Riwaya: Kiguu na njia

nameless girl

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
4,036
Points
2,000

nameless girl

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
4,036 2,000
Gari moshi liendalo Mpanda hulazimika kueleka magharibi kwa kilometa kadhaa kabla ya kuchepuka kuelekea kusini. Kwangu mimi ilikuwa sawa na kuelekea nyumbani, Kigoma. Tuliiacha stesheni ya Tabora, tukatafuna reli hadi Usoke. Toka hapo tuliingia Urambo. Tuliacha Urambo na kufika Kaliua ambako tulianza safari ya kusini.
Kama ilivyokuwa safari ya kutoka Mwanza safari hii pia ilikuwa sawa na kusafiri katikati ya bustani ya Eden. Kila upande tulizungukwa na ama misitu minene iliyoashiria kila aina ya hazina, ama mapori ya kutisha yaliyonona juu ya wingi wa mbolea katika ardhi yake.
Mara kwa mara tulipishana na wanyama ainaaina waliokuwa kando wakitushangaa, pamoja na ndege ainaaina walioruka hapa na pale juu ya miti, wakifaidi asali ya maua na wadudu wadogowadogo. Baadhi ya maeneo kulikuwa na mabwawa makubwa yaliyoshawishi kilimo cha mpunga au mito ambayo ilinikumbusha samaki wa ziwa Nyanza.
Toka Kaliua tuliingia Mfulu, baadaye Ugalla na hatimaye tukawasili Mpanda. Huo ulikuwa mwisho wa reli hii, lakini haikuwa mwisho wa safari yangu.
Pamoja na shahuku yangu kubwa ya kuondoka Tabora, ndoto yangu ya kuja Mpanda ilikuwa na malengo yake. Zilikuwepo fununu za hapa na pale kuwa maeneo mbalimbali ya huku yalikuwa dhahabu. Uchimbaji wa dhahabu hiyo sikuona kama kwa namna yoyote ile ungenishinda. Kuchimba udongo hadi ufikie mchanga maalumu kuchekecha mchanga huo hadi uone chembechembe za dhabahu na kuiokoteza, vipi kungenishinda?
Hilo lilikuwa wazo la kwanza. Wazo la pili, ambalo nilikuwa na hakika nalo zaidi ni uvuvi. Toka Mpanda hadi Ikola au Kerema ambayo ni miji ya kandokando mwa ziwa Tanganyika haikuwa safari ndefu. Ningeweza kufika huko hata kwa miguu. Nilipanga, kama kazi ya kuchimba dhahabu ingeshindikana ningeelekea huko na kujiunga na uvuvi. Ndiyo, nasikia ziwa Tanganyika lina kina kirefu kuliko maziwa yote duniani. Kama kuna ukweli kwa hilo bila shaka samaki wake pia ni wengi zaidi na watamu zaidi. Ningekuwa mmoja kati ya walaji wake. Wala nisingeishia kula tu; samaki hao wangenipatia fedha za mtaji ili nirudipo kwetu nirudi kishujaa.
Hiyo ndiyo ilikuwa ndoto yangu. Kwa bahati, nzuri au mbaya, haikwenda kama nilivyotarajia. Hali hiyo ilitokana na kukutana kwangu ana kwa ana na mtu ambaye sikutarajia kamwe kumwona tena katika maisha yangu, mtu ambaye sikupata hata kulifahamu jina lake. Alikuwa mmoja kati ya wale Wamanyema wawili waliofuatana na Mwarabu katika safari yetu ya miguu toka Buha hadi kwa Wahaya, miaka zaidi ya mitano iliyopita.
Ni yeye aliyeniona kwanza, “We mtoto wewe! Kama nakufahamu vile?”
Nikageuka kumtazama. Mara moja nilimkumbuka, “Mmanyema! Unafanya nini huku?” niliuliza kwa mshangao.
“Wewe je? Umefikaje huku?”
Sikujua nimweleze nini.
“Babu yako hajambo?”
Sikuwa na jibu. Nikainamisha uso kwa aibu.
Nadhani Mmanyema alisoma kitu fulani katika uso wangu, kwani alinitazama kwa muda kabla hajanikaribisha chai kwa mihogo ambayo alikuwa akiila. Nikapokea kikombe cha chai ya maziwa na kipande cha muhogo. Njaa iliyoanza kuninyemelea ikakimbia mara moja.
Wakati tukinywa chai hiyo yapata saa kumi na moja za alfajiri. Gari moshi lilikuwa limechelewa sana njiani kutokana na mafuriko katika maeneo mbalimbali. Ilibidi gari hilo liendeshwe taratibu sana. Tulikuwa tumeketi nje ya stesheni, kwenye benchi la chuma ambalo bila shaka lilijengwa kwa ajili ya wasafiri.
Nilishangaa pale Mmanyema aliponiambia kuwa tulisafiri katika behewa moja toka Tabora hadi hapo. Kuwa aliniona lakini hakuwa na hakika na macho yake hadi aliposikia sauti yangu na kuniona nikimkumbuka.
Alikuwa mzungumzaji sana mzee huyu. Alinieleza jinsi alivyoacha kazi ya kumtumikia yule Mwarabu baada ya kufilisika. “Yaelekea Mwarabu yule hakuwa na ujuzi wowote zaidi ya biashara ya watumwa. Kila alichojaribu kushika kiliteleza. Hata mishahara yetu alishindwa kulipa. Tukaachana naye na kuanza shughuli zetu binafsi,” Alinieleza kwamba yeye sasa alikuwa akifanya biashara ya kununua dagaa toka kwa wavuvi wadogowadogo wa kandokando ya ziwa Tanganyika na kuwauza kwa walanguzi wakubwa ambao waliwapeleka Tabora, Dodoma na Dar es Salaam kwa matumizi ya binadamu na mifugo. Kwamba sasa hivi alikuwa na mtaji wa kutosha ambao utamwezesha kupeleka mwenyewe dagaa hao hadi Dar es Salaam ili apate faida kubwa zaidi. “Toka huku nitanunua nyavu na vifaa vingine vya uvuvi na kuwauzia watu Kigoma na Kongo. Nikijaliwa miaka miwili baadaye nitakuwa mmoja wa matajiri wakubwa wa nchi hii,” alisema kwa kujipamba.
“Sasa unakwenda wapi? Mbona huku hakuna dagaa?” nilimuuliza.
“Nakwenda Sumbawanga.”
“Kufanya nini?”
Alinitazama na kucheka kidogo kabla hajasema, “Unaonekana wewe ni mtoto mdogo sana kuliko umbile lako. Hujui watu huenda Sumbawanga kufanya nini?”
Mie: Sijui
Yeye: Pole sana. Kwa hiyo, hata maana ya jina Sumba - Wanga hujui?
Mie : Sijui
Alitikisa kichwa kwa namna ya kunisikitikia. Kisha alisema, “Sumba-Wanga maana yake ‘Tupa Uchawi.’ Kwa maana ya kuwa mji huo ni wa watu wazito, watu waliokomaa. Hivyo, ukiingia huko na vijiuchawiuchawi vyako utaumbuka. Ni huko ambako watu wazima huenda kugangwa, ili wasichezewechezewe ovyo kishirikina. Huwezi kufanya biashara kama hujafundwa ukafundika.”
Ilikuwa habari mpya kwangu. Niliipokea kwa mshangao na kutoamini. “Lakini Biblia inasema…” nilijaribu kumwambia.
“Achana na Biblia. Mimi ni Mwislam. Tunatumia Msahafu wa Mwenyzi Mungu. Ulioshushwa toka peponi kwa mkono wa mtume Mohamed S.A.W.”
“Lakini hata Uislam unakataza ushirikina.”
“Kujikinga sio ushirikina. Hayo ni mambo ya wakoloni tu, walipoamua kututawala miili na mioyo yetu. Walitarajia kuwa mila na tamaduni zetu kupotea huku wao wakihifadhi za kwao. Kila binadamu ana nyota na anahitaji kuisafisha mara kwa mara. Kila binadamu ana wahenga ambao anahitaji kuwaenzi kwa sadaka na tambiko. Asiyefanya hivyo kamwe hawezi kufanikiwa.”
Lilikuwa somo jipya kwangu, somo ambalo sikuwa na ujuzi nalo. Nikaamua kunyamaza. Mmanyema alichukulia ukimya wangu kama dalili ya kumwelewa.
“Haya na wewe nieleze ukweli wa kile kilichokufanya ufike huku. Kama nakumbuka vizuri babu yako alikupeleka Uhayani ukasome. Nadhani ulipata shule kwani nilipoonana naye mwaka mmoja baadaye alinidokeza kuwa ulishaingia shuleni,” alisema.
Nusura niruke kwa shauku, “Ulionana na babu?”
“Ndiyo!”
“Wapi?”
“Nyumbani kwenu. Kasulu. Tulilala pale siku mbili na alituchinjia beberu mkubwa sana. Babu yako ni mkarimu sana.”
Bila kutegemea nilijikuta nikitokwa na machozi. Babu yuko hai! Babu alirudi salama! Sikupata kupokea habari njema kama hiyo kwa miaka nenda rudi.
Sikuiona haja yoyote ya kumficha chochote Mmanyema huyu. Nilimwona kama baba yangu. Kama malaika, kwa kuweza kunipa walao fununu tu ya habari za nyumbani. Nikamweleza kila kilichonisibu, toka mwanzo wa mikasa yangu hadi nilipofikia.
Alinisikiliza kwa makini sana, mara kwa mara akitikisa kichwa kwa masikitiko. Mwisho wa maelezo yangu alinishika mkono na kuninong’oneza, “Pole sana mtani. Usijali. Hujafika mwisho wa safari yako kimaisha. Nitakusaidia.”
Nilimwamini. Sikujua kwa nini nilimwamini haraka kiasi hicho.
* * *​
Safari ya Ikola au Karema ilikufa. Ndoto ya kuchimba dhahabu nayo ilikufa. Safari ya Sumbawanga ikazaliwa.
Tulikaa kwa siku mbili kabla ya kupata gari lililotufikisha Sitalike. Hapo tulipumzika tena kwa siku tatu tukifaidi nyama pori ambazo zilikuwa tele toka katika mbuga za Katavi. Tukaondoka hadi Kisi, Chala, Nkundi na hatimaye Sumbawanga.
Wakati huo Sumbawanga kilikuwa kimji kidogo tu, chenye wakazi wachache lakini kikiwa na mambo makubwa. Mandhari ya mji, ambayo yalipambwa na mlima Malonje wenye urefu wa mita 2418 toka usawa wa bahari, mito na misitu tele yalifanya nitamani kuishi hapo kwa muda mrefu zaidi.
Lakini Mmanyema ambaye baadaye alinitajia jina lake kuwa ni Baraka Khalfan alikuwa na ratiba tofauti na yangu. Alikuwa na majina ya vijiji mbalimbali na waganga mbalimbali ambao alipanga kuwaona. “Huku ni Ufipa, mdogo wangu. Lyampa Iya Mfipa, umepata kulisikia?”
Sikupata.
“Lyampa Iya Mfipa kwa tafsiri ya kawaida ni mlima mdogo tu, ambao unatambaa hadi kando ya ziwa Tanganyika na kupita chini hadi Kongo, katika eneo la Moba, nchi ya Watabwa. Lakini kwa wajuzi wa mambo Lyampa Iya Mfipa linabeba uzito wa pekee. Ni jiwe la tambiko ambalo ukikaangwa juu yake hakuna mtu yeyote atakayekuchoma. Na hayo hafanyiki mjini, isipokuwa vijijini kwa wazee, waliofundwa na babu zao,” alinieleza.
“Watu wengi wenye nafasi zao wamepitia huku. Watu toka sehemu mbalimbali za dunia huja huku kufanyiwa mambo. Watabwa wa Kongo nao huja huku, ingawa ni kweli pia kuwa wazee wa huku katika kuimarisha uwezo wao huvuka ziwa kwenda Kongo,” aliongeza.
Hivyo, zilianza safari za hapa na pale. Mara Chapota, mara Kasanga, mara Wampembe na kwingineko. Safari hizo zilitufikisha Pwani ya ziwa Tanganyika na kuniwezesha kuona milima ya Kongo mbele yetu na ile ya Zambia kushoto kwetu. Ziwa hilo lilinikumbusha hamu ya kurudi nyumbani, kwani kwa kuambaa nalo tu, nikielekea kulia ningeweza kufika Kigoma. Kwa bahati mbaya, sikuwa tayari kwa safari hiyo.
