Riwaya: Kiguu na njia

K

kisukari

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2010
Messages
4,395
Points
2,000
K

kisukari

JF-Expert Member
Joined Jul 16, 2010
4,395 2,000
Hadithi nzuri ni ya kihistoria. Enzi hizo watu waliamini dini tofauti kabla ya dini ya ki kristo na kiislamu kutambulishwa.
 
nameless girl

nameless girl

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
4,027
Points
2,000
nameless girl

nameless girl

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
4,027 2,000
KWA ANAYEKIHITAJI KITABU HIKI CHA KIGUU NA NJIA NA VINGINE VYA BEN MTOBWA KAMA DAR ES SALAAM USIKU, SALAMU TOKA KUZIMU, TUTARUDI NA ROHO ZETU NA VINGINE VINGI, NITAFUTE KWA KUPITIA 0712504985 AU 0763044459. KARIBUNI.
Laiti ningejua kuwa agano hilo lilikuwa la mwisho, kwamba nisingemwona tena babu yangu, nisingekubali kuachana naye kirahisi kiasi kile.
Endeleaaaaaaaaa
* * *​
“A!”
“Ahaaaaaaaaa!”
“E!”
“Eheeeeeee!”
“I!”
“Ihiiiiiiiii!”
“Oh!”
“Ohoooooo!”
“U!”
“Uhuuuuuuuu!”
“a,” inaandikwa kama punje ya harage….’e’ iko kama ndizi iliyovimba juu…. ‘I’ ni kama msumari… ‘o’ ni kama yai…. ‘u’ ni kama shimo. Mnanielewa?”
“Ndiyoooo!”
Mtukwao, bin Karimanzira bin Kionambali nilikuwa nimeanza shule. Hapana! Sikuwa tena Mtukwao, wala Karimanzira. Nilikuwa na jina jipya, Petro Kionambali. Ndivyo nilivyoandikishwa. Ndivyo nilivyokuwa nikiitwa na walimu na wanafunzi wenzangu katika maisha na mazingira hayo mapya.
Tuliishi katika mabweni, tukiwa wavulana wapatao sitini au sabini hivi. Wengi wetu tulikuwa watu wa makabila tofauti, utamaduni tofauti na hata maumbile tofauti. Tulitofautiana pia katika umri. Wakati mimi nilijiona mdogo kwa umri wangu wa miaka kumi na mitatu, walikuwepo kaka zetu wenye umri wa miaka kumi na saba katika darasa hilohilo la kwanza. Wengine walikuwa wadogo kabisa kwa miaka yao kumi hadi minane.
Tulifundishwa kusoma na kuandika. Lakini mkazo mkubwa hata kabla hatujaanza kusoma na kuandika ulikuwa wa mafundisho ya dini. Tulifundishwa upendo, kusali pamoja na kuimba nyimbo za kumsifu bwana. Tulifundishwa kila kitu juu ya Mungu wa Izrael, aliyemtuma mwanawe wa pekee, ili azaliwe kama binadamu katika zizi la kondoo, ateswe, asulubiwe na kufufuka siku ya tatu baada ya kifo chake kwa ajili ya kutukomboa na dhambi zetu. Zaidi, tuliambiwa kuwa tayari siku zote, kwani haikujulikana siku wala saa ambayo angerudi tena duniani na kuwachukua ‘wateule’ wake na wale wasio wake kutupwa jehanamu ambako wangeungua kwa moto mkali wa milele.
Nikijua kuwa nilikuwa nimetembea safari ndefu na ngumu kuifuata fursa hiyo ya kupata elimu nilitilia maanani kila nilichofundishwa na kuzingatia kila fundisho la dini. Jambo hilo lilinifanya baada ya siku chache tu niwe mmoja wa wanafunzi hodari sana shuleni hapo. Walimu walinipenda, wanafunzi walinisikiliza. Hivyo, haikuwa ajabu pale, ulipofika mwisho wa mwaka huo nilipoteuliwa kuwa kiranja wa darasa langu.
Mafunzo ya dini pia niliyazingatia sana. Sikuwa na sababu wala wasaa wa kuiba, sikuwa na haja ya kumtukana mtu wala kumzulia uongo. Kama kuna dhambi pekee, ambayo siku zote ilinisuta moyoni basi ilikuwa ile ya kundelea kuthamini na kuivaa kwa siri hirizi yangu niliyoachiwa na babu. Sikuwa tayari kuitoa kwa shemasi au kasisi ili ichomwe moto. Nilichukulia ile kama kiungo pekee baina yangu na familia yangu, kiungo ambacho kukitoa ingekuwa sawa na kuukata mzizi wa mwisho; kati yangu na asili yangu.
Elimu niliyoipata katika nchi hiyo ya Wahaya haikuwa ile ya darasani wala ya dini pekee. Nilipata elimu ya mitaani ambayo kwa kweli ilinisaidia sana. Kwa mfano, wakati shule hazikufundisha lugha ya Kihaya, huko mitaani nilifundishwa. Ndani ya mwaka mmoja tu nilikuwa tayari nikisikia na kuzungumza Kihaya kwa ufasaha kama Muhaya yeyote yule.
Shule hatukufundishwa kuogelea. Lakini mimi katika kipindi hichohicho cha mwaka mmoja tayari nilikuwa hodari wa kucheza na maji kama samaki. Niliweza kuelea juu ya maji kama boya au kupiga mbizi kama sangara. Hali kadhalika, nilijifunza kupiga makasia na kuvuta aina kwa aina za samaki. Kwa kushika maji au kuangalia mwenendo wa mawingu angani nilijua ni wakati gani ziwa lingechafuka kwa upepo mkali, wakati gani limepungua.
Kwa kiasi kikubwa ‘utundu’ wangu ziwani ulichangiwa na mapenzi makubwa niliyokuwa nayo kwa ziwa hilo toka pale nilipoliona kwa mara ya kwanza. Nililichukulia kama hazina ya pekee tuliyojaaliwa na Muumba kwa kuzingatia kuwa nchi nyingine badala ya maji hayo mengi wao wamejaliwa majangwa yaliyojaa mchanga na joto kali. Nililichukulia ziwa hilo kama hazina ndani ya hazina. Wingi wa samaki waliojaa katika ziwa hilo, aina waliokuwa wakiishi ndani au kando mwa ziwa hilo ulikuwa ushahidi tosha wa utajiri huo.
Mtu aliyechangia kunipa elimu na ujuzi mwingi juu ya ziwa hakuwa mwingine zaidi ya mzee Buberwa, baba yangu wa kufikia. Kila nilipopata likizo nilikuwa nikienda kwake ambako nilishirikishwa katika uvuvi na kuweza kujipatia si ujuzi tu bali pamoja na vijisenti vya matumizi kutokana na mchango wangu katika uvuvi. Mtoto wake mkubwa, Muleju, aliondokea kuwa rafiki yangu mkubwa na ndiye aliyenipa darasa la awali la kuogelea. Madarasa yaliyofuata nilijifunza mwenyewe kutokana na ujasiri na jitihada zangu.
