Riwaya: Chokoraa

Riwaya: Chokoraa

Hii utakua hujaiona, ukiipenda kesho ntakutumia muuza ubuyu

SIMULIZI: SAFARI NDEFU KUELEKEA KABURINI
MTUNZI: Nyemo Chilongani

SEHEMU YA KWANZA

Muda ulikuwa ukizidi kwenda mbele huku dereva wa gari ndogo aina ya Prado akiwa amesimama nje ya gari hilo huku akimsubiri msichana mrembo, Patricia Thomson aweze kutoka ndani ya nyumba yao na hivyo kuanza safari ya kuelekea shuleni alipokuwa akisoma kidato tatu, Salma Kikwete Secondary School iliyokuwa Kijitonyama. Muda ulikuwa ukizidi kwenda lakini bado Patricia alikuwa ndani akiendelea kujiremba, bado alikuwa akiendelea kujipaka mafuta ya gharama pamoja na kujipulizia manukato ya bei kubwa.
Muda mwingi dereva wa gari lile, Sam alikuwa akipiga honi kama hatua moja ya kumfanya Patricia ndani alipokuwa afanye haraka lakini hiyo wala haikuweza kusaidia. Bado Patricia alikuwa akiendelea kujiremba kana kwamba honi zile ambazo zilikuwa zikiendelea kupigwa hakuwa akizisikia masikioni mwake.
“Mbona unamchelewesha mwenzio?” Bi Beatrice alimuuliza Patricia mara alipoufungua mlango wa chumba cha binti yake.
“Nakuja mama. Kuna kitu namalizia” Patricia alimwambia mama yake huku akiendelea kujiremba.
Zilipita dakika thelathini na ndipo Patricia alipomaliza kujiremba na hivyo kutoka ndani ya chumba kile. Kitu cha kwanza alichokifanya ni kumfuata mama yake sebuleni alipokuwa na kisha kumbusu na kumuaga. Bi Beatrice alibaki akimwangalia Patricia huku uso wake ukiwa na tabasamu pana, uzuri wa binti yake ulionekana kumvutia hata yeye mwenyewe.
Patricia akaingia garini bila ya kumsalimia Sam ambaye alionekana kukasirika. Akajifunga mkanda na kutulia kimya mpaka pale Sam alipoingia garini na kasha kuwasha gari na kuliondoa mahali hapo. Ukimya mkubwa ulikuwa umetawala garini, Patricia hakutaka kuongea kitu chochote kile kwani aliamini kwa kile alichokuwa amekifanya cha kuchelewa kutoka ndani ya chumba chake kilikuwa kimemkasirisha Sam.
“Naomba unisamehe kaka Sam” Patricia alimwambia Sam ambaye alionekana kuwa bize na usukani.
Patricia akaonekana kuumia, ni kweli alijua kwamba alikuwa amefanya kosa na ndio maana kwa wakati huo alikuwa radhi kuomba msamaha lakini ukimya wa Sam ukaonekana kumuumiza, hakupenda kumuomba msamaha mtu halafu asijibu kitu chochote kile, alipenda kusikia Sam akiongea neno lolote lililomaanisha kumsamehe kwa kile alichokifanya cha kumchelewesha.
“Naomba unisamehe kaka Sam” Patricia alimwambia kwa mara nyingine tena.
“Nimekwishakuzoea Pat” Sam alimwambia Patricia.
“Hapana. Usiseme hivyo kaka. Nakuahidi sitokuchelewesha tena” Patricia alimwambia Sam.
“Sawa. Hakuna tatizo. Nimekusamehe” Sam alimwambia Patricia huku tayari wakiwa wamekwishafika Magomeni Morocco. Kidogo Patricia akaonekana kuwa na furaha moyoni mwake, kitendo cha Sam kumsamehe kilionekana kumfariji, amani ikaanza kumjaa moyoni mwake.
