Hassan Mboneche
Member
- Jun 15, 2020
- 61
- 197
- Thread starter
- #41
RIWAYA: MKOLONI MZAWA—2
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
SEHEMU YA 23.
Hali ya Babigamba ilikuwa mbaya. Katika yale matupiano ya risasi kuna kadhaa zilimpata mwilini. Zilizoshambuliwa kupitia pembezoni mwa ukuta uliotengenezwa na Luteni Jenerali Kipozi na Luteni Mwaipeta. Zilimpata begani, nyingine mguuni. Ilhali muda wote hakuwa mwenye fahamu.
Na walivyoondoka eneo la tukio, kituo chao kilikuwa kwenye makazi yao kule Ngowe. Wakamuhifadhi Babigamba ndani ya chumba kimoja wapo, kisha pasi na kukawia, akaanza kupatiwa matibabu. Makamu wa Rais, Lilian alimtafuta daktari pamoja na vifaa tiba vitakiwavyo.
Pindi Babigamba akiendelea kupatiwa matibabu wao waliketi pembeni wakishuhudia. Makamu wa rais, Lilian. Ambaye alikuwa amevaa suruali ya jinzi-rangi ya kahawia, fulana nyekunde na raba rangi ya njano chini. Juu alipigilia boshori aliyoiteremsha na kuzuia masikio. Jenerali Namkumba, alivaa pensi rangi ya khaki, shati lenye mchanganyiko wa rangi; nyeusi, nyeupe na kijani. Chini alivaa sendoz. IGP Lukanga, alivaa kanzu rangi ya hudhurungi, chini sendoz. Ndalama naye alipigilia kanzu rangi nyeusi. Luteni Mwaipeta, Koplo Namaya na Konstebo Babaa nao walikuwepo pia.
Kila kitu walikielekezea kwenye matibabu. Kuanzia akili, masikio, macho; na mwili wote kwa ujumla. Ijapokuwa, hawakuacha kuwa na mashaka juu ya Luteni Jenerali Kipozi kwa muda fulani.
“Muna uhakika...” Makamu wa Rais, Lilian aliongea. Kabla hajamalizia kauli yake kikasikika kishindo kilichomshtua kila mmoja. Kilikuwa kishindo cha nguvu.
Luteni Mwaipeta akainuka na kwenda kuchungulia apate kufahamu nini tatizo. Alikumbana na sura za kina Kinyonga, Mauten na Shida. Akawarejea wenzie.
“Tumevamiwa,” aliwataarifu. Akiwa na muonekano wa wajihi wenye wahka.
Mshtuko ukawazidi! Hasa Makamu wa Rais, Lilian, Jenerali Namkumba, Ndalama na IGP Lukanga.
“Vijana, njooni tupambane,” Luteni Mwaipeta alisema. Baada ya kauli hiyo Koplo Namaya na Konstebo Babaa waliinuka na kumfuata Luteni Mwaipeta.
Cha kwanza walipiga hatua hadi kwenye chumba fulani wakabeba bunduki. Luteni Mwaipeta na Konstebo Babaa walibeba bunduki watumiazo siku zote kwenye majukumu yao. Isipokuwa Koplo Namaya. Alibadili. Alibeba LRR (Long Range Rifle) M 93. Baada ya hapo waliondoka.
Makamu wa Rais, Lilian, Jenerali Namkumba, Ndalama na IGP Lukanga walisalia mule mule chumbani apatiwapo Babigamba matibabu wakiwa wenye hofu. Mioyo yao ilikuwa juu juu, huku muda wote wakiomba, Luteni Mwaipeta na wenzie wafanikiwe kuwadhibiti kina Kinyonga haraka iwezekanavyo. Walihofia bainikolao la wazi kama nao ni sehemu ya mkumbo unaohitaji Rais Sharabu ang’oke madarakani.
