Riwaya: Mkoloni Mzawa

Riwaya: Mkoloni Mzawa

RIWAYA: MKOLONI MZAWA—2
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
SEHEMU YA 16.

Jioni, timu ya Luteni Jenerali Kipozi ilikutana Ngowe kama ilivyo ada. Awamu hii Makamu wa Rais, Lilian, IGP Lukanga na Jenerali Namkumba hawakuwepo. Alikuwepo Luteni Jenerali Kipozi, Babigamba, Ndalama, Luteni Mwaipeta, Koplo Namaya na Konstebo Babaa. Walikuwa wameketi sofani, kwa kuizunguka meza iliyowekwa ule ujumbe ulioachwa nyumbani kwa Babigamba juu yake.
“Vijana, tunafanyaje kuiokoa familia ya mwenzetu?” Luteni Jenerali Kipozi aliuliza.
Konstebo Babaa alidakia, baada ya kupita ukimya kwa muda mfupi toka Luteni Jenerali Kipozi aulize, “Huu ni mtego. Na naamini, sote hapa tunamfahamu muhusika aliyetega. Azma ya kufanya hivi, ni kumuona Babigamba hashiriki kwenye kinyang’anyiro, sasa je, tupo tayari kuona hilo likitokea?”
Wengine walijibu kwa pamoja, isipokuwa Babigamba pekee. Muda wote alikuwa kimya. “Hapana.”
“Una maoni gani?” Luteni Jenerali Kipozi alipachikia ulizo.
“Mmmmmh! Nadhani itakuwa vyema Babigamba akatii agizo lao.”
“Unamaanisha awapigie simu?”
“Yeah!”
“Huoni kuwa tukifanya hivyo tutapoteza dhamira yetu jumla? Maana ataamriwa apeleke na fomu aliyoichukua.”
“Sote hapa ni makamanda. Hatuwezi kuruhusu aende peke yake...”
Luteni Jenerali Kipozi alidakia, “Nahisi kukuelewa. Kwamba aende, halafu wengine wawe nyuma yake kwa ulinzi...”
Konstebo Babaa naye alidakia kabla Luteni Jenerali Kipozi hajamalizia kauli yake, “Na ndiyo watakaokuwa sehemu ya ukombozi. Familia haitodhurika, na fomu itabaki mikononi mwetu.”
“Good idea,” Ndalama alipongeza.
Kama walivyokubaliana, Babigamba alipiga simu kwa ile namba. Haikuchukua muda mrefu ikapokelewa, sauti nzito iliyojaa ngurumo ikasikika upande wa pili.
“Babigamba?” Sauti ya upande wa pili iliuliza. Sauti ya kiume.
Babigamba aliitikia kwa sauti iliyojaa unyonge. Wenzie wakiwa makini kumsikiliza, “Ndiyo ni mimi.”
“Nakusikiliza.”
“Nipo tayari kutii agizo lenu.”
Mtu wa upande wa pili alicheka kwa kebehi kwa muda, kisha alitokwa na kauli, “Fika Nufa Tower. Saa tano usiku.”
“Hamna shida. Nitakuwa hapo muda huo.”
“Msisitizo.”
“Ndiyo.”
“Njoo peke yako. Usitoe taarifa sehemu yoyote, na la mwisho...” alisema na kutulia.
Babigamba akadakia, “Ndiyo.”
“Usisahau fomu.” Akakata simu kabla Babigamba hajajibu.
Wenzie wakamvaa kwa wajihi ulio pomoni kwa shauku ya kutaka kufahamu alichoambiwa. Hakuwa na budi, aliwaeleza maagizo yote aliyoambiwa.
Baadaye Luteni Jenerali Kipozi aliwataarifu Makamu wa Rais, IGP na Jenerali Namkumba kuhusu hatua waliyofikia. Nao hawakupinga, walibariki wazo hilo huku wakitoa msisitizo wa umakini, ili mambo yasiangukie pua.
***
Ilivyowadia saa tano usiku tayari Babigamba alishawasili Nufa Tower. Akiwa amebeba bahasha yenye ile fomu ndani yake. Muda wote mwili ukimtetema, kutokana na mawazo yaliyokuwa yanakinzana pasi na kuyapatia ufumbuzi. Nguo alizovaa; prova yenye rangi nyeusi, kadeti rangi ya hudhurungi na raba alizozifunga vyema miguuni havikumfanya ajione yupo huru. Alijihisi yupo uchi, kwa namna ambavyo alikosa amani. Kwa kuamini kila mmoja anafahamu matatizo apitiayo.
Ilivyogota saa 5:05 usiku alipiga simu kwenye ile namba. Ilivyopokelewa alitaarifu uwepo wake mahali hapo.
“Kuwa na subira. Acha papara Makamu,” mtu wa upande wa pili wa simu aliongea kwa kebehi. Mwisho wa kauli alimalizia cheko dogo lenye mguno.
Dakika saba baadaye toka alivyopiga simu iliwasili gari ndogo mbele yake. Noah. Aliikumbuka, ni ile ile waliyotumia watu waliomvamia mchana. Mmoja kati ya watu waliomo ndani ya gari aliteremsha kioo, na kumpa ishara Babigamba aingie. Mlango ulifunguliwa. Babigamba akaingia.
Safari ilipamba moto.
Akiwa ndani ya gari, Babigamba alifungwa kitambaa cheusi na kizito usoni. Lengo, asifahamu uelekeo wa safari aendayo. Hivyo baada ya pita pita za hapa na pale zilizowachukua takribani saa mbili, hatimaye walifikia ukomo wa safari. Bondeni. Karibu na mpaka wa kuingia mkoa wa Makong’onda.
Babigamba aliteremshwa na kuingizwa ndani ya mjengo fulani wa kifahari, ambao hauleti mashaka kwa wapita njia, kama unahusika kuficha maovu. Hasa watendewayo wapingaji wa utawala wa Rais Sharabu. Lilikuwa jengo la ghorofa moja.
Walivyofikia ukomo mule ndani, Babigamba alifunguliwa kile kitambaa. Akapikicha macho apate kuona vyema. Alishtuka kuwaona mkewe na mwanaye wamefungwa kwenye viti huku wakitokwa na machozi. Uchungu ukachipua upya. Nafsi ilitokota kwa hasira maradufu, kiasi kwamba alitamani awe na nguvu za miujiza apambane na wapinzani wake.
“Tulia, hupaswi kuwa na papara kupambana nao,” kuna sauti aliisikia ikimuonya. Akatua pumzi kwa nguvu.
Ukiachilia mbali familia yake, mwingine ambaye alikuwepo mule ndani ni Shida. Ikamfanya afahamu, huyo ndiye aliyehusika kuwateka. Alitokea kumchukia, na kujipa kazi ya kumsaili anafananaje na uhalifu anaoufanya.
“Endapo nitatoka hapa salama, sitowaacha hai mbwa ninyi,” alijisemeza. Taratibu mboni zikilengwa na machozi.
Baadaye aliingia Maua mule ndani. Hakuamini, kama naye ni sehemu ya timu. Akafuatwa hadi pale aliposimama.
“Oooh! Mgombea,” Maua aliita kwa kejeli. Akiwa amesimama takribani umbali wa mita moja, toka aliposimama Babigamba. Babigamba akamtupia jicho la shari.
“Acha nikuweke wazi, tuna uwezo wa kukufanya lolote na hakuna mtu atakayetuongelea kwa ubaya huko nje. Kwa usalama wako, usijihusishe na hiki ukitakacho kukifanya. Umenielewa?”
Babigamba hakujibu. Maua akaona isiwe shida, akaendelea kuzungumza. Muda wote, mikono yake kaiweka mifukoni mwa koti alilovaa. Koti kubwa la manyoya manyoya. Kichwani alivaa boshori.
“Hivyo tupatie fomu yetu, kisha tukurudishie familia yako.”
Wakati wote huo, mkewe na mwanaye walikuwa wanalia kwa uchungu, huku kilio kikiomba huruma yake katika maamuzi.
Airudishe fomu aikomboe familia? Ili aachane na mpango kama alivyoambiwa. Ama atafute namna ya kupambana nao vitu vyote vibaki mikononi mwake. Alikuwa na wakati mgumu wa kuamua.
***
Luteni Mwaipeta, Koplo Namaya na Konstebo Babaa walikuwa mita chache toka kwenye ule mjengo alioingizwa Babigamba. Mjengo ulizongukwa na wigo mrefu kiasi. Lakini haukuzuia baadhi ya mazingira kuonekana, kutokana na urembo uliopo.
Muonekano wao ulikuwa wa ki-komando zaidi. Kwani walivaa kombati za mtumba rangi ya khaki ya majeshi ya nje, walibeba bunduki kubwa za kimapigano ya mbali, pasi na kusahau mapeki mgongoni. Bunduki walizobeba ni jamii ya SMG; Luteni Mwaipeta alibeba M21, Koplo Namaya alibeba M21S na Konstebo Babaa alibeba M21BS.
Ndani ya mapeki waliweka vilipuzi na mabomu kadhaa ya mkono, yatumikayo kutulizia ghasia. Hasa mabomu yenye moshi mwingi unaowasha. Vilevile waliweka kamba ngumu, ambazo mara nyingi hutumika kuvukia vikwazo.
Pasi na kusahau holster. Zilizofungwa pajani zikiwa na bastola.
Hivyo ndivyo vifaa vya kazi walivyobeba. Wakati kwenye mavazi, ukiachana na kombati, chini walipigilia buti, vidoleni walivaa glavu na kichwani boshori, ambazo walizishusha hadi usoni, huku zikiwa na tundu kadhaa zilizowawezesha kuona na kupumua.
Kwa haraka haraka waliweza kufahamu, mjengo huo upo chini ya ulinzi mkali. Walibaini kupitia kamera za CCTV zilizofungwa kona mbalimbali. Na juu ya ule wigo, kulikuwa na nyaya zenye mionzi ya umeme. Ikawapatia wakati mgumu wa kuwazua mbinu watakayotumia kuingilia.
“Daima majengo ya namna hii haikosi milango ya nyuma,” Konstebo Babaa aliongea. Mboni zake kazitupia kwa udadisi mkubwa mjengoni.
“Kwa hiyo unashaurije?” Luteni Mwaipeta aliuliza.
“Tutumie mlango wa nyuma kuingia. Tukitumia huku mbele tutawashtua mapema na kupelekea walengwa wetu kuwaweka kwenye hatari zaidi.”
“Kama hakuna mlango?”
“Hauwezi kukosa.”
Walivyoafikiana walipiga hatua za mnyato huku wakizikwepa kamera hadi upande wa nyuma wa lile jengo. Hakika, ulikuwepo mlango mdogo wa dharura. Wakatabasamu. Wakiwa takribani umbali wa mita sitini toka wigo ulipo.
“Koplo Namaya,” Luteni Mwaipeta aliita.
“Ndiyo afande wangu.”
“Ewe ndiyo mlinzi wetu. Hivyo hautopaswa kuingia ndani. Take camouflage, and you will be our sniper.”
Koplo Namaya alijibu kwa kutingisha kichwa.
“Kingine...” Luteni Mwaipeta alisema na kutulia kwa muda. Koplo Namaya akamtumbulia pima mboni zake kumwashiria aendelee kuzungumza anamsikiliza. Luteni Mwaipeta akaendelea, “...hakikisha unatulinda dhidi ya kamera zote zilizopo upande huu.”
“Hamna shida. Kwangu ni utekelezaji.”
Dakika tatu zijazo Koplo Namaya alikuwa juu ya mti wa muembe uliopo umbali wa takribani mita mia moja na nusu toka jengo lilipo. Akatega moja ya tawi, kisha akaanza shughuli ya kuangaza mazingira yote yazungukayo jengo kupitia darubini iliyofungwa juu ya bunduki. Kila kamera aliyoiona hakuacha kufanya alivyoambiwa. Alizishambulia, zikapoteza uelekeo wa kurekodi matukio, zingine zilikatika na kuanguka chini.
“Njia nyeupe kwenu,” Koplo Namaya aliwataarifu wenzie kwa kutumia redio maalumu za mawasiliano. Ambazo walichomeka waya na kubandika visikilizio masikioni.
“Vipi ndani?” Luteni Mwaipeta aliuliza.
“Kwa upande wa nyuma nako ni kweupe. Sijajua upande wa mbele maana siuoni.”
“Okay! Endelea kutupa ulinzi.”
Baada ya mrejesho huo Luteni Mwaipeta na Konstebo Babaa walifungua mapeki na kutoa kamba, ambazo upande mmoja ilifungwa nondo iliyotengenezwa mfano wa ndoano. Wakazirushia ndani ya wigo usawa wa ule mlango. Ambao juu yake hakukuwa na zile nyaya za umeme.
Walifuatia kuzivuta kidogo na kugota sehemu. Ndicho walichokitaka, hivyo sekunde kadhaa baadaye walikuwa wanapanda kwa msaada wa mlango kuingia uani. Walivyofika juu walirukia chini na kuziondoa zile kamba kwa haraka wakazirejesha pekini.
Hawakupoa, kitendo hicho kilifanyika kwa muda mfupi sana, walivyomaliza walipiga hatua taratibu zenye mshindo mdogo hadi mlango wa nyuma wa jengo. Wakajibanza ukutani, mbele akiwa ametangulia Luteni Mwaipeta, nyuma Konstebo Babaa.
Pele mlangoni walisikilizia kwa muda mfupi, kuona kama watasikia mshindo wowote aidha kutoka ndani, au upande mwingine hapo uani.
Ukimya ulitamalaki.
Walivyojihakikishia kupo shwari, Luteni Mwaipeta alichomoa kilipuzi kutoka kwenye moja ya mfuko wa suruali akapachika pale mlangoni, usawa wa kitasa kilipo.
Wakaanza kuzihesabu sekunde, ilivyogota kumi, ulitokea mlipuko wenye mshindo mkubwa ulioambatana na moshi mwingi. Hawakusubiri ule moshi upungue, waliingia vivyo hivyo, wakiwa wamejigawa na mitutu ipo juu usawa wa ulengaji.
***
Vijana wawili waliopo chumba cha kuongozea kamera za lile jengo waliwaona kina Luteni Mwaipeta wanavyoingia mara baada ya mlango kulipuka. Walinaswa na kamera iliyotegwa moja ya kona, kabla Konstebo Babaa hajaishambulia.
Hawakuvumilia tukio hilo. Haraka sana, mmoja wao alivuta kiwambo cha simu ya mezani na kubonyeza vitufe kadhaa kisha alikisogeza kile kiwambo sikioni. Iliita kwa sekunde chache, ilivyopokelewa na mtu wa upande wa pili, Killa, wakawa kwenye mazungumzo.
“Tumebaini uwepo wa wavamizi pale mjengoni. Wamefanikiwa kuingia ndani kupitia mlango wa nyuma,” yule kijana alimtaarifu.
“Ahsante kwa taarifa.” Killa alijibu na kushusha kiwambo mahali pake.
Killa aliipokea ile taarifa kwa mshtuko sana. Hao wavamizi alioambiwa wamewezaje kupafahamu mahali hapo? Alitatizika. Na kumfanya aghadhibike, kwa sababu hakuwa na matarajio ya kupata habari ya namna hiyo.
“Babigamba unajifanya mjanja? Unajifanya don-town?” alijiuliza akiwa anabonyeza bonyeza kwenye simu janja yake. Baada ya muda, alikuwa kwenye maongezi na mtu wa upande wa pili. Mmoja ya walinzi wa lile jengo.
“Kuna wavamizi wameingia kwa kutumia mlango wa nyuma. Hakikisheni hawafiki juu.”
“Sawa bosi.” Akakata simu.
Akaunga mawasiliano kwa mtu mwingine. Maua.
“Usimchekee huyo mbwa.”
“Kuna’ni?” Maua aliuliza akimtupia Babigamba mboni za kumsaili kulingana na maelezo anayopatiwa.
“Hapo hajaja peke yake.”
Simu ikakatwa. Maua akaongeza usaili kwa Babigamba. Wa awamu hii ulijaa dhihaka.
“Ooooh! Babi...” alimuita kwa ufupi na kutulia kwa sekunde chache. Akaendelea, “...unadhani utaweza kutoka salama kwa huo mchezo ulioufanya?” akapiga hatua taratibu kumfuata Babigamba aliposimama.
Babigamba hakumjibu. Aliishia kumwangalia kwa aibu huku akitafakari kauli aambiwayo.
Killa alivyomaliza maongezi alijiandaa kwenda kuongeza nguvu. Wakati vijana wa ulinzi; wawili, waliopo geti la mbele, walitoka nduki wakiwa wamekamatia vyema bastola zao mikononi kuelekea walipoelekezwa. Upande wa nyuma wa jengo, ambao Luteni Mwaipeta na Konstebo Babaa wametumia kuingilia.
Vilevile Maua hakukaa nayo ile taarifa, aliwatonya Kinyonga na Shida. Nao chap, walibeba zana za kazi na kuteremka chini kwa kunyemelea. Hatua taratibu zisizo na mshindo, mboni zikikesha huku na kule, walipeleka kila kona, tena kwa uangalifu mkubwa ili wasipate kuhadhirika dhidi ya maadui zao.
Haikuchukua muda mrefu Killa kuwasili. Aliwasili kwa mingi mihemko, ya kuhakikisha hakuna atakayetoka salama katika watu hao waliovamia mjengoni mwao. Ambao alifahamu fika, lengo la ujio wao ni kumuokoa Babigamba na familia yake.