Patricia Thomson alikuwa msichana mrembo ambaye alikuwa na mchanganyiko wa rangi huku baba yake akiwa mzungu kutoka nchini Marekani na mama yake akiwa Mtanzania mweusi kutoka mkoani Kilimanjaro. Wazazi wake walikutana miaka kadhaa iliyopita mkoani Arusha na hivyo kukutana kimwili nay eye kuzaliwa miaka kumi na saba iliyopita.
Baada ya Patricia kuzaliwa, Bwana Thomson hakuendelea kukaa nchini Tanzania, akaamua kurudi nchini Marekani kuendelea na kazi zake katika jiji la Washington. Kutokana na ubize mwingi ambao alikuwa nao katika kazi zake wala hakupata nafasi ya kurudi nchini Tanzania, aliendelea kuishi kwa miaka mingi zaidi huku ni mara chache sana akiwasiliana na mzazi mwenzake, Bi Beatrice kwa ajili ya kujua hali ya binti yake.
Katika kipindi kirefu cha maisha yake, Patricia alikuwa amelelewa na mama yake, Bi Beatrice. Alimfahamu vilivyo baba yake kutokana na picha kadhaa ambazo alikuwa nazo na hata mzee huyu wakati mwingine kuja nchini Tanzania katika kipindi ambacho alikuwa na miaka kumi na nne.
Mara kwa mara alikuwa akiwasiliana na baba yake ambaye alikuwa akimtaka sana kuelekea nchini Marekani kuishi nae lakini Beatrice alikuwa akikataa katakata. Kamwe hakutaka kuelekea nchini Marekani, alitamani kuendelea kubaki nchini Tanzania pamoja na mama yake ambaye alikuwa amemzoea kuliko mtu yeyote yule.
Ni kweli kuna wakati alikuwa akitamani sana kukaa pamoja na baba yake lakini kila alipokuwa akimfikiria sana mama yake, wala hakutaka kuishi mbali nae, bado alijiona kuwa na uhitaji mwingi wa kuendelea kukaa pamoja na mama yake. Mzee Thomson hakuishia hapo, bado alikuwa akimhitaji binti yake aende akaishi nae nchini Marekani pamoja na kuwaonyeshea wazazi wake msichana ambaye alizaa pamoja na mwanamke wa Kiafrika. Beatrice haku wa na jinsi, kitu alichokifanya ni kumuahidi baba yake kwamba ni lazima angekwenda kuishi nchini Marekani mara tu atakapomaliza kidato cha nne.
Ahadi hiyo alikuwa amempa baba yake mwaka jana katika kipindi ambacho alikuwa kidato cha pili na hiyo ilimaanisha kwamba ulikuwa umebakia mwaka mmoja tu hata kabla hajaenda nchini Marekani kuanza maisha mapya pamoja na baba yake, Bwana Thomson.
Bwana Thomson hakutaka binti yake, Patricia aishi maisha ya tabu jambo ambalo lilimfanya kila mwezi kutuma zaidi ya dola elfu tatu, zaidi ya milioni nne na nusu kwa ajili ya matumizi ya binti yake pamoja na Bi Beatrice. Patricia alikuwa na uhuru wa kuishi maisha ya kifahari ambayo alikuwa akijisikia kuishi lakini wala hakupenda kuishi maisha hayo hata kidogo.
Kutokana na kusoma shule za gharama ya juu kuanzia darasa la kwanza mpaka darasa la saba, Patricia hakutaka tena kusoma katika shule za aina hiyo jambo lililomfanya kidato cha kwanza kuanza katika shule ya Sekondari ya Salma Kikwete iliyokuwa Kijitonyama
Aliishi maisha ya kifahari, na sasa alijiona kuwa na nafasi ya kutamani kuishi pamoja na watu ambao walikuwa wametoka katika familia za chini. Hiyo ndio ilikuwa sababu kubwa iliyomfanya kuanza kusoma katika shule hiyo ya mchanganyiko na kukutana na wanafunzi ambao walikuwa wakiishi maisha ya chini kabisa.