Buberwa alikuwa mzee aliyependa sana utani. Hakuchoka kuniambia mara kwa mara, “Mwanangu tumekupeleka shule kuchukua elimu. Hatukukupeleka pale kujifunza utawa na upadri. Chukua elimu yako, usichukue upadri wao. Nataka ukimaliza shule nikupe msichana mrembo wa Kihaya, umuoe na kurudi naye kwenu. Watu wa huko wajue mungu alivyopendelea nchi ya Wahaya si kwa samaki na maji pekee, bali pamoja na wajihi murua wa wakazi wake.”
Kuoa! Nililichukulia kama jambo ambalo lingenitokea baada ya karne nyingine zijazo. Sikupata kumjibu kwa hilo. Naye nadhani hakutegemea jibu langu. Ilikuwa kama mtu anayenikumbusha jambo fulani, mara kwa mara, ili lisije likanitoka akilini.
Nimezungumza mengi juu ya raha za ziwani, raha za kula samaki watamu, raha za kuelea juu ya maji, raha ya kupata fedha kutokana na mauzo hayo. Pengine haitakuwa haki kama sitataja chochote pia juu ya karaha zake pia.
Wanasema, wavuvi wengi kwamba ukiwa ziwani ujue kuwa unatembea na ‘kifo mkononi.’ Madai ambayo niliyathibitisha kwa vitendo kwa uhai wangu wa ziwani hapo.
Tukio la kwanza lilikuwa lile la kupotea ziwani. Siku hiyo tulikwenda kuvua samaki usiku. Ghafla, ulizuka upepo mkubwa ulioambatana na mvua nzito ambayo ilifanya karabai tulilokuwa tukilitumia kwa ajili ya mwanga lizimike. Upepo huo ulisababisha mawimbi makubwa yaliyofanya mara kwa mara maji yaingie ndani ya mtumbwi. Huku nikitetemeka nilipewa kazi ya kuondoa maji hayo yaliyoingia huku wenzangu wawili waliobakia wakijitahidi kupiga makasia kurudi ufukweni. Zilikuwa jitihada zisizo na matunda. Kwanza, kutokana na kiza kilichotanda hakuna aliyefahamu nyumbani ni upande upi. Pia, kasi ya maji kuingia katika mtumbwi ilikuwa kubwa kuliko ile ya kuyaondoa. Muda mfupi baadaye wenzangu walikata tamaa ya kupiga makasia bila kujua kama wanakwenda mbele au wanarudi nyuma. Wakajiunga nami katika jukumu la kuondoa maji katika mtumbwi. Haikusaidia. Muda mfupi baadaye mtumbwi wetu ulizama na kupinduka. Tukaogelea na kupanda juu ya mgongo wake huku tukipiga kelele kuomba msaada.
Katika purukushani hizo mwenzetu mmoja alipotea. Nadhani alichoka kuendelea kuung’ang’ania mgongo wa mtumbwi ambao ulikuwa ukiyumba na kutupwa huku na kule kwa mawimbi hayo. Mimi na Muleju tuliendelea kung’ang’ania hadi alfajiri, upepo huo ulipopoa.
Tulishinda ziwani humo, juu ya mgongo wa mtumbwi huo tukiwa hatuna la kufanya. Makasia yetu yalikuwa yamechukuliwa na mawimbi na uwezo wa kuufunua mtumbwi huo hatukuwa nao.
Siku ya kwanza na usiku wake ukapita. Siku ya pili, jioni sana, tukiwa tayari taabani kwa njaa na uchovu, tuliona mtumbwi wa wavuvi ukitujia. Hawa walituzoa na kutupakia kwenye mtumbwi wao kisha wakajitahidi kuubinua mtumbwi wetu na kuondoa maji yaliyokuwemo. Wawili kati yao waliingia katika mtumbwi huo na kuupiga makasia kuelekea ufukoni. Ufukwe huo uliondokea kuwa kisiwa kidogo cha Bumbire, mbali sana kutoka Kashozi tulikoanzia safari.
Tulipumzika kisiwani humo kwa siku tatu zaidi, kabla ya kurejea nyumbani ambako walikwishakaa matanga wakiamini kuwa nilikwishakufa. Tuliopona tulifanyiwa sherehe ndogo, mwenzetu aliyepotea aliombolezwa kwa taratibu za kimila.
Nikiwa na hakika kuwa kilichoniokoa katika mkasa ule ilikuwa ile hirizi yangu niliyopewa na babu, ambayo muda wote ilikuwa kifuani mwangu, niliibusu na kuikumbatia kwa furaha, “Nitakulinda daima, ili nawe unilinde,” niliinong’oneza.
Katika hali ya kawaida, tukio hilo lingetosha kabisa niliogope ziwa hilo kama simba mla watu. Lakini, kwa jinsi ziwa lilivyokwishaniingia akilini nilichukulia tukio zima kama jambo la kawaida tu, katika pilikapilika za maisha. Nikaendelea na shughuli zangu bila hofu wala wasiwasi wowote.
Tukio lililofuata, ambalo pia sikulitegemea kiasi lilikuwa kama la kuchekesha. Nilikuwa nikiogelea kando ya ziwa, baada ya kazi ya kutwa nzima za mchana huo. Nadhani nilikuwa nimeogelea kwa muda mrefu kiasi, kwani nilijihisi uchovu mwingi. Mara nikaona kitu kama gogo likielea juu ya maji mbele yangu. Nikalifuata na kuparamia juu yake ili nipumzike kidogo. Nilishangaa kuona gogo hilo likizama ghafla na kisha likiibuka hatua chache mbele yangu na kufunua domo lake kubwa ama kupiga mwayo ama kunifokea.
Mamba!
Nilikuwa nimeparamia mgongo wa mamba. Kwa kujua kuwa mamba hana uwezo wa kumnasa mtu katika maji mengi niliogelea harakaharaka kupanda ziwani. Zilipogeuka nilimwona mamba yule akiogelea kurudi ufukoni. Ama alikuwa ameshiba sana, ama alishtuka mie kukimbia.
Hilo na lile la kukoswakoswa na kiboko mmoja aliyefanikiwa kupindua mtumbwi wetu ni miongoni mwa matukio mengi, ya kutisha yaliyoambatana na maisha yangu katika ziwa hilo.
Kwa kupona hatari baada ya hatari, huku nikiendelea kupata mafanikio kimaisha na kitaaluma niliamini kabisa kuwa hirizi yangu ilikuwa ikitimiza wajibu wake. Mara kwa mara niliibusu na kuinong’oneza, “Nitakulinda daima ili nawe unilinde.”
 
