi, mweupe. Anafahamika kwa jina la Dorice.

“Lakini usivuke hatua. Rudi hiyo kesho kutwa uwasikilize, kama ubabaishaji utazidi, ndiyo ufanye hilo jambo.”

“Hamna shida.” Cheyaya akainuka sofani na kupiga hatua taratibu kupotelea ushorobani.

“Sipati picha ungelikuwa mgeni wangelikuzungushaje?” Dorice akampazia sauti.

Cheyaya akadakia kwa uharaka, “Halafu ni jambo la kujitolea.”

Dorice akaguna.

***

Asubuhi ya saa 2:35 siku iliyofuata Cheyaya aliegesha gari yake aina ya Toyota Harrier eneo la maegesho ya ofisini kwake. Ofisi ya kampuni ya CHEKA. Ikiwa na maana ya muunganiko wa wahusika wa kampuni hiyo, Cheyaya na Kasembe. Shughuli kuu ya kampuni yao ni uuzaji wa mafuta ya vyombo vya usafiri na hoteli.

Wana matawi mbalimbali ya biashara kwa mikoa ya kusini. Makao makuu ya ofisi wakayaweka Mangaka-mtaa wa Soweto.

“Ooh! Bosi,” Kasembe aliita, akiwa ameanza kupanda vidato vya ngazi kuingia ndani ya jengo. Jengo la ghorofa moja. Wakati huo Cheyaya alikwishateremka garini mwake na kupiga hatua za kuufuata uelekeo aliochukua Kasembe.

“Niambie kamanda wangu,” Cheyaya alisema, tayari alikwishamfikia Kasembe.

Wakaongozana kupotelea ndani ya lile jengo.

Ukomo wa safari yao uliishia kwenye chumba kilichotambulishwa na bandiko lililosomeka Director mlangoni. Cheyaya akaketi katika kiti kilichoonesha hukaliwa na mwenye ile ofisi. Kasembe, akaketi kiti cha mgeni.

Wote kwa ujumla walikuwa na maumbo yanayofanana; warefu, wembamba, rangi iliyopamba ngozi ni nyeusi.

“Ripoti ipoje?” Kasembe aliuliza. Akakunja mzungu wa nne, kisha kutumbua mboni zake pima kwa Cheyaya amwone aongeavyo.

“Inanibidi nirudi kesho. Leo wapo kwenye baraza la maamuzi.”

“Mbona wanachukua muda mrefu hivi? Walishindwa kuitisha baraza kwa dharura kujadili hili?”

“Nami nashindwa kuelewa ndugu yangu. Lakini tusife moyo, tutaupendezesha mji wetu kwa namna yoyote ile. Lazima tugawane sehemu ya mafanikio na jamii yetu.”

“Endapo wakikataa umefikiria kufanya nini?”

“Wiki ijayo anakuja Waziri Mkuu, alhamis. Nitajitahidi nipate nafasi kuwasilisha tatizo langu.”

“Ndiyo maana nakukubali.”

Wakaangua tabasamu.

***

Unyuma wa kimaendeleo wilayani Nanyumbu kuliwachachafya Cheyaya na Kasembe kiasi cha kuishawishi bodi ya wakurugenzi wa kampuni warudishe fadhila kwa jamii, kwa kugawa sehemu ya faida ya miradi yao kufanya miradi ya maendeleo. Miradi itakayofanya wilaya iwe yenye uangavu.

Miradi waliyokubaliana kufanya uwezeshaji ni maji na utengenezaji wa barabara. Walikubaliana kuuremba mji wa Mangaka kwa barabara za mitaani kuwa na lami. Halafu za katani, ziwe za moramu. Katika suala la maji, wawezeshe maji kwa uchimbaji wa visima vitakavyokuwa na uwezo wa kutoa maji ya kutosha kila kata.

Makubaliano haya waliyawasilisha kwa barua katika serikali ya wilaya. Lakini isivyobahati, toka wawasilishe, takribani miezi minne iliyopita hawajapatiwa majibu.

Kila walivyofuatilia walikesha kupatiwa jibu moja tu, njooni kesho. Au subirini kikao fulani. Kikashakaa, tutawaiteni.

Asubuhi ya siku aliyoambiwa Cheyaya arejee ofisi za halmashauri ilikuwa yenye uangavu. Hali ilikuwa tulivu. Naye aliamka mapema sana, ili apate kuwahi kisha akishatoka ofisini huko aendelee na ratiba zingine za biashara yake.

Ilivyogota saa 3:00 asubuhi tayari alikwishaegesha gari lake eneo la maegesho na kuteremka garini. Kwa hatua fupifupi, akawa ananyanyasa ardhi kupotelea ndani ya jengo. Jengo lililobeba karibia ofisi zote za idara ya halmashauri. Lilipatwa kujengwa kijiji cha Ngalinje.

Ukomo wa mwendo wake ulikuwa ofisi ya masijala ya Mkurugenzi wa halmashauri. Hapo alipokelewa na binti akadiriaye miaka ishirini na tano. Tena alipokelewa kwa bashasha ya hali ya juu. Jambo lililopelekea wasailiane kila baada ya sekunde kadhaa.

Ilimchukua takribani nusu dakika pale masijala, kisha akaanza upya mwendo mara baada ya kutaarifiwa jambo na yule binti. Akapotelea mlango uliofuata ulio na bandiko la utambulisho lililosomeka Mkurugenzi.

“Karibu sana Bw. Cheyaya,” m-baba aliye na umbo nene kiasi, mfupi, mweusi alimlaki.

“Nimeshakaribia bosi.” Cheyaya akaangua tabasamu.

Yule m-baba, aliyemkuta mle ofisini naye akaangua tabasamu. Baadaye walipeana mikono kusabahiana, wakafuatia kuketi.

“Nimetii wito,” Cheyaya alisema.

“Nakumbuka. Tena almanusra nikupigie simu.”

“Oooh!”

“Yeah. Sasa nipe subira kidogo,” yule m-baba alisema akiwa ameshainuka. Na kabla hajapata mrejesho wa Cheyaya aliondoka mle ofisini.

Alirejea dakika tatu baadaye. Akiwa ameambatana na watu watatu ambao hawakumpa shida Cheyaya kuwafahamu. Walisabahiana, kisha kila mmoja akachukua nafasi ya kuketi.

Katika wale watatu, wawili walikuwa wanaume; mmoja alipambwa kwa umbo jembamba, mrefu, mweupe. Umri alikadirika kuwa na miaka thelathini na ushei. Mwingine, ni mzee; alipambwa kwa umbo nene kiasi, mfupi, mweusi. Rika lake lilikadirika kuwa na miaka hamsini na ushei. Aliyesalia alikuwa mwanamke. Mfupi, mnene, maji ya kunde.

Awamu hii ya uketiji yule m-baba aliyekuwa ameketi kiti cha mhusika mkuu wa ile ofisi pindi Cheyaya alivyoingia, hakuketi kwenye kile kiti. Aliketi yule kijana-Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu. Wale wengine; yule mama ni Mwenyekiti wa Halmashauri. Mzee, Mbunge wa jimbo la Nanyumbu-na Waziri wa fedha.

“Tuwie radhi kwa kukawia Bw. Cheyaya,” Mkuu wa wilaya, afahamikaye kwa jina la Rudu alisema. “Ulipasa utukute wote tupo tayari.”

“Hamna shida mheshimiwa,” Cheyaya alimwondoa hofu.

“Mkurugenzi,” Rudu aliita.

Mkurugenzi akainuka. Akachukua hatamu ya uzungumzaji, “Bw. Cheyaya, kama nilivyokutaarifu mara ya mwisho, jana baraza limekaa na kuchukua maamuzi juu ya hoja yako uliyoiwasilisha,” akatulia kwa muda. Cheyaya akiwa anamsaili aongeavyo na kutega masikio vyema anase kwa uzuri kisikikacho.

Mkurugenzi akaendelea, “Maamuzi yaliyofikiwa na baraza ni kama ifuatavyo; halijakubaliana na takwa lako.” Akatulia tena.

Wakati huo Cheyaya moyo ukikita kwa mshtuko. Hakuamini. Tarajio la jibu si lile lililotoka.

“Sababu iliyofanya wasiafikiane nawe,” Mkurugenzi aliendelea. “Mpango mkakati wa halmashauri ni kuratibu hiyo miradi kwa hii awamu. Hivyo ipo kwenye mpango sera.”

Cheyaya akatikisa kichwa kuafikiana naye.

“Sambamba na hilo, baraza limekupongeza na kukupa shukrani kwa uamuzi uliochukua. Linakuomba, usife moyo,” Mkurugenzi alihitimisha. Akaketi.

“Cheyaya,” Rudu aliita. “Kwa niaba ya serikali, nakupongeza sana kwa uamuzi huu. Kushindwa kwa sasa sio kushindwa kwa baadaye.”

“Sahihi,” yule mzee akaingilia kati. Mbunge na Waziri wa fedha. “Serikali inawahitaji watu kama ninyi. Nikuahidi, tutahitaji uwezeshaji wako kwa siku zijazo.”

“Sawa. Nami nashukuru kwa kunielewa. Nipo mguu sawa kwa uwezeshaji wa namna yoyote nitakapohitajika.”

“Tunafurahi kusikia hivyo,” wale viongozi waandamizi wa wilaya walijibu kwa pamoja.

Kikao kikahitimishwa.

Cheyaya alitoka mle ofisini akitawaliwa na unyong'onyo kiasi kwamba alishindwa kupiga hatua kwa uzuri. Alipoifikia gari yake, aliegamia mlango kwa sekunde kadhaa kabla hajaufungua na kuingia.

“It's real, kwamba uwepo wa ile miradi kwenye mpango sera ndiyo sababu ya kutoafikiana na nia yangu?” Cheyaya alijiuliza. Lakini isovyobahati, hakupata jibu ridhisho.

Baadaye alitoa simu kwenye moja ya mfuko wa suruali, akapotelewa na sekunde chache za ubonyezaji, kisha aliiweka usawa wa sikio.

“Mmnh! Bosi,” ilisikika sauti ya upande wa pili.

“Njoo hapa halmashauri. Usitumie usafiri wako binafsi.”

Akakata simu hata kabla yule wa upande wa pili hajajibu.

Akajiegemeza kitini, huku akiruhusu mafikirio.

Aliondoka kwenye ile hali punde alivyowasili yule aliyewasiliana naye. Akateremka garini, wakaungana kusimama ubavuni mwa gari.

“Nini shida?” yule mtu aliuliza, Kasembe.

“Nataka uendeshe gari tuelekee ofisini.”

“Nini kimetokea hadi ushindwe kuendesha?”

“Tutahabarishana ofisini.” Cheyaya akachukua nafasi ya kuketi.

Kasembe akaketi nyuma ya usukani, safari ikaanza.

Walikuja kufungua uwanja wa mazungumzo walipowasili ofisini pindi wakichukua nafasi ya kuketi. Ofisini kwa Cheyaya.

“Imekuaje?” Kasembe aliuliza.

“Mambo hayako poa. Ombi letu halijakubaliwa.”

“Aisee! Jambo la kujitolea limekataliwa?”

“Wanadai yale mambo tuliyoyadhamiria yapo kwenye mpango sera wa serikali kwa utekelezaji awamu hii.”

“Unadhani hiyo sababu ina uhalisia?” Kasembe aliuliza na kutulia kwa sekunde chache. Akamsaili Cheyaya namna alivyosawajika, kisha aliendelea, “Uhisi mrengo wa kisiasa tulionao ndiyo sababu ya kukataliwa huko?”

“Nimelihisi hilo. Lakini sijalipa uzito.”

“Mimi nahisi hiyo ndiyo sababu kwa asilimia zote,” Kasembe alisema na kutulia kwa muda. Akamsaili Cheyaya, kisha aliendelea, “Utofauti wa kisiasa ndiyo sababu. Tungelikuwa...” hakumalizia kauli yake, akakatishwa na mwito wa simu ya mezani.

Cheyaya akaipokea.

“Mruhusu,” ndilo neno pekee lililotamkwa na Cheyaya, kisha alikirejesha kiwambo mahali pake.

“Kuna mgeni uliahidiana naye kuonana? Nataka niondoke ili niwaachie nafasi,” Kasembe alisema.

“Haina haja ya kuondoka. Ni mgeni wa kawaida.”

Mlango ukagongwa. Mgeni kusudiwa akaingia ndani.

Alikuwa yule mzee mnene kiasi, mfupi, mweusi-mbunge wa jimbo la Nanyumbu.

“Karibu mheshimiwa,” Kasembe alimlaki. Wakainuka kitini kumpa heshima. Alivyochukua nafasi ya kuketi, nao waliketi.

“Nimekuja kuwapa pole Bw. Cheyaya. Nina hakika maamuzi ya baraza sio mazuri. Hukuyategemea. Nami nikiwa kama mdau wa maendeleo, sijafurahishwa na maamuzi yale. Ninatamani kuyatumia mawazo yako yawe timilifu,” Mbunge alisema. Afahamikaye kwa jina la Pius Nalimuka.

“Hamna jinsi mheshimiwa. Ni maamuzi ya kiserikali, hivyo ni ngumu kupingana nayo,” Cheyaya alijibu.

“Lakini kuna namna tunaweza tukaifanya kwa ushirikiano wetu; kati yenu, nami-kama mnahitaji hilo jambo.”

Cheyaya na Kasembe wakashawishika zaidi kumsikiliza.

Nalimuka akaendeleza ufafanuzi, “Sote tuna kiu ya kuona jimbo letu likiwa endelevu, hivyo kama hautojali, unaweza kufanya uwezeshaji kwa kunitumia mimi. Nikiwa na maana utumie mgongo wangu kutimiza ukitakacho.”

“Bado sijakuelewa vizuri,” Cheyaya alisema na kubadili aina ya mkao.

Hakuuelewa ule ufafanuzi. Kiasi cha Nalimuka kuingiwa na tahayari kwa kiasi kabla hajaendelea kumfafanulia. “Mnaweza kufanya uwezeshaji kwa kunitumia. Nikiwa na maana mnanikabidhi kiasi cha pesa mnachotaka kukiwezesha kwa mradi husika, kisha ninaenda kulishawishi baraza.”

Cheyaya akavuta mdomo na kutoa mguno wa kimoyomoyo. Jambo lililozalisha ukimya kwa sekunde kadhaa.

Baadaye Cheyaya aliufukuza, “Siwezi nikafanya hivyo. Ni heri hiyo hela nichome moto sio kukupatia wewe. Kwanza nikupatie kwa misingi ipi?” kauli hii ilimtoka kwa ukali.

“Na hakika,” Kasembe alichangia. “Kama serikali imeshasema hakuna nafasi ya sisi kufanya hivyo ya nini kujipendekeza?”

“Aaah, ni ushauri tu. Nimefanya hivyo ili mkamilishe takwa lenu,” Nalimuka alisema, wajihi ukijaa haya.

“Ulishindwa kulishawishi baraza? Kwa nini hukuwashawishi wao? Sisi hatuwezi kukupa hela zetu kiholela hivyo mzee.”

“Nimekuja kukushauri hilo, kama utaafikiana nalo si vibaya ukalitekeleza.”

“Naomba utuache. Na utumie mlango uliokuja nao urejee ulipotokea.”

“Sawa, nitaondoka. Lakini jaribuni kuufanyia kazi,” Nalimuka alisema pindi akiinuka. Alivyokuwa wima, aliwasaili kwa sekunde chache kina Cheyaya kisha akaanza hatua za uondokaji.

“Mlishakataa, hivyo tutatafuta sehemu nyingine waliyo na maono ya uhitaji wa jambo letu. Tutaenda kuwezesha hapo,” Cheyaya alisema, wakati Nalimuka akimalizikia kuondoka mle ofisini.

Kwa pamoja, wakamsindikiza kwa mboni kali.

“Naamini sasa umepata uthibitisho kwa asilimia zote, kuwa hawa jamaa walikataa nia yetu kwa sababu ya mrengo wa kisiasa tulionao,” Kasembe alisema.

“Wakafie mbele huko. Kwa hiyo wanadhani kile tulichokipangilia kingelitekelezeka tungelipata credit kwa wananchi?”

“Ndiyo mawazo yao.”

“Wapumbavu sana,” Cheyaya alisema pindi akiinuka kitini. Mwisho, alimalizia msonyo.

Baadaye alikusanya vitu fulani pale mezani-hasa simu. Akazihifadhi mfukoni, kisha waliambatana taratibu kuondoka mle ofisini.

TUKUTANE TOLEO LIJALO.
 
MNYONGA TAI—02
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
MAWASILIANO: 0673056571

Ilikuwa asubuhi ya saa tatu, Cheyaya alivyochukua nafasi ya kupata kifungua kinywa sehemu husika ya maakuli nyumbani kwake. Kilikuwa kitendo cha taratibu sana, kwani funda alizokuwa anapiga hazikuwa za nguvu. Alikunywa ile chai kama mtoto mdogo, huku wajihi ukimtambulisha yuko mbali ki-fikra.

Hatua za mkukumkuku kutoka kwa mkewe aliyekuwa anakuja usawa aliopo ndizo zilimwondoa katika hali hiyo. Alitua bilauri mezani, akamwangazia akujavyo.

“Vipi, kuna tatizo?” Cheyaya aliuliza. Wakati huo mkewe alishafikia lile eneo la maakuli na kuchukua nafasi ya kuketi.

“Nikuulize wewe, tatizo nini? Unapigiwa simu hutaki kupokea.”

Cheyaya akauhimiza mkono usafiri kwa haraka hadi mfukoni. Alipoutoa, ulikuwa mwambatano na simu.

Kweli.

Kama alivyotaarifiwa na mkewe, alikuta orodha kubwa ya namba zilizompigia. Alipotaka kupangusa ili achambue kujua wahusika waliopiga, simu ikaita. Hakuchelea kumfahamu mpigaji.

“Niambie Chiku,” Cheyaya aliita, mara baada ya kupokea.

“Kuna tatizo bosi,” ilisikika sauti ya upande wa pili. Sauti ya Chiku.

“Ofisini?”

“Ndiyo.”

“Nini tena?”

“Wamekuja maafisa wa mamlaka ya mapato pamoja na askari wa jeshi la polisi. Wanalazimisha kufanya ukaguzi.”

“Nakuja hapo sasa hivi.” Akakata simu.

Taarifa hii ikamnyima hamu ya kila kitu. Na kumlazimu aianze safari ya kuelekea ofisini pasi na utimilifu wa mavazi. Aliondoka koti la suti likining'inia mkononi. Ilhali shati hakulichomekea.

Alivyoingia ndani ya gari kabla hajaruhusu ungurumishaji wa injini, akapokea simu kutoka kwa Kasembe.

“Nimeshapokea taarifa,” Cheyaya alisema kabla ya Kasembe hajazungumza jambo. “Hivyo nisubiri nyumbani kwako ili tuelekee pamoja ofisini.”

“Fanya hima basi.”

Cheyaya akakata simu, kisha akaitupia siti jirani.

Dakika moja baadaye akawa ameuanza mwendo. Akili ikichukuliwa umakini na mawazo kuhusiana na taarifa aliyopatiwa. Halikuwa jambo la kawaida, kwani tangu waanzishe biashara zao hiyo ndiyo mara ya kwanza kuvamiwa na maafisa wa aina hiyo.

“Itakuwa ni yule mshenzi. Yule mshenzi ndiyo amehusika na haya,” Cheyaya alijisemeza. Wakati huo akiiumba taswira ya yule aliyemwita mshenzi. Nalimuka.

“Na hatopata chambi yoyote hata kama watanitingisha kwa kiasi gani,” alindelea kujisemeza. Awamu hii alishaufikia mtaa aishiyo Kasembe.

Alivyoifikia nyumba husika, akaegesha gari karibu na wigo, akaanza kupiga honi kwa nguvu kiasi cha kuwakeresha baadhi ya majirani. Honi hiyo ilikuwa mwito kwa Kasembe. Kwani baada ya Cheyaya kusitisha, haikuchukua muda mrefu Kasembe kuwasili.

“Baadaye nikirejea nitakuta malalamiko dazani kwa hiki kitendo chako. Ina maana ulishindwa kuteremka?” Kasembe alimuuliza akiwa anafunga mkanda wa siti. Cheyaya akiingiza gari barabarani kuendelea na safari.

“Watanisamehe. Maana sipo sawa kabisa.”

“Na umepata taarifa hao watu wamevamia matawi yote ya ofisi zetu?”

Cheyaya akafunguka breki kwa ghafla, kisha akamtupia mboni za mkazo Kasembe. Taarifa aliyopatiwa muda huo, ilipigilia msumari wa moto ile ya mwanzo.

“Ndiyo hivyo. Asilimia kubwa biashara zetu hazijafunguliwa siku ya leo,” Kasembe alimsititizia.

Cheyaya akasonya. Baadaye akatokwa na kauli, “Huyu mjinga! Kwa hiyo anahisi njia aliyotumia itamrahisishia kufanikisha akitakacho?”

“Unamzungumzia nani?”

“Uhisi huyo Mbunge wako-Waziri wa fedha, ndiyo sababu ya haya kwa kile tulichomjibu jana?”

“Aiseee! Ndiyo unanifumbua,” Kasembe akahamaki.

“Yeye ndiyo sababu. Lakini ngoja kwanza tufike ofisini tukajihakikishie.” Akarejelea mwendo.

Iliwachukua dakika sita kuwasili ofisini. Hata kabla hajaegesha gari vizuri, wakateremka na kupiga hatua za haraka hadi walipokusanyika baadhi ya wafanyakazi. Wakapokelewa na wajihi zilizojaa huruma.

“Wameshaondoka bosi,” Chiku aliwataarifu.

“Muda mrefu?” Cheyaya aliuliza.

“Hapana.” Wafanyakazi wote katika lile kusanyiko walijibu.

“Wamesemaje?”

“Waliacha hii barua baada ya kufanya waliyoyadhamiria.”

Akakabidhiwa Kasembe.

“Wamefanya nini na nini?”

“Wamefunga baadhi ya ofisi, kisha wakaondoka na mafaili fulani.”

Cheyaya akajiondoa kwenye lile kusanyiko na kupotelea ndani ya jengo. Chiku alikuwa nyuma yake. Kasembe akachukua nafasi kuisoma ile barua.

Kule ndani Cheyaya alizunguka kila sehemu aliyoarifiwa maafisa wa mamlaka ya mapato walipita. Mwisho alipotelea muda mrefu ofisini kwake.

“Ukiachana na barua, hakuna kingine walichokizungumza?” Cheyaya aliuliza, wakati huo akihangaika kuchambua chambua kwenye baadhi ya saraka.

“Walikuwa wanajiongelesha ongelesha wenyewe. Hivyo sikubahatika kunyaka wazungumzacho,” Chiku alijibu. Binti mwembamba, mrefu-mweusi.