ITAENDELEA...

HABARI NJEMA.

KITABU CHA RIWAYA YA #NENDA KINAENDELEA KUPATIKANA #RENICS_BOOKSHOP TAWI LA MOSHI KWA GHARAMA YA TSH. 10,000/= MAWASILIANO: 0767826134
received_2945314115533687.jpg
 
shukran mkuu lakini bado sijashiba,please tuwekee tu kimoja nijue kama watafanikiwa kutoka salama
 
RIWAYA: MKOLONI MZAWA—2
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
SEHEMU YA 17.

Luteni Mwaipeta aliongoza timu kwa mwendo wa mnyato, huku Konstebo Babaa akizunguka kama pya kila baada ya hatua kadhaa, kuhakikisha nyuma watokako kuko shwari.

Milango waliyoikuta imefungwa walitumia vilipuzi kuvunja kisha walizama ndani kwa uchunguzi wenye tahadhari. Walifanya hivyo kila chumba. Walivyomaliza vyumba vyote vya chini, walipiga hatua kuelekea juu. Pindi wanapanda tu ngazi, likatokea shambulizi la risasi kutoka waelekeako. Wakarudi nyuma chap na kujificha kwenye ukuta wa ile ngazi. Mapigo ya moyo yakiwaenda kasi, ki-jasho chembamba kikiwatiririka.
“Tupe hali ya mazingira huko nje,” Luteni Mwaipeta aliongea kwa unong’ozi.
“Nawaona vijana wawili wanaingia kupitia huku nyuma. Nadhani tayari wamefahamu uwepo wenu humo ndani,” Koplo Namaya alijibu.
“Huku ndani nako hakuko shwari. Uwepo wetu umefahamika. Hivyo ulinzi wako ni muhimu kwetu.”

Walivyomaliza mazungumzo Koplo Namaya alikoki bunduki na kuikita vyema kwenye nyama ya bega. Taratibu akaanza kuwapimia wale walinzi ambao tayari walishaufikia mlango wa kuingilia kwa mwendo wa unyapio. Yule aliyetangulia alivyoingia hatua kadhaa toka mlangoni, Koplo Namaya akamweka kwenye shabaha stahiki na kuruhusu risasi kumfuata.

Akiwa hana hili wala lile, mboni kaziangazia kwa uchunguzi, aliwaona Kinyonga na Shida kule juu, wakamkonyeza kwa kumgutusha wapi maadui zao walipojificha. Akanyoosha mkono kwa nia ya kushambulia, hakufanikiwa. Kwani alirushwa pasi na mpangilio umbali wa mita moja toka aliposimama na kufikia kuanguka, huku akiwa na tobo kichwani lililoruhusu damu kutoka kwa wingi. Alitingishika kwa muda na kutulia. Tuli, ishara iliyomfahamisha kila mmoja hana uhai tena.

Kinyonga na Shida walipatwa na mshtuko kule juu. Kiasi cha kutamani wateremke waende kumwangalia, lakini walishindwa, kutokana na uwepo wa kina Luteni Mwaipeta pale chini. Yule aliyekuwa ameongozana na mlinzi mwenzie akageuka nyuma kuangalia kulikoni, naye hakupoozwa, alipigwa risasi katika paji la uso na kupoteza maisha.

Pindi mlinzi wa pili anadondoka chini kukasikika purkushani za kufunguliwa mlango wa mbele. Luteni Mwaipeta akainuka na kupiga hatua hadi mlangoni pasi na kuonwa na kina Kinyonga. Akajibanza, kumsubiri atakaye kuingia. Wakati huo pumzi kazibana kwa kiasi ili asiwe na mhemo mkubwa. Akaushuhudia mlango ukifunguliwa taratibu.

Mfunguaji, ambaye ni Killa, baadaye aliubamiza ule mlango kwa nguvu kwa nia ya mtu ambaye yupo upande huo, ambao mlango unafungukia apigwe. Lakini Luteni Mwaipeta alivyohisi hilo jambo, aliruka hatua kadhaa nyuma, hivyo pindi unabamizwa haukumgusa.

Katika hali asiyotarajia, kitendo cha kuuachia mlango kwa uwazi kilimuweka Killa kwenye wakati mgumu. Kwani anatokeza tu mlangoni, mtutu wa Konstebo Babaa ulikuwa mbele yake. Haja zikamtingisha pasi na kutarajia, mapigo ya moyo yakamwenda kasi, kijasho kikamtiririka, mwili ukamtetema kwa woga.
“Shubamit!” Konstebo Babaa alisema, akimvuta karibu yake na kumpiga kabali.

Luteni Mwaipeta alitoka kule alipojificha, akampapasa, na kumchukulia vitu vyote ambavyo vingeleta athari juu yao. Baadaye alichukua kamba ya kudu akamfunga nayo mikononi na miguuni. Wakamvuta na kwenda kumficha kwenye ule ukuta walioketi awali. Walivyomtua, Luteni Mwaipeta alimtwanga ngumi nzito shingoni na kumnyamazisha. Alipoteza fahamu.

Vitendo hivi vyote kina Kinyonga hawakuvishuhudia, walikuwa wamekula maficho kule kule juu, kitendo cha kushambuliwa wale walinzi kiliwapa kitisho cha kutojitokeza tokeza ovyo.
“Tunafanyaje kukabiliana na hao wajinga wa huko juu?” Konstebo Babaa alimnong’oneza mwenzie.

Luteni Mwaipeta hakujibu kwa uharaka. Alitafakari kwanza kwa sekunde kadhaa, alipopata muafaka ndipo alijibu, “Wewe baki hapa. Acha mimi nitumie njia nyingine ya kuingilia. Hakikisha unawahadaa, wasirudi walipowaacha walengwa wetu.” Luteni Mwaipeta akanyanyuka na kuondoka kwa kupitia mlango wa mbele.

***

Kule ukumbini Babigamba aliwapimia kwa chati Mauten na Maua. Nafsi ilishachoka, hakuwa radhi kunyanyasika tena. Mauten alikuwa amebeba bunduki aina ya assault rifle MO5E1, wakati Maua, hakuwa na silaha yoyote.

Kwa namna walivyokuwa wamesimama hawakuwa mbalimbali, hiyo ikamrahisishia Babigamba alenge mahesabu yake vizuri. Muda huo alikuwa na tamanio moja pekee. La kupambana nao.
“Weka hiyo bahasha hapo mezani,” Maua alisema na kusogea kidogo pembeni. Babigamba apate nafasi ya kupita.

Babigamba alitekeleza alivyoambiwa. Alipiga hatua kadhaa hadi mezani, akaitua ile bahasha juu yake. Akafuatia kupiga hatua mbili za kurudi nyuma. Maua akatoa ishara fulani kwa Mauten, iliyoashiria aichunguze. Akatii.
“Yeah! Ndiyo yenyewe,” Mauten alijibu baada ya kujihakikishia.
“Sasa bwana Babi, rudi nyumbani. Familia yako italetwa baada ya muda mfupi,” Maua aliongea, akipiga hatua taratibu kuisogelea meza.

Babigamba alishtuka! Anaambiwaje?

Akajifanya kama hajaisikia vizuri ile kauli, “Unaweza kurudia ulichozungumza?” aliuliza.
Maua alijibu akiwa anakatiza mbele yake, “Hatutoruhusu uondoke hapa pamoja na familia yako. Rudi, tutaku...” kabla hajamaliza kuzungumza, Babigamba alimvuta ukosi wa koti na kumkita kiwiko cha mkono wa kushoto. Mkono aliotumia kumvuta.

Maua akaona vimuli muli, na kusikia sauti ya nyesele kwa mbali.

Kwa kasi ya ajabu, aliruka na kupanda juu ya meza kisha alirusha teke lilioenda kumpata Mauten kifuani. Mauten aliyumba na kukosa uhimili, uzito wa bunduki ulimuelemea, hivyo ilimfanya adondoshe bunduki naye kuanguka. Babigamba akateremka pale juu ya meza na kumfuata alipoangukia.

Hakumpa nafasi ya kuinuka, alimpiga teke la nguvu mahali salama, na kumfanya Mauten agugumie kwa nguvu huku akijishika kupooza maumivu. Baadaye alimuinua na kumtandika ngumi kadhaa za chap chap za usoni. Mauten akafumuka uso, na kumvimba kama ngano iliyotutumuka kwa kuwekwa hamira mara baada ya kukandwa.

Matendo haya yote aliyafanya kwa kasi ya umeme. Alifanya kiasi cha kufikirisha kama hana mifupa mwilini mwake.

Maua alivyokaa sawa alikimbilia ile bunduki ya Mauten na kuiokota. Hakujalisha hawezi kuitumia, alivyoimiliki vizuri mkononi alijiandaa kumpiga nayo Babigamba kama fimbo. Hivyo akiwa na pupa, aliinua, na alivyokuwa tayari kuiteremsha alishangaa kuona ubaridi ukipenya mikononi mwake. Pasi na kutaraji, alijikuta akiiangusha ile bunduki, alivyoona damu inamchuruzika akapata ufahamu ameshambuliwa na risasi. Akageuka kuangalia risasi ilipotokea.

Alikumbana na Luteni Mwaipeta.

Wote wakashikwa na butwaa.

Lakini sio kwa Luteni Mwaipeta na Babigamba. Wao walitumia nafasi hiyo kujiokoa. Babigamba alienda kuwafungulia mkewe na mwanaye kwenye vile viti wakati Luteni Mwaipeta alichukua jukumu la Babigamba kukabiliana na Mauten na Maua.

Nafasi ya kujiokoa kwa Mauten na Maua ilikuwa kwenye huruma ya Luteni Mwaipeta. Naye hakutaka kuwapatia nafasi hiyo, kutokana na hasira zilizochangamana na uchungu uliomkaba koo.

Hivyo pindi Babigamba anaifungulia familia yake, yeye alipiga hatua hadi alipo Mauten. Mauten alikuwa chini akigaa gaa kwa maumivu.
“Uthubutu wa kumtumikia shetani umekuponza,” Luteni Mwaipeta alisema akiwa anamuinua Mauten pale chini. Alivyomsimamisha wima, japo kwa ulegevu alimpiga ngumi ya taya na kumgonganisha meno. Akiwa anataka kuanguka, akamsindikizia na kiwiko.

