Riwaya: Chokoraa

Riwaya: Chokoraa

RIWAYA: CHOKORAA
MTUNZI: George Iron Mosenya


SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI

"Nilikwambia..haooo wameanza kupiga simu…ile simulizi yako lazima kwa mwanadamu mwenye nyama aguswe ipasavyo. Huyu aliyepiga simu ni mmoja kati ya wadau wakubwa hapa nchini kwa kuwezesha yatima." Alisema bwana Kasuku huku akinyanyua mabega yake juu.
"Anakuja kesho jioni utamuona. Usimuogope kuwa muwazi. Atakusaidia amini Frida amini kuwa bado unao umuhimu mkubwa sana katika hii jamii. Jiamini kuwa Tanzania inakuhitaji sana." Kasuku alisisitiza.


Frida alijenga tumaini jipya baada ya kusikia kuwa atakutanishwa na muwezeshaji wa yatima na watoto wasiokuwa na makazi.
Muda mwingi Frida alikuwa akizungumza na Kasuku mambo mbalimbali ambayo yalimjenga tena kisaikolojia.
"Frida..hutakiwi kuwa mtu wa kukata tamaa, ni kweli maisha ya mtaani yana kero kubwa lakini jiulize, mfano sasa u mjamzito. Ulitaka kukiua hicho kiumbe bila kosa. Ni upendo gani unao wewe hadi kufikia kuiua damu yako?? Lazima ujifikirie na iwapo ni sahihi basi wasilaumiwe wale waliowatupa watoto wao, asilaumiwe mama aliyekuzaa akiwa gerezani na hata mkuu wa gereza, mkuu wa kituo cha watoto yatima wote wasilaumiwe. Wapo sawa." Maneno haya makali na yenye kuuweka ukweli wazi yalimgusa sana Frida. Sasa akajutia kitendo chake cha kujaribu kujitosa majini ili aweze kufa.
"Hivi ulijifikiria nini na wewe ukajirusha baharini. Ungekufa je?" hatimaye alimuuliza huku akitabasamu, kana kwamba haamini kabisa kuwa inawezekana mwanadamu wa kawaida kujitosa majini kwa ajili ya kumwokoa mtu.
"Ni kiherehere changu tu, naitwa Kasuku napenda kujua mengi hata yasiyonihusu." Alijibu kwa sauti iliyojaa utani. Wakacheka kisha kugonganisha mikono.


Wakati wakifanya hayo, jicho kali sana liliwatazama bila wao kujua kama wametazamwa. Jicho hili likafanya tafsiri ya kuchezewa shere ama kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa. Wivu ukatambaa na kuusulubisha moyo wake wa nyama.
Furaha ya Kasuku na Frida haikumpendeza.
Akakimbilia chumbani, kukiwahi kilio chake kisiweze kusikiwa na wengi.
Akiwa chumbani binti huyu alijikuta akiilaani kazi aliyokuwa anaifanya Kasuku, kazi ya uandishi wa habari. Kwani kazi hii ilimfanya kukutana na wanawake wengi tena wenye mvuto kumshinda yeye.
"Emiliana amka amka umelala.." aliongea maneno hayo huku akijipigapiga kichwa chake. Hakika alikuwa amelala. Analetewa mwanamke nyumbani kwake!!
Hisia potofu zikamtuma kuwa Frida na Kasuku wana mahusiano na wanatumia kigezo cha uandishi wa makala kuficha maovu yao.
Emiliana alikuwa na haki ya kulalamika, alikuwa na haki ya kuwa na wivu. Mara ya kwanza alimkuta Kasuku akiwa anambembeleza yule binti tena akiwa amemlaza mapajani.
Mara ya pili akaenda naye kumfanyia manunuzi ya nguo. Tena nzurinzuri zilizoufanya urembo wake uanze kuonekana. Na zile nywele zenye asili ya kiarabu kwa mbali zikang'ara.
Sasa amewafumania wakicheka kisha wakagonga mikono.
Hata!! Wanafahamiana hawa, tena siku nyingi. Alipitisha jibu hilo binti huyu ambaye ndio kwanza alikuwa anakaribia kufunga ndoa na Kasuku. Mwandishi wa habari na makala katika magazeti.
Leo namweleza kila kitu!!


Ulipofika wakati wa chakula cha mchana, Emmy akiwa analazimisha tabasamu usoni alimwandalia mumewe mtarajiwa chakula chumbani badala ya meza ya kulia kama ilivyo kawaida.
Meza kuu akasalia Frida peke yake. Hilo halikumuumiza kichwa.
Huko chumbani Emmy akautua uchungu wake!!
"Kwa hiyo kuna mawili Kasuku, aidha niondoke ama huyo hawara yako aiache nyumba hii. Msaada uliompatia imetosha. Iam not mtoto mdogo ujue." Alipandisha jazba, Kasuku akaamua kuyatatua haya kwa busara. Alijua yale ni mapenzi tu na si kwamba Emmy ana roho mbaya.
"Ataondoka mpenzi usijali!!" alikubali yaishe.
"Lini?"
"Nimekwambia usijali." Alizungumza kwa hasira kiasi, hakupendezwa na yale maswali ya mahakamani.


Chakula hakikulika tena.
Kasuku aliporejea mezani ili kuzungumza na Frida. Tayari muda wa kumpokea mgeni ulikuwa umefika.
Ni kama alikuwa mzungu mwenye ngozi nyeusi bwana Mathias.
Alifika kwa wakati. Akapokelewa.
Furaha ya Kasuku ikarejea kiasi fulani.
Walifika nyumbani na kuingia moja kwa moja katika mazungumzo.
Walizungumza mengi sana. Mathias Dembele akionekana kuguswa sana na yaliyomtokea Frida.
Kwa kumtazama mbele yake hakuamini kama kweli yule ni chokoraa. Alikuwa amependeza tena kwa hizo siku kadhaa alizoishi kwa Kasuku.
Baadaye Kasuku ili kupata ushauri aliamua kumuelezea Mathiasi juu ya tatizo la mchumba wake.
"Hiyo ni kawaida ya wanawake. Ila anyway usijali, naweza kukusaidia bwana Kasuku. Nitampeleka mahali kama utaniruhusu. Nimeguswa sana." Mathias alitoa kauli ambayo ilimpa ahueni Kasuku.


Wakati wa kuondoka waliandamana na Frida.
Akahakikishiwa kuwa yu katika mikono salama.
Mikono ya Mathias Dembele.


*****


Nyumba kubwa ya kifahari iliyozungushiwa uzio unaodhibitiwa na umeme ilimshangaza mwanadada Frida. Nyumba hizi alizoea kuziona mandhari yake ya nje tu maeneo ya posta na kwingineko Kariakoo.
Baada ya kengele kubonyezwa geti lilifunguliwa.
Gari ikazama ndani!! Injini ikazimwa. Wakashuka.
Kimya kikubwa kilikuwa kimetanda, ndege aina ya kasuku akawapokea kwa shangwe. Mathias akachekelea kuitwa bosi na yule kasuku.
Akamshika kichwa kasuku akajichekesha. Frida naye akacheka.
Maajabu haya ndege anaongea!!
Mlango ulikuwa wazi, akakaribishwa, ndani aliwakuta watu wawili wanaume. Wakatoa tabasamu na kumkaribisha kwa Kiswahili kibovu. Baada ya hapo hakujua linaloendelea maana walikuwa wakiongea lugha ya kigeni.
Frida akawa mgeni katika hili.


Kisha mathias akamvuta kando wakanong'ona kidogo. Mathias akatoweka, Frida akabaki na wenyeji wasioelewa Kiswahili.
Frida akatamani kuwa mtaani alale nje usiku kuliko kuishi mahali pazuri bila kuwa na amani.


*****


Mwanaidi baada ya kuwa amempoteza Frida katika mazingira ya kustaajabisha. Sasa aliikumbuka furaha yake nyingine iliyosahaulika.
Alimkumbuka mama yake George. Ile sura aliyokutana nayo usiku ule ikamkimbiza haikutaka kutoweka katika ubongo wake. Akajiuliza kwa nini iwe hivyo.
Kwa mara nyingine akaamua kurejea katika maeneo yale. Sasa alikuwa anaulizia kwa kila namna aliyoweza.
Kuhusu mama mlemavu hapo hakuambulia kitu.
Lakini mama kichaa, hapa majibu kadhaa yalikuwepo.
"Yule si ndo aliyechukuliwa na Dembele au?" alijibu bwana mmoja kwa njia ya kuwauliza wenzake.
Wote wakakubaliana kuwa ni kweli. Frida akawalipa pesa kwa malipo ya kuuliza na kujibiwa.
Hapo ndiyo Dar es salaam!! Kila kitu ni biashara.
Malipo yaliyofuata ni kupelekwa nyumbani kwa Dembele.
Mwanaidi akapatazama siku hiyo lakini hakuingia nia yake ilikuwa kumfahamu kwanza Dembele.
Alikuwa maarufu haikumchukua muda kumfahamu baada tu ya kupita na gari lake.
Kama ilivyo kawaida yake, hakurupuki anafanya mambo kwa hatua.
Alianza rasmi kuzifuatilia nyendo za Dembele. Hatimaye akapata nafasi ya kuingia kwake kama msichana anayetafuta kazi. Aliingia akiwa anatambua fika kuwa Dembele hayupo nyumbani.
Japo hakupata kazi. Hata huyo mama anayesadikiwa kuchukuliwa na Dembele hakuweza kumuona pia.
Duniani hakuna siri, katika harakati zake za kumfuatilia bwana huyu alizipata habari za juu juu kuwa bwana Mathias ni ‘zungu la unga'. Tetesi hizi zikamkuna. Akahisi kuna jambo.
Hatua iliyofuata ni kuonana moja kwa moja na Mathiasi Dembele, lakini katika njia ya siri sana.
Subira yavuta heri. Siku ikawadia aliyoingoja Mwanaidi.
Mathias Dembele alikuwa analewa na rafiki zake.
Mwanaidi akaivaa fani ya uigizaji, akayaigiza maisha yake halisi ya uchokoraa. Akamvamia Dembele huku akiwa na huzuni, akamlilia sana akalia akiuhitaji msaada wake. Kwa kilio chake hata walevi walishikwa na huruma.
Mathias Dembele akauvaa mkenge.
Akakatisha shughuli ya kujiongezea ulevi kichwani.
Akamchukua Mwanaidi hadi garini.
Akaaga na kuondoka naye. Mwanaidi akaombea mahesabu yake yaende sawa. Alikuwa na ile silaha yake ya kila siku ya kujilinda.
Kisu!!


*****


Suala la Frida kuwa mjamzito na mzigo mkubwa uliokuwepo kwa ajili ya kusafirishwa kuelekea ughaibuni lilimuumiza kichwa Mathiasi. Ni kweli aliguswa sana na maisha aliyopitia Frida lakini baada ya kumweka katika himaya yake ile huruma ikatoweka akawa Mathias yuleyule.
Alijiuliza ni wapi anaweza kupata mtu wa upesiupesi kuubeba mzigo ule. Sasa bahati ikajileta mbele yake.
Akakutana na binti aliyepevuka katika kilabu cha walevi.
Mwanaidi!!
Kwa umbo lake komavu aliamini kuwa anaweza kubeba kete kadhaa za madawa ya kulevya bila wasiwasi.
Kisha hiyo inakuwa safari yake ya mwisho maana akirejea Tanzania atazua tafrani.
Mbebaji aliyeruhusiwa kwenda Tanzania na kurudi alikuwa ni mmoja tu. Mwanamke mnene asiyekuwa na akili timamu. Huyu hata akiachiwa kuingia mitaani bado hataweza kusema lolote.
Nani wa kumuamini?


Mathiasi aliamua kumfikisha Mwanaidi moja kwa moja katika machinjio yake. Nyumba inayomwaga damu za yatima na chokoraa.
Kwa mtazamo wan je alimchukulia Mwanaidi kama chokoraa wengine dhaifu wa kike waliobakwa sana na hatimaye kuwa legelege wanaokubali kusukumwa hovyo.
Akamfikisha katika jumba lile akamkabidhi kwa wale wanaume wasiojua kishwahili vizuri.
Akaagana naye kwa ahadi kama alizompa Frida siku tano zilizopita.


Kisha akatoweka na gari lake akiamini kila kitu kitaenda barabara.
Alipofika nyumbani alipokelewa na magazeti. Akafunua ukurasa wa kasuku.
"MATHIAS DEMBELE: Mwanadamu mmoja kati ya mamilioni ya watu!!" ilikuwa makala ya kumpongeza kwa moyo wake wa kujitolea na kufanikisha ndoto za Yatima wengi.
Mathias akatabasamu.
Wajinga ndio waliwao!!
Alidhihaki!!
Kisha akalala akitegemea kila kitu kitaenda kama alivyopanga.
Mzigo ulitarajiwa kuondoka alfajiri sana!!


***DEMBELE anawatoa kafara watoto kwa faida zake binafsi..sasa amemuweka kikaangoni Mwanaidi. Je ndo mwisho wake?? Je ataonana na Frida? Vipi kuhusu mama mwendawazimu?
***GEORGE NA ISHA NA mimba yao kitajiri nini???


ITAENDELEA!! !!

VAN HEIST muuza ubuyu amina mabata shabani hassani culbby sam II ram BPM mbalu saljar MAVUNO Khantwe
 
Shusha mzigo mwingine tena Casuist kwa ajili ya kupumzikia jioni hii!
 
Last edited by a moderator:
Inavutia, naona mwisho wa dembele umefika
Chezea chokoraaa weye
 
RIWAYA: CHOKORAA
MTUNZI: George Iron Mosenya




SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU




Kwa mtazamo wa nje alimchukulia Mwanaidi kama chokoraa wengine dhaifu wa kike waliobakwa sana na hatimaye kuwa legelege wanaokubali kusukumwa hovyo.
Akamfikisha katika jumba lile akamkabidhi kwa wale wanaume wasiojua kishwahili vizuri.
Akaagana naye kwa ahadi kama alizompa Frida siku tano zilizopita.


Kisha akatoweka na gari lake akiamini kila kitu kitaenda barabara.
Alipofika nyumbani alipokelewa na magazeti. Akafunua ukurasa wa kasuku.
"MATHIAS DEMBELE: Mwanadamu mmoja kati ya mamilioni ya watu!!" ilikuwa makala ya kumpongeza kwa moyo wake wa kujitolea na kufanikisha ndoto za Yatima wengi.
Mathias akatabasamu.
Wajinga ndio waliwao!!
Alidhihaki!!
Kisha akalala akitegemea kila kitu kitaenda kama alivyopanga.
Mzigo ulitarajiwa kuondoka alfajiri sana!!


******


Chokoraa asipoonekana mtaani kwa siku zaidi ya tano. Fikra ambazo huibuka ni aidha amekamatwa na doria ya usiku ama ameamua kuhama kambi kwa sababu zake mwenyewe. Kama alikuwa ni mtumiaji wa mabaya ya kulevya huisiwa kuwa amekamatwa kijiweni. Mara chache sana huisiwa kuwa amekufa.
Licha ya kuwa na maisha magumu. Chokoraa huishi miaka mingi sana. Wakihangaika huku na kule. Hali hii ya kuishi muda mrefu katika maisha yaliyojaa mateso huwafanya waamini kuwa wamesahauliwa na Mungu.
Hali hii iliwakumba pia George na Isha. Baada ya harakati za kumtafuta Frida kugonga mwamba waliamua kuendelea na maisha yao ya upweke.
George akakubaliana na Isha wakasimamisha zoezi la kuitoa mimba ile.
Maisha yakaendelea. Chokoraa akijiandaa kuwa baba mtarajiwa, mwenzake naye akijiandaa kuwa mama.
George alikulia maisha ya kudekezwa sana alipewa kila kitu alichokuwa anakihitaji wakati akiishi katika utumwa bila kujua yu utumwani kwa bwana Emmanuel.
Sasa akili yake ilikuwa imefunguka na mambo mengi kwake yalikuwa mageni. Lakini alikuwa ameyazoea baada ya muda mfupi sana.
Hali ya kuwa baba mtarajiwa ilimuogopesha sana, hakuamini kama aulikuwa wakati muafaka wa kubeba majukumu hayo.
Shilingi mbili alizokuwa akizipata kwa kusota mtaani kufanya kibarua hiki na kile hazikutosheleza kabisa gharama za kwenda kliniki, ama dharula iwapo Isha ataugua.
Siku alipokutana na tangazo linalohusu kuhitajika mwalimu wa somo la hesabu kwa ajili ya masomo ya ziada (Tution). Alivutika na kujihisi kuwa anaweza kuipata nafasi hiyo.
Visenti alivyokuwanavyo alivitumia kununua suruali ya bei chee pamoja na shati. Hakuweza kununua viatu. Akaamua kuvipeleka kwa fundi vile vibovu alivyokuwanavyo.
Utumwa huu wa kuwa chokoraa ulianza kumkinai na kujihisi kuwa hajitendei haki yeye na chokoraa wengine.
Alimini kuwa ni lazima waonyeshe njia huenda na serikali itawasikia.
Siku ya usaili, George alikuwa mmoja wao.
Isha alimsindikiza.
Akabaki chini ya mti wakati mwalimu mmoja baada ya mwingine wakiingia.
Ilipofika zamu ya George wanafunzi walipiga kelele sana. Walikuwa wanamfahamu. Alikuwa muokota makopo tupu na vyuma chakavu. Hata katika uvaaji wake alionyesha kuwa amejilazimisha kuwa vile.
Suruali haikumkaa vyema kiunoni. Na shati lilikuwa kubwa.
George alijua hizo kelele ni juu yake.
Isha naye alijua hilo. Akainama chini, akaomb a dua huku akiwa anajipa matumaini kidogo sana kuwa George anaweza kufanya vizuri. Japo alimuamini vyema linapokuja suala la kutumia busara.
Wanafunzi walipotulia, George alikuwa mbele yao.
Chokoraa anaijaribu bahati yake.
Mapigo ya moyo yalikuwa yanaenda kasi akiwa mbele ya wanafunzi. Walikuwa kimya lakini ilisikika minong'ono.
"Mi sifundishwi na choko aisee." Mwanafunzi mmoja aliyeonekana kutokea familia bora aliyasema hayo huku akijivuta na kutoka nje.
Macho yake yakatazamana na George.
Uliniumba niwe chokoraa, umenipa mzigo huu wa adhabu nimeukubali, ulimuumba mama yangu awe na roho mbaya ya kunitupa yote hayo nimeyabeba, na baba ukamfanya asinithamini bado ninakupenda bwana, ukanitupia katika familia ya kitajiri, bado haukupooza machungu yangu bali kuyaongeza. Najua unanijaribu baba.
Kwani nipo peke yangu baba hadi unipe adhabu nyingine ya aibu mbele ya viumbe hawa wasiokuwa wastahimilivu. Mbona sikuwahi kumdharau mtu katika maisha yangu? Mbona nidharauliwe.
Nitue mzigo huu baba nakiri kuwa, nimeelemewa.
Naamini leo utanitetea!!! George alitumia nusu dakika kuzungumza na Mungu wake.
Alipoyafumbua macho msaili alikuwa akimngoja aanze somo.
"Simameni mmsalimie mwalimu!!" aliamuru msimamizi. Ili kuijenga tena saikolojia ya George ambayo ilikuwa pabaya.
Robo ya darasa walisimama, robo tatu hawakusimama.
Na hata waliosimama, wachache walimaanisha. Wengi wao walikejeli.
George akauma meno kwa nguvu, akaizuia hasira iliyotaka kumtawala.


