Riwaya: Chokoraa

Riwaya: Chokoraa

casuist riwaya bado inaendelea au ndo imefika tamati?
 
SEHEMU YA 12
RIWAYA: CHOKORAA
MTUNZI: George Iron Mosenya


SEHEMU YA KUMI NA MBILI



Frida na Isha walisikilizwa na daktari, wakafanyiwa vipimo kisha wakapatiwa dawa za bei ya kawaida. Wakatoweka.
Wakati wanatoka hospitali walipishana na mtu ambaye alisababisha Frida na Mwanaidi wote watazamane na kugundua kuwa wameona kitu cha kufanana. Mwanaidi aliukunja uso wake kwa hasira.
"Mungu atatulipia.." Alisema Frida. Mwanaidi hakutaka kukubaliana na hilo ombi.
Roho mbaya ikamuingia. Roho isiyokuwa na uoga.
Akaitamani tena roho ya mwanadamu!!
Hyu alikuwa ni mkuu wa kituo cha kulea yatima kule Mbagala. Aliyemnyanyasa Frida kisha akamtelekeza akiwa na mimba.
Sasa anaingizwa hospitali. Wawili hawa wanamuona.
Frida anaweka ubinadamu mbele.
Mwanaidi anauvaa unyama!!!
Hawashirikishi lolote akina Isha na Frida lakini anawaza juu ya kumuadabisha yule mwanaume asiyekuwa na utu.


Baada ya kutoka pale hospitali. Frida alimpigia simu George ambaye alikuwa amejiweka tayari akiisubiri simu hiyo!
Wakapanga wakutane mchana wa siku hiyo. Akiwa na rafiki zake wawili.
Ni mkutaniko huu ulioharibu mipango ya Mwanaidi kumuadabisha yule mkuu wa kituo cha watoto yatima. Lakini moyoni alijipa ahadi kuwa atamsaka hadi ampate na kumtimizia anachostahili.


George alikuwa muongeaji mkuu katika mkutaniko huu. Frida, Isha na Mwanaidi wakiwa wasikilizaji.
Sauti ya utulivu ya kijana George pekee ilileta faraja na kuangusha ngome za majonzi kwa muda. Kila nukta aliyoweka, ilistahili kuwekwa. Na alivuta pumzi kisha akaendelea tena kuzungumza.
George aliwatamkia wazi kuwa anawahitaji katika harakati zake za kumtetea yatima mwenzake anayeteseka mtaani. Aliamini kuwa kwa kuwa na watatu wale ambao wanaujua mtaa vyema anaweza kuzianzisha harakati zake.
Hapakuwa na maswali zaidi. George akawapakia katika gari lake. Wakaanzia katika maduka ya nguo. Hapa kila mmoja akajichagulia nguo anayodhani inampendeza.
Wakarejea garini. Likafuata suala la kutafuta nyumba ya kuishi. Hili nalo halikuwa tatizo. Nyumba ikapatikana maeneo ya Magomeni Mikumi. George akalipia vyumba viwili.
Siku hiyo hawakuhamia katika nyumba ile, walilala nyumba za kulipia tena. Siku iliyofuata walikutana tena na George,
Kwa siku hii, hata kama una elimu ya kiwango cha uprofesa usingeweza kubashiri kuwa watatu hawa wanaonata katika barabara walikuwa yatima, tena walioishi maisha ya kichokoraa.
Frida hakuwa amerejewa afya yake vyema, japo alipendeza Mwanaidi aling'ara kupita wote. Kwa mara ya kwanza wakatokwa na tabasamu la moja kwa moja kutoka mioyoni mwao.
Wakakutana eneo la Best Bite, mazungumzo yakasindikizwa na chakula. Kisha wakatoweka tena. Siku hii vitu vya msingi vinavyofaa kuwa ndani ya nyumba vilinunuliwa. Kitanda, godoro, vyombo, mashuka na vingine vingi bila kusahau burudani ya muziki. Nyumba ikapendeza. Frida akaangua kilio kikubwa kwa ukarimu huu wa kijana huyu wa maajabu!!
Kilio cha Frida kikaungwa mkono na Mwanaidi kisha Isha, George naye akashindwa kujizuia.
Watatu hawa wakakumbatiana huku wakilia sana. Machozi ya yatima yakaifungua rasmi nyumba hii!!


Ndani ya mwezi mmoja, ile picha ambayo Frida, Mwanaidi ama Isha ambayo angepiga akiwa chokoraa isingefanana hata kidogo na hii ya sasa. Walikuwa watu wengine kabisa.
Ofisi aliyofungua George kwa kupewa ufadhili na walezi wake ilikuwa inahusika na mambo ya kijamii zaidi, hasahasa kusaidia na kutoa elimu kwa watoto wa mitaani na yatima. Jitihada kamilifu zilizofanywa na George akishirikiana na akina Frida ziliisimamisha imara kampuni hiyo. Kila mmoja alifanya kazi kwa moyo mmoja akiamini kuwa anawasaidia ndugu zake mitaani.


****


Ilikuwa siku ya kupendeza kama zilivyokuwa siku nyingine. Chokoraa wanne walikuwa chumbani wakibadilishana mawazo. Walikuwa wakijadili juu ya mikakati yao kemkem ya kuhakikisha yatima na chokoraa wanaishi walau kwa tumaini.
Siku hiyo walikuwa wakishangilia baada ya kumpata mdhamini kwa ajili ya kujenga kituo cha watoto yatima. Lazima wafurahie maana hii kwao ilikuwa ndoto ya muda mrefu.
Ule utani wa hapa na pale ulioinogesha furaha yao mara ukaingia doa baada ya George kuanza kukohoa. Alikohoa sana mara akaanza kutema damu. Macho yakiwa mekundu sana. Hakuweza kuongea alifanya ishara ambazo hakuna ambaye alizielewa. Frida alikimbia na kurejea na maji ya kunywa lakini George alikataa kwa ishara huku sasa akiwa anakoroma tu bila kukohoa.
Baada ya muda akajinyoosha chini akatulia tuli.
Wasichana hawa wakapiga mayowe! Majirani wakafika. Damu ilikuwa imetapakaa mle ndani. Hakuna aliyediriki kumgusa George.
Hofu ikatanda!! Frida akawapigia simu walezi wa kijana huyu. Aliwaelezea kwa ufupi juu ya tukio lililojitokeza.
Baada ya muda baba mtu akawasili akiwa na gari yake binafsi, na daktari binafsi.
George akabebwa na kuingizwa garini upesi. Gari ikatoweka bila kujulikana inaelekea hospitali gani.
Furaha ikatoweka, taharuki ikatawala. Hakuna aliyejua nini tatizo hadi jambo hili likatokea.
Walisafisha zile damu.
Wakalala wakiwa na maswali kedekede!! Hakuwepo wa kuwajibia. Mwanaidi hakulala hapo siku hiyo.
Palipokucha, waliamshwa na mlango uliokuwa unagongwa kwa nguvu sana. Walipofungua walikuwa ni askari.
Frida na Isha walitakiwa kituoni kwa ajili ya kusaidia upelelezi. Juu ya aliyemnywesha sumu George.
Taarifa hiyo iliwashtua sana! Hawakutegemea wanaweza kuwa washukiwa wa kwanza kabisa. Lakini ilikuwa hivi!!
Kilio chao hakikuwasumbua askari. Pesa ya bwana Emmanuel tayari ilikuwa imewatembelea mifukoni na ilikuwa lazima ajulikane aliyeyafanya haya kwa mtoto wake.


Kwa mara nyingine tena Frida Gereza na Isha wakarejeshwa mahabusu. Kwa kesi ya kumnywesha George sumu, lengo likiwa kumuua.


Mwanaidi aliipata taarifa hii kupitia kwa majirani. Hata kabla hajaingia ndani. Akapatwa na mshtuko mkubwa, lakini hakutaka mtu yeyote ajue kuhusu hili.
Dakika mbili baadaye hakuwa tena eneo lile akashtukia kuwa kuna hila zimefanywa na wabaya wao lengo likiwa kuwarudisha kwenye msoto mwingine.
Hasira zikamfukuta kichwani. Akaelekea katika vibanda vinavyotoa huduma ya kuweka na kutoa pesa akatoa kiasi kidogo alichokuwanacho, kisha akatafuta nyumba ya kulala wageni akajihifadhi.
"Kabla hawajanitafuta..ninawatafuta!" alijiapiza. Zile hasira na chuki za uchokoraani zikarejea maradufu kifuani mwake. Akakumbuka chanzo cha haya yote. Ile damu ya yule mwanaume mnene katika nyumba ya kulala wageni ikasimama tena katika akili yake.
Siku iliyofuata Mwanaidi akiwa amejitanda baibui, huku akiacha macho pekee yakitazama. Alitembea kiujasiri hadi katika hospitali ambayo vyombo vya habari vilitangaza kuwa George alikuwa amelazwa na bado akiwa hajarejewa na fahamu zake. Alipofika mlangoni, alisikia sauti ikimuita a kuomba msaada wake.
Akageuka na kutazama
Alikuwa ni mwanamke ambaye alikuwa amezeeka sana na alikuwa mlemavu alitembea kwa kujivuta chini, nguo zake zilikuwa chafu sana. Mwanaidi akarejea na kumsikiliza, alikuwa anaandaa kutoa chochote kitu katika pochi yake. Alijua yule mwanamke anataka pesa.
Lakini haikuwa hivyo. Mwanaidi akamsogelea na kumtazama machoni.
Katika macho haya aliona kitu cha ajabu, ilikuwa inashangaza sana lakini bado hakuwa na uhakika kama ni kweli ama la! Alivutiwa akachuchumaa aweze kumsikiliza.
Baada ya kumsalimia alitega sikio kumsikiliza.
Yule mama alianza kuzungumza mazungumzo ambayo yalimpa hamasa Mwanaidi ya kuendelea kusikiliza zaidi na zaidi.


