Riwaya: Chokoraa

Riwaya: Chokoraa

SEHEMU YA SABA
RIWAYA: CHOKORAA
MTUNZI: George Iron Mosenya
MAWASILIANO: 0655 727325


SEHEMU YA SABA


"Her name is Fridah! I need her right now!" (Anaitwa Frida, namuhitaji hapa sasa hivi!) alikoroma mzungu!
Mkuu wa kituo akatoka nje akiwa anatetemeka!!
Ndio. Lazima atetemeke maana kwa namna yoyote Frida lazima atamtaja kuwa yeye ndiye muhusika wa mimba ile!! Kibarua kitaota majani!!
Hofu ikatanda sana!! Hadi anafika nje hakujua afanye nini!!!


Wakati mnyanyasaji huyu akiwa katika hofu kuu. Frida alikuwa katika mawazo ya ataweza vipi kuzungumza na yule mzungu mwenye upendo wa hakli ya juu. Alihitaji kutoa shtaka lake dhidi ya mkuu wa kituo. Uamuzi huu hakumshirikisha Mwanaidi. Aliuhifadhi moyoni.
Mara akiwa katika mawazo hayo mazito. Akasikia akiitwa jina lake kwa mbali. Akageuka!! Alikuwa mkuu wa kituo!!
Moyo ukamwenda mbio Frida. Na ilikuwa kawaida kila alipomuona mwanaume huyu alimchukulia kama mnyama mkali.


*****


Hakuna kitu kinachokera nakuumiza kichwa kama kutafuta kazi na hakuna kingine kibaya kama kuipoteza kazi uliyoitafuta kwa kutumia nguvu nyingi.
Ni fedheha hii ilimkumba msimamizi mkuu wa kituo. Ni kweli alifurahia kujistarehesha na Frida kwa kutumia mamlaka aliyokuwa nayo lakini hakutaka huyo Frida awe chanzo cha yeye kupoteza kazi yake.
Akiwa amehamaki sana huku akiwa ameogofyeka na ukali wa mzungu yule. Mwanaume huyu katili asiyekuwa na upendo hata kidogo alitoka nje. Alipoagizwa kumuita Frida
Akazurura huku na huko! Akamuona aliyetaka kumuona. Frida!
Akamuita! Hakutegemea kama tukio hilo linaweza kutokea. Aligeuka mtu asiyemtegemea japo huyo ndiye aliyehitajika.
"Sio wewe!" alimwambia kwa sauti ya kuamuru!!
"Frida!" aliita tena, sasa yule aliyemtaka akageuka. Akapunga mkono kuashiria amfuate.
Alipomfikia akamtaka amfuate anapoelekea. Yule binti mrefu mwembamba akamfuata akinyata kama hataki. Hawakuzungumza lolote wakaingia katika kile chumba alichokuwa mzungu.
Binti akaendelea kusimama wima, nywele zake ndefu kiasi fulani zikiwa zimemziba jicho moja. Akazirusha nyuma na kushindwa kutoa salamu kwa mzungu kwa sababu ya kutojua lugha.
Mzungu hakuwa na papara. Na aliujua ujanjaujanja wa wa afrika. Hakumuaga mtu pale chumbani akatoka na kurejea baada ya dakika chache akiwa ameongozana na muhusika mwingine wa kile kituo.
"I want you to translate! (Nahitaji ufanye tafsiri)" aliamuru huku uso wake ukiwa umeiva kwa hasira.
"What's you are real name! (Jina lako halisi ni nani)"
"Winifrida…" alijibu bila wasiwasi.
"Famous name! (Jina maarufu)"
"Frida.." akatoa jibu ambalo mkuu wa kituo alikuwa analingojea kwa hamu.
Mahojiano yakaendelea kwa hatua ndogondogo. Hadi wakaifikia nia yao. Mimba!
Hapo huyu binti akaruka maili mia. Akakataa katakata.
Mzungu akabadili tena mtu wa kumtafasiria. Alifanya hivyo ili kuepukana na wabongo hawa waliomzunguka wasije kucheza dili ili kumdanganya.
Hali ikawa ile ile.
"Tunaweza kukupima tena??" aliulizwa. Hakungoja kujifikiria akakubali kuwa yu tayari tena mbele ya watu wote.
Vipimo vikafanywa tena, majibu yakatoka. Hayakuwekwa hadharani. Wakapima tena. Frida hakuwa na mimba!!!
Hapa sasa madaktari walioaminiwa na yule mzungu aibu ikawa juu yao. Mzungu akahamishia hasira zake kwao. Hawakuwa na cha kujibu. Heshima kwa mkuu wa kituo ikarejea maradufu. Akamwomba msamaha kwa lugha za ukali alizotumia dhidi yake.
Maskini bwana huyu hakujua kuwa mkuu wa kituo ni mbongo halisi, tayari alikuwa amemchezea mchezo. Aliyeletwa mbele yake alikuwa ni mtu mwingine kabisa. Huyu alikuwa ni Winifrida na wala sio Frida yule chokoraa kutoka gerezani.


Mzungu akiwa na hasira tele, kipara chake kikitokwa jasho. Hakutaka tena kuzungumza na mtu na hata mtoto mnene kiasi, mwenye sura inayotangaza msiba huku macho yake yakiwa mekundu. Alimkimbilia. Alikuwa ana haja ya kuonana naye kwaajili ya kumueleza kitu kizito sana.
Alimfikia akamkumbatia. Mzungu akamkumbatiakisha akawaambia waliokuwa pembeni yake, "Tell her that I will be back (Mwambie nitarejea).
"Yuko bize siku nyingine" mbongo akafanya tafsiri anayojua yeye.
Huyu binti alikuwa ni Frida Gereza. Akawa ameikosa nafasi ya kuzungumza na mzungu huyo.


Kwa pona pona aliyoipata mkuu wa kituo. Hakutaka tena kucheza karata hizi mbovu. Hata kabla huyo mzungu hajarudi tena tayari alikuwa ameweka mambo sawa. Mwanaidi na Frida walikuwa maeneo ya Posta wakitafuta mahali pa kulala. Makazi ya usiku ya chokoraa!!
Walikuwa wamefukuzwa kimyakimya!!
Mkuu wa kituo akabaki na tabasamu usoni huku akijisifu kuwa yu mshindi katika vita kuu. Hakuiwaza tena mimba ya Frida.
Dada mkuu yule w zamani katika shule ya msingi alikuwa na akili ya kuzaliwa. Kitendo cha wawaili hawa kufukuzwa mapema baada tu ya mzungu kuwatembelea na kuwapima mimba kilimtia mashaka. Uhusiano wa Winifrida kuitwa na kutuhumiwa kuwa ana ujauzito kisha kupimwa na kukutwa salama pia kulimshtua. Hakutaka kumweleza Frida mapema. Lakini baada ya muda kidogo alifanya maamuzi. Kwa senti chache alizokuwanazo alinunu Pregnant Tester (PT). Hiki ni kifaa binafsi cha kupimia ujauzito kwa njia ya mkojo.
Frida akaamriwa kukikojolea. Akafanya hivyo.
Machale na hisia sahihi kabisa. Frida alikuwa ana mimba!!!
Msichana huyu alichanganyikiwa kusikia hivyo. Lakini bado Mwanaidi alikuwa jasiri. Alimshauri kuwa kuamua kubaki nayo ni kujiua kwa mateso kabla ya wakati.
"Kwa hiyo nitafanyaje mimi."
"Usijali!! Lala hapa nakuja."
Mwanaidi akatoweka tena na kutafuta duka la madawa lililokuwa wazi usioku ule. Akanunua madawa aliyoyajua yeye. Akafanikiwa kupata na maji ya kunywa ya bei chee. Frida akapewa sharti akatii. Akanywa yale madawa. Kisha akalala.


Mambo yakaanza kubadilika baada ya masaa machache. Ule usiku ukageuka kuwa usiku wa uchungu mtakatifu.
Tumbo likamsokota Frida. Mwanzoni alijikaza lakini uvumilivu ukamshinda akaanza kupiga kelele. Akalia sana Mwanaidi kazi yake kumbembeleza.
Damu ikaanza kumtoka. Hatimaye uchungu uliopitiliza ukaondoka na fahamu zake. Alipoamka alfajiri hakuwa mjamzito tena.
Mungu alikuwa pamoja naye! Njia hii hatarishi ingeweza kuondoka na uhai wake.


****


Hakuna kipindi watoto wa mitaani wananyanyasika kama kipindi cha masika. Mvua hizi za masika huvuruga kabisa makazi yao ya kulala. Watoto hukesha kama popo. Sehemu zao za kulala zote huwa majimaji na magunia yao ambayo ni vitandavyenye thamani huwa chepechepe.
Usiku huu ulikuwa usiku wa namna yake kwa Mwanaidi na Frida. Hawakuitegemea hali hii lakini sasa ilikuwa imewakumba. Walizurura huku na huko bila kuupata muafaka wa watalala vipi. Baridi kali iliwapuliza na manyunyu yaliyoambatana na upepo mkali yaliilowanisha miili yao.
Baada ya kuzurura sana!! Mwanaidi akaanza kupunguza mwendo na hatimaye akasimama. Frida aliyekuwa ametangulia akageuza na kurudi nyuma kutazama nini kimemsibu rafiki yake.
"Frida…" Mwanaidi aliita huku midomo yake ikichezacheza na meno yakigongana mdomoni.
"Naumwa!! Naumwa sana" Mwanaidi alimweleza. Kifua kilikuwa kinambana. Frida alibaki anashangaa, mtu ambaye anamtegemea. Sasa anaumwa. Na ni yeye aliyekuwa mwalimu wake mtaani.
"Kaninunulie dawa. Dawa ya kupuliza naanza kukosa hewa." Alizidi kujieleza Mwanaidi huku sasa akiwa amekaa chini.
Hali tete!! Hakika palikuwa na tatizo.
"Inaitwaje…na hela sasa." Aliuliza Frida huku akiwa na hofu kubwa.
"Nenda watakuelewa waambie siwezi kupumua. Nitakufa Fri…Fri…" Sauti ikazidi kupotea.
Ilikuwa saa tatu usiku. Mitaa ya posta haikuwa imejikita vyema katika akili ya Frida. Alijaribu kukata huku na kule. Hatimaye akalipata duka.
Akawaeleza kama Mwanaidi alivyomuelezea. Akawalilia akalia sana chokoraa huyu. Hatimaye akaeleweka.
Akapewa bure dawa ile ambayo hata aliyempa aliamini kuwa hawezi kuwa na nia mbaya na dawa ile ya kupuliza ambayo hutumiwa hasahasa na wagonjwa wa pumu.
Frida akatimua mbio aweze kumuwahi Mwanaidi.
Unapajua Posta unapasikia?
Hilo swali alilijibu Frida kwa vitendo. Mtaa huu na mtaa ule inafanana. Jingo hili na lile la awali yanalingana urefu. Kila mahali panafanana na ikulu ya Tanzania. Frida akwa amepotea.
Alijaribu kuituliza akili yake. Akapunguza mwendo aweze kuwa makini lakini bado hali ikawa ileile.
Alitaka kuwauliza watu lakini hakujua atawauliza wamuelekeze wapi maana hata pahali alipokuwa awali na Mwanaidi hakupajua vizuri.
Frida akaanza kulia. Mvua kubwa ikayatwaa machozi yake na kuyasafirisha mbali. Nguo zikanata katika mwili.
Sasa Frida alikuwa anaomboleza kana kwamba Mwanaidi amekufa tayari. Usiku huu ukapita. Asubuhi anakuja kugundua alilala nyuma ya jingo ambalo Mwanaidi alikuwa akimngojea. Dawa yake mkononi ndiyo ilimgutusha akamkumbuka. Mwanaidi.
Akaangalia sehemu zote hapakuwa na kiumbe anayeishi!
Mwanaidi alikuwa ametoweka!
Kilio kikaanza upya kwa yatima huyu. Aliugulia maumivu sana.
Ile hali ya kumfikiria Mwanaidi kuwa amekufa kwa kusombwa na maji ikamfanya ajisikie kitu kama chuki kikitambaa katika mtima wake. Chuki dhidi ya wanaume. Akamuweka katika orodha mkuu wa kituo kama muhusika namba moja wa kifo cha Mwanaidi.


Waarabu wa pemba hujuana kwa vilemba. Na hata yatima na machokoraa hujuana kwa vilio vyao. Chokoraa mmoja akafahamu kuwa Frida alikuwa katika majonzi. Kwanza alimgawia kipande cha muhogo alichokuwa anatafuna. Frida akapokea.
"Unaonekana mgeni maeneo haya. We ni wa kempu ipi?"
"Kempu ni nini?" aliuliza Frida.
Yule msichana aliyejitambulisha kwa jina la Isha akatabasamu. Hakuendelea kuuliza maswali. Frida akajiumauma akaelezea juu ya kupotea kwa Mwanaidi.
"Hiyo ni kawaida, wengine hubakwa na wengine huchunwa ngozi. Sijui watakuwa wameenda naye wapi." Alijibiwa kwa tahadhari.
"Mama yangu alichukuliwa mikononi mwangu. Mimi wakanibaka yeye aliondoka nao moja kwa moja hadi leo. Majangili na wanyang'anyi ni watu wabaya."


Isha aliongozana na Frida. Wakaelekea feri. Huko wakapanda pantoni. Iliyowavusha ng'ambo ya pili. Isha akiwa kiongozi wa Frida walizifikia nyumba nyingi walizokuwa wanaishi wanafunzi wa chuo kikuu cha IFM.
"Huwa tunawafulia nguo. Nifuate!"
Walianzia mlango wa kwanza. Wenyewe hawakuwepo. Mlango wa pili hawakuhitaji huduma. Mlango wa tatu bahati ikawa upande wao. Kijana mnene aliyenukia raha, akawakabidhi lundo la nguo.
"Jinsi mia tatu, suruali na shati mia mbili, soksi na fulana huwa tunafanya mia mia." Isha alimtajia bei.
Yule kijana akawapatia ndoo na sabuni. Akawaelekeza bomba lilipo. Wakaanza kufua. Frida alikuwa mwepesi zaidi kuliko Isha na hakuonekana kuchoka. Isha hakuitegemea hali hiyo.
Mchana wakapokea ujira wao na kuondoka.


Urafiki wao ukaanzia hapa. Mwanaidi akaanza kusahaulika ili kutimiza ule usemi usemao ‘mavi ya kale hayanuki!'
Kila mwisho wa juma walikuja na kutafuta kibarua cha kufua nguo za wanafunzi. Kwa siku za kawaida waliokota makopo tupu ya maji na soda na kuyauza kwa kilo katika viwanda vya wahindi na waarabu.
Maisha yakaendelea!!
Ni huku Kigamboni ambapo Frida alikutana na maajabu!!


***MAAJABU gani FRIDA anakutana nayo Kigamboni!!
***MWANAIDI na ugonjwa wake wa PUMU….ameishia wapi.
**JE MKUU WA KITUO ataishi milele na roho yake mbaya.
mbalu amina mabata
 
Last edited by a moderator:
SEHEMU YA NANE
RIWAYA: CHOKORAA
MTUNZI: George Iron Mosenya



SEHEMU YA NANE


Yule kijana akawapatia ndoo na sabuni. Akawaelekeza bomba lilipo. Wakaanza kufua. Frida alikuwa mwepesi zaidi kuliko Isha na hakuonekana kuchoka. Isha hakuitegemea hali hiyo.
Mchana wakapokea ujira wao na kuondoka.
Urafiki wao ukaanzia hapa. Mwanaidi akaanza kusahaulika ili kutimiza ule usemi usemao ‘mavi ya kale hayanuki!'
Kila mwisho wa juma walikuja na kutafuta kibarua cha kufua nguo za wanafunzi. Kwa siku za kawaida waliokota makopo tupu ya maji na soda na kuyauza kwa kilo katika viwanda vya wahindi na waarabu.
Maisha yakaendelea!!
Ni huku Kigamboni ambapo Frida alikutana na maajabu!!


*****


SIKU hii ya jumapili Frida alikuja pekee kufua nguo. Isha alibakia katika makazi yao waliyokuwa wamepanga na kulipia shilingi elfu tano kila mwezi. Haikuwa nyumba bali kibanda tu ambacho wangeweza kujilaza walau kwa amani kiasi fulani.
Kibanda hiki walipewa kwa minajiri ya kuwa walinzi wa nyumba kubwa iliyokuwa inajengwa isiweze kuingiliwa na watoto na watu wazima wasiojiheshimu na kuibadili matumizi kuwa choo.
Licha ya ulinzi huu lakini bado walimlipa mwenye nyumba kiasi hicho cha pesa. Unyanyasaji!
Isha alikuwa anasumbuliwa na matatizo yanayowakabili wanawake kila mwezi na tumbo lilikuwa linamuuma sana hivyo hakuweza kwenda katika majukumu hayo. Frida akaenda.


Siku hii yule bwana waliyezoea kumfulia nguo alikuwa ametembelewa na rafiki yake wa kike hivyo aliyatimiza majukumu yote ya kumfulia na shughuli nyingine za usafi.
Riziki ya akina Isha na Frida ikawa imezibwa.
"Kaka, samahani..hakuna rafiki yako ambaye naweza kumfulia hata kwa nusu bei. Rafiki yangu anaumwa. Anahitaji dawa." Frida alimueleza yule kijana. Ambaye alimtazama huku akijikuna tumbo lake kubwa lenye vinyweleo vingi.
Njoo huku! Alimuita.
Akaenda hadi mlango wa tatu kutoka chumba chake. Akabisha hodi akafunguliwa. Akanong'ona jambo na yule bwana. Kisha wakageuka kumtazama yule binti. Macho ya yule bwana yakagongana na yule binti. Yakaganda kwa muda, binti akawahi kuinama chini.
Bwana mnene akaondoka, huku akimfanyia yule binti ishara kuwa sasa anaweza kuzungumza na yule kijana mrefu.
"Za saa hizi" alisalimia akajibiwa. Kisha akajieleza
"Nilikuwa nimemwambia yule kaka kuwa kama una nguo nikufulie hata kwa nusu bei..nipate pesa kidogo, rafiki yangu anaumwa."
"Usijali amenieleza kila kitu. Sawa eeh!"
"Bei zenu ni shilingi ngapi?" aliulizwa akazitaja bei kwa mpangilio maalumu kama alivyofunzwa na Isha.
Yule bwana akaingia ndani mwake. Akarejea na shati mbili ambazo hazikuwa na uchafu wowote na suruali moja. Nguo hizi kwa nusu bei zilikuwa zinagharimu shilingi mia tatu. Hii haitoshi hata kununulia pedi.
Frida akafua kwa moyo mkunjufu akazianika.
Akarejesha ndoo na sabuni iliyobakia.
Safari hii hakuishia nje. Alikaribishwa mpaka ndani.
Akaingia akiwa na uoga. Nguo zake zilikuwa na hali fulani ya uchafu kutokana na kuvaliwa mara kwa mara.
"Naitwa George, nawe waitwa nani?"
"Frida Ge.." hakumalizia jina lake.
"Naitwa Frida." Alirudia. Macho yake yalikuwa yamepepesa hapa na pale na kutambua vitu vingi vya thamani katika kasri ile ndogo.
"Yule ni mama yangu!! Marehemu lakini" George alieleza huku akimwonyesha Frida picha kubwa ukutani ya mwanamke akiwa anatabasamu.
Frida akataka kutoa pole lakini George akaendelea na mazungumzo ya hapa na pale. Kisha akamkabidhi Frida noti ya shilingi elfu kumi. Wakaagana.
"Uwe unakuja kunifulia." George alimwambia Frida. Frida akamtoa wasiwasi.
Siku ikapendeza. Noti ya shilingi elfu kumi kwa nguo tatu. Bahati iliyoje.
Fridah akanunua mahitaji ya msingi. Akarejea nyumbani akiwa na furaha tele. Isha ambaye hali ilikuwa kidogo inatia matumaini alimpokea Frida akiwa na jiko la mkaa.
Ukawa mwisho wa kuumia na moto wa kuni!
Isha alishangazwa na ukarimu wa yule bwana!! Kila mmoja kwa imani yake akamshukuru Mungu.


*****


SIKU nne zilipita. Isha akarejea katika hali ya kawaida. Lile jiko wakalitumia kujiingizia kipato. Kwa mtindo wa kuazima azima vifaa hatimaye wakaanzisha biashara ya kukaanga mihogo na kuuza majira ya asubuhi na jioni.
Maisha yao walau yakabadilika kwa kiasi fulani. Japo waliendelea kuishi katika kijumba kile lakini uhakika wa kula ulikuwepo asubuhi na usiku.
Mihogo haikuwa na faida sana lakini walau ule utembezi wa kutafuta makopo tupu ya plastiki kwa ajili ya kuuza ukakoma.


Si kila mwanadamu anaridhika akiona mwenzake anpiga hatua ya kimaendeleo. Licha ya yatima hawa kujibunia mbinu hii ya kujiingizia kipato. Wapo binadamu wenye roho za unyama hawakujiweka mbali.
Usiku wa saa tatu. Mlango wa kuegesha ulisukumwa ukaachia. Wanaume watatu wakavamia ndani. Mmoja akamziba mdomo Frida na mwingine akamziba Isha. Yule mwingine akaanza kupekua hadi akaipata akiba yao ya shilingi elfu thelathini. Akabeba na jiko lao. Akatoka nje. Wale wengine wakakosa kingine cha kuchukua. Wakabahatika kupata mihogo ya kukaanga iliyosalia jioni hiyo. Wakaitwaa.
Huruma ipo wapi!!
Msichana msichana tu! Wawili hawa hawakuweza kupiga kelele. Kila mmoja alikuwa anatetemeka. Isha alikuwa amejikojolea tayari. Frida alikuwa anatokwa machozi.
Roho ziliwauma. Pesa ya jasho lao ilikuwa imebebwa na vibaka. Wakamlilia Mungu kwa lawama zote.
"Mungu upo wapi? Mbona watuacha yatima tunanyanyasika, kwani tulipenda kuachwa na wazazi Mungu, kwani tulipenda kuzaliwa sisi Mungu, kwanini adhabu za wazazi wetu waziacha ziishi nasi. Mbona dunia imetutenga nawe hautupiganii!! Ni kosa gani tulifanya katika matumbo ya mama zetu baba!! Zitwae roho zetu sasa kama hatuhitajiki dunianai na kama ulituumba ili tuteseke baba nasema imetosha baba tumekuwa funzo kwa wengine imetosha baba zitwae hizi roho sasa" Frida alikuwa analaani. Alikuwa analia kwa uchungu. Isha akasimama akamkumbatia huku na yeye akilia sana.
Vilio vya watu wawili vikageuka kuwa vya watu watatu lakini huyu mmoja hakutoa sauti kabisa japo machozi yalikuwa yanamtiririka.


*****


GEORGE EMMANUEL, hakuridhika na mazungumzo aliyoyafanya na Frida siku yao ya kwanza kukutana. Japo walizungumza kwa ufupi lakini maisha ya Frida yalimgusa kwa namna ya kipekee. Hayakumtesa kwa namna ya ulimwengu wa huruma tu! Bali alitambua kuwa lile jicho la Frida lilipomtazama liliutetemesha moyo wake.
Akatambua kuwa kuna kitu alihitaji kukijua zaidi.


Walipoagana na Frida. Alifanya kitendo cha upesi cha kubadilisha njia ya kupita. Lakini lengo likiwa kuelekea kule anapoelekea Frida.
Wakajikuta wapo ndani ya Pantoni pamoja. Bila Frida kujua lolote.
Waliongozana tena hadi katika daladala. Bado Frida hakujua lolote.
Kituo cha Davis Corner Tandika alichoshuka Frida na George naye akatelemka. Frida akaanza kwenda kwa miguu. George naye akiwa mamini kabisa na miwani yake usoni aliendelea kumfuatilia Frida. Ulikuwa umbali mrefu lakini hakuchoka. Frida alipoingia dukani yeye alijiweka mita kadhaa mbali naye.
Hatimaye wakafika katika jumba ambalo halijakamilika maeneo ya Abiola. Hapa akatokea dada mmoja kuja kumpokea Frida. Chumba walichoingia kikakaririwa na George. Kisha akatoweka huku akijuta kumpatia Frida shilingi elfu kumi. Kwani haikukidhi kabisa haja yake.


Aliondoka pale akidhani atangoja mpaka mwisho wa juma Frida atakapokuja kumfulia nguo. Lakini alipofika nyumbani kwake tu akagundua kuwa alikuwa anatamani kumuona ama kumsikia Frida mara kwa mara.
Alitamani kumsikia kwa sababu aliamini kuwa atajifunza mengi ambayo yatamsaidia katika fani yake ya uandishi wa simulizi. Hasahasa simulizi za maisha halisi ya mwanadamu wa daraja la chini.
"Lakini mbona nimekutana na wengi sana na sikujali kama nionavyomjali huyu?" George alijiuliza. Hakupata jawabu.
Siku ya pili aliendesha gari yake tofauti na awali alivyokuja kwa miguu. Akaiegesha mbali na kujipitisha jirani na ile nyumba aliyomuona Frida akiingia. Akawamkuta Frida akiwa amejikita katika kuuza mihogo. George akashangaa sana. Hakutegemea.
Ile hali ya kutaka kumjua zaidi Frida ikaongezeka.
Muda wa kufunga genge ulikuwa ni saa mbili usiku.
Baada ya siku kadhaa George aliwasili pale usiku zaidi.
Kama kawaida aliiegesha gari yake mbali na ile nyumba.
Akajongea kwa mguu. Kundi la watu watatu likampita. Akalipuuzia lakini kisha akalitilia maanani baada ya kuwaona wakifanya mnyato kuelekea nyumbani kwa akina Frida.
George akajiweka katika kigiza na kutulia tuli huku nguo zake nyeusi zikimfanya asionekane.
Alishuhudia kila kitu kilichotokea. Sasa alikuwa jirani kabisa na nyumba ile. Kilio cha Frida kilichoambatana na maneno ya kumlaumu muumba mbingu na nchi yakamgusa. Funda kubwa likajifinyanga kooni. Alipojaribu kulilegeza halikulegea. Alipomeza mate akawa ameyaruhusu machozi kumtoka.
Watu watatu wakawa katika kilio kikuu!!!


Akiwa amejisahau kuwa hakuwa amefanya ugeni rasmi.
Mara kimya kikatanda. Kisha likatokea jambo la ajabu asilolitegemea.
Jambo lililoifanya siku hii ibaki kuwa ya kukumbukwa.


***Ni jambo gani linamtokea GEORGE.
**Nini hatma ya YATIMA HAWA…je warejee UCHOKORAA!!!
NB: Bashiri NINI KITATOKEA HAPO?
 
SEHEMU YA TISA
RIWAYA: CHOKORAA
MTUNZI: George Iron Mosenya




SEHEMU YA TISA


George akajiweka katika kigiza na kutulia tuli huku nguo zake nyeusi zikimfanya asionekane.
Alishuhudia kila kitu kilichotokea. Sasa alikuwa jirani kabisa na nyumba ile. Kilio cha Frida kilichoambatana na maneno ya kumlaumu muumba mbingu na nchi yakamgusa. Funda kubwa likajifinyanga kooni. Alipojaribu kulilegeza halikulegea. Alipomeza mate akawa ameyaruhusu machozi kumtoka.
Watu watatu wakawa katika kilio kikuu!!!


Akiwa amejisahau kuwa hakuwa amefanya ugeni rasmi.
Mara kimya kikatanda. Kisha likatokea jambo la ajabu asilolitegemea.
Jambo lililoifanya siku hii ibaki kuwa ya kukumbukwa.