“Sasa sikia,” Cheyaya alisema, akaacha shughuli ya uchambuaji akamgeukia Chiku. “Kabla sijasoma ile barua, nafahamu kusudio lake ni kufunga biashara zetu. Nasi tutafanya hivyo...”

Chiku akadakia, “Ina maana tutapoteza ajira zetu?”

“Hatuna jinsi. Inatulazimu tufanye hivyo. Lakini kuna jambo nahitaji unisaidie.”

“Nini bosi?”

“Si umekuja na begi lako?”

“Ndiyo.”

“Lilete kwanza.”

Chiku akatii. Kwa kuondoka mle ofisini. Cheyaya akaendelea na zoezi la awali.

Chiku alivyorejea, alimkuta Cheyaya amejituliza kitini, juu ya meza kukiwa na mafaili na vitabu kadhaa.

“Naomba uchukue hivi vitu,” Cheyaya alisema akimkabidhi Chiku mafaili mawili. “Usimwambie wala kumwonyesha mtu yeyote. Vihifadhi sehemu tulivu, ambayo ni wewe tu ndiyo utakuwa unafahamu.”

“Sawa bosi,” Chiku aliitikia pindi akaiyahifadhi yale mafaili begini.

Uwepo wao ofisini uliishia hapo. Wakarejea walipo wenzao, Cheyaya akiwa amekamatia vile vitabu. Wakapokelewa kama walivyoondoka. Wengi wao wajihi ulijaa huruma.

Hali hiyo ilikuwa hadi kwenye maeneo mengine ya biashara zao. Wasimamizi wa hayo maeneo walikesha kupiga simu muda wote kuuelezea kilichotendeka na hali ya wafanyakazi.

“Wamefunga biashara bosi. Sasa itakuaje kuhusu sisi? Tutapata wapi nguvu ya kusogeza mkono mdomoni?” wafanyakazi walilalamika. Sauti ikiwa nyongefu.

“Hatuna jinsi ndugu zanguni. Inabidi tukubaliane na kilichotokea pindi tukifanya taratibu za utatuzi,” Cheyaya alijibu. Wakati wote akimsaili mmoja baada ya mwingine.

Aliwaonea huruma. Kwani naye aliumizwa na hali hiyo, lakini ilimpasa ajikaze kwa sababu ndiyo bosi.

“Ina maana hawajaona namna nyingine hadi wawafungie biashara? Sisi tutakula wapi jamani?” mmoja kati ya wale wafanyakazi alilalama. Mwisho, aliangusha ukunga.
Ikabidi wenzie wamtulize.

Hali ilivyotulia Cheyaya alichukua hatamu ya uzungumzaji. Kuwatuliza wafanyakazi wao. Wakubaliane na kilichotokea. Kwani ni sehemu ya mapitio ya maisha.

“Baba, wameshindwa kutuonea huruma? Eeh! Watatupatia wao ajira baada ya hiki kitendo walichokifanya?”

“Tuwe wavumilivu. Turudi nyumbani huku tukifanya subira, kwani siku zote haki haipotei, bali hucheleweshwa.”

“Tunawaombea mambo yakae sawa kwa haraka baba, turejee kibaruani,” wafanyakazi walisema pindi wakitawanyika. Wengi wao walikuwa kina mama.

***

Wafanyakazi walivyoondoka, Cheyaya na Kasembe waliongozana hadi walipoegesha gari. Waliingia, kisha kuchukua dakika kadhaa mle garini kabla ya kuondoka. Dakika walizozitumia kwa mazungumzo.
“Mkurugenzi anahitajika ofisi za mamlaka ya mapato mkoa,” Kasembe alisema, akaitua ile barua juu ya dashibodi.

Cheyaya alivuta pumzi, akazitua kwa nguvu. “Lini?” baadaye aliuliza.

“Kesho.”

“Naliona rungu la uhujumu uchumi na utakatishaji fedha. Mwisho, nadondokea jela.”

“Nina ushauri.” Cheyaya akamgeukia. “Sote ni wakurungenzi. Hivyo napendekeza mimi nichukue nafasi ya kuhudhuria ofisi ya mamlaka ya mapato mkoa, pindi ewe ukiratibu mipango ya uwasilishaji wa nia yetu kwa Waziri Mkuu hiyo wiki ijayo.”

“Upo sahihi. Lakini kuna moja la muhimu linalopaswa kushughulikiwa kwa haraka kabla hatujaanza hiyo mipango mingine.”

“Ipi?”

Cheyaya akachukua vile vitabu. Akamkabidhi.
Kasembe alivyopokea, alivichambua. Akakutana na karatasi kadhaa za marisiti. “Unataka tufanyaje?”

“Tufanye namna ya kuhifadhi hizo nyaraka. Zitatusaidia mambo yakiwa mabaya.”

Kasembe akazisaili kwa sekunde chache, baadaye akamtupia ulizo, “Umepata namna ya uhifadhi?”

“Hapana. Nimefikiria sana, lakini sijang'amua hiyo namna.”

Ukapita ukimya mfupi. Uliowapeleka wote kwenye fikirio.

Ulikuja kufukuzwa na Kasembe baadaye, “Tumtafute mtu nje ya mfumo wetu tumkabidhi. Maana sio vizuri kuhifadhiwa na watu wa karibu yetu, itakuwa rahisi kufikiwa.”

“Unamaanisha mtu baki?”

“Ndiyo.”

“Nani tutakayemwamini naye atuamini?”

“Yupo. Nipishe hapo kwenye usukani nikupeleke.”

Wakabadilishana siti, kisha Kasembe akaianza safari kuelekea sehemu paswa.”

***

Aliiteremsha darubini. Akaingia garini kwa haraka. Gari ndogo, aina ya Nissan-Extrail. Hakuchelea, aliiungurumisha injini, akaanza kuifuatilia gari iliyopo mbele yake. Gari waliyopanda kina Cheyaya.

Mwendo alioondoka nao ulikuwa wastani. Huku akitengeneza takribani umbali wa mita arobaini toka lilipo gari la kina Cheyaya.

Alikuwa ni yule Kijana; mwembamba, mrefu-mweusi. Aliyekabidhiwaga picha ya mtu anayepaswa kuuwawa.

Dakika kadhaa baadaye, akili ikiwa imelala kwenye ufuatiliaji wa mwendo wa gari la kina Cheyaya, alipigiwa simu. Alivyosaili mpigaji, alimfahamu. Akapunguza mwendo, akaipokea.

“Matokeo yakoje?” ilisikika sauti ya mtu wa upande wa pili.

“Kama ulivyotarajia. Nimemwona akitoka ofisini na mzigo fulani wa vitabu. Nadhani vitakuwa vina umuhimu,” yule kijana alijibu. Afahamikaye kwa jina la Jovin Kigwa.

“Unahisi ni hivyo tu? Hakuna nyaraka zingine alizozigawa gawa kwa wafanyakazi wake?”

“Sina uhakika. Ijapokuwa nilimwona akipotelea mle ofisini na msichana fulani hivi.”

“Kipi cha utofauti ulichomwananacho huyo msichana?”

“Sijakuelewa.”

“Namaanisha, pindi huyo msichana anapotelea ofisini alikuwa katika hali gani? Na pindi anatoka ofisini alikuwaje kuwaje.”

Jovin hakujibu kwa haraka. Alivuta kumbukizi kwa muda. Kumbukizi iliyomsafirisha apate taswira ya mazingira ya nje ofisini kwa kina Cheyaya pindi akiyasaili kwa darubini.

“Sikubahatika kumwona wakati watokao,” baadaye aliuondoa ule ukimya.

“Ina maana kwamba hukumwona huyo binti?”
“Yeah!”

“Lakini mkusudiwa wetu ulimwona?”

“Ndiyo. Nilimwona pindi wakiteta jambo na wafanyakazi wao. Sikumwona wakati anatoka ofisini.”

“Kama huyo binti hakuonekana baada ya kuingia ndani, basi kutakuwa na namna. Kuna mzigo amekabidhiwa huyo binti sio bure. Jaribu kulifanyia kazi na hilo.”

“Sawa.”

Simu ikakatwa.

Jovin akatua pumzi kwa nguvu. Kisha akaurejelea mwendo wake wa awali. Aliurejelea mawazo yakishika hatamu kumhusu Chiku.
Atampataje?

***

Hatamu ya mawazo ilimfanya apoteze shabaha. Alipoteza ufahamu wa uelekeo waliochukua kina Cheyaya. Tukio hilo lilimtokea akiwa maeneo ya nyuma ya uwanja wa mpira wa miguu wa shule ya sekondari Mangaka. Akaegesha gari pembeni. Akateremka.

Kwa mkazo, akazihimiza mboni kusaili uelekeo wa matairi. Akauona. Na kujipa imani iliyomrejesha garini aufuatilie. Aliendesha gari kwa kufuata matairi yalipoelekea.

Alivyofika karibu na maeneo ya nyumba ya kulala wageni iitwayo Mkova, kwa upande wa nyuma wa jengo, akasitisha mwendo. Zile alama za matairi hazikuonekana kuendelea mbele. Akateremka.

Alivyosaili kwa umakini, akabaini gari liliishia mahali pale. Kutokana na mwingiliano wa zile alama.

“Walielekea wapi baada ya hapa?” Jovin (watu wengi maeneo aishiyo walipenda kumwita jina la ubini wake-Kigwa) alijiuliza. Ulizo lililomsukuma aangaze angaze majengo yaliyopo jirani.

“Au kuna mtu walikuja kukutana naye hapa?” aliendelea kujiuliza. “Walivyohitimisha mambo yao, huyo mtu aliondoka, nao wakarudi walipotokea.” Alivuta picha namna ilivyokuwa, huku akizidi kusaili; kwa ukaribu na umbali.

Mwisho wa usaili wake, yale mazingira ya karibu yakampa kitu kilichomfanya atilie mashaka. Aliona mlalo wa nyasi, uliomtambulisha kuna watu, au kitu kilichopita sehemu hiyo. Akaamua kuufuata. Mboni zikiwa kupikupi-kupikupi kuangaza huku na kule.

Baada ya mwendo wa hatua kadhaa akasimama. Ule mlalo wa nyasi haukuwepo tena.

“Au ni watu wengine sio walengwa wangu ndiyo walipita hapa?” Jovin alijiuliza. Huku akiisaili kwa makini nyumba iliyopo mbele yake. Takribani umbali wa mita sabini toka aliposimama.

Aliisaili ile nyumba; iliyopambwa kwa nyasi na tofali zilizochomwa vyema. Zoezi lililomchukua takribani dakika mbili, baadaye akarejea alipoegesha gari lake.

“Wamenizidi vipi ujanja?” Jovin alijiuliza pindi akiingia ndani ya gari.

Alivyoketi sitini, alitia moto na kuondoka.

***

Nyendo za Jovin zilihisiwa na Kasembe. Alipata hisio kupitia side mirror. Jambo lililomshinikiza awe na mwendo usiotabirika tabirika. Cheyaya alivyouliza nini sababu, alitulizwa. Na kujibiwa ataambiwa wakisharejea kutoka kwenye ile safari.

Kwa stadi zake makini za udereva Kasembe alifanikiwa kumtoroka Jovin. Walipowasili sehemu kusudiwa wala hawakukawia. Walimkabidhi mlengwa wao vile vitabu, wakaondoka. Walikabidhiana palepale nyuma ya Mkova loji. Kisha mkabidhiwa akapotelea kwenye ile nyumba aliyokuwa anaisaili Jovin baada ya kufuata ule mlalo wa nyasi.

“Mmnh! Nieleweshe sasa sababu ya kufanya vile,” Cheyaya alisema, wakiwa wamechukua mapumziko sebuleni nyumbani kwake.

Mkewe na mwanaye wakiwa pembeni wakiwasikiliza.

“Kuna mtu alikuwa anatufuatilia.” Kasembe akateka viwambo vya wote.

“Acha bhana.”

“Hakika.”

Cheyaya alivuta pumzi, kisha akazitua kwa nguvu. “Kwa maana hiyo shughuli si ndogo?” alitokwa na ulizo baadaye.

“Ndiyo maana yake.”

Dorice akaingilia kati, “Tuwekeni wazi, kuna tatizo?”

Cheyaya akawageukia. Akawasaili kwa muda, kisha akawaeleza ukweli wa yote yaliyojiri. Maelezo yaliyosinyaisha nyoyo zao.

“Hapo jipangeni tu kukutana na Waziri Mkuu wiki ijayo,” Dorice alishauri. “Yaani hawa viongozi wa siku hizi? Mmnh! Sijui hata wanapimwa kwa kigezo gani kupatiwa hayo mamlaka? Watu mnataka mjitolee anawabanieni. Watafaidika na nini sasa, kama sio kuwaumiza wale mliokuwa mnawalenga kuwasaidia?”

“Hatuna jinsi shem. Tutakabiliana nao kwa namna yeyote ile.”

“Fanyeni muwakomeshe. Wajinga sana. Mambo ya siasa siasa yanafaida gani kwenye maendeleo?”

“Labda, hao wakubwa wao wawaunge mkono. Hapo tutashindwa. Lakini kama watatupa nafasi ya kutusikiliza, tutachukua ushindi mapema tu.”

“Na msikate tamaa hata kama watawapatia vitisho vya namna gani.”

“Ni bora tugawe bure bidhaa zetu. Lakini sio kukubaliana na matakwa ya hao wajinga.”

Dorice akaangua kicheko kidogo.

Mwito wa simu ya Stella ndiyo ulimkatisha. Wote wakamgeukia. Kwa staha, Stella aliondoka pale sebuleni akapotelea chumbani kwake.

Alikaa kule chumbani takribani dakika tatu. Alipokuja tena pale sebuleni wala hakukaa. Badala yake aliwaaga.

“Wazazi wangu naomba niwaache mara moja,” Stella alisema.

“Wapi tena?” mama'ke aliuliza.

“Nafika hapo mnazi mmoja.”

“Usikawie kurudi.”

“Sawa mama.” Akapiga hatua za haraka kuelekea nje.

“Jamanii, hata nami naomba nijiondoe.” Kasembe akainuka. Alivyokuwa wima akaendelea, “Inabidi tuonane kabla sijaelekea Mtwara hiyo kesho.”

“Hamna shida.”

Kasembe akaondoka.

***

Ukomo wa safari ya Stella ulikuwa sehemu maarufu kwa starehe mjini Mangaka. Baa ifahamikayo Cloud 9. Kabla hajachukua nafasi ya kuketi, alisimama lango la kuingilia na kuangaza mazingira ya mle ndani kwa dakika kadhaa. Alionekana kumtafuta mtu. Alivyompata, alipiga hatua za madaha kuelekea. Moja ya kona, katika meza iliyotengwa na zingine.

“Karibu sana Stella,” yule mkusudiwa alimlaki. Jovin. Aliinuka pale alipoketi, akamwonesha Stella sehemu ya kuketi.

Stella akatii.

“Kinywaji?” Jovin aliuliza, pindi akichukua nafasi ya kuketi.

“Maji.”

Jovin akamwita mhudumu. Mboni amezitumbua kumsaili Stella; binti aliyepambwa kwa umbo nene wastani, mrefu kiasi-mweupe. Alibarikiwa urembo. Ule utazamiwao kisasa.

“Halafu unaonekana kutokuwa sawa darling,” Jovin alisema, mboni zimelala pima kumsaili Stella.

Stella akaguna. Baadaye akatokwa na kauli, “Kuna mambo hayapo sawa huko nyumbani.”

“Nini shida?”

Kabla Stella hajajibu, mhudumu alikwishawasili. Akayatua yale maji mezani, kisha akaondoka. Hapo akapata wasaa mzuri wa kujibu lile swali. Alimweleza Jovin mkasa mzima umhusuo baba'ke katika shughuli za kibiashara.

“Pole sana,” Jovin alisema kwa sauti ya upole, Stella alivyohitimisha usimuliaji.

“Mmmh! Sidhani kama kuna uafadhali katika hili.”

“Ndiyo viongozi wetu hao, tuliotokea kuwaamini. Sasa unadhani utafanyaje? Hakuna namna. Au mzee amepata wazo la kukabiliana nao?”

Stella hakujibu kwa haraka. Alimimina maji kiasi kidogo kwenye bilauri, akayagugumia kwa haraka, aliposafisha koo kwa ukohozi mdogo ndipo alijibu, “Wamepanga kuonana na Waziri Mkuu wiki ijayo.”

“Kwenye hiyo ziara yake?”

“Ndiyo.”

Jovin akavaa umakini wa kutafakari jambo kwa sekunde chache. Alipomaliza, alikifakamia kinywaji chake kilichopo kwenye bilauri.

“Nimekukumbuka sana leo ndiyo maana nikahitaji uwepo wako karibu yangu,” Jovin alisema, alipotua bilauri.

“Naomba uniwie radhi kwa leo, sipo vizuri.”

“Oooh! Mbona unanikatili?”

“Vumilia. Hata kesho nayo ni siku, nitakaa sawa na kukupatia unachokihitaji.”

“Nitajaribu. Ijapokuwa ni kwa maumivu sana.”

Walipomaliza vinywaji uwepo wao mahali hapo ulihitimika. Waliondoka, kwa gari alilokuja nalo Jovin. Soga za kimahaba na mengineyo; hasa kumhusu Chiku zikichukua hatamu. Vicheko na tabasamu navyo havikusahaulika.

Walipowasili usawa wa nyumbani kwa Cheyaya, Jovin akaegesha gari pembezoni mwa barabara. Stella akateremka, Jovin akaendelea na safari.

Mwendo ulikuwa kawaida. Uliomwezesha kujihangaisha na mambo mengine. Miongonimwe, alipata wasaa wa kupiga simu. Ikapokelewa na yule aliyemkabidhigi picha. Nalimuka.

“Ndiyo kijana,” ilisikika sauti ya Nalimuka.

“Naenda kumaliza mchezo, hivyo niandalie kiasi changu.”

“Tayari umeshaandaa mazingira ya kifo chake?”

“Naam. Tena nakupongeza sana kwa ile siku uliyochagua kupatiwa taarifa.”

“Kwa nini?”

“Jamaa amepanga aonane na Waziri Mkuu siku atakayofika.”

Nalimuka akaangua kicheko cha nguvu kwa sekunde kadhaa. Baadaye akatokwa na kauli, “Ataenda kumpatia malaika huko mbinguni.” Akacheka kwa mara nyingine. Alivyokatisha, akauliza. “Kwa hiyo umepanga kifo chake kiwe cha namna gani?”

“I’ll pull trigger on his head.”

“Kila la heri katika hilo.”

Jovin akakata simu, kisha akaongeza mwendo.

TUKUTANE TOLEO LIJALO.
 
MNYONGA TAI—03
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
MAWASILIANO: 0673056571

Saa 4:24 asubuhi Kasembe aliegesha gari uga wa ofisi ya mamlaka ya mapato mtaa wa Ligula. Ilikuwa jumamosi. Alivyoteremka, aliongoza hadi ndani ya jengo. Akaishia mapokezi. Hapo alitumia dakika chache kisha akaongozwa na mhudumu aliyemkuta ofisini kwa Meneja wa mamlaka ya mapato mkoa.

“Karibu,” Meneja alisema. Huku akiliumba tabasamu la bashasha wajihini.

“Nimeshakaribia kiongozi,” Kasembe alisema pindi akichukua nafasi ya kuketi.

“Mmnh! Nikusaidie nini?”

“Nimekuja kutii wito.” Kasembe akaitua ile barua ya wito mezani na kumsogezea Meneja. “Mkurugenzi mtendaji kampuni ya Cheka,” alikazia.

Meneja akaichukua na kuisoma. Alipomaliza, alitokwa na ulizo, “Wewe ndiyo Mkurugenzi wa ile kampuni?” Akamtumbulia mboni za usaili.

“Ndiyo. Lakini kuna mwenzangu pia anaitwa Cheyaya.”

“Ina maana kampuni ina wakurugenzi wawili?”
“Ndiyo.”

“Sasa yeye mbona hajaja?”

“Barua imetoa wito kwa Mkurugenzi. Sio wakurugenzi.”

Meneja akazidi kumtumbulia Kasembe mboni za udadisi.

“Okay, naomba unisubiri kwa muda.” Meneja akainuka na kuondoka mle ofisini.

Mwisho wa ondoko lake ulikuwa nje tu ya ofisi. Akatoa simu mfukoni, akaperuzi kwa sekunde kadhaa kisha aliisogeza sikioni. Kuna mtu alimpigia.

“Bosi,” Meneja aliita, mara baada ya simu kupokelewa.

“Matokeo yapoje?” ilisikika sauti ya upande wa pili.

“Amekuja mtu mwingine, tofauti na yule uliyemzungumzia wewe.”

“Kwa maana ipi?”

“Kampuni ina wakurugenzi wawili.”

“Kwa hiyo amekuja yule mwenzake?”

“Ndiyo.”

Ukapita ukimya kwa muda. Kabla haujashika hatamu, yule wa upande wa pili, Nalimuka, aliufukuza. “Wanajifanya kutuzidi ujanja! Sasa sikia...”

“Ndiyo bosi.”

“Choma nyavu huyo, pindi nikitafuta namna ya kumdhibiti huyu aliyebaki.”

“Sawa bosi.”

Akakata simu. Akarejea ofisini.

***

Palikuwa na takribani umbali wa mita mia moja na kumi, kutoka Jovin alipoegesha gari na pale alipopakusudia kupafuatilia. Moja ya nyumba, mtaa wa Chang'ombe. Katu hakuteremka garini, kwani alitaraji kufanya uchunguzi kisasa zaidi, ili asitoe mashaka kwa watu wengine. Mashaka yatakayochangia dili lake kuharibika.

Hivyo baada ya kutulia kwa muda, alivuta begi ndogo kutoka siti za nyuma. Alivyolimiki vyema, alilifungua, akatoa darubini, begi akalirejesha. Hakuchelea, akaipachika darubini usawa wa mboni na kuangazia ile nyumba.

Pindi Jovin anafanya haya ilikuwa alasiri. Na kikubwa alichokishuhudia nje ya ile nyumba ni mabinti watatu waliokuwa wameketi kiambazani wakipiga soga. Wawili kati yao walikuwa wanasukana. Alivyoisaili sura ya mmoja baada ya mwingine, akaibaini ile aliyoihitaji. Chiku. Akaganda papo hapo kufuatilia nyendo zake.

Wakati anaendeleza umakini wa kumchunguza Chiku, akili ikafungua zoezi lingine la ufikiriaji wa mbinu itakayomwezesha kumnasa mrembo huyo na kupata alichoagizwa. Mbinu kadha wa kadha zilijizalisha na kupotea baada ya kuonekana hazina ushawishi wa ufanikishaji. Lakini ni mbili pekee, ndizo angalau zilishindwa kupotea kwa urahisi kila alivyojaribu kuzifutilia mbali.