Haikuchukua muda mrefu, milio ya risasi ikaanza kusikika kwa ukaribu. Iliyoashiria maadui zao wameshafanikiwa kuingia ndani ya jengo. Nao walivyokuwa wajinga, walishambulia ili mradi tu. Pasi na kuangalia kama kuna umuhimu kwa upande wao. Tena walishambulia huku wakisonga mbele.
Luteni Mwaipeta na wenzie wakatega kwenye moja ya kuta koridoni kuwapimia.
“Koplo Namaya, take your position,” Luteni Mwaipeta aliongea. Kauli iliyotekelezwa kwa vitendo na Koplo Namaya. Aliondoka pale walipojificha, akaingia kwenye moja ya chumba.
Pindi anaondoka alionwa na Shida. Aliyekuwa anaangaza huku na kule kwa uchunguzi zaidi wa mazingira.
“Wamejificha kule mbele,” Shida aliwanong’oneza wenzie.
Wakapiga hatua kwa hadhari kuelekea walikoambiwa.
Luteni Mwaipeta akamuamuru Konstebo Babaa avukie upande wa pili. Konstebo Babaa alivyotekeleza alionwa. Kitendo kilichowashinikiza Kinyonga, Mauten na Shida wamshambulie kwa pamoja. Lakini shabaha yao haikuzaa matunda.
Muundo wa nyumba mule ndani; ulikuwa na vyumba vinne, sebule, sehemu ya chakula, jiko, stoo na choo cha umma. Achilia mbali vyoo vya kila chumba. Vyumba viletenganishwa na korido, wakati sebule iliambatana na sehemu ya chakula. Huku stoo, jiko na choo vikiwa mbele mara baada ya vyumba. Ikiwa na maana upande wa nyuma wa nyumba hiyo. Lakini palikuwa na korido pia iliyotenganisha vyumba, choo, stoo na hilo jiko. Hapo ndipo walijificha Luteni Mwaipeta na Konstebo Babaa.
Kinyonga na wenzie nao walijigawa; wawili waliambaa ambaa kiambaza hiki-Kinyonga na Shida, mmoja-Mauten, kile kiambaza kingine. Mwendo wao ukawa wa mnyato, mitutu ya bunduki imeelekezwa usawa wa mapambano. Katikati ya vile viambaza pale koridoni kulikuwa na mapipa mawili. Yakawa kama kinga kwa kina Kinyonga.
Luteni Mwaipeta akatoa ishara kwa Konstebo Babaa ya kuwataka washambulie kwa pamoja.
Wakafanya hivyo. Kwa kujitokeza kidogo mbele ya korido na kushambulia risasi kadhaa kisha walijirudisha mafichoni. Risasi zao zikaenda kugonga kwenye yale mapipa. Kinyonga na wenzie waka-dash down kwa kuchuchumaa.
Pale chini Kinyonga na wenzie walitulia kwa sekunde kadhaa, baadaye Mauten alinyanyuka na kushambulia mitupo mitatu ya risasi moja ya kona, aliyojificha Konstebo Babaa kisha alijirudisha chini.
Kabla harufu ya baruti haijapoa kufukiza, Shida naye alinyanyuka. Mnyanyuko ulioambatana na bunduki kuketishwa kwenye nyama ya bega. Akakumbana na Luteni Mwaipeta titi fo tati. Naye akiwa ameiketisha vyema bunduki yake.
Kwa pamoja wakaruhusu shambulizi. Lakini Luteni Mwaipeta alikuwa kasi sana. Alivyominya kifyatulio tu, alilala chini na kujirudisha mafichoni kinyume nyume. Mtupo wa risasi wa Shida ulipita kapa, na kwenda kukita mlango wa choo. Ilipasua na kupotelea upande wa pili.
Mtupo wa risasi wa Luteni Mwaipeta ulimpata Shida kwenye bega ya mkono wa kushoto. Ulimyumbisha. Na kumpotezea uhimili wa kusimama na umiliki wa bunduki mikononi. Baadaye alitoa mguno uliobeba hisia za kiasi cha maumivu ayasikiayo.
Kinyonga akamvuta chini kwa nguvu.
“Amenishambulia huyo mbwa,” Shida alilalama.
Kinyonga akamtuliza, “Punguza jazba.” Akatoa kitambaa katika mfuko wa suruali aliyovaa, akamfunga Shida kwenye lile jeraha.
Yakaibuka mashambulizi ya kuviziana.
Baadaye, takribani muda wa nusu saa toka waanze kushambuliana, timu ya makomando iliyoandaliwa ile siku kumpatia ulinzi Rais Sharabu ikaongeza nguvu. Ilikuwa timu ya watu watano. Hawakuvaa mavazi ya kijeshi, walivaa kiraia, kila mmoja akiwa na bunduki ya kivita.
Ujio wao ulitokana na mkazo kutoka kwa Rais Sharabu. Kusipambazuke vyema pasipo kusikia mabadiliko ya majina ya wabaya wake. Wauwawe.
Ule mgawanyiko walioufanya awali uliweza kuwasaidia kina Luteni Mwaipeta. Kwani kule alipoelekea Koplo Namaya alifikia kupanda darini na kwenda kuweka pozi kwenye moja ya kona, karibu na siling board iliyokaribia kudondoka. Hivyo mazingira ya chini, hasa pale sebuleni na koridoni aliyaona vyema.
Makomando walivyoiingia kwa papara yenye hadhari, Koplo Namaya alikoki bunduki na kuanza ushambuliaji. Alimshambulia mmoja baada ya mwingine. Tena sio kwa kuwarembesha, shabaha zote alizielekezea kichwani.
Kitendo hicho kiliwashtua kina Kinyonga pale walipo. Na komando wawili waliobakia. Waliona ngoma ni nzito, ijapokuwa walishahisi mshambuliaji wapi amejificha. Wakaamua kutoka nduki hadi walipoegesha gari zao. Walipanda kwa haraka, kisha komando mmoja wao alichukua RPG (Rocket Propelled Grenade) akapachika kombora na kuliachia kuelekea lilipo lile jengo. Walilopo kina Luteni Mwaipeta.
Halikuwa kombora moja pekee, alirusha makombora manne, yaliyopelekea kuisambaratisha ile nyuma kama imetokwa kujengwa juzi.
***
“Kwa mantiki ya maelezo yao ina maana wameshindwa kutambua sura za wahusika waliopo ndani ya ile nyumba,” Rais Sharabu aliongea. Akionekana kuwa mwenye ghadhibiko kubwa nafsini mwake.
“Sahihi mheshimiwa,” Killa alijibu kwa sauti iliyojaa unyenyekevu.
Rais Sharabu alimaka, “Ni ujinga huo. Sasa tutawatambuaje hao watu kama ndiye wale tuwadhaniao?”
“Shambulizi walilolifanya hawawezi kutoka salama. Kwa namna yoyote lazima wafe. Hivyo kama watakuwa wameshafariki, kutoonekana kwao ndiyo utakuwa uthibitisho.”
“Hawakupaswa kuuwawa ki-rahisi hivyo. Ilibidi wapite mbele yangu kabla ya vifo vyao. Lakini bado siamini kama hao watu watakuwa wamefariki.”
“Kama huamini mwamuru Sacp Chiwila apeleke vijana wake eneo la tukio wakalidhibiti,” Killa alishauri.
“Umeshauri kitu sahihi,” Rais Sharabu aliafiki huku akitingisha kichwa. Baadaye alitoa simu kwenye mfuko wa suruali, alibonyeza vitufe kadhaa na kuisogeza usawa wa sikio.
Ilivyopokelewa, akawa kwenye mazungumzo na mtu wa upande wa pili.