nameless girl

nameless girl

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
4,027
Points
2,000
nameless girl

nameless girl

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
4,027 2,000

KWA ANAYEKIHITAJI KITABU HIKI CHA KIGUU NA NJIA NA VINGINE VYA BEN MTOBWA KAMA DAR ES SALAAM USIKU, SALAMU TOKA KUZIMU, TUTARUDI NA ROHO ZETU NA VINGINE VINGI, NITAFUTE KWA KUPITIA 0712504985 AU 0763044459. KARIBUNI.SURA YA NNE
Hirizi yazua jambo.
Hirizi iliyokuwa ikinilinda ndiyo iliyoondokea kuwa kisa na mkasa uliosababisha safari yangu kielimu ikome baada ya miaka mitano tu.
Wakati huo nilikwishashuhudia watu wote waliovuka miaka kumi na minane wakihesabiwa katika kile kilichoitwa sensa ya kwanza nchini Tanganyika. Tukio hilo lililofanyika Julai mosi, mwaka 1931. Mimi sikuhesabiwa kwa ajili ya umri na hata kama ningekuwa na umri nisingehesabiwa, kwani Makarani wa kazi hiyo walikuwa wakihesabu wakuu wa kaya pekee na kisha kwenda kutengeneza hesabu zao. Jambo hilo lilileta manung’uniko kuwa kazi hiyo haikufanyika kwa ufanisi.
Pia, wakati huo nilikuwa nikidonoadonoa maneno kadhaa yaliyoandikwa katika gazeti la Kiingereza lililoitwa Tanganyika Standard, ambalo lilikuwa limeanzishwa huko Dar es Salaam mwaka uleule wa hesabu ya watu.
Ni kupitia gazeti hilo nilipofahamu kuwa Gavana wa nchi wakati huo aliitwa H.A MacMichael akiwa amemrithi G.S Symes ambaye naye alimrithi D.C Cameron. Wote hao walikuwa wamemfuatia Gavana wa kwanza wa Uingereza nchini aliyeitwa H.A Byatt, aliyepewa wadhifa huo mara baada ya Wajerumani kupokonywa nchi ya Tanganyika mwaka 1920.
Naikumbuka vizuri sana siku ya balaa. Ilikuwa tarehe 4 Novemba, 1934. Kule Dar es Salaam kulikuwa na kikao muhimu cha watawala kilichoitwa Kamati ya Ushauri wa Elimu kwa Mwafrika. Kamati hiyo ilipinga wazo la wanafunzi wa Kiafrika kuchangia mitaala na madarasa ya Wazungu au Waasia kwa madai kuwa uwezo wa watoto wa Kiafrika kuelewa wanachofundishwa ulikuwa duni sana ukilinganishwa na Wazungu na Wahindi. Hata hivyo, mjumbe mmoja, aliyeitwa Martin Kayamba, alipinga vikali madai hayo. Alisema, “Huwezo wa mtoto wa Kiafrika haukuwa na tofauti yoyote na ule wa Wazungu au Wahindi bali tatizo pekee lililosababisha hisia hizo zijitokeze ni watoto hao kutopewa nafasi sawa na wengine.”
Habari ambazo shuleni hapo, miongoni mwa walimu na wanafunzi, zilikuwa kubwa sana. Kayamba alisifiwa na kupongezwa sana kwa kitendo chake cha kuwapa wakoloni ukweli.
Kwa utoto wetu tuliamini kauli yake ingekuwa mwisho wa kutengwa na mwanzo wa kuruhusiwa kusoma pamoja na watoto wa Wazungu na Wahindi ambao walikuwa na shule bora mara kadhaa zaidi yetu. Tulikuwa katika vijikundi vidogovidogo tukijadiliana juu ya hilo baada ya masomo ya kutwa nzima tulipozinduliwa na kelele za baadhi yetu ambao walikuwa tayari wakikimbilia nyuma ya shule wakibeba mifuko na mabakuli.
“Senene!” mmoja wetu alitamka. Mara alikurupuka na kupiga mbio kuwafuata wengine.
Ulikuwa msimu wa senene. Mara nyingi msimu huo uliambatana na ule wa kumbikumbi ambao ni jamii ya mchwa ambao huota mbawa na kuruka kwa makundi makubwa angani kwa muda mfupi. Baadaye kuishiwa uwezo wa kuruka na kudondoka ardhini huku mbawa zao zikinyofoka.
Wakishapoteza uwezo wa kuruka kumbikumbi huzagaa ardhini wakitafuta namna ya kurudi katika vichuguu vyao. Wengi huishia kuwa kitoweo cha binadamu na ndege. Kati ya wachache ambao hubaatika kunusurika mmoja wao hugeuka Malkia ambaye hutaga maelfu kwa maelfu ya mayai hivyo kuanzisha upya kizazi chao. Hao ni kumbikumbi.