Patricia hakupenda kabisa kupelekwa na gari shuleni lakini mama yake hakutaka kukubaliana na suala hilo, kwake, Patricia alikuwa kila kitu, hakutaka apate shida ya aina yoyote ile na wala hakupenda binti yake atumie mwendo mkubwa ardhini na wakati alikuwa na uwezo wa kuzuia jambo hilo.
Msichana huyu, Patricia ndiye ambaye alikuwa akiongoza kwa uzuri shuleni hapo. Alikuwa akionekana msichana wa tofauti, mchanganyiko wa rangi ambao alikuwa nao ulimfanya kuvutia zaidi. Kila mwanafunzi alitamani kuwa pamoja na Patricia ambaye alikuwa amefanana sana na mwanamuziki wa kike, Alicia Keys kwa kila kitu kana kwamba walikuwa mapacha.
Patricia hakuwa msichana wa majivuno, alikuwa akiishi maisha ya kawaida shuleni, alichangamana na kila mwanafunzi ambaye alikuwa akihitaji urafiki pamoja nae. Japokuwa wavulana wengi walikuwa wakitamani kumtongoza Patricia lakini walionekana kutokuwa na nguvu za kufanya jambo kama hilo kutokana na ukaribu mkubwa ambao alikuwa nao Patricia kwao.
Patricia akawa akipendwa sana na kila mwanafunzi shuleni hapo isipokuwa baadhi ya wasichana ambao walikuwa wakijiona kuwa bora zaidi yake. Patricia hakutaka kujali kitu chochote kile, kwake, heshima na kuwathamini watu wengine ndio aliliona jukumu lake alilokuwa nalo.
Uwezo wake darasani wala haukuwa mkubwa sana japokuwa alikuwa akifahamu mambo mengi kutokana na kununuliwa vitabu vingi vya kujisomea. Kile ambacho hakuwa akikifahamu, alikuwa akifundishwa na wanafunzi wengine na hata vile ambavyo alikuwa akivifahamu basi alikuwa akiwafundisha wanafunzi wengine.
“Ni msichana mzuri sana. Hapana, acha mimi nijaribu kuwa nae” Martin aliwaambia wanafunzi wenzake.
“Acha utani bwana. Hebu muangalie Patricia halafu jiangalie wewe. Mnaendana?” Juma alimuuliza Martini.
Martin akayapeleka macho yake mwilini mwake, miguuni alikuwa na kandambili huku miguu yake ikiwa michafu kutokana na kucheza mpira pekupeku katika kipindi cha mapumziko. Akayaamisha macho yake na kuyapeleka katika shati lake, shati lilikuwa limechakaa, chafu huku likiwa limechanika makwapani. Kila alipokuwa akijiangalia, kulikuwa na utofauti mkubwa sana na Patricia.
“Mmhh!” Aliguna.
“Vipi tena?” Ashrafu aliuliza.
“Mmesema kweli. Manake kila nikijiangalia sipati jibu kama mimi ni mwanadamu au mnyama aliyeachwa porini” Martin aliwaambia na wote kuanza kucheka.
Martin ndiye alikuwa kijana ambaye alikuwa akivutiwa sana na Patricia kuliko mvulana yeyote shuleni hapo. Kila siku alikuwa akipenda kumwangalia Patricia, moyo wake ukatokea kumpenda sana msichana huyo kiasi ambacho kama ilipita siku pasipo kumuona basi alikuwa akipata shida sana usiku.
Alitamani kumfuata Patricia na kumwambia ukweli kwamba alikuwa akimpenda sana lakini hakujua ni wapi alitakiwa kuanzia. Maisha yake yalikuwa ya kimasikini sana, ingawa alikuwa akikaa mbali na shuleni hapo lakini kila siku alikuwa akienda shuleni hapo kwa miguu. Si kwamba hakuwa akipenda kupanda daladala, alikuwa akitamani lakini umasiki ulikuwa umeitawala familia yao.