***
Zilipita dakika tano, toka Rais Sharabu atoe amri kwa Kamanda wa polisi kanda maalum ya Nufaiko. Gofu la jengo walilokuwemo kina Luteni Mwaipeta likazingirwa na askari polisi; kutoka vitengo vya kutuliza ghasia, Upelelezi (Makachero), Intellijensia na wa General Duty (GD). Sacp Chiwila ndiyo aliongoza vikosi vyote hivyo, kwa kusaidizana na wakuu wa Kamandi husika.
Askari wa kutuliza ghasia walikuwa mahususi kwa ulinzi, Makachero, kwa ajili ya uchunguzi, General Duty kudhibiti halaika ya watu waliokusanyika kushuhudia tukio, wakati wa Intellijensia kukusanya taarifa.
Kwa uhitaji wa kufanya kazi vuzuri, askari walizungusha utepe wa njano kulizunguka gofu umbali wa mita kumi kila upande. Wananchi wakasimama nje ya utepe huo.
Uchunguzi ukachukua nafasi.
Pindi askari wa vyeo vya chini wakiwa bize kufanya uchunguzi na ulinzi sehemu za nje ya jengo, Sacp Chiwila aliteka vyombo vya habari. Kuuhabarisha umma juu ya tukio lililotendeka.
“Kwa muda mrefu tulipata taarifa za uwepo wenye nia ovu ndani ya hii nyumba. Watu waliobeba maono ya uasi dhidi ya serikali yetu. Nimshukuru mtoa taarifa wetu, na niwaombe wananchi wengine, pale mtakapowabaini watu wa namna hii.
“Na kwa kuwahakikishia, wote ambao walikuwa wahusika katika hii nyumba tutawakamata, kisha hatua za kisheria zitachukua mkondo wake.”
“Aah! Kamanda, mumebahatika kuwafahamu japo kwa sura au majina?” mmoja wa waandishi wa habari alimtupia swali.
“Hilo suala la ki-upelelezi. Hatuwezi kuweka wazi kwa sasa. Mambo yakishakamilisha tutawabainisha wananchi wawatambue.”
***
Shambulizi la makombora liliharibu kila kitu kwa kina Luteni Mwaipeta na timu nzima. Kule juu alikokuwa Koplo Namaya alifurumushwa na kuanguka chini kama mtu asiye na utimamu wa akili. Alipofikia mgongo ukampa tahadhari ya maumivu yaliyopo kutokana na mwanguko ulivyokuwa. Juu yake yakafuatia mabati, mbao na matofali.
Ilikuwa vivyo hivyo kwa Luteni Mwaipeta na Konstebo Babaa, waliangukiwa na vitu kadha wa kadha. Pasi na kusahau Makamu wa Rais, Lilian, Jenerali Namkumba, Ndalama na IGP Lukanga. Daktari na Babigamba nao pia. Kwa ujumla waliangukiwa na kifusi, huku moto ukiteketeza vitu mbalimbali vyenye uwezo wa kuungua.
Lakini chumba cha matibabu kulikuwa na nafuu kiasi. Hawakupata madhara makubwa sana, hivyo waliweza kujiinua kutoka kwenye kifusi na kuanza kupanga mbinu za kujinusuru.
“Hapa si salama tena kwetu,” Ndalama alisema. Akiwa anafuta vumbi kwenye kope.
“Hakika. Na yatupasa tuwe faster, tukizembea tunaweza kukutwa,” Jenerali Namkumba alikazia kauli ya Ndalama.
“Tuwaangalie na vijana tuone wapo katika hali gani,” Makamu wa Rais, Lilian naye hakuwa nyuma kuchangia. Muonekano wake ukibadilishwa na vumbi lililomzingira.
Wawili baina yao; Jenerali Namkumba na Ndalama wakatoka kwenda kuwaangalia. Walipiga hatua moja tu kutoka chumbani. Walivyohitaji kupiga kupiga ya pili waifikie korido, vikasikika ving’ora umbali mfupi toka hapo vilivyowabainisha kuwa ni magari ya polisi. Wakarudi ndani chap.
“Kuna magari ya polisi. Nahisi yanakuja hapa,” Ndalama aliongea. Mapigo ya moyo yakimwenda kasi.