******


Ilikuwa ni simulizi ya miaka mingi sana iliyopita lakini ilisisimua sana kama vile imejitokeza siku mbili zilizopita. Ilikuwa inaliza na kustaajabisha.
Mwanamke masikini asiyeijua kesho yake. Wazazi maskini walioshindwa kumsomesha huenda ndiyo chanzo chamaisha yake kuwa magumu kiasi kile. Wazazi walioshindwa kumpatia elimu ya darasani wakashindwa walau kumpatia elimu ya duniani hasahasa ya uzazi.
Alipokomaa hakujua nini kinafuata baada ya hapo.
Hakupajua mjini ipasavyo. Alipoingia kwa mara ya kwanza mjini Morogoro kwa nia ya kufanya kazi za ndani ndipo alipokutana na kizaazaa ambacho kiliyahamisha maisha yake kutoka hatua ya kuwa mabaya na kuwa mabaya zaidi.
Aligundua ana mimba akiwa amechelewa sana. Kwani yule bwana aliyempa hiyo mimba alikuwa ametoweka mjini tayari.
Bosi wake naye hakuwa tayari kulea watu wawili. Akamtimua!
Je? Arejeshe aibu hiyo kwa wazazi? Hapana!! Ndio jawabu alilolipata. Akaamua kubaki mjini.
Bila rafiki wala ndugu!!
Akiwa katika kuhangaika huko na huku anakutana na bwana mwenye huruma. Alikuwa masikini kama yeye lakini walau alikuwa na mahala pa kujihifadhi kidogo.
Waliishi vizuri kama mume na mke hadi pale alipojifungua, mtoto alipofikisha miezi saba ndipo yakatokea ya kutokea.
Mwanamke akapooza!! Bwana alishtuka sana lakini kinyume na matarajio ya yule mwanamkea kuwa yule bwana atampa huduma zote za msingi. Haikuwa hivyo japo maisha yalibadilika.
Yule mwanaume akapata pesa akaanza kung'ara, akaanza majivuno.
Kisha kama vile filamu akatoweka kimauzauza na yule mtoto mdogo waliyemuita jina la Matatizo. Mwanamke aliyepooza miguu akabaki mwenyewe katika kijumba kibovu.
Mateso yakaanza upya. Ofisi ya kata haikuwa na lolote la kumsaidia kwani hata wenyewe walikuwa na matatizo yao na walihitaji msaada kutoka serikali kuu.
Miaka ikaanza kukatiza. Huyu mama akaungana na ombaomba wengine katika stendi ya msamvu na maeneo ya mjini kati.
Maisha yake yakabadilika kuwa hayo.
Akayazoea na hatimaye miaka mingi ikapita akiwa mzoefu wa shida.
Siku moja katika mazingira ya kuomba omba alijiburuza akaingia sehemu ya hoteli kuomba chakula.
Huku alipatiwa msaada wa sahani ya chakula akaanz kuisasambua upesi.
Wakati anakula alishtushwa na habari katika luninga. Habari hii ilimuhusisha mtu ambaye alimjua kabisa.
Alitamani kumuuliza mtu yeyote pale ndani lakini hawakuwa wakifahamu analojua yeye.
Alikuwa amemuona baba aliyekimbia na mtoto wake.
Uchungu wa miaka mingi alioupitia aliamini iwapo atampata mtoto wake basi walau anaweza kumsaidia.
Mama ni mama tu..sura ya mwanaye hata ifinyangwe vipi lazima ataibaini. Ndivyo ilivyokuwa kwa mama huyu wakati George Emmanuel anayedhaniwa kuwa amepewa sumu afe. Alivyoonyeshwa katika taarifa ya habari.
Mama huyu hakutaka kulaza damu.
Shughuli ya kuomba omba ilikuwa imempatia kipato cha kuweza kusafiri hadi jijini Dar es salaam. Akafanya maamuzi akasafiri!!!
Japo alipata bughudha na mahangaiko makubwa kutoka katika kituo cha mabasi ubungo lakini sasa alikuwa mbele ya ile hospitali ambayo ilitangazwa kuwa George Emmanuel alihifadhiwa akiwa hajitambui.
Mwanaidi anavutiwa naye anamsikiliza na sasa anapata jambo jipya kabisa ambalo ni wachache wanalitambua ulimwenguni!!!!
SIRI KUU!!! Siri inayoweza kuwaokoa Frida na Isha, siri ambayo itamuweka mwenye haki mahala pake na yule mkosefu katika sawa yake!!!


***KUMBE GEORGE ana mzazi??? Ilikuwaje sasa huyu bwana Emmanuel akamchukua na kudanganya kuwa wazazi walimtupa???
Vipi akijua???


NINI HATMA YA CHOKORAA NA MAISHA HAYA.


ITAENDELEA

VAN HEIST muuza ubuyu amina mabata shabani hassani culbby sam II ram
BPM
 
Last edited by a moderator:
Asante sana Mkuu huyu mbaba anajifanya aliokota na kulea ndiye aliyefanya jaribio la mauaji ya George.
 
SEHEMU YA 13
RIWAYA: CHOKORAA
MTUNZI: George Iron Mosenya


SEHEMU YA KUMI NA TATU


Japo alipata bughudha na mahangaiko makubwa kutoka katika kituo cha mabasi ubungo lakini sasa alikuwa mbele ya ile hospitali ambayo ilitangazwa kuwa George Emmanuel alihifadhiwa akiwa hajitambui.
Mwanaidi anavutiwa naye anamsikiliza na sasa anapata jambo jipya kabisa ambalo ni wachache wanalitambua ulimwenguni!!!!
SIRI KUU!!! Siri inayoweza kuwaokoa Frida na Isha, siri ambayo itamuweka mwenye haki mahala pake na yule mkosefu katika sawa yake!!!


Mwanaidi sasa aliamini alichokiona katika macho ya yule mwanamke mlemavu! Alikuwa ameiona sura ya George katika macho yale, hivyo hakuwa na maswali mengi kwani alikuwa amekubaliana na ukweli hata kabla ya maongezi.
Alijiuliza maswali mengi sana kichwani hasahasa kuhusu maisha ya George, alijiuliza kwanini mlezi wake alifanya unyama kama huo? Hakupata jawabu.
Mwanaidi akatumia kama dakika sita kufikiri kisha akapata maamuzi ya kufanya. Kwanza alikodi teksi upesi yule mama akachukuliwa pamoja naye hadi katika nyumba ya kulala wageni aliyokuwa amefikia. Alimuhifadhi mama huyu ili aweze kuwa huru zaidi katika kufanya maamuzi thabiti.
Mama hakuwa na kipingamizi baada ya kuthibitishiwa kuwa kila jambo litaenda sawasawa.
Alipotoka pale akiwa na baibui kama awali, alirejea kule hospitali. Kikubwa alichokifuata pale ni kumjua ipasavyo baba mlezi wa George. Wapi anapoishi? Lilikuwa jambo kubwa zaidi.
Kwa mazungumzo ya watu wawili watatu akapata kuyajua majibu hayo.
Akatoweka!!


*****


Kikundi kikubwa kilikuwa kinamsikiliza msichana ambaye alikuwa na umbo kubwa kiasi. Ukorofi wao ulikuwa kando kabisa. Kilichosimuliwa kiliyagusa maisha yao kiundani, lazima watulie.
Mwanaidi alikuwa amewakusanya machokoraa wengi wa kempu ya feri, aliwaeleza juu ya kisa cha George, wengi wao walikuwa wanamjua kutokana na harakati zake za kuwasaidia kutoka katika hali hiyo ngumu. Wengine waliacha kutumia madawa ya kulevya kutokana na harakati zake, tumaini jipya likajijenga katika mioyo yao.
Mtu anayekupa chakula wakati unakihitaji ni vigumu sana kumsahau. Ndivyo ilivyokuwa kwa hawa! Walikikumbuka chakula cha kule Biafra.
Suala la George kunyweshwa sumu liliwashangaza mno na kwa pamoja wakakiri kuwa mtukufu yule hakustahili adhabu hiyo kwa mema anayoyatenda.
Lakini kubwa zaidi lililowaacha katika kizungumkuti ni simulizi juu ya kupatikana kwa mama yake. Mama mlemavu anayeishi maisha ya shida. Shida zilizosababishwa na mlezi wa George.
Sasa hapa matusi ya kila namna yalimwagika. Kila chokoraa akamtamani huyo mlezi wa maajabu kwa ajili ya kumwadabisha. Mwanaidi akawatuliza kwa maneno yote wakatulia.
"Yule ana pesa sana tunahitaji kujipanga kwa ajili ya kuwaokoa ndugu zetu waliopo gerezani bila makosa, pia kumuokoa mkombozi wetu. George!" alisema kwa sauti kuu. Kila mtu kimya!!
Kijana mmoja ambaye alikuwa muathirika wa madawa ya kulevya kabla ya harakati za George hazijaanza alitoa wazo la kutafuta msaada wa kisheria. Hili aliomba aachiwe yeye kwani kuna watu waliokuwa wakimpa tiba hapo nyuma wanayafahamu mambo haya.
Akakabidhiwa jukumu hilo!!