Mbinu ya kwanza iliyomshawishi kuitumia ni mapenzi. Amtongoze mrembo huyo na kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi. Kwa namna yoyote ile, imani ya kwenye mahusiano atapata akitakacho. Lakini ni mbinu itakayomchukua muda mrefu. Na vipi kama hatokubaliwa?

Hapo pakawa na kizingiti kikubwa. Kilichomsukuma airidhie mbinu namba mbili aliyoifikiria. Kuonyesha uhalisia wa majukumu ya misheni aliyokabidhiwa. Amvamie, na kumshinikiza atende atakalomwamuru.

Akajiapiza kuitekeleza mbinu ya pili, ili aendane na muda.

Baada ya uchunguzi wa muda mrefu aliwaona wakihitimisha shughuli. Akazidi kuendana na Chiku. Alimfuatilizia kila hatua. Aliacha, alipomwona akifunga mlango wa nyumba na kuondoka na wenzie. Akateremsha darubini, akaihifadhi begini. Naye uwepo wake ulihitimika hapo. Aliungurumisha gari na kuondoka. Aliondoka huku akijenga taswira ya tukio lijalo atakalolifanya kwa mrembo huyo.

***

Starehe ya mazungumzo yao, yaliyojumuisha familia, yalikatishwa na sauti ya kike iliyokuwa inabisha hodi. Kabla hajajitolea mmoja wao kwenda kufungua mlango, walisailiana kwanza, ishara tosha ya udadisi kama kuna mtu aliyewekeana miadi na mgeni.

“Stella, nenda kafungue,” Cheyaya alisema, baada ya mbishaji hodi kuendeleza ombi.

Stella aliinuka. Akapiga hatua za taratibu hadi mlangoni.

Kabla hajafungua mlango. Alichungulia kwenye kitobo kidogo kilichopo katikati ya mlango ambaini afanyaye kitendo hicho. Alivyomtambua, aliwageukia wazazi wake kuwafahamisha. “Ma’mdogo.”

“Mfungulie,” Cheyaya aliidhinisha.

Stella akatii. Alifungua mlango, mgeni akaingia.

Alikuwa ni mwanamke wa makamo; mwembamba, mrefu wastani-mweupe. Umri wake unakadiria miaka thelathini na saba. Alifahamika kwa jina la Pendo.

“Karibu shemela wangu,” Cheyaya alimkaribisha. Wajihi ukiwa umejaa bashasha.

“Hata sijaja kukaa,” Pendo alisema.

“Nini shida?”

“Mwenzio hapatikani hewani.”

Cheyaya akabadilisha mkao. Akazitumbua mboni kama zote kuashiria Pendo aendelee kuzungumza.

Na akafanya hivyo.

“Ni zaidi ya mara nne sasa, kila ninavyopiga haipatikani,” Pendo aliendelea kueleza.

Ilikuwa taarifa chachafya. Iliyomhimiza Cheyaya akumbuke alipoihifadhi simu yake. Alivyoimiliki vyema mkononi, akaperuzi kwa sekunde chache kisha akaisogeza sikioni.

Ikiwa imesalia nukta chache simu iguse sikio, sauti ya mvumo wa gari ikamsitisha. Akaiteremsha ile simu. Akazihimiza mboni kuangaza dirishani. Pazia lililokuwepo liliwezesha kuonyesha upande wa pili japo si kwa uwazi sana.

Stella akamrahisishia, kwa kwenda dirishani na kufunua pazia. “Mmh! Mbona kama polisi?” Aliwageukia, akawataarifu.

Taarifa iliyowanyanyua wakaenda kujazana pale dirishani.

Waama, waliowasili walikuwa askari. Askari wa jeshi la polisi. Lakini walivaa kiraia. Idadi yao ilipata kuwa watano. Huku baadhi yao wakiwa wamebeba bunduki za kivita.

Jambo lililowataarifu ujio wao sio wa wema.

“Shemeji,” Pendo aliita. Cheyaya akamgeukia, “Ondoka. Ujio huu hauwezi kuwa na matokeo mazuri hata kidogo,” Pendo alizidi kumwasa.

Cheyaya akarejesha mboni kuwasaili wale askari. Akamwona kiongozi (Ocd) akiwagawa vijana alioongozana nao namna ya kulikabili jengo. Walidhibiti, watu wa ndani wasipate mwanya wa kuwatoroka. Hapo akapata uhakika, mambo sio mazuri kwa upande wao. Akamkumbuka Kasembe.

“Ondoka mume'ngu. Ondoka,” Dorice akamsisitiza huku akimsukuma.

Hakuwa na budi, Cheyaya alipiga hatua za haraka zenye mshindo mdogo kupotelea ushorobani uliomfikisha chumbani kwake. Hakukaa, alivuta chuma kizito wastani, chenye urefu wa mita moja uvunguni mwa kitanda, akalifuata dirisha. Hapo kwa ustadi wa hali ya juu, akakazana kuzitanua nondo hadi aliporidhishwa na nafasi iliyomhakikishia anaweza kupita.

Wakati anatupa kile chuma tayari kwa kutaka kuondoka, mkewe na mwanae wakaingia mle chumbani. Wajihi ulijaa huzuni, iliyotafsiri hali waliyonayo mtimani. Wakasailiana kwa muda, huku chozi likianza kuwalenga.

“Tumwombe Mungu, atufanyie wepesi mambo yawe sawa ndani ya muda mfupi,” Cheyaya alisema, akiwafuata walipo.

Alipowafikia, aliwakumbatia.

Sauti ya kugongwa kwa mlango kwa nguvu ndiyo iliwatenganisha. Cheyaya akarudi tena dirishani, akajisukumiza kupenya kwenye ile nafasi, hadi akafanikiwa. Dorice na mwanae walirejea sebuleni mpaka Cheyaya alivyopanda wigo uliozunguka nyumba yao na kurukia nje.

Lakini isivyobahati, mshindo wa mtuo ulikuwa wa nguvu mno. Hivyo ulisikika. Kitendo kilichowahimiza askari waliokuwa wamepangwa uwanda huo wakajionee kwa haraka.

Pindi Cheyaya anainuka ili aanze mbio, ndiyo kipindi askari wawili wa kiume, wenye rika la miaka thelathini-kila mmoja akiwa amebeba AK 47 walipotokezea.

“Simama!” mmoja wao akaamuru, huku akikoki bunduki kwa nia ya kumwogopesha Cheyaya.

Lakini Cheyaya hakubabaishwa na amri hiyo. Alifungulia riadha iliyowastaajabisha wale askari. Hawakuishia hapo, waliunga nyuma yake, yule aliyekoki akiruhusu mitupo ya risasi hewani pamoja na makelele ya kumwonya.

Walipotelea kichakani.

Wengine, waliokuwa mlangoni baada ya kusikia purukshani hizo wakaenda kuungana na wenzao. Ikawa mtafuteni, huku mitupo ya risasi hewani na pembezoni mwa usawa akimbiliao Cheyaya ikizidi kurindima.

***

Ilikuwa saa tano usiku, baada ya uchosho wa kuangalia runinga kwa muda mrefu Chiku aliamua kwenda kujipumzisha. Akazima taa, na kupiga hatua taratibu kuelekea chumbani. Kabla hajamaliza sebule aufikie ushoroba utakaomfikisha chumbani kwake, sauti ya kugongwa kwa mlango ikamkatisha mwendo. Akasimama, akatega viwambo kusikiliza kwa umakini.

Sauti iliendelea kusikika.

Uvumilivu ulivyomshinda, akaamua kuuliza, “Nani?”

“Ni mimi,” ilisikika sauti ya kiume.

“Ndiyo ni wewe. Nani?” Awamu hii Chiku alishaanza kurudi sebuleni. Nafsi ikiwa nyongefu kiasi. Ugeni wa usiku ule ni ugeni gani?

“Bosi wako.”

Kauli hii ikamwondolea hofu iliyoanza kujikumbata. Akawasha taa, akaenda kufungua mlango.

Alivyoruhusu mlango kuwa wazi, mbishaji hodi akajitokeza. Tokezo la kushtukiza lililorejesha hofu ya Chiku. Mgeni wake alijitokeza kwa kuogofya. Na kabla hajamng'amua, alisukumizwa kurejea ndani halafu mgeni akaingia kwa hatua za madaha. Hakusahau kufunga mlango. Kisha akauchukua ufunguo.

Alikuwa Jovin.

Mavazi aliyovaa yalimfanya asitambulike kwa wepesi. Alivaa koti kubwa rangi nyeusi-lililoshuka hadi magotini. Boshori nyeusi kichwani, suruali ya jinzi rangi ya bluu, buti-kasulu, pasi na kusahau glavus mikononi.

Alivyoitawala vyema sebule, alichomoa vitu fulani kwenye mifuko ya koti, akaviunganisha. Ilikuwa bastola na kiwambo. Akaendeleza hatua kuzidi kusonga mbele. Kwani Chiku alivyosukumizwa muda ule hakubaki pale sebuleni. Alikimbilia chumbani kwake.

Kwa sababu ya giza, akachukua simu yake imsaidie kupamulika alipopahitaji. Hivyo akawa anawasha na kuizima. Hadi alipoweka tuo mlango wa mwisho kwenye ule ushoroba. Kabla hajafanya chochote, akatega vyema viwambo kusikilizia kiendeleacho ndani. Alifanya hivyo kwa sekunde chache, na hakusikia kitu chochote cha kumwaminisha kuna mtu ndani. Lakini imani iliyomtawala nafsini ilimhakikishia mlengwa wake yupo humo.

Baadaye alikata shauri. Alikamata kitasa, akakinyonga. Isivyobahati mlango haukutoa mrejesho wa manufaa. Ulikuwa umefungwa. Hakupoteza muda kufikiria mara mbilimbili, akaruhusu mitupo kadhaa ya risasi mpaka kitasa kilivyokuwa nyang'anyang'a kwa kutotamanika.

Awamu hii alipokinyonga hakupata ugumu, ulifunguka. Lakini hakuingia muda huohuo. Alivuta subira kwanza. Takribani dakika moja, ndipo akapiga hatua za mnyato kuingia.

Alivyopiga hatua mbili kutoka mlango ulipo, zikamfikisha chumbani. Akauhimiza mkono ulio tupu kutafuta swichi ukutani. Hakuchukua muda kuipata. Alivyoruhusu kuwasha, hakukuwa na mapokeo ya mwanga. Kitendo kilichomsukuma awashe tochi ya simu.

Pindi ananuia kutembeza taratibu kukiangaza chumba, alishtuka kitu kizito kikitua usoni. Kabla hajafahamu ni nini, alijikuta akisukumizwa kisha msukumaji kuondoka mle chumbani. Chiku. Aliondoka kwa mbio, huku akipiga makelele ya kuomba msaada.

Kule chumbani Jovin alijitingisha kidogo kuweka mwili sawa, kisha aliondoka kwa haraka kumfuata Chiku. Alimkuta sebuleni akihangaika kupata namna itakayomsaidia kufungua mlango.

“Jamani nakufaaa. Nakufaaa mimi, nakufaaa,” Chiku alipiga makelele, chozi likimbubujika, jasho ndiyo zaidi. Wakati huo alishaacha zoezi la kugonga gonga mlango, akawa anamsaili Jovin anavyozidi kumsogelea.

Usaili wake ulijikita namna atakavyomhadaa na kupata nafasi ya kumkimbia. Sambamba na hilo, maombi yalishika hatamu, kelele alizopiga zisikike na majirani ili aje kusaidiwa. Lakini isivyobahati, hadi zinasalia hatua chahe kufikiwa hakuna tumaini lililojitokeza.

Cha kufia nini?

Akazima taa na kuchukua uelekeo ambao Jovin hakuudhibiti. Hata kabla hajamliza hatua, Jovin alishaihisi ile hila akajisogeza usawa huo. Hivyo Chiku alijikuta akigongana naye.

Alipotaka kuchukua uelekeo mwingine, Jovin aliruhusu mitupo miwili ya ngumi za uzito wa juu zikaenda kukita kwenye taya. Ule uzito, ukamsukumiza Chiku na kujikuta akiparamia sofa kabla hajaenda kujipigiza sakafuni na kutoa mguno mdogo kisha kutulia.

Kutulia kwake kukatengeneza ukimya. Uliokuja kufukuzwa baadaye na mwito wa sauti kutoka nje.

“Chiku, Chiku, Chiku,” ilisikika sauti iliyochanganyikana; ya kike na ya kiume, huku waitaji wakigonga gonga mlango kuleta msisitizo wa uitaji.

***

Cheyaya alizidi kukata chochoro, mwisho aliingia maporini na kutafuta uelekeo asioutarajia. Muda wote huo hofu ilikesha kumkumbata. Jasho likamtawala chapachapa, huku akipotezea maumivu mbalimbali aliyokumbana nayo ili ajinusuru. Kwani wahasama wake hawakumwachia. Na walitengeneza umbali mfupi toka Cheyaya alipo.

Kama hiyo haitoshi, walizidi kumfanya mwenye hofu kwa kuruhusu mitupo ya risasi hewani na pembezoni. Kuna muda zilitua sehemu aliyobandua mguu na kutimua vumbi. Lakini aliendelea kutojali. Aliuhusudu u-mbulu kwa muda, ili pumzi isimtoke.

Lakini kadri sekunde zilivyozidi kusonga mbele ndivyo nguvu na pumzi zilivyoanza kumwisha. Alipoteza nguvu miguuni, kifua kikamtaka apunguze kasi kama sio kuchukua mapumziko kabisa.

Cha kufia nini? Akatii takwa la moyo.

Pasi na kujali hali, alichukua maficho chini ya mkorosho huku akitoa mhemo juujuu.

Sekunde kadhaa baadaye, alivyojiona amerejewa na nguvu kwa kiasi fulani, alitoa simu ndogo kwenye moja ya mfuko wa suruali, akajihangaisha kubonyeza vitufe kadhaa.

Alikuwa anaandika ujumbe. Ulipokamilika, akautuma mahali.

Kitendo cha kuonekana tiki iliyoashiria ujumbe umeshaingia sehemu kusudiwa simu ikazima. Alijaribu kuiwasha lakini haukupatikana mrejesho wa maana. Haikuwaka. Jambo lililompa ghadhibiko kwa muda, baadaye akalipotezea.

Akairejesha mfukoni, kisha akaanza kuuendeleza mwendo. Awamu hii alianza kwa kutembea, alivyohisi si jambo jema kufanya hivyo ndipo mbio zilichukua nafasi. Alikimbia, muda wote mawazo mbalimbali yakimsumbua; wapi utakuwa mwisho wake ambao utamfanya awe salama, itakuaje atakapokamatwa?

Hakupata jibu, zaidi ya kumwomba Mwenyezi Mungu amwezeshe asikamatwe.

Kwa namna alivyofumbwa na zile mbio alijikuta akitokezea barabarani. Barabara ya kuelekea Masasi. Alitokezea maeneo ya machinjioni, umbali wa mita kadhaa kutoka kituo cha magari yaendayo miji mbalimbali kutoka Mangaka. Wala hakujali usalama wake, akajitoma vivyo hivyo barabarani. Lengo, avukie upande wa pili.

Mwanga mkali wa taa za gari na honi zilizosikika kwa ukaribu akiwa katikati ya barabara ndizo zilimvumbua. Akatoweshwa mawazoni, na kuletwa kwenye tukio lile. Afanyaje?

Akaduwaa kwa muda. Akatamani aelekee kote; mbele na nyuma. Lakini gari ilishamkaribia, kujitingisha kwa lolote ni kumbabaisha dereva.

Ufundi wa hali ya juu uliofanywa na dereva, kwa kufunga breki mshituko ya nguvu. Yaani alifunga na kuachia. Alifunga tena na kuachia huku akiitoa ile gari nje ya barabarani, ndiyo ikawa salimika ya Cheyaya. Na hakutaka kusubiri. Asubiri apigwe! Akageuza kurudi atokako.

Dereva alipojihakikishia gari imesimama vyema aliteremka na kuanza kumkimbiza. Kwa sababu Cheyaya hakuwa na nguvu toshelevu wala hakufika mbali, akakamatwa.

“Hivi ewe ni mjinga?” mkimbizaji aliuliza. Ulizo lililoenda sambamba na ngwara iliyomtua Cheyaya chini kama nazi.

“Unataka unitafutie mabalaa, sio?” awamu hii aliuliza huku akikitua kisigino cha mguu wa kuume mwilini mwa Cheyaya. Ambaye alikuwa amejilaza, hajiwezi kwa lolote.

“Nisamehe. Sijafanya hivyo kwa makusudi...” Cheyaya alisema na kutulia. Akafuatia kutoa mguno wa maumivu baada ya kile kisigino kutua usawa wa tumbo. Akajaribu kuunyanyua mguu, lakini hakuweza. “Usiniue brother. Niokoe. Niokoe nitoke ndani ya mji huu.”

Kauli hii ikamfikirisha yule mkimbizaji. Kiasi kwamba aliingiwa huruma iliyomshinikiza apunguze mori. Akauondoa mguu, na kunuia kumwinua.

Ilikuwa pindi yule mkimbizaji alipoanza kumwinua Cheyaya, uliposikika mvumo wa hatua za kasi zikiwasogelea walipo. Akamwacha, na kujiinua taratibu ili abaini ni ujio wa kina nani.

“Mikono juu,” amri kali ikasikika kabla hata ajawa wima vyema. Amri hiyo iliambatana na mvumo mwingine wa sauti wa kugongana kwa vyuma. Ikamfahamisha imesababishwa na nini. Ukokiji wa bunduki.

Utambuzi wa watu waliowavamia wana moto ukamfanya yule mkimbizaji anywee kidogo. Na wala hakuleta ukaidi, alitii alivyoamriwa. Cheyaya pia. Aliinuka na kusimama nyuma ya yule mkimbizaji.

“Acha kujificha nyuma ya mwenzio. Sogea hapo,” sauti ya nguvu ikaamuru kwa mara nyingine. Wakati huu walikuwa wanamulikwa na tochi zilizopo simuni.

“Ulidhani utatukimbia milele?” yule mwenye sauti ya nguvu aliendelea kusema. Walikuwa wale askari waliokuwa wanamkimbiza Cheyaya. “Eeh! Ulidhani utatukimbia milele?” Akapiga hatua kuwasogelea. Ndiyo alikuwa kiongozi wa wale askari. Mkononi alikamatia bastola.

Wengine walisimama hatua kadhaa, mitutu ya bunduki wamewaelekezea kina Cheyaya.

Alipowafikia, alimtolea mboni za utisho Cheyaya. Kutokana na hofu, akawa anarudi nyuma kwa hatua fupifupi.

“Unaenda wapi?” yule askari, ambaye ni Ocd aliuliza. “Unaenda wapi nakuuliza?” alikazia. Mkazo ulioambatana na kofi la ubapa wa bastola shavuni kwa Cheyaya.

Halikuwa kofi la kawaida. Lilirushwa kwa nguvu, kiasi kwamba Cheyaya alipoteza uhimili na kupepesuka.

“Rudi hapa,” Ocd alisema kwa mkazo wa kumwonyesha mahali kwa kusimama.

Akahamia kwa yule mkimbizaji.

“Nawe unajifanya msamaria mwema sio?” alimuuliza, huku akimsaili kwa unyali. “Una nguvu zinakuwasha na hujui sehemu ya kuzitumia sio? Sasa ngoja tukaku...” hakumalizia kauli yake, alishtuka rundo la mate likitua usoni. Akastaajabu.

“Aisee!” Ocd alisema baada ya kufuta yale mate. “Unapata wapi jeuri ya kumdhihaki kiongozi wa ki-jeshi?” akaambatanisha na mrusho wa ngumi. Lakini halikufua dafu mbele ya mkimbizaji.

Kwani aliishusha mikono yake kwa haraka na kupangua lile pigo. Ocd akastaajabu kwa mara nyingine. Kabla hajapata ufahamu mtu huyo amepata wapi ujeuri huo, ngumi nzito ikatua usoni kwake iliyozidi kumchanganya. Maana hakuisha kufumba macho na kutingisha kichwa kusikilizia pigo.

Hakuachiwa hapo, alivutwa na kupigwa kabari iliyomshinikiza aiachie bastola. Askari wenzie wakaja juu, kwa kupiga hatua za haraka alipo wamdhibiti yule mkimbizaji. Lakini kabla hawajamfikia, alichomoa bastola na kuwaamuru wale askari wasizidi kusogea mbele.

“Mkithubutu namtandika risasi huyu mbwa wenu,” yule mkimbizaji alisema huku amemwelekezea Ocd bastola kichwani.

Wale askari wakasimama. Wakati huo Ocd akifurukuta kutafuta nafuu.

Afanyaje asipoteze muda?

Akamtwanga ngumi kadhaa Ocd kichwani, lengo azidi kumpa wenge, kisha akamwachia. Wale askari wengine walivyotaka kupiga hatua wamvamie akawaelekezea bastola.

“Kwa usalama wenu, nawaamuru mwondoke,” yule mkimbizaji alisema kwa sauti iliyoshamiri ubabe.

Askari wakaingiwa hofu.

Hata Ocd naye.

Nini ajivuniacho yule mtu? Ndicho kilichowatetemesha.

“Hamjanielewa?” yule mkimbizaji aliuliza kwa mara nyingine. “We mzee, ondoka haraka na vijana wako kabla sijawachukulia hatua zaidi.”

“Hivi unajua...” Ocd alisema, kauli yake ikaishilizia kati, yule mkimbizaji alimchabanga teke mbavuni lililomshinikiza ajikunyate.

Askari wengine walivyotaka kuingilia akawaelekezea bastola kama ilivyo awali.

“Mwenye nguvu athubutu kusogea zaidi.” Akaruhusu mitupo kadhaa ya risasi ardhini hatua chache kutoka waliposimama.

Hawakukaa tena eneo lile. Walikimbia kurudi watokako huku wakiwazua namna ya kumdhibiti mpinzani wao. Kwani hawakukimbia umbali mrefu kabla hawajageuka na kuchukua maficho. Lakini mpinzani wao naye hakuwa mjinga. Walivyokimbia wale vijana, alimvuta Ocd na kumpiga kabari. Akawa anarudi naye nyuma huku akiangaza kumwangalia Cheyaya. Hakuwepo.

“Ameenda wapi huyu mjinga?” alijiuliza.

Ukomo wa hatua ulikuwa alipoegesha gari lake. Akamsukumiza Ocd barabarani, kisha akapotelea ndani ya gari na kuianza safari. Mwendo alioondoka nao haukuwa wa kawaida. Mwendo nginjanginja ili aepukane na hila za wale askari.

Alipojihakikishia yupo umbali mrefu ndipo alipunguza mwendo. Na alipata ushawishi huo baada ya kuingiwa na kumbukizi kumhusu Cheyaya. Wapi alipotelea?