Akauendea mkebe uliokuwa na chaki za kutosha.
Akatwaa mbili akautazama ubao kisha akawageukia wanafunzi. Akakutana na nyuso zisizokuwa na imani naye, mavazi yao yalikuwa ya kushindana, kila mmoja aliamini amevaa vizuri kuliko mwenzake.
Twisheni zina mambo!!
Somo likaanza kwa sauti ya chini, licha ya kuwa alipendelea kuwa mtunzi wa hadithi lakini bado alikuwa mzuri sana katika somo la hesabu. Na mada aliyopangiwa kuwafundisha wanafunzi wale wa kidato cha nne ilikuwa mada iliyoganda vyema katika kichwa chake.
Matrix!!
George akapandwa na mizuka. Dakika thelathini zikapotea kama upepo.
Alipoambiwa muda umekwisha wanafun zi wakapiga kelele kuwa aendelee. Kelele za sasa hazikuwa na kejeli ndani yake. Zilikuwa kelele za uhitaji.
Ama kwa hakika Mungu hujibu pale unapokiri kuwa unauhitaji msaada wake!!


Japokuwa George aliwashangaza wamiliki wa kituo kile kwa kutokuwa na vyeti. Lakini nani angejali hilo wakati kwa matendo ameonyesha kuwa anaweza.
Kwanza vyeti vya nini wakati ni masomo ya ziada na ni ajira ya muda? Havina maana.
Usiku wa siku hii. Isha na George walikuwa wamekumbatiana katika kajumba kao. Mkeka ukiwatazama. Walikuwa wanalia kilio cha furaha.
George alikuwa amepita katika usaili. Chokoraa alikuwa amepata ajira ya muda.
Usiku huu wenye furaha ya kwanza kabisa kwa chokoraa hawa baada ya muda mrefu kupita.
Chokoraa wengine walikuwa katika kuipigania haki ya chokoraa.