Senene, ambao ni jamii ya panzi, ni maarufu zaidi kwa wakazi wa eneo hilo jirani. Wao wana tabia ya nzige, ingawa hawana madhara makubwa kama ndugu zao hao ambao wanaweza kugeuza pori kuwa jangwa kwa muda mfupi sana.
Senene, ni chakula maarufu zaidi, na kwangu mimi walivutia zaidi. Hivyo, kama wenzangu wote sikuweza kujizuia. Nilikimbia huko na huko na kuwakamata wengi tu ambao niliwajaza katika mfuko ili kesho niweze kuwaanika na kisha kuwahifadhi kwa matumizi ya baadaye.
Na baada ya pilikapilika hizo, wakati tukiwa katika sala ya mwisho kabla ya kulala nilipohisi upungufu fulani katika mwili wangu. Nimepoteza nini? Nilijiuliza huku nikijipapasa. Haikunichukua muda kubaini kuwa hirizi yangu, ambayo tunapokuwa darasani nilikuwa na tabia ya kuhifadhi mfukoni, ilikuwa imetoweka! Bila shaka ilidondoka katika zile purukushani za kunasa senene.
Hirizi yangu! Niliwaza kwa uchungu, nikihisi nguvu zote zikiniisha mwilini. Ibada iliyokuwa ikiendelea haikuniingia akilini. Nilitamani kutoka nikaitafute lakini tayari ulikuwa usiku mwingi, kwanza nisingeiona, pili nisingeruhusiwa kutoka.
Usiku huo usingizi ulinikata kabisa. Alfajiri sana, kabla ya mtu yeyote kuamka mimi tayari nilikuwa nje nikijaribu kupita kila mahala nilipohisi kuwa ningeweza kuidondosha. Sikuipata.
“Unatafuta nini?” nilisikia sauti ya mtu ikizungumza nyuma yangu. Nilipogeuka nilimwona Byabato, mwanafunzi mfupi, mnene, ambaye kwa kweli hakupata kuwa rafiki yangu.
“Natafuta kalamu yangu,” nilidanganya.
“Kalamu! Utaiona kweli saa hizi? Kwa nini usingoje jua lichomoze?”
“Siyo kazi yako!” nilimwambia
Byabato alinitazama kwa mshangao. Mara nikamwona yeye pia anaanza kutafuta kitu huko na huko kama mimi. Ilikuwa zamu yangu kushangaa.
“Unatafuta nini?” nikamuuliza.
Naye akanipa jibu lilelile ambalo mimi nilimpa dakika mbili zilizopita, “Siyo kazi yako!”
Kihoro kilinipanda. Kwa jinsi nilivyomfahamu Byabato nilijua kuwa kama angeipata hirizi ile asingesita kubaini kuwa ndiyo nilikuwa naitafuta. Na kwa tabia yake asingekuwa mtu wa kuniwekea siri. Ingemchukua dakika chache sana kuitangazia shule na dunia nzima kuwa nilikuwa na hirizi. Sikuwa na namna ya kumzuia. Nilichofanya nilijaribu kumpoteza kwa kutafuta sehemu ambayo nilikuwa na hakika kuwa sikuifikia. Lakini, kwa mshangao wangu yeye alielekea upande wa pili, ambako ndiko hasa nilikopita katika nyendo zangu.
Nilishukuru pale kengele ya kujiandaa kuingia madarasani ilipolia kabla sijaipata wala kumwona Byabato akiiokota. Nikaondoka kinyonge na kurejea bwenini kujiandaa.
Nilikuja kuiona tena hirizi hiyo saa nane za mchana. Kuiona, siyo kuipata rafiki yangu! Kwani ilikuwa mikononi mwa Padri Backhove aliyekuwa ametembelea eneo hilo ili kukagua maendeleo ya shule na maendeleo ya wanafunzi na waumini wengine kiimani.
Ilikuwa baada ya mlo wa mchana, ambao mimi niliula kidogo sana, kengele ya dharura ilipigwa na wote tukakusanyika katika ukumbi wa ibada. Padri alianza kwa kutoa nasaha au somo refu juu ya raha inayotusubiri huko mbinguni na mateso makali ya moto wa milele unaowasubiri huko jehanamu wote ambao watakwenda kinyume na amri kumi za Mungu. “Mungu wetu ni mwenye wivu,” aliongeza Padri. “Moja ya amri zake kumi, alizozileta kwa mkono wa mtumishi wake Musa pale kwenye mlima Sinai inasema waziwazi, ‘Usiitumikie miungu mingine ila mimi’ Sawa?”
“Sawa,” wote tuliitikia.
“Mungu wetu ni msafi,” Padri Backhove aliendelea, “Anapenda wote tuwe wasafi wa miili na mioyo yetu. Sawa?”
“Sawa.”
“Kumfuata bwana maana yake ni kukana dhambi. Kukana mila na desturi zetu zote potofu na kuanza maisha mapya ndani ya Kristo. Maisha safi kimwili na kiroho. Mkristo wa kweli hatakiwi kuamini uchawi. Hatakiwi kuabudu sanamu… Hatakiwi kuvaa hirizi… sawa?”

Mara lilipotajwa neno ‘hirizi’ nilijua wapi mahubiri hayo yanaelekea. Nilihisi miguu yangu ikiishiwa nguvu na mwili wangu ukitetemeka. Sikuwa na uwezo wa kusikia tena chochote ambacho padri aliendelea kusema hadi pale nilipomwona akiwa ameishika hirizi yangu na kuining’iniza mbele yetu, huku akisema, “… Nauliza kwa mara ya pili nani kati yenu aliyeidondosha hii?”
Wote tulitazamana. Macho yangu yalikutana na yale ya Byabato ambayo yalinitazama kwa namna ya kunisuta na kunidhihaki. Macho yaliyokuwa yakisema, “Unajua kuwa najua kuwa ni yako!”
“Nitauliza kwa mara ya tatu,” Padri aliendelea. “Nani kati yenu aliyedondosha hirizi hii jana?”
 
mangonifera indica

mangonifera indica

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2017
Messages
415
Points
1,000
mangonifera indica

mangonifera indica

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2017
415 1,000
Ukitupia uni tag
 
nameless girl

nameless girl

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Messages
4,027
Points
2,000
nameless girl

nameless girl

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2012
4,027 2,000
Wote tulitazamana. Macho yangu yalikutana na yale ya Byabato ambayo yalinitazama kwa namna ya kunisuta na kunidhihaki. Macho yaliyokuwa yakisema, “Unajua kuwa najua kuwa ni yako!”