Hakujua mwendelezo wa maisha yake ya mbele ungekuwaje hapo baadae. Njia za kutoka kimaisha zikawa zimekwisha akilini mwake jambo lililomfanya kuanza kufikiria kufanya muziki. Kila siku shuleni alikuwa akiandika mistari ya muziki aina ya RnB huku akiwaimbia wanafunzi wenzake.
Baada ya miezi miwili kupita, shule nzima ikajua kwamba mwanafunzi masikini asiyekuwa na mvuto wowote ule, Martin alikuwa mwanamuziki chipukizi ambaye hakuwa na mbele wala nyuma. Walimu walijaribu kumuita ofisini na kumshauri kwamba ingekuwa vizuri kama angetilia maanani masomo lakini Martin hakuonekana kujali, kitu alichokuwa akikitaka ni kuwa mwanamuziki mkubwa wa muziki tu.
“Kila ninapomsikiliza R Kelly, ananitia mzuka sana” Martin aliwaambia wanafunzi wenzake.
“Unataka kuwa kama yeye?”
“Unaulizia chumvi baharini. Ndio, ninataka kuwa kama yeye” Martin alijibu.
Hizo ndizo zilikuwa ndoto zake za kila siku, aliupenda sana muziki kwani aliamini kwamba huo ndio ungekuwa njia ambayo ingemfanya kutoka kimaisha na kuwa mwanamuziki mkubwa ambaye angekuja kuwa na fedha nyingi hapo baadae.
Ingawa alikuwa akiendelea na juhudi zake za kutunga nyimbo mbalimbali lakini bado ndoto yake ya kuwa na msichana Patricia ilikuwa kichwani mwake, alikuwa akimhitaji sana msichana huyo kiasi ambacho usiku kwake ulikuwa ukionekana kuwa wa shida sana. Alitamani kumfuata na kumwambia kile ambacho alikuwa akijisikia moyoni mwake juu yake lakini alionekana kuogopa.
Kwanza kila alipokuwa akiiangalia hali yake, hakuamini kama msichana Patricia angekubali na kuwa nae. Alijidharau sana na kutokuamini kama alistahili kuwa na msichana huyo. Kwake, kuwa na msichana Patricia ilionekana kuwa kama ndoto ya mchana wa saa saba.
Kila alipokuwa akifikiria utofauti mkubwa ambao ulikuwepo kati yake na Patricia, wala hakutamani kuwa pamoja nae, aliona ni bora kuendelea kutunga muziki ili kama kungekuwa na siku angekuja kupata fedha, kurekodi na kuwa maarufu basi isingekuwa jambo gumu kumpata Patricia. Kwake aliona fedha kuwa kila kitu katika maisha yake, kutokuwa na fedha kulionekana kuwa tatizo kubwa ambalo lilikuwa likimkosesha kufanya jambo lolote la maana.
“Ngoja niachane nae na nijiingize moja kwa moja kwenye muziki. Naamini kuna siku utanitoa tu, na hapo ndipo nitakapokuja kumwambia Patricia ukweli kwamba sinywi, sili wala silali kwa ajili yake. ....mwisho wa siku nakuja kumuoa. Hahahahaha...Sijui itatokea au ndio ndoto za mchana. Ila poa. Mziki kwanza halafu mapenzi baadae” Martin alijisemea katika kipindi ambacho Patricia alikuwa akipita mbele yake pamoja na wanafunzi wengine wa kike.

Je ni nini kitaendelea?
Je uamuzi aliouchukua Martin utaweza kudumu moyoni mwake?
Je nini kitaendelea katika maisha ya watu hawa hapo baadae?