****
Pesa zilikuwa tatizo jipya lilijitokeza katika harakati hizi za ukombozi wa mwenye haki na hukumu kwa mwenye stahili hiyo. Kwa ujasiri usiku wa kutisha kabisa mwanadada Mwanaidi alinyata akamuacha yule mama chumbani akiwa anakoroma, akatoka na kuelekea ‘club Ambians' maeneo ya Sinza Afrikasana, shughuli zinazofanyika hapa asilimia kubwa ni za kuuza vyakula, burudani ya muziki na biashara ya kuuza miili ya akina dada.
Mwanaidi hakwenda tena kwa kulazimishwa bali safari hii alifanya kwa hiari yake lengo likiwa kupata pesa kwa ajili ya kufanikisha harakati zake za kuwakomboa waliostahili. Alifika pale alipohitaji akiwa katika mavazi ya kulalia. Alikuwa nusu uchi! Huku akiwa makini kabisa na kifaa chake alichokihifadhi katika nguo yake kisiweze kuonekana. Kisu kidogo!!
Hadi majira ya saa saba usiku alikuwa ameingia mara mbili katika huduma na alikuwa ana kiasi kidogo tu cha pesa. Alitamani kuondoka kwa kuona kuwa biashara ni mbovu lakini machale yake ya siku zote yalikuwa yanamshawishi abaki.
Laiti kama angeendelea kusoma zaidi na zaidi huenda angekuwa mpelelezi mashuhuri sana. Alikuwa anayaheshimu sana machale pale yanapomcheza. Hali hii imekuwa ikimsaidia mara kwa mara, hata siku ambayo George anapatwa na haya maswahibu yeye alijikuta bila sababu anaondoka na kulala alipojua yeye.
Hata baada ya kuwaeleza chokoraa wa feri kuhusu jambo linalowakabili. Hakujiaminisha sana kuwa usalama upo wa kutosha. Aliendelea kujiweka katika wasiwasi na kuheshimu kila hisia inayokatiza mbele yake.


Kwa siku nyingine tena machale yake yalimbeba binti huyu. Aliishuhudia sura aliyoifahamu fika katika mawindo ya kusaka machangudoa. Alikuwa peke yake na ni kama alikuwa muoga na mgeni sana eneo lile.
Huyu alikuwa ni Emmanuel baba mlezi wa George!!
Au ananitafuta!! Alijiuliza Mwanaidi huku akijificha kwa kutumia kitambaa cha mkononi.


Tofauti na Mwanaidi alivyodhani kuwa anatafutwa, kichwani mwa Emmanuel jambo lilikuwa jingine kabisa alikuwa katika kutafuta changudoa ili aweze kutimiza masharti magumu aliyopewa na mganga wa jadi kwa ajili ya kuimarisha utajiri wake dhidi ya wapinzani ambao muda wowote siri ikifichuka mambo yatakuwa mabaya kwa upande wake.
Baada ya kudumu imara miaka mingi bila ya kujutia uamuzi wake wa kujipatia utajiri kwa njia za kishirikina, kwa kumtoa kafara mwanamke masikini asiye na kosa kisha kumweka mtoto wa mwanamke huyo kama ngao, sasa alikuwa ana hangaika. Ilikuwa ni lazima afanye uzinzi na changudoa usiku huo kabla ya kuendelea n masharti mengine.
George hakutakiwa kuwa mkarimu kiasi kile, alitakiwa kuwa na roho mbaya ili katika urithi wa mikoba ya kichawi ya kumshikia utajiri mzee Emmanuel asiweze kuogopa.
Emmanuel alijifanya kuwa mcha Mungu sana. Lakini haya yote aliyafanya kwa ajili ya kujiweka katika kivuli kitakachomlinda na watu wabaya wanaoweza kutilia mashaka utajiri wake.
Sasa George anaonekana dhahiri kuwa katika upande usiowapendeza wale waliompatia utajiri Emmanuel.
Hivyo anatakiwa kufata masharti yote. Sharti la kwanza likiwa kumlaza kitandani George asiendelee na jambo lolote lile katika maisha hadi masharti yatimie. Aharibiwe akili yake na kuanza kupelekeshwa wanavyotaka wao.
Sasa George yupo kitandani na serikali inaamini amenyweshwa sumu. Daktari aliyezoea rushwa amechukua pesa kutoka kwa Emma na sasa anasema kile bosi wake anataka.
Frida na Isha wanatupiwa mzigo huu!! Emma aliamini kabisa kwa mchezo huu hakuna wa kuweza kumshtukia.


Mwanaidi aliendelea kumfuatilia Emma hadi alipomuona anasemezana na msichana aliyekuwa eneo lile kibiashara. Maelewano yakawa mazuri wakaelekea sehemu ya tukio.


Baada ya kutoka pale mzee Emma alizengea huku na kule kisha akaanza kuelekea alipopajua yeye mwenyewe.
Mwanaidi chokoraa mzoefu asiyeogopa jua, mvua, giza wala mwanga aliendelea kumfuatilia kwa tahadhari kubwa sana. Hadi alipofika katika mtaro na kuibuka na kifurushi fulani.
Bado Mwanaidi hakuchoka akaendelea kufuatilia nyendo za tajiri huyu wa mchana.
Bila kujua kama anafuatiliwa bwana Emma alipoifikia njia panda alitazama kushoto na kulia kisha akazamisha mkono wake katika ule mfuko akaibuka na nazi. Akanong'ona maneno machache kisha akaivunja.
Haya yote Mwanaidi aliyashuhudia bila kuogopa. Kwani kwa maisha yake ya uchokoraa ni mengi ameyashuhudia ya kutisha na kushangaza zaidi ya hayo.
Upelelezi huu kwa kiasi fulani ukawa umemtosheleza!!
Akachukua hamsini zake!! Akimwacha mzee Emma akiendelea na safari zake.
Kumbe ni mshirikina!! Alipata jawabu Mwanaidi.


*****


Ule wakati ambao Mwanaidi anaamua kuachana na Emma na kuendelea na mambo yake ndio wakati ambao Emma anapokea simu kutoka kwa rafiki yake ambaye ni mwanasheria. Mwanasheria huyu anamsihi na kumsihi bwana Emma kuwa siku inayofuata mapema sana waweze kuonana kuna tatizo linalotakiwa kusawazishwa kabla mambo hayajawa mabaya.
Mwanasheria hakutaka kumueleza lolote juu ya tatizo hilo maana lilikuwa gumu sana kuelezeka.
Emmanuel aliahidi kuwa siku inayofuata mapema kabisa atakuwa pale.


Siku iliyofuata asubuhi wakat Emma akiwa katika gari lake kuelekea kwa huyo mwanasheria. Na Mwanaidi naye alikuwa pamoja na yule kijana aliyeagizwa kumsaka mwanasheria wakielekea kwa huyo mwanasheria kumuelezea juu ya tukio la bwana Emma kuonekana usiku akiwa na changudoa kisha akafumaniwa bila kujua akivunja nazi njia panda. Mwanaidi aliamini ni yeye anayeweza kukielezea kisa hicho vizuri sana hakuna mwingine!!
Sasa wanaelekea katika ofisi ambayo mbaya wao naye anaenda kwa ajili ya kuvujishiwa siri.


****


****EMMANUEL anayemiliki utajiri kwa kutoa kafara…je ataonana na MWANAIDI…….nini kitatokea.
***Harakati za CHOKORAA kuwapigania wenzao zitafanikiwa!!!


ITAENDELEA

VAN HEIST muuza ubuyu amina mabata shabani hassani culbby sam II ram BPM mbalu
 
Last edited by a moderator:
SEHEMU YA 14
RIWAYA: CHOKORAA
MTUNZI: George Iron Mosenya


SEHEMU YA KUMI NA NNE


Siku iliyofuata asubuhi wakat Emma akiwa katika gari lake kuelekea kwa huyo mwanasheria. Na Mwanaidi naye alikuwa pamoja na yule kijana aliyeagizwa kumsaka mwanasheria wakielekea kwa huyo mwanasheria kumuelezea juu ya tukio la bwana Emma kuonekana usiku akiwa na changudoa kisha akafumaniwa bila kujua akivunja nazi njia panda. Mwanaidi aliamini ni yeye anayeweza kukielezea kisa hicho vizuri sana hakuna mwingine!!
Sasa wanaelekea katika ofisi ambayo mbaya wao naye anaenda kwa ajili ya kuvujishiwa siri.


