Riwaya: Kiguu na njia

mangonifera indica

mangonifera indica

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2017
Messages
414
Points
1,000
mangonifera indica

mangonifera indica

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2017
414 1,000
Unitag ikiendelea pls
 
nameless girl

nameless girl

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
4,027
Points
2,000
nameless girl

nameless girl

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
4,027 2,000
KWA ANAYEKIHITAJI KITABU HIKI CHA KIGUU NA NJIA NA VINGINE VYA BEN MTOBWA KAMA DAR ES SALAAM USIKU, SALAMU TOKA KUZIMU, TUTARUDI NA ROHO ZETU NA VINGINE VINGI, NITAFUTE KWA KUPITIA 0712504985 AU 0763044459. KARIBUNI.
“Nani anasema uongo, nani anasema ukweli kati yenu?” aliniuliza. “Juzi tu,” aliongeza. “Alikuja huyu kijana, akatuambia kwamba anaitwa Cheyo na ni mtoto wa chifu Masanja. Kwa maelezo yake baba yake hataki aje shule, anataka akae nyumbani kusubiri kurithi Uchifu wake atakapokufa. Kwamba amekuja hapa shuleni kwa kutoroka baada ya jitihada za kumsihi baba yake kumruhusu kushindikana. Na kwa jina na nafasi yake ilikuwa wazi bado tumempokea na kumruhusu kuendelea na masomo. Leo umekuja wewe. Unadai wewe ni Cheyo mtoto wa Chifu Masanja na una barua yake ya kuomba upokelewe hapa. Nataka kujua nani mkweli nani mwongo kati yenu,” aliniuliza akitutazama kwa zamu. Cheyo naye alishangaa. Akageuka kunitazama. Nilijitahidi kuinua uso wangu nimtazame pia, ilikuwa kazi ngumu kuliko zote nilizopata kufanya. Hicho kidogo nilichobahatika kuona katika uso wake kilionyesha wazi kuwa si kwamba hatufahamiani tu, bali pia tulikuwa hatufanani kwa namna yoyote ile. Pale ambapo mimi nilikuwa mng’avu yeye alikuwa mweusi tii, pale nilipokuwa mrefu yeye alikuwa mfupi na mwenye kiribatumbo.