Mauten akaanguka mithili ya tairi la akiba literemshwapo garini.

Baadaye Luteni Mwaipeta alifuatwa na Babigamba akiwa ameongozana na familia yake pale alipo.
“Kuna kamba hapo dirishani. Unaweza kuteremka nayo uondoke eneo hili,” Luteni Mwaipeta alimnong’oneza Babigamba.

Babigamba alifikiri kwa muda, wakati huo Luteni Mwaipeta akiachana na Mauten akamfuata Maua. Maua ukamjaa mtetemeko, haja ndogo ikamtoka, cha kufia nini? Akaamua kutoka mbio kuelekea walipo kina Kinyonga.

***

Dakika nane baadaye ziliwafanya Babigamba na familia yake wawe ndani ya gari waliyokuja nayo kina Luteni Mwaipeta. Walikumbatiana kwa furaha, huku mioyo ikikesha kuwa na hofu, yawezekana wabaya wao watawafuata pale walipo. Furaha ya kutoka mikononi kwa mabaradhuli haikuwafanya waache kutokwa na machozi. Ijapokuwa awamu hii hayakuwa sawa na yale ya ndani ya mjengo.
“Tulieni. Sasa tupo salama, hakuna mtu yeyote atakayewagusa tena,” Babigamba aliwatoa hofu.

Walijumuika na kina Luteni Mwaipeta dakika nne baada ya wao walivyoingia garini. Nyuma ya usukani aliketi Konstebo Babaa, akaungurumisha injini na kuondoka. Mwendo wa mita kadhaa wakahisi uwepo wa gari nyuma yao iliyokuwa inawafuata kila uelekeo waendao.

Gari waliyoihisi wanafuatilia wao walikuwepo; Killa, Kinyonga na Shida. Hali ya Mauten haikuwa nzuri, walimuacha mule mjengoni. Hata Kinyonga na Shida nao hawakuwa kwenye uimara unaotakikana. Walijaa maumivu waliyoweza kuyamudu.
“Mheshimiwa!” Killa aliita, mara baada ya kumpigia simu Rais Sharabu na kupokelewa. Alizungumza akiwa mwenye wasiwasi na tamaa ya kuwafikia wawafuatiliao kwa haraka.
“Ndiyo Killa, nipe habari.”
“Tumewakosa kwa mara nyingine.”
“Killa!”

Killa alishindwa kuitika.

Rais Sharabu akaendelea kuzungumza, “Ni mafunzo gani ya kijeshi ambayo mulifuzu? Mbona kila awamu mnashindwa?”
“Ni wale vijana. Ni wale vijana ndiyo wanaomsaidia Babigamba.”
“Wepi?”
“Waliohusika kuwauwa wateule wako.”
“Ina maana kwamba wote wapo nchini?”
“Ndiyo mheshimiwa. Na hivi sasa tupo mbioni kuwafukuzia. Kwani wamefanikiwa kututoroka.”

Ukapita ukimya mfupi, uliomshurutisha Rais Sharabu afikiri jambo. Baadaye aliufukuza ule ukimya, “Sikia,” alisema na kutulia kwa sekunde chache. Killa naye akatega sikio vyema kule upande wa pili asikie kwa uzuri atakachoambiwa. Rais Sharabu aliendelea, “Waacheni. Musisumbuke nao, kuna sehemu ya kuzuia hizo harakati zao.”
“Tupo tayari kwa kutekeleza maagizo yako mheshimiwa,” Killa alitii. Wakati huo aliyekamatia usukani akipunguza mwendo kidogo.
“Nendeni nyumbani kwa Katibu Mkuu wa chama, Tuachie Chilumba. Mkishafika mwambieni, kamwe asipokee hiyo fomu ya huyo mpumbavu.”
“Hamna shida mheshimiwa.”

Simu ikakatwa.

Simu ilivyokatwa tekelezo lilifuatia. Walibadili ueleko na kukamata barabara itakayowafikisha nyumbani kwa Tuachie Chilumba. Haikuwachukua muda mrefu kuwasili. Maeneo ya Nyikeni, mita chache kutoka maeneo ya Chuo kikuu cha Nufaiko (UN-University of Nufaiko). Killa aliteremka na kupiga hatua hadi langoni. Akapiga hodi.

Isivyo bahati, hodi yake haikuitikiwa. Wenzie wakamfuata, wakasaidizana kubisha hodi wakati huo wakizunguka huku na kule kuangaza mazingira ya ndani. Ilikuwa nyumba iliyozungukwa na wigo uliowezesha mazingira ya uani kuonekana.

Baadaye Killa alimpigia simu Rais Sharabu kumjuza matokeo waliyokutana nayo.
“Tumebisha hodi vya kutosha, lakini hakuna mrejesho wowote kutoka ndani.”
“Subiri.”

Rais Sharabu akamsubirisha Killa na kumpigia Tuachie. Simu ya Tuachie haikupatikana. Akamrudia Killa.
“Kama kuna uwezekano wa kuingia ndani, ingieni.”

Simu ikakatwa.

Killa hakujadili. Kauli yoyote iliyotoka kwa Rais Sharabu kwake ilikuwa kama amri. Hivyo walitekeleza kauli aliyoambiwa haraka sana. Waliingia ndani, kwa kupanda wigo na kurukia uani. Huko walizunguka kila kona, walibisha hodi kwa mara nyingine lakini hakukuwa na matokeo yenye manufaa kwa upande wao.
“Mheshimiwa hakuna mtu ndani,” Killa alirudisha matokeo ya tukio kwa Rais Sharabu pindi wakiingia ndani ya gari kwa njia ya simu.

Rais Sharabu akaghadhibika. Hayakuwa matokeo yenye furaha kwa upande wake. Alijaribu kumtafuta Tuachie kwa mara nyingine simuni lakini matokeo yalisalia yale yale. Hayakubadilika.

ITAENDELEA...

HABARI NJEMA.

KITABU CHA RIWAYA YA #NENDA BADO KINAPATIKANA #RENICSBOOKSHOP TAWI LA MOSHI. MAWASILIANO: 0767826134
received_2945314115533687.jpg
 
RIWAYA: MKOLONI MZAWA—2
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
SEHEMU YA 18.

Killa hakujadili. Kauli yoyote iliyotoka kwa Rais Sharabu kwake ilikuwa kama amri. Hivyo walitekeleza kauli aliyoambiwa haraka sana. Waliingia ndani, kwa kupanda wigo na kurukia uani. Huko walizunguka kila kona, walibisha hodi kwa mara nyingine lakini hakukuwa na matokeo yenye manufaa kwa upande wao.
“Mheshimiwa hakuna mtu ndani,” Killa alirudisha matokeo ya tukio kwa Rais Sharabu pindi wakiingia ndani ya gari kwa njia ya simu.
Rais Sharabu akaghadhibika. Hayakuwa matokeo yenye furaha kwa upande wake. Alijaribu kumtafuta Tuachie kwa mara nyingine simuni lakini matokeo yalisalia yale yale. Hayakubadilika.

***

Rais Sharabu alikutana na Killa na Maua usiku ule ule. Maua alipatiwa matibabu, na kumfanya mwenye unafuu. Makutano yao yalikuwa nyumbani, katika mazingira yale yale ya Ikulu. Waliketi sebuleni, kila mmoja akiwa na bilauri lililo na chai yenye uvugu vugu. Jagi lililohifadhi ile chai liliwekwa juu ya meza katikati ya masofa waliyokalia.
“Nahitaji kumtumia Tuachie. Yeye ndiyo msaada wa mwisho kwangu.”
“Kumtumiaje?” Maua aliuliza. Na kugida funda kadhaa za chai. Akatua bilauri kwenye kisosa alichokuwa ameweka juu ya kingo ya sofa.

Rais Sharabu alipiga mwayo, alipomaliza ndipo alijibu lile swali. “Killa kama nilivyokutuma mwanzo, Tuachie inabidi apate ujumbe wangu kwamba fomu ya Babigamba asiipokee.”
“Mimi nilishakuelewa toka mwanzo,” Killa alijibu.

Maua alitingisha kichwa kuafiki.

“Sasa huku kutopatikana kunanipa mashaka.”

Maua akadakia, “Usisumbuke sana, sisi tupo acha tuwajibike.”
“Kwa nini nisisumbuke wakati kila muda mnafeli?”

Killa na Maua wakajawa na aibu wajihini.

“Natoa pendekezo,” Killa na Maua wakainua nyuso zao kumwangalia. “Tumeni vijana usiku huu pale ofisini. Ofisi ndogo ya chama. Hapa namaanisha; vijana wako Killa, na ewe Maua wale wa chama.” Rais Sharabu akainuka na kuanza kupiga hatua huku na kule pale sebuleni. Mkononi alikamatia bilauri lake la chai. “Ninachotaka, endapo Babigamba atapata wasaa wa kufika ofisini, vijana wa chama wamwanzishie vurugu, halafu vijana wako Killa, watumie mwanya huo kumuondoa katika sura ya dunia.” Alipiga funda moja la chai na kuweka tuo la utembeaji. Akamsaili mmoja baada ya mwingine.

Kauli za Rais Sharabu ziliendelea kuchukuliwa kama amri.

Kwani walivyohitimisha mazungumzo na kuondoka waliwataarifu vijana hitajika kile walichoambiwa. Nao walitekeleza pasi na kujadili, hivyo robo saa baadaye walivyopita kukagua, waliwakuta vijana hao wakiranda randa karibu na jengo la ofisi.

Vijana wa chama walioandaliwa walipangwa kumkataa Babigamba kama mtia nia. Likiwa kama tukio la kwa niaba ya watu wengine, huku wakijionyesha kuwa na mapendo ya dhati kwa Rais Sharabu na ndiyo chaguo la wanachama wengine.

Vijana hao walikaa hapo usiku kucha. Ile asubuhi walianza kujenga matumaini ya kumnasa mlengwa wao, Babigamba. Wakati Tuachie alingojewa kupatiwa ule ujumbe wa kutopokea fomu. Isivyo bahati aliendelea kutopatikana.

***

Ule usiku walivyoondoka kina Luteni Mwaipeta, Luteni Jenerali Kipozi alipokea simu kutoka kwa Makamu wa Rais, Lilian.
“Mheshimiwa,” Luteni Jenerali Kipozi aliita.
“Kuna sehemu inabidi tuidhibiti haraka iwezekanavyo. Tukiiacha, Rais Sharabu ataitumia kutukwamisha,” Makamu wa Rais aliongea kwa sauti yenye unyenyekevu.
“Wapi?”
“Bwana Tuachie Chilumba.”
“Bado sijakuelewa. Kwa namna ipi?”
“Rais Sharabu anaweza kumtumia asipokee fomu ya Babigamba...”

Luteni Jenerali Kipozi akamkatisha Makamu wa Rais, Lilian hata kabla hajamaliza kauli yake. “Umenigutusha. Sikuwahi kufikiri kuhusu hilo.”
“Kwa sababu upo nje ya siasa.”

Luteni Jenerali Kipozi akaangua kicheko kwa muda mfupi. “Enhe!”
“Inabidi tumuwahi Tuachie kumweka himayani kabla ya Rais Sharabu. Kufanya hivyo itatusaidia sana.”
“Tena sana. Naomba uelekeo wa huyo mtu, ili nitekeleze hili jukumu usiku huu.”
“Unachotakiwa kufanya...”
“Ndiyo.”
“Wateke wanaye. Itaturahisishia kumwendesha.”
“Sio kwamba tumteke mwenyewe?”
“Hapana. Kumteka mwenyewe hakutufanyi kufanikiwa kwa usahihi tukitakacho. Watoto wake ndiyo vizuri.”
“Sawa. Nipe tu hiyo anuani yake.”

Simu ikakatwa. Muda mfupi baadaye ukaingia ujumbe kwenye simu ya Luteni Jenerali Kipozi uliofafanua anuani ya Tuachie, Katibu Mkuu wa chama cha Chautu.

Nusu saa baadaye toka wamalize yale mazungumzo Luteni Jenerali Kipozi alishawasili nyumbani kwa Tuachie. Muonekano wake ulikuwa wa tofauti kidogo, alivaa; kapelo yenye rangi nyeusi kichwani, aliyoiteremsha karibu na kope, koti kubwa, rangi ya ugoro-ndani alivaa shati la drafti. Pasi na kusahau, glavu, jinzi rangi nyeusi pamoja na raba rangi nyekundu.

Pale aliwasili na gari, akaiegesha umbali wa mita kadhaa, kisha alichukua kitambaa kutoka siti jirani, akakinyunyuzia unga na kuteremka garini.

Hatua alizopiga kuifuata ile nyumba zilikuwa za kikakamavu. Alivyofika langoni alibisha hodi, ikaitikiwa sekunde chache baadaye, na mlinzi kutoka kwenye moja ya kampuni mashuhuri jijini hapo. NOS
“Nikusaidie nini?” aliuliza yule mlinzi, akiwa amesimama katikati ya mlango mdogo wa lango hilo. Moja ya mkono kakamatia bunduki. Jamii ya Pump action.

Luteni Jenerali Kipozi akapiga hatua moja mbele zaidi. Yule mlinzi akataka kurudi nyuma, lakini kabla hajautua mguu, alishikwa ukosi wa shati na kupigwa ngumi kadhaa za shingoni, zilizo na mchanganyiko wa kwenye taya. Akazima. Luteni Jenerali Kipozi akapata nafasi kiulaini kuingia ndani.

Mlango wa jengo alitumia funguo malaya kufungulia. Ulivyofunguka alizidi kuzama ndani bila wasi, huku akibashiri chumba cha watoto kilipo.