****


Kwa kuwa Emma alikuwa anatumia usafiri wake binafsi ilikuwa ni lazima awe wa kwanza kufika katika ofisi ya mwanasheria.
Baada ya maongezi ya dakika kadhaa, jasho lilianza kumtoka Emmanuel. Alikuwa kama mtoto mdogo asijue nini cha kufanya kwa wakati ule. Kwa mwanasheria hili halikuwa jambo kubwa la kwanza kusikia jambo kwa kiasi fulani lilimshangaza na kumfanya ile heshima aliyokuwa nayo kwa bwana Emmanuel ishuke kwa kiasi fulani.
Sauti yenye kitetemeshi na iliyokosa utulivu ya bwana Emma ilipenya katika mlango na kumfikia Mwanaidi aliyekuwa pamoja na yule kijana aliyeileta taarifa kwa mwanasheria. Sauti hizo zilikuja katika mithili ya miungurumo hivyo ilikuwa ngumu sana kutambua neno linalosemwa. Hakuitilia maanani sana aliendelea kuvuta subira ili mteja anayehudumiwa aweze kumaliziwa shida zake na wao waweze kusikilizwa.
Dakika zikasogea hatimaye zikafiki sitini. Saa moja
Masaa mengine mawili yakapita, ndipovikasikika viti vikiburuzwa ishara ya mtu kusimama. Tendo hilo nalo likatwaa dakika tano ndipo mlango ukafunguliwa. Wakati mlango unafunguliwa Mwanaidi alikuwa anayapikicha macho yake ili aweze kuona mbele sawasawa baada ya kuwa amesinzia kwa kitambo fulani pale alipokuwa amekaa.
Macho yake yaliyotandwa na ukungu yaliweza kuona kitu. Alimuona Emma, yule mlezi wa George. Mwanaidi aliganda kama picha katika luninga. Akatulia tuli mapigo yake ya moyo ndo kitu pekee kilichojitahidi kwenda kasi.
"Ingia we dada watu tuna haraka" sauti za makaripio ndio zilimrudisha katika uhai wa kufikiri, akaingia katika ofisi ya mwanasheria.
Kijana waliyekuwa naye akabaki nje, alikuwa amesinzia! !.


Mwanasheria huyu aitwaye Kindo alimkaribisha mteja wake kwa tabasamu hafifu. Uso wake ulikuwa kama una hatia inayojaribu kujificha, sura ya mwanadada huyu nayo haikufanya makosa ikajibu tabasamu la bandia. Mwanasheria akajichekesha. Sarafi hii Mwanaidi hakutabasamu wala hakucheka.
"Naitwa Suzan." Alijitambulisha bila kuulizwa huku akiiegemea meza. Kabla hajaendelea zaidi mlango ulisukumwa akaingia mteja mwingine lakini kwa shida ile ile. Huyu alikuwa ni kijana ambaye Mwanaidi alikuwa amefika naye eneo lile. Sasa alikuwa ameamka kutoka usingizini.
"Ohoo. Masha, karibu sana." Alizungumza mwanasheria.
Masha akatoa salamu kisha akakaa.
"Nipo na huyu dada." Masha alijielezea. Mwanasheria akaonyesha ishara ya mikono kuwa wanaweza kuongea.
Mwanaid ambaye alikuwa ameshtuka kutokana na uoga aliouonyesha mwanasheria huyu alikuwa hana nguvu kabisa za kuweza kusema jambo. Lakini alijikaza na kutaka kuanza kuzungumza.
Kabla mazungumzo hayajakolea simu ya mwanasheria iliita.
Akawataka radhi akatoka nje.
Mwanaidi alitamani sana kumweleza Masha kuwa huenda siri yao imevuja tayari na hakuna msaada wowote kwa bwana huyu, lakini alihofia kumchanganya kijana huyu na kumsababisha daktari awashtukie.
Mwanadada wa kizaramo, yatima na chokoraa mzoefu akakaa kimya.
Baada ya dakika kadhaa mwanasheria akarejea, akiwa anaukuna upara wake na kuiweka sawa suti yake mwilini.
"Ndio nakusikiliza. Mmesema mpo wote?" aliuliza.
Wakatikisa vichwa kukubali.
Mwanaidi akajivika tena ujasiri lakini safari hii hakuweza kuendelea zaidi. Na yeye akasingizia udhuru kuwa anhitaji kuzungumza na Masha kando.


Walipotoka hawakurejea!


Mwanaidi alimueleza Masha kwa kifupi juu ya wasiwasi wake. Masha akamuelewa kabisa. Wakarejea kule walipomwacha mama George. Masha hakufika hadi eneo husika, aliondoka kuelekea feri.
Jioni kwa kupitia taarifa ya chokoraa wenye nia njema, Mwanaidi aliipata taarifa ya kuwa anatafutwa na mtu wasiyemfahamu anadai kuwa ni ndugu yake.
Mwanaidi hakudanganyika kirahisi. Aliyasikia maneno haya na kuyafanyia kzi upesi. Akili yake komavu ikayachambua na kugundua kuwa anawindwa sana na alijua pia Emma tayari ameambiwa juu ya uwepo hai wa mama yake George. Akafanya tabasamu la kujilazimisha!


*****
George aliendelea kuwa kama gogo katika kitanda cha hospitali. Jambo la maajabu ni kwamba alikuwa anapumua bila shida. Lakini alilazimika kulishwa kwa kutumia mipira.


Pesa nyingi alizozichukua daktari kwa ajili ya kuuficha umma juu ya ukweli uliojificha ziliendelea kumfanya awe jasiri. Manesi walikuwa wakimsikitikia George. Lakini ukweli ni kwamba kijana huyu asiye na hatia alikuwa mbali kabisa. Alikuwa katika kuwatumikia watu wabaya.
Pale kitandani, walikuwa wanahudumia gogo bila kujua.
Nguvu za maajabu walitunukiwa hawa wachawi!
Juma zima lilikatika. Hali ya George ilikuwa tete sana. Mke wa Emmanuel alishangazwa sana na hatua hii ya kuendelea kumuacha mgonjwa huyu katika hospitali hii kwa muda mrefu wakati uwezo wa kumpeleka nje ya nchi ulikuwepo.
Siri kuu ikasalia kichwani mwa bwana Emma aliyekuwa amemtoa kafara Mama yake George na mwanaye ili aupate utajiri, na mwingine aliyejua walau kidogo ni daktari aliyempima George na kugundua kuwa hana ugonjwa wowote.
Frida na Isha wakaendelea kusota rumande kwa kosa wasilolifahamu! Uonevu uliokithiri.


Bwana Emmanuel alikuwa amebadilika sana, hakuwa na furaha tena, alikondeana ndani ya siku chache. Mkewe hakujua nini tatizo na aliogopa sana kumuuliza kwa sababu ya hasira za ajabu ajabu alizokuwanazo. Mabadiliko haya yalikuwa wazi hata kwa watoto wake wa kuzaa, hali hii iliwashangaza.
Lakini siri aliijua yeye na nafsi yake. Tatizo lilikuwa kubwa.
Mali za lelemama zilikuwa zinampeleka puta. Suala la kuambiwa na mwanasheria juu ya uwepo wa mama anayemtuhumu kuwa alimuibia mtoto, ni jambo ambalo lilimchanganya sana. Akiwa hajakaa sawa huku akitegemea kumpata kirahisi mwenye siri hiyo.
Simu anayopokea kutoka kwa mwanasheria kuwa wale wenye siri wapo naye kisha anapofika anaambiwa wametoweka bila kuaga inamchanganya zaidi. Sasa ameagiza vijana watatu maalumu kwa ajili ya operesheni sana Mwanaidi ama kwa jina la uficho Suzan.
Alitegemea kuwa shughuli hii itakuwa nyepesi lakini sasa inakuwa ngumu sana. Hapati anachokihitaji na muda unazidi kwenda huku aibu nayo ikijongea kwa kasi.
Alitia huruma mzee huyu, lakini alistahili kuaibika!