Swali hili likamfanya awazue nini sababu ya kuwindwa kwake na wale askari.

“Itakuwa kuna jambo halipo vyema,” alijisemeza mwisho wa kumbukizi. Askofu Ponera.

Ndiyo. Alikuwa Askofu Ponera.

TUKUTANE TOLEO LIJALO.
 
MNYONGA TAI—04
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
MAWASILIANO: 0673056571

Magazeti mengi yaliyotoka asubuhi hiyo kurasa ya mbele yalipambwa na habari ya ‘wakurugenzi kampuni ya Cheka kufunguliwa mashtaka ya uhujumi uchumi na utakatishaji fedha.’ Waliambatanisha na picha ya Kasembe amefungwa pingu pembeni yake amezungukwa na askari waliobeba bunduki za kivita. Picha ilionesha mazingira ya kituo cha kati cha polisi Mtwara.

Miongoni mwa waliofikiwa na magazeti hayo ni kina Dorice na Pendo pale nyumbani kwao. Waliletewa na mama aishiyo nyumba jirani. Walivyosoma habari kwa kina, matokeo waliyoyatoa mwisho ni kilio. Waliangua kilio kutokana na habari jinsi ilivyoelezewa; nyakati wakurugenzi hao walivyotenda makosa.

“Haina haja ya kulia. Jikazeni,” yule mama aliyewaletea gazeti aliwaasa.

“Inauma mama. Inauma,” Dorice alisema kwa uchungu, chozi likimbubujika hasa. “Kwa nini wanawabambikizia vitu visivyokuwa na ukweli? Hawana njia nyingine ya kupata pesa mpaka wawadhulumu wafanyabiashara?”

“Hayo mambo yataisha tu.”

Pendo akaingilia kati, “Nani atakayefanya haya mambo yakae sawa? Viongozi wote wanafanana mama. Hakuna hata mmoja mwenye uwezo wa kumshika mkono mlala hoi.”

“Hapana. Wapo wenye mioyo safi, ambao wanaweza kusikiliza kero zilizowakabili.”

Pendo akamgeukia yule mama jirani, “Wepi? Na kutoka wapi? Hao unaowamaanisha wewe ni wa kutoka ndani ya...” akakatishwa na sauti ya ufunguzi wa mlango. Wote wakageuka kumwangalia mfunguzi.

Alikuwa Stella.

Wakajifuta machozi wasigutukiwe. Lakini walikwishachelewa. Stella alishahisi tatizo miongoni mwao. Wajihi ndiyo uliwatambulisha.

“Mama kuna tatizo?” Stella aliuliza, pindi akipiga hatua fupifupi kuelekea mama'ke alipoketi. Sofani.

Badala ya kujibu, Dorice alivuta lile gazeti akamtupia. Stella hakuwa na budi, alilichukua na kuanza kuperuzi. Alivyosoma kichwa cha habari tu, wala hakuwa na haja ya kuzidi kufunua kurasa zingine. Alifahamu sababu ya kupatiwa ni ile habari.

Moyo ukasinyaa. Nuru ikapotea wajihini.

“Halafu...” Stella alisema na kutulia. Akateka umakini wa wenzake. Kwani walimtupia mboni za hitajio la kumtaka aendelee kuzungumza.

“Kuna nini?” mama'ke aliuliza.

“Inasadikika Chiku ametekwa.”

“Wewe!”

“Alivamiwa jana usiku. Watu walivyoenda kumpa msaada, hawakumkuta,” Stella aliwahakikishia.

“Balaa gani sasa hili?” Pendo akaangua kilio kwa mara nyingine.

Wenzake nao wakaambukizwa, isipokuwa yule mama jirani. Akafanya kazi ya kuwatuliza.

Iliwachukua takribani dakika kumi ndipo jitihada za mama jirani zilivyozaa matunda. Walitulia, na kuwaasa waangalie namna watakayoifanya kama wanaweza kuwasaidia waume zao.

“Naamini waume zenu waliwafundisha muwe wajasiri. Hivyo sasa tumieni ujasiri waliowaambukiza kuwanusuru na hili.”

“Unadhani tutawanusuru vipi?” Dorice aliuliza.
“Kwanza nendeni mkaonane na Kasembe...”

“Halafu?” Pendo akaingilia kati.

“Mnaweza mkashauriana jambo, baada ya hapo ndipo mlichukulie hatua. Au la, mwende kwa kiongozi wa ngazi za juu wa kiserikali.”

“Hawa! Hawa wanaobebana? Unahisi watatupa haki stahiki na kuwaacha wenzao wakihangaika? Thubutu.”

“Ndiyo njia pekee za utatuzi zinazoweza kuwapa mafanikio.”

Ukapita ukimya mfupi, uliowahimiza kuwa tafakurini kwa kauli za yule mama. Zilionekana kuwaingia na kuwapa ushawishi wa kuzitekeleza.

***

Kilikuwa chumba kikubwa kilichotawaliwa na mwanga wastani kwenye moja ya jengo nje ya mtaa wa Naparavi, kama unaelekea mwambani. Hali ya ki-mazingira ndani ya kile chumba haikuwa nzuri. Kilitawaliwa na mpangilio duni wa vitu vilivyomo. Na asilimia kubwa vilikuwa sehemu ya uchafu.

Hakikutamanika kwa makazi ya namna yoyote ile. Lakini haikumzuia Jovin kumhifadhi Chiku mahali hapo. Alimfungia kwenye kiti, kisha alimbandika utepe wa gundi mdomoni ili asitoe bughudha itakayomgharimu.

Na muda wote wa uwepo wake chumbani humo Chiku alikuwa mwenye hofu. Hofu iliyoteka sehemu kubwa ya akili kuwazua nini hatma kwa sekunde ijayo. Uhakika wa usalama wake ulikuwa haba. Hakuwa na chembe ya kumwaminisha kwamba atakuwa na amani mara baada ya kutoka hapo.

Nani wa kumwokoa?

Ulikuwa mtihani kwake. Mtihani uliomliza na kukufuru zaidi ya mara mia.

Karibu na jua kutua mlango wa chumba alichopo ukafunguliwa. Mfunguzi hakuingia muda huohuo. Alijipa subira kwanza, kwa kupisha hali fulani ipotee mle ndani akaingia.

Jovin.

Chiku, moyo ukapiga kite kwa hofu. Na kwa namna alivyokuwa anatembea kwa madaha ikamfahamisha ujio huo si wa heri. Moto ndiyo unaanza kumwakia. Kwani toka alivyoletwa mahali hapo, hakuguswa, wala kumwona mwenyeji wake kwa lolote.

Alivyofikiwa, Jovin alivuta kiti, akaketi jirani naye. Mkononi kuna kitu alikikamatia, ambacho kilitoa harufu fulani iliyokosha moyo wa Chiku. Kibakuli kilicho na chakula ndanimwe.

Akamfungua ile gundi. Chiku akatoa mhemo wa nguvu.

“Ewaaah!” Jovin alisema, akimtumbulia Chiku jicho lenye utisho. “Upo sehemu salama wala usiogope. Lakini panaweza kuwa pachungu endapo utaenda tofauti na ninalolihitaji.” Jovin akatulia kwa mara nyingine. Akamsaili Chiku apokeavyo, kisha akaendelea, “Hapa pana chakula, ili ukipate, nitahitaji majibu sahihi ya maswali yangu.”

Chiku akabaki kumshangaa, hofu ikizidi kumtawala.

Ina maana asipojibu itakuaje? Atanyimwa tu kile chakula? Au kuna kitendo kingine cha ziada atakachotendewa?

“Nadhani umenielewa?” Jovin akamgutusha. Lakini Chiku hakufungua kingo zake kuzungumza jambo, kitendo kilichozalisha ukimya kwa sekunde kadhaa.

Karibu na ukimya kushika hatamu, Jovin akaufukuza, “Unakumbuka chochote ile siku mliyofungiwa ofisi?”

Chiku akashtuka. Mapigo ya moyo yakamwenda kasi na kurejesha kumbukizi siku pasa aliyotajiwa pindi akiteta jambo na Cheyaya ofisini kwake. Mwisho wa hilo, alikumbuka sehemu aliyohifadhi vile vitu alivyokabidhiwa nyumbani kwake.

“Kuna vitu ulikabidhiwa na bosi wako. Ndivyo ninavyovihitaji.”

Chiku akaendeleza kawaida, ya kutofungua kingo za mdomo kuzungumza. Jovin akaona isiwe shida, akainuka kitini na kuondoka. Kile chakula akaenda kukitua mezani, mita kadhaa kutoka Chiku alipo.

***

Ni asubuhi, yapata saa tano, pindi Dorice, Pendo na Stella walipowasili kituo cha kati cha polisi Mtwara. Wakapokelewa kaunta na askari polisi wa kiume mwenye cheo cha Koplo. Hakukuwa na purkushani nyingi za wahudumiwa.

“Niwasaidie nini?” yule askari aliuliza.

“Tumekuja kumwona ndugu yetu,” Dorice alisema, wakati huo moyo ukimpwita pwita. Hata wengine walikuwa wamekaa ki-wasiwasi. Woga wa kufika kituo cha polisi, ukizingatia ndiyo mara ya kwanza. Halafu kosa lililosababisha mtu wao ashikiliwe ni la kuogofya zaidi.

“Nani kawaambia hii ni sehemu ya kuonana? Au mumemletea chakula?” yule askari aliwakoromea.

“Kuna ndugu yetu anashikiliwa hapa toka jana, anaitwa Kasembe.” Dorice akalichukua lile gazeti, lionyeshalo picha ya Kasembe akamwonyesha yule askari. “Huyu hapa.”

Yule askari akaitathmini ile picha, kisha akamwangalia Dorice. “Kwa hiyo mnatakaje?” akauliza.

“Tuonane nae. Tuna jambo tunahitaji tuzungumze nalo, tafadhali tunakuomba.”

“Hatuna mtu wa namna hiyo hapa kituoni kwetu.”

“Afande, hizi picha si zinaonyesha kabisa ni mazingira ya hapa.”

“Unataka kunifundisha kazi? Njoo vae hizi nguo. Njoo vae,” yule askari akamkoromea na kumtolea jicho la utisho. “Nendeni mkamtafuteni sehemu nyingine sio hapa.”

“Afande.”

“Ondokeni,” akapigiza mikono yake juu ya meza.

Nguvu ya lile pigizo likawatetemesha na kuwashinikiza kurudi nyuma hatua moja.

“Sitaki kuwaona hapa,” yule askari alisema na kupotelea ndani ya moja ya chumba.

Hawakuwa na budi, walijiondoa taratibu huku mboni zikiruhusu machozi kuwatiririka. Matokeo waliyokutana nayo hayakuwa tarajiwa. Japo walikwishayahisi hapo awali.

Ukomo wao ulikuwa nje ya jengo ya kile kituo. Chini ya miti kando ya barabara ya kuelekea ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara. Wakaketi hapo, na kuzidi kuangua kilio. Iliwachukua takribani dakika nane, ndipo wakaja kutulia. Huku wakiamini wameutua kiasi uchungu walionao.

“Kwa nini tusiende kwa wakubwa wao?” Stella aliuliza.

“Si lazima tupelekwe na hawa. Sasa unadhani watakuwa ridhaa kuturuhusu?” Dorice alijibu kwa mtindo wa swali.

“Sasa tutalia mpaka saa ngapi mama? Inabidi tupate utatuzi.”

“Mi'nashauri tuende kwa viongozi wa ki-serikali; aidha Mkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa,” Pendo alishauri.

“Mkuu wa wilaya ipi?”

“Wa hapa mjini.”

“Mmmh!” Dorice aliguna na kutulia kwa sekunde kadhaa. Alionekana kufikiria jambo, alivyolipatia ufumbuzi aliendelea, “Bora kwa Mkuu wa Mkoa. Hao wa ma-wilayani hawana maana.”

“Basi twendeni,” Stella alisema, akiwa ameshainuka.

Baada ya muda walifanya walivyokubaliana, walijiondoa kituoni kwa mwendo mdogomdogo. Kwa sababu hakukuwa na umbali mrefu, haikuwachukua muda mrefu kuwasili. Wakafanya mizunguko ya hapa na pale kisha waliangukia ofisini kwa msaidizi wa Mkuu wa Mkoa.

“Mna miadi naye?” msaidizi wa Mkuu wa Mkoa aliuliza.

“Hapana. Lakini shida yetu ni ya muhimu sana kuonana naye,” Dorice alijibu.

“Haitofaa kwa leo, ukizingatia muda umeshaenda sana na mkuu ana wageni ofisini kwake.”

“Tafadhali, naomba utusaidie. Tumetoka Mangaka kuja kuelezea shida yetu kwake, tusaidie,” Pendo alikazia.

“Kwa leo ni ngumu.”

“Jaribu kutuonea huruma. Jaribu kuvuta picha umbali tuliosafiri kwa ajili ya kutafuta nafasi hii.

“Sina msaada mwingine zaidi ya nilichokizungumza.”

“Mama! Hebu tuonee huruma. Hata dakika moja tu, sisi itatutosha kuelezea kilichotusibu. Kama hiyo haitoshi, tukishindwa kuingia wote, ruhusu basi japo mmoja.”

“Sitorudia kuongea nilichowajibu. Au niwaitieni walinzi?” msaidizi wa Mkuu wa Mkoa; m-mama, aliyepambwa kwa umbo nene wastani, mweupe- mfupi alisema, wajihi umekunja ndita kukasirishwa na hali iendeleayo mbele yake.

Neno walinzi likawatisha kina Dorice. Wakajiondoa kiunyonge, kuta za mioyo yao ikikumbatwa na tamanio la kuangua kilio. Walitamani waendelee kulia, watue masahibu wayapitiayo.

Walivyofika nje, hawakujihangaisha kutoka kwenye uga uzungukao jengo la ofisi hiyo. Waliangaza huku na kule, wakaweka tuo eneo la maegesho ya vyombo vya usafiri. Hasa kwa maafisa wa ofisi hiyo. Kilichowavuta wakakae hapo ni moja ya gari waliloliona. Gari la Mkuu wa Mkoa.

“Akitoka tu, tusipoe. Tumvae vae hadi atuelewe,” Dorice alishauri.

“Asipotuelewa?” Stella aliuliza.

“Tutajua nini cha kufanya papo hapo.”

Ilichukua takribani dakika arobaini toka walivyokubaliana, mkusudiwa wao akatokeza ndani ya ofisi kuelekea walipo. Mkuu wa Mkoa; m-mama wa makamo, kadirio la rika ni miaka hamsini na ushee, mnene-mweupe.

“Anakuja,” Stella akawajuza wenzie.

Wakajisogeza karibu na gari.

Ilikuwa pindi msaidizi wa Mkuu wa mkoa anafungua mlango, pale Dorice alivyopiga magoti chini na kukamata miguu ya Mkuu wa mkoa akaanza kumlilia. Kilio kilichoambatana na kauli za uchungu kuyatema yaliyomo moyoni.

“Tunahitaji msaada wako mkuu. Tusaidie, kwani tumekuja muda mrefu lakini msaidizi wako akatunyima nafasi ya kuonana nawe...”

Mkuu wa mkoa akajitingisha kidogo mguu na kumfanya Dorice apepesukie umbali mfupi. Dereva akasaidia kwa kusukuma sukuma Pendo na Stella.

“Hebu ondokeni. Kama mna shida si mngelikuja kwa staha,” dereva alisema.

Mkuu wa mkoa akadakia, “Na mumekuja hapa kama nani?” Awamu hii alikwishaingia ndani ya gari.

“Kama wahanga mkuu. Viongozi wa chini yako wanadhulumu haki zetu bila sababu.”

“Mumeshafikisha malalamiko yenu kwa viongozi wa wilaya?”

“Hatuwaamini. Hao hatuwaamini ndiyo maana tumekuja kwako,” Dorice alijibu. Alikwishajiinua muds tu, na sasa walizonga mlangoni, usawa alioketi Mkuu wa mkoa.

“Hamuwezi kuvuta hatua. Rudini kwao wawasikilize, wakishindwa, wao watawasilisha kwangu.”

“Tafadhali, tunaomba...” Dorice alisema, lakini hakuhitimisha kauli yake, akakatishwa na Mkuu wa mkoa.

“Dereva ondoa gari.”

Dereva alitii. Aliondoa gari kwa mwendo wa wastani, walipofika getini akasimamisha.

“Walinzi,” Mkuu wa mkoa aliita.

“Naam, mama,” sauti ya kiume ilisikika kutoka bandani (sentry box).

“Waondoeni wale watu pale haraka iwezekanavyo.” Waambiwa wakaangaza walikoelekezwa.

Gari iliendelea na safari, kisha walinzi wawili, waliongozana kuwafuata kina Dorice walipo.

***

Timu ya CAT (counter assault team) na CT&HR (counter terrorist & human rescue) ziliunganishwa pamoja na kuwa chini ya ofisi ya Fadhy Njau-Afisa mwandamizi ahusikaye na operesheni ndani ya Idara ya usalama wa Taifa. Kilichochangia muunganiko huo ni weledi wa kazi walizokwishafanya kipindi cha nyuma (riwaya ya Afrika Yangu) nchini Burundi.

Weledi huo ulimshawishi Rais, kiasi kwamba akamkaimisha mamlaka Fadhy ya kushughulikia operesheni mbalimbali; ndani na nje ya nchi zitakazoifanya Tanzania inabaki kuwa salama. Operesheni hizo pasi na kujalisha utaifa na wadhifa wa wahusika wa utendaji wa uhalifu.

Hivyo ule ujumbe uliotumwa na Cheyaya ulimfikia Fadhy. Wakati huo alikuwa amelala. Sauti ya mwito ikamshtua, kabla hajapiga hatua kuifuata simu ilipo, alijinyoosha kuweka viungo sawa kisha akajiinua.

Aliihifadhi juu ya meza, iliyopo umbali wa mita moja na nusu kutoka kilipo kitanda.

Fadhy na Cheyaya ni ndugu-waliochangia baba.

“Kaka, nipo matatizoni. Nahitaji msaada wako.”
Ndivyo ulivyosomeka ujumbe. Na kumfanya abadilike ghafla, kwani si sura, wala moyo; vyote havikutuliana.

Baadaye aliamua kumpigia simu Cheyaya, kutaka ufafanuzi wa ule ujumbe. Lakini isivyobahati, hakupatikana. Hata alivyofanya kwa mara nyingine, matokeo hayakubadilika.

Cha kufia nini?

Akajirudisha kitandani. Lakini hakupata amani katu. Ule ujumbe ulizidi kumsumbua kwa kuutafakari na kuvuta picha aina ya matatizo anayokumbana nayo Cheyaya. Akampgia tena.

“Nini shida ndugu?” akamtumia ujumbe baada ya Cheyaya kuendelea kutopatikana.

Asubuhi kulipopambazuka alielekea kazini. Kabla hajafanya jukumu lolote la ki-kazi, akampigia Cheyaya. Hali kadhalika, aliendelea kutopatikana.

Akastaajabu.

Na kumpa shinikizo la kuumba matukio mbalimbali. Matukio yaliyomchukulia furaha yake kwa kiasi fulani.

Tulizo la ile hali, akaamua kupitia magazeti yaletwayo ofisini kwake kila siku. Ilikuwa kawaida kupitia habari za magazetini ili afahamu yaendeleayo ulimwenguni. Magazeti hayo huwasilishiwa ofisini kwake na binti wa masjala.

Lilikuwa gazeti la pili kulikamata, aliposoma tu kichwa cha habari ukurasa wa mbele, akili ikahama na kupatwa kumbukizi ya ule ujumbe kutoka kwa Cheyaya. Kabla hajasoma habari kiundani, akampgia tena Cheyaya. Hakupatikana.

Akarejesha umakini gazetini. Aliisoma ile habari hadi mwisho, kisha alifuatia na magazeti mengine, alipomaliza, aliruka hewani kwa shemejiye, Dorice.

“Mambo yapo sawa shemeji?” Fadhy aliuliza, pasi na hata salamu.

Dorice alijibu sauti ikiwa nyongefu, na kwa mbali kukiwa na ambatano la kilio, “Hali sio nzuri shemeji. Tuna matatizo. Tuna matatizo makubwa sana, kiasi kwamba hatufahamu tutakavyojinasua.”

“Nimeona habari gazetini. Nikimpigia simu ndugu, hapatikani.”

“Ni vigumu kupatikana. Hao wanamamlaka wenu...” akakatishwa kabla hajahitimisha.

“Fanya uje Dar es salaam, tuone namna utakavyosaidiwa.”

“Sawa. Nitakuja na wenzangu; Stella na mke wa mshirika wa nduguyo.”

“Hamna shida. Cha muhimu...”

“Ndiyo.”

“Msimweleze mtu yeyote juu ya safari hiyo.”

“Sawa shem.”

Fadhy akakata simu.

***

Dorice, Stella na Pendo waliwasili jijini Dar es salaam jioni ya siku iliyofuata. Kwa sababu haikuwa mara ya kwanza kwa Dorice kufika nyumbani kwa Fadhy, aliwaongoza wenzie uelekeo wanaopaswa kuuchukua. Waliondoka kituo cha mabasi kwa teksi ya kukodi.

Walipowasili, Fadhy akawalaki kwa bashasha.
“Karibuni sana, na poleni kwa uchovu wa safari.”

“Mmmh! Hata kuna kupoa shem kwa namna mambo yalivyotukaba kooni?” Dorice alijibu kwa mtindo wa swali.

“Tutayaweka sawa tu, ondoeni hofu,” Fadhy aliwatuliza.

“Mmmnh! Sina uhakika. Tutawaweza kweli hawa wenye mamlaka?” Akatua begi na kujitupia sofani.

Wengine vivyo hivyo.

Baada ya kupata chakula na mapumziko kwa muda, usiku, Fadhy aliwakusanya sebuleni wakafungua uwanja wa mazungumzo kuhusu kusudio lililowafungisha safari. Dorice alihadithia mkasa mzima. Alihadithia kuanzia Cheyaya na Kasembe walivyopata wazo la kujitolea hadi walivyogeuziwa kibao cha kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi.

“Ina maana wanahitaji fedha?” Fadhy aliuliza, mara baada ya Dorice kuhitimisha simulizi.
“Ndiyo.”

“Mnawafahamu kwa majina au sura?”

Ukapita ukimya mfupi uliotanabaisha waulizwa wanatafakari jambo.

Pendo akaufukuza, “Hapana. Lakini ni haohao wanaojifanya viongozi wakuu wa wilaya. Hamna wengine.”

“Kwa nini mnawahisi wao?”

“Aaah! Shem, kwani kuna wengine wenye mamlaka ya kumpatia mtu kesi ya uhujumu uchumi zaidi yao?”

“Okay, tutasaidiana kutafuta suluhu.”