Wengine wakatega masikio vyema kusikilizia. Sauti ya ving’ora ilizidi kusogea.
“Tunafanyaje?” Makamu wa Rais, Lilian aliuliza.
“Tunaweza kutumia huu upande wa nyuma kutoroka,” IGP Lukanga alishauri.
“Vipi kuhusu vijana?”
“Mmmh! Ni mtihani. Yumkini wamepatwa na tatizo, laiti kama wangelikuwa sawa wangerejea humu ndani.”
“Kwa hiyo tuwaache? Na ukizingatia hatuna uhakika; kama ni wazima ama wameshafariki.”
Ukapita ukimya mfupi. Ulifukuzwa na Jenerali Namkumba baadaye, “Babigamba ndiyo mwenye umuhimu wa kwanza kwetu. Tupiganie uhai wake, ili tukamalizie hatua zilizosalia.”
“Kwa hiyo tuondoke?” Makamu wa Rais, Lilian alipachika swali lingine. Kisha alimsaili mmoja baada ya mwingine.
IGP Lukanga alijibu kwa niaba ya wengine, “Hatuna namna. Tufanye hivyo.”
Wakajiandaa kutoka. Kwa kugawana majukumu, kwamba wawili baina yao wabebe machela atakayolazwa Babigamba. Ndalama na Makamu wa Rais, Lilian walijitolea kutekeleza jukumu hilo. Wakati Jenerali Namkumba na IGP Lukanga walijipa jukumu la ki-ulinzi. Daktari, aliendelea kubaki sehemu yake. Ya uangalizi wa afya ya Babigamba.
Kabla hawajatoka, Jenerali Namkumba aliangazia njia wanayohitaji kutumia kwa ajili ya kutoroka. Uwepo wa askari waliozunguka kwa ulinzi ukamnyong’onyesha. Akawapa taarifa wenzie, “Askari wamezingira karibia kila pande. Tutatokaje?”
Wote walipigwa na butwaa.
***
Kutokana na ukubwa wa kifusi ililetwa Katapila kwa ajili ya kusawazisha kwa haraka ndani ya jengo. Sanjari na gari la zimamoto, kuzima ule moto uliozidi kuongezeka kadri sekunde zilivyozidi kusonga mbele. Wahusika wakafanyiana zamu; walianza wa zimamoto, walivyomaliza ndipo watu wa katapila nao walianza shughuli yao.
Muda wote askari paswa wa uchunguzi hawakuingia ndani. Walisubiri mazoezi hayo yakamilike ndipo waianze shughuli kwa upande wa ndani.
Ile mwaga mwaga ya maji ilimpatia nguvu Koplo Namaya pale alipoangukia. Alianguka na bunduki yake. Akajitutumua, lakini sehemu ya paa iliyomwangukia ilimpa kizuizi. Hakukata tamaa. Aliendelea kujitutumua, baada ya muda alipata nafasi ya kuliinua lile paa kiurahisi na kupata mwanya wa kujiondoa. Lakini kabla hajaondoka, alisaili mazingira kwa jicho kengeza. Alimuona dereva wa katapila akipiga mwendo kusonga mbele.
“Huyu anaweza kuwa kikwazo cha kujinusuru,” Koplo Namaya alijisemeza. Taratibu akivuta bunduki yake na kuipakata vyema kifuani.
Baadaye aliikita ile bunduki kwenye nyama ya bega. Akaisaili changing liver, akabaini ipo wazi. Ipo sehemu ya kuruhusu mashambulizi. Hakuremba, alioanisha shabaha kwenda sehemu kusudiwa. Kwa dereva.
Mtupo mmoja tu wa risasi ulimwezesha kuwa malengoni. Alimpiga dereva kwenye paji la uso. Dereva akatulia tuli na uelekeo wa katapila kupotea. Askari wakashikwa na bumbuwazi, wananchi pia. Mbona katapila halisongi mbele?