*****


Mwanaidi alijiweka mbali tena na wale machokoraa wa feri nap engine popote pale. Viwanja vya kuuza mwili wake pia alibadili. Ni katika kukwepana na watu wa Emma ambao aliamini usiku na mchana wanamsaka ili awaeleze ni wapi yule mama yupo waweze kumuua afe na siri yake kifuani. Afe na ushahidi ambao utawaweka wengi huru.
Mwanaidi hakuwa tayari!
Gharama za kuendesha maisha ya pale hotelini zikaanza kumzidia. Kurejea kule walipokuwa wanaishi ili aweze kuchukua chochote na kuuza haikuwezekana alihofia usalama wake.
Hakuwa na mbinu nyingine ya ziada zaidi ya kuuza mwili wake kwa jitihada. Kilichopatikana alimuhudumia yule mwanamke.
Kibaya zaidi hakujali tena iwapo kinga inatumika ama la. Akawa makini kuikwepa mimba kuliko kuvikwepa virusi.
Mpaka lini? Alijiuliza Mwanaidi ikiwa zimepita siku saba tangu amuhifadhi yule mama huku rafiki zake wakisota rumande kusubiri kesi yao iliyokuwa katika upelelezi wa kitaalamu. Mtaalamu mwenyewe ni daktari ambaye tayari amenunuliwa na kuusema uongo ukisikika kama ukweli.
Ilikuwa siku ya jumatatu asubuhi. Mwanaidi hakuwa sawa kiafya, alisumbuliwa na mafua na kichwa kilikuwa kinamuuma. Hii ilitokana na kunywa pombe kwa mara ya kwanza.
Angefanya nini wakati mteja wake ndicho alichohitaji!
Hakika alimlipa pesa nzuri lakini alimuathiri.
Mwanaidi alimtazama yule mama aliye katika usingizi, uzo wake wenye makunyanzi ukijionyesha dhahiri shahiri kuwa tegemezi lake hapo mjini ni Mwanaidi pekee. Uso huu ulimsikitisha sana Mwanaidi.
Akahamishia macho yake katika miguu isiyoweza kutembea bali kujiburuza. Akachukua kiganja chake na kulifuta chozi lake lililokuwa linatiririka kutoka katika jicho la kuume.
Mwanaidi akasikia kifua chake kikijawa na kitu ambacho hakikufanana na hasira lakini kilipasha joto kifua chake. Akasimama akijisikia ana ujasiri wa hali ya juu.
Akaingia maliwatoni akausafisha mwili wake. Akatoka bila kuaga.
Safari yake hii ya kutatanisha alikuwa anenda pia eneo la kutatanisha lisilokuwa na amani.
Alimfuata mwanasheria!
Yuleyule ambaye walimtoroka siku kadhaa nyuma.
Bahati nzuri siku hiyo hakumkuta na watu kabisa. Akaingia ndani. Wakagonnganisha macho, Mwanaidi akapatwa na mshtuko akajisahau hata kutoa salamu.
Akajiruhusu mwenyewe kuchukua nafasi katika kiti.
Mwanasheria kabla hajamuuliza binti huyu anahitaji nini, Mwanaidi alianza kuzungumza. Bila kumpa nafasi mwanasheria kusema lolote.
"Nimejileta mwenyewe baba, najua ninasakwa sana kuliko thamani yangu ilivyo, ni heri angekuwa ananisaka mama yangu ili anirudishe tumboni nisiishi tena duniani. Sina hadhi ya kuwa katika dunia hii. Huenda nilikuja kimakoda, mwenyezi mungu aliwaumbia ninyi wenye elimu dunia hii iwe makazi yenu. Unao watoto kama mimi. Unajisikiaje mwanao akichelewa kurudi nyumbani, unajisikiaje ukisikia ana mahusiano na mwanaume fulani. Sasa huyo mtoto mfanye awe mimi, nimezaliwa katika tabu na ninaishi katika hizo tabu, nimenyanyasika, sijawahi kuwa na amani, ni kitu gani mimi cha udhalilishwaji mwanaume hajanifanyia, ni tusi gani sijatukanwa! Na sasa ninasakwa kwa ajili ya kutetea haki. Ewe mwanasheria mimi sijasoma na wala siwezi kukukosoa, mimi ni uchafu tu ambaye wanadamu wanazidi kunibebesha uchafu wao. Sina wa kunitetea mimi, hebu kuwa nasi watoto yatima kuwa nasi japo kidogo watoto wa mitaani na mwenyezi Mungu atakubariki.
Kwanini uwatetee hao watesaji, Emmanuel anamtesa mwanamke ambaye analingana na mke wako, anaweza pia kuwa mama yako, unatetea mama yako kunyanyaswa, unaweza kutabasamu iwapo mkeo amevunjwa miguu maksudi?" Mwanaidi hakuweza kuongea zaidi, kilio kilikuwa kimemshinda. Akainama chini kwa muda kisha akayasema maneno haya ya mwisho, "Mikono yangu hii hapa, sina silaha, nifunge kamba umwite anikamate na kunifanya anavyotaka na amani iwe nanyi!.
Hapa sasa mwanasheria aliusikia mgongo wake ukilowana. Alikuwa amepigwa na shambulio kali asiloweza kulielezea. Alijaribu kumbembeleza Mwanaidi lakini haikuwa kazi nyepesi.
Picha za matukio machafu yote aliyotendewa zilipita kichwani, akajiona afai tena kuishi. Akajisalimisha.
Mwanaidi alipoona kuwa mwanasheria hakuwa na la kufanya na kuna wateja wengine walihitaji kuingia katika chumba chake cha ofisi, alisimama wima akatoka bila kuaga.
Uso wa mwanasheria ukashikwa na soni!
*****


Mkuu wa shule alikuwa makini sana kumsikiliza dada huyu ambaye kabla ya kutoweka alikuwa ni kiongozi mkuu pale shuleni. Dada huyu alimuelezea mikasa yote aliyoipitia hadi kufikia hatua hiyo aliyopo.
Alielezea maisha ya uchokoraa na kunyanyaswa jinsi yalivyopoteza uelekeo wa maisha yake.
Kilio cha Mwanaidi kikapokelewa kikamilifu na mkuu huyu wa shule ya msingi aliyokuwa anasoma hapo awali.
Hii ikawa safari yake ya pili kwa siku hiyo.
Umoja wa shule za msingi unaweza kuwa ni umoja kamilifu kupita aina nyingine za umoja. Wakiandama wanaandamana wote. Wakipiga kelele ni wote wanapiga kelele.
Walipoelezwa jambo hili. Wengi wao walilia sana.
Mwanaidi alikuwa anapendeka sana pale shuleni!
Vilio vyao viliambatana na ahadi kemkem, kuwa siku ya mahakama watakwenda kuwatetea watoto waliofungwa pasipo makosa.
Kuwatetea watoto wa mitaani!


Tofauti na utendaji wao kuanza siku ya mahakama, hali ilianza siku hii wakati Mwanaidi anatoweka eneo lile.
Kilio chake kikali cha mara moja katika uchochoro kiliwashtua wengi. Wakawahi kukimbilia kilipotokea. Waliokuwa wanataka kumteka Mweanaidi hawakuhitaji kusali sala zao za mwisho ili waingie katika safari ya milele. Walikuwa watatu. Na dakika hizo hizo tatu ziliwatosha kuwa nyang'anyang'a. na dakika kumi baadaye walikuwa maiti.
Bahati mbaya hawakusema ni nani aliyewatuma!
Mwanaidi pekee alijua kuwa hiyo ni mipango ya bwana Emma kumkamata ili aifiche siri yake.


Kelele za wanafunzi na tukio walilolifanya liliifikia serikali.
Kwa kuwa kuna roho tatu zimetoweka. Jambo hili halikufumbiwa macho.
Akasakwa aliyeshukiwa kutekwa! Jina la Mwanaidi likawekwa katika orodha kuu. Sawali likawa ni wapi pa kumpata??.


Kupatikana kwa Mwanaidi ilikuwa sawa na taarifa ya msiba kwa Emmanuel ambaye alitegemea vijana wake aliowaagiza watamleta binti huyo mikononi mwake. Lakini badala yake wameuwawa kinyama kwa kupigwa na wanafunzi.
Hali hii ilizidisha ugumu kwa upande wake. Alijiuliza itakuwaje endapo mkewe atagundua maasi haya ya miaka mingi iliyopita. Itakuwa vipi akigundulika na jamii kuwa yu mshirikina??


****
Emmanuel akajaribu kucheza karata ya mwisho kwa kuingia mtaani kumsaka Mwanaidi ambaye alimjua sura yake kwa mbali sana. Emma akaamua kuwawahi polisi katika kuwania kuificha siri yake.
Wakati Emma anaingia mtaani. Kuna kiumbe mwingine naye baada ya kuguswa na maneno ya Mwanaidi aliamua kuingia mtaani kumsaka mtoto huyo ambaye alionyesha kuwa amekata tama na maisha. Japo alikuwa mwanaume aliyeyapitia mengi, bwana Kindo alitokwa machozi kutokana na maneno ya Mwanaidi.
Bahati ya maajabu wote wakajikuta wakianzia feri, mwanasheria akimtafuta Masha ili apate pa kuanzia, Emma akimtafuta Mwanaidi moja kwa moja.
Hakuna aliyejua mwenzake anawaza nini kichwani


***HARAKATI ZA UKOMBOZI WA CHOKORAA NA YATIMA. Je watafanikiwa……..nini hatma ya FRIDA na ISHA Gerezani…..


ITAENDELEA.

VAN HEIST muuza ubuyu amina mabata shabani hassani culbby sam II ram BPM mbalu
 
dah jamn ,kwanza hongera kaka kwa simuliz nzur ya chokoraa...kwel chorakaa huwa wanapitia mitihan ming ...mpka nashindwa zuia choz listokee..Ubarikiwe mtunzi
 
RIWAYA: CHOKORAA
MTUNZI: George Iron Mosenya




SEHEMU YA KUMI NA TANO


Wakati Emma anaingia mtaani. Kuna kiumbe mwingine naye baada ya kuguswa na maneno ya Mwanaidi aliamua kuingia mtaani kumsaka mtoto huyo ambaye alionyesha kuwa amekata tama na maisha. Japo alikuwa mwanaume aliyeyapitia mengi, bwana Kindo alitokwa machozi kutokana na maneno ya Mwanaidi.
Bahati ya maajabu wote wakajikuta wakianzia feri, mwanasheria akimtafuta Masha ili apate pa kuanzia, Emma akimtafuta Mwanaidi moja kwa moja.
Hakuna aliyejua mwenzake anawaza nini kichwani


Mtaa ukajikuta ukihangaishwa na watu wawili wakiwa na nia tofauti. Mmoja akimtetea chokoraa huku mwingine akitaka kumgandamiza.
Siri aliyoigundua Mwanaidi inamtesa Emmanuel, Emmanuel anaamini kuwa yupo bega kwa bega na mwanasheria Kindo, kumbe tayari amesalitiwa.
Sasa kila mmoja yupo ha lake mtaani!!


Wakati wawili hawa wakihangaika kumsaka kiumbe mmoja asiyekuwa na silaha kubwa zaidi ya siri. Msakwa mwenyewe alikuwa ananyemelea mahali. Akalifikia geti akatazama kushoto na kulia, akajihisi unyonge kuibofya kengere ili waliopo ndani waweze kuufungua mlango. Akatumia sekunde chache tu kufanya tafakari kasha akakikumbuka kisu chake alichokificha mahali ambapo ni yeye pekee anaweza kupafikia kwa urahisi. Akajenga ujasiri kasha akajinong'oneza.
Mimi ndo Mwanaidi aisee!!
Akabofya kengere!!