Itaendelea

mkuu naomba unitiunitmie hii kitu nimeitafuta sana bila mafanikio. tafadhali kama unayo naom
 
Last edited by a moderator:
Hii utakua hujaiona, ukiipenda kesho ntakutumia muuza ubuyu

SIMULIZI: SAFARI NDEFU KUELEKEA KABURINI
MTUNZI: Nyemo Chilongani

SEHEMU YA KWANZA

Muda ulikuwa ukizidi kwenda mbele huku dereva wa gari ndogo aina ya Prado akiwa amesimama nje ya gari hilo huku akimsubiri msichana mrembo, Patricia Thomson aweze kutoka ndani ya nyumba yao na hivyo kuanza safari ya kuelekea shuleni alipokuwa akisoma kidato tatu, Salma Kikwete Secondary School iliyokuwa Kijitonyama. Muda ulikuwa ukizidi kwenda lakini bado Patricia alikuwa ndani akiendelea kujiremba, bado alikuwa akiendelea kujipaka mafuta ya gharama pamoja na kujipulizia manukato ya bei kubwa.
Muda mwingi dereva wa gari lile, Sam alikuwa akipiga honi kama hatua moja ya kumfanya Patricia ndani alipokuwa afanye haraka lakini hiyo wala haikuweza kusaidia. Bado Patricia alikuwa akiendelea kujiremba kana kwamba honi zile ambazo zilikuwa zikiendelea kupigwa hakuwa akizisikia masikioni mwake.
"Mbona unamchelewesha mwenzio?" Bi Beatrice alimuuliza Patricia mara alipoufungua mlango wa chumba cha binti yake.
"Nakuja mama. Kuna kitu namalizia" Patricia alimwambia mama yake huku akiendelea kujiremba.
Zilipita dakika thelathini na ndipo Patricia alipomaliza kujiremba na hivyo kutoka ndani ya chumba kile. Kitu cha kwanza alichokifanya ni kumfuata mama yake sebuleni alipokuwa na kisha kumbusu na kumuaga. Bi Beatrice alibaki akimwangalia Patricia huku uso wake ukiwa na tabasamu pana, uzuri wa binti yake ulionekana kumvutia hata yeye mwenyewe.
Patricia akaingia garini bila ya kumsalimia Sam ambaye alionekana kukasirika. Akajifunga mkanda na kutulia kimya mpaka pale Sam alipoingia garini na kasha kuwasha gari na kuliondoa mahali hapo. Ukimya mkubwa ulikuwa umetawala garini, Patricia hakutaka kuongea kitu chochote kile kwani aliamini kwa kile alichokuwa amekifanya cha kuchelewa kutoka ndani ya chumba chake kilikuwa kimemkasirisha Sam.
"Naomba unisamehe kaka Sam" Patricia alimwambia Sam ambaye alionekana kuwa bize na usukani.
Patricia akaonekana kuumia, ni kweli alijua kwamba alikuwa amefanya kosa na ndio maana kwa wakati huo alikuwa radhi kuomba msamaha lakini ukimya wa Sam ukaonekana kumuumiza, hakupenda kumuomba msamaha mtu halafu asijibu kitu chochote kile, alipenda kusikia Sam akiongea neno lolote lililomaanisha kumsamehe kwa kile alichokifanya cha kumchelewesha.
"Naomba unisamehe kaka Sam" Patricia alimwambia kwa mara nyingine tena.
"Nimekwishakuzoea Pat" Sam alimwambia Patricia.
"Hapana. Usiseme hivyo kaka. Nakuahidi sitokuchelewesha tena" Patricia alimwambia Sam.
"Sawa. Hakuna tatizo. Nimekusamehe" Sam alimwambia Patricia huku tayari wakiwa wamekwishafika Magomeni Morocco. Kidogo Patricia akaonekana kuwa na furaha moyoni mwake, kitendo cha Sam kumsamehe kilionekana kumfariji, amani ikaanza kumjaa moyoni mwake.