“Afande, mbona katapila halitembei tena?” mmoja wa askari alimtaarifu Sacp Chiwila kwa mfumo wa swali.
Sacp Chiwila aliacha kuzungumza na wanahabari akaangazia kule lilipo katapila. Naye hakuelewa picha lililopo.
“Hebu twendeni kwanza,” Sacp Chiwila aliwaamuru wakuu wa Kamandi.
Kwa pamoja walitekeleza.
Koplo Namaya alitumia hiyo nafasi kutoka pale alipoangukia kwa mbio yenye upindo hadi chumba alichokuwa anapatiwa matibabu Babigamba.
Wote walishtuka walipomuona.
“Upo vizuri?”
“Hali vipi?”
“Ulikuwa wapi muda wote huo? Vipi wenzako, nao wapo wapi?”
Walimtupia maulizo lukuki. Huku wakijitahidi kumsaili muonekano wa mwili wake ulivyo.
“Nipo vizuri, japo si sana. Nina maumivu kidogo upande wa mbavu za kushoto na kifuani,” Koplo Namaya alijibu, huku akijinyoosha nyoosha kuweka mwili sawa.
“Vipi kuhusu wenzio?” Makamu wa Rais, Lilian aliuliza.
“Tuligawana majukumu. Wao walikuwa chini, mimi nikapanda darini. Hamjawaona?”
Makamu wa Rais, Lilian alijibu kwa kuanza kutingisha kichwa, “Hatujawaona.”
“Kuwatafuta?”
“Tumeshindwa kuwatafuta kutokana na hiyo hali ya huko nje. Kingine, sura zetu hazipaswi kuonekana.”
Koplo Namaya alivuta pumzi na kuzitua kwa nguvu, “Kuna lolote mlilokubaliana?” baadaye alitokwa na ulizo.
“Yeah! Tumedhamiria kuo...” Jenerali Namkumba alijibu. Kabla hajahitimisha, alikatishwa kauli na ujio wa Luteni Mwaipeta na Konstebo Babaa. Waliingia mule chumbani kwa mwendo wa mitambao. Hasa crowing.
Nao hawakuwa na hali nzuri ki-afya. Walikuwa na majeraha machache yaliyoruhusu damu kuwatoka pasi na kusahau maumivu. Hasa mgongoni.
“Tumedhamiria kutoroka, kupitia huu upande wa nyuma,” Makamu wa Rais, Lilian alifukuza hoja ya usaili wa afya. Na kuingiza namna watakavyojikomboa.
“Hamna shida. Kila kitu kimeshapangwa?” Luteni Mwaipeta aliuliza.
“Yeah! Na laiti kama musingelitokea, tungeliwaacha.”
“Okay! Tusipoteze muda, tuondokeni.”
Wahusika wa kumbeba Babigamba walimtwaa na kuanza kuondoka. Wengine walifuata nyuma yao. Huku sehemu ya ulinzi wakiongezeka Luteni Mwaipeta, Koplo Namaya na Konstebo Babaa.
Mwendo ulikuwa wa unyapio wenye haraka pale ndani. Walivyofikia uwazi, yaani baada ya kuliacha jengo, walipiga hatua za haraka zaidi ili waupite kwa muda mfupi na kupotelea msituni.
Ile nyumba ilizungukwa na msitu wa miti ya kupanda. Ukiacha zile mita kumi kila upande zilizozungushwa utepe. Ambazo zimepambwa kwa nyasi fupi.
Wananchi walivyowaona, walianza kupiga yowe. Lililowashtua askari, na kuwafanya wazidi kupiga hatua kuelekea walipo. Nao walivyowaona, walijipanga na kuruhusu mashambulizi kuwaelekezea.
ITAENDELEA...
HABARI NJEMA
KITABU CHA RIWAYA YA NENDA SASA KINAPATIKANA RENICS BOOKSHOP TAWI LA MOSHI KWA GHARAMA YA TSH. 10,000/= MAWASILIANO: 0767826134