Mwisho wa ubashiri aliingia kimoja wapo, kilichoshinikizwa na msukumo wa moyo. Kikawa chenyewe. Aliwakuta watoto wawili wa jinsia ya kike, wakadiriaye miaka kumi, wamelala usingizi wa fofofo. Alitoa kile kitambaa na kuwawekea usawa wa puani, alivyoridhishwa na kuvutwa kwa yale madawa alimbeba mmoja baada ya mwingine akawapakiza ndani ya gari na kuondoka.

Alivyowasili mjengoni kwao Ngowe, aliwateremsha garini akawafunga kwenye viti katika moja ya chumba kilichotamalaki kiza. Wakati wote huo, walikuwa bado hawajazinduka. Walivyozinduka, na kujikuta wako mazingira tofauti na nyumbani walipiga makelele yaliyomfanya Luteni Jenerali Kipozi awarekodi picha ya video.

***

Saa kumi na moja alfajiri simu ya Tuachie iliita kwa mlio wa nguvu ulioambatana na mtetemo uliomfanya aamke pasi na mapendo. Aliamka angali bado anatamani kuendelea kulala. Si hivyo tu, alionekana kughadhibika pia.

Hakuwa na jinsi. Juu ya hali zote hizo, mwishowe aliinuka kitandani na kupiga hatua za uchovu. Alivyofikia sehemu alipoihifadhi simu aliweka tuo na kuichukua. Alimsaili mpigaji, ilikuwa namba ngeni, almanusra aipotezee, lakini baadaye kuna kauli iliyomshinikiza kutaka kuipokea. Alivyopeleka dole gumba ili aipokee, simu ikakata. Sekunde chache baadaye ukaingia ujumbe wa kawaida.

Tuachie akapikicha macho kwa muda mfupi kisha aliusoma. “Kuna zawadi yako whatsapp.”

Ule ujumbe ukampa shauku ya kuingia whatsapp ajionee zawadi aliyoambiwa. Wakati huo, mkewe alikuwa amelala. Lakini kwa mang’amu ng’amu, kwani hakuisha kugeuka geuka kila baada ya muda fulani.

Alivyofungua whatsapp alikutana na picha jongefu iwaonyeshayo watoto wake. Akawehuka, kiasi cha kutaka kuidondosha simu na kumwamsha mkewe kutoka usingizini.
“Nini shida?” mkewe aliuliza, akiwa anaamka na kuketi.

Hakumjibu, aliiacha ile simu mezani na kutoka mbio hadi chumbani kwa wanaye. Mkewe akaona isiwe shida, aliinuka, pajama aliyovaa ikimuonesha vyema uhalisia wa uzuri wa umbo alilonalo. Alikuwa na umbo lenye kujazilisha mate aonekapo kwa kidume yeyote. Akaichukua simu na kumfuata mumewe aelekeapo.

Alizidi kuchanganyikiwa alivyowakosa wanaye chumbani kwao. Jasho likamtoka mithili ya mtu aliyetoka mbio ndefu.
“Mume nini tatizo?” mkewe aliuliza. Kutowaona wanaye kukampa presha na shinikizo la kuangusha kilio cha hofu.

Tuachie aliendelea kutomjibu. Akatoka mule chumbani mkuku huku akiita majina ya wanaye. Lakini hakupata muitikio wowote.

Alipita kila chumba, na sehemu ambayo aliamini mtu anaweza kujificha, lakini hakuwaona wanaye. Humo mote, mkewe alikuwa nyuma yake. Machozi yakimbubujika kama mtoto mdogo. Mwisho, alimfuata mlinzi getini, alichoka, alipomkuta hana fahamu.

Kutokana na shauku ya kutaka kufahamu kilichotokea alimtingisha tingisha yule mlinzi kwa dakika hadi akazinduka.
“Nini kimetokea?” Tuachie aliuliza. Akiwa amekamata ukosi wa koti alilovaa mlinzi, na kumtingisha ili awe sawa.

Mlinzi; mzee kwa rika, mwenye umbo nene na urefu wa wastani, aliangaza pima huku na kule, akafuatia kupiga mwayo na kunuia kujibu lile swali. Taratibu, alikenua kingo za mdomo, hata kabla hajatoa sauti, simu ya Tuachie ilianza kuita upya. Mkewe alimkabidhi, naye kuipokea pasi na kutafakari.

Akawa anaongea huku akisogea pembeni.

“Watoto wako wapo sehemu salama. Lakini unaweza kuwakosa endapo utakaidi maagizo nitakayokupatia,” ilisikika sauti ya upande wa pili wa simu.
“Yapi?” Tuachie aliuliza.
“Nahitaji uipokee fomu ya Babigamba na kumweka katika orodha ya watania nia.”

Tuachie akapoa.

Kauli aliyoambiwa ilikuwa nzito kwake kuiamua pasi na kuifikiria kwa kina.

Mtu wa upande wa pili wa simu, Luteni Jenerali Kipozi akakata simu. Na kumwacha Tuachie akiendelea kuwa mwenye walakini mwingi.

ITAENDELEA...

HABARI NJEMA

KITABU CHA RIWAYA YA #NENDA BADO KINAPATIKANA #RENICSBOOKSHOP TAWI LA MOSHI. MAWASILIANO: 0767826134
received_2945314115533687.jpg
 
mkuu hujui tu mimi ulivyoniteka alafu dozi unayonipa hainitoshi,sasa nakufata huko huko tumalizane
 
RIWAYA: MKOLONI MZAWA—2
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
SEHEMU YA 19.

Baada ya kukaa sawa siku iliyofuata Babigamba alijaza ile fomu na kumkabidhi Ndalama. Ndalama alipaswa kukamilisha sehemu zilizosalia. Nafasi za wadhamini. Hapa walitumika wale watu aliowaandaa. Cha kushukuru, hawakumgeuka.

Taratibu zilipokamilika Ndalama alimrejeshea Babigamba ile fomu. Ikasalia hatua moja pekee; namna ya kuirejesha.
“Kila kitu kipo tayari?” lilikuwa swali kutoka kwa Makamu wa Rais, Lilian, timu nzima ilipokutana Ngowe kujadili namna ya uwasilishaji.
“Yeah! Imeshajazwa kwa jinsi inavyotakikana,” Babigamba alijibu, huku akimkabidhi Makamu wa Rais ile fomu.

Makamu wa Rais, Lilian aliipokea na kuisaili. Alivyoridhika nayo alimrejeshea Babigamba.

“Kuna mwenye ushauri wowote?”

Luteni Jenerali Kipozi alijibu, “Tumedhamiria kuirudisha leo hii.”

“Mupo mawazoni mwangu,” Makamu wa Rais, Lilian alisema na kulichanua tabasamu.
“Itakuwa vyema tukisikia mawazo yako pia,” Ndalama naye hakuwa nyuma kuchangia.
“Katika yote tunayoendelea, tutambue na wapinzani wetu nao wapo makini kuratibu mipango ya kutukwamisha. Tulichowashinda, hawatambui nguvu tuliyonayo...”

Babigamba akadakia, “Sahihi.”

“Hivyo niwaombe, tuuendeshe huu mchezo ki-akili zaidi, na kutumia nguvu ndogo sana.”
“Unamaanisha nini? Utaratibu wetu upo hivyo toka mwanzo,” Luteni Jenerali Kipozi aliingilia kati.
“Katika hili tunahitaji akili nyingi zaidi.”

Ndalama alidakia akionekana kuchoshwa na namna Makamu wa Rais anayowasilisha wazo, “Acha kuzunguka zunguka.”

Makamu wa Rais, Lilian akatoa mguno mdogo wa dhihaka. Alitambua michoyo aliyoileta wenzie hawaifurahii. “Sikia, nina hakika, pale ofisini hapawezi kutulia kwa hiki tulichokifanya. Kwa namna yoyote, kutakuwa na watu walioandaliwa kutaka kukwamisha hili; namaanisha wanachama wa chama chetu. Hivyo tukihitaji tuwaweze, inabidi tutumie vitu tofauti ambavyo Babigamba hajazoeleka kuvitumia.”
“Kama?”
“Usafiri. Inabidi airudishe fomu na usafiri tofauti na wa kwake. Lakini katika kwenda, ataongozana na huo usafiri wake. Na iwe karibia na mida ya kufunga ofisi.”
“Kumbe nawe ni so talented katika uhalifu?” Luteni Jenerali Kipozi aliuliza na kumalizia cheko.

Wengine pia nao walifuatia kuangusha kicheko.

***

Tuachie hakuwa mwenye amani kabisa nafsini mwake. Fikra zimuhusuzo Babigamba na Rais Sharabu ziliunyanyasa moyo wake na kuuchezesha msamba utakavyo.

Ndiyo madhara ya kuwa kibaraka.

Hakika zilimkinzanisha. Tena sana, kiasi kwamba nuru wajihini ilimponyoka.
“Naiamuaje hii?” alijiuliza. Moja ya mkono wake kakamata tama, mboni kazitupia pima ukutani-kwenye saa iliyobandikwa hapo. Aliisaili namna mshale wa sekunde unavyofanya kazi.

Dakika kadhaa baadaye simu yake iliita. Alivyomsaili mpigaji, alibonyeza kitufe cha sauti na kufanya sauti kutosikika. Lakini huo haukuwa mwisho wa kupigiwa; sio simu binafsi, wala simu ya ofisini-ziliita kwa kupokezana.

Alivyoona usumbufu akazizima. Lengo, apate wasaa mzuri wa kutafakari kile alichoamriwa na Luteni Jenerali Kipozi. Atekeleze? Au atekeleze takwa la Rais Sharabu?

Akajikuta anaingia kwenye lindi nzito la ufikiriaji.

Alitoka kwenye lindi hilo alivyoingia mmoja wa wafanyakazi wa pale ofisini.

“Zakia!” Tuachie aliita. Jina la yule aliyeingia. Binti wa makamo, akadiriaye miaka ishirini na saba. Mrefu, mnene kiasi, huku akipambwa na rangi nyeupe mwilini mwake.
“Mheshimiwa Rais anakutafuta kama nini? Hebu pokea simu, mimi nimechoka kukujibia,” Zakia alilalama na kuondoka. Uondokaji wa ghadhibiko, kwani baada ya kutoka aliubamiza mlango kwa nguvu.

Tuachie aliishia kumwangalia kupitia kioo cha mlangoni, kionyechasho korido ambayo binti huyo alikuwa anaipita kwa kunyanyasa marumaru kwa viatu virefu alivyovaa. Na kumfanya atembeapo, aonekane akinesa nesa kama twiga. Huku makalio yakimwongezea mzigo.

Si haba, alijaliwa.

Kama kujaza mate midomo ya waume, naye alikuwa miongoni mwake. Zakia alikuwa mrembo. Mrembo wa asili. Alirembeka kila kilichomo mwilini mwake. Kwani ngozi ilikuwa nyororo, pua ilimchongoka kiasi, macho yalikuwa na muito usioelezeka. Kifuani ndiyo kuzidi. Avaapo blauzi ziachazo sehemu ndogo ya matiti kuonekana, aliacha vidume vikiweweseka kwa matamanio ya kugusa gusa.

Zakia alivyopotea katika upeo wake aliziwasha zile simu. Sekunde tano hazikufika, simu ya ofisi ikaanza kuita. Alilamba kingo za mdomo kisha akapokea.
“Unataka nikuelewaje?” sauti ya upande wa pili ilimfokea. Sauti ya Rais Sharabu.

Tuachie hakujibu. Rais Sharabu aliendelea kurusha makombora mfululizo.
“Au nawe ni sehemu ya hujuma? Toka usiku unatafutwa upatiwe maelekezo hupatikani. Ukipatikana simu haipokelewi. Kwa nini? Aisee, ndugu, nikibaini una chembe chembe za kutaka kuua mipango yangu ni heri uhame nchi mapema kabla huo wakati wa ugunduzi haujawadia. Maana sitokuacha salama...”

Tuachie akashusha kiwambo kabla ya Rais Sharabu kuhitimisha kauli yake. Akatoa leso na kufuta ki-jasho kilichokuwa kinamtoka wajihini, ilhali panga boi ilikuwa inapepea.

Saa 9:10 alasiri ulionekana kuwasili msafara wa magari mawili kwenye ofisi ndogo ya chama cha Chautu maeneo ya Zuumba. Moja ya gari, ilikuwa ya Babigamba, Toyota Prado, rangi nyeupe. Na ndiyo ilitangulia. Nyuma, kulikuwa na Toyota Land cruiser V8 rangi nyeusi.

Gari ya Babigamba ilipunguza mwendo na kuonyesha ishara inakona upande wa kushoto. Ile ya nyuma nayo ilipunguza mwendo pia. Ya Babigamba ilivyoelekea upande wa kushoto, ile ya nyuma iliongeza kasi kidogo. Ilivyofikia usawa wa lango la kuingilia ofisini ikasimama.

Vijana waliokuwa wanafanya subira wakaipapalikia ile ya Babigamba. Ambayo ilipakiwa eneo jirani na la ofisi ya chama. Waliikimbilia na kuivaa kwa kuipiga piga. Hata kina Kinyonga mboni zao walizielekeza huko.
Pindi wao wanahangaika na gari ya Babigamba, Babigamba alikuwa kwenye ile Toyota Land cruiser V8. Aliendeshwa na Luteni Jenerali Kipozi. Siti ya nyuma aliketi Jackson. Yote yaendeleayo waliyashuhudia.
“Yule mama aliwaza mbali sana,” Luteni Jenerali Kipozi aliongea.

Babigamba alitikisa kichwa kuafikiana naye.

ITAENDELEA...

HABARI NJEMA

KITABU CHA RIWAYA YA NENDA SASA KINAPATIKANA RENICS BOOKSHOP TAWI LA MOSHI. MAWASILIANO: 0767826134
received_2945314115533687.jpg
 
RIWAYA: MKOLONI MZAWA—2
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
SEHEMU YA 20.