Baada ya dakika takribani tatu geti likafunguliwa katika kitundu kidogo.
"Nani?" akaulizwa. Hakujibu.
Geti likafunguliwa. Mtoto amabye angeweza kujiona kuwa yu mtu mzima kutokana na kuwa na mwili mkubwa alitokezea kwa nje akiwa amevaa fulana iliyomkaa vyema.
Alikuwa amenuna, ni kama alikuwa ametoka usingizini.
Wakatazamana na Mwanaidi nani aanze kuzungumza?
"Naitwa Mwanaharusi ni mgeni wa bwana Emma."
"Hayupo…" alijibu kwa shari bila kuuliza zaidi. Mwanaidi akamtazama vyema akamkazia macho makali yaliyozoea kutazamana na mgambo wa jiji. Yule mvulana akainama chini.
"Je mama?" aliongeza swali.
"Subiri!!" alimalizia hivyo.
Akalifunga geti akatoweka. Hakurejea tena badala yake akafika mama mtu mzima. Mrembo wa haja ambaye enzi za usichana wake halikuwa jambo la kushangaza kwa mwanaume kupiga magoti kubembeleza apate penzi


Akamtazama Mwanaidi kwa jicho lililoonyesha kuwa hajawahi kumuona hapo kabla au iwapo aliwahi kumuona basi tayari amemsahau.
"Shkamoo mama…naitwa Mwanaidi."
"Mwanaidi? Mwanaharusi?" aliuliza yule mama. Mwanaidi tayari alikuwa amesahau kuwa mwanzoni alijitambulisha kama Mwanaharusi kwa yule aliyekuja awali kumsikiliza.
Mwanaidi hakujibu!!
"Haya unasemaje?"
Mwanaidi alimtazama yule mama ambaye hapakuwa na haja ya kujiuliza kama ni mama mwenye nyumba ama la.
Mwanaidi akajiegesha katika mlango wa kuingilia. Yule mama akaagiza kuletewa viti viwili. Upesi vikaletwa.
Sasa mazungumzo yakaanza!!
Mwanaidi alifumba macho yake, kuna jazba alikuwa anaizuia. Sasa akaanza kuzungumza.
"Mama, mama yangu mzazi. Bila shaka u mke wa bwana Emma." Alianza Mwanaidi kasha akayafumbua macho akamtazama yule mama aliyekiri kwa kunyanyua na kushusha kichwa kwamba kweli ni mke wa Emma.
"Nimejileta peke yangu bila kulazimishwa mama. Nimejileta kwako unihukumu kama ni sahihi…" alianzia hapo Mwanaidi, akayafumba macho na kusimulia kuanzia mwanzo wa maisha yake hadi hapo alipofikia huku akimuelezea juu ya George na utata uliopo kwa mama yake mzazi kutelekezwa na bwana Emma miaka mingi iliyopita.
"Mama, mimi simjui mama yangu sijui kama naye alitendwa hivi, sijui kama yupo hai nimeishi uyatima miaka yangu yote, nimekuwa chokoraa, nimetendwa na dunia bila kikomo. Naamini u mwanamke mwenye uchungu, uchungu wa kunizaa mimi, uchungu ambao hata mimi nitaupata ndio uchungu ulionileta hapa. Nateseka mama, nab ado nasakwa niuwawe, watoto wako wengine wapo rumande hadi sasa. Amewaweka bwana Emma. Unyama alioutenda miaka mingi iliyopita haujamtosha sasa ananyanyasa yatima kwa kuwa yu hai."
Mwanaidi alizungumza sasa wazimu ukiwa umempanda, uchungu uliopitiliza ukayaruhusu machozi kuendelea kububujika. Kilio cha kwikwi nacho kikatawala. Sasa alikuwa analia na hakuweza kuzungumza.
Alipojaribu kuyafumbua macho yake. Mama mwenye nyumba alikuwa anatiririka jasho. Na alikuwa ametulia tuli.
Mwanaidi akajiweka sawa kitini. Akamuita mama, hakujibu. Akaita tena na tena bado hakujibiwa!!
Machale yakamcheza, ule ujasiri ukatoweka.
Akatazama kushoto na kulia. Geti likamuita, akachomoka upesi.
Sasa alikuwa anaogopa tena!!


*******


UNAPOKUWA katika tatizo la aina yoyote ile, lazima unakuwa mtu wa kujishtukia. Kila kitu kwako kinakuwa ni adui. Hautakuwa na amani moyoni mwako na imani kwa kila mtu inapooza.
Ni hali hii ilikuwa inamkabili bwana Emma. Huku akiwa na taarifa kuwa Mwanaidi alikuwa huru, huku akijua fika kuna siri nzito anaimiliki moyoni mwake, hakutaka kumuamini mtu yeyote kwani aliamini kila mmoja ni adui na kwa namna moja au nyingine anaweza kuwa anashirikiana na polisi kuweza kumkamata. Jambo ambalo hakutaka kabisa litokee.
Umakini huu alifika nao feri, hakutaka kukurupuka na kuanza kumsaka Mwanaidi. Aliamua kuwa kimya na muangalifu ili aweze kufanya msako wa hayawani!!
Utulivu wake ukampa majibu mapema.
Alipoiona pajero nyeupe ikitafuta mahali pa kuegesha alisita kushuka garini. Kupitia vioo vilivyowekewa utepe mweusi wa kuzuia aliyeko nje asione ndani. Emma aliweza kushuhudia namba za gari alizokuwa anazifahamu. Zilikuwa namba za Mwanasheria.
Emma alivuta subira na hatimaye aliyekuwa ndani akashuka. Hakika alikuwa mwanasheria kindo.
Baada ya mwanasheria kutembea hatua kadhaa. Emma naye alishuka.
Akaanza kumfuatilia. Alikuwa makini asionekane kama anayefuatilia jambo.
Aliweza kumuona akiongea na watoto kadhaa waliopo maeneo ya feri na hatimaye alikutanishwa na mtu mwingine. Huyu walionekana kufahamiana. Baada ya mazungumzo marefu wakaongozana hadi wakaifikia gari wakaingia ndani. Gari ikawasha injini na kuanza kuondoka.
Emma alijipongeza kwa kutumia gari ambayo haikuwa ikijulikana sana na watu hivyo hata alipoamua kumfungia tela bwana Kindo hakuwa na mashaka kabisa.
Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kwa kawaida huwa haina msongamano mkubwa wa magari na isitoshe siku hii ilikuwa ya mapumziko.
Hivyo Emma hakupata tabu kumfuatilia Kindo ili ajue mwisho wake.
Safari ya waliomtangulia ikaishia Kinondoni kituo cha Studio, wakaingia upande wa kulia na kupaki gari. Emma akawapita kidogo naye akapaki kwa mbele zaidi. Alikuwa anatumia kioo cha pembeni kutazama wawili hawa walipokuwa wanaelekea.
Aliamini kabisa kuwa mwanasheria alikuwa amemgeuka. Na kama ni hivyo basi kwa namna yoyote alikuwa anafahamu wapi yupo Mwanaidi.
Emma alipotelemka garini aliingia dukani akanunua miwani kubwa. Akaiweka machoni. Kasha upesi akaanza kuwafuatilia wawili hawa bila wao kujijua.
Waliposimama na kuanza kuelekezana pia alikuwa makini kuwatazama. Kasha mwanasheria akatoa kiasi cha pesa na kumkabidhi yule kijana. Akatoweka.
Wakati anaondoka alipishana na Emma.


Hatua kwa hatua hatimaye wakaifikia nyumba ya kulala wageni yenye hadhi ya kawaida. Kindo akaingia. Emma anaye kwa ukaribu akaingia. Akajiweka mapokezi isiyokuwa na wahusika kisha kwa makini kabisa akatega sikio na kusikiliza hatua za Kindo zinaishia wapi.
Mahesabu sahihi kabisa, chumba namba kumi na nane (18) !!
Alisimama mlangoni kwa dakika kadhaa akasikia mazungumzo kati ya mwanaume na mwanamke mwenye wasiwasi wa hali ya juu.
Ngoja ngoja yaumiza matumbo!! Alijisemea Emma, kisha akaufungua mlango akaingia ndani, ana kwa ana na mwanasheria Kindo.