Endeleaaaaa....
“Mnafahamina?” mkuu wa shule aliuliza baada ya kutupa dakika za kutumbuliana macho.
Wote tulitikisa vichwa kukataa.
Mkuu wa shule akacheka, “Iweje watoto wa mtu mmoja, tena wanaotumia jina moja wawe hawafahamiani?”
Hatukumjibu.
Haikumchukua mkuu wa shule muda mrefu kubaini ukweli wa mambo hayo. Kutokana na udadisi wa Chifu Masanja juu ya kumpeleka mwanae shule, bila shaka kwa muda mrefu sasa, ndipo akabuni hila ya kuteua mtu mwingine ili aache kusumbuliwa, jambo ambalo limetibuka baada ya mwanawe kutoroka nyumbani na kuja shuleni bila ridhaa wala khiari yake.
Mkuu huyo alinikazia macho kama anayesubiri uthibitisho wa kile kinachopita katika fikra zake bila kutamka. Nilitamani asome jibu la ‘ndiyo’ katika nafsi yangu ili yaishe, niondokane na aibu hiyo. Nadhani alisoma hilo katika macho yangu, kwani nilimsikia akisema taratibu, “Sipendi kuchezewa. Sipendi kudanganywa. Natoa dakika kumi tu, yule ambaye anafahamu kati yenu kuwa si mtoto halali wa Chifu Masanja aondoke mbele yangu na ndani ya eneo la shule yangu. Vinginevyo, nitamchukulia hatua kali za kisheria.”
Sikungojea dakika hizo kumi. Moja tu ilinitosha. Niliinuka, nikachukua begi langu na kutoka taratibu. Nyuma yangu nilisikia kicheko, kicheko ambacho kiliashiria mwisho wa ndoto yangu ya kupata elimu zaidi ya ile ndogo niliyokuwa nayo.
* * *​
Niliduwaa kwa muda nje ya eneo la shule. Nilihisi akili yangu ikiwa imedumaa kiasi kwa kuwa mvivu wa kufikiri, hali ambayo ilitokana na uchovu wa ubongo wangu kwa ajili ya tukio hilo zito. Nikatafuta kivuli na kukaa.
Kelele za wanafunzi ambao walikuwa wakitoka, ndizo zilizonizindua hapo chini ya mwembe nilipoketi. Nikainuka nikachukua begi langu na kuitumia miguu yangu kuniondoa hapo. Sikujua naelekea wapi. Lakini sikushangaa pale miguu yangu iliponifikisha stesheni ya treni, mbele ya dirisha la mkata tiketi.
“Nipe tiketi,” nilimwamuru.
“Ngapi?”
“Moja.”
“Ya kwenda wapi?”
Niende wapi? Nilijiuliza. Sikuhitaji kujiuliza sana, “Tiketi yoyote ile. Kigoma, Dar es Salaam au Mpanda,” nilimjibu.
Mkata tiketi huyo alinitazama kwa macho ya mshangao wa muda, akinichungulia toka katika kijidirisha chake.
“Unaumwa?” baadaye alinihoji.
Sikutarajia swali hilo, “Kuumwa! Kuumwa nini?”
“Chochote kile. Kama akili hivi?”
Ikawa zamu yangu kumshangaa, “Kwa nini uniambie hivyo?” nikafoka.
“Mtu yeyote asiyejua anakokwenda ama ni mngonjwa wa akili, ama ameiba anataka kukimbia. Wewe uko katika kundi gani katika hilo?”
Lilikuwa swali la kifedhuli kuliko yote. Lakini nadhani alikuwa akinitendea haki. Mwenyewe pia nilianza kujishuku. Ninakwenda wapi? Ninakimbia nini? Nimechanganyikiwa kwa kupoteza nafasi yangu nyingine ya kupata elimu? Lakini mara ngapi nimesikia kuwa kukosa elimu ya darasa siyo mwisho wa elimu duniani? Wangapi duniani wamefanya maajabu na kuingia katika vitabu vya kihistoria kwa kiwango cha elimu kama yangu au ndogo zaidi.
Wazo hilo lilinifanya niangue kicheko. Nilicheka kwa muda wa dakika mbili nzima mpaka nikapaliwa. Nikaanza kukohoa.
Kicheko changu kilifanya mkata tiketi huyo aamini hisia zake, kuwa naumwa. Na siumwi kitu kingine zaidi ya akili. Nilimwona akichukua simu na kuzungusha namba kadhaa. Alizungumza kwa sauti ya kunong’ona huku akiwa amenikazia macho ya tahadhari. Baada ya hapo alifunga dirisha lake.
Huku nikicheka niliinua begi langu na kuanza kuondoka eneo hilo. Lakini sikuweza kupiga zaidi ya hatua kumi kabla sijajikuta nikivamiwa na watu wawili waliovaa sare za polisi, shati na kaptula za kaki, kofia zilizovaliwa upande, soksi na viatu vyeusi. Mkononi kila mmoja alikuwa na rungu.
“Polisi! Tulia kama unanywolewa!” mmoja aliniamuru.
Nikiwa nimeshikwa na mkanda wa suruali kwa nyuma, hali iliyofanya nining’inie juu juu na kutembelea ncha za vidole vyangu sikuwa na nguvu zozote za kujitetea. Niliburuzwa hadi katika chumba chao kidogo ambako nilisukumwa na kufungiwa kwa nje bila kuulizwa swali lolote.
“Nimefanya nini jamani?” niliwapigia kelele.
Hakuna aliyenijibu.
 