Pindi wao wanahangaika na gari ya Babigamba, Babigamba alikuwa kwenye ile Toyota Land cruiser V8. Aliendeshwa na Luteni Jenerali Kipozi. Siti ya nyuma aliketi Jackson. Yote yaendeleayo waliyashuhudia.
“Yule mama aliwaza mbali sana,” Luteni Jenerali Kipozi aliongea.

Babigamba alitikisa kichwa kuafikiana naye.

Baadaye Babigamba aliteremka, Jackson akiwa nyuma yake. Wakatembea hatua za madaha, huku Jackson akipiga picha mnato na jongefu. Mwendo wa dakika kadhaa uliwawezesha kufika ofisini kwa Tuachie na kukabidhi ile fomu. Hawakukawia, walivyokamilisha tu walirejea garini na kuondoka.

Gari ya Babigamba nayo iliondoka kule ilipoegeshwa. Wale vijana wakaangusha nderemo kwa kuamini wamemkomoa baada ya kuona hajateremka. Kinyonga na wenzie nao walipoteza shabaha, hivyo hawakufanya shambulizi lolote. Waliishia kuitazama namna gari inavyochanja mbuga kuondoka, ikiifukuzia ile V8.

Kinyonga akampandia hewani Killa.

“Aliwasili. Vijana wamefanya kama walivyoambiwa, lakini cha kushangaza hajateremka. Hivyo tumeshindwa kufanya shambulizi,” Kinyonga alimueleza Killa hali iliyotokea.
“Si vibaya, ukizingatia dirisha la urudishaji fomu limesalia muda mfupi lifungwe. Yumkini kaenda kujipanga ili arudi upya. Endeleeni kuwa makini.”
“Sawa mkuu.”

Simu ikakatwa.

***

Saa 11:15 jioni Tuachie alijitokeza mbele ya vyombo vya habari kuzungumzia mchakato wa uchukuaji fomu ulivyofanyika. Pindi anazungumza, alikuwa anaongea kiunyonge sana. Unyonge uliomtanabaisha kila mmoja hali aliyonayo.
“Anaonekana kutokuwa sawa,” wanahabari walinong’onezana.

Rais Sharabu, Luteni Jenerali Kipozi na timu zao wakawa mbele ya runinga kushuhudia. Hawakutaka kupitwa na nobe! Chembe yoyote ya kauli. Wote mapigo ya moyo yakiwaenda kasi kadri kila sekunde ilivyozidi kusonga mbele. Shauku ya ufahamu iliwatesa.
“Ndugu wanahabari, naomba nitumie wasaa huu kuwasomea watia nia wa chama chetu. Mpaka kufikia sasa, nikiwa na maana kuhitimisha zoezi la uchukuaji na urudishaji fomu, wamejitokeza watia nia wawili pekee. Naomba niwasome; Ndg. Baraka Sharabu na Patrick Babigamba. Waliofanikisha kurudisha fomu...” Tuachie akasita kwa muda. Alivuta bilauri lililo na ujazo wa maji nusu, alipiga funda kadhaa na kuitua mimbarini. Akajikohoza na kuendelea.

“Mpaka kufikia muda wa ukomo, watia nia wote walifanikiwa kurudisha fomu. Na wote wamekidhi vigezo na masharti yanayotakiwa. Kwa utaratibu wa chama, haya majina yatawasilishwa mbele ya Kamati Kuu, yatachujwa, kama yote yatakubaliwa, yatawasilishwa kwenye Mkutano wa halmashauri kuu, yatapigiwa kura ili lipatikane jina moja.
“Endapo, kama Kamati Kuu litatoka jina moja, hilo hilo litawasilishwa kwenye Mkutano wa halmashauri kuu.”

Mapokeo ya taarifa hii haikuwa nzuri kwa Rais Sharabu. Presha ilimpanda, akadondoka na kupoteza fahamu. Haraka sana, alichukuliwa na kupelekwa hospitalini kwa matibabu.

Kwa upande wa Luteni Jenerali Kipozi na wenzie walifungua uwanja wa bashasha kufurahia ushindi uliopatikana. Waliamini hiyo ni hatua nzuri kwao kufikia mafanikio.
“Huu ndiyo ushindi tuliokuwa tunaupigania siku zote. Mwanga umeshaonekana, hivyo hautoishia kwetu tu, lazima uwafikie wananchi,” Makamu wa Rais, Lilian aliongea. Wenzie; Jenerali Namkumba, IGP Lukanga, Luteni Jenerali Kipozi, Ndalama na Babigamba wakiwa makini kumsikiliza. Kwa pamoja waliizunguka meza wakipata chakula.
“Na wazee wetu; Jenerali na IGP waendelee kujificha ili iwe rahisi kukamilisha hatua zilizosalia,” Luteni Jenerali Kipozi alitoa dukuduku lake.
“Binafsi, nahitaji hata iwe sasa huyu jamaa atoke madarakani. Kwa sababu akifanyacho ni kinyume na matakwa ya katiba. Sijui anahisi hii katiba ipo kwa ajili yake pekee?” Ndalama aliingilia kati.

Wengine wakaangua kicheko. Makamu wa Rais, Lilian akatokwa na kauli baada ya kile kicheko, “Na amekunyoosha.” Wakaangua kicheko kwa mara nyingine tena. Cha awamu hii kilikuwa cha nguvu zaidi.

Tuachie aliporudi nyumbani aliwakuta wanaye wamerejea wakiwa salama. Alifurahi, kana kwamba kakaa miaka mingi pasi na kuwatia machoni. Kiasi cha furaha alichonacho alishindwa kujizuia kukionesha kwa namna alivyowakumbata wanaye. Aliwakumbatia na kuwapiga mabusu mfululizo, mkewe akiwa pembeni akibubujikwa machozi ya furaha.

***

Rais Sharabu alirejewa na fahamu. Akaruhusiwa kutoka hospitalini lakini akiwa mwenye hasira kama ilivyokuwa awali muda aliodondoka.
“Naomba muniletee Tuachie sasa hivi,” Rais Sharabu aliongea punde, alivyoteremka garini na kupiga hatua za kuingia ndani ya nyumba aishiyo.

Alitoa agizo hilo kwa Killa na Maua. Ambaye aliambatana nao kutoka hospitalini.

Maua ndiye alitii hilo agizo. Alimpigia simu Tuachie, lakini isivyo bahati iliishia kuita pasi na kupokelewa. Haikuwa mara moja pekee, ni zaidi ya mara tatu, jibu likasalie lile lile.
“Haipokelewi,” Maua alitoa mrejesho.
“Huyu mshenzi ananitakia nini? Tumeni mtu akamlete hapa haraka sana,” Rais Sharabu alifoka. Hadi akapepesuka kidogo kiasi cha kutaka kuanguka lakini aliwahiwa kushikwa na Killa.

Rais Sharabu hakuwa tofauti na mtu atokaye ndani ya nyumba akasimama nje, halafu atemee mate ndani.

Mmoja wa vijana wa usalama wa taifa akaagizwa aelekee nyumbani kwa Tuachie. Akafanya hivyo, na kurejea saa moja na nusu baadaye.
“Hayupo Mkuu. Na nyumba ipo tupu,” yule kijana alieleza matokeo aliyokutana nayo.
Rais Sharabu akazidi kuwa mwenye ghadhabu.
“Huyu mtu! Huyu mtu!” Rais Sharabu alimaka. “Hivi anafahamu kweli kwa kina upande wangu wa pili wa shilingi ulivyo?” aliendelea kumaka.
“Anaonekana anataka akupotezee tonge wakati limeshafikia mdomoni,” Maua alichangia hoja.
“Sasa nitamdhibiti vipi?”

Killa akaingilia kati, “Kuna Kamati Kuu mheshimiwa. Nina hakika ni sehemu salama kwa upande wako.”
“Una hakika?”
“Yeah!”
“Vipi, unafahamu genge lililopo nyuma ya Babigamba? Kama kwenye Kamati Kuu wapo itakuaje kwa upande wangu?”
“Nina hakika, wajumbe wa Kamati Kuu hawawezi kukuangusha.”

Ukapita ukimya mfupi. Uliomshinikiza kila mmoja aingie kwenye fikirio.

***

Wajumbe waundao Kamati Kuu ya chama cha Chautu hawakuisha kugawanyika. Mgawanyo uliobeba siri nzito vifuani mwao, kwa kila mmoja kuegema upande aupendao. Wale waliogema upande wa Rais Sharabu walikesha karibia dakika zote kumtafuta Tuachie, lakini hawakupata mafanikio chanya.

Tuachie aliendelea kutopatikana hewani.
“Muache. Tutakutana kamatini, huko ndipo tutamuonyesha kwamba sisi ni wajanja wa mjini kitambo.”
“Hakika unenacho. Rais Sharabu ni lazima aongoze awamu ijayo.”

Yalikuwa baadhi ya maongezi baina ya wajumbe wachache wa Kamati Kuu ya chama cha Chautu.

Ilikuwa ni alhamis, Kamati Kuu ya chama cha Chautu ilivyokutana kujadili majina ya watia nia. Ilikutana jijini Kondeni. Kwa kawaida, Kamati Kuu huongozwa na Mwenyekiti wa chama taifa. Ambaye ndiye Rais Sharabu. Lakini kutokana alikuwa kwenye orodha ya watia nia, hakupaswa kuongoza kikao. Wajumbe walimchagua Mwenyekiti wa muda, kwa sababu Makamu Mwenyekiti ambaye alipaswa kuongoza, naye ni mtia nia pia. Hivyo hawakupaswa kuwepo kikaoni.

Kikao kiliongozwa na Makamu wa Rais, Lilian Mkumba. Wajumbe walimpatia wadhfa huo kwa kura walizopiga.

Kikao kilikuwa kizito. Kutokana na mtafaruku wa moto wa maneno waliyokuwa wanapandishiana. Katika kamati ile walikuwa nusu nusu. Nusu walimkubali Rais Sharabu, nusu wengine walimkubali Babigamba. Haikuwa rahisi kupata maamuzi. Lakini palipo wengi, hamna kishindikanacho. Hivyo mwisho wa mzozano wao waliafikiana, kwa namna ile ile waliyogawanyika. Majina yote yalihalalishwa kufikishwa mbele ya mkutano wa halmashauri kuu (NEC).
“Mbona haya mambo yanazidi kuwa magumu kwangu?” Rais Sharabu aliuliza kwa kufoka mara baada ya kupatiwa maamuzi ya Kamati Kuu.
“Nami nimeshindwa kuelewa, wale wajumbe wengine wameshawishika vipi na Babigamba. Na wameshawishika muda gani?” Maua naye alitoa mashaka aliyonayo.
“Yakifika kwenye mkutano wa halmashauri kuu una hakika nitapita? Hayatotokea haya ya kushangaza yaliyotokea Kamati Kuu?”
“Mheshimiwa, nashindwa nikuahidi nini. Nimechanganyikiwa kupita maelezo.”
“Mmmh! Tuachie.” Rais Sharabu alisema na kutikisa kichwa. Akionekana mwenye kutafakari jambo, baadaye aliendelea, “Nina wasiwasi mpango wake unaratibiwa na watu makini sana. Tena waliopo ndani ya mfumo wa serikali na chama. Na kafanya hivyo kwa muda mrefu. Babigamba, kwa nini sikukutambua mapema?”
“Kila uwazacho muda huu kipo sahihi. Isivyo bahati, tumefahamu kwa kuchelea. Hatuna namna zaidi ya kusubiri maamuzi ya wajumbe wa mkutano wa halmashauri kuu. Masubirio hayo yasiwe ya kukaa tu...” Maua alishauri. Hakufanikiwa kumaliza kauli yake.

Rais Sharabu akamkatisha, “Unataka tufanye nini?”
“Turefushe mikono, ili huruma yao kwako iwe yenye thamani.”

***

Usiku wa siku ya kikao cha Kamati Kuu Rais Sharabu alikutana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama Ikulu ndogo jijini Kondeni. Lengo la makutano yake nao, ni kuhakikisha dhamira aliyonayo haiangukii pua. Hakuwa tayari kuona anapigwa chini kwenye kura za maoni na kuikosa nafasi ya u-Rais. Alihitaji kubaki madarakani kwa gharama zozote. Ili aepuke aibu ya kuwa Rais aliyeongoza kwa muhula mmoja. Wakati huo huo afute makando kando yaliyoumiza wananchi.
“Mimi ndiye niliyewaweka kwenye hizo nafasi mulizonazo sasa. Je, kuna yeyote ambaye yupo tayari kupingana nami?”
“Hapana,” wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama waliitikia kwa pamoja.
“Vizuri,” Rais Sharabu alisema na kutulia kwa sekunde chache. Akaendelea, “Yupo yeyote ambaye ataona sawa tu mimi nikichezewa?”
“Hapana,” walijibu pamoja kwa mara nyingine.

Rais Sharabu alitingisha kichwa juu-chini na kumuangazia kila mmoja. Aliwasaili wote, alivyomaliza, alitokwa na kauli. “Ninyi ndiyo mkono wangu wa kulia. Kuna watu wanataka kunichezea, mchezo ambao unanionyesha naenda kuikosa nafasi ya kuliongoza hili taifa kwa muhula wa pili. Nami sihitaji hicho kitendo kitokee. Nitadhalilika.
“Hivyo wito wangu kwenu, ni kunilinda katika hili.”
“Kwa namna ipi?” Jenerali Namkumba aliuliza.
“Chamani hali si ya kuaminika. Nipo mguu ndani, mguu nje-naweza kuangushwa. Kuepuka aibu hii, nahitaji nitangaze hali ya hatari, itakayosimamisha shughuli zote. Hapo uchaguzi utasimama, nami nitapata nafasi upya ya kukabiliana na wapinzani wangu.”

Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama walishusha pumzi na kuzitua kwa nguvu. Ukimya ukachukua nafasi.

Sababu yeye ndiye final say, hakuna aliyetokea kupinga wazo lake. Wote waliafikiana naye. Ijapokuwa, kwa Jenerali Namkumba na IGP Lukanga waliridhia kwa nia ya kutompa hofu itakayomfanya agundue sio sehemu ya mkakati wake.

ITAENDELEA...

HABARI NJEMA

KITABU CHA RIWAYA YA NENDA KINAENDELEA KUPATIKANA RENICS BOOKSHOP TAWI LA MOSHI KWA GHARAMA YA TSH. 10,000/= MAWASILIANO: 0767826134
 
RIWAYA: MKOLONI MZAWA—2
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
SEHEMU YA 21.

Siku ya mkutano wa halmashauri kuu ya chama cha Chautu iliwadia, ijumaa. Wajumbe wengi waliwasili ukumbini. Wengi wao wakiwa wenye bashasha, na shamra shamra nyingi. Kutimiza wajibu wao kuliwafanya hivyo. Wajumbe zaidi ya mia tatu, kutoka mikoa na wilaya tofauti tofauti nchini.

Makamu wa Rais, Lilian aliendelea kuongoza kama Mwenyekiti. Mwenyekiti wa muda. Mchakato utakapomalizika, na wadhfa huo utafikia ukomo.

Kutokana na hasira, zilizompelekea baadaye awe na hofu, Rais Sharabu alifuata ushauri wa Maua, wa kurefusha mkono. Alimwaga mlungula kwa wajumbe kadhaa kwa kutumia vijana wachache aliowaandaa.

Uzuri, hakuna aliyewabaini. Hivyo mambo yalienda kimya kimya. Wakati huo huo aliratibu mpango wa pili aliozungumza nao wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Lengo, pale apatapo tu tetesi za kupigwa chini, aondoke ukumbini, akahutubie taifa na kutangaza hali ya hatari kama alivyoona inafaa kwa ukombozi wake. Chombo cha habari cha taifa ndicho kiliandaliwa rasmi kwa kazi hiyo. TCB (Tuleane Company of Broadicasting).

Hii ilikuwa sambamba na kuandaliwa kwa kikundi maalumu cha usalama wa taifa (PSU) na baadhi ya makomando watakaompatia ulinzi pindi anahutubia.

***

Mtaji pekee waliokuwa nayo timu iongozwayo na Luteni Jenerali Kipozi ni maneno. Waliamini katika ushawishi wa kauli. Hivyo Ndalama alizidi kuwashawishi watu wake nao wawashawishi watu wengine-wajumbe wa mkutano wa halmashauri kuu, siku ya uchaguzi waende na Babigamba.
“Sisi hatuna tatizo. Lakini kuna harufu imeshaanza kufuka.”
“Kutoka wapi?”
“Kwa Rais Sharabu.”
“Harufu ya nini?”
“Hongo. Kwa tetesi nilizonazo, baadhi ya wajumbe wamepewa mtonyo wamchague Sharabu, unadhani tutaweza kuwabadilisha?”

Ndalama alivuta pumzi na kuzitua kwa nguvu. Alikuwa anazungumza na Bi. Siti Likuluta.
“Mbona kimya?” Bi. Siti alimtupia ulizo lingine.
“Umenifanya niwe mwingi wa mawazo kufikiri namna ya kukabiliana na hilo tatizo.”
“Pasi na kukuongopea, tulishaanza kusambaza hila zetu. Kabla hatujamaliza, ndipo ilipojitokeza hiyo harufu. Tunaiondoaje?”
“Musikate tamaa. Endeleeni kufanya. Vitendo vyao visiwavunje nguvu.”
“Wacha tuone. Ijapokuwa uhakika wa ufanikishaji ni mdogo. Kwa sababu hakuna anayebadilisha maamuzi kwenye pesa. Labda, kama mpinzani atapanda dau.”

***

Siku ya uchaguzi, jumamosi. Wajumbe walikuwa na wingi wa shamra shamra. Kila aonekanaye, alionekana kuwa na bashasha tele wajihini. Bashasha lililoundwa kwa cheko.
“Siku ya kuchinja mtu.”
“Leo ndiyo leo. Tunaenda kuua.”

Wajumbe wengi walisikika. Wengine walipiga vijifo, mbizi, ili mradi waonyeshe kiasi cha furaha walichonacho.

Wengine walisikika wakiimba pia.

Tuna imani na Sharabuuu
Oyaaa, oyaaa, oyaaa
Tuna imani na Sharabuuu
Oyaaa, oyaaa, oyaaa
Sharabu kweli!
Kweliii
Kweli!
Kwelii, kwelii, kwelii kabisa.
Sharabu kweli!

Muda paswa ulivyowadia shughuli ikaanza. Hakukuwa na mambo mengi, utaratibu uliwekwa wazi, namna gani wajumbe wanapaswa kupiga kura, baada ya hapo mchakato ukahalalishwa.

Wajumbe walifanya yao.

Upigaji kura ulivyomalizika ukaanza mchakato wa kuhesabu. Kamati ya uhesabuji ilichukua nafasi, chini ya uangalizi mkali kuhakikisha hakuna hujuma yoyote. Wakati huo kila pande ikiwa na mwakilishi wake. Wa kufuatilia zoezi zima.

***

Saa tisa alasiri ndipo kamati ya uhesabuji ilimaliza shughuli. Wakarejea ukumbuni, wajumbe wakiwa kimya kwa hamu ya kutaka kufahamu matokeo. Hata wanakamati walivyoleta mbwembwe za kucheza michezo kadhaa, hakuna sauti iliyosikika kutoka kwa wajumbe kushangilia mchezo husika. Zaidi, walifungua kingo za midomo kuonyesha tabasamu.

Matokeo yalipokabidhiwa kwa Makamu wa Rais, Lilian, ambaye ndiye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo, ndipo lilipoibuka shangwe la nguvu kutoka kwa wajumbe.

Shangwe hilo lilikuwa la kila aina, kwa sababu kila mmoja alitokwa na kile alichojisikia. Awamu hii, wimbo ulibadilika. Hata waimbaji pia, hawakuwa wale walioimba mwanzo. Ijapokuwa wimbo ulikuwa ule ule, walibadili neno tu, Sharabu. Wakaweka Babigamba.

***

Rais Sharabu alipata simu. Akatoka ukumbini, mlinzi wa karibu akiwa nyuma yake.
“Mheshimiwa, hali si hali. Mambo ni mabaya upande wako,” sauti ya upande wa pili wa simu ilisikika. Sauti ya kiume-nzito nzito.

Rais Sharabu akageuka nyuma kuutathmini ukumbi. Makelele ya wajumbe wakiendelea kuimba yakapenya vilivyo masikioni mwake. Akajaa hasira, kiasi cha kutamani arejee ndani haraka iwezekanavyo, awanyamazishe na kughairisha mkutano.

Sauti ya upande ikaendelea, “Babigamba ameongoza, kwa asilimia zaidi ya sabini.”
Rais Sharabu akakata simu.

Aliifikiria kwa muda ile kauli. Mlinzi akiwa jirani naye, akimshuhudia vilivyo namna anavyopata tabu. Alitamani amuulize, lakini alipotezea.

Baadaye Rais Sharabu alimpigia simu Killa. Ikiwa imepita dakika moja toka alivyodokezewa matokeo ya uchaguzi yalivyo.
“Nindalie mazingira. Naja hivi sasa.” Akakata simu.

Alivyokata simu, sekunde chache baadaye iliwasili gari mbele yake. Aliingia, sambamba na yule mlinzi, kisha gari ikaondoka.
Ukumbini.

Ukimya ulifuatia baada ya shangwe za muda mrefu. Kimya kikatawala kama ilivyokuwa awali pindi wanasubiri matokeo. Lakini kimya cha sasa kilikuwa na masubirio ya Rais Sharabu. Arejee ukumbini, matokeo yatangazwe.

Dakika zilikatika, moja baada ya nyingine, Rais Sharabu hakutokea ukumbini. Ikabidi atumwe mtu akamuangalie, alivyorejea, jibu alilowapatia viongozi waliopo meza kuu likawaacha na sintofahamu. Ni Makamu wa Rais, Lilian pekee, ndiye hakushangazwa na lile jibu. Yeye alifinya tu kingo za mdomo, wakati wajumbe wakiwatumbulia mboni zao kutaka kufahamu kiendeleacho.

Ikaanza minong’ono.

Haikuchukua muda mrefu, ilikatishwa na badiliko la matangazo ya runingani. Kuna runinga zilifungwa mule ukumbini, ambazo zilikuwa zinaonyesha mubashara tukio la mkutano wao.
“Nini tena hii!”
“Amaaah!”

Kila mmoja alishangaa kwa namna yake.

Badiliko hili lilijitokeza karibia idhaa nyingi za runinga za ndani. Lilitoka onyesho la mkutano wa halmashauri kuu, na kusikika wimbo wa taifa, huku bendera ya taifa ikipepea mlingotini, ishara, Rais anaenda kuhutubia taifa.
“Jamani, mbona maajabu haya!”
“Haijawahi kutokea. Mkutano ughairishwe tu.”

Wajumbe waliendelea kustaajabishwa. Na kutoa mapendekezo nini kifanyike kwa kitendo kilichojitokeza. Macho, masikio, mioyo na akili, wakaielekeza kwa Makamu wa Rais, Lilian, kuona nini ataamua.

***

Msafara umsindikizao Rais Sharabu kuelekea Ikulu ndogo, ndani ya jiji la Kondeni ulikuwa na jumla ya magari manne; mbele mawili, ya maafisa wa usalama wa taifa, escort one (E1) na escort two (E 2). Gari ya tatu ndiyo alipanda Rais Sharabu, halafu ya nyuma, ilikuwa ya maafisa wa usalama wa taifa pia. Escort three (E 3).

Huko ndipo alipaswa kwenda kuhutubia taifa. Ili aepuke aibu ya matokeo ya kura za maoni. Mbwembe zote zile! Ataongozaje muhula mmoja? Wakati kila uchao alikesha kujitapa yeye ndiye Rais pekee makini, zaidi ya waliotangulia.

Ndani ya gari mulitawaliwa ukimya. Kila mmoja alionekana kujali la kwake. Hakuna aliyejitokeza kujali la mwingine nobe! Kumsemesha kwa jambo fulani tu. Rais Sharabu alikuwa mwingi wa ufikiriaji, mlinzi wa karibu, kaangazia mboni zake kwa umakini barabara waelekeayo, wakati dereva naye kawa makini kwenye uendeshaji.

Cha kustaajabisha! Nafasi ya dereva ilikaliwa na Luteni Jenerali Kipozi. Alikuwa amevaa kiraia. Kaunda suti-rangi nyeusi. Ikiwa na mfanano wa kila kitu na ile iliyokuwa imevaliwa na dereva husika wa Rais Sharabu. Ambaye alitekwa mapema tu, baada ya Rais Sharabu kuingia ukumbi wa mkutano. Alitekwa, kwa usiri mkubwa, pasi na watu wengine kufahamu, akaenda kufichwa umbali mdogo toka kwenye jengo la ukumbi wa mkutano.

Hakuna aliyeshtukia, wala aliyekumbuka kumsaili.

Msafara ulivyofika kwenye mzunguko; uunganishao barabara tatu, zile gari mbili zilizotangulia, za maafisa usalama wa taifa zilipita upande wa kushoto mwa mzunguko na kunyoosha kuifuata barabara ielekeayo Ikulu ndogo. Ambayo ilijengwa nje kidogo ya jiji.

Luteni Jenerali Kipozi akafanya jambo la tofauti.

Hakuzifuata zile gari. Aliuzunguka kabisa ule mzunguko na kuirudia ile ile barabara waliyokuja nayo. Gari ya nyuma ikawafuata. Hapo ndipo Rais Sharabu na yule mlinzi wake-Kanali wa Jeshi la Ulinzi waliposhtuka, wakamtupia mboni kwa mihemko iliyopelekea kuihangaisha miili yao.

Wale waliopo magari ya mbele nao walishtushwa na kitendo hicho. Wakafunga breki ghafla na kurudi kuifuata gari ya Rais Sharabu ielekeako. Hawakutambua, kama kuna kupe kaingia kuvuruga mambo.
“Weee!” Rais Sharabu alimaka. Akiwa amejiinua kidogo sitini kumvaa Luteni Jenerali Kipozi.

Luteni Jenerali Kipozi akaachia moja ya mkono, wa kushoto, kwenye usukani na kumkita kiwiko usoni Rais Sharabu. Rais Sharabu akarudi nyuma na kuketi wakati huo lile pigo la kiwiko likimpata kwenye kingo za mdomo. Likamchana sehemu ndogo iliyofanya atokwe na damu, huku akiugulia maumivu kwa kiasi.

Yule mlinzi wa karibu akataka kuleta purkushani. Kwa kuinua moja ya mkono amkabe Luteni Jenerali Kipozi shingoni akose uhimili wa kuendesha. Wakati mkono mwingine, akiuhangaisha mgongoni kwake. Alionekana kutoa kitu, kilichompa utambuzi Luteni Jenerali Kipozi kuwa ni bastola. Hivyo ule mkono uliolekezwa kwake aliukamata kwa nguvu kabla haujamfikia na kuunyonga.

Yule mlinzi aligugumia kwa maumivu, hata kabla hajakaa sawa, Luteni Jenerali Kipozi alirusha ngumi mfululizo zilizoenda kumpata kwenye taya na sehemu ya shingo. Akazima.
“Usalama wako ni kukaa kimya,” Luteni Jenerali Kipozi alimuonya Rais Sharabu. Akanywea. Kama gunia la pamba likichovywa kwenye maji.