“Na iwe hivyo shem. Kwani ukiachana na hilo la nduguzo, kuna binti alikuwa mfanyakazi wao naye amepotea katika mazingira ya kutatanisha. Sisi tunahisi inahusiana na hili.”

“Anaitwa nani?”

“Chiku,” Dorice alijibu. Akakazia kumwelewesha mwonekano wa Chiku ufananavyo. “Wasaidie nduguzo shemeji. Hawana makosa yoyote. Tafadhali tunakuomba, fanya jambo. Fanya jambo uwaokoe.” Machozi yakamlenga.

“Nimewaelewa. Nawaahidi kulifanyia kazi,” Fadhy aliwahakikishia, kisha kuwasaili mmoja baada ya mwingine. Kilikuwa kitendo cha kuwapima, wame-mwelewaje?

TUKUTANE TOLEO LIJALO.
 
MNYONGA TAI—05
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
MAWASILIANO: 0673056571

Kasembe alipandishwa kizimbani, katika mahakama kuu Mtwara. Watu wengi wakahudhuria, kwani kile kilichotolewa magazetini kilivuta macho na bongo za wengi wafahamu hatma yake.

Kwa taratibu, na kwa sababu ndiyo ilikuwa mara ya kwanza, mahakama ilisikiliza maelezo ya upande mmoja-wa jamhuri. Mwendesha mashataka akafanya kazi ya ziada kuelezea watuhumiwa; Cheyaya na Kasembe walivyotenda makosa yao kiasi cha kuisababishia hasara serikali. Kasembe akabaki kutokwa machozi tu, kwani juu ya wingi wa maelezo yote yalijaa uongo.

Mwendesha mashtaka alivyohitimisha uelezeaji, Jaji akaamuru jeshi la polisi lifanye jitihada limtafute mtuhumiwa mwingine-Cheyaya, ajumuishwe kwenye kesi.

Hakuna mpinzani aamuapo, zaidi ya utii. Kesi ikaghairishwa, kisha Kasembe akarudishwa mahabusu.

***

Ni asubuhi, Fadhy alipokutana na washirika wake. Vijana wa kazi waliopo chini ya ofisi yake; Luteni Ringo, Pte Bayo na Pte Pemba. Kwa ujumla walikuwa katika mwonekano wa kiraia.

“Kuna moja la muhimu lililonisukuma nihitaji uwepo wenu mahali hapa muda huu,” Fadhy alisema.

Waambiwa wakawa makini kumsikiliza.

“Pindi nakabidhiwa hili jukumu Rais alinipatia maagizo, kwa namna yoyote ile nihakikishe usalama unatamalaki ndani. Kusitokee tukio, hata kama ni ndogo tukalipuuzia.”

“Lipi lililochachafya?” Luteni Ringo aliuliza.

Badala ya kujibu kwa kauli, Fadhy alifungua saraka akatoa gazeti na kulipigiza juu ya meza waliyoizunguka. “Awamu hii ni kazi ya ndani.” Akakazia.

Luteni Ringo akalivuta lile gazeti, akaperuzi. Alivyomaliza, alimsambazia mwenzie-hadi walivyomalizika.

“Kazi ipi hapo inayopaswa kushughulikiwa?” Luteni Ringo aliuliza.

“Kuna fukuto huko Mangaka wilayani Nanyumbu, mkoa wa Mtwara, ambalo tukilifumbia macho litaharibu picha nzuri ya Taifa letu. Inatubidi tulifanyie kazi kwa haraka mno kabla halijazidi kuchukua nafasi kubwa.

“Sakata la hao wafanyabiashara wa Cheka; Cheyaya na Kasembe, linachafua taswira ya nchi. Si wao tu, kuna wafanyabiashara wengi wafanyiwavyo hivi, na hakuna mamlaka yoyote inayowasaidia zaidi ya kuwakandamiza. Sasa mimi nataka kulivalia njuga hili swala tulete uhakika wa haki kwa wafanyabiashara.”

“Una sababu zinazokuaminisha kuna uonevu katika hili? Au mzee amekupa amri ya kuchunguza?” Pte Bayo aliuliza.

“Alinitaka nifanye mambo yatakayoifanya nchi inakuwa salama, hili ni moja wapo. Hivyo jiandaeni kwa kulifanyia kazi mara mwondokavyo hapa.” Fadhy akainuka na kuwaacha vijana wake wasijue nini cha kuamua. Akapotelea ofisini kwake.

Huko alivuta kiwambo cha simu ya mezani, akabonyeza vitufe kadhaa kisha kukisogeza sikioni. Haikuchukua muda, sauti ya upande wa pili ikaunguruma.

“Askofu!” Fadhy aliita.

“Yes, Chief.”

“Huduma yako inahitajika.”

“Wapi?”

“Mangaka.”

“Kuna tatizo gani?”

“Kuna binti anaitwa Chiku, amepotea katika mazingira ya kutatanisha siku kadhaa zilizopita katika mji tajwa. Namwihitaji huyo binti upenuni mwangu akiwa hai.”

“Ina uharaka kiasi gani?”

“Iwe zaidi ya haraka. Kwani naiaminia sana intellijensia yako.”

“Sawa Chief.”

Fadhy akarejesha kiwambo mahali pake.

***

“Kwa hiyo hajakenua kabisa mdomo kuzungumza jambo?” Nalimuka aliuliza, akiwa na Jovin nje ya chumba alichohifadhiwa Chiku. Wakati huo Jovin alikuwa anajihangaisha na ufunguaji wa kufuli.

“Hajazungumza. Lakini hiyo isitusumbue, kwani huyu ni mtoto wa kike, hana uvumilivu kiasi hicho,” Jovin alijibu.

“Inabidi atuambie jambo huyu binti kuhusu yule Cheyaya. Maana kwa taarifa nilizopatiwa na wapashnaku wangu wake wa wale wafanyabiashara wameonekana Mtwara mjini wakiomba msaada kwa viongozi.”

“Kwa nilivyomnadhiria, naamini muda huu lazima afunguke.”

“Haina haja ya kutumia kiasi kingi cha nguvu kwa hapa mwanzo. Ukaidi ukizidi, hapo ruksa kutumia namna yoyote ile, ili tupate tukitakacho.”

Mlango ulivyofunguka, Jovin akawasha taa, wakafuatia kuingia. Kabla hawajamsogelea alipo, walisimama pale mlangoni kwa sekunde kadhaa, walimtathmini mtu wao, waliporidhishwa, wakapiga hatua za madaha kumfuata.

“Mrembo,” Nalimuka aliita, pindi wakichukua nafasi ya kuketi vitini. Hatua chache toka alipo Chiku.

Chiku akawatolea jicho la husda. Lakini wao halikuwateteresha.

“Binti huitaji uhuru?” Nalimuka aliuliza kwa mara nyingine.

Chiku akaendeleza kawaida.

“Kuna jambo nataka utusaidie. Ukifanya hivyo, tutakuachia huru. Tunataka kile ulichoachiwa na kuambiwa na Cheyaya.”

“Sina nilichoachiwa,” Chiku akajibu kwa sauti ya jeuri.

“Sikia binti, hatuna mzaha katika hili...”

Chiku akamkatisha, “Nami sina mzaha katika majibu yangu.”

Nalimuka akainuka na kuminya mashavu ya Chiku. Hakuishia hapo, akamtingisha kichwa kwa sekunde kadhaa, alipomwachia, ni kiwewe tu ndicho kilishamiri wajihini kwa Chiku.
“Mkiweza mniue kabisa,” Chiku akapayuka, wakati huohuo kilio kikichukua hatamu.

Pindi Chiku anapunguza uchungu Nalimuka na Jovin waliinuka kitini wakasogea pembeni.

“Tunafanyaje? Ukizingatia familia nayo imeshaanza kuhangaika huko kutafuta msaada,” Nalimuka alieleza wasiwasi wake.

“Hamna namna nyingine zaidi ya kuwapata,” Jovin alijibu.

“Ni sahihi. Sasa tunawapataje na huyu chawa haonyeshi ushirikiano nasi? Au uende nyumbani kwa huyu binti ukafanye ukaguzi? Maana sina amani kabisa.”

“Nami nilifikiria hilo.”

“Basi fanya kwa haraka. Tena hakikisha unakagua kila kona.”

“Hamna shida bosi.”

***

Kama ilivyo jadi ya wana-intellijensia; Askofu Ponera alipowasili Mangaka hakutuliza damu, alianza kutekeleza jukumu alilokabidhiwa siku hiyohiyo. Makazi, yalikuwa kwenye nyumba ya kanisa kama ilivyo ada. Kwa sababu alishatumiwa taarifa chache za mhusika, haikumuwia ugumu kufikia makazi ya Chiku.

Kwa nyakati tofauti, alipanga ratiba iliyomwezesha kutembelea na kusaili makazi hayo. Kila lililompa shaka hakuacha kuliandika pembeni kisha kulifanyia kazi wakati unaofuata. Yote, apate kitu chenye uhakika kitakachokamilisha jukumu kwa haraka. Kwani sambamba na la Chiku, aliamriwa kwa mara nyingine afanyie kazi sakata la kina Cheyaya kufungiwa ofisi yao kisha kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi.

Alivyohoji kwa nini?

Jibu la Fadhy lilikuwa fupi tu, “hakuna anayepigania haki za wafanyabiashara serikalini.”

Hivyo jioni moja, akiwa umbali wa mita kadhaa kutoka nyumba aishiyo Chiku, mboni kupikupi-kupikupi kuangaza pande mbalimbali alibahatika kumwona kijana mmoja akinyemelea kuingia. Alikuwa Jovin. Akamwekea umakini.

Haikuchukua dakika tano, yule kijana alipotelea ndani. Kitendo kilichoshtua mapigo ya moyo kidogo kwa Askofu Ponera na kumpa mashaka. Mashaka yaliyomtaka azidi kuwa makini asipotelewe mara Jovin atakavyotoka ndani. Alitaka kuanza naye, kwani kupitia yeye aliamini atapata akitakacho- kumkomboa Chiku, na taarifa za ndani za mahasimu wa kina Cheyaya.

Jovin alitumia takribani robo saa mle ndani. Alivyotoka, akawa amekamatia yale mafaili aliyokabidhiwaga Chiku. Mwendo wa awamu hii ukiongezeka kidogo tofauti na wakati wa uingiaji. Alipiga hatua ndefundefu zenye kasi zilizoashiria anataka kuliacha eneo hilo kwa haraka.

Askofu Ponera hakushtushwa na huo mwendo. Alimpiga picha kwa kutumia kamera ya kijasusi, kisha alimsubiri alipoufikia umbali fulani, takribani mita arobaini, ndipo alitekenya gari akafuata nyendo zake. Mbele, Jovin aliingia ndani ya gari na kutimua vumbi. Alivyoongeza mwendo, Askofu Ponera naye alifanya vivyo hivyo.

Mwisho wa safari ulikuwa mtaa wa Nampungu. Jovin aliegesha gari kwenye moja ya nyumba yenye hadhi ya ufahari, akapotelea ndani. Askofu Ponera aliipita kidogo tu ile nyumba, akasimama. Hakuwa mwenye papara, aliteremka, akapiga hatua ndogondogo kurudi atokako. Lengo awe karibu na lile jengo.

Alivyoridhishwa na umbali alioutengeneza, alipiga picha ile nyumba na mazingira jirani, kisha alizituma zote; imwonyeshayo Jovin, na ya sasa, akamtumia Fadhy.

“Fanyia kazi, kwa uchunguzi zaidi,” aliambatanishia kauli yenye msisitizo.

Mle ndani, kwenye ile nyumba, Jovin alikutana na Nalimuka. Akamkabidhi yale mafaili, baada ya hapo kila mmoja alichukua uelekeo wake. Kwani hata kusemeshana, hawakusemeshana. Yalikuwa makutano ya muda mfupi sana. Jovin alirejea garini, akaendelea na safari.

Askofu Ponera akazidi kumfuatilia.

Mara hii Jovin alielekea nyumbani kwake. Alivyopotelea ndani na kuona anakawia, Askofu Ponera aliteremka garini, akapiga hatua nyemelezo, mboni amekaza huku na kule kusaili mazingira kwa umakini. Kilichomshawishi kufanya hivyo ni kupata taarifa za kina zimhusuzo Chiku. Alijua, kwa namna yoyote ile, kijana huyo kipo anachokijua ndiyo maana amevamia nyumba ambayo ipo chini ya uangalizi.

Alipofikia mlango, alipapasa mgongoni kuhakikisha uwepo wa kitu fulani. Baada ya hapo aliweka tuo kiambazani, kama nusu mita kutoka mlangoni. Alisikilizia kwa muda, aliponuia afanye jambo litakalomfanya awe ndani, alisikia purkushani zilizomteka azifuatilie kwa makini. Baadaye akafahamu, zinatokana na mlango kufunguliwa.

Sekunde kadhaa baadaye mlango ukafunguliwa. Kabla mtu hajajitokeza, sauti ya kidume ikaunguruma. Wakati huohuo ya kike ikilalamika. Alikuwa analia.

“Hebu jikaze, kulia hakutokusaidia kwa namna yoyote ile, maana tulikupa nafasi ya kujinusuru kwa kushirikiana nasi ukazembea. Sasa hauna faida, kwani tumepata tulichokuwa tunahitaji kutoka kwako. Hivyo mwombe Mungu akupeleke vizuri katika makao ya wafu.”

Haikuchukua muda mrefu, Askofu Ponera akakishuhudia kitendo kilichompa huruma. Moyo ulisinyaa kwa muda, kwa kutoamini alichokishuhudia. Alimwona yule mwanamke akitoka ndani kwa mtindo uliompa taarifa kuwa amesukumwa. Halafu alipofikia, akaanguka. Akakosa nguvu za kujiinua kwa haraka.

“Hiyo ndiyo dawa yako mjinga wee,” Jovin alisema, akiwa ameshatoka ndani, anafunga mlango.

Alivyogeuka tu, mara baada ya kufunga mlango ili amfuate yule mwanamke-ambaye ni Chiku pale alipoangukia, ndipo Askofu Ponera alipojitokeza. Alijitokeza kwa mrusho wa ngumi iliyoenda kukita kichwani kwa Jovin.

Kutokana na nguvu ya ule mrusho, na ukosefu wa matarajio ya kitendo hicho, Jovin aliyumba kidogo kisha akatazamia pigo lilipotokea. Akastaajabu. Lakini kabla hajapata ung'amuaji, Askofu Ponera alirusha teke lililokusudiwa likatue usawa wa mbavu. Jovin akaliona. Akalidaka na kumsababishia Askofu Ponera apoteze uhimili.

Akaanza kumzungusha.

Askofu Ponera akisimamia mguu mmoja, mikono ikiyumba huku na kule kutafuta sehemu atakayojishikiza. Hakufanikiwa, akakatwa ngwara iliyomtupa chini kama papai lililooza. Lakini hakuruhusu uzembe, alijiinua kwa haraka akamkwida Jovin na kusukumizana mpaka ukutani. Huko akapata wasaa murua wa kumfanyia Jovin kila alichokihitaji.

Alianza kwa kumwangushia makonde mazito sehemu mbalimbali za mwili, akafuatia pigo la kichwa kabla hajamalizia na miguu kwa pigo la goti. Wakati wote huo Jovin alisulubiwa na maumivu yaliyofunga akili kwa muda. Alipokuja kuzinduka atajiokoaje, ni baada ya pigo la goti lililotua tumboni usawa wa kitovu. Hapo akafahamu, akizembea, atapigwa kwenye miliki ya jinsia na hatimaye akamatwe kama kuku mwenye kideri.

Kwa sababu mikono ilikuwa huru, mmoja wapo akauelekeza nyuma usawa wa kiunoni, akachomoa kitu-bastola. Alivyokimiliki vyema mkononi, alijitutumua akapata nafasi kidogo ya kumsukuma Askofu Ponera. Ikamsaidia, hakukawiza, alikoki bastola na kuruhusu mtupo wa risasi.

Kilikuwa kitendo cha ghafla mno, lakini Askofu Ponera alifanya bidii ya kujihadhari, kwa kuhama eneo kisha kupambanua mbinu itakayomdhibiti Jovin. Naye alichomoa bastola na kuruhusu mitupo kadhaa ya risasi. Isivyobahati, risasi zilipita kapa. Tena milimita chache kutoka alipo Jovin. Lakini mtupo wa Jovin ulikuwa wenye shabaha, Askofu Ponera alipatwa na risasi ya bega.

Sauti ya mshindo ikamtetemesha Jovin na aukimbie uwanja wa mapambano. Bastola haikuwa kitu, kama mwili umetawaliwa maumivu na ukosefu wa nguvu.

***

Askofu Ponera na Chiku walibisha hodi moja ya chumba nyumba ya kulala wageni iitwayo Meswaki. Hali yao haikuwa na uridhisho, kuvuja damu kwa wingi kulimfanya Askofu Ponera apoteze nguvu, ilhali njaa na kifungo kikimdhoofisha Chiku.

Askofu Ponera aligonga mlango mara kadhaa, kisha alijitambulisha.

Mlango ukafunguliwa. Nao wakaingia.

“Nini shida?” mfunguzi wa mlango aliuliza, Luteni Ringo.

“Katika jitihada za upambanaji wa uokozi wa huyu binti, mpinzani wangu alifanikiwa kunichapa risasi,” Askofu Ponera alijibu.

“Oooh, pole sana,” Luteni Ringo alimliwaza huku akipiga hatua hadi yalipohifadhiwa mabegi yao; hakuwa pekee, aliambatana na Pte Bayo na Pte Pemba.

Alitumia dakika chache kufanya jambo kwenye moja ya begi kati ya mabegi matatu yaliyopo. Akatoka na ki-boksi kilicho na utambulisho wa huduma ya kwanza. Akarejea walipo wenzie. Akaanza zoezi la kumshughulikia. Wakati Pte Bayo akiondoka kutafuta chakula kwa ajili ya Chiku.

Baada ya mihangaiko kukamilika; Askofu Ponera kutibiwa, na Chiku kupata chakula, walipatiwa muda wa kupumzika. Walivyotoshelezwa, walifungua uwanja wa mazungumzo.

“Sasa kuna jambo la kufanya ili tuwaweke karibu waovu na kujitengenezea urahisi wa kuwakamata.” Luteni Ringo alisema. Wengine wakitega umakini kusikiliza.

“Taratibu za wahalifu tunazifahamu, lindo lao lisipotoa matokeo tarajiwa, hawaachi kulinyemelea kwa ajili ya kutimiliza kiu yao kwa mara nyingine,” Luteni Ringo aliendelea kuwapa mikakati huku akiwasaili wapokeavyo.

“Daima huwa hivyo,” Askofu Ponera alichangia hoja.

“Hivyo basi, huyu binti...” Chiku akageuka na kumwangalia Luteni Ringo, wakati huo mapigo ya moyo yakimbadilika. Luteni Ringo akaendelea, “Nataka atusaidie jambo.”

“Lipi?” Chiku aliuliza, akiwa vilevile amemtumbulia mboni zilizojaa hofu Luteni Ringo.

“La ukamataji wa hawa watu.”

“Nyie wapumbavu nini? Msitake kucheza na maisha yangu,” Chiku alisema kwa ukali.

Ukapita ukimya kwa muda, uliotoa picha kila mmoja anaitafakari ile kauli ya Chiku. Hasa neno wapumbavu.

“Tumekuja kufanya maisha yenu yawe yenye amani, hivyo ni wajibu kutii kwa utekelezaji,” Luteni Ringo aliufukuza.

“Siwezi. Nataka nikaihimarishe afya yangu kwanza.”

“Utaifanya hii kazi punde afya yako itakavyokuwa imara. Kazi yenyewe ni kutembelea nyumbani kwa Cheyaya.”

“Hapana,” Chiku alisema kwa sauti iliyojaa mkazo, huku akijiinua pale alipoketi na kupiga hatua za haraka kuelekea mlangoni.

Lengo aondoke.

Lakini alivyoshika kitasa na kuuvuta mlango akabaini umefungwa.

“Njooni mfungue hapa niondoke.” Akawatolea jicho kali.

“Sikia binti,” Luteni Ringo akainuka. “Tupo hapa kuhakikisha rejesho la vitu vyenu; amani, shughuli mlizokuwa mnajihusisha nazo, hivyo utake, usitake, hili jukumu lazima ulifanye.”

Chiku akanywea.

Luteni Ringo akaendelea kuongea, “Na jukumu lako katika hili sio kubwa, kama nilivyosema, ni kutembelea tu nyumbani kwa Cheyaya, wakati huo sisi tukiwa mahali tukikufuatilia. Hautokuwa peke yako.”

Chiku na Luteni Ringo wakatazamana. Awamu hii, kama alishaanza kuuelewa mkakati hitajika. Lakini lipo lililompa hofu kiasi kwamba baada ya muda alianza kutiririkwa na machozi.

Luteni Ringo akamsogelea, akamkumbatia, kisha akampapasa taratibu mgongoni kumtuliza. “Usiwe na hofu, tumekuja kwa ajili ya kuweka mambo sawa. Tutakulinda kwa gharama yoyote ile katika hili.” Akajiondoa kwenye kumbatio. Akazidi kumsaili Chiku. Akaishuhudia hofu ikijihimarisha wajihini. Hali ya sitaki-nataka.

TUKUTANE TOLEO LIJALO.
 
MNYONGA TAI—06
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
MAWASILIANO: 0673056571

Ilikuwa jioni, Fadhy alivyojumuika na kina Dorice, Pendo na Stella ndani ya ukumbi wa ofisini kwake. Kwa pamoja waliizunguka meza, mboni wakazielekeza ukutani, kwenye runinga kubwa iliyokuwa inaonyesha picha mnato. Ile picha ya nyumba iliyopigwa na Askofu Ponera.

“Mnamfahamu mhusika?” Fadhy aliuliza, mboni amezitumbua kumsaili kila mmoja.

Swali hili halikujibiwa kwa haraka. Na kufanya watengeneze ukimya kwa sekunde kadhaa kabla haujafukuzwa tena na Fadhy. “Fanyieni kazi, ndani ya muda mfupi tu muwe mumeshamfahamu mhusika.”

Dorice akamgeukia Stella.

Ilikuwa kama amri za kijeshi kwa lile geuko, kwamba mgeukiwa anapaswa kufanyia kazi kilichozungumziwa.

“Nitajitahidi baba,” Stella ikabidi akubaliane na amri ya mama'ke.

“Sio kazi ya mtu mmoja. Shirikianeni nyote,” Fadhy aliwaamuru.

Hawakuwa na budi, wakaafikiana naye.

***

Baada ya lile tukio Jovin alielekea nyumbani kwa Nalimuka. Akapokelewa kwa ari sana. Huku akiwakuta wageni wengine ambao hawakumshangaza; Ocd na mfanyabiashara maarufu Mangaka.