ENDELEAAAAA...
“Nitauliza kwa mara ya tatu,” Padri aliendelea. “Nani kati yenu aliyedondosha hirizi hii jana?”
Macho ya Byabato yalikuwa yameganda juu ya macho yangu, yakinicheka. Sikuweza kustahimili zaidi. Niliinua mkono wangu juu na kisha kusimama huku nikijibu taratibu, “Ni yangu, Padri.”
Si Padri wala wanafunzi wenzangu walioamini masikio yao. Kwa darasa langu, kwa shule nzima na hata jamii nzima ya eneo hilo mimi nilikuwa mfano bora zaidi kimasomo na kikanisa. Nilikuwa hata nikiwasaidia mashemasi katika huduma ndogo ndogo za kanisa.
“Ni yako?” Padri aliniuliza tena, kana kwamba alitaka nibadili kauli na kuikana hirizi yangu. Sikuwa tayari kwa hilo.
“Unajua kuwa mwili wako ni hekalu la Mungu? Aliniuliza Padri.
“Najua!”
“Kwa nini basi unavaa uchafu? Kwa nini unahifadhi dhambi na kuishi nayo? Hutaki kuingia katika ufalme wa Mungu?”
Sikumjibu.
“Sio neno,” Padri aliendelea. “Leo Bwana amefanya muujiza kwa ajili yako. Ameifichua hirizi hii chafu, ambayo umeivaa kwa muda mrefu, ili ujitakase upya. Tutawasha moto hapo nje, utaichoma hirizi hii kwa mkono wako mwenyewe. Kisha tutakuombea na kukubariki kwa kitendo hicho cha kuachana na upagani milele.”
Tulitolewa nje. Zikaletwa kuni, moto ukawashwa. Huku wenzangu wakiimba pambio mbalimbali, mimi na Padri Backhove tulisimama mbele ya kadamnasi hiyo, mikononi mwake akiwa na Biblia na hirizi yangu.
“Wakati nikianza kusali, ichukue hirizi hii uitupe ndani ya moto ukitamka maneno yafuatayo ‘Shetani nakuteketeza sasa na milele, kwa jina la Yesu’ Umeelewa?”
Niliitikia kwa kichwa.
Nyimbo zilipamba moto. Sauti ya Padri akisoma sala ilisikika waziwazi. Lakini mkono wangu uliokuwa na hirizi uliishiwa nguvu huku nikitetemeka mwili mzima. Niliishikilia kwa zaidi ya dakika mbili, nikiining’iniza juu ya miale murua ya moto huo lakini vidole vyangu vilielekea kunigomea. Hisia zangu zilikwenda mbali sana toka hapo. Zilisafiri hadi usiku ule tulipoagana na babu uchochoroni. Masikio yangu yalisafiri pia. Yalikuwa pamoja nami huko uchochoroni, gizani, yakimsikia babu akisema; Hii ni hirizi ya bahati. Ilinde nayo itakulinda maishani mwako. Sauti hiyo ilikuwa wazi wazi kabisa masikioni mwangu.
“Ichome!” Padri alikatiza sala na kuniambia kwa ukali.
“Siwezi!” Nilimjibu.
“Huwezi nini?” aliniuliza kwa mshangao. “Tupa uchafu huo ndani ya moto!” nilishindwa kabisa kuviamini vidole vyangu kufanya hivyo. Mara nikageuka na kuanza kuondoka. Padri hakuyaamini macho yake. Akanifuata na kujaribu kunishika. Nikamsukuma.
Padri Backhove alikuwa mtu mnene na mzito sana. Lakini hakuwa na nguvu nyingi. Nilimsukuma kidogo tu, lakini akaanguka chali, kama gunia. Sehemu ya kanzu yake ndefu, iliyofika miguuni iliangukia ndani ya moto huo na kuanza kuungua.
“Nakufa!” Padri alipiga kelele akijiviringisha huku na kule katika jitihada za kujizoa ainuke toka mavumbini hapo.
Nilishikwa na hofu kubwa. Wakati wenzangu wakihangaika kuzima moto katika mwili wa padri, wengine wakijaribu kuinua mwili wake wenye zaidi ya kilo mia na sitini mimi nilianza kukimbia kwa nguvu zangu zote huku nikihisi sauti za watu wanaonifuata wakizomea nyuma yangu. Sikugeuka wala kusimama hadi nilipofika vichakani, mbali sana, ambako niliamini mtu yeyote asiye na uwezo wa kukimbia kama mimi na ujuzi wa mambo ya porini kama mimi, asingeweza kunipata.
* * *​
Nilijipumzisha kwa muda chini ya kivuli cha mti aina ya mvule, ulioonekana kupevuka sana. Nikaketi na kuegemea shina lake huku nikiitumia akili yangu kutafakari mustakabali wa maisha yangu baada ya tukio lile. Moyo wangu ulijaa kiza, hofu kubwa ikiwa imetanda katika nafsi yangu kwa kufikiria tu uzito wa mkasa ule.
Sikuwa na hakika kama padre Backhove alikuwa hai au la kwa moto na mweleka ule. Hata hivyo, hakika niliyokuwa nayo ni kwamba alikuwa ameathirika sana kimwili na kisaikolojia. Kwa vyovyote vile kama angenitia mkononi adhabu ambayo ningeipata isingekuwa kifani. Wazo ambalo lilinifanya nisahau kabisa ndoto ya kurudi shuleni pale na kuomba msamaha.
Zaidi ya hayo, hata kama ningerudi na kusamehewa ningeishi maisha gani shuleni pale bila kuwa kituko na kichekesho kwa kila mtu kwa miaka nenda miaka rudi? Sikuwa radhi kwa hilo.
Halafu, hata kama ungetokea muujiza nirejee shule na yote mengine yasahauliwe, jambo moja tu lisingeweza kusahauliwa kamwe. Hirizi. Kwa vyovyote vile msamaha wangu na kutakasika kwangu kungeendana na kuiteketeza hirizi ile hadharani, hirizi ambayo ni urithi wangu pekee! Kiungo cha mwisho kati yangu na familia yangu!
Mara nikaikumbuka hirizi hiyo! Iko wapi? Nilijiuliza nikitia mkono wangu mfukoni kuitafuta. Haikuwemo. Nilikagua mifuko yangu yote na kujipapasa mwili mzima, wapi. Hirizi yangu ilikuwa imepotea, bila shaka katika zile purukushani za kukimbia!
Nilihisi nikiishiwa nguvu. Kwa muda nilipoteza mapigo kadhaa ya moyo, huku macho yakiingia kiza. Hirizi yangu ambayo ilikuwa kila kitu maishani mwangu. Hirizi ambayo ilisababisha nipoteze kila kitu maishani mwangu! Imepotea!
Wanasema binadamu katika uhai wake, anaweza kufa kidogo! Kama madai hayo ni ya kweli basi mimi Petro Kionambali, siku hiyo, chini ya mti ule wa mvule nilikufa kidogo.
Na hata pale uhai uliponirejea sikuwa mtu yuleyule tena. Sikuwa na pa kwenda. Nisingeweza kurudi Kashozi kwa mzee Buberwa na kumsimulia kuwa nimeshindwa shule kwa ajili ya hirizi. Kadhalika, nisingeweza kurudi kwetu Buha na kumwambia babu na wazazi wangu kuwa nimeacha shule kwa ajili ya hirizi ambayo haipo tena. Shule nako kusingeendeka. Iko wapi hirizi tuichome? Ningeulizwa kabla ya mengine yote. Imepotea! Lingekuwa jibu langu. Nani ambaye angeniamini? Zaidi nani ambaye angenithamini? Haikuwepo namna.
Ghafla nikajiona yatima. Hapana, nilikuwa mwana mpotevu, asiye na mbele wala nyuma.
Nikainuka na kujitazama. Tayari nilikuwa kijana mrefu kuliko watu wote katika familia yangu. Nilikuwa mwembamba lakini mkakamavu. Mikono yangu ilikuwa na nguvu, miguu yangu ikiwa na uwezo. Zaidi ya kaptula, shati na viatu nilivyovaa sikuwa na chochote mkononi wala mfukoni mwangu. Nilikuwa masikini. Lakini nilijiamini. Afya yangu, elimu yangu na ari yangu vilifanya niamue jambo moja; sirudi kwetu wala sirudi shule. Nitapiga mguu, kutafuta maisha upya. Hata kama nitafika mwisho wa dunia!
* * *​
Nilipiga mguu kuelekea Kanazi. Nilifika usiku sana. Kwa kuhofia kuwa habari zangu zilishafika hapo nililala porini, juu ya mti. Alfajiri nilianza tena safari. Kiguu na njia hadi Muhutwe. Hapo niliomba hifadhi kwa wavuvi waliokuwa wamejenga vibanda vyao pwani. Hawakuwa na hiyana, ingawa mavazi ya shule niliyoyavaa yalifanya wanishuku kuwa nimetoroka shule. Sikukosa uwongo wa kuwaambia hata mashaka juu yangu yakaisha.
Katika elimu yangu fupi shuleni nilikuwa nimepata ufahamu wa kutosha wa Jiografia. Baada ya kughairi kurudi kwetu au kwenda kwa mzee Buberwa niliamua kwenda nchi ya Wasukuma. Mengi yalikuwa yakizungumzwa juu ya nchi hiyo ambayo nilitamani kuyaona kwa macho.
Zilikuwepo hadithi za Msukuma aliyeitwa Ng’wanamalundi ambaye alisemekana kuwa mganga aliyewashinda wachawi wote kwa kutumia ngoma zake. Mtu huyo wa miujiza alisemekana pia kuwa alikuwa na macho yenye nguvu za ajabu, ambayo yaliweza kukausha miti na hata binadamu aliowakazia macho, jambo lililopelekea awe akitembea huku akiwa amejifunga kitambaa usoni kufunika macho yake. Mtu huyo alidaiwa kuwa katika moja ya hafla zake alipata kukausha msitu mkubwa na mamia ya watu waliokuwa mbele yake. Jambo hilo liliifanya serikali ya mkoloni imkamate na kumhukumu kunyongwa. Lakini hakuna aliyethubutu, kwani kabla ya hukumu hiyo kutekelezwa alifungwa katika kimojawapo cha visiwa vidogovidogo vilivyo baharini katika pwani ya Bahari ya Hindi, huko Dar es Salaam. Hata hivyo, ilielezwa kuwa Ng’wanamalundi huyo kila jioni alionekana katika vilabu vya pombe Dar es Salaam akiwa amevuka bahari kwa kutembea juu ya maji. Wakoloni wakalazimika kumwachia.
Sifa nyingine ya nchi ya Wasukuma ni zile hadithi kuwa kulikuwa na milima ya mawe, ama majini ama nchi kavu. Baadhi ya milima hiyo ilielezewa kuwa ilikuwa katika maumbile ya binadamu, ikiwa imesimama miaka nenda rudi kama inayosubiri mwujiza fulani utokee, ili ipate uhai na kuanza kutembea kama binadamu wengine.
Nchi hiyo pia ilikuwa ikisifiwa sana kwa ukubwa wa ardhi na wingi wa rutuba yake. Kilimo cha mazao ya chakula na yale ya biashara kama pamba na katani kilielezewa kuwa hakikupata kumtupa mtu. Kwa bahati mbaya, mimi sikupata kuwa mkulima wa haja. Wala sikuona kama ningeweza kuwa na ustahimilivu wa kulima leo kusubiri mavuno miezi au miaka kadhaa baadaye. Mimi nilikuwa mtu wa maji. Mtu wa kutupa nyavu na kuzitupa huku tayari zimejaa samaki! Hivyo, sababu kubwa iliyonipa msukumo wa kutamani kufika huko hasa lilikuwa ziwa. Jiografia yangu ilionyesha kuwa Wahaya na Wasukuma walichangia ziwa hili. Wakati Wahaya wakiwa Magharibi wakilitumia kwa shughuli zilezile.