*****


Frida alikuwa amejuta sana na kugundua kuwa majuto yake hayana maana kwani anayemlaumu hatoi majibu kama wanadamu tunavyotaka. Yeye ni Mungu aliye karibu wala si Mungu aliye mbali.
Frida alibakia kuwa katika kilio cha kwikwi akisaidiana na Isha. Macho yake yaliyokuwa yamevikwa ukungu yaliweza kuona kwa mbali mfano wa kivuli kikitikisika. Akatulia tuli akiwa bado amekumbatiana na Isha. Hakuweza kuyasikia maneno ya ziada ambayo Isha alikuwa anamueleza. Akili yake ikamtuma mbali sana. Hasira ikampanda na ule uwazimu wa kimbwamwitu aliourithi bila kujua kutoka kwa mama yake mzazi ukampanda. Hakutaka kuwaza zaidi. Harufu ya kifo ikamtawala.
Bora nife! Akawaza! Akamsukuma Isha kisha akafanya tukio la ghafla akapiga hatua mbili kubwa akatoka nje.
Kelele alizozitoa zilitosha kumwamsha mtoto mchanga aliyelala fofofo na hata mlevi wa gongo lazima ashtuke.
Mwiziiiii!!1 Mwiziii!! Alipiga kelele. Hakika alikuwa sahihi kile kivuli kilikuwa ni mtu na sasa kikaanza kukimbia!!
Kosa kubwa! Kivuli kile hakikujua kama Frida amepandwa na mashetani makali sana yaliyochoka kunyanyaswa!!
Zile kelele sasa zikawa maradufu! Isha ambaye hakujua lolote linaloendelea na yeye aliunga mkono mbio hizi zisizokuwa na umbali maalumu dhidi ya mwizi huyo.
Bahati ilikuwa mbaya kwa yule mwizi! Siku hiyo palikuwa na mechi ya mpira wa miguu. Na sasa ilikuwa imemalizika na masgabiki wanarejea katika familia zao. Walioshinda wakiwa wanashangilia sana huku wale wanyonge timu zao zikiwa zimefungwa.
Hawa wanyonge walikuwa wa kwanza kumuona mwizi yule!! Hasira ya kufungwa ikahamia kwa mwizi huyu.
Mara alikuwa ardhini akihangaika kujibizana na sauti za watu wengi. Kila mmoja akisema la kwake.
Frida alifika katika kundi lile huku roho ya kuua ikiwa imemuandama. Hasira kali zikiwa zimemjaa kichwani.
Pishaaaaa!!! Sauti kali ya kike ilisikika kutokea nyuma. Wadau wa kumpiga mwizi walipogeuka walikumbana na mwanamke akiwa kasi na jiwe kubwa mkononi. Wakampisha afanye alilokusudia. Huku kimya cha ghafla kikitanda! Ulikuwa mshtuko hakuna aliyeweza kudhania mwanamke anaweza kuwa jasiri kiasi kile.
Mwizi yule alinyanyua mkono wake akijaribu kumsihi yule anayekuja na jiwe. Alijaribu kupaza sauti lakini sauti haikutoka.
"Friiiidaa!!" jiwe lililotua katika mguu wake wa kuume lililainisha koo. Akatoa sauti kuu ya mwisho!!
Kisha kimya kikatanda. Damu ikichuruzika kwa fujo.
Frida na Isha walishangazwa na hali hii. Ni nani yule aliyemtambua Frida kwa jina.
Kundi moja baada ya jingine lilianza kutoweka eneo la tukio baada ya mwizi kunyooka na kukaa kimya. Kila mmoja akatambua kuwa ni maiti.
Hatimaye akabaki Frida, Isha na wanaume wawili.
Frida akainama ili kumtambua yule mwizi. Japo alikuwa ameumuka usoni lakini kuna kitu alikiona. Mwanya!
Ule mwanya ukamrudisha nyuma siku kadhaa. Akatazama vyema zaidi. Akamtambua kuwa huyu mwizi alikuwa ni George Emmanuel wa kigamboni!!
Maajabu!!
Frida alimueleza Isha kwa ufupi!! Wote wakataharuki.
Watafanya nini? Hilo likawa swali.
Usiku ulikuwa umeenda.
Ukarimu wa George na tukio hili la wizi wa shilingi elfu thelathini havikuendana hata kidogo. Alikuja kufanya nini sasa?
Swali jingine!!


Frida akafanya maamuzi, akaingiza mikono katika nguo za mwili huu unaopumua kwa shida.
Pesa nyingi zikajaza mikono ya Frida. Zilikuwa ni mara kumi ya ile pesa iliyoibiwa. Hapana huyu sio mwizi!!


Isha akakimbia na kutafuta teksi.
Safari ya kuelekea hospitali ya Temeke.


*******


Majira ya saa nane usiku baada ya kuongezewa maji ya ‘insuline' chupa mbili. Fahamu zikarejea katika mwili wa George. Frida na Isha walikuwa pembeni yake. Jicho lake likakutana tena na jicho la Frida. Akatabasamu! Frida naye akajibu tabasamu lile.
Huu ukawa mwanzo wa rejeo la tumaini lililokaribia kupotea!
Mguu ulifungwa bandeji ngumu (P.O.P), bahati nzuri haukuwa umevunjika. Frida aitumia pesa ya George kwa ajili ya matibabu!
Iliyosalia alimkabidhi! George hakusema neno bado alitabasamu.


Siku hiyo wawili hawa walikesha na mgonjwa hadi asubuhi.


"Gari yangu ipo salama kweli." George alimuuliza Frida. Frida hakuwa na la kujibu maana hakujua lolote kuhusu gari ya George.
George aliwapa maelekezo kadhaa juu ya wapi aliiegesha gari hiyo.
Maelekezo sahihi kabisa yakawafikisha wawili hawa eneo lilipoegeshwa gari lile. George alikuwa amewaomba wamchukulie pia simu mbili alizozihifadhi garini. Wakafanya hivyo!
Wakarejea hospitali. George bado alikuwa kitandani. Alipokea zile simu na kupiga simu mbili tatu. Alizungumza kwa lugha ya kigeni hakuna aliyemuelewa aidha nesi, ama machokoraa hawa. Kilichoonekana ni kuwa mazungumzo hayo yalikuwa na mvutano kiasi fulani.


Siku hiyo aliwapatia kiasi fulani cha pesa huku akiwashukuru sana kwa kuuokoa uhai wake. Alikiri kuwa bila Frida huenda angekuwa mfu tayari. Walijikuta wote wakitokwa machozi.


Siku iliyofuata walipofika hospitali hapo. George hakuwepo tena.
Manesi hawakuwa na majibu iwapo ameruhusiwa ama la! Madaktari nao hawakutoa maelekezo kwa Frida na Isha.


