Mjue James Hardley Chase, Mwandishi maarufu wa Vitabu vya Riwaya

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,886
155,869
Mjue james Hardley Chase, kipenzi cha wapenda riwaya za kusisimua, aliyehamasisha wengi kupenda utamaduni wa kusoma vitabu na ung'eng'e

1686518822020.png

Taja jia la James Hadley Chase na wahenga wenzangu wengi watakuambia huyo alikuwa ni mmoja wa waandishi maarufu sana wa riwaya za kusisimua wa wakati huo, na watu wengi wamesoma vitabu vyake kati ya miaka ya 1970 na 1990, wakiwa sekondari (kati ya form one hadi form four), vikiwa ni mojawapo ya burudani na nyenzo muhimu za kuujua ung’eng’e.

Ukichanganya na utamaduni wa kupenda kusoma wa wakati huo, vijana wengi walikuwa wakishindana nani kasoma “Chase” nyingi kuliko wengine, na soga vijiweni ilikuwa kujadili vitabu hivyo na vingine vya kusisimua kama vya akina John Creasy, Raymond Chandler, Agatha Christie, Mickey Spillane, Graham Greene na wengineo.

Yaani kama ulikuwa hujasoma vitabu hivyo, ukiwa kijiweni ama sehemu ya mkusanyiko wa vijana unaweza ukaaga kwa kukosa cha kusimulia.

Hata hapa Tanzania katika kipindi hicho kuliibuka kina “Chase” wengine kibao, akiwemo Elvis Musiba, Hammie Rajab, Ben Mtobwa, Jackson Kalindimya, Eddie Ganzel, Salim Bawji na wengineo wengi walioutendea haki utamaduni wa watu kusoma vitabu.

Inasikitisha kuona siku hizi utamaduni wa kusoma vitabu uko hoi bin taabani huko ICU ukiugulia "maradhi ya mitandao" ya Insta, Facebook, TikTok na YouTube.

Na hapo hata sina uhakika kama waandishi wa riwaya kama bado wapo, na kama wapo wana hali gani. Je, Bookshop nazo zina hali gani?

Turudi kwake Chase. Huyu bwana, ingawa jina lake la kuzaliwa lilikuwa René Lodge Brabazon Raymond, lakini yeye alijulikana zaidi kwa majina yake mbalimbali ya kiuandishi ya bandia, ikiwa ni pamoja na hilo la James Hadley Chase, na mengine yakiwa James L. Docherty, Raymond Marshall, R. Raymond, na Ambrose Grant.

Kasha la kazi za Chase, likijumuisha jumla ya vitabu 90, lilimpa sifa ya kuwa mfalme wa waandishi wa riwaya za kusisimua huko Ulaya. Pia alikuwa mmoja wa waandishi bora kimataifa, na hadi leo vitabu vyake 50 vimegeuzwa kuwa filamu.

René Lodge Brabazon Raymond alizaliwa tarehe 24 Desemba 1906 huko London, Uingereza. Alikuwa mtoto wa Kanali Francis Raymond wa Jeshi la India la Kikoloni, mtaalamu wa upasuaji wa wanyama. Baba yake, akitaka mwanawe awe na taaluma ya kisayansi na alimpeleka shuleni King's School, Rochester, Kent.

Hata hivyo, Chase aliondoka nyumbani akiwa na umri wa miaka 18. Mwaka 1932,Chase alimuoa Bi. Sylvia Ray, na walijaaliwa mtoto mmoja. Mwaka 1956, walihamia Ufaransa. Mwaka 1969, walihama kwenda Uswisi.

Baada ya kuondoka nyumbani akiwa na umri wa miaka 18, Chase alifanya kazi katika maduka ya vitabu. Pia alikuwa msaidizi wa muuzaji wa vitabu, kabla ya kugeukia kazi ya kuandika ambayo ilimletea zaidi ya vitabu 90 vya hadithi za upelelezi. Hobby zake Zaidi zilikuwa upigaji picha, kwa kiwango cha juu, kusoma, na kusikiliza muziki wa classical na opera.

Hali ngumu ya uchumi kupata kutokea nchini Marekani (1929-1939) vilisababisha kuibuka kwa utamaduni wa uhalifu mkubwa kabla ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Wimbi hilo la uhalifu liliambatana na uzoefu wa biashara ya vitabu wa Chase, ambaye aliona fursa kubwa imejitokeza ya mahitaji hadithi za uhalifu.

Basi baada ya kusoma na kuhamasika na riwaya ya mtunzi gwiji James M. Cain ya "The Postman Always Rings Twice” (1934) na kusoma kuhusu uhalifu wa mwanamama wa Marekani Ma Barker na wanae, na kwa msaada wa ramani na kamusi ya lugha ya mtaani, aliandika kitabu chake cha kwanza cha "No Orchids for Miss Blandish" ambacho kilipata umaarufu mkubwa na kuwa moja ya vitabu vilivyotafsiriwa katika lugha nyingi katika muongo huo.
1686518509441.png

Kitabu hicho kiliandikwa pia kwenye makala ya mwaka 1944 "Raffles and Miss Blandish" na George Orwell. Baadaye Chase na na rafikiye mmoja aitwaye Robert Nesbitt waliibadilisha kuwa tamthilia ambayo ilifanyika katika eneo la West End huko London na kusifiwa mno.