Kati ya jambo ambalo mwanasheria hakulitegemea ni kufungiwa tela na Emma bila kujijua. Mshtuko alioupata alitamani iwe ndoto lakini haikuwa.
Emma alikuwa katika munkari ya kufanya lolote ilimradi aweze kuitetea heshima yake mtaani. Hata kuua kwake ilikuwa sahihi kwa wakati ule. Alipotembea na kisu hakuwa amefanya bahati mbaya.
"Umekuja kufanya nini huku?" aliuliza Emma huku akiwa anatetemeka.
Kosa alilofanya mwanasheria bila kutegemea ni kuamini kuwa anaweza kutumia maneno yake ya kisheria kumhadaa Emma.
"Bwana Emma unamfahamu vipi huyu mama hapa kitandani na yule binti..ambaye…" kabla hajamalizia. Bwana Emma akachomoa kile kisu kutoka katika kiuno chake.
Mwanasheria akatumbua macho.
"Ulikuja kufanya nini na Mwanaidi yupo wapi?" aliulizwa.
Jibu lilipoonekana kuwa mbali sana. Emma aliamua kujichagulia jibu.
Akamrukia. Kisu kikazama alipohitaji. Yule mama pale kitandani akapiga kelele mara moja na kupoteza fahamu damu iliporuka juu ikitokea katika kifua cha Kindo, aliyekuwa mwanasheria kabla ya haya mauti.
Simu ya mkononi ndiyo iliyomgutusha Emma aliyekuwa ameganda kana kwamba hakutegemea kama anaweza kufanya jambo kama lile.
"Nani Mama Jenny amekuwaje…." Aliuliza, akathibitishiwa kilichotokea nyumbani.
Ilikuwa ni taarifa kuhusu mkewe ambaye alikuwa epooza upande mwa mwili, baada ya kuwa amepewa taarifa ya mauzauza na Mwanaidi.
Hakika alikuwa anmpenda sana mke wake.
Alisahau yote aliyokuwa anayatetea sasa akauwaza uhai wa mkewe. Akatupa kile kisu bila hata kusafisha alama za vidole, akatoka ndani. Akakimbilia garini, akaondoa kwa mwendo mkali sana huku akimkosakosa msichana aliyevuka bila uangalifu barabarani.


*******


Mwanaidi aligeuka na kuitazama gari iliyomkosa kiduchu kumgonga. Akafanya ishara ya dua, akaisindikiza kwa macho hadi ilipotokomea.
"Kuna watu wanaendesha hovyo..au ni mimi mawazo yangu!!" alijiuliza. Kisha akapuuzia akaendelea na safari yake, moyo ukiwa bado unamdunda. Kwanza kwa hali iliyomkuta mama Emma kule nyumba kisha kukoswakoswa na gari sentimeta chache.
Akaingia hadi ndani. Akapigwa na mshtuko tena. Mlango wa chumba chake ulikuwa wazi.
Nani ameufungua!! Alijiuliza huku akiingia kwa umakini mkubwa.


Maajabu mengine makubwa kubebeka.
Picha ya mama Emma akiwa anatokwa jasho, kukoswakoswa na gari, mlango kwa wazi na sasa anashuhudia damu.
Alitokwa na yowe moja kubwa kisha akazirai.
Aliporejewa na fahamu alikuwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Mauaji ya mwanasheria aliyeheshimika sana yalikuwa yanamuhusu.
Mwanaidi alijikuta akikata tama na kuamini sasa harakati zake zimefikia kikomo. Yote aliyoyahangaikia yameishia hapa alipofikia.
Hakuna wa kumpigania mtaani. Ni nani atakayemtetea.
Pingu zikaiunganisha mikono yake. Akapandishwa katika gari ya polisi.
Safari ya kuelekea rumande!!
Harakati za chokoraa zikaingia doa. Mkono wa dola ukamnasa.


***Ni nani wa kuuweka ukweli wazi tena. Mwanaidi aliyekuwa katika harakati za kuwakomboa wenzake sasa ametiwa hatiani….je FRIDA na ISHA mwisho wao ni gerezani????


***EMMA na uovu wake…je atasalimika……vipi kuhusu mama George naye?????


VAN HEIST muuza ubuyu amina mabata shabani hassani culbby sam II ram BPM mbalu saljar MAVUNO Nyamonoro
 
Last edited by a moderator:
Aisee...... So sad but kila lenye mwanzo lina mwisho
 
RIWAYA: CHOKORAA
MTUNZI: George Iron Mosenya




SEHEMU YA KUMI NA SITA


Akaingia hadi ndani. Akapigwa na mshtuko tena. Mlango wa chumba chake ulikuwa wazi.
Nani ameufungua!! Alijiuliza huku akiingia kwa umakini mkubwa.


Maajabu mengine makubwa kubebeka.
Picha ya mama Emma akiwa anatokwa jasho, kukoswakoswa na gari, mlango kwa wazi na sasa anashuhudia damu.
Alitokwa na yowe moja kubwa kisha akazirai.
Aliporejewa na fahamu alikuwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Mauaji ya mwanasheria aliyeheshimika sana yalikuwa yanamuhusu.
Mwanaidi alijikuta akikata tama na kuamini sasa harakati zake zimefikia kikomo. Yote aliyoyahangaikia yameishia hapa alipofikia.
Hakuna wa kumpigania mtaani. Ni nani atakayemtetea.
Pingu zikaiunganisha mikono yake. Akapandishwa katika gari ya polisi.
Safari ya kuelekea rumande!!
Harakati za chokoraa zikaingia doa. Mkono wa dola ukamnasa.


*****


Emmanuel aliwasili hospitali saa moja baadaye akiwa amepita njia za uchochoro hapa na pale kuweza kuikwepa foleni ambayo haikuwa ya kutisha sana. Mwanzoni hakufahamu iwapo mkewe alikuwa amefikishwa hospitali, taarifa hiyo aliipata baada ya kufika nyumbani.
Aliambiwa msaidizi wa kazi za ndani.


Sasa alikuwa hospitali na kama alivyoambiwa awali kuwa mkewe yupo hoi. Kweli alikuwa hoi. Tena aliyepooza.
Emma alichanganywa na habari hii. Alijaribu kuuliza huku na kule hatimaye mwanaye wa kumzaa alimueleza juu ya ujio wa binti aliyeitwa Mwanaharusi.
"Sasa alimfanya nini hadi akawa hivi." Emma aliuliza swali la kijinga wakati tayari alikuwa ameelezwa kuwa hakuna aliyeshuhudia tukio hili moja kwa moja. Bali wamemkuta mgonjwa katika hali mbaya zaidi ya hiyo aliyokuwa nayo wakati ule. Hakupata jibu.
Akahaha huku na huko. Bado hali haikuwa shwari.
Hospitali aliyolazwa mama Emma haikuwa mbali sana ana alipolazwa George asiyejitambua.
Huduma za madaktari ziliendelea kwa kasi ili kuokoa uhai huu.


Muda ulikwenda upesi sana. Msongo wa mawazo ukiwa umekijaza kichwa cha Emma. Siri na hatia kubwa aliyoandamana nayo ikaanza kumzidia. Alitamani kumshirikisha mtu lakini alikuwa amechelewa sana. Alikuwa ameua tayari!!.
Emma alikumbuka kuiangalia saa yake baadaye sana. Akagutuka ilikuwa saa tatu usiku!!
Akili ikafyatuka. Ikakimbia maili mia nyuma. Akakumbuka kitu!!
Sharti!!
Sharti alilopewa na mganga wa kienyeji. Muda ulikuwa unakaribia!!


Hakuna kitu kibaya kama kumtegemea mwanadamu katika jambo lolote lile na kumkabidhi maisha yako akuongoze. Kosa hili lilifanywa na mtu mzima huyu aliyehitimu chuo kikuu kasha kuwa mzembe katika kuisaka ajira hatimaye akajiingiza katika vitendo vya kishirikina.
Sasa ule utajiri wa kupewa na mwanadamu ukaanza kumtafuna.
Emma akaanza kulia. Waliomtazama walidhani anamlilia mkewe, lakini akilini alikuwa analia kilio cha majuto ambaye sasa anadeka kama mjukuu. Majuto ambaye hakutambuliwa wakati safari inaanza amejitokeza wakati huu mbaya.
Alikuwa na masaa matatu tu!!
Kuuondoa uhai wa mama George, kasha baada ya hapo atakuwa huru.
Atampatia wapi sasa mama George?? Hilo lilikuwa swali.


Emma akasimama wima kama mwendawazimu. Akaifikia gari yake. Akaingia ndani na kuiwasha kasha kwa mwendo wa kasi akaanza kuitafuta barabara ya Bagamoyo. Aweze kumuwahi mganga na kumwomba amuongezee muda. Hali ilikuwa tete.
Safari ilianza vyema sana. Lakini siku ya kufa nyani, miti yote huteleza. Na vita ya ardhini haiwezi.
Polisi wa usalama barabarani wenye njaa kali walimsimamisha.
Lahaula!! Alikuwa hajatembea na leseni wala kadi gari. Na kibaya zaidi alikuwa na kiasi kidogo sana cha pesa ambacho kisingewatosheleza askari wale kupeleka mboga nyumbani kwa ajili ya siku inayofuata.
Maneno matupu hayavunji mfupa!! Alibembeleza sana.
Walimwachia baada ya kuwaachia simu yake kama dhamana.
Dakika thelathini zikatokomea.


Sasa aliweza kuondoka.
Wakati Emma anaondoka. Kitanda kilichotulia kwa muda mrefu sasa kiliweza kuchezacheza kwa kiasi Fulani. Kasha kikacheza sana. Macho yakafunguka.
"George…..George yupo wapi." Mwanamke aliyepooza upande mmoja aliuliza. Nesi wa zamu akatabasamu!! Mwanamke akaendelea kuuliza.
Hapo sasa akaitwa ndugu yake!! Swali lilikuwa lile lile.
"Namuhitaji hapa sasa hivi." Aliamrisha.
Yule mtoto akatoweka na kwenda katika hospitali aliyokuwa amelazwa George.
Ilikuwa saa tano kamili usiku. George akashtuka kutoka katika usingizi wake wa kifo. Akaangaza huku na huku. Ile akili yake iliyofungwa na mwanadamu, ikawa huru.
Binadamu aliyeahidi kumuachia George akamuachia kweli baada ya muda wa masharti kupita.
Lile gogo pale kitandani. Likakaa kitako.
Hapakuwa na mtu chumbani. Na hakuna aliyetegemea gogo lile ipo siku litazinduka.
Aliyeagizwa akakumbana na maajabu haya.
George hakuwa chumbani!!
Nesi wa zamu na daktari aliyekabidhiwa jukumu la kulinda gogo lile kwa siri wakapigwa butwaa.
Daktari akajaribu kumpigia simu Emmanuel ili kumpa taarifa hii ya maajabu. Hakumpata hewani.
Hofu!!