Kwa kuzingatia hali yangu ya kutokuwa na kazi wala ujuzi wowote wa kuweza kupata ajira nyingine nililichukulia ziwa hili kuwa mkombozi wangu pekee. Nilitegemea ziwa liniajiri, linilee, kwani taaluma ya uvuvi niliyoipata katika likizo zangu ilitosha kabisa kunipatia ajira hiyo.
Ni kwa mtazamo huo ndipo nilipojikuta nikijiunga na vikundi mbalimbali vya uvuvi kwa lengo la kujipatia fedha. Siku zote za uvuvi wangu nilifuata ziwa kuelekea upande wa kushoto kwangu badala ya upande wa kulia. Kama ningeelekea kushoto, ningelazimika kufika Uganda na baadaye Kenya, kabla ya kuingia Tarime, Musoma, Bunda hadi kufika Mwanza. Ingekuwa safari ndefu isiyo na sababu yoyote.
Mimi nilielekea kulia. Nilivua katika pwani na visiwa mbalimbali kama Bambire, Iroba, Rubondo na Nyamiende. Ilikuwa safari ndefu na ngumu sana. Takribani mwaka mzima uliishia njiani. Ama nilikwamishwa na ukosefu wa majahazi yanayoelekea huko nilikokuwa nikielekea, ama upepo mkali wa siku kadhaa ziwani ulifunga kabisa njia. Msimu wa masika ulioambatana na mvua kubwa za radi na mingurumo ya kutisha ni miongoni mwa sababu nyingine iliyonichelewesha njiani. Nililazimika kusubiri kwa zaidi ya miezi minne katika kijiji fulani huko Biharamulo.
Urefu huo wa safari ulikuwa na faida moja. Kwanza, ulinipa fursa ya kupata ukomavu na uvumilivu mkubwa katika pilikapilika za ziwani na nchi kavu. Ningeweza kuvumilia mvua ya siku mbili au tatu ikinipiga mwilini, niliweza kustahimili jua kali linalochoma kama mkaa wa moto. Niliweza pia kuipuuza njaa kwa muda mrefu. Zaidi, mwili wangu ulijenga uwezo mkubwa wa kuyashinda maradhi madogomadogo kama homa au tumbo bila haja ya kutumia dawa za madukani au mitishamba tele niliyopata kuelekezwa na babu.
Faida nyingine kubwa niliyoipata kutokana na urefu wa safari hiyo ilikuwa udugu. Nilikutana na watu mbalimbali, nikashirikiana nao kwa hili na lile na kujikuta nimepata ndugu na marafiki tele, ambao kila nilipoondoka kuendelea na safari yangu walisikitika sana, lakini haikuwa kabla ya kunitakia kheri na baraka za safari.
Nilikosa raha kiasi pale tulipofika kisiwa cha Kome tukikaribia kabisa Mwanza. Rafiki zangu hao walishauri tubadili mwelekeo na kwenda kwanza Ukerewe. Tulifika Nansio. Tukafanya shughuli zetu za uvuvi hapa na pale, katika kijiji hiki na kile hadi tukajikuta tumeingia katika kisiwa kingine kidogo kiitwacho Ukara.
Ulipata kuona au kusikia juu ya mawe yanayocheza muziki? Kama hujapata hata kusikia mwenzio niliyaona kwa macho yangu katika kisiwa hicho cha Ukara. Kisiwa hicho kina mawe yaliyokaa kiajabu ajabu. Mtu anaweza kufikiria kuwa yalipangwa na binadamu, kwani baadhi yako juu ya mengine, yakiwa yamegusana kwa sehemu ndogo sana lakini hayadondoki si kwa mawimbi wala dhoruba la ziwani. Nilikuwa nikiyakodolea macho mara kwa mara mawe yale hadi mwenzangu mmoja aliposema, “Unashangaa kuyaona yalivyokaa, jee ukiyaona yanacheza?”
Nilidhani ni mzaha. Tulipobishana jamaa hawa walinipeleka katika kijiji cha Kome, ambako tulipata mwenyeji aliyetupeleka eneo la Kululibha yalipo mawe haya ya ajabu. Mwenyeji wetu alitoa amri kwa lugha yake ya Kikara. Mara mawe hayo yakaanza kucheza kama watoto mapacha moja juu ya jingine. Hadi leo sijui ni kitu gani kilichotokea hadi mawe hayo yamtii binadamu.
Lakini huo si muujiza pekee wa Ukara. Pale kijijini kuna kisu chenye makali pande mbili. Unapotokea uhalifu wa aina yoyote watuhumiwa hupelekwa kwa mtaalamu na kuamriwa kukalia kisu hicho. Lakini si kwa mhalifu. Yeye hukatwa mara moja, hata awe amevaa nguo nzito kiasi gani. Kwa yale niliyoyaona, ya mawe kucheza, sikuwa na ubishi wowote kwa jambo hilo.
Maajabu mengine ambayo niliyaona kwa macho yangu, ni mti mmoja kijijini Chilabi huko Ukara. Mti huo ulipigwa na radi ukang’oka. Wenyeji wakaanza kujipanga ili waupasue mbao na kuni. Wakati kabla kazi hiyo haijaanza, mti huo ulisimama na kuota tena palepale ulipokuwa awali. Hata hivyo, haukuwa na majani. Mti huo upo hadi leo. Niliutazama, nikaupapasa. Unaonekana mkavu lakini unaishi.
Maajabu hayo yalifanya tulipoanza tena safari ya Mwanza niwe nimechangamka zaidi.
 

Forum statistics

Threads 1,336,208
Members 512,562
Posts 32,530,658
Top