Maafisa usalama wa taifa waliopo gari zingine iliwasukuma kufanya mawasiliano kuona nini tatizo hadi uelekeo ubadilike. Waliita, call sign ya gari ya Rais, lakini haikupokelewa. Wakampandia hewani Mkurugenzi wao, Killa. Kwa kutumia redio za upepo.
“Gari ya Tiger (neno la siri limaanishasho Rais kwa lugha ya intellijensia) imebadili uelekeo, tunawatafuta hewani hawatoi mrejesho. Nikiwa na maana redio haipokelewi. Kuna lolote?”

Killa alishtuka. Baada ya sekunde kadhaa ndipo alijibu, “Nipeni subira, nitawarejea.”

Alivyotoka kwenye mawasiliano na vijana wake alitoa simu janja mfukoni mwake akampigia Rais Sharabu. Iliita pasi na kupokelewa. Akapiga mara ya pili, ikawa vivyo hivyo.

Akawarudia vijana wake.

“Nadhani kuna jambo, ambalo si zuri kwa upande wetu. Hakikisheni gari ya Tiger mnai-stopisha.”
“Five-five!”

Gari za maafisa usalama wa taifa zikaongezwa mwendo ili waiwahi gari ya Rais Sharabu. Lakini Luteni Jenerali Kipozi naye alikuwa haendeshi mwendo wa kitoto.

Maafisa usalama wa taifa waliifukuzia pasi na mafanikio. Kwani waliikuta gari imeshaegeshwa usawa wa lango la kuingilia ukumbini. Luteni Jenerali Kipozi akamzindua yule mlinzi kisha aliwaamuru kwa pamoja wateremke waingie ukumbini. Hawakuwa na namna, hasa Rais Sharabu, zaidi ya kutii.

Rais Sharabu aliingia ukumbini kwa bashasha bandia alilolitengeneza wajihini, nafsi ikiwa imejaa hasira maafisa usalama wa taifa ambao walikuwa kwenye gari ya E 1, 2 na 3 walimvaa mvaa Luteni Jenerali Kipozi. Walimwamuru ateremke garini, naye kutii.

Aliteremka, mmoja wao akataka kumkwida kwa kumshika ule mtindo wa Tanganyika jeki. Watumiao sana askari wa jeshi la polisi.
“Nini mnafanya?” Luteni Jenerali Kipozi aliuliza.

Wale maafisa usalama wa taifa hawakumjibu. Mmoja wao alimpiga kofi la nguvu shavuni wakati wawili waliopo nyuma yake na kumkamata ule mtindo walimshinikiza atembee. Waliopo pembeni wakabaki kushuhudia filamu ya bure.
“Hebu angalieni juu kwanza, katika baadhi ya majengo yanayotuzunguka hapa tulipo, ndipo mufanye mnachotaka kukifanya,” Luteni Jenerali Kipozi aliongea huku akileta ubishi wa kupiga hatua kwenda mbele.

Juu, baadhi ya majengo, na jengo lenyewe la ukumbi wa mkutano kulikuwa na wadunguaji waliochomoza mitutu ya bunduki kuelekezea usawa wa pale walipo.

Wavamizi!

***

Makamu wa Rais, Lilian alimtangaza Babigamba kuwa mshindi. Ukumbi ukalipuka shangwe, vifijo na kila aina ya nderemo. Tukio lililochukua muda mrefu kiasi kuja kuhitimika. Watu walifurahi, tena wengi tu, huku Rais Sharabu akitengeneza chuki kali dhidi yao.

Kutokana na hasira alizonazo zilizokaba koo, alishindwa hata kuzungumza vizuri wakati wa kushukuru na kumpongeza Babigamba. Chuki yake ilijionyesha dhahiri. Kiasi kwamba, hata kabla hajahitimisha hotuba alidondoka na kupoteza fahamu.

***

Rais Sharabu alizinduka saa tatu baadaye. Akiwa Ikulu ndogo. Kitu cha kwanza, aliomba kukuonana na Killa. Killa Lauma. Killa anayeshindwa kutumia tabia ya neno kumfanikishia Rais Sharabu mipango yake.

Killa alivyowasili walifungua uwanja wa maongezi.

“Tunahisi uwepo wa orodha kubwa iliyoongoza hujuma dhidi yako...” Killa alieleza. Rais Sharabu kamtumbulia mboni zake kwa umakini, masikio nayo kayatega vyema aambiwacho kisimponyoke. Akikamate vyema na kukihifadhi kwa usahihi. Killa aliendelea, “Wa kwanza Luteni Jenerali Kipozi...”

Rais Sharabu akakamkatisha, “Huyo ni sahihi. Nimemuona. Ni mshenzi sana.”
“Wa pili, Ndalama.”

Rais Sharabu akauliza kwa mshangao, “Etii! Huyu aliyekuja kwangu kuungama?”
“Yeah! Tunahisi naye yumo kwenye mkumbo.”
“Subiri kwanza.” Rais Sharabu akajipa nafasi ya kufikiria. Ilikuwa kwa sekunde chache, baadaye alimruhusu Killa aendelee.
“Wengine, Lilian.”
“Huyu Makamu wangu?”
“Hakika.”
“Na kwa kumalizia, Mkuu wa Majeshi na IGP sio watu wa kuwaamini kwa asilimia zote.”
“Kwa nini?”
“Nahisi nao wanauhusika. Kwa sababu ushirikiano wao kwangu hauna nguvu. Ni wa kusua sua.”
“Tufanyaje kuwabaini? Ikiwezekana hata huyo mbwa wao asifikie muda wa dirisha la vyama kuanza kampeni.”
“Ajali. Tumtengenezee ajali, tena iwe ajali kweli, ambayo hawezi kuchomoka akiwa mzima,” Killa alishauri.

Rais Sharabu alifikiria kwa muda. Kitendo kilichozalisha ukimya, baadaye aliufukuza, “Nadhani upo sawa. Hawa mbwa wote ulionitajia lazima niwanyooshe.”

Naam! Rais Sharabu alijaa roho yenye ukatili iliyofunikwa na ushamba wa sura.

ITAENDELEA...

HABARI NJEMA

KITABU CHA RIWAYA YA NENDA SASA KINAPATIKANA RENICS BOOKSHOP TAWI LA MOSHI KWA GHARAMA YA TSH 10,000/= MAWASILIANO: 0767826134
 
RIWAYA: MKOLONI MZAWA—2
MTUNZI: HASSAN MBONECHE
SEHEMU YA 22.

Luteni Jenerali Kipozi aliongoza timu katika hafla ya kupongezana kufanikisha sehemu ya mkakati wao. Hafla iliyofanyika usiku wa manane, kwenye moja ya hoteli katikati ya jiji la Nufaiko.

Walikula, walikunywa na kusaza. Mwisho ulivyowadia, saa kumi usiku kila mmoja alielekea kwenye usafiri aliokuja nao tayari kwa kurudi nyumbani.
“Tusisahau, mchana wa leo tukutane,” Makamu wa Rais, Lilian aliwakumbusha jambo wenzie.
“Hilo hali...halisaaaa...uliki,” Babigamba aliongea kwa sauti ya ulevi. Akiwa anaelekea alipoegesha gari yake. Alipoifikia, aliingia ndani ya gari, aliungurumisha injini safari ikaanza.

Safari na ulevi. Tena chakari, kiasi cha kudhania yeye ndiyo kiwanda cha utengenezaji.

Mwendo alioenda nao Babigamba ulikuwa wa kushtuka shtuka. Hakuumiliki vyema; kuna sehemu aliendesha kasi, sehemu nyingine aliendesha mwendo mdogo, pasi na mpangilio wowote. Ukiachana na hilo, alikuwa anayumba sana barabarani.

Hatua chache nyuma yake kulikuwa na gari ya kina Kinyonga ikimfuata. Babigamba hakufahamu.
“Anakuja,” Kinyonga alisikika akiongea na simu. Nyuma ya usukani aliketi Mauten-alirejea kwenye hali nzuri.
“Hamna shida. Nimeshajiandaa vya kutosha. Nauona mwanga kwa mbali,” ilisikika sauti ya kike kutoka upande wa pili wa simu. Sauti ya Shida.

Mwanga ulivyokaribia zaidi Shida alisogeza gari barabarani. Akafunga breki ghafla, akateremka na kujiviringisha kwa kasi. Aliviringikia upande ambao aliamini gari haiwezi kumpata endapo kile akitakacho kitajitokeza. Babigamba agonge ile gari yake.

Ikawa hivyo.

Babigamba akiwa hana hili wala lile, aliiparamia ile gari-Fuso, iliyokuwa imepakizwa mchanga nyuma, sehemu ya tela. Na kufanya ajali mbaya kutokea. Kwani fuso iliviringika, na gari ya Babigamba nayo iliviringika mara mbili, ilivyokuja kutulia, ikapinduka kwa matairi kutazamia juu.

Pindi Babigamba anapambana na uokozi wa ajali, gari la kina Kinyonga liliwasili alipo Shida. Shida alipanda ndani ya gari, pasi na kujali hali aliyonayo-alipata michubuko midogo usoni. Kinyonga akaliondoa gari na kwenda kutega mahali. Wakaangazia ajalini kuona kiendeleacho.

Watu walivyojazana eneo la tukio, Kinyonga na wenzie walijirudisha kuwa sehemu ya mashuhuda. Hawakwenda na gari. Waliliacha pale pale walipolificha. Hawakuacha kufuatilia kila hatua.

Babigamba alitolewa ndani ya gari yake akiwa hana fahamu na kupakizwa kwenye gari la jeshi la polisi. Ambao waliwasili muda mchache mara baada ya kupatiwa taarifa. Hawakumkawiza, safari ya kuelekea hospitalini ikaanza. Huku washuhudiao wakibaki wenye manung’uniko ya kuamini ameshafariki dunia. Ijapokuwa wengi wao hawakumfahamu kama ni Babigamba, zaidi ya askari na watu wachache waliosaidiana nao wakati wa kumtoa garini.

Gari la polisi lililombeba Babigamba lilipofika umbali wa mita kadhaa, Kinyonga aliwashtua Shida na Mauten warejee garini kwao.

Walirudi. Tena kwa haraka sana. Dakika nne baadaye wakawa nyuma ya ile gari la jeshi la polisi.
“Anapelekwa hospitalini. Lakini haonekani kuwa mzima. Sisi tupo nyuma ya gari husika hadi mwisho,” Kinyonga alimtaarifu Killa kwa njia ya simu. Alimpigia.
“Usiache kunipa taarifa yoyote. Juu ya hilo niwapongeze kwa kazi nzuri. Kifo chake ndiyo hitajio la bwana mkubwa.”
“Sawa mkuu. Kwetu ni utii pekee. Awamu hii, kamwe hatuwezi kuwaangusha.”

Kinyonga akakata simu.

***

“Vijana wameshatekeleza. Hali yake si nzuri, muda wowote tutarajie matarajio yetu,” Killa alisikika. Akiwasiliana na mtu wa upande wa pili kwa njia ya simu. Rais Sharabu.
“Kazi nzuri. Kwa sasa wako wapi?” Rais Sharabu aliuliza.
“Wanaelekea hospitali.”
“Waambie watulie mahali. Mimi nawe ndiyo twende huko. Nahitaji nihakikishe kifo chake. Na ili kama bado hajafa, nimuue mwenyewe.”
“Hamna shida mheshimiwa.”

Rais Sharabu alivyomaliza mazungumzo aljiandaa kwa mtoko kama alivyomuahidi Killa. Ulikuwa mtoko haswa, uliozuia utambuzi kwa watu wengine. Kichwani alivaa mzula rangi nyeusi, akauteremsha karibu na nyusi. Pasi na kusahau koti kubwa, lililoshuka hadi chini ya magoti-ndani yake alivaa fulana mchingo rangi ya maziwa.

Suruali, alivaa jinzi. Buti kubwa chini na glavus zilizokatwa kidogo sehemu ya vidole. Hivyo vidole vilionekana.

Dakika kumi baadaye alikuwa ndani ya gari sanjari na Killa. Gari ya kiraia. Killa ndiye alikuwa anaendesha. Safari hospitalini.
“Leo ndiyo mwisho wa uwepo wake hapa duniani huyu mbwa,” Rais Sharabu alinuia.

***

Ilivyogota saa 11 alfajiri Rais Sharabu na Killa waliyafikia maegesho ya vyombo vya usafiri hospitali aliyopelekwa Babigamba. Hospitali ya taifa Marupi. Wakateremka garini na kupiga hatua kuelekea ndani ya moja ya jengo la hospitali.

Upande wa pili, eneo lile lile la maegesho, napo alionekana Luteni Jenerali Kipozi akiteremka garini na kuingia ndani ya jengo waliloingia Rais Sharabu na Killa. Naye hakuvaa ki-wema. Alivaa kinyemela kwa nia ya kupoteza uhalisia wake.

Alivaa kapelo rangi ya kijivu. Koti jeusi, ndani fulana rangi ya bluu-bahari, suruali ya jinzi rangi nyeusi na raba chini.

Kwa pamoja shabaha yao ilikuwa moja tu. Kufikia chumba cha wagonjwa walio chini ya uangalizi maalumu (ICU-Intensive Care Unit). Babigamba alilazwa ndani ya chumba hicho kwa matibabu zaidi. Kutokana na hali yake kuwa mbaya sana, kiasi cha kupoteza matumaini ya kuwa hai tena.

Kila mmoja mwendo wake ulikuwa wa taratibu lakini wenye haraka. Cha zaidi, walitembea kwa hadhari pasi na kuonana wala kufahamu mafuta na maji yanafuata mkondo mmoja.

Rais Sharabu na Killa walivyofikia chumba cha ICU, Killa alifungua mlango taratibu mboni zao wakizitupia kilipo kitanda.

Hakukuwa na mtu. Mioyo ikapiga kite kwa uchungu.