Patricia Thomson alikuwa msichana mrembo ambaye alikuwa na mchanganyiko wa rangi huku baba yake akiwa mzungu kutoka nchini Marekani na mama yake akiwa Mtanzania mweusi kutoka mkoani Kilimanjaro. Wazazi wake walikutana miaka kadhaa iliyopita mkoani Arusha na hivyo kukutana kimwili nay eye kuzaliwa miaka kumi na saba iliyopita.
Baada ya Patricia kuzaliwa, Bwana Thomson hakuendelea kukaa nchini Tanzania, akaamua kurudi nchini Marekani kuendelea na kazi zake katika jiji la Washington. Kutokana na ubize mwingi ambao alikuwa nao katika kazi zake wala hakupata nafasi ya kurudi nchini Tanzania, aliendelea kuishi kwa miaka mingi zaidi huku ni mara chache sana akiwasiliana na mzazi mwenzake, Bi Beatrice kwa ajili ya kujua hali ya binti yake.
Katika kipindi kirefu cha maisha yake, Patricia alikuwa amelelewa na mama yake, Bi Beatrice. Alimfahamu vilivyo baba yake kutokana na picha kadhaa ambazo alikuwa nazo na hata mzee huyu wakati mwingine kuja nchini Tanzania katika kipindi ambacho alikuwa na miaka kumi na nne.
Mara kwa mara alikuwa akiwasiliana na baba yake ambaye alikuwa akimtaka sana kuelekea nchini Marekani kuishi nae lakini Beatrice alikuwa akikataa katakata. Kamwe hakutaka kuelekea nchini Marekani, alitamani kuendelea kubaki nchini Tanzania pamoja na mama yake ambaye alikuwa amemzoea kuliko mtu yeyote yule.
Ni kweli kuna wakati alikuwa akitamani sana kukaa pamoja na baba yake lakini kila alipokuwa akimfikiria sana mama yake, wala hakutaka kuishi mbali nae, bado alijiona kuwa na uhitaji mwingi wa kuendelea kukaa pamoja na mama yake. Mzee Thomson hakuishia hapo, bado alikuwa akimhitaji binti yake aende akaishi nae nchini Marekani pamoja na kuwaonyeshea wazazi wake msichana ambaye alizaa pamoja na mwanamke wa Kiafrika. Beatrice haku wa na jinsi, kitu alichokifanya ni kumuahidi baba yake kwamba ni lazima angekwenda kuishi nchini Marekani mara tu atakapomaliza kidato cha nne.
Ahadi hiyo alikuwa amempa baba yake mwaka jana katika kipindi ambacho alikuwa kidato cha pili na hiyo ilimaanisha kwamba ulikuwa umebakia mwaka mmoja tu hata kabla hajaenda nchini Marekani kuanza maisha mapya pamoja na baba yake, Bwana Thomson.
Bwana Thomson hakutaka binti yake, Patricia aishi maisha ya tabu jambo ambalo lilimfanya kila mwezi kutuma zaidi ya dola elfu tatu, zaidi ya milioni nne na nusu kwa ajili ya matumizi ya binti yake pamoja na Bi Beatrice. Patricia alikuwa na uhuru wa kuishi maisha ya kifahari ambayo alikuwa akijisikia kuishi lakini wala hakupenda kuishi maisha hayo hata kidogo.
Kutokana na kusoma shule za gharama ya juu kuanzia darasa la kwanza mpaka darasa la saba, Patricia hakutaka tena kusoma katika shule za aina hiyo jambo lililomfanya kidato cha kwanza kuanza katika shule ya Sekondari ya Salma Kikwete iliyokuwa Kijitonyama
Aliishi maisha ya kifahari, na sasa alijiona kuwa na nafasi ya kutamani kuishi pamoja na watu ambao walikuwa wametoka katika familia za chini. Hiyo ndio ilikuwa sababu kubwa iliyomfanya kuanza kusoma katika shule hiyo ya mchanganyiko na kukutana na wanafunzi ambao walikuwa wakiishi maisha ya chini kabisa.