Ng'ombe wa masikini hazai. Wahenga walisema! Wakati Frida wakiwa katika maswali mengi juu ya kutoweka ghafla kwa George, likazuka jingine.
Walikuwa njiani kuelekea nyumbani. Siku hii walipanda daladala mara mbili. Yaani kutoka Temeke na pia kuelekea Abiola.
Isha alitangaza hisia zake juu ya kifo cha George, Frida hakukubaliana naye japo pia hakuwa na jibu sahihi ni kipi kimemsibu kijana huyu ambaye hawajui nivipi alipajua nyumbani kwao na hatimaye kukumbwa na maswaibu ya kupigiwa kelele za mwizi na mwisho kuvunjwa mguu.
"Jumapili twende kule wanapoishi lazima rafiki zake watakuwa wanajua alipo…." Frida alitoa wazo. Isha akaliunga mkono lakini akiongezea na maneno yake mengine ya kujishangaa kwa nini wamfuatilie George iwapo hakuna analowahusu.
Wakati Frida anataka kujibu. Akaona kitu! Kitu kama mkeka. Mkeka wenye rangi mithiri ya ule ambao wawili hawa walikuwa wameununua katika siku chache nyuma kwa ajili ya kulalia.
Mkeka huu ulikuwa juani na juu yake kulikuwa na kisufuria kidogo, vikombe viwili, ndoo ndogo ya maji na sahani kadhaa zikiwa zimechanganyika na vibakuli.
Kabla hajamshirikisha Isha naye aliona tukio hilo. Wawili hawa wakaongeza mwendokasi, kisha wakaupunguza baada ya kumuona baba mwenye jengo. Alikuwa amevaa msuli na alikuwa anapiga mluzi usiokuwa rasmi.
Wakamfikia na kumsalimia. Hakujibu!! Akawatazama kuanzia juu mpaka chini.
"Chukueni virago vyenu na huo umalaya mkaufanyie mlipokuwa mnaufanyia awali." Alizungumza kwa sauti nzito.
Hakuongea tena. Alimaanisha anachosema.
Nguvu zikawaishia. Wakauliza hawakujibiwa. Safari hii hawakulia. Huenda waliamini kuwa wameumbwa kwa ajili ya kuja kuteseka duniani.
Mchana kweupe wakavitwaa virago vyao. Wakatoweka kimya kimya. Mahali ilipokuwa gari iliyosadikika kuwa ni ya George hapakuwa na kitu tena!


Wakarejea mtaani!


******


Moshi wa sigara ulipepea juu kwa fujo. Kikohozi kikasikia kikitokea eneo lile. Mvutaji hakuwa mzoefu!
Mara likapita kundi la wanaume wawili. Mmoja akajongea hadi eneo lile. Baada ya dakika kadhaa akajongea eneo la siri na msichana ambaye alionekana kuwa muoga sana.
Licha ya kupiga kelele za maumivu lakini kilichotakiwa kilifanyika.
Huyu alikuwa ni mteja wa kwanza.
Biashara ikazidi kukolea alipofika tena mteja wa pili na wa tatu. Msichana mdogo akahisi kuchoka lakini yule mpokea pesa alimbembeleza kuwa asichoke!
Yalikuwa ni maeneo ya Buguruni jijini Dar es salaam. Majira ya usiku eneo ambalo wasichana huuza miili yao.
Huenda hawa wengine kwa hiari yao wenyewe walifika eneo lile. Lakini huyu mmoja alikuwa analazimishwa na ilikuwa siku ya nne.
Alilazimika kukubaliana na hali kutokana na makubaliano baina yake na yule mama. Makubaliano ambayo sasa yalikuwa yanamtesa.
Hakuwa na wa kumtetea kwa sababu alikuwa yatima. Tena chokoraa mzoefu!
Pesa aliyoingiza ilitumika kumnunulia nguo zinazomuacha uchi mwili wake, nguo maalumu kwa ajili ya biashara ya kujiuza.


"Unaitwa nani mpenzi!" mwanaume ambaye kwa umri alikuwa analingana kabisa na mzazi asiyejulikana wa mtoto huyu alimuita kimapenzi wakiwa garini. Huyu alikuwa amelipia huduma ya kulala na mtoto huyu hadi asubuhi popote atakapo na vyovyote awezavyo ilimradi amelipia itakiwavyo.
Yule msichana hakujibu!! Alikuwa katika majonzi!
Mwanaume asiyekuwa na aibu akanyoosha mkono usiokuwa na nidhamu akamminya chuchu. Mapigo ya moyo yakaenda kasi kwa hasira.


Hatimaye gari ikapaki katika hoteli ya kifahari!
Chumba kilikuwa kimelipiwa tayari. Mtoto na baba yake wakaingia chumbani kama mtu na mpenzi wake.
Walianzia kuoga. Hapa binti alivumilia japo hakupendezwa na biashara hii isiyomfaidisha yeye.
Walipotoka kuoga chakula kilichoagizwa kwa njia ya simu kilikuwa tayari pia. Wakaanza kula huku yule mwanaume mwenye tumbo kubwa akijaribu kutabasamu kila mara.
Ukafika wakati wa kuzima taa. Giza likaambatana na mambo ya giza. Mwanaume akaanza kumpapasa mtoto. Mara amfinye huku mara kule. Chokoraa akawa ametulia tuli. Hakuwa na jinsi.
Akafikia hatua aliyotaka akatimiza haja zake mara nyingi awezavyo. Binti akavumilia adhabu hii.
Kilichotokea baada ya hapa ndio kilibadili hali ya hewa na historia ya huyu binti.
Yule mwanaume akaanza kumlazimisha kufanya jambo ambalo yule binti kwa elimu yake ndogo alikuwa anafahamu madhara yake. Yule mwanaume asiyekuwa na staha wala huruma sasa alikuwa akimtaka mapenzi kinyume na maumbile.
Haikuwa ombi bali lazima.
Hapa zikaibuka zile kumbukumbu zote chafu tena za kuumiza za vituko wanavyofanyiwa chokoraa. Kila chokoraa ni chokoraa. Analotendwa chokoraa huyu basi na kwa mwenzake linaleta uchungu.
Mimba za kubakwa, vifo kwa sababu ya njaa, matusi kutoka kwa watoto wenye wazazi, ulawiti kwa watoto wa kiume. Aliyakumbuka hayo yote kisha akamkumbuka rafiki yake wa muda mfupi lakini uliojaa mengi mtaani.
Frida!
Alipokumbuka jina hilo, akashambuliwa na hisia kuwa huenda Frida alikufa kwa mateso kama haya anayotaka kupewa yeye.
Akapingana na roho ya mauti, akajisikia ujasiri.
"Sifi kabla ya kukulipia kisasi Frida. Popote ulipo wewe na machokoraa wengine na damu hii iwe juu yangu kwa kuwatetea ninyi!" alijisemea kimoyomoyo huku akijaribu kupambana na yule bwana aliyekuwa anakaribia kufanikisha uovu ule kwa nguvu!
Nguvu za ajabu zikauvaa mwili wake. Udhaifu ukaondoka bila kuaga, akazikumbuka mishemishe zote za kufukuzana na polisi mitaani, kupigana na machokoraa wakorofi. Akajisikia ni shujaa wa kike na anatakiwa kuthibitisha ushujaa wake.
Hakuwa tayari kufanya mapenzi kinyume na maumbile.
Kama risasi akajichomoa mikononi mwa yule mwanaume. Aliposhuka kitandani akaikanyaga sahani waliyotumia kulia chakula.
Ule mlio wa kisu na uma ukawa kama umemuita. Akarejea akainama akaokota vyote viwili. Kisu upande wa kulia na uma upande wa kushoto.
Maumivu aliyoyapata huyu bwana pendapenda. Ni heri angeuwawa kwa risasi. Hayasimuliki.
Mwanadada huyu chokoraa aliyegeuzwa kitega uchumi alichoma popote alipoweza. Palikuwa na giza. Aliporidhika akachukua nguo zake akavaa. Bila akajifuta mikono yake. Kisha akawasha taa. Hakutaka kuona kiumbe kinachokoroma kitandani.
Akahakikisha hana damu mikononi. Akaufungua mlango. Kama vile mzuka akatoka nje akimpita mlinzi kama kivuli.
Pale nje akawakuta chokoraa wawili wakiwa wamelalia mkeka. Alitamani kuwasogelea ili ajue kama ni wa kike ama kiume lakini akahofia kushtukiwa alichofanya ndani.
"Nimefanya kwa ajili yenu!" alisema kwa sauti ya chini.
"Ewe mzazi wa Mwanaidi, mwanao nimefanya jaribio la kujiokoa sijui kama nimeua!" alizungumza akizitazama mbingu.
Laiti kama Mwanaidi angepata ujasiri wa kuwajulia hali chokoraa wale. Angekutana na rafiki yake mpenzi. Frida!!


Lakini hakufanya hivyo!!!


Siku iliyofuata mauaji haya yakapamba vichwa vya magazeti!


***MWANAIDI anaamini harakati za kujikomboa na udhalilishwaji ni kuua….je yupo sahihi chokoraa huyu? Na je alifikaje hapo alipo kutokea kuwa mgonjwa mahututi na kupotezana na Frida???


***GEORGE naye amepotelea wapi?? Je ni kweli amekufa!!!


***FRIDA na ISHA mtaani tena!!!
culbby sam II
 
Last edited by a moderator:
Dah, Casuist hadithi yako imenigusa! Hongera kwa kuelezea maisha ya hawa viumbe kiustadi ili ulimwengu ujue!
 
Last edited by a moderator:
SEHEMU YA KUMI
RIWAYA: CHOKORAA
MTUNZI: George Iron Mosenya


SEHEMU YA KUMI
Mwanadada huyu chokoraa aliyegeuzwa kitega uchumi alichoma popote alipoweza. Palikuwa na giza. Aliporidhika akachukua nguo zake akavaa. Bila akajifuta mikono yake. Kisha akawasha taa. Hakutaka kuona kiumbe kinachokoroma kitandani.
Akahakikisha hana damu mikononi. Akaufungua mlango. Kama vile mzuka akatoka nje akimpita mlinzi kama kivuli.
Pale nje akawakuta chokoraa wawili wakiwa wamelalia mkeka. Alitamani kuwasogelea ili ajue kama ni wa kike ama kiume lakini akahofia kushtukiwa alichofanya ndani.
"Nimefanya kwa ajili yenu!" alisema kwa sauti ya chini.
"Ewe mzazi wa Mwanaidi, mwanao nimefanya jaribio la kujiokoa sijui kama nimeua!" alizungumza akizitazama mbingu.
Laiti kama Mwanaidi angepata ujasiri wa kuwajulia hali chokoraa wale. Angekutana na rafiki yake mpenzi. Frida!!


Lakini hakufanya hivyo!!!


Siku iliyofuata mauaji haya yakapamba vichwa vya magazeti!
****
TABASAMU pana lilijitengeneza katika uso wa mwanamama Diana, alifurahia kuhesabu pesa alizokuwa amejikusanyia usiku uliopita. Ilikuwa biashara nzuri sana yenye faida kubwa bila kutokwa jasho. Alichokifurahia katika biashara hii ni kwamba walioteseka na kuumia ni watoto wa wengine sio wa kwake.
Hakubahatika kupata mtoto! Hivyo uchungu wa mwana hakuujua.
Mfanyakazi wake mpya alikuwa akimuingizia kipato kizuri sana. Alifurahia kuwa naye na hakujuta kumchukua usiku ule alipokuwa na hali mbaya ya kukimbilia mauti maeneo ya posta jijini Dar es salaam.
Haikuwa bahati mbaya kwa mama huyu. Hiyo ilikuwa kawaida yake kuzurura usiku na kuwatafuta watoto wa mitaani jinsia ya kike kwa ajili ya biashara yake inayomuweka mjini. Biashara ya kuuza miiili ya wasichana.
Alipomaliza kuhesabu pesa zake ndipo akakumbuka kuwa Mwanaidi hakuwa amrejea hadi muda huo. Hakushtuka sana, aliujua usumbufu wa wateja hasahasa waliolipia huduma kwa pesa nyingi.
Ngoja ngoja huumiza matumbo!!! Subira ikamshinda ilipotimu saa nne asubuhi. Akaamua kumpigia mteja wake simu. Simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Alipiga mara ya pili. Haikupokelewa pia.
Akaamua aendelee kusubiri.
Akiwa katika kusubiri alipokea mgeni. Akajiandaa kwa kunawa uso wake akajitia vipodozi bila hata ya kuingia bafuni. Akatoka!!
Mzungu!!!
Biashara nyingine nzuri.
Huyu alikuwa ni mmoja kati ya wateja wake wakongwe. Katika mazungumzo, huyu mzungu naye alikuwa anahitaji huduma za Mwanaidi. Diana akafanya tabasamu huku akiendelea kujisifia kwa kumsaidia Mwanaidi sasa anatoa matunda!!
Mzungu alilipa kwa dola huku akiahidi kurejea majira ya usiku kumchukua Mwanaidi.


Masaa yakasogea hatimaye jua likazama, hapakuwa na dalili ya Mwanaidi kuonekana. Pesa za watu zikaanza kumtokea puani Diana. Akajiuliza kulikoni hadi muda huo Mwanaidi hajarejea wala mteja hajapokea simu!!!
Halafu sipajui kwake dah! Alifanya majuto Diana. Si kwa kumuonea huruma Mwanaidi bali kulilia pesa alizopokea kutoka kwa mzungu zisije zikapeperuka.
Hofu ya jambo hili ilimfanya Diana ashindwe hata kuwakagua vyema watoto wanne wageni walioletwa kwa danganya toto ya kufanya kazi za ndani wakati ukweli ukiwa ni kugeuzwa biashara katika danguro hilo ambalo mchana huwezi kudhania kuna uchafu huo ndani. Na hata usiku usipokuwa mwenyeji utaambulia patupu.
Majira ya saa mbili usiku, hapa ndipo simu ya Diana huanza kuwa bize. Na siku hii kama kawaida simu zilianza kuingia. Mmoja kati ya wateja wake alikuwa ni Saimon, huyu alimweleza kuwa yeye ni mgeni na anahitaji kuonana naye. Alitumia lugha za kiujanja ujanja hatimaye Diana akampa maelekezo yote. Jinsi ya kumfikia anapopatikana.
Magomeni Mapipa!!
Wakakubaliana kuonana baada ya masaa kadhaa!!


*****
MWANADAMU ni mnyama lakini ana utofauti mkubwa sana na wanyama wengine. Binadamu ana damu ya ajabu. Damu ambayo ukiimwaga basi inakukaa kichwani.
Hali hii ilimtokea Mwanaidi baada ya kuondoa uhai wa bwana mnene aliyetaka kumdhalilisha kijinsia. Akili yake ikamruka na ikagoma kutulia. Alikuwa na hasira siku nzima. Alijiona yu tofauti na wanadamu wengine alikuwa na chuki huku ujasiri ukiwa umemtawala.
Alikuwa anatamani damu nyingine tena na tena!!


Usiku huo alimalizia safari yake katika sehemu maarufu kwa kuwa na machokoraa wenye hasira na wakorofi.
Feri!!
Mwanaidi hakuwa katika hali ya msichana dhaifu bali alikuwa jasiori sana. Ni kama alikuwa ameuvaa uanaume katika mwili wake wa ndani.
Wavulana aliowakuta pale walitaka kumsumbua lakini hakuonekana kutetereka na alithibitisha kuwa alikuwa na uenyeji wa mahali hapo miezi mingi iliyopita.
Mwanaume mmoja akamvuta Mwanaidi pembeni. Mwanaidi akamueleza shida yake.
Akataja neno ambalo linachukiwa na machokoraa wote na yatima popote pale. UONEVU!!
Mwanaidi akadai kuwa kuna mtu anamuonea.
Unataka kuijua hasira ya chokoraa!! Muonee mwenzao mmoja wakujeruhi wote kwa pamoja!! Hivi ndivyo ilivyokuwa.
Machokoraa sita, Mwanaidi akiwa mmoja wao. Waliusubiri usiku. Wakati Mwanaidio akiwaza kumuadabisha Diana, wengine waliwaza na kingine cha ziada. Kuadabisha na kuiba!!! Maisha yalikuwa yamewabadili watoto hawa na kujikuta katika mkumbo huu.


Majira ya saa mbili usiku. Danguro likiwa kimya kabisa. Kichwa kimoja kiliingia ndani. Vingine viwili vikingojea kwa makini. Nyumba ilikuwa imezungukwa kimya kimya.
"Mwanaidi mwanangu jamanii…..yaani nilikuwa nimechanganyikiwa." Diana alimkumbatia Mwanaidi baada ya kuwa ameingia ndani. Mwanaidi naye alimkumbatia kinafiki huku hasira ikizidi kumkaa kooni.
Walizungumza mawili matatu. Katikati ya maongezi Mwanaidi akapaliwa. Akaanza kukohoa kwa sauti ya juu sana. Diana akaanza kumpigapiga mgongo. Wakati akiendelea na shughuli hiyo aliguswa mgongoni. Alipogeuka alikutana na sura za kitoto lakini zilizokomaa.
Alipojaribu kupiga kelele. Aliwahi kuzibwa mdomo.
Baada ya dakika chache. Mwili wake ulitua chini ukiwa haujiweza kunyanyuka tena milele. Na mahali pale hapakuwa sahihi yake. Alitakiwa kuhifadhiwa mochwari!!
Simu yake ilikuwa inaita wakati kiumbe huyu anaaga dunia!! Bila shaka na dhambi yake ilimfuata.


Viumbe wale wakatoka nje!!
Walipokuwa wanatoka gari dogo lilipaki nje ya ile nyumba!!!
Hawakujali. Wakapotelea gizani.
Wawili waliompekua Diana walikuwa na pesa kadhaa mifukoni.
"Dili kama hizi ndo tunataka. Safi sana komando." Walimpongeza Mwanaidi. Ambaye bado hakuwa akijielewa elewa.


****


GARI dogo lililopaki nje ya danguro lilikuwa la Saimoni. Alikuwa amechukua ruhusa kazini kwenda kutimiza wajibu wa kuipeleleza kesi ya mauaji ya mwanaume katika hoteli. Alizitazama namba zilizokuwa zikimpigia mara kwa mara na kuzihifadhi namba zolizokuwa zinampigia marehemu. Namba ya Diana ikawa inapiga mara nyingi zaidi.
Akaamua kufuatilia. Kwa mbinu za kikachero akafanikiwa kuiteka akili ya Diana. Hatimaye wakakubaliana kuonana usiku.
Kwa maelekezo ya Diana, mkongwe huyu wa jiji la Dar asingeweza kupotea.


Maajabu! Baada ya kufika eneo lile simu zikaacha kupokelewa. Alipiga zaidi ya mara mbili nab ado hali ilikuwa ile ile.
Saimon akaamua kuingia ndani, baada ya kugonga mlango bila kujibiwa. Nyumba ilikuwa imejigawanyagawanya katika vyumba vingi.
Akausikia mlio wa simu akaamini huko patakuwa na mwenyeji. Akajongea. Kila simu anayopiga ilivyoanza kuita na mlio wa simu ndani ya nyumba uliitika.
Upesi akavamia kile chumba kwa tahadhari.
Kimya!! Akawasha tochi. Akakutana na mwili wa mwanamke mnene ukiwa umejikunyata ardhini na damu zikiwa zinamtiririka.
Tatizo!!
Simu ikapigwa kituoni.
Baada ya muda nyumba ikazungukwa.
Msako mkali ukapitishwa pale ndani.
Wakakutwa watoto wanne. Walilia kuwa hawajui lolote. Lakini kilio chao hakikuwasaidia kitu.
Frida na Isha walikuwa kati ya watoto hawa!!!
Ilikuwa ni siku yao ya kwanza katika kazi hii waliyoipata. Kazi ya ndani!! Na ni siku hii hii walipigwa makofi na kuambulia kulala katika kituo cha polisi magomeni Usalama.
Walitakiwa kusaidia upelelezi!
Hawakurundikwa katika chumba kimoja.
Walitengwa!! Frida kivyake na Isha kivyake.
Matatizo juu ya matatizo.
Sasa wanakabiliwa na kesi ya mauaji wasiyoyajua.


Siku waliyoulizwa kuhusu uwepo wa wazazi wao. Wakadai kuwa hawana wazazi wao ni watoto wa mitaani ndipo uzito wa kesi hii uliongezeka.
Kila mtu aliamini kuwa watoto wa mitaani hawana utu! Wanauwezo wa kuua na kujeruhi bila wasiwasi.
Mahakamani hawakupata dhamana!!
Ukikosa dhamana mahakamani ukiwa umetokea rumande ya kituo cha polisi. Unahamishiwa mahabusu katika gereza!!
Frida akatupwa Segerea.
Isha makazi yake yakawa gereza la Keko!


Nani wa kuwatetea watoto hawa!! Hawakuwa na mtetezi. Hivyo mtu wa kufanya msukumo wa kesi yao kutajwa hakuwepo. Wakaendfelea kusota gerezani, kula mlo mmoja kwa siku.
Kulala kwa tabu! Yalikuwa mateso ambayo hawakuyatarajia.
Dunia ilikuwa kimya ikitazama yote haya.
Bila kutoa msaada!


Mwanaidi aliipata taarifa hiyo ya chokoraa kutuhumiwa kumuua mwajiri wao, kupitia magazeti. Picha za wale machokoraa waliovimba kutokana na kipigo hazikuonekana vyema sana. Lakini kuna jambo Mwanaidi aliliona. Na kumfananisha mmoja wao na mtu ambaye wamewahi kuonana hapo kabla.
Ni Frida huyu ama mwingine!! Alijiuliza baada ya kuyasoma majina ya chokoraa hawa.
Akapanga siku aende kuwapelekea chakula!


Jumamosi!! Hii siku ikafika akajiunga na watanzania wengine kwenda kusalimia wafungwa na mahabusu!


***FRIDA na ISHA ndani ya mahabusu kwa kesi ya mauaji wasiyoyajua.
***MWANAIDI anajua kitu na sasa anaenda kuhakikisha kama kweli ni Frida