Mwanaidi alikuwa katika kuitetea nafsi yake na kutoka na majibu aliyoyahitaji. Dembele je? Ni kweli anayoyafanya? Mama George je? Yupo hai? Na je? yeye atatoka hapo akiwa hai.
Alipokelewa vyema. Akaishi kwa tahadhari ndani ya chumba hicho cha kifahari alichokaribishwa na watu hawa wasiojua Kiswahili.
Hakuhitaji kunywa chochote kile cha kuandaliwa na watu wale. Kila walipoandaa chakula ama chochote. Mwanaidi aliwasemesha kwa Kiswahili, hawakuelewa. Walipompigia Dembele simu. Mwanaidi alimueleza kuwa ameshiba na hana uhitaji wa chochote.
Hawa wanaume huenda walikuwa makini sana na kazi yao. Lakini kosa moja huzaa goli moja.
Ndo kilichowagharimu wanaume hawa weusi.
Walijisahau kuwa walimuandalia maji ya matunda Mwanaidi.
Baada ya kuyakataa wakasahau palepale mezani.
Mtu mweusi mwingine akajongea mezani akiwa na maji ya machungwa kama ya Mwanaidi, lengo likiwa kumhadaa ili aweze kunywa. Mwanaidi akajikita yupo makini na luninga.
"Me take water drink." Ghafla Mwanaidi, alimwambia yule mtu mweusi kwa kiingereza kisichokuwepo katika ulimwengu huu. Akaeleweka ilhali neon maji limesikika vyema.
Yule bwana akafanya kosa la kukurupuka.
Chokoraa makini kabisa na mwepesi akamwongezea juisi kwa kumimina ile ya kwake ambayo hata hajaionja.
Mtu mweusi alirejea akiwa anatabasamu. Mwanaidi akayapokea maji.
Akayashikilia bila kunywa huku akiendelea kutazama luninga.
Mtu mweusi naye akafanya kuwa hajali kuhusu Mwanaidi. Akaigida juisi yake.
Dakika kumi na tano zilikuwa nyingi sana yule bwana kugeuka mzoga unaopumua.
Hapa sasa Mwanaidi akajipongeza kwa machale yaliyomcheza.
Hasira zikachemka kichwani. Akakitoa kisu chake na kukikamata vyema.
Alijua kuwa yule mwenzake ni lazima tu atarejea muda wowote. Na akimkuta mwenzake katika hali ile lazima achukue hatua mbaya kwa Mwanaidi.
Hapo sasa akajiweka makini maradufu.
Sikio lake likanasa mawimbi ya sauti ya mwanamke akipiga kelele.
Akaanza kufuatilia sauti huku akijiapiza atakayekutana naye aidha afe yeye ama huyo mtu lakini sio kufungwa kamba na kuwekwa mateka.
"Maicon….Maicon…..Maicon"…sauti ya kiume sasa ilipaza ikiita kwa namna ya kuomba msaada. Ilikuwa sauti ile iliyobakia isiyojua Kiswahili.
Mwanaidi akakaza mwendo zaidi. Mara jicho lake likakutana na jambo la kuvutia.
Kisu kikubwa, tena chenye makali. Ukubwa wake ulikaribiana na panga. Akatabasamu akahifadhi kile kisu kidogo akatwaa panga.
Damu nyingi amewahi kumwaga tayari. Hakuna alichoogopa.
Kukurukakara zikazidi kumuweka katika tahadhari kubwa. Mara vikafuata vishindo.
Hapa mwanadada akalikamata jisu lile kwa mikono miwili.
Mara akapigwa kikumbo. Akayumba kidogo kisu kikiwa mkononi. Akataka kumfuata aliyempiga kikumbo lakini akasita yule mtu asiyeongea Kiswahili naye akaonekana akiwa katika mbio.
Hapa haisimuliki ni ujasiri wa namna gani na pia hayaelezeki maumivu aliyoyapata bwana huyu.
Kisu kikapenya katikati ya tumbo lake.
Kwa Mwanaid lilikuwa jambo la kawaida.
Akasonga mbele kwenda kukutana na maajabu mengine.
Damu ikiwa imetapakaa.
Damu kila mahali.
Kisha akamuona mtu. Naye alikuwa anavuja damu vilevile.
Akasita kuingia katika chumba hicho.
Akiwa bado hajajua nini cha kufanya. Sasa alikuwa na kisu chake kidogo, bila kutilia maanani, mshangao ukamtwaa.
Ghafla kisu chini, miguu ikaanza kunyanyuka juu ikilifuata shingo lililokabwa.
Alijaribu kupiga kelele. Sauti haikutoka.
Akafurukuta. Bado hakufanikiwa kukitoa kilichomkaba shingo.
Akazidi kukabwa na uwezo wa kupumua ukizi kwenda likizo.
Hali ya hatari. Mwanaidi akauona mwisho wake ukiwa unakuja kwa kasi.




***Harakati za Mwanaidi katika kikwazo tena…je ndo mwisho wa enzi???
**Chokoraa amepata nafasi ya kuwafundisha watoto wa wadosi na wa masikini wenzake. Je ni nafasi ya kuwatetea watoto wa mitaani???

muuza ubuyu ram
 
Last edited by a moderator:
Hapa hadi kieleweweke mwanaidi, muokoe frida na mama george please
 
Chuma kikoli moto, Casuist leo umekonga nyonyo mwanawane.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Casuist, usidhani tumesahau kaka! Tunasubiri kwa hamu utushushie mizigo miwili kwa leo!
 
Last edited by a moderator:
RIWAYA: CHOKORAA
MTUNZI: George Iron Mosenya




SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE




Mara akapigwa kikumbo. Akayumba kidogo kisu kikiwa mkononi. Akataka kumfuata aliyempiga kikumbo lakini akasita yule mtu asiyeongea Kiswahili naye akaonekana akiwa katika mbio.
Hapa haisimuliki ni ujasiri wa namna gani na pia hayaelezeki maumivu aliyoyapata bwana huyu.
Kisu kikapenya katikati ya tumbo lake.
Kwa Mwanaid lilikuwa jambo la kawaida.
Akasonga mbele kwenda kukutana na maajabu mengine.
Damu ikiwa imetapakaa.
Damu kila mahali.
Kisha akamuona mtu. Naye alikuwa anavuja damu vilevile.
Akasita kuingia katika chumba hicho.
Akiwa bado hajajua nini cha kufanya. Sasa alikuwa na kisu chake kidogo, bila kutilia maanani, mshangao ukamtwaa.
Ghafla kisu chini, miguu ikaanza kunyanyuka juu ikilifuata shingo lililokabwa.
Alijaribu kupiga kelele. Sauti haikutoka.
Akafurukuta. Bado hakufanikiwa kukitoa kilichomkaba shingo.
Akazidi kukabwa na uwezo wa kupumua ukizi kwenda likizo.
Hali ya hatari. Mwanaidi akauona mwisho wake ukiwa unakuja kwa kasi.


Roho ya mwanadamu si nyepesi kupotea, uhangaika sana kabla haijakubali kuuacha mwili. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Mwanaidi. Aliruka huku na huko kujitoa katika ile kabala huku fahamu zikimweleza waziwazi kuwa anaelekea katika kufa.
Katika kujirusha rusha alifanikiwa kugeukia upande mwingine lakini roba ikiwa palepale.
Ilisikitisha lakini hakuupata ule uwezo walau kufanya sala yake ya mwisho.
Kwanza hata angeipata nafasi ile bado asingeweza kuitendea haki. Alijiona mkosaji mwenye dhambi nyingi sana.
Mwanaidi akaukubali kwa shingo upande mwaliko wa Israel yule malaika mtoa roho.
Mwanaidi akatambua kuwa amempata mjanja wake siku hiyo na iwe isiwe lazima afe.
Anakufa bila kutimiza azma yake. Lakini anakufa akiwa amejaribu sana.
Anakufa kijasiri. Japo kifo ni kifo tu.


Wakati anamngojea yule mtoa roho mwenye tamaa achukue kilicho chake kwa wakati anaoutaka yeye. Likatokea tukio la ghafla, Mwanaidi akajikuta yu sakafuni tena kwa kishindo kikubwa sana.
Fahamu zilizoanza kupotea zikarejeshwa na hewa mwanana ya kiyoyozi iliyopenyeza katika pua zake na koromeo.
Jambo lililofuata ni kufufuka kutoka katika wafu. Mwanaidi akayafunua macho yake hakika alikuwa hai.
Mbele yake palikuwa na kioo, jambo la kwanza kuona baada ya kufumbua macho ni kujiona yeye mwenyewe.
Tatizo hakuwa peke yake!
Nyuma yake alikuwepo kiumbe mwingine. Huyu alionekana miguu pekee katika kile kioo.
Mwanaidi akatazama kushoto na kulia, kisu chake kilikuwa kimedondoka mbali naye.
Hakuwa na silaha nyingine. Alitaka kujihami lakini hakujua adui yake ana silaha gani hapo alipo.
Akaamua kutulia!
Dakika mbili zikapita, adui bado alikuwa ametulia bila kusema lolote.
Uvumilivu ukamshinda Mwanaidi akaamua kuvunja ukimya.
"Wewe ni nani?"
hakujibiwa.
Akauliza tena, bado hakujibiwa.
Akajitoa muhanga binti huyu akageuka kukabiliana na adui yake.
Maajabu! Mdomo wazi!Hakuwa adui bali...bali...
Picha ikajengeka katika vichwa viwili wakati huyu akikumbuka siku ya balaa la kukoswakoswa kujeruhiwa na chokoraa wenzake, muhusika mwingine alijikuta katika kumbukumbu asizozitarajia. Aliukumbuka ukaribu wa binti aliyepo mbele yake. Akaikumbuka mara ya mwisho alikuwa yu katika nyumba ya kulala wageni. Akitegemea kukutanishwa na mtoto wake.
Ahadi haikutimia, yakatokea maajabu ndani ya chumba kile,bwana Emanuel akavamia na kufanya mauaji. Tangu alipozimia na tangu alipozinduka sasa mwanamke huyu anamwona Mwanaidi mbele yake.
Mwanaidi yu katika sintofahamu, huyu mama ndiye ama siye?
"Mwanaidi...Mwanaidi..." mara yule mama alianza kusema kwa kurudia rudia jina la Mwanaidi kama anayejaribu kukumbuka kitu.
"Mama!" Mwanaidi alijikaza akajibu.


Yule mwanamke akaanza kumsogelea aweze kumkumbatia.
Hapa sasa Mwanaidi na ushujaa wake hakuna kitu alikuwa anahofia katika maisha yake kama ushirikina na mauzauza.
Hivi mizimu huwa inakuwa hivi? Alijiuliza huku akitetemeka. Kile kiwiliwili kikaendelea kumsogelea.
Alitamani kukimbia lakini miguu ikawa mizito. Mara akajikuta katika mikono ya yule mama aliyeaminika kuwa mama yake George.
Joto la upendo likapenya, Mwanaidi akaupoteza uoga wake! Akamkumbatia yule mama.
Mzimu uliokuwa unamsumbua siku zote sasa ulikuwa mbele yake. Mama George alikuwa na Mwanaidi.
Sasa aliweza kutembea mwenyewe, yale masharti aliyoshindwa kuyatekeleza bwana Emmanuel yakawa faida kwa mama huyu aliyekuwa amefungwa kwa muda mrefu. Ile miguu iliyopooza kwa roho mbaya ya bwana Emanuel, roho ya tamaa ya utajiri sasa ilikuwa thabiti.
Aliweza kusimama tena. Alikuwa mzima.


Kifo cha Mwanasheria Kindo mbele yake kilimvuruga kabisa, aliporejewa fahamu hakuwa sawasawa. Sasa alikuwa timamu na alimtambua Mwanaidi. Lakini hakuweza kuongea sana.


Walipoachana mama huyu alifunua tumbo lake, Mwanaidi akapatwa na msisimko wa ajabu ambao hajawahi kuupata hapo kabla.
Alisisimka kwa kile alichokiona. Mishono isiyokuwa ya kitaalamu sana na vidonda vibichi katika tumbo la yule mama. Mwanaidi akahisi kwa mbali joto. Kisha jasho likachuruzika, katika mfereji wa uti wa mgongo wake.
Alikuwa amesisimka. Yule mama hakusema neno lolote lakini alijiumauma kama anayelalamika na kulaani.
Mwanaidi akatoa chozi.
Zile soga zilizozagaa mtaani kuwa bwana huyu anajihusisha na madawa ya kulevya sasa zikaanza kuwa katika vitendo, mwanaidi hakuwa na utaalamu lakini mambo haya amewahi kuyasikia mtaani.
Mama huyu ambaye aliitwa mwendawazimu alikuwa akitumikishwa na Dembele katika biashara yake.
Biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Inakera!! Inaumiza.