Patricia hakupenda kabisa kupelekwa na gari shuleni lakini mama yake hakutaka kukubaliana na suala hilo, kwake, Patricia alikuwa kila kitu, hakutaka apate shida ya aina yoyote ile na wala hakupenda binti yake atumie mwendo mkubwa ardhini na wakati alikuwa na uwezo wa kuzuia jambo hilo.
Msichana huyu, Patricia ndiye ambaye alikuwa akiongoza kwa uzuri shuleni hapo. Alikuwa akionekana msichana wa tofauti, mchanganyiko wa rangi ambao alikuwa nao ulimfanya kuvutia zaidi. Kila mwanafunzi alitamani kuwa pamoja na Patricia ambaye alikuwa amefanana sana na mwanamuziki wa kike, Alicia Keys kwa kila kitu kana kwamba walikuwa mapacha.
Patricia hakuwa msichana wa majivuno, alikuwa akiishi maisha ya kawaida shuleni, alichangamana na kila mwanafunzi ambaye alikuwa akihitaji urafiki pamoja nae. Japokuwa wavulana wengi walikuwa wakitamani kumtongoza Patricia lakini walionekana kutokuwa na nguvu za kufanya jambo kama hilo kutokana na ukaribu mkubwa ambao alikuwa nao Patricia kwao.
Patricia akawa akipendwa sana na kila mwanafunzi shuleni hapo isipokuwa baadhi ya wasichana ambao walikuwa wakijiona kuwa bora zaidi yake. Patricia hakutaka kujali kitu chochote kile, kwake, heshima na kuwathamini watu wengine ndio aliliona jukumu lake alilokuwa nalo.
Uwezo wake darasani wala haukuwa mkubwa sana japokuwa alikuwa akifahamu mambo mengi kutokana na kununuliwa vitabu vingi vya kujisomea. Kile ambacho hakuwa akikifahamu, alikuwa akifundishwa na wanafunzi wengine na hata vile ambavyo alikuwa akivifahamu basi alikuwa akiwafundisha wanafunzi wengine.
"Ni msichana mzuri sana. Hapana, acha mimi nijaribu kuwa nae" Martin aliwaambia wanafunzi wenzake.
"Acha utani bwana. Hebu muangalie Patricia halafu jiangalie wewe. Mnaendana?" Juma alimuuliza Martini.
Martin akayapeleka macho yake mwilini mwake, miguuni alikuwa na kandambili huku miguu yake ikiwa michafu kutokana na kucheza mpira pekupeku katika kipindi cha mapumziko. Akayaamisha macho yake na kuyapeleka katika shati lake, shati lilikuwa limechakaa, chafu huku likiwa limechanika makwapani. Kila alipokuwa akijiangalia, kulikuwa na utofauti mkubwa sana na Patricia.
"Mmhh!" Aliguna.
"Vipi tena?" Ashrafu aliuliza.
"Mmesema kweli. Manake kila nikijiangalia sipati jibu kama mimi ni mwanadamu au mnyama aliyeachwa porini" Martin aliwaambia na wote kuanza kucheka.
Martin ndiye alikuwa kijana ambaye alikuwa akivutiwa sana na Patricia kuliko mvulana yeyote shuleni hapo. Kila siku alikuwa akipenda kumwangalia Patricia, moyo wake ukatokea kumpenda sana msichana huyo kiasi ambacho kama ilipita siku pasipo kumuona basi alikuwa akipata shida sana usiku.
Alitamani kumfuata Patricia na kumwambia ukweli kwamba alikuwa akimpenda sana lakini hakujua ni wapi alitakiwa kuanzia. Maisha yake yalikuwa ya kimasikini sana, ingawa alikuwa akikaa mbali na shuleni hapo lakini kila siku alikuwa akienda shuleni hapo kwa miguu. Si kwamba hakuwa akipenda kupanda daladala, alikuwa akitamani lakini umasiki ulikuwa umeitawala familia yao.