“Unaonekana kutokuwa sawa,” Nalimuka alieleza mashaka yake baada ya kumtathmini Jovin.

Ukapita ukimya kwa muda Kabla Jovin hajajibu. Picha ya ukimya ilikuwa jibu tosha, lakini baadaye alikazia. “Mambo yameanza kuharibika.”

Akavuta umakini wa wote.

“Unamaanisha nini?”

Jovin akawasaili kwanza, ndipo akajibu, “Kuna mtu amevamia nyumbani kwangu akamwokoa...” akakatishwa.

“Acha masihara dogo,” Nalimuka alisema, akamtolea Jovin mboni kali za kutoamini.

“Ndiyo hivyo. Amemwokoa Chiku.”

“Unamfahamu? Hata kwa kutambua mwonekano wake.” Ocd aliingilia kati, huku akipatwa na kumbukizi ya umbo na sura ya Askofu Ponera ile siku aliyoshikishwa adabu.

Jovin hakuwa na hiyana, aliwafafanulia kila kitu.

“Sasa tutafanyaje tena kumweka himayani? Tukimwacha uraiani anaweza kuwa kinong'ona mwisho wa siku maneno yafike kwa wazee,” Nalimuka alitoa wasiwasi wake.

“Nina wazo,” yule mfanyabiashara alisema.

“Lipi?” Nalimuka akamgeukia, asikie na aelewe kwa makini kitakachozungumzwa.

“Kwa namna yoyote ile, yule binti ataenda nyumbani kwa Cheyaya...”

Nalimuka akamkatisha, “Fahamu kwamba hakuna mtu kwenye ile nyumba.”

“Sawa. Lakini yule binti hafahamu hilo. Hivyo atakuwa na nia ya kwenda akawaahadithie kilichomtokea. Safari hizo, ndiyo zitatupa nafasi ya kumrudisha tena chini yetu.”

“Unamaanisha tuwe na kawaida ya kuilea rada ile nyumba?” Nalimuka aliuliza.

“Swadakta.”

“Yeah, ni mpango mzuri mheshimiwa,” Ocd alidakia. “Tena kwa nyongeza, mtu yeyote atakayeonekana mahali pale tule nae sahani moja. Yumkini atatusaidia kufahamu wahusika wengine wa familia walipo.”

“Basi sawa. Mimi sina tatizo.” Wakatabasamu.

***

Ni chumba kidogo ambacho hakikuwa na mwanga wa kutosha. Kwani madirisha hayakuwa makubwa, na yalizuiliwa na mabati kama pazia kwenye nyumba ndogo ya vyumba viwili na sebule iliyoezekwa kwa nyasi. Ndani ya chumba kile alikuwepo Cheyaya amejipumzisha kitandani. Ndipo nyumbani kwa yule mtu waliyemkabidhigi vitabu na Kasembe.

“Cheyaya,” sauti kutoka nje ikasikika ikimwita.
“Nipo kaka.”

Mwitaji akaingia mle chumbani. Mwenye nyumba. Cheyaya akainuka.

“Umeshapata namna ya kufanya kukabiliana na hili jambo?” mwenye nyumba aliuliza.

“Bado ndugu. Ijapokuwa kuna mpango tulishauandaaga kwa muda tu, kwamba mambo yakienda ndivyo sivyo tufanye hilo.”

“Jambo gani?”

“Kuwasilisha tatizo letu katika mkutano wa Waziri Mkuu.”

“Oooh, mliwaza vyema. Nami nashauri, endelea kubaki hapa kwa siku zote mpaka itakapowadia ile atakayowasili Waziri Mkuu.”

“Yeah, upo sahihi. Sasa...”

“Ndiyo.”

“Niazime kwanza simu niicheki familia.”
Mwenye nyumba akatekeleza pasi na ubishi.

Dakika mbili baadaye tayari Cheyaya aliipachika simu usawa wa sikio akiisikilizia iitavyo. Haikuchelea kupokelewa.

“Mke wangu!” Cheyaya aliita, alivyoitambua sauti ya mtu wa upande wa pili.

Isivyobahati, kabla ya itikio simu ikakata. Akatoa sikioni na kuisaili, ilizima chaji. Hata alivyojaribu kuwasha, hakukuwa na matokeo chanya.

“Vipi?” mwenzie aliuliza.

“Naona imezima,” Cheyaya alijibu, huku akiendeleza zoezi la uwashaji.

“Haikuwa na chaji ya kutosha, yumkini tayari bar zimeshapukutikana.”

Cheyaya akanung'unika.

“Ngoja basi nikafanye jitihada za kuiwezesha ipate moto.”

Cheyaya akamkabidhi, kisha mwenye nyumba akaondoka.

Mpigiwa, Dorice, aliiteremsha simu yake akiwa mwenye mihemo juujuu ya mashaka. Kwani ule wito ulibadilisha mapigo ya moyo, na alivyotambua sauti ya mhusika, ndivyo ile hali ilivyomzidi hadi wenzie wakafahamu uwepo wa jambo ambalo halipo sawa. Bado walikuwa ofisini kwa Fadhy.

“Nini shida?” Fadhy alihoji.

“Nduguyo.”

Fadhy akatekwa na ile kauli. Akasogea hatua moja mbele awe karibu na Dorice.

“Mpigie basi tumsikilize,” Fadhy alishauri.

Dorice naye alitii kwa haraka. Lakini matokeo ile namba haikuwa hewani. Mwisho, Fadhy aliinakiri kwenye shajara, kisha akawapa msisitizo wa kufanyia kazi yote mawili.

“Hakikisheni mnampata mhusika wa ile nyumba, na kujaribu kuitafuta hii namba. Ikiwa hewani, na mkabahatika kufanya naye mawasiliano mnitaarifu. Wakati huohuo nami nitaendeleza jitihada.”

“Sawa shem.”

Kina Dorice walivyoondoka, Fadhy akatumia wasaa kufanya mawasiliano na Askofu Ponera.

“Kuna jambo limejitokeza ambalo linaweza kutupa mwanga wa ufanikishaji.”

“Ndiyo chifu,” Askofu Ponera alitii kwa usikilizaji.

“Mhusika wetu amepatikana...”

“Askofu Ponera akamkatisha, “Yupi?”

“Cheyaya.”

“Umefahamuje na yuko wapi muda huu?”

“Alipiga simu kwa mkewe, lakini hakukuwa na maongezi ya kina, simu ikakata. Kwa hiyo hakueleza alipo kwa sasa. Hivyo basi, nakutumia namba ya simu aliyotumia kufanya naye mawasiliano, kupitia mhusika wa hiyo namba tutafanikiwa kufahamu tukitakacho.”

“Hamna shida bosi. Kwani hata yule binti tayari yupo mikononi mwetu.”

“Chiku?”

“Ndiyo chifu.”

“Kazi nzuri. Basi hakikisheni na hili linafanikiwa kwa haraka, pasi na kusahau uchunguzi wa kumtambua mhusika wa ile nyumba.”

“Copy and out.”

Fadhy akakata simu.

***

Chiku hakuwa na budi, kwa lile amriao ikamlazimu kutii takwa alilopendekeza Luteni Ringo, ijapokuwa kwa shingo upande. Kujiingiza kwa mara nyingine kwenye kifo ilihitaji moyo wa ujasiri haswa,hata kama alihakikishiwa ulinzi. Hakuamini.

Hivyo kila siku kwa nyakati tofautitofauti, alijenga mazoea ya kutembelea nyumbani kwa Cheyaya. Afikapo, hupotelea ndani kwa dakika kadhaa kisha huondoka. Aliweza kuingia ndani kwa kutumia hila iliyofanywa na Luteni Ringo usiku mmoja wa kuharibu kitasa cha mlango kabla Chiku hajaanza zoezi. Na siku zote hizo, Askofu Ponera alikuwa nyuma yake. Alitega mahali, umbali wa mita kadhaa kutoka nyumba ilipo. Kwa lolote baya litakalomkuta Chiku, basi yeye awe msaada wa kwanza.

Ilikuwa vivyo hivyo kwa Jovin na wale askari waliopo chini ya Ocd. Nao walitembelea mahali hapo na kujificha umbali wa mita kadhaa kuyasaili mazingira yote ya nyumba ya Cheyaya. Wakawa makini kuwa-mark wote watembeleao. Wakabahatika kumwona Chiku na kufikisha ripoti kwa wakuu wao haraka sana.

“Haina haja ya kupoteza muda, tufanye tulichodhamiria. Huyo binti itakuwa ana vingi anavyovifahamu,” Nalimuka aliamuru.

Hakuna aliyempinga, zaidi ya kumtii.

Zilishapita siku nne toka Chiku alianze lile zoezi, ilivyowadia siku ya tano, alielekea nyumbani kwa Cheyaya akiwa ameongozana na Askofu Ponera. Jovin na wenzie wakashuhudia kila kitu. Kiasi cha kuwapa mshawasha wawavamie kwa haraka. Na kilichowashawishi zaidi ni lile ambatano na mtu mwingine.

Hivyo walisubiri kwa sekunde chache tu, toka kina Chiku walivyopotelea ndani, wao wakajiondoa pale walipochukua maficho kwa hatua za mnyato zenye kasi. Wakati huo walipunguza kidogo maumbo yao-kwa kupindisha mgongo.

Kule ndani kina Askofu Ponera waliishia sebuleni, wakajibweteka sofani. Hakukuwa na lolote la kufanya, zaidi ya kupiga soga za hapa na pale kusubiri ufikie muda utakaokomesha uwepo wao mazingira hayo.

Mshindo wa hatua za mkimbio ndizo zilikuja kukatisha maongezi yao. Wakajipa utulivu kuzitafakari, walipoona zinazidi kusogea, Askofu Ponera aliinuka na kwenda dirishani. Alifunua pazia, akamshuhudia mmoja kati ya wasababishao. Alibahatika kumwona mmoja kati ya wale askari waliopo chini ya Ocd. Akamkumbuka sura.

“Kuwa mtulivu, kuna ugeni umetutembelea,” Askofu Ponera alisema, akilifunika pazia kisha kurejea alipoketi awali.

Hali ya Chiku ikabadilika. Hofu ikamkumbata. Kumbukizi ya wabaya ikajishikiza kwenye kuta za ubongo wake.

“Kuwa na amani, halitojitokeza baya lolote kama lililokupata awali mbele yangu,” Askofu Ponera akazidi kumsihi. Akatoa simu janja kwenye moja ya mfuko wa suruali, kisha akahangaika kubonyeza vitufe kadhaa. Akitakacho kilipokamilika, akakituma kwa mlengwa. Ulikuwa ujumbe. Baada ya hapo walielekea ushorobani ugawanishao vyumba, wakachukua maficho.

Kwa sababu mlango ulikuwa wazi, kina Jovin hawakuhangaika kuingia ndani. Hatua zikiwa fupifupi na nyemelezo. Pindi wanasonga mbele kwa utafutaji wa walengwa wao, mlango ukafungwa kwa nje. Jovin na wenzie wakahamaki. Kabla hamaniko halijaisha, Askofu Ponera akajitokeza pale alipojificha kwa mshindo wa nguvu.

“Ni mtego!” Jovin alijisemeza. Mboni zikiwa kodo kutathmini tukio hilo.

Aliyefunga mlango ni Luteni Ringo.

“Karibuni,” Askofu Ponera aliwakaribisha kwa dhihaka. Hatua ndogondogo apigazo akatengeneza ukaribu. Alipoona umbali uliopo ni kisio la hatua moja, akasimama.

“Niwasaidie nini?” Askofu Ponera aliuliza kwa mara nyingine.

“Sisi ni maafisa wa jeshi la polisi kutoka kituo cha...” Jovin alijitutumua kutumia wadhifa wa wale vijana. Kauli yake haikufika mwisho, ngumi iliyorushwa na Askofu Ponera na kumpata moja ya jicho ikamsitisha.

Wale askari wakaingilia.

Lakini Askofu Ponera alikuwa kwenye nafasi nzuri aliyoitumia vyema. Wale askari; walioumbwa kwa ma-umbo membamba, warefu, walikuwa wepesi kuingilika kwa kila pigo lililomtoka Askofu Ponera. Asilimia kubwa alitumia mateke, na yalimwezesha kumpatia uwanda wa ushindi.

“Hivi unajivunia nini kupigana na dola? Unaifahamu dola wewe?” mmoja wa wale askari aliuliza.

“Dola ndiyo inayowaruhusu mfanye maovu, sio?” Askofu Ponera naye alimtupia ulizo badala ya jibu. Ulizo lililoambatana na ngumi aliyoikita tumboni kwa muulizaji. Alishindwa kuihimili, akarudi nyuma hatua moja, akakumbatia tumbo kupooza maumivu.

Askofu Ponera akamsogelea Jovin. Ambaye alisimama hatua kadhaa kuliweka jicho lake vyema. Lile ngumi alilopigwa halikuwa manyama uzembe. Liliyumbisha mfumo wake wa akili. Lakini hiyo haikumzuia kufahamu hila za Askofu Ponera. Alipobaini ondoko ni kwa ajili yake, alifungua mbio kupotelea ushorobani alikokuwa Askofu Ponera awali.

Wale askari walivyonuia wafanye Jovin alichofanya, Askofu Ponera alimuwahi mmoja wao akampiga ngwara iliyomsukuma sukuma akawaangukia wenzake. Nao wakafuata mkumbo pasi mapendo.

Jovin alilokimbilia akaingia kwenye moja ya chumba. Hakuchukua muda mrefu mahali hapo, maji yalikuwa mengi kwake, hakuwa na ubavu wa kuyamudu. Hivyo alivunja dirisha, akaendeleza ondoko.

Bahati, Luteni Ringo, Pte Pemba na Pte Bayo walimwona. Hawakujadili mara mbili, gari iliungurumishwa, wakaunga nyuma yake. Wakati Askofu Ponera aliwadhibiti wale askari. Chiku akajiondoa mafichoni.

***

Mfukuzano ulikuwa mkubwa, kwani Jovin alivyoliacha jengo la Cheyaya alipiga hatua za haraka hadi alipoegesha gari lake. Alipoingia ndani ya gari ndipo alifahamu anafuatiliwa. Haraka sana, aliliwasha, na kuondoka kwa kasi.

Walizunguka mitaa mingi ndani ya mji wa Mangaka. Mwendo ukiwa wanguwangu, kiasi cha kuvuta umakini wa wawaonao. Katika pitapita hizo walijikuta wakitokezea kwenye lile jengo walilo na taarifa za kumfahamu mhusika. Walipatiwa habari na Askofu Ponera. Bahati, wote waliliona. Dereva-Pte Pemba, akapunguza mwendo, kisha wakajipa umakini wa kulisaili jengo.

Tukio la kumfuatilia Jovin likaishia hapo.

Kipo kilichowasukuma kufanya hivyo. Walivutwa na uwepo wa m-baba aliyekuwa anajihangaisha na mazoezi mbele ya nyumba hiyo.

“Anaweza kuwa mhusika?” Pte Bayo aliuliza.

“Dah, sina jibu la moja kwa moja,” Luteni Ringo alijibu, wakati huo akijihangaisha kuchukua kitu mfukoni. Kamera ya kijasusi. Pasi na kukawia, akamchukua picha kadhaa, akaziwasilisha kwa Fadhy.

“Anaweza kuwa msaada kwetu. Msimwache,” Fadhy akawaamuru.

***

Baada ya chengachenga nyingi na usaili wa kujiiba kama anazidi kufuatiliwa, Jovin aliweka tuo mtaa wa Mchangani alipojihakikishia wamfukuzao hawapo nyuma yake. Tuo lilikuwa mita chache kutoka eneo maarufu watumialo kama check point askari wa usalama barabarani. Akazitua pumzi kuupa mwili utulivu, kisha akafungua uwazuaji wa kipi kimfaacho kwa utendaji.

Alipopata, hakusita kukitekeleza. Alimpigia Nalimuka.

“Nipo Mchangani huku bosi, karibu na check point ya polisi. Kwa juu huku,” Jovin alimweleza.

“Kulikoni tena?” Nalimuka alihoji.

“Itakuwa vyema sana endapo utakuja nilipo.”

“Okay, nipe dakika, nitakuwa hapo.”

Jovin akakata simu.

Kama alivyoahidi, Nalimuka alimfikia baada ya dakika chache sana. Aliteremka garini, akaungana na Jovin garini mwake.

“Kuna tatizo?” Nalimuka aliuliza, pindi akichukua nafasi nzuri ya kuketi sitini.

“Tena kubwa sana.”

Nalimuka akauvaa umakini. Mboni kazikodolea wajihini kwa Jovin awasilishavyo habari yake. Wakati huohuo mapigo ya moyo yakimbadilika-yalianza kumwenda mbio.

“Yule aliyenivamia nyumbani bado anazengea zengea mazingira yetu.”

“Kwa nini?”

“Tulichokutana nacho nyumbani kwa Cheyaya ni mtego.”

“Anaitoa wapi jeuri ya kufanya hivyo huyo mpumbavu?”

“Nami nimejaribu kuwazua kwa kina nimeshindwa kupata jibu. Nahisi ni mtu hatari, maana mtu gani wa kawaida ambaye hawaogopi askari?”

Nalimuka akavuta pumzi, kisha akazitua kwa nguvu. Unyong'onyo ukamtapakaa, ni nani huyo mwenye jeuri agusaye njia zake?

Fikirio likatengeneza ukimya.

“Tuelekee Nampungu tukalijadili hili kwa kina,” Nalimuka alishauri.

Utekelezaji ukafuata.

Pindi Nalimuka na Jovin wanawasili kwenye lile jengo kina Luteni Ringo waliwashuhudia. Kwani hawakuondoka. Walichukua maficho umbali mfupi toka jengo lilipo.

***

Usiku ule kwa mara nyingine Fadhy alijumuika na kina Dorice ofisini kwake. Runinga iliyopo ukutani ikawashwa, wote mboni wakaziangazia huko. Wakapata wasaa wa kuziangalia picha. Fadhy alitumiwa na Luteni Ringo.

Picha zilikuwa za mnato. Ya kwanza iliwaonyesha pindi Nalimuka na Jovin walivyowasili kwenye lile jengo. Ya pili, ilimwonyesha Ocd, na ya mwisho ni yule m-baba waliyemhisi ni mwenye nyumba. Kwa pamoja; Dorice, Pendo na Stella walishtushwa na zile picha-kwa sababu ni watu wanaowafahamu. Lakini mshituko wa Stella ulikuwa maradufu, hasa kwa kumwona Jovin.

Fadhy alishtushwa na ile ya Nalimuka. Iweje kigogo huyo ajihusishe katika mchezo huo?

Yakampitia maswali mengi aliyoshindwa kuyaamulia.

“Mnawafahamu hao?” Fadhy akawatupia ulizo, mshtuko ulivyopoa.

Ukapita ukimya kabla hajajibiwa.

“Kasoro mmoja, huyo kijana,” Dorice alijibu.

“Basi hawa ndiyo washukiwa wa matukio yawahusuyo waume zenu.”

“Hata huyo?” Pendo aliuliza.

“Yupi?”

“Huyo-mwenye uwalaza. Si mfanyabiashara pale Mangaka. Mume wa Mwamvua. Alikuwa anafanya biashara zake Newala ndiyo akahamia pale kwetu. Tukampokea kwa ukarimu, kiasi cha kumtwika mke, ajabu kumwona anajihusisha kuwaweka wafanyabiashara wenzake hatarini.”

“Yapo mengi ya ajabu tutakayoyashuhudia hadi mwisho wa hili jambo.”

Wakati wao wakihangaika kuweka wazi mishtuko yao, Stella alikuwa mbali ki-fikra. Kumbukizi mbalimbali za maongezi baina yake na Jovin zilibadilishana kila baada ya muda fulani. Ilimuuma, pale alipobaini yeye ni sehemu ya uhusika wa kuuza siri za baba'ke kwa wabaya.

“Huyu mjingaaaa,” Stella alijisemeza, taswira ya Jovin ikajaa wajihini, mboni nazo zikashindwa kuhimili na kuruhusu machozi.

Kuondoa maulizo kwa wenzie, akainuka na kukimbilia chooni.

“Sasa shem, kuna uwezekano wa kuwakamata hao watu? Ukizingatia ni vigogo, isipokuwa huyo mfanyabiashara,” Dorice alihoji. Matarajio ya kupata haki yalishaanza kutoweka.

“Mlianza kwa kuniamini. Hivyo endeleeni na imani mliyoijenga kwangu. Hata kama itachukua muda mrefu, lakini ni lazima, hii mambo ikae sawa,” Fadhy aliwahakikishia.

Dorice na Pendo wakabaki kumsaili, huku wakijenga picha namna itakayotumiwa na Fadhy kuleta ufanikishaji.

Baadaye Fadhy alimpigia simu Luteni Ringo-hawakuondoka mahali pale.

“Chifu,” Luteni Ringo aliita.

“Fanyeni uvamizi haraka iwezekanavyo.”
“Sawa chifu.”

Simu ikakatwa.

Kwa kuwa Luteni Ringo aliyaweka yale maongezi katika mfumo wa mpazo wa sauti, Pte Bayo na Pte Pemba walikisikia kilichoamriwa. Hivyo simu ilivyokatwa tu, waliteremka garini kila mmoja akijipapasa papasa kwa hakikisho la uwepo wa kitu fulani, walipojiridhisha, walipiga mwendo wa mnyato kulisogelea jengo.

TUKUTANE TOLEO LIJALO.
 
MNYONGA TAI—07
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
MAWASILIANO: 0673056571

Walipofanikiwa kuondoka nyumbani kwa Cheyaya, Askofu Ponera na Chiku waliongozana na wale mateka wao hadi alipokuwa anaishi Chiku. Wakawahifadhi wale askari kwenye moja ya chumba, kisha wao wakajipa utulivu. Walipumzika sebuleni.

Mazingira ya nyumba kwa ujumla hayakuwa vyema. Uchafu ulikithiri kwa kukosa matunzo, lakini hiyo haikuwa sababu ya kuwazuia wasitumie. Walipoona utulivu unaanza kuwakinai, ndipo walijiondoa hadi chumbani kwa wale askari. Waliwafunga kudu mikononi.

“Naamini mumeshatafakari vya kutosha,” Askofu Ponera alisema, akiwa anachukua pozi la uketiji kitini. Chiku alisimama mlangoni.

Wale askari hawakumjibu. Badala yake walimkodolea mboni zilizompa picha wanapitia katika hali ngumu ya ukinzani akilini kumtafakari mwanaume huyo anajivunia nini.

“Chiku.” Askofu Ponera akamgeukia. “Njoo wakague hawa.”

Chiku alitii.

“Usiache kitu chochote utakachowakutanacho,” Askofu Ponera akamsisitizia.