*******


Mimi ni chokoraa!! Ni neno la kwanza alilokiri baada ya kuingia mtaani. Akili yake ilikuwa nyepesi sana. Tofauti na awali.
Mambo yote aliyoayaishi akiwa katika usingizi mzito lakini akinyanyaswa na sura ya Emmanuel ilimpatia picha ya yeye ni nani.
Emmanuel hakuwa mtu mzuri. Alikuwa ni shetani.


George akiwa ananuka madawa ya hospitali anaingia mtaani. Mtaa ambao alikuwa ni nia kubwa ya kuuokoa sasa anaingia akiwa anahitaji kuokolewa.
Frida, Isha, na Mwanaidi. Hili likawa wazo la kwanza juu ya wapi pa kuanzia aweze kupata hifadhi na kuusema ukweli wote anaoufahamu. Alihitaji kuusema ukweli huu ili amtie hatiani Emma aliyekuwa akimnyanyasa katika kijiji cha maajabu asichokijua.
Simulizi za akina Frida zilimbeba sana na kujua jinsi gani ya kuishi na watoto wa mitaani ili wasikuone kuwa u mgeni sana eneo lao. George hakutaka kujulikana kama yule George mtoto wa kitajiri. Hakutaka kuheshimika mtaani, alitaka kuishi alivyotakiwa kuishi.
Alitaka kuishi kichokoraa na afe akiwa chokoraa. Kama alivyozaliwa na kuamini kuwa alitupwa.
Usiku huu ukawa mwanzo wa safari ya George kuishi kichokoraa, ile hali ya kulala kitandani muda mrefu, kukosa chakula bora mtaani. Mabega yakapanda juu, macho yakabonyea ndani.
Watoto wa mtaani wakampachika jina jipya kabisa. Bonge!! Ikiwa ni utani wa waziwazi.
Bonge alikuwa mcheshi, asiyependa makuu, mkarimu. Na alionekana kama wa maajabu kwa jinsi alivyokuwa tayari kuwatetea wenzake hata mbele ya mgambo wa jiji. Alikuwa na majibu ambayo yaliburudisha masikio ya mgambo wa jiji na kushusha hasira zao.
Bonge alikuwa ni mtunzi wa hadithi na aliyajua maneno ya kuiteka hadhira yake.


Ni nadra sana kwa watoto wa mtaani kuheshimiana, lakini katika kempu hii ya Kariakoo mtaa wa gerezani heshima ilikuwepo. Kila mmoja kwa wakati wake alijikuta akimuheshimu mwenzake kutokana na nasaha za George ambaye alizoeleka kama Bonge.
Bonge aliyafurahia haya maisha.


Bonge naye ni mwanaume, tena mwenye hisia, japo moyo wake mkubwa uliwahi kumsumbua na kuingilia kipaji chake cha kucheza soka. Hii haikuwa na maana moyo ule ulipigwa ganzi katika suala la hisia.
Usiku huu palikuwa na baridi kali haswa. Handaki dogo walilokuwa wamejihifadhi watoto hawa wasiokuwa na kwao, lilipenyeza upepeo uliozidi kuwasulubisha. Bonge alikuwa kimya sana tofauti na kawaida yake ya kuwa msema mengi ili kuwaliwaza chokoraa wenzake.
Akiwa ametulia tuli. Alivamiwa na pepeo la maajabu, akahisi upweke na kujiona kuwa kuna kitu alikuwa anahitaji. Alihitaji joto.
Pepo la ngono likampanda bila kutarajia. Tena katika mzingira ya kustaajabisha.
"Kelvin…Kelv…" Bonge aliita kwa kunong'ona. Kelvin aliyekuwa anahangaika kuusaka usingizi aligeuka bila kusema lolote.
"Hivi Regina analala chimbo lile la ng'ambo bado."
"Mh!! Analala palepale vipi kwani."
"Aaah!! Basi tu..lala" alisema Bonge.
Kelvin hakujali akaendelea kuusaka usingizi.
Bonge akasimama kimya kimya. Akatoweka, hadi ng'ambo. Akamshtua Regina. Regina akaitikia wito.
Bonge akajielezea dhahiri kuwa amezidiwa. Regina akacheka sana kwa sauti ya chini. Hakuamini kama Bonge ana uhitaji huo.
"Namaanisha Regina kama una kiumbe nisaidie lakini usiambie mtu." Alisihi Bonge.
"Nisubiri pale ‘chemba' Bonge la bwana." Aliongeza nakshi katika lile jina. Wote wakacheka.
"Regy…..asiwe ananijua…" alitoa maelekezo Bonge.


Kisha akachukua nafasi katika chemba aliyoelekezwa. Baada ya muda akasikia hatua zikijongea eneo lile.
Mapigo ya moyo ya Bonge yakaongezeka huku tama nayo ikichukua nafasi.


*******




*****


Mcha Mungu kamwe hawezi kumficha mwovu.
Licha ya kukosa nafasi ya kuzungumza na George baada ya kuwa amerejewa na fahamu. Hakusita kuuelezea umma juu ya kilichojiri, hasahasa polisi ambao walichukulia hili jambo uzito.
Emma alitoweka kwa siku tatu. Siku zisizokuwa na mafanikio.
Alirejea nyumbani kisirisiri ili kuchukua pesa katika amana zake ili aweze kumpatia mganga waendelee na zoezi la kumsaka George ambaye alikuwa ameachwa huru.
Siku aliyorejea kwake ikawa siku ya mwisho kuwa huru mtaani.
Mama mcha Mungu. Akauweka uongo kando akayatua mapenzi ya kupendana na mfuasi wa shetani. Akatoa taarifa polisi.
Bwana Emma akakamatwa.
Ikiwa ni mara yake ya kwanza kulala rumande tangu azaliwe.


Maswali mawili matatu ya mitego. Akanasa.
Makofi mawili matatu. Akausema ukweli.
Kipigo kitakatifu akakiri kuwa alimuua Mwanasheria Kindo.


Salamu za kushangaza tena za wakati muafaka zikawafikia wale wanaoonewa gerezani. Mwanaidi, Frida na Isha. Wote wakaachiwa huru. Aliyetakiwa amepetikana. Chokoraa wasiokuwa na hatia wakarejea mtaani. Bado hakuwepo wa kuwapokea, ni mtaa uleule usiobadilika ukawasabahi.
Kila mmoja alitolewa kwa wakati wake.
Mwanaidi kivyake lakini Frida na Isha walioshtakiwa kwa kosa moja waliachiwa pamoja.
Ilikuwa majira ya mchana. Wakaingia tena mtaani wakiwa hoi. Lakini huru.
Mtaa mmoja baada ya mwingine, hatimaye mguu wao wa mwisho unaishia mtaa wa Kariakoo gerezani.
Ni hapa waliamini wanaweza kujihifadhi na wenzao.
Usingizi wa mang'amung'amu unakatizwa na amri kutoka kwa dada mkubwa wa kempu.
Frida akiwa amesinzia, Isha anaamshwa na kuamriwa afunge tela amfuate dada mkubwa.
Safari yao inaishia katika chemba yenye giza.


Anasukumiwa ndani, anapokelewa na mikono kakamavu ya kiume. Hakuna mazungumzo
Anajua nini kinachoendelea binti huyu analia kwa kusihi, "Kondomu…kondomu…." Kinga pekee ndiyo msaada anaoamini anaweza kufanyiwa lakini sio chokoraa kusamehewa katika kubakwa. Ni kawaida yao kubakwa. Wanaonewa.
Mwanaume anasita kwa muda anafanya tafakari kilio kile cha mwanamke. Tamaa inazidi nguvu maamuzi. Anamkumbatia yule msichana aliyekondeana.
"Bonge kuna UKIMWI…kuna kisonono, kuna fangasi…Bonge…Bonge!! Shauri zako." Sauti ilimwambia katika nafsi yake. Akatamani kuacha lakini alikuwa amtamanika tayari!! Angefanya nini.
Akaitawanya kanga ya yule binti. Akaanguka naye chini. Badala ya kutua chini wakatua katika kitu kingine. Kikaunguruma.
Wakatulia. Bonge suruali magotini, binti kanga pembeni.
Kikaunguruma tena.
Hapa sasa Bonge akawa mwanariadha mzuri, huku Isha akimfuatia kwa kasi.
Walienda pande mbili tofauti.
Dada mkubwa Regina naye alishtushwa na hali hii. Chokoraa hana ngojangoja. Naye akatimua mbio.
Walifurahisha kuwatazama.


****Ni kitu gani kimekatisha dhambi hii ya CHOKORAA…….


****BONGE, ISHA NA MWANAIDI NA FRIDA je wataonana tena!!


VAN HEIST muuza ubuyu amina mabata shabani hassani culbby sam II ram BPM mbalu saljar MAVUNO

 
Back
Top Bottom