Hakujua mwendelezo wa maisha yake ya mbele ungekuwaje hapo baadae. Njia za kutoka kimaisha zikawa zimekwisha akilini mwake jambo lililomfanya kuanza kufikiria kufanya muziki. Kila siku shuleni alikuwa akiandika mistari ya muziki aina ya RnB huku akiwaimbia wanafunzi wenzake.
Baada ya miezi miwili kupita, shule nzima ikajua kwamba mwanafunzi masikini asiyekuwa na mvuto wowote ule, Martin alikuwa mwanamuziki chipukizi ambaye hakuwa na mbele wala nyuma. Walimu walijaribu kumuita ofisini na kumshauri kwamba ingekuwa vizuri kama angetilia maanani masomo lakini Martin hakuonekana kujali, kitu alichokuwa akikitaka ni kuwa mwanamuziki mkubwa wa muziki tu.
"Kila ninapomsikiliza R Kelly, ananitia mzuka sana" Martin aliwaambia wanafunzi wenzake.
"Unataka kuwa kama yeye?"
"Unaulizia chumvi baharini. Ndio, ninataka kuwa kama yeye" Martin alijibu.
Hizo ndizo zilikuwa ndoto zake za kila siku, aliupenda sana muziki kwani aliamini kwamba huo ndio ungekuwa njia ambayo ingemfanya kutoka kimaisha na kuwa mwanamuziki mkubwa ambaye angekuja kuwa na fedha nyingi hapo baadae.
Ingawa alikuwa akiendelea na juhudi zake za kutunga nyimbo mbalimbali lakini bado ndoto yake ya kuwa na msichana Patricia ilikuwa kichwani mwake, alikuwa akimhitaji sana msichana huyo kiasi ambacho usiku kwake ulikuwa ukionekana kuwa wa shida sana. Alitamani kumfuata na kumwambia kile ambacho alikuwa akijisikia moyoni mwake juu yake lakini alionekana kuogopa.
Kwanza kila alipokuwa akiiangalia hali yake, hakuamini kama msichana Patricia angekubali na kuwa nae. Alijidharau sana na kutokuamini kama alistahili kuwa na msichana huyo. Kwake, kuwa na msichana Patricia ilionekana kuwa kama ndoto ya mchana wa saa saba.
Kila alipokuwa akifikiria utofauti mkubwa ambao ulikuwepo kati yake na Patricia, wala hakutamani kuwa pamoja nae, aliona ni bora kuendelea kutunga muziki ili kama kungekuwa na siku angekuja kupata fedha, kurekodi na kuwa maarufu basi isingekuwa jambo gumu kumpata Patricia. Kwake aliona fedha kuwa kila kitu katika maisha yake, kutokuwa na fedha kulionekana kuwa tatizo kubwa ambalo lilikuwa likimkosesha kufanya jambo lolote la maana.
"Ngoja niachane nae na nijiingize moja kwa moja kwenye muziki. Naamini kuna siku utanitoa tu, na hapo ndipo nitakapokuja kumwambia Patricia ukweli kwamba sinywi, sili wala silali kwa ajili yake. ....mwisho wa siku nakuja kumuoa. Hahahahaha...Sijui itatokea au ndio ndoto za mchana. Ila poa. Mziki kwanza halafu mapenzi baadae" Martin alijisemea katika kipindi ambacho Patricia alikuwa akipita mbele yake pamoja na wanafunzi wengine wa kike.

Je ni nini kitaendelea?
Je uamuzi aliouchukua Martin utaweza kudumu moyoni mwake?
Je nini kitaendelea katika maisha ya watu hawa hapo baadae?
Itaendelea
Kaka ntumie hii plz plz
 
Back
Top Bottom