Zoezi hilo lilichukua dakika chache sana, Chiku akawasilisha alivyowakutanavyo kwa Askofu Ponera. Vitambulisho na pingu. Baadaye Askofu Ponera alimwita mmoja baada ya mwingine kwa kufuatisha majina yaliyopo kwenye vitambulisho. Mmoja kati yao alikuwa na cheo cha koplo. Wengine ni ma-konstebo.

“Koplo Mvuanyingi,” Askofu Ponera aliita, mboni amezitoa kumwangalia mwitwaji. “Nataka tushirikiane kubadilishana taarifa. Vipi, upo tayari?”

Koplo Mvuanyingi hakujibu. Ndiyo kwanza, alibadili uelekeo wa utazamaji. Wengine vivyo hivyo walivyoulizwa.

“Okay, sio kesi. Nawapa muda zaidi mtafakari. Nitawarudia baadaye.” Askofu Ponera akainuka, na kuondoka mle chumbani kwa mwambatano na Chiku.

“Una uhakika watasema?” Chiku alidadisi.

“Usiwe na shaka.”

“Nahofia tukikutwa na ma-askari wenzao, watatufanyia kitu mbaya hatujawahi ona. Au nawe ni askari?” Chiku akamgeukia Askofu Ponera, huku wakizidi kupiga hatua kupotelea ushorobani.

“Hapana. Mimi ni mtu wa kawaida niliye na machungu na nchi yangu. Napenda kuona haki ikitawala.”

“Huogopi polisi? Maana unajichukulia sheria mkononi.”

Askofu Ponera akasimama na kumgeukia Chiku. Alimsaili kwa muda, kabla hajatokwa na kauli, “Upo na mtu makini sana.”

Wakaendeleza mwendo.

Dakika kumi baadaye Askofu Ponera akawa anamtoa askari mmoja baada ya mwingine anahojiana naye sebuleni. Akishamaliza, humpeleka chumba kingine tofauti na cha awali. Mahojiano ya muda huu hayakuwa na wema. Alitembeza vitu fulanifulani mwilini kwa walengwa vilivyowashinikiza wafunguke baadhi ya mambo.

“Tumeahidiwa donge nono tukifanikisha kumkamata Cheyaya,” Koplo Mvuanyingi alifunguka. Ndiyo alikuwa wa mwisho kuhojiwa. Viadhabu vya kuchomwa chomwa sindano vilipeperusha msimamo wake.

“Nani mtoaji wa hiyo hela?”

“Mbunge. Mheshimiwa Mbunge ndiyo kila kitu katika hili.”

“Nanyi mnajiona mko sahihi?”

“Njaa kaka. Njaa. Kwani hata ungekuwa ewe, usingelikataa ofa yake.”

Askofu Ponera akatabasamu.

“Kwa nini huyo Mbunge anamtaka Cheyaya?”

“Aaah! Hilo nitakudanganya, sijui sababu.”

“Umesahau kazi yake hii?” Askofu Ponera akamwonyesha sindano.

Koplo Mvuanyingi akatokwa na kauli huku akitetemeka, “Kweli ndu... Ndugu sijui...te. Sijui chochote ndugu. Nisamehe bure.”

Kwa kiasi fulani Askofu Ponera aliyaamini maneno ya Koplo Mvuanyingi. Hivyo hakuona haja ya kuendelea kumsulubu. Alimwacha, kisha alitoa taarifa kwa Fadhy kwa njia ya simu.

“Nimefanikiwa kupata madini yenye manufaa kwa ustawi wa nchi yetu,” Askofu Ponera alimtaarifu.

“Yawahishe mahali salama kwa ulinzi zaidi.”

“Timamu kwa utekelezaji.”

“Hakikisha unakuwa usafirishaji salama.”

“Hamna shaka chifu.”

Simu ikakatwa.

***

Luteni Ringo aliongoza timu kama ilivyoamriwa. Mwendo ulikuwa wa mnyato, hadhari wameikumbata vya kutosha wasishtukiwe kiasi cha kuwapa taarifa walengwa wao. Kila mmoja alikuwa na bastola, kwa kujihami na shambulizi lolote lihusishalo zana.

Walivyoufikia mlango wa mbele wakajibanza ukutani kwa mgawanyiko; wawili upande huu-Luteni Ringo na Pte Pemba. Halafu mmoja upande mwingine-Pte Bayo. Mlango waliuweka kati. Baada ya mtuo wa mihemo ya utulivu Luteni Ringo akatoa ishara kwa Pte Bayo. Naye kwa utiifu, aliitekeleza kwa haraka sana. Alibisha hodi kwa kugonga mlango na viganja vya vidole.

Kama ilivyo jadi ya wema kwa watanzania wengi, mlango ulivyogongwa kwa mara ya pili mwenye nyumba akampa subira mgongaji.

“Naja,” ilisikika sauti kutoka ndani. Pasi na umuhimu wa kuhoji mgongaji ni nani.

Ilipita dakika moja toka itikio litolewe, mlango ukashughulishwa na hatimaye kufunguliwa. Yule waliyemhisi awali kuwa mhusika wa nyumba ndiyo alifungua. Akajijaza mlangoni. Mboni zote akazielekeza kwa Pte Bayo.

“Karibu.”

“Nashukuru mzee. Naitwa...” Pte Bayo akakatishwa.

“Nikusaidie ni...?” naye hakumalizia kauli yake, pigo la wastani lilitua shingoni. Alivyonuia kugeuka amwangalie afanyaye, alipigwa kabali akavutwa nje zaidi. Yote hayo yalifanywa na Luteni Ringo.

Pale alipopepesukia mwenye nyumba akafikia kudakwa na Pte Pemba. Kabla hajafungua mdomo kuzungumza jambo akazibwa kwa mkono, kiasi cha kupelekea aheme kwa tabu. Kwani viganja viliziba sehemu ya pua pia.

“Kamwihifadhi garini, wacha sisi tuingie,” Luteni Ringo alipendekeza.

Pte Pemba alifanya alivyoombwa. Luteni Ringo na Pte Bayo wakafanya kusudio lao pia. Waliingia ndani kwa hatua fupifupi, hadhari wameikumbata kidete.

Baada ya hatua kadhaa waliikaribia sebule. Wakaweka pozi kwa muda, kisha kusikilizia maongezi ya wahusika waliopo. Waliyanasa barabara viwamboni. Waliyasikilizia mazungumzo kwa takribani dakika mbili, walipoanza kuingiwa mashaka dhidi ya mwenye nyumba kutorejea wala kumsikia, ndipo Luteni Ringo na Pte Bayo walipojitokeza mbele yao.

Walijitokeza bastola wakiwa wamezielekeza usawa wa ushambuliaji.

“Mikono juu,” Luteni Ringo aliwaamuru kwa sauti kali.

Hakuna ajawaye ujasiri kwenye uvamizi.

Hivyo, Nalimuka na wenzie walipata hofu kwa muda, iliyowashurutisha wajiinue walipoketi kutafuta sehemu ya uficho-kila mmoja alipoona panamfaa. Lakini kabla hawajayafikia, Luteni Ringo aliruhusu mitupo kadhaa ya risasi ukutani. Hakukuwa na amani tena, wakabaki kugongana gongana mithili ya kuruta wapatapo ruhusa ya kupumzika wakiwa kwenye kusanyiko.

Kwa kuwa ile bastola haikufungwa kiwambo, mshindo wa sauti ukawa mkubwa. Huo ndiyo uliwatetemesha zaidi.

“Kwa amani, wote rudini hapa kabla sijawafumua bongo zenu,” Luteni Ringo aliwaamuru kwa mara nyingine. Ile bastola akimwelekezea mmoja baada ya mwingine.

Fikra ya haraka iliyotapakaa bongoni kina Nalimuka kwamba wamevamiwa na majambazi. Wafanye nini zaidi ya kukubaliana na waamriwacho? Walitii bila shuruti.

Kwa hofu, Nalimuka na u-waziri wake, jasho chapachapa limemkithiri, aliwaongoza wenzie hadi walipoamriwa wakae. Mkao wa pigo la goti.

“Hivi mnafahamu sisi ni kina nani?” Ocd alijitutumua kuuliza. Si kamanda wa jeshi bhana!

“Haitotusaidia,” Pte Bayo alijibu. “Kwanza, nyoosheni mikono juu mwite mvua.” Akawazawadia vibao. Wazee walinyanyasika hadi huruma.

Wakatii.

Pindi wanakazana kuita mvua, Luteni Ringo alinuia kutumia wasaa huo kuwafunga pingu. Alianza na Jovin. Alimfunga mkono mmoja, alipotaka kuunganisha mkono wa pili, Jovin aliteremsha mikono na kumsukuma. Luteni Ringo akateleza na kuanguka. Anguko lililomtanguliza makalio sakafuni, huku mkono aliokamatia bastola ukishindwa zoezi la udhibiti na kuruhusu imponyoke.

Pte Bayo akaiwahi ile bastola.

Wapewe nafasi mara ngapi tena? Waliinuka na kufungua riadha kuelekea nje. Pte Pemba akabaki kuwashangaa asijue nini cha kufanya.

“Tutapata taarifa zao kupitia huyu mwenzao,” Luteni Ringo alisema, wakiwa wamesharejea garini.

“Mambo hayajaenda vyema?” Pte Pemba aliuliza.

Pte Bayo ikabidi amweleze kilichojiri.

Mwisho wa maelezo hayo wakatoa mboni kali kwa yule mfanyabiashara, aitwaye Mjimile. Walimtathmini, ataonyesha ushirikiano kiasi gani utakaowasaidia.

***

Walihema juujuu pale walipopumzika, wakiwa wamekimbia umbali wa takribani kilomita mbili kutoka nyumbani kwa Mjimile. Kwani hawakutumia magari. Walihisi yatawachelewesha kiasi cha kukutwa na wabaya wao pindi wanafanya taratibu za ufunguaji na uwashaji. Sambamba na hilo, magari yalikuwa target rahisi kwa wao kushambuliwa na risasi.

“Tunaliamuaje hili kiongozi?” Ocd aliuliza.

“Hata sijui tunafanyaje. Na vipi kuhusu Mjimile? Au ametugeuka na kuamua kutuuza?”

“Sidhani.”

“Ametugeuka bhana. Iweje baada ya yeye kutoka ndiyo yametutokea haya?”

Jovin akadakia. Ile pingu iliendelea kuwepo mkononi, “Sahihi bosi. Ameamua kuuza mechi kwa wapinzani wako.”

Nalimuka akasonya. Ishara ya kujipuuzia namna mambo yaendavyo kombo. Baadaye akatokwa na kauli, “Kuna jambo limenitamanisha kufanya katika hisia zangu.”

Akavuta umakini wa wenzie. Wakamtolea mboni zilizomwashiria aendelee kuzungumza.

“Nataka nikaonane na Kasembe,” alisema na kutulia. Akawasaili kwa muda, bado walikuwa wenye umakini. “Nataka ifanyike namna Kasembe aonane na familia yake na ile ya Cheyaya, wakae wayajenge watamalizaje kesi.”

“Umewaza mbali sana.” Jovin aliafiki.

“Na litatupunguzua mihangaiko.” Ocd akapigilia msumari.

Siku iliyofuata Nalimuka alitekeleza alichokiwazua. Alizuru mahabusu, akiambatana na Meneja wa mamlaka ya mapato mkoa wa Mtwara. Nia ya Nalimuka kwa wakati huo ni uhitaji wa pesa na kifo cha Cheyaya. Cheyaya alimchukia mazima-kwa sababu zake binafsi.

Mazingira ya maongezi yaliandaliwa vyema na uongozi wa gereza. Si waziri bhana! Lolote atakaloliamuru, hutekelezwa kwa utii.

“Kasembe, tajiri,” Nalimuka aliita kwa dharau.

Badala ya kuitika, Kasembe akamwonyeshea dharau.

“Nimekuja kukusabahi, ikiwezekana tukubaliane jambo.”

Kasembe aliendelea kutotoa ushirikiano.

“Inaonekana unayafurahia sana maisha ya gerezani. Sasa vuta picha, ndiyo yanakuwa maisha yako milele, unahisi itakuaje?”

Kasembe hakujibu.

“Haa! Hutaki kuongea?”

“Sema kilichokuleta kisha uondoke,” Kasembe akakata mzizi wa fitna.

“Namtaka Cheyaya humu ndani tumalize hili jambo. Ongea na familia yako, kama haiji, mimi nitafanya mpango waje, uongee nao, mwone jinsi gani watampata Cheyaya. Akipatikana, tufanye mambo ya kiutu uzima ili muurejee uhuru wenu.”

Kasembe ikawa kama ametoneshwa jeraha. Hasira zilimpanda. Kifua kikapwitapwita kama mbogo aliyejeruhiwa. Mpwito ulivyopoa, alivuta kohozi na kuliachia wajihini kwa Nalimuka. Akafuatia kuinuka na kuondoka eneo lile kwa hatua fupifupi za kibabe.

Nalimuka na yule meneja mamlaka ya mapato nao waliinuka. Akachukua leso kutoka mfuko wa nyuma wa suruali, kisha akalifuta lile kohozi kwa hadhari. Asije kulieneza.

“Nimekuja kwa amani ili usiteseke huku, kwani pesa lazima ichukuliwe. Hivyo ridhia nilichokuambia usije kupoteza vyote viwili; pesa na uhuru wako.” Nalimuka alijigamba. Kasembe alisimama na kuwageukia. Ile kauli ilimwingia kwa kiasi fulani.

“Habari ndiyo hiyo. Hivyo chagua moja,” Nalimuka alisisitiza.

***

“Tunazidi kupiga hatua,” Fadhy alisema. Dorice, Stella na Pendo wakiwa makini kumsikiliza. Awamu hii ilikuwa nyumbani kwake wakipata chakula-mlo wa mchana.

“Kwa maana hiyo?” Dorice aliuliza.

“Vijana wangu walifanya uvamizi kwenye ile nyumba pindi wakusudiwa wetu wakiwemo. Isivyobahati, wamefanikiwa kumshikilia mmoja-yule mwenye nyumba, wengine walifanikiwa kutoroka.”

“Walipataje mwanya wa kufanya hivyo?” Dorice aliuliza. Ndiyo aliyekuwa wa kwanza wa kuhoji. Pendo moja ya sifa yake ya ukimya, ilimwondolea kuwa kimbelembele.

“Makosa ni jambo la kawaida katika haya mambo yetu. Ni kama mchezo wa mpira, one mistake, one goal.”

Ufafanuzi huu kwa Stella uliendeleza hasira dhidi ya Jovin.

“Kama ameweza kutoroka, basi ni mkomavu katika maovu,” Stella alijisemeza. Wakati huo akimpambanua Jovin, mwanaume aliyetokea kumwamini. “Lakini siwezi kuruhusu huyu mjinga azidi kufurahia maisha. Lazima nimkamatishe. Akamatwe kwa malipo ya ulaghai alionitendea.” Uchungu ukamkaba, uliomshinikiza atamani kulia, lakini akajikaza.

Kitendo cha kubaini amegawa siri nyingi za nyumbani kwao kwa mwanaume huyo kilimuumuza sana.

“Unaonekana kutokuwa sawa. Vipi, kuna tatizo?” Dorice ndiyo alikuwa wa kwanza kumgundua.

“Niliahidiana na rafiki yangu nimtembelee.”

“Wewe nenda tu, lakini kuwa makini.”

“Sio safari ya siku moja.”

“Siku ngapi? Na wapi huko unakoenda?”

“Morogoro. Na nahitaji nikakae japo kwa siku nne.”

Wote wakamgeukia na kujenga umakini wajihini pake.

Alionesha kiasi fulani cha hofu, lakini baadaye alipiga moyo konde, “Namtembelea yule mtoto wa mzee Koba, niliyekuwa naye pamoja chuo.”

“Unaweza kumruhusu. Kikubwa ni umakini tu-awe mwangalifu.” Fadhy alipendekeza.

“Sawa, unaweza kwenda. Lakini fanya kama ulivyoshauriwa na baba'ko.”

“Nashukuru mama.” Stella akaondoka.

Dhamirio la Stella halikuwa kama alivyoomba ruhusa. Alitaka kusafiri. Lakini sio kuelekea alipowatajia wazazi wake. Lengo afike Mangaka akakutane na Jovin-akamwonyeshe machungu aliyonayo.

***

Cheyaya alisaidizana na mwenyeji wake kuandika mabango yenye jumbe mbalimbali aliyoyakusudia kumwonyesha Waziri Mkuu atakapowasili. Waliyaandika kwenye vipande vya boksi kwa kalamu kubwa. Yalikuwa mabango kumi. Mengine alinuia kuwapa wananchi watakaohudhuria mkutanoni wamsaidie kupaza sauti.

“Hili ndilo nitakalolichukua mwenyewe,” Cheyaya alisema, akilishika shika moja ya bango, lililobeba ujumbe usomekao, ‘Sina amani tena na Taifa langu. Jitihada nilizopigania usiku kucha kwa kuvuja jasho, nataka kudhulumiwa na mliowaamini mkawapatia mamlaka.’

“Inabidi ukae mbelembele ili lionekane kwa urahisi.”

“Upo mawazoni mwangu. Tena ikibidi Waziri Mkuu atakavyoingia tu jukwaani, ninyanyuke na kumkimbilia.”

Mwenyeji akacheka kwa muda. Ile hoja ilimvunja mbavu, “Walinzi hawatokuacha salama.”

“Bora iwe hivyo. Maana si ndiyo nitaonekana kwa uwazi?”

Mwenyeji akatoa msonyo mdogo, kisha akaafikiana na wazo la Cheyaya. “Upo sahihi. Fanya vivyo hivyo. Walinzi wakileta za kuleta unaangua kilio. Yule mzee hawawezi akakuchunia. Lazima akuite tu, afahamu shida yako.”

Wakatabasamu. Matumaini ya ushindi yakajitwalia nafasi kwenye kuta za moyo wa Cheyaya.

“Hapa kilichobakia ni misumari, ili tupigilie kwenye hivi vibao.”

“Nitaenda kununua,” mwenyeji wake alijitolea.

“Kwa sababu ki-giza kimeshaingia, na nimekaa humu ndani kwa muda mrefu, acha nikaoshe oshe macho kwanza.”

“Lakini...” mwenyeji akakatishwa.

“Tulia. Usiku huu, hamna kushangaana.”

“Sawa. Lakini umakini ni muhimu.”

“Hamna noma.”

Dakika kadhaa baadaye Cheyaya alikuwa kwenye badiliko la mavazi. Yule mwenyeji alimnunulia nguo mpya. Chini alipigilia raba. Akavaa suruali ya kadeti rangi ya kahawia. Fulana mchinjo-juu yake prova. Akafunga kazi kwa kapelo rangi nyeusi aliyoiteremsha hadi usawa wa nyusi.

Ilikuwa ngumu kubainika kwa urahisi.

Mara baada ya hapo akauanza mwendo kwa hatua fupifupi zenye ukakamavu kuutafuta mji. Yalipo maduka yatakayomwezesha kupata misumari.

***

Jovin alikuwa amejitawala akiisafisha moja ya silaha anazozimiliki sebuleni-nyumbani kwake. Bunduki, aina ya Dragunov. Lilikuwa zoezi alilolitekeleza kwa utulivu wa hali ya juu. Alipomaliza usafishaji, akawa anafunga taratibu, huku mdomo ukifanya kazi ya ziada ya kuunda mabiti mbalimbali kwa mluzi.

Karibu na hitimisho, kikisalia kifaa kimoja akamilishe ufungaji, mlango ukagongwa. Akasitisha zoezi, akajipa utulivu kusikiliza kwa makini. Ulipogongwa kwa mara nyingine, ndipo alipojihakikishia mbisha hodi yupo mbele ya mlango wa kuingilia nyumbani kwake. Akaacha bunduki tenge, akaenda kumfunglia.

“Stella!” Alistaajabu.

“Ndiyo mimi laazizi. Niambie,” Stella akajibebisha-kwa sauti laini iliyoficha machungu aliyonayo.

“Imekuwa ghafla mno.”

“Kwani ulikwishanipangia muda wa kukutembelea?”

Jovin hakujibu. Alishikwa na kigugumizi kwa muda. Na kilichosababisha ni ile bunduki aliyoiacha kihasarahasara. Atamruhusu vipi aingie ndani?

“Ni mgeni wako kwa hii wiki. Nimekuja kukuondolea manung'uniko ya kunipata mara chache kutibu hisia zako,” Stella aliendelea kusema huku akimrembulia. Alishajidhatiti kuweka makazi hapo, kwani alibeba begi ndogo lililo na utuno kiasi uoneshao kuna kilichobebwa ndanimwe.

***

Cheyaya alishapata huduma, katika moja ya duka lililopo maeneo ya Jangwani. Pindi anaondoka, kukatokea purkushani za hapa na pale za wateja kwenye upishani. Isivyobahati, Cheyaya alikuwa mmoja wa waathirika na kitendo hicho, aligongwa, akasukumizwa mita kadhaa huku akiwaparamia wenzie. Mparamo, ukamdondoshea kofia.

Aliyemgonga akaiokota na kumkabidhi.

“Naomba uniwie radhi, kuna mtu alinisukuma kutoka nyuma nikashindwa kujihimili,” msukumaji alisema.

“Hamna shida ndugu,” Cheyaya alimwondoa hofu pindi akiichukua ile kapelo.

Wakatazamana.

Hamad! Kila mmoja mapigo ya moyo yakambadilika kwa kutoamini. Hata hamu ya kuipokea ile kapelo, Cheyaya ikamtoka. Alikuwa Nalimuka.

Kabla yale matazamano hayajashika hatamu, Cheyaya alimsukumiza Nalimuka kisha akafungua mbio. Nalimuka naye akaunga nyuma yake. Mashuhuda hawakukosekena, wengine wasio na kazi wakathubutu kufuata mkumbo wamsaidie mheshimiwa wao.

“Mwizii huyoo... Mwizii huyooo, mwizii... mwizii,” baadaye ikawabidi wapaze sauti iwarahisishie katika ukamataji kwa kuwashirikisha watu wengine waliopo uelekeo akimbiliao Cheyaya.

TUKUTANE TOLEO LIJALO.MNYONGA TAI—07
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
MAWASILIANO: 0673056571

Walipofanikiwa kuondoka nyumbani kwa Cheyaya, Askofu Ponera na Chiku waliongozana na wale mateka wao hadi alipokuwa anaishi Chiku. Wakawahifadhi wale askari kwenye moja ya chumba, kisha wao wakajipa utulivu. Walipumzika sebuleni.

Mazingira ya nyumba kwa ujumla hayakuwa vyema. Uchafu ulikithiri kwa kukosa matunzo, lakini hiyo haikuwa sababu ya kuwazuia wasitumie. Walipoona utulivu unaanza kuwakinai, ndipo walijiondoa hadi chumbani kwa wale askari. Waliwafunga kudu mikononi.

“Naamini mumeshatafakari vya kutosha,” Askofu Ponera alisema, akiwa anachukua pozi la uketiji kitini. Chiku alisimama mlangoni.

Wale askari hawakumjibu. Badala yake walimkodolea mboni zilizompa picha wanapitia katika hali ngumu ya ukinzani akilini kumtafakari mwanaume huyo anajivunia nini.

“Chiku.” Askofu Ponera akamgeukia. “Njoo wakague hawa.”

Chiku alitii.

“Usiache kitu chochote utakachowakutanacho,” Askofu Ponera akamsisitizia.

Zoezi hilo lilichukua dakika chache sana, Chiku akawasilisha alivyowakutanavyo kwa Askofu Ponera. Vitambulisho na pingu. Baadaye Askofu Ponera alimwita mmoja baada ya mwingine kwa kufuatisha majina yaliyopo kwenye vitambulisho. Mmoja kati yao alikuwa na cheo cha koplo. Wengine ni ma-konstebo.

“Koplo Mvuanyingi,” Askofu Ponera aliita, mboni amezitoa kumwangalia mwitwaji. “Nataka tushirikiane kubadilishana taarifa. Vipi, upo tayari?”

Koplo Mvuanyingi hakujibu. Ndiyo kwanza, alibadili uelekeo wa utazamaji. Wengine vivyo hivyo walivyoulizwa.

“Okay, sio kesi. Nawapa muda zaidi mtafakari. Nitawarudia baadaye.” Askofu Ponera akainuka, na kuondoka mle chumbani kwa mwambatano na Chiku.

“Una uhakika watasema?” Chiku alidadisi.

“Usiwe na shaka.”

“Nahofia tukikutwa na ma-askari wenzao, watatufanyia kitu mbaya hatujawahi ona. Au nawe ni askari?” Chiku akamgeukia Askofu Ponera, huku wakizidi kupiga hatua kupotelea ushorobani.

“Hapana. Mimi ni mtu wa kawaida niliye na machungu na nchi yangu. Napenda kuona haki ikitawala.”

“Huogopi polisi? Maana unajichukulia sheria mkononi.”

Askofu Ponera akasimama na kumgeukia Chiku. Alimsaili kwa muda, kabla hajatokwa na kauli, “Upo na mtu makini sana.”

Wakaendeleza mwendo.

Dakika kumi baadaye Askofu Ponera akawa anamtoa askari mmoja baada ya mwingine anahojiana naye sebuleni. Akishamaliza, humpeleka chumba kingine tofauti na cha awali. Mahojiano ya muda huu hayakuwa na wema. Alitembeza vitu fulanifulani mwilini kwa walengwa vilivyowashinikiza wafunguke baadhi ya mambo.

“Tumeahidiwa donge nono tukifanikisha kumkamata Cheyaya,” Koplo Mvuanyingi alifunguka. Ndiyo alikuwa wa mwisho kuhojiwa. Viadhabu vya kuchomwa chomwa sindano vilipeperusha msimamo wake.

“Nani mtoaji wa hiyo hela?”

“Mbunge. Mheshimiwa Mbunge ndiyo kila kitu katika hili.”

“Nanyi mnajiona mko sahihi?”

“Njaa kaka. Njaa. Kwani hata ungekuwa ewe, usingelikataa ofa yake.”

Askofu Ponera akatabasamu.

“Kwa nini huyo Mbunge anamtaka Cheyaya?”

“Aaah! Hilo nitakudanganya, sijui sababu.”

“Umesahau kazi yake hii?” Askofu Ponera akamwonyesha sindano.

Koplo Mvuanyingi akatokwa na kauli huku akitetemeka, “Kweli ndu... Ndugu sijui...te. Sijui chochote ndugu. Nisamehe bure.”

Kwa kiasi fulani Askofu Ponera aliyaamini maneno ya Koplo Mvuanyingi. Hivyo hakuona haja ya kuendelea kumsulubu. Alimwacha, kisha alitoa taarifa kwa Fadhy kwa njia ya simu.

“Nimefanikiwa kupata madini yenye manufaa kwa ustawi wa nchi yetu,” Askofu Ponera alimtaarifu.

“Yawahishe mahali salama kwa ulinzi zaidi.”

“Timamu kwa utekelezaji.”

“Hakikisha unakuwa usafirishaji salama.”

“Hamna shaka chifu.”

Simu ikakatwa.

***

Luteni Ringo aliongoza timu kama ilivyoamriwa. Mwendo ulikuwa wa mnyato, hadhari wameikumbata vya kutosha wasishtukiwe kiasi cha kuwapa taarifa walengwa wao. Kila mmoja alikuwa na bastola, kwa kujihami na shambulizi lolote lihusishalo zana.

Walivyoufikia mlango wa mbele wakajibanza ukutani kwa mgawanyiko; wawili upande huu-Luteni Ringo na Pte Pemba. Halafu mmoja upande mwingine-Pte Bayo. Mlango waliuweka kati. Baada ya mtuo wa mihemo ya utulivu Luteni Ringo akatoa ishara kwa Pte Bayo. Naye kwa utiifu, aliitekeleza kwa haraka sana. Alibisha hodi kwa kugonga mlango na viganja vya vidole.

Kama ilivyo jadi ya wema kwa watanzania wengi, mlango ulivyogongwa kwa mara ya pili mwenye nyumba akampa subira mgongaji.

“Naja,” ilisikika sauti kutoka ndani. Pasi na umuhimu wa kuhoji mgongaji ni nani.

Ilipita dakika moja toka itikio litolewe, mlango ukashughulishwa na hatimaye kufunguliwa. Yule waliyemhisi awali kuwa mhusika wa nyumba ndiyo alifungua. Akajijaza mlangoni. Mboni zote akazielekeza kwa Pte Bayo.

“Karibu.”

“Nashukuru mzee. Naitwa...” Pte Bayo akakatishwa.

“Nikusaidie ni...?” naye hakumalizia kauli yake, pigo la wastani lilitua shingoni. Alivyonuia kugeuka amwangalie afanyaye, alipigwa kabali akavutwa nje zaidi. Yote hayo yalifanywa na Luteni Ringo.

Pale alipopepesukia mwenye nyumba akafikia kudakwa na Pte Pemba. Kabla hajafungua mdomo kuzungumza jambo akazibwa kwa mkono, kiasi cha kupelekea aheme kwa tabu. Kwani viganja viliziba sehemu ya pua pia.

“Kamwihifadhi garini, wacha sisi tuingie,” Luteni Ringo alipendekeza.

Pte Pemba alifanya alivyoombwa. Luteni Ringo na Pte Bayo wakafanya kusudio lao pia. Waliingia ndani kwa hatua fupifupi, hadhari wameikumbata kidete.

Baada ya hatua kadhaa waliikaribia sebule. Wakaweka pozi kwa muda, kisha kusikilizia maongezi ya wahusika waliopo. Waliyanasa barabara viwamboni. Waliyasikilizia mazungumzo kwa takribani dakika mbili, walipoanza kuingiwa mashaka dhidi ya mwenye nyumba kutorejea wala kumsikia, ndipo Luteni Ringo na Pte Bayo walipojitokeza mbele yao.

Walijitokeza bastola wakiwa wamezielekeza usawa wa ushambuliaji.

“Mikono juu,” Luteni Ringo aliwaamuru kwa sauti kali.

Hakuna ajawaye ujasiri kwenye uvamizi.

Hivyo, Nalimuka na wenzie walipata hofu kwa muda, iliyowashurutisha wajiinue walipoketi kutafuta sehemu ya uficho-kila mmoja alipoona panamfaa. Lakini kabla hawajayafikia, Luteni Ringo aliruhusu mitupo kadhaa ya risasi ukutani. Hakukuwa na amani tena, wakabaki kugongana gongana mithili ya kuruta wapatapo ruhusa ya kupumzika wakiwa kwenye kusanyiko.

Kwa kuwa ile bastola haikufungwa kiwambo, mshindo wa sauti ukawa mkubwa. Huo ndiyo uliwatetemesha zaidi.

“Kwa amani, wote rudini hapa kabla sijawafumua bongo zenu,” Luteni Ringo aliwaamuru kwa mara nyingine. Ile bastola akimwelekezea mmoja baada ya mwingine.

Fikra ya haraka iliyotapakaa bongoni kina Nalimuka kwamba wamevamiwa na majambazi. Wafanye nini zaidi ya kukubaliana na waamriwacho? Walitii bila shuruti.

Kwa hofu, Nalimuka na u-waziri wake, jasho chapachapa limemkithiri, aliwaongoza wenzie hadi walipoamriwa wakae. Mkao wa pigo la goti.

“Hivi mnafahamu sisi ni kina nani?” Ocd alijitutumua kuuliza. Si kamanda wa jeshi bhana!

“Haitotusaidia,” Pte Bayo alijibu. “Kwanza, nyoosheni mikono juu mwite mvua.” Akawazawadia vibao. Wazee walinyanyasika hadi huruma.

Wakatii.

Pindi wanakazana kuita mvua, Luteni Ringo alinuia kutumia wasaa huo kuwafunga pingu. Alianza na Jovin. Alimfunga mkono mmoja, alipotaka kuunganisha mkono wa pili, Jovin aliteremsha mikono na kumsukuma. Luteni Ringo akateleza na kuanguka. Anguko lililomtanguliza makalio sakafuni, huku mkono aliokamatia bastola ukishindwa zoezi la udhibiti na kuruhusu imponyoke.

Pte Bayo akaiwahi ile bastola.

Wapewe nafasi mara ngapi tena? Waliinuka na kufungua riadha kuelekea nje. Pte Pemba akabaki kuwashangaa asijue nini cha kufanya.

“Tutapata taarifa zao kupitia huyu mwenzao,” Luteni Ringo alisema, wakiwa wamesharejea garini.

“Mambo hayajaenda vyema?” Pte Pemba aliuliza.

Pte Bayo ikabidi amweleze kilichojiri.

Mwisho wa maelezo hayo wakatoa mboni kali kwa yule mfanyabiashara, aitwaye Mjimile. Walimtathmini, ataonyesha ushirikiano kiasi gani utakaowasaidia.

***

Walihema juujuu pale walipopumzika, wakiwa wamekimbia umbali wa takribani kilomita mbili kutoka nyumbani kwa Mjimile. Kwani hawakutumia magari. Walihisi yatawachelewesha kiasi cha kukutwa na wabaya wao pindi wanafanya taratibu za ufunguaji na uwashaji. Sambamba na hilo, magari yalikuwa target rahisi kwa wao kushambuliwa na risasi.

“Tunaliamuaje hili kiongozi?” Ocd aliuliza.

“Hata sijui tunafanyaje. Na vipi kuhusu Mjimile? Au ametugeuka na kuamua kutuuza?”

“Sidhani.”

“Ametugeuka bhana. Iweje baada ya yeye kutoka ndiyo yametutokea haya?”

Jovin akadakia. Ile pingu iliendelea kuwepo mkononi, “Sahihi bosi. Ameamua kuuza mechi kwa wapinzani wako.”

Nalimuka akasonya. Ishara ya kujipuuzia namna mambo yaendavyo kombo. Baadaye akatokwa na kauli, “Kuna jambo limenitamanisha kufanya katika hisia zangu.”

Akavuta umakini wa wenzie. Wakamtolea mboni zilizomwashiria aendelee kuzungumza.

“Nataka nikaonane na Kasembe,” alisema na kutulia. Akawasaili kwa muda, bado walikuwa wenye umakini. “Nataka ifanyike namna Kasembe aonane na familia yake na ile ya Cheyaya, wakae wayajenge watamalizaje kesi.”

“Umewaza mbali sana.” Jovin aliafiki.

“Na litatupunguzua mihangaiko.” Ocd akapigilia msumari.

Siku iliyofuata Nalimuka alitekeleza alichokiwazua. Alizuru mahabusu, akiambatana na Meneja wa mamlaka ya mapato mkoa wa Mtwara. Nia ya Nalimuka kwa wakati huo ni uhitaji wa pesa na kifo cha Cheyaya. Cheyaya alimchukia mazima-kwa sababu zake binafsi.

Mazingira ya maongezi yaliandaliwa vyema na uongozi wa gereza. Si waziri bhana! Lolote atakaloliamuru, hutekelezwa kwa utii.

“Kasembe, tajiri,” Nalimuka aliita kwa dharau.

Badala ya kuitika, Kasembe akamwonyeshea dharau.

“Nimekuja kukusabahi, ikiwezekana tukubaliane jambo.”

Kasembe aliendelea kutotoa ushirikiano.

“Inaonekana unayafurahia sana maisha ya gerezani. Sasa vuta picha, ndiyo yanakuwa maisha yako milele, unahisi itakuaje?”

Kasembe hakujibu.

“Haa! Hutaki kuongea?”

“Sema kilichokuleta kisha uondoke,” Kasembe akakata mzizi wa fitna.

“Namtaka Cheyaya humu ndani tumalize hili jambo. Ongea na familia yako, kama haiji, mimi nitafanya mpango waje, uongee nao, mwone jinsi gani watampata Cheyaya. Akipatikana, tufanye mambo ya kiutu uzima ili muurejee uhuru wenu.”

Kasembe ikawa kama ametoneshwa jeraha. Hasira zilimpanda. Kifua kikapwitapwita kama mbogo aliyejeruhiwa. Mpwito ulivyopoa, alivuta kohozi na kuliachia wajihini kwa Nalimuka. Akafuatia kuinuka na kuondoka eneo lile kwa hatua fupifupi za kibabe.

Nalimuka na yule meneja mamlaka ya mapato nao waliinuka. Akachukua leso kutoka mfuko wa nyuma wa suruali, kisha akalifuta lile kohozi kwa hadhari. Asije kulieneza.

“Nimekuja kwa amani ili usiteseke huku, kwani pesa lazima ichukuliwe. Hivyo ridhia nilichokuambia usije kupoteza vyote viwili; pesa na uhuru wako.” Nalimuka alijigamba. Kasembe alisimama na kuwageukia. Ile kauli ilimwingia kwa kiasi fulani.

“Habari ndiyo hiyo. Hivyo chagua moja,” Nalimuka alisisitiza.

***

“Tunazidi kupiga hatua,” Fadhy alisema. Dorice, Stella na Pendo wakiwa makini kumsikiliza. Awamu hii ilikuwa nyumbani kwake wakipata chakula-mlo wa mchana.

“Kwa maana hiyo?” Dorice aliuliza.

“Vijana wangu walifanya uvamizi kwenye ile nyumba pindi wakusudiwa wetu wakiwemo. Isivyobahati, wamefanikiwa kumshikilia mmoja-yule mwenye nyumba, wengine walifanikiwa kutoroka.”

“Walipataje mwanya wa kufanya hivyo?” Dorice aliuliza. Ndiyo aliyekuwa wa kwanza wa kuhoji. Pendo moja ya sifa yake ya ukimya, ilimwondolea kuwa kimbelembele.

“Makosa ni jambo la kawaida katika haya mambo yetu. Ni kama mchezo wa mpira, one mistake, one goal.”

Ufafanuzi huu kwa Stella uliendeleza hasira dhidi ya Jovin.

“Kama ameweza kutoroka, basi ni mkomavu katika maovu,” Stella alijisemeza. Wakati huo akimpambanua Jovin, mwanaume aliyetokea kumwamini. “Lakini siwezi kuruhusu huyu mjinga azidi kufurahia maisha. Lazima nimkamatishe. Akamatwe kwa malipo ya ulaghai alionitendea.” Uchungu ukamkaba, uliomshinikiza atamani kulia, lakini akajikaza.

Kitendo cha kubaini amegawa siri nyingi za nyumbani kwao kwa mwanaume huyo kilimuumuza sana.

“Unaonekana kutokuwa sawa. Vipi, kuna tatizo?” Dorice ndiyo alikuwa wa kwanza kumgundua.

“Niliahidiana na rafiki yangu nimtembelee.”

“Wewe nenda tu, lakini kuwa makini.”

“Sio safari ya siku moja.”

“Siku ngapi? Na wapi huko unakoenda?”

“Morogoro. Na nahitaji nikakae japo kwa siku nne.”

Wote wakamgeukia na kujenga umakini wajihini pake.

Alionesha kiasi fulani cha hofu, lakini baadaye alipiga moyo konde, “Namtembelea yule mtoto wa mzee Koba, niliyekuwa naye pamoja chuo.”

“Unaweza kumruhusu. Kikubwa ni umakini tu-awe mwangalifu.” Fadhy alipendekeza.

“Sawa, unaweza kwenda. Lakini fanya kama ulivyoshauriwa na baba'ko.”

“Nashukuru mama.” Stella akaondoka.

Dhamirio la Stella halikuwa kama alivyoomba ruhusa. Alitaka kusafiri. Lakini sio kuelekea alipowatajia wazazi wake. Lengo afike Mangaka akakutane na Jovin-akamwonyeshe machungu aliyonayo.

***

Cheyaya alisaidizana na mwenyeji wake kuandika mabango yenye jumbe mbalimbali aliyoyakusudia kumwonyesha Waziri Mkuu atakapowasili. Waliyaandika kwenye vipande vya boksi kwa kalamu kubwa. Yalikuwa mabango kumi. Mengine alinuia kuwapa wananchi watakaohudhuria mkutanoni wamsaidie kupaza sauti.

“Hili ndilo nitakalolichukua mwenyewe,” Cheyaya alisema, akilishika shika moja ya bango, lililobeba ujumbe usomekao, ‘Sina amani tena na Taifa langu. Jitihada nilizopigania usiku kucha kwa kuvuja jasho, nataka kudhulumiwa na mliowaamini mkawapatia mamlaka.’

“Inabidi ukae mbelembele ili lionekane kwa urahisi.”

“Upo mawazoni mwangu. Tena ikibidi Waziri Mkuu atakavyoingia tu jukwaani, ninyanyuke na kumkimbilia.”

Mwenyeji akacheka kwa muda. Ile hoja ilimvunja mbavu, “Walinzi hawatokuacha salama.”

“Bora iwe hivyo. Maana si ndiyo nitaonekana kwa uwazi?”

Mwenyeji akatoa msonyo mdogo, kisha akaafikiana na wazo la Cheyaya. “Upo sahihi. Fanya vivyo hivyo. Walinzi wakileta za kuleta unaangua kilio. Yule mzee hawawezi akakuchunia. Lazima akuite tu, afahamu shida yako.”

Wakatabasamu. Matumaini ya ushindi yakajitwalia nafasi kwenye kuta za moyo wa Cheyaya.

“Hapa kilichobakia ni misumari, ili tupigilie kwenye hivi vibao.”

“Nitaenda kununua,” mwenyeji wake alijitolea.

“Kwa sababu ki-giza kimeshaingia, na nimekaa humu ndani kwa muda mrefu, acha nikaoshe oshe macho kwanza.”

“Lakini...” mwenyeji akakatishwa.

“Tulia. Usiku huu, hamna kushangaana.”

“Sawa. Lakini umakini ni muhimu.”

“Hamna noma.”

Dakika kadhaa baadaye Cheyaya alikuwa kwenye badiliko la mavazi. Yule mwenyeji alimnunulia nguo mpya. Chini alipigilia raba. Akavaa suruali ya kadeti rangi ya kahawia. Fulana mchinjo-juu yake prova. Akafunga kazi kwa kapelo rangi nyeusi aliyoiteremsha hadi usawa wa nyusi.

Ilikuwa ngumu kubainika kwa urahisi.

Mara baada ya hapo akauanza mwendo kwa hatua fupifupi zenye ukakamavu kuutafuta mji. Yalipo maduka yatakayomwezesha kupata misumari.

***

Jovin alikuwa amejitawala akiisafisha moja ya silaha anazozimiliki sebuleni-nyumbani kwake. Bunduki, aina ya Dragunov. Lilikuwa zoezi alilolitekeleza kwa utulivu wa hali ya juu. Alipomaliza usafishaji, akawa anafunga taratibu, huku mdomo ukifanya kazi ya ziada ya kuunda mabiti mbalimbali kwa mluzi.

Karibu na hitimisho, kikisalia kifaa kimoja akamilishe ufungaji, mlango ukagongwa. Akasitisha zoezi, akajipa utulivu kusikiliza kwa makini. Ulipogongwa kwa mara nyingine, ndipo alipojihakikishia mbisha hodi yupo mbele ya mlango wa kuingilia nyumbani kwake. Akaacha bunduki tenge, akaenda kumfunglia.

“Stella!” Alistaajabu.

“Ndiyo mimi laazizi. Niambie,” Stella akajibebisha-kwa sauti laini iliyoficha machungu aliyonayo.

“Imekuwa ghafla mno.”

“Kwani ulikwishanipangia muda wa kukutembelea?”

Jovin hakujibu. Alishikwa na kigugumizi kwa muda. Na kilichosababisha ni ile bunduki aliyoiacha kihasarahasara. Atamruhusu vipi aingie ndani?

“Ni mgeni wako kwa hii wiki. Nimekuja kukuondolea manung'uniko ya kunipata mara chache kutibu hisia zako,” Stella aliendelea kusema huku akimrembulia. Alishajidhatiti kuweka makazi hapo, kwani alibeba begi ndogo lililo na utuno kiasi uoneshao kuna kilichobebwa ndanimwe.

***

Cheyaya alishapata huduma, katika moja ya duka lililopo maeneo ya Jangwani. Pindi anaondoka, kukatokea purkushani za hapa na pale za wateja kwenye upishani. Isivyobahati, Cheyaya alikuwa mmoja wa waathirika na kitendo hicho, aligongwa, akasukumizwa mita kadhaa huku akiwaparamia wenzie. Mparamo, ukamdondoshea kofia.

Aliyemgonga akaiokota na kumkabidhi.

“Naomba uniwie radhi, kuna mtu alinisukuma kutoka nyuma nikashindwa kujihimili,” msukumaji alisema.

“Hamna shida ndugu,” Cheyaya alimwondoa hofu pindi akiichukua ile kapelo.

Wakatazamana.

Hamad! Kila mmoja mapigo ya moyo yakambadilika kwa kutoamini. Hata hamu ya kuipokea ile kapelo, Cheyaya ikamtoka. Alikuwa Nalimuka.

Kabla yale matazamano hayajashika hatamu, Cheyaya alimsukumiza Nalimuka kisha akafungua mbio. Nalimuka naye akaunga nyuma yake. Mashuhuda hawakukosekena, wengine wasio na kazi wakathubutu kufuata mkumbo wamsaidie mheshimiwa wao.

“Mwizii huyoo... Mwizii huyooo, mwizii... mwizii,” baadaye ikawabidi wapaze sauti iwarahisishie katika ukamataji kwa kuwashirikisha watu wengine waliopo uelekeo akimbiliao Cheyaya.

TUKUTANE TOLEO LIJALO.
 
Back
Top Bottom