Ubadilishaji wa kitabu hicho kuwa filamu wa mwaka 1948 ulilaaniwa sana kwa sababu ya jinsi ilivyokuwa ikionyesha vurugu na ngono. Mwandishi mwingine, Robert Aldrich alikifanyia marekebisho, na filamu ya "The Grissom Gang," ikazaliwa mwaka 1971.

Wakati wa vita, Raymond alikuwa mhariri wa jarida rasmi la jeshio la anga la Uingereza (RAF) na kutoka kwenye kipindi hicho ilizaliwa hadithi fupi ya Chase "The Mirro in Room 22", ambapo alijaribu mkono wake nje hadithi za uhalifu.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Chase alifanya urafiki na Merrill Panitt (baadaye mhariri wa TV Guide), ambaye alimpa kamusi ya lugha ya mtaani ya Marekani, ramani na vitabu vya marejeleo vya ulimwengu wa uhalifu wa Marekani.

Hii ilimpa Chase msingi wa vitabu vyake vya awali vilivyouzwa huko Marekani, ambavyo vingi vilitokana na matukio halisi yanayotokea huko. Chase kamwe hakukaa Marekani ingawa alifanya ziara mbili fupi, moja huko Miami na nyingine wakati akielekea Mexico.

Miaka iliyofuata, Chase aliendeleza mtindo wa kipekee katika uandishiwake ambao ulikuwa wa kasi, bila maelezo mengi au vionjo juu ya mazingira au hali ya hewa, na wahusika wasioaminika. Wahusika katika riwaya zake na hadithifupi walikuwa thabiti na wepesi kuamua na kufanya jambo.

Sentensi fupi, mazungumzo mafupi katika lugha ya mtaani pamoja na staili nyingine nyingi zilikuwa ni sifa za uandishi wake.

Vitabu vyake vyote vilikuwa vitamu sana, kiasi msomaji alijikuta anafunua kurasa bila kukoma ili kufikia mwisho wa kitabu. Ukurasa wa mwisho mara nyingi ulikuwa na hitimisho la ghafla sana na hata mashabiki wake wakubwa kabisa walikuwa wakishangazwa.

Vitabu vyake vya awali vilikuwa na vurugu ambayo ililingana na wakati ambao vilikuwa vimeandikwa, ingawa hii ilipungua sana wakati hadithi zilianza kuwa zimezingatia hali za mazingira ili kuunda kiwango kikubwa cha mvutano ambao ulikuwa sifa ya uandishi wake. Ngono kamwe haikuwa wazi na, ingawa mara nyingi ilionyeshwa kidogo, mara chache ilifanyika.

Katika hadithi kadhaa za Chase, mhusika mkuu anajaribu kuwa tajiri kwa kufanya uhalifu - udanganyifu wa bima au wizi. Lakini mpango huo daima hushindwa na kusababisha mauaji na hatimaye njia panda, ambapo mhusika anajikuta hana ujanja wa kuepuka matatizo. Wanawake mara nyingi ni warembo, wenye akili, na wenye hila; wanaua bila kusita ikiwa wanahitaji
kuficha uhalifu.

Hadithi zake kwa kawaida zinahusu familia zilizovurugika, na kilele chake mwishoni aghalabu kilikaribia jina la kitabu.

Katika riwaya nyingi za Chase, wanawake wenye hila au "Wadangaji" wanachukua nafasi kubwa sana. Shujaa anapendwa na mmoja wao na yuko tayari kumuua mtu kwa ajili yake. Ni baada tu ya kuua ndipo anagundua kwamba mwanamke huyo alikuwa akimchezea akili kwa ajili ya malengo mengine kabisa!

Kwa bahati mbaya, Chase hakuwa maarufu sana nchini Uingereza au Amerika ya Kaskazini kama alivyokuwa sehemu zingine za Ulaya. Kwa miaka mingi aliishi katika majumba makubwa na kuendesha magari ya kifahari, hata hivyo, alijikuta akiwa na matatizo ya kifedha na akafa maskini akiacha madeni makubwa nyuma yake.

Chase alifariki mnamo tarehe 6 Februari, mwaka 1985 nyumbani kwake huko Corseaux-sur-Vevey, kando ya Ziwa Geneva, Uswisi.
 
Mjue james Hardley Chase, kipenzi cha wapenda riwaya za kusisimua, aliyehamasisha wengi kupenda utamaduni wa kusoma vitabu na ung'eng'e

View attachment 2654456

View attachment 2654455

Mimi ni mlevi mbwa wa novel zake japo alikuwa bonge la mbaguzi kwa weusi! Kati ya novel zake 88 nilibahatika kusoma si chini ya 75
Alikuwa na wachapishaji wawili wa novel zake... Panther ndio alichagua zile novel kali .. Ilikuwa niliona novel ya Chase na mchapishaji ni Panther aisee nilikuwa napagawa mbaya
One bright summer Morning
Come easy go easy
A point of no return
Believed Violet
Mission to Vienna
Believe this you believe anything
Tiger by tail
Good night Miss Elliot
....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu uzi unawahusu Legends.
 
Amen amen
 
Hakika wewe ulikuwa ni mpenzi sana wa novel za Chase
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom