RIWAYA: CHOKORAA
MTUNZI: George Iron Mosenya
SEHEMU YA KUMI NA SABA
Mwanaume anasita kwa muda anafanya tafakari. Tamaa inazidi nguvu maamuzi. Anamkumbatia yule msichana aliyekondeana.
Bonge kuna UKIMWI
kuna kisonono, kuna fangasi
Bonge
Bonge!! Shauri zako. Sauti ilimwambia katika nafsi yake. Akatamani kuacha lakini alikuwa amtamanika tayari!! Angefanya nini.
Akaitawanya kanga ya yule binti. Akaanguka naye chini. Badala ya kutua chini wakatua katika kitu kingine. Kikaunguruma.
Wakatulia. Bonge suruali magotini, binti kanga pembeni.
Kikaunguruma tena.
Hapa sasa Bonge akawa mwanariadha mzuri, huku Isha akimfuatia kwa kasi.
Walienda pande mbili tofauti.
Dada mkubwa Regina naye alishtushwa na hali hii. Chokoraa hana ngojangoja. Naye akatimua mbio.
Walifurahisha kuwatazama.
Bonge hakugeuka nyuma, japo zilikuwa njia za kubumba lakini aliweza kufika katika handaki bila kukosea. Alikuwa anathema juu juu, wakati wa kuondoka hakuaga mtu lakini mwanasoka huyu wa zamani baada ya matatizo haya sasa anamkurupua Kelvin.
Anamtoa nje ya handaki na kumsimulia mkasa wote. Hapa akiwa ameikamata vyema suruali yake kiunoni isiweze kudondoka. Miguuni palikuwa patupu, viatu vyake alivisahau maksudi kutokana na kashkash aliyokumbana nayo huko alipotoka. NDIYO, asingeweza kujiuliza mara mbilimbili iwapo achukue kwanza viatu ama atimue mbio kuokoa uhai wake.
Kelvin alikuwa akicheka tangu simulizi ile inaanza kuhadithiwa. Hadi Bonge alipoweka kituo cha mwisho. Hapakuwa na la kushauriana zaidi ya kungoja asubuhi waende kutazama kulikoni.
Wakarejea ndani ya handaki waweze kulala tena.
Baada ya dakika chache walikuwa wanakoroma.
Wakati chokoraa hawa wanakoroma na kuota ndoto mbalimbali za utajiri siku za usoni, kuna watu walikuwa wanaamka na kuingia katika shughuli zao. Na wengine hawakuwa wamelala kabisa.
*****
Huyu alitamani kulala lakini usingizi ulizidiwa nguvu na maumivu ya ajabu aliyokuwa anayapata katika sehemu zake za siri. Alikuwa anajikuna kwa jitihada zote lakini bado hali ilikuwa tete.
Akaanza kutetemeka, alitokwa machozi hakuwepo wa kuyafuta. Alikuwa peke yake nje ya chumba cha hospitali ya Mwananyamala jijini Dar. Hapakuwa na dalili yoyote ya kuhudumiwa. Kwani yeye nani?
Wamelia wanawake wengi miaka nenda rudi. Yeye kilio chake kina tofauti gani?
Mbaya zaidi hana pesa. Ilimuumiza.
Muwasho ulizidi kukua na kusambaa. Mwili nao ukashikwa ganzi.
Ni kama alikuwa anaumwa uchungu.
Hali hii ya kuwashwa kwa siku hii ilikuwa imezidi siku mbili zilizopita alipoanza kuwashwa akiwa katika chumba cha mahabusu akingoja kesi yake kuanza kusikilizwa.
Hakuwahi kuyajua magonjwa ya zinaa zaidi ya kusikia mara moja moja katika vyombo vya habari na kwa kutumia elimu yake ndogo ya shule ya msingi.
Sasa alikuwa anadhani ni muwasho wa kawaida, lakini muwasho huu sasa unamtesa.
Umefanya ngono lini? Na nani? daktari alimuuliza.
Sikumbuki.. alijibu huku akitetemeka kwa uchungu unaomkabiri.
Daktari akakerwa na jibu hilo akamtupia tusi la nguoni, akimtukania ukoo wake mzima.
Binti hakusema lolote.
Daktari aliendelea na yake baada ya kuwa amemchukua vipimo na kupata majibu kuwa binti huyu alikuwa na kisonono kilichokomaa ndani kwa ndani kutokana na kukosa tiba ya upesi.
Dawa kwa ajili ya kisonono kilichokomaa ilikuwa inagharimu pesa ambayo kwa namna yoyote yule binti asingeweza kuipata kwa wakati ule.
Mwanaidi nakupatia dawa ya kutuliza muwasho kwa masaa. Nenda ukatafute pesa kwa ajili ya dawa. Msaada wangu wa mwisho umekuwa huo mdogo wangu. Hakikisha unaipata hiyo pesa vinginevyo hautaweza kutibika tena ugonjwa huo Daktari alijieleza kwa utulivu. Mwanaidi akatikisa kichwa kukubali. Alikuwa ana hofu!!
Daktari akaandika madawa kasha akamsogelea na kunongona, Ukipona mwambie awe anatumia kinga
.
Mwanaidi akakubali yaishe!! Hakujua hata huyo mtu anayezungumziwa ni nani. Je ni yule askari aliyembaka siku mbili zilizopita wakiwa rumande ama ni yule mwanaume aliyelala naye kabla ya kutiwa mikononi mwa polisi.
Akapatiwa dawa na kuimeza pale pale.
Unaishi wapi. Daktari huyu aliyekuwa na matusi alimuuliza.
Magomeni Mikumi. Alijibu huku akijua kuwa anaishi mitaani katika jamii yake ya chokoraa.
Daktari akampatia shilingi elfu mbili. Akaondoka na kujituliza nje katika viti.
Dawa ikafanya kazi, muwasho ukapungua hatimaye ukapoa.
Mwanaidi akatoweka. Akaenda katika mtaa aliouzoea akajichanganya hapa na pale akapata mahali akajilaza.
Saa kumi na moja alfajiri alikuwa macho tayari. Wima anajiuliza aanzie wapi, kuitafuta pesa ya madawa.
Kama ilivyokuwa ngumu kupata jibu la aanzie wapi kuipata pesa. Ndivyo ilivyokuwa ngumu kwa upande wa pili.
Isha naye alikuwa wima akijiuliza arejee kuifuata kanga yake aliyoisahau kule chemba alipotakiwa kubakwa, ama atimue mbio kuelekea atakapojua yeye.
Kutimua mbio halikuwa jibu la swali lake. Akaamua kumuamsha Frida.
Wakajikongoja pembeni ambapo hawakuweza kusikiwa na mtu. Isha akahadithia kilichotokea.
Frida alikuwa na asili ya uoga. Hakukubaliana na suala la kurejea tena kule katika chemba kutazama nini kilichokoroma na kuwashtua wawili hawa.
Hapa tuondoke mwenzangu
bora hata posta. Frida alishauri.
Saa kumi na mbili hawakuwa eneo lile.
*****
Upande wa Mwanaidi naye alikuwa amepata jawabu baada ya kujizungusha hapa na pale, jua likachomoza, akatafuta kibanda cha hadhi ya chini kabisa cha mama ntilie, akaingia kuitibu njaa yake. Kasha akapanda gari.
Safari ya kwenda nyumbani kwa Emma ambaye alikuwa mikononi mwa polisi. Nia ya Mwanaidi ilikuwa kuonana na yule mama.
Aliamini anaweza kupata msaada. Walau wa pesa ndogo.
Alifika akiwa na tumaini kubwa sana la kuitatua shida yake tena huenda ni zaidi ya hapo anapofikiri.
Aliamini huruma ya yule mama hasahasa baada ya kuujua ukweli itakuwa juu yake na atamsaidia maradufu.
Imetamkwa kuwa baada ya dhiki ni faraja lakini kwa Mwanaidi dhiki moja inapanda juu ya dhiki mwingine na kuzua dhiki maradufu.
Mama Emma na familia yake hawakuwepo, nyumba ilikuwa kama haijawahi kukaliwa na watu.
Geti lilikuwa limefungwa.
Mwanaidi akajikongoja kichwa chini mikono nyuma. Akarejea katika kituo cha mabasi alichotoka.
Akapanda basi bila kujua atashuka kituo gani.
Maskini, hakuwa na kwao msichana huyu!!
Kipati!! Wakushuka Kipati!! kondakta akapiga kelele. Mwanaidi akakurupuka kutoka katika mawazo yake. Akasema ashushwe!!
Kondakta akatii akamshusha!!
Kwanza hakuwahi kutegemea kuwa ipo siku atarejea katika kituo alichowahi kufukuzwa kwa kufanyiwa njama. Lakini sasa anarejea kutokana na shida inayomkabili.
Anarejea katika kituo cha watoto yatima. Alipolitazama geti la kuingilia akaanza kumkumbuka rafiki yake mpenzi Farida!!
Akayakumbuka mabaya aliyotendewa na mkuu wa kituo. Alivyobakwa kwa ahadi kwamba ataishi kituoni milele.
Mawazo yake yakakatishwa na honi kubwa ya gari.
Alipotazama pembeni kina sura ilikuwa inatabasamu. Sura hii ilizibwa na miwani nyeusi ya jua.
Miwani ilipotolewa.
Mkuu wa kituo akaonekana.
Mwanaidi akamsalimia kwa heshima ya uoga. Moyoni alimchukia.
Akajieleza kwa ufupi kuwa alikuwa anamtafuta yeye.
Akaamuriwa kupanda ndani ya gari. Akapanda gari likatoweka.
Mbagala Kuu, Kijichi. Nje ya jiji la Dar es salaam huku ndipo gari lilisimama.
Wakashuka na kuingia katika nyumba ambayo ilikuwa mpya kabisa.
Nyumba yangu hii
nimemaliza kuijenga mwezi uliopita naishi mwenyewe
.vipi nzuri eeh! alizungumza kwa ,majivuno Mwanaidi akamuunga mkono. Moyoni akilaani sana jinsi watu hawa wanavyotumia misaada inayotumwa kwa yatima kujinufaisha.
Hata kabla Mwanaidi ajajieleza shida yake tayari yule bwana mwenye tama akaanza kumgusa. Mara amtoe uchafu katika nywele mara amfute shavuni.
Ni kweli Mwanaidi alikuwa anavutia. Hakuwa amekaa rumande siku nyingi. Bado alikuwa Mwanaidi yuleyule. Lakini huyu bwana aliwahi sana kuonyesha tamaa kwa yatima huyu.
Mwanaidi mwenye shida alikuwa annakubali kila jambo lakini moja tu alilojiwekea moyoni ni kwamba. Udhalilishwaji wa Frida ulikuwa unatosha sana. Kwake itakuwa uzembe kudhalilishwa.
Bwana mpenda sifa akajitapa zaidi ili kumvuta Mwanaidi. Akaonyesha pesa zake nyingi. Mwana akajichekesha.
Akajifanya naye ni mwepesi kama wasichana wa mjini mbele ya pesa.
Chumba kikawapokea kwa furaha. Mashuka meupe yakachukia kuvurugwa na viumbe hawa.
Bwana matamaa, akawasha kiyoyozi. Kasha akasaula nguo zake moja baada ya nyingine.
Mwanaidi akamtazama huku mengi yakipita kichwani mwake.
Nani atajua huenda alikuwa anamchagulia aina ya kifo ambacho kitamfaa
.au
au
.hakika ilikuwa hivyo.
Papara za dakika mbili tu zilitosha kuyafanya mashuka yashangae kulikoni huyu bwana amaebaki peke yake kitandani halafu hata hachezichezi. Mashuka yakakosa jawabu.
Alipoanza kuharibika tena mashuka yakajiuliza kulikoni?
Hapakuwa na jibu, lakini safari hii swali lao lilipata jibu.
Mkuu wa kituo cha watoto yatima anagundulika kuaga dunia baada ya kugandamizwa na mto wa kulalia na kukosa pumzi hadi umauti ulipomkuta.
Marehemu alikuwa mtu wa watu!, alikuwa mkarimu, mwenye upendo, aliyejitolea kwa ajili ya yatima na wasiojiweza. Mungu amlaze pema pepeoni.
Wasiojua maovu yake wakajibu Amin!.
*****
Viwiliwili viwili vya vilikuwa vinafuatilia tukio moja katika nyakati na umbali tofauti.
Kiwiliwili cha kiume kilikuwa kinanyata huku kikishangaa ili kupata uhakika kama kinachoshuhudia ni sahihi ama la.
Kile cha kike kilikuwa kimepata uhakika kabisa na jambo lile.
Kikatimua mbio na kumsimamisha mwanamke wa makamo aliyekuwa katika mizunguko yake isiyokuwa na uelekeo rasmi.
Kanga yangu hii umeitoa wapi. Aliuliza kwa shari huku akiwa na furushi lake la chupa tupu za plastiki.
Mwanamke badala ya kujibu alitoa tabasamu. Kasha kicheko.
Huyu vipi? Hivi viatu vyangu ujue. sauti ya kiume iliuliza katika kuhamaki na kushangaa.
Kanga yangu hii
namwam
.. alishindwa kuendelea kuzungumza akamtazama mwanaume aliyekondeana. Mabega juu kama mgonjwa wa Ukimwi.
Mwanaume akadondosha zigo lake la machuma.
Isha!! aliita.
Msichana akazidi kuduwaa, alikuwa hajapata uhakika kama yule ndiye ama siye.
Alipomuita jina akaamini alikuwa ni George.
George mkombozi wa yatima na chokoraa.
George ambaye sasa anaitwa Bonge!!
Mwanamke waliyemshutumu kuwa ana vitu vyao alikuwa anawatazama kama anayeyafuatilia maongezi yao na kuyapenda.
Mara akawasogelea. Isha akajisogeza kwa George, mwanamke akazidi kuwasogelea huku akicheka.
Mara akawakamata nguo zao.
Wakachomoka. Akaokota mawe!!
Riadha mpya ikaanza tena.
Ni katika namna yao ya kukimbia kila mmoja akauvuta ule usiku. Usiku wa ubakaji.
Ubakaji ulioingiliwa na kukoroma.
Wakakimbia. Sasa ni mchana wanakimbia tena.
Wanamkimbia mwanamke wanayeweza kumuona sasa.
Kila mmoja anajiuliza iwapo ni kweli juu ya kuwa kwao pamoja usiku ule.
Hakuna mwenye jibu. Mbio zikaendelea kumkimbia mwanamke mwenye mawe aliyedhaniwa kuwa ni mwendawazimu.
****ISHA na BONGE
.ana kwa ana
kumbuka BONGE alitaka kumbaka ISHA
..je watatazamana kweli???
***MWANAIDI amemuondoa duniani mkuu wa kituo
bila shaka alichukua pesa
.je nini kitaendelea katika riwaya hii
..
ITAENDELEA
VAN HEIST muuza ubuyu amina mabata shabani hassani culbby sam II ram BPM mbalu saljar MAVUNO