nameless girl

nameless girl

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
4,027
Points
2,000
nameless girl

nameless girl

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
4,027 2,000
KWA ANAYEKIHITAJI KITABU HIKI CHA KIGUU NA NJIA NA VINGINE VYA BEN MTOBWA KAMA DAR ES SALAAM USIKU, SALAMU TOKA KUZIMU, TUTARUDI NA ROHO ZETU NA VINGINE VINGI, NITAFUTE KWA KUPITIA 0712504985 AU 0763044459. KARIBUNI.
SURA YA SABA
Lyampa Iya Mfipa
Nilipohoojiwa na polisi kwa dakika kumi tu kabla hawajathibitisha kuwa nilikuwa na akili zangu timamu. Lakini ilikuwa baada ya kufungiwa chumbani humo kwa siku nzima.
Alikuja mmoja kati ya wale walionikamata, akiwa amefuatana na mtu mwingine mfupi, mnene, ambaye alinukia dawa za hospitali. Sikuhitaji kuambiwa kuwa mtu huyo alikuwa daktari, pengine wa maradhi ya akili, toka hospitali ya Kitete. Walipoingia ndani yule daktari aliketi mbele yangu na kunikazia macho. Mie pia nikamkazia macho. Hata hivyo, nusu dakika baadaye niliyakwepa macho yake kwa kuinamisha uso wangu.
Akiwa bado amenikazia macho daktari yule alitabasamu, mimi sikutabasamu. Aliangua kicheko. Mimi sikufanya hivyo. Kisha alitikisa kichwa chake kwa kujiyumbisha huku na kule kama aliyekusudia nifuate mfano wake. Sikufanya hivyo. Nikamwona kama mtu aliyepatwa na mshangao.
“jina lako?”
Nikamjibu kwa kutaja lile nililopewa na chifu Masanja, “Cheyo.”
“Kabila lako?”
“Msukuma. Ingawa sikijui vizuri.”
“Kwa nini?”
“Nilizaliwa na kukulia Buha. Nafahamu Kiha kuliko kisukuma.”
“Mwakeye!” Akanijibu.
“Saa hizi sio mwakeye, ni mwidiwe,” nikamsahihisha.
Akatabasamu. Nadhani akiba yake ya Kiha ilikuwa inaishia pale, kwani alirudi kwenye Kiswahili. “Enhe, una tatizo gani?” alihoji.

“Nadhani hawa walionifungia hapa ndio wenye matatizo. Wamenikamata bila sababu na kunifungia humu bila maelezo,” nilisema kwa sauti yenye hasira.
Daktari huyo alinitazama kwa makini, toka kichwani hadi miguuni. Mavazi yangu yalikuwa safi, viatu vyangu viking’ara kwa kiwi. Hata mwili wangu pia ulikuwa safi, ukimeremeta kwa afya na mafuta niliyopaka kabla ya kwenda mbele ya mkuu wa shule ile iliyonikataa. Begi langu pia lilikuwa safi, jipya, lililofura mali ambazo mgonjwa wa akili hawezi kuwa nazo. Daktari huyo aliacha kunitazama mie akawa akimtazama yule askari. Nilihisi kuwa alikuwa katika wakati mgumu wa kuamua nani mgonjwa wa akili kati yangu na hao walionikamata. “Wamekuhangaisha bure,” alisema baadaye. “Ilikuwa tukukamate, upelekwe Dodoma kwenye hospitali ya wenye maradhi ya akili. Unaonekana huna tatizo loolote.”
Askari huyo hakuweza kunitazama usoni kwa aibu.
Mara niliporuhusiwa, nilichukua begi langu na kurudi katika dirisha lilelile la mkata tiketi. Nilimkuta karani yuleyule bado akiwa kazini. “Nataka tiketi,” nilimwamuru.
Aliponitazama alishtuka kama aliyeguswa na waya wa umeme. “Ya kwenda wapi?” alinihoji kwa sauti ambayo haikuwa imara kama awali.
“Popote,” nilimjibu kama awali.
Alitazama huko na huko kama anayetaka kuomba msaada. Kisha akasema, “Leo kuna treni mbili. Moja inakwenda Kigoma, itapita usiku. Nyingine inakwenda Mpanda, itaondoka hapa baada ya nusu saa.”
Nipe ya Mpanda.” Nilisema bila ya kufikiri sana.
“Shilingi tano, njia moja.”
“Nipe,” nilimjibu nikimlipa. Nikapokea tiketi na chenji zangu na kuzitia mfukoni. Nikaenda mgahawa mmoja uliokuwa karibu ambapo nilinunua wali kwa maharage, nikayashushia kwa chai ya rangi. King’ora cha abiria wa treni ya Mpanda kilipolia nilikuwa mmoja wa abiria wa kwanza kuiparamia.
* * *​
Sikuhitaji kufikiri sana kabla ya kukata tiketi hiyo kwa sababu nyingi. Kwanza, nilikuwa na hisia kuwa Tabora haukuwa mji wangu wa bahati. Kuumbuliwa na mkuu wa shule kwa kiwango kile kulinitia doa na dosari kubwa iliyofanya nijisikie aibu isiyo na kifani. Mimi sio yatima. Nina baba na mama. Nina babu mwerevu kuliko mamia ya mababu ninaowajua. Kiu ya elimu haikuwa sababu nzuri ya kunifanya nikubali wazo la kipuuzi la kufanywa mtoto wa kambo wa Chifu Masanja.
Ni wazo hilo lililofanya nitupilie mbali wazo la kurejea Usukumani. Ningemwambia nini Chifu?
Nimebainika. Mtoto wako halisi yuko shuleni, kwa hiyo nitafutie hifadhi mpya!’ Aibu iliyoje. Ningemwambia nini mkewe na watumishi wa himaya yake ambao bila shaka wengi waliijua kinachoendelea?
Ndipo nilipowaza juu ya kurudi nyumbani. Nipande garimoshi hadi Kigoma, huko nitafute njia ya kufika Kasulu. Huenda tayari kulikuwa na malori ambayo yalibeba watu na mizigo kama sehemu nyingine za nchi.
Hata hivyo, hilo pia sikulitekeleza kwa sababu tele. Moja ilikuwa aibu. Mwanamume akitoka ametoka. Akirudi ana kitu cha kuonyesha kijijini. Ama vyeti vya kuhitimu masomo yake ama fedha au mtaji au kujenga nyumba bora zaidi. Mimi ningerudi na aibu tupu. Sikuwa tayari kufanya hivyo.
Sababu nyingine iliyonizuia kwenda nyumbani ni babu yangu. Ni kweli alinipenda sana na angefurahi sana kuniona. Lakini sikupenda kujitokeza mbele yake kichwa kitupu, mikono mitupu. Alitegemea nirudi na elimu. Alitegemea nirudi na mali. Kamwe asingefurahi kuona nikirudi mnyonge, kama kinda la ndege, linalotegemea mama akutafutie, akutafunie, umeze.
Lakini kuna sababu nyingine, kubwa zaidi, iliyonifanya nisijisikie kumtazama babu machoni. Hirizi yake. Hirizi hiyo ya familia, ambayo kwa mujibu wa maelekezo yake ilivaliwa na babu yake, baba yake na kisha yeye mwenyewe. Hirizi ambayo ilimpeleka Ughaibuni na kumrejeshha salama. Naam, hirizi ambayo aliivua na kunivisha mimi, badala ya baba, ili nipate kile ambacho aliamini kingeinua ukoo na familia yetu.
Hirizi ambayo niliipoteza kwa uzembe!
Haikuwa kweli kuwa chanzo cha migogoro yangu hii mipya, ikiwa pamoja na kukataliwa nafasi ya kusoma, kwa namna moja au nyingine ilihusiana na kupotea kwa hirizi ile? Mara kwa mara niliwaza.
 
Jackal

Jackal

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Messages
5,096
Points
2,000
Jackal

Jackal

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2012
5,096 2,000
Haaahhaa nimeipenda hii :
Mwanamume akitoka ametoka. Akirudi ana kitu cha kuonyesha kijijini. Ama vyeti vya kuhitimu masomo yake ama fedha au mtaji au kujenga nyumba bora zaidi. Mimi ningerudi na aibu tupu.
 

Forum statistics

Threads 1,336,205
Members 512,562
Posts 32,530,421
Top