“Mbona hakuna mtu?” Rais Sharabu aliuliza. Mboni akizihangaisha huku na kule kwa uchunguzi zaidi. Lakini hakukuwa na mabadiliko ya matokeo.
“Yumkini amepata nafuu, wakaamua kumuhamisha. Tukamuangalie kwenye wodi za kawaida,” Killa alishauri.

Walishinda mule ndani kwa dakika tatu tu, wakatoka wakiwa na nuio aliloshauri Killa. Wakamuangalie kwenye wodi za wagonjwa wa kawaida. Ambao hawana hali mbaya. Walivyouacha mlango wa chumba cha ICU, tayari kwa kuelekea wodi za kawaida, walimuona mtu aliyevaa kiraia mbele yao umbali wa mita kumi na tano akisukuma kitanda cha magurudumu manne kwa kasi. Wakamtilia shaka.

Alikuwa Luteni Jenerali Kipozi. Wakamuungia.

Walimfuatilia kwa mbio. Lakini katika hali ya kushangazwa, walikuja kuachwa kwenye mataa. Luteni Jenerali Kipozi alipita chocho zilizowachanganya na kuwafanya watokee walipoanzia utafutaji awali.

“Itakuwa ameelekea wapi huyu mtu?” Killa aliuliza. Akiwa mwenye kuhema juu juu, jasho jembamba likimtiririka.
“Una uhakika ndiye mlengwa wetu? Na umebahatika japo kutambua sura ya mtu mwenyewe?” Rais Sharabu alijibu swali la Killa kwa mtindo wa swali. Naye akiwa katika hali aliyonayo Killa.
“Ingelikuwa sio mlengwa asingelitukimbia.”
Wakapiga hatua hadi dirishani na kutupa mboni zao nje.

Kwa msaada wa taa chache zilizokuwa zinawaka, walimuona yule mtu wamfuatiliaye akiingiza machela iliyolaliwa na mgonjwa juu yake ndani ya gari.
“Twende tumuwahi. Pia waandae vijana,” Rais Sharabu aliamuru na kutoka mbio kuelekea nje. Walizishuka ngazi kwa kasi. Wakati huo huo Killa akijitahidi kufanya mawasiliano kwa njia ya simu kama alivyoamriwa.
“Mupo jirani na hospitalini?” Killa aliuliza. Mara baada ya simu kupokelewa.
“Ndiyo mkuu,” sauti ya upande wa pili ilijibu. Sauti ya Kinyonga.
“Kaeni usawa wa barabara inayoruhusu magari yatokayo hospitalini. Hakikisheni gari inayotoka kuanzia sasa haiwapotei machoni mwenu.”
“Tunaruhusiwa kuishambulia?”

Badala ya kujibu, Killa alimtupia swali Rais Sharabu, simu ikiwa bado ipo hewani, “Waishambulie?”
“Ikibidi,” Rais Sharabu alijibu.

Killa akamrudia Kinyonga. “Munaruhusiwa kuishambulia endapo mtahisi anawapatia usumbufu.”
“Sawa mkuu.”

Simu ikakatwa.

Kinyonga na wenzie walitii maagizo waliyopatiwa. Rais Sharabu na Killa nao walivyoifikia gari yao walipanda na kuunga nyuma ya gari la Luteni Jenerali Kipozi.

***

Baada ya mwendo wa dakika kadhaa Luteni Jenerali Kipozi aliegesha gari maeneo ya kichani, pembezoni mwa barabara. Mita chache kutoka hospitalini. Muda mfupi baadaye ikawasili gari nyingine pale alipo. Walikuwa ni Luteni Mwaipeta, Koplo Namaya na Konstebo Babaa.
“Yatupasa kumwamishia kwenye gari yenu, kisha muondoke kwa kupita njia tofauti na nitakayopita,” Luteni Jenerali Kipozi aliwaeleza.
“Kuna lolote?...” Koplo Namaya aliuliza. Kabla hajahitimisha Luteni Jenerali Kipozi akamkatisha.
“Upande wa pili wapo nyuma yangu. Niliwawahi, lakini wamenishtukia pindi natoka.”

Maelewano yalivyopita walitekekeleza. Tena kwa uharaka wasipate kufumaniwa. Mmoja wao, Konstebo Babaa, alipanda ndani ya gari iliyokuwa inaendeshwa na Luteni Jenerali Kipozi, halafu mwingine, Koplo Namaya akawa anaivuta ile machela taratibu kuitoa nje. Luteni Mwaipeta alikuwa anasaidia kuishika kati. Luteni Jenerali Kipozi akifanya ulinzi kwa kuangaza huku na kule. Wakati huo akizidi kuwasihi wafanye kwa haraka zaidi.

Walivyofanikiwa kumteremsha na kuanza kupiga hatua kuelekea gari yao ilipo, umbali wa mita kumi, kina Kinyonga waliwavamia na kuanza kuwashambulia. Walivamia eneo lile kwa mguu, gari yao waliiacha umbali mdogo nyuma.

Wakajipanga.

Kwa Luteni Jenerali Kipozi kuvuta bunduki yake toka siti za mbele ya gari. Halafu, Luteni Mwaipeta aliachia machela akawa anasaidizana na Luteni Jenerali Kipozi kujibu mashambulizi. Koplo Namaya na Konstebo Babaa waliendelea kuishikilia machela, na kupiga hatua za uviziaji kukwepa mwenendo wa mtupo wa risasi kwa kutegemea uelekeo wautembeaji wa kina Kinyonga na wenzake.

Kwa namna Luteni Jenerali Kipozi na vijana wake walivyojipanga, walileta mfanano mithili ya kundi maalumu la usalama wakimuokoa VIP mara baada ya shambulizi kutokea. Kwani Luteni Jenerali Kipozi na Luteni Mwaipeta waliunda mstari mlalo-kama ukuta, uliowashinikiza kugandana, pasi na kutoa mwanya japo kidogo utakaoruhusu risasi kupita na kuwafikia waliopo nyuma yao; Koplo Namaya na Konstebo Babaa.

Usimamaji wao walipinda kidogo, kuwezesha bunduki kukita vyema kwenye nyama ya bega. Wakati Koplo Namaya na Konstebo Babaa wakiutumia ukuta ulioundwa kuzidi kujificha na kupiga hatua.

Baadaye, takribani muda wa robo saa toka kina Kinyonga walivyovamia, Rais Sharabu na Killa nao waliwasili kuongeza nguvu.
“Musiruhusu watutoroke,” Rais Sharabu aliamuru. Akiwa anachomoa bastola aliyokuwa ameisundika kiunoni upande wa mgongoni. Alikoki na kuruhusu mashambulizi.

Ilikuwa bastola aina ya Glock 17.

“Ninyi hampaswi kuwa hapa. Ondokeni. Luteni, ongoza timu muondoke,” Luteni Jenerali Kipozi aliwataarifu. Wakati mashambulizi yakizidi kupamba moto, kwa wao kushambulia huku wakirudi nyuma hatua fupi fupi bila kuusambaratisha ule ukuta-walizidi kugandana.
“Tutakuachaje peke yako?” Luteni Mwaipeta aliuliza.
“Noop! Go, go, go...” Luteni Jenerali Kipozi aliendelea kusisitiza.

Kwa msisitizo huo, Luteni Mwaipeta akautengua ukuta kwa kurudi nyuma hatua za kasi zaidi ya Luteni Jenerali Kipozi. Lakini hakupoteza uelekeo wake wa ushambuliaji.

***

Luteni Mwaipeta, Koplo Namaya na Konstebo Babaa walifanikiwa kumtorosha Babigamba. Luteni Jenerali Kipozi akasalia kuendelea mashambulizi, lengo, maadui zao wasipate nafasi ya kufuatilia. Hivyo alizidi kupambana kiume, akiwa amejificha nyuma ya mti mkubwa kwa ajili ya kujikinga.

Kina Kinyonga, walivyoona baadhi wamefanikiwa kutoroka, waliishambulia gari la Luteni Jenerali Kipozi na kulichakaza kiasi cha kutotamanika. Wakati huo, wengine wakimzunguka Luteni Jenerali Kipozi na kufanikiwa kumuweka kati.
“Jisalimishe,” Killa aliamuru.

Luteni Jenerali Kipozi alijaribu kupepesa huku na kule na kuona hakuna mwanya utakaomuwezesha kujinusuru. Hakuwa na namna, alitupa bunduki chini na kunyoosha mikono juu. Ishara kuwa amesalimu amri.

Killa alipiga hatua taratibu hadi pale alipo, muda wote bastola aliyokuwa ameishikilia ikiwa high ready kwa lolote litakalojitokeza. Rais Sharabu, Kinyonga, Mauten na Shida nao mitutu ya silaha zao zilikuwa ki-makabiliano endapo Luteni Jenerali Kipozi atajaribu kujitingisha kwa lolote.

Killa alivyomfikia Luteni Jenerali Kipozi aliiteremsha bastola yake akaisundika kiunoni, kisha aliikamata mikono ya Luteni Jenerali Kipozi kwa pamoja na kuiteremsha pia. Aliielekezea mgongoni, na kuifunga pingu.

Hawakukawia, walirejea walipoegesha gari zao, waliingia na kuondoka. Kila mmoja akiwa na chanuzi la tabasamu wajihini. Safari yao iliishia Bondeni, kwenye lile lile jengo lao la maficho. Walimtua Luteni Jenerali Kipozi, wakamfunga kwenye kiti na kuanza kumpatia mateso. Kinyonga ndiye aliyeanza, huku wakimtupia maswali yenye hitajio la kutoa siri za kundi lake.
“Ewe mbwa ulihisi hatutokupata?” Rais Sharabu alimuuliza. Akiwa anachukua mjeredi juu ya meza. Akapiga hatua chache hadi pale alipofungiwa Luteni Jenerali Kipozi.

Akamuinua kichwa kwa moja ya kiganja chake cha mkono na kumsaili kwa kebehi.

Rais Sharabu aliongea huku akitikisa kichwa, “Sasa upo mikononi mwangu. Mikono ya shetani aliyelaaniwa. Uta...” kabla hajamalizia, Luteni Jenerali Kipozi alivuta kohozi na kulitemea kwa nguvu usoni kwa Rais Sharabu. Kohozi lililochanganyikana; mate na damu.

Rais Sharabu akapandwa na jazba.

Alilifuta lile kohozi kwa kiganja chake, alipomaliza, aliinua mjeredi na kuanza kumtandika Luteni Jenerali Kipozi sehemu mbalimbali za mwili wake. Luteni Jenerali Kipozi hakuwa na la kufanya, zaidi ya kugugumia kwa maumivi yatokanayo na kipigo.
“Kambi yenu ipo wapi?” Rais Sharabu aliuliza. Akiwa amekamata koromeo kwa kiganja chake na kuzamisha makucha kwa nguvu ngozini.

Luteni Jenerali Kipozi hakujibu.

Rais Sharabu aliendelea, “Nakuuliza kwa mara nyingine. Kambi yenu ipo wapiii?” awamu hii alimuuliza huku akimtingisha kichwa kupitia sehemu ile ya koromeo aliyoikamata.

Luteni Jenerali Kipozi naye aliendelea kuwa kimya. Hakujibu. Muda wote akitiririkwa na jasho lililoambatana na damu. Mwili umemvimba, maumivu yakimtawala sehemu zote.
“Hawa ndiyo unaoshirikiana nao?” Rais Sharabu akamuonyesha Luteni Jenerali Kipozi picha mnato iliyoambatanisha sura za watu kadhaa; Makamu wa Rais, Lilian, Jenerali Namkumba, IGP Lukanga na Ndalama.

Ijapokuwa uono wake ulikuwa wa tabu, kwa sababu ya macho kuvimba vimba kutokana na kipigo, lakini aliweza kuzitambua sura alizoonyeshwa. Akashtuka! Mapigo ya moyo yakamwenda kasi, huku akijiuliza, wamewatambuaje? Ama wanawahisi?
“Hebu chukueni simu yake mukaichunguze,” Rais Sharabu aliwaamuru timu yake. Kauli iliyoambatana na pigo la ngumi mbili mfululizo usoni kwa kutumia ule mkono aliokuwa amekamatia koromeo awali. Luteni Jenerali Kipozi akaanguka kama mzigo wa kuni uliofungwa na kamba pori.

Simu ya Luteni Jenerali Kipozi ilichukuliwa na Killa kwenda kupekuliwa.

Luteni Jenerali Kipozi kule alipodondokea akafungua uwanja wa kuwazua. Imekuaje zile sura zihisiwe katika hila ya kumwangusha Rais Sharabu? Na nini kitajiri ukweli utakapobainika?

Saa moja baadaye ndipo Killa alirejea pale mjengoni. Hata kabla hajatulizana kuketi, Rais Sharabu alimlaki kwa maswali.
“Umefanikisha?”
“Ndiyo mheshimiwa,” Killa alijibu kisha akampatia simu Rais Sharabu.

Rais Sharabu alianza kupekua sehemu moja baada ya nyingine, kulingana na maelezo aliyokuwa anapatiwa na Killa.

Mikakati ya kina Luteni Jenerali Kipozi ilibainika; kuanzia ushiriki wa timu nzima-watu waliopo, namna watakavyofanikisha malengo na wapi makazi yao yapatikanapo. Kule Ngowe.
“Tuma vijana haraka wakawadhibiti hawa watu,” Rais Sharabu aliamuru baada ya kumaliza upekuzi.

Kauli iliyosikika vyema viwamboni mwa Luteni Jenerali Kipozi.

Atawasaidiaje wenzake?

ITAENDELEA...

HABARI NJEMA

KITABU CHA RIWAYA YA NENDA SASA KINAPATIKANA RENICS BOOKSHOP TAWI LA MOSHI KWA GHARAMA YA TSH. 10,000/= MAWASILIANO: 0767826134
 
Back
Top Bottom