Mmanyema alikuwa na pilikapilika nyingi. Mara kwa mara aliniacha peke yangu na kwenda hapa na pale na aliporudi alikuwa kachanjwa chale ama za kwenye paji la uso ama katika viwiko vya mikono na miguu. Wakati mwingine alinituma kumtafutia vifaa mbalimbali kama mayai viza, mizoga ya paka au njiwa weusi.
Siku moja aliondoka alfajiri na hakurudi. Nililala peke yangu katika chumba tulichofikia cha mwenyeji wetu mmoja. Kwa kuwa nilikuwa peke yangu nililala mapema sana, mara baada ya chakula cha usiku. Nilipofumbua macho tena ilikuwa alfajiri. Baridi kali iliyotokana na upepo ziwani nadhani ndiyo iliyoniamsha. Nilipotazama huko na huko sikuweza kuyaamini macho yangu. Nililala ndani, juu ya kitanda, lakini niliamka nikiwa nje, tena juu ya mbuyu mkubwa ulikuwa mbele ya nyumba hiyo. Isitoshe nilikuwa mtupu, bila nguo yoyote mwilini!
Nilishuka harakaharaka na kuingia ndani. Nguzo zangu zilikuwa zimetupwa ovyoovyo chumbani humo. Nikaziokota na kuvaa harakaharaka. Ni wakati nikivaa nilipobaini kuwa nilikuwa nimechanjwa chale mbili katika paji langu la uso na kupakwa vitu vyeusi kama masizi ya mkaa.
Nilikosa raha. Niliduwaa katikati ya chumba hicho huku nikitetemeka kwa hasira.
Mara mlango uligongwa na kufunguka kabla sijaitikia. Mwenyeji wetu, mzee Imilio Kahigi aliingia ndani. Alikuwa akicheka huku anatikisa kichwa. “Mtoto, mbona unasafiri ukiwa mwepesi hivyo?” aliniuliza.
Sikumwelewa, hivyo sikumjibu.
“Uko mtupu mno. Mwepesi kupita kiasi. Kwani hukuaga kwenu?” aliuliza tena.
“Niliaga!” nilimjibu.
Alicheka kabla ya kusema, “Hukuaga. Na kama uliaga wazazi wako ni watoto vilevile. Jana watoto wenzako wameamua kukupima baada ya kuona huelewekiheleweki. Wakakuta ni mwepesi mno. Ndiyo maana wakakuacha pale juu ya mti baada ya kukuchezea usiku kucha.”
Sikujua mzee huyo alitarajia jibu gani kwangu. Hivyo, niliendelea kukaa kimya wima, nikiwa nimemkodolea macho.
“Utafanyaje?” aliniuliza ghafla.
Nilijua nitakachofanya. “Nitaondoka, leo hii hii,” nilimjibu.
Alicheka tena kabla hajasema, “Unadhani utafika unakokwenda?”
“Nitafika. Kwa nini?”
“Wenzako wamekutia alama. Popote utakapokwenda wajuzi wa mambo watakubaini mara moja na kukugombea kama mpira wa kona, maana una alama, alama ya shari.”
Nilizidi kuduwaa. Nadhani hata mdomo wangu niliusahau ukiwa wazi wakati nikiwa nimemtumbulia macho.
“Huyu Mmanyema unamfahamu kwa kiwango gani?” Aliniuliza ghafla.
“Simfahamu vizuri. Tulikutana naye safarini miaka mingi iliyopita. Tumekutana naye tena majuzi na kufuatana naye. Basi.”
Mzee Kahigi alitikisa kichwa kwa namna ya kunihurumia sana. Kisha aliongeza swali jingine, “Alikuambia anatafuta nini huku?”
“Waganga.”
“Wa?”
“Kujiganga. Anataka kinga.”
Mzee akacheka tena. “Humjui vizuri,” alisema. “Humjui hata kidogo. Huyu bwana anatafuta kizimba, dawa ya mali. Ametakiwa kutoa kichwa cha mtu. Alitakiwa atoe mtoto wake wa kwanza, ageuzwe ndondocha, awekwe chini ya maji kumswagia dagaa. Hana mtoto wake wa kuzaa. Anachofanya sasa ni kukutoa wewe. Utageuzwa akili, utawekwa chini ya maji maisha yako yote, hadi kifo cha kweli kitakapokutokea.”
Sikuyaamini masikio yangu.
“Mmanyema!”
“Naam!”
“Mimi!”
“Naam… tena mipango yake inakwenda vizuri sana. Kesho au keshokutwa utakufa, tutakuzika. Lakini wajuzi wa mambo tutaona tunavyozika mgomba huku wewe ukiongozwa kikondoo kupelekwa ziwani.”
Baada ya taarifa yake hiyo ‘njema’ alinikazia macho kabla hajaniuliza tena, “Utafanya nini?”
Bado sikujua alitaka nimjibu nini, “Nitaondoka,” nilimjibu.
“Nimekwishakwambia umetiwa alama. Hutafika mbali.”
“Nitaondoka nikafie mbali. Siyo hapa.”
Baada ya kuwaza sana alisema, “Nitakusadia. Utaondoka hapa salama ufike salama kokote uendako. Siwezi kukubali mtu wa kuja afanye ushenzi katika milki yangu. Kaa kama kawaida, kula kama kawaida, usiku ufunge vitu vyako vyote tayari kwa safari.”
Sikujua ilinipasa kumshukuru au la. Kwa ujumla, sikujua kama nilipaswa kumwamini au kutomwamini. Nilichojua ni kwamba maisha yangu yalikuwa katika mashaka makubwa. Unapopigania roho yako, bila kumjua nani adui nani rafiki, sio suala la mzaha.
Nilifanya kama nilivyoelekezwa. Sikumwambia mtu yeyote juu ya masaibu yaliyonipata usiku huo. Nilioga, nilikula na baadaye kutembeatembea kijijni hapo kana kwamba hakuna lolote la ajabu lililonipata.
Mmanyema alirudi mida ya saa nne hivi. Alionekana mtu mwenye furaha na matumaini makubwa. Huku akitabasamu alinivuta chemba na kuninong’oneza, “Mdogo wangu mambo yamekwisha. Kama nilivyokuambia baada ya miaka miwili tutakuwa watu katika watu. Pesa halitakuwa tatizo tena. Wewe, kwa kuwa umesoma kuliko mimi utakuwa mhasibu. Utatunza hesabu ya fedha na mali zetu zote.” Aliongeza kwa kunidokeza kuwa jioni hiyo angesafiri tena. Atakaporudi tutakuwa tayari kurudi Kigoma.
“Unakwenda wapi safari hii?” Nilimuuliza.
“Nakwenda Kipili hadi Mtakuja. Nitajitahidi kurudi keshokutwa. Nikirudi tu yamekwisha,” alinijibu. Kisha alinitazama usoni na kuniuliza “Hapo umefanya nini?”
“Nilijikuna,” nikamjibu.
Nilihisi hakuniamini. Alizikagua chale zile kwa muda mrefu kidogo.
“Sidhani,” alisema. “Nikirudi tutaangalia suala lako vilevile. Isije kuwa washenzi wanakuchezea, maana umekaa mweupemweupe kama kinda la ndege.”
Nilitamani sana kumwamini. Sikubahatika kuipata fursa hiyo.
Mara tu alipoondoka nilifunga vifaa vyangu katika begi langu. Baada ya mlo wa usiku nilijilaza mapema nikisubiri usingizi unichukue ili kesho ifike nione mzee Kahigi atanisaidia vipi ili niweze kuondoka nchi hiyo ya Wafipa salama.
Sikujua usingizi ulitokea wapi. Nilihisi ghafla kama naota, mlango ukifunguka na mzee Imilio Kahigi akiingia chumbani humo. Alikuwa mtupu, isipokuwa kwa kipande kidogo cha kaniki alichofunga mbele ya kiuno chake. “Inuka,” aliniamuru. Niliinuka. “Chukua begi lako unifuate,” nilifanya kila alichoniamuru na kumfuata hadi nje ya nyumba.
Hapo kulikuwa na ungo mkubwa wenye vikorokoro mbalimbali ambavyo sikuweza kuvifahamu. “Ingia ukae hapo,” aliniamuru tena. Nikamtii.
Mara alianza kuimba kwa lugha ya Kifipa, maneno ambayo sikuweza kuyaelewa. Akaninyunyizia kitu fulani chenye harufu mbaya kwa usinga wake huku akiendelea kuimba. Ghafla nikaona ungo ukianza kupaa. Ulipaa, ukapaa, ukapaa hadi mawinguni. Naota? Nilijiuliza. Kama ilikuwa ndoto, basi ilikuwa ndoto ya aina yake ambayo ningependa nirudie kuiota mara kwa mara.
 
Lee van

Member
Joined
Sep 28, 2019
Messages
18
Points
45

Lee van

Member
Joined Sep 28, 2019
18 45
ʍʐɨɢօ ʍtaռɨ, sɦʊsɦa ʍʐɨɢօ ʍաɨռɢɨռɛ ҡaʍa upo

Nimerudi....
Lakini kabla ya mzigo, naomba niwatangazie wakazi wa Zanzibar, kwa anayehitaji vitabu hivi, nitakuwepo Zanzibar siku ya tarehe 16.10.2019. Kama ulikuwa unahitaji hivi vitabu lakini unaogopa kutuma pesa, sasa unaweza kuweka oda yako na nikakuletea siku hiyo. Kwa mawasiliano nipigie namba 0712504985.
Vitabu vipo aina kumi na tatu.
1. Kiguu na njia
2. Dar es salaam usiku
3. Pesa zako zinanuka
4. Zawadi ya ushindi
5. Mikononi mwa nunda
6. Mtambo wa mauti
7. Mikataba ya kishetani
8. Malaika wa shetani
9. Salamu toka kuzimu
10.Tutarudi na roho zetu
11. Roho ya paka
12. Dimbwi la damu
13. Najiskia kuua tena
Karibuni sana.
 
nameless girl

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
4,036
Points
2,000

nameless girl

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
4,036 2,000
SURA YA NANE
Kwa Ungo Hadi Mbeya
Nilizinduka toka usingizini. Nadhani kilichonizindua ni baridi kali iliyoambatana na upepo wa kipupwe ambao ulinipiga mwili na kunifanya nijikute nikitetemeka, meno yangu yakigongana. Nilikuwa katika kituo cha mabasi, peke yangu. Jogoo waliokuwa wakiwika huko na huko waliniashiria kuwa ilikuwa alfajiri.
“Niko wapi?” nilijiluliza nikiinuka na kutazama huko na huko. Begi langu lilikuwa miguuni mwangu, kama nilivyolifunga jana. Kwa mbali nilianza kuona mtu mmojammoja wakipita hapa na pale, baadhi yao wakija kituoni kuwahi usafiri. Baadhi ya magari yalianza kuwashwa.
Niliinama na kuliinua begi langu, ambalo nililiinua kwa taabu sana. Vidole vyangu vilikuwa vimekufa ganzi. Hata pale nilipojaribu kutembea miguu yangu ilikuwa kama haipo kwa ajili ya baridi hiyo kali. Nikajikongoja hadi nilipomfikia taniboi mmoja ambaye alikuwa akimimina maji katika injini ya gari lake, tayari kwa safari.
“Samahani, hapa ni wapi?” Nilimuuliza.
“Huwa tunasalimiana kwanza,” alisema akinitazama kwa mshangao.
Sikumjibu. Si kwa ajili ya ujeuri bali kwa kuwa sikujua alitaka salamu za aina na lugha gani, kwani lafudhi yake ilikuwa tofauti kabisa na ile ya watu wa Sumbawanga. Alipoona kimya aliniuliza kwa mshangao, “Kwani wewe umetoka wapi hata uulize hapa ni wapi?”
“Nimetokea Sumbawanga.”
“Umekuja na gari gani?”
Sikuwa na jibu, jambo ambalo lilimshangaza zaidi.
“Ulilewa?”
“Hapana.”
“Ulikuwa unaumwa?”
“Hapana.”
“Sasa umewezaje kutoka Sumbawanga hadi hapa Mbeya bila kujua unapokwenda?”
Sikuendelea kumsikiliza. Mbeya! Niliwaza kwa mshangao. Niliyakumbuka maongezi yangu na Mzee Imilio Kahigi na ahadi yake ya kunisaidia. Nikakumbuka tukio la usiku, aliponijia katika mavazi ya ajabuajabu na kuniamuru kuketi katika ungo, nikiwa nimepakata begi langu. Nilikumbuka kwa mbali nyimbo zake alizoimba akichezesha usinga wake hata nikaanza kupaa! Mbeya! Nimekuja Mbeya kwa ungo! Sikuamini.
Lakini sikuwa na sababu ya kutoamini. Baridi kali ambayo ilianza kunila mifupa ilikuwa ushahidi tosha kuwa niko katika eneo jingine, lililo juu zaidi ya usawa wa bahari zaidi ya Sumbawanga. Hata mavazi ya watu wengi waliokuwa wakiongezeka mitaani yaliashiria hali ya hewa nyingine kabisa. Makoti au majaketi makubwa, kofia au vitambaa kichwani na viatu vizito miguuni. Majina mengi yaliyokuwa yakitajwatajwa pia yalikuwa mapya masikioni mwangu; Mwakipesile, Mwangonda, Mwamasika, Mwanjelwa na kadhalika.
Nilipapasa mifuko yangu. Pesa nilizopewa na Chifu Masanja bado zilikuwemo. Nikajikongoja hadi nilipopata mgahawa mdogo na kujinunulia chai ya moto sana. Nilikunywa vikombe viwili chapchap na cha tatu taratibu kabla ya kubaini kuwa chai hiyo ilinichubua midomo na ulimi kwa kiwango kikubwa sana.
Toka hotelini hapo nilitafuta nyumba ya wageni ya bei nafuu ambamo nilionyeshwa mapipa ya maji ya moto na kuchota ndoo moja niliyoitumia kuoga. Baada ya hapo nilipanda kitandani na kujilaza, nikiwa nimejifunika mablanketi mazito mawili. Usingizi mzito ulinichukua na kwa muda ukawa umenisahaulisha masaibu yote yaliyonitukia katika muda mfupi wa maisha yangu. Hata hivyo ulikuwa usingizi wa mang’amung’amu kwani niliandamwa na ndoto za kutisha, mara nikiwa juu ya mbuyu, mara nikipaa angani, mara nikiwa nimezingirwa na wachawi wanaopanga kunila nyama na kadhalika.
Nililala mchana kutwa na usiku kucha. Nilipoamka kesho yake jambo la kwanza nililofanya ilikuwa kwenda madukani ambako nilinunua mavazi yanayoendana na hali ya hewa ya Mbeya; koti, sweta zito, kofia na soksi nzito.
Katika pitapita yangu mjini hapo niliingia duka la vitabu ambamo nilinunua ramani ya mji na vitongoji vya Mbeya. Nikaketi mahala na kuisoma. Jambo la kwanza lililovuta macho yangu ni urefu wa safari ambayo nilisafiri kwa miujiza toka Sumbawanga hadi Mbeya. Kama ningelazimika kusafiri kwa gari ningetumia zaidi ya siku mbili njiani kwa kupita katika miji na vijiji mbalimbali kama Mpui, Ndalambo, Tunduma, Ihanda, Iwanda na hatimaye Mbalizi.
Jambo jingine lililovuta macho yangu ni kubaini kuwa mkoa wa Mbeya ulikuwa mpakani mwa Tanganyika na Zambia kwa upande mmoja, nchi ya Malawi kwa upande wa pili. Mji mkubwa zaidi wa mpakani kwa upande wa Zambia ukiwa Tunduma na kwa upande wa Malawi mji mkubwa zaidi ukiwa Kyela na Itundi. Mbeya ilikuwa na sifa nyingine. Ilibahatika kuwa na ziwa kama yale ya Nyanza na Tanganyika, ingawa kwa asilimia ndogo. Bahati hiyo iliwezesha si kuvua samaki tu, bali pamoja na kuwawezesha kuwa na bandari, Itungi, ambayo ilihudumia miji ya Karonga kwa upande wa Zambia na mikao kama Iringa kupitia wilaya ya Ludewa.
Ramani hiyo ilinionyesha kuwa Mbeya haukuwa mji mdogo kama ulivyokuwa ukionekana. Ulikuwa na mengi ya kusisimua kiutamaduni, kiuchumi na kimazingira. Pamoja na ukweli kuwa kabila lililojulikana zaidi la mkoa huo lilikuwa la Wanyakyusa bado kuna makabila mengine tele kama Wandali, Wasafa na Wasangu ambao ni wenyeji asilia. Aidha, kuwepo kwa mkoa huo mpakani kulichangia kufanya uhamiaji wa kutokea nchi za Malawi na Zambia kuwa sehemu ya wakazi.
Sikuhitaji ramani hiyo kusoma ukweli kuwa wakazi wengi walikuwa wakulima. Mazao kama mahindi, mpunga, migomba, viazi na mimea mengine ilikubaliana sana na ardhi na hali ya hewa ya huko, jambo lililofanya katika pitapita zangu nipishane na wakulima waliobeba mazao ama kwenye baiskeli ama katika mikokoteni wakielekea sokoni.
Lakini Mbeya ilikuwa na kitu kingine cha ziada. Dahabu. Purukushani za kutafuta dhahabu, kwa mujibu wa maelezo toka kwa baadhi ya watu niliobahatika kuzungumza nao, zilianza tangu mwaka 1905 kufuatia fununu za kuwepo kwa madini hayo. Hata hivyo, miaka kumi na mitano baadaye ndipo ilipodhihirika rasmi kuwepo kwa madini hayo katika mji wa Chunya. Hali hiyo iliyopelekea mji huo mdogo upanuke ghafla na kupokea watu wa aina mbalimbali, wa makabila na mataifa mbalimbali, kila mmoja akijaribu kuutumia mwujiza wa dhahabu kujipatia chochote. Walikuwemo wachimbaji, madalali, wanunuzi, wauzaji wa vifaa vya uchimbaji na vyakula na wengineo.
“Nafikiria kwenda huko kesho,” nilimwambia mmoja kati ya watu niliobahatika kuzungumza nao juu ya suala hilo. Alikuwa mtu wa makamo, ambaye muda mwingi nilimwona kakaa mbele ya hoteli niliyofikia. Sikupata kujua kazi yake ilikuwa ipi.
Mtu huyo alinitazama kwa mshangao, “Nani, wewe?” aliniuliza.
“Ndiyo,” nilimjibu.
“Unakwenda kufanya nini?”
“Kuchimba.”
Akacheka na kunitazama kwa dharau ya dhahiri. “Inahitaji mtu kichaa sana kwenda kuchimba madini,” alisema.
Ikawa zamu yangu kumshangaa. “Kwa vipi?” nilihoji.
“Kwanza hutarudi salama. Na ukirudi utakuwa masikini kuliko hapo ulipo.” Alinionya.
Sikumwelewa. “Mbona kuna watu huko na wanachimba?”
“Mdogo wangu, hao walioko huko huwa hawarudi. Kazi ile ni kama laana hivi. Unaweza kuchimba maisha yako yote bila kupata chochote cha maana. Unaweza kubahatika kupata mali ya maelfu lakini siku mbili tatu ukawa huna hata shilingi moja. Fedha za madini ni kama za mashetani. Hupotea kimiujiza kama zinavyopatikana.”
“Na hawa wanaotajirika?” nilihoji.
“Hao sio wachimbaji. Ni wanunuzi au wamiliki wa maeneo utakayochimbia. Wachimbaji wa kawaida wako huko, wanazeekea huko na kufa huko!” alisisitiza.
Laiti angejua taarifa yake ilinikata maini. Toka nilipofika mjini hapo kimiujiza nilikwishafanya uamuzi. Uamuzi wangu ulikuwa kwenda Chunya, kujiunga na wachimbaji madini ili nikibahatika nirudi kwetu sina elimu lakini nina mali. Taarifa za kwenda kuzeekea huko na kufia huko ziliniacha hoi, taabani.
Mshauri wangu aliweza kusoma msuguano wa mawazo yangu, nilidhani, kana kwamba anapigilia msumari wa mwisho kichwani mwangu, aliongeza, “Kama umetoka kwenu kwa nia ya kwenda machimboni isahau kabisa ndoto hiyo. Utakufa siku si zako. Utaugua kifua kikuu kwa vumbi la machimboni, utazikwa hai kwa kubomokewa na kuta za shimo, utauawa na wachimbaji wenzako ukibahatika kupata mali nyingi. Kuna hatari elfu moja na moja.”
Ushauri wake wa bure ulianza kunichosha. “Kuna kazi gani duniani ambayo haina hatari kwa namna moja au nyingine?”
“Nyingi tu,” alijibu harakaharaka.
“Kama?”
“Udaktari kwa mfano,” alijibu harakaharaka.
Nikacheka. “Daktari lazima asome kwa miaka nenda rudi. Huwezi kuamua tu kwamba unataka kuwa Daktari.”
“Tunazungumzia kazi, sio kisomo.”
Nikabaini kuwa nazungumza na mtu mweye asili ya ubishi. Nikaamua kumuuliza yeye binafsi anafanya kazi gani.
“Wengine kazi zetu huwa hazitajwi hovyo.” Alisema.
Nikaanza kuamini hisia zangu kuwa hana kazi. Hiyo ilikuwa siku yangu ya tatu toka nilipofika Mbeya na kila siku namwona ameketi anazungumza na watu mbalimbali. Nikaamua kupuuza hata mawaidha yake juu ya hatari za uchimbaji madini. Watu hujiunga na jeshi, wakijua fika kuwa kazi yao ni kwenda vitani ambako kifo ni jambo la kutarajiwa. Watu hujifunza urubani, wakiwa wanajua vizuri sana kwamba ndege ikidondoka kupona ni nadra sana.
Nadhani sihitaji ushauri wako zaidi, nilitamani kuwambia hivyo. Hata hivyo, sikuthubutu. Nilimwona kama mtu ambaye asingekuwa mwepesi wa kusahau na kwa kila hali sikuhitaji maadui bila sababu za msingi.
 
Jackal

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Messages
5,178
Points
2,000

Jackal

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2012
5,178 2,000
Hii kiboko.Nimepata kitu hapa:
"Uamuzi wangu ulikuwa kwenda Chunya, kujiunga na wachimbaji madini ili nikibahatika nirudi kwetu sina elimu lakini nina mali. Taarifa za kwenda kuzeekea huko na kufia huko ziliniacha hoi, taabani."
 
Forum statistics

Threads 1,343,317
Members 515,007
Posts 32,780,373
Top