Mwanaidi alikuwa amezizima kwa hofu na msisimko.
Alimwona mama huyu kama ambaye muda wowote ule anaweza kuupoteza uhai.
Mama alizidi kulalamika katika sauti za chini, sasa alionyesha mkono wake kuelekea katika chumba kimoja. Mwanaidi hakuelewa ana maana gani hadi yule mama akiwa bado hajafunika tumbo alipomshika mkono na kumvuta kuelekea anapomaanisha. Wakakifikia chumba, mama akakifungua Mwanaidi akakutana na mshangao mwingine lakini huu haukudumu sana akakumbuka kuwa yupo eneo hatarishi.
Akazivamia kamba na kuzifungua, hazikuwa zimekazwa sana.
Frida Gereza chokoraa aliyezaliwa gerezani akawa huru.
Mwanaidi akajipongeza kimyakimya kuwa ameua ndege wawili kwa jiwe moja.
Honi ya gari ikasikika nje. ikawashtua!!
Ikaendelea kupigwa kwa fujo. Wote wakabaki katika bumbuwazi.


****


WIVU WA MAPENZI huteketeza nafsi nyingi chini ya jua. Wivu huja ukipata wasiwasi juu ya mwenzako. Mbaya zaidi moyo wako ukiwa unampenda kwa dhati.
Kila anapoenda unahisi anakusaliti. Kila akipigiwa simu unahisi hawala amempigia. Hata akitabasamu baada ya kusoma ujumbe katika simu unahisi ametumiwa na mwanamke wan je.
Tena akirejea nyumbani huku ana hasira, ndio mbaya kabisa unaweza kuamini kuwa yule msaidizi wake wa kazi amemkasirisha baada ya kumkatalia penzi.


Hali hii ilikuwa inampeleka puta mwanadada aliyelala katika kitanda cha futi tano kwa sita alichoamini kuwa ni kikubwa kumzidi.
Usingizi uligoma kabisa kumchukua tangu mume wake mtarajiwa amuage kuwa amepata dharula kuna mahali anakwenda.
Hofu yake kuu ilikuwa kauli ya mume wake huyo kuwa anampenda sana msichana fulani aliyeishi nao kwa siku kadhaa.
Wivu ukampiga kikumbo akayumba.
Hali ya hewa ya jijini Dar es salaam siku hiyo ilikuwa ya ubaridi.
Akashtuka !!
Akahisi vibaya kuwa mume wake huyo amekwenda kulitafuta joto mahali.


Akafanya tabasamu la karaha kisha akasimama. Akiwa na nguo zake hizo hizo za kulalia. Akajitazama katika kioo baada ya kuwasha taa, alikuwa mwekundu sana.
Hasira !!
Akatembea hadi nje. Akawaza kwenda kufumania.
Akajipa uhakika kuwa anapotegemea kuwa mume wake yupo basi atakuwa hapohapo.
Hivi hanijui huyu mwanaume eeh!! leo atanikoma na hicho kisichana chake.
Akaliendea gari lililoachwa na mumewe. Akatazama lilikuwa na mafuta ya kutosha.
Akawasha injini akatoweka kwa makini kabisa huku akijipongeza kwa uamuzi wa kumfuatilia Kasuku ambaye alikuwa akimfuatilia Dembele siku aliyomwondoa Frida na kumkabidhi kwa Dembele.
Kasuku hakutegemea kama mke wake alimfuatilia siku ile lakini ilikuwa hivyo na sasa mke anafurahia matunda.
Aliamini kuwa Kasuku alikuwa ameenda kukutana na Frida.
Huyu mwanamke anayepelekeshwa na wivu alikuwa ni Emiliana mke mtarajiwa wa bwana Kasuku.


Alifika katika nyumba ile majira ya saa tisa usiku.
Akiwa amepagawa kabisa alibonyeza kengele baada ya kupiga honi bila kufunguliwa. Bila kujali bughudha anazowaletea wamiliki wa nyumba ile.
Mapenzi bana!! Acha yaitwe mapenzi. Hayo hakujali.


Alibonyeza mara kadhaa bila kujibiwa.
Wakati akihangaika kubofya ile kengele, viumbe wawili walikuwa katika hofu huku yule wa tatu akiwa hajui lolote.
Frida na mwanaidi walikuwa wametaharuki.
"Ni yeye amekuja huyo." Frida alimwambia Mwanaidi huku akitetemeka.
Mwanaidi akamtazama mama George aliyekuwa anacheka bila sababu. Akakutanisha macho na lile tumbo lililoshonwa hovyohovyo.
Damu ikachemka. Akatazama nyuma yake akakutana na ule mwili aliousulubu kwa kisu kikali.
Akauendea akiwa amepandwa na mizimu asiyoijua asili yake akachomoa kile kisu.
Frida akapiga kelele ya hofu.
Mwanaidi akaondoka bila kuaga mtu.
"Mwanaidi…Mwana…." Aliita kwa kunong'ona Frida. Mwanaidi hakugeuka.
Akapiga hatua hadi akalifikia geti lililokuwa linagongwa.
Uoga ukamshika lakini hakusita. Aliamini mpinzani wake hakuwa amejiandaa kikamilifu na kamwe asingetegemea pigo kama lile kukumbana naye.
Mwanaidi akalitazama geti akashika kitasa bila kuuliza lolote akafungua.
Kiwiliwili kilichojaa shari kikaingia kichwa kichwa.
Mwanaidi asiyekuwa na akili zake timamu akatii kiu yake. Akaamini kuwa aliyempa mgongo na Dembele.
Kisu chenye urefu wa mita kadhaa kikazama katika mgongo huu laini. Kikatoka kilio kikali cha mwanamke. Kisha kikatua chini.
Wivu ukawa umemponza Emiliana na sasa alikuwa katika kuipigania roho yake pasipo mafanikio.
Mwanaidi akashtuka lakini hakutaka kujua yule ni nani akamuwahi ili asipige kelele nyingi. Akamziba mdomo.
Baada ya dakika chache akasimama. Hakutaka kufuatilia iwapo amepoteza fahamu ama amekufa.
Roho ya paka ilikuwa imemkaa kifuani.
Upesi akaingia ndani, ile hali ya kuliona geti wazi ikampa wazimu.
Baada ya dakika tano. Majira ya usiku mnene unaoikaribia alfajiri.
Mwanaidi, mama George na Frida walikuwa katika jitihada ya kutokomea kuelekea popote pale wanapojua wao.


Taharuki ilimkumba bwana Dembele Mathias, geti lilikuwa wazi na gari la mwandishi mpekunuzi wa mambo lilikuwa limeegeshwa kwa nje.
Gari la bwana Kasuku.
Ilikuwa saa kumi na moja alfajiri.
Mshenzi amenigundua!! Aliwaza Dembele.
Akarejea katika gari lake akarejea na pilipili ya kupulizia na dawa ya usingizi.
Aliamini kwa kumkabili kwake bwana Kasuku huu utakuwa ushindi mkubwa kwake kuukwepa mkono wa sheria lakini vinginevyo alikuwa anatakiwa kujiandaa kusoma makala mbaya zaidi kati ya zote ambazo amewahi kusoma. Makala itakayomvua nguo na kumwacha uchi.
Aliingia ndani huku akihemea juu juu. Kile kitambi kikaanza kuwa mzigo mzito.
Ile anaanza tu kuingia ndani akakutana na mwili ukiwa umetulia sakafuni. Mwili wa mwanamke. Akausukuma kwa mguu, ulikuwa mzito sana.
Akatamani kukimbia lakini hiyo haikuwa njia ya kulikimbia tatizo.
Akasonga mbele hadi akaifikia sebule. Hapa akamkuta msaidizi wake mweuzi asiyejua Kiswahili akiwa amelala fofofo.
Akamtandika kofi hakutetereka wala hakulalamika.
Akaachana naye.
Hatua kadhaa mbele akakutana na maiti nyingine. Na damu zikiwa zimetapakaa.
Hapa sasa shinikizo la damu likaanza kupanda.
Ujasiri ukakosa nafasi.
Akalainika. Akasalimiana na sakafu.
Cha kuchekesha alidhani kuwa atapoteza fahamu kisha aibuke kutoka ndotoni. La alibaki akiwa anaona kinachoendelea. Hakuwa ndotoni.
Dembele matatani!!


****


George Emmanuel alishangazwa na jinsi darasa lilivyojaa likimsubiri kwa ajili ya kuwafundisha. Alipoingia kila mmoja alisimama na kumsalimia kwa heshima zote.
Katika msafara wa mamba hata kenge hujiweka humo bila kujulikana. Ndivyo ilivyokuwa pale sauti ya mwanafunzi mmoja ilipomsalimia kwa kesema ‘Shkamoo mwalimu Choko'
Ubaya wa wanafunzi huwa ni wagumu kumtaja anayekuwa amefanya kosa fulani hata kama wanamfahamu fika. Hata huyu hakutajwa.
"Popote ulipo uliyediriki kuniita mimi hivyo, endelea kuniita hivyo sana kabla Mungu hajauchukua uhai wa wazazi wako. Jisifu sana, lakini ujue kuwa si mimi wala wewe anayeyapanga haya"
Neno likamfikia mlengwa akainama kwa aibu. Hatia ikaanza kuishi naye.
George hakujali!!
Kabla ya kuanza kufundisha alifanya sala fupi kisha akaukabili ubao.
Hali ilikuwa zaidi ya awali.
Alipotoka darasani wanafunzi wakamzunguka. Kila mmoja alitaka huduma zake kwa malipo.
George aliwa na shida na pesa hakukataa hata ofa moja.
Baada ya wiki mbili alikuwa katika mabadiliko.
Siku waalimu walipopewa pesa yao ya awali ‘advance'. George akawa na pesa inayohesabika na kushikika walau.


Ni nani haupendi umeme. Nani asiyependa kuishi katika nyumba yenye uhai kidogo wa kuitwa nyumba.
Hata chokoraa pia alihitaji hivi vitu.
George akiwa na Isha walihama katika nyumba ile , wakahamia nyumba yenye umeme.
Historia ya kulalia mkeka ikafutika. Ukabaki kuwa kwa ajili ya kukalia na kulia chakula. Godoro ndani ya nyumba.
Tabasamu likachukua nafasi.


****


Kichwa kilikuwa kinamuuma sana Kasuku. Kifo cha mpenzi wake na mkewe mtarajiwa kilikuwa kimemchanganya sana.
Gari lilikutwa limeegeshwa katika hoteli, mwili wa marehemu ukakutwa katika mtaro mkubwa ukiwa na mpini wa kisu uliozama ipasavyo katika mgongo wake.
Kifo hiki sio kwamba kiliishia kumsisimua na kumuumiza Kasuku lakini kilimtia wazimu kabisa.
Alijiuliza maswali mengi. Hakupata jawabu.
Huzuni!! Huzuni ikawa rafiki yake.
Akachukua likizo isiyokuwa na malipo aweze kuipumzisha akili yake.


***WIVU unaua??wivu umemuua EMILIANA.
***MWANAIDI anaokoka katika kifo kisha anawaokoa wenzake kutoka katika mikono mibaya. Harakati za ukombozi wa chokoraa zinamfanya aue…hilo hajali.
***KASUKU…..je atagundua chanzo cha mkewe kuuwawa.
****DEMBELE hajua Frida na mama George wametoweka vipi?? Je atakuwa na amani??
***MAMA GEORGE AKIKUTANA NA GEORGE WAKE AMBAYE SASA NI MWALIMU…ITAKUWAJE????


ITAENDELEA


muuza ubuyu ram culbby mbalu BPM
 
Last edited by a moderator:
Asante sana Mkuu duu!!! naiona saa ya ukombozi wa chokoraa....twende kazi Casuist
 
Last edited by a moderator:
Asante sana! Usisahau kutupia kitu kingine kabla ya mchana wa leo haujaisha!
 
Mimi nimeji subscribed tu nangoja iishe nianze kuisoma sitaki presha za kukimbizana na Casuist
 
Last edited by a moderator:
Mie siwezi kusubiri aisee, nitabanana hapa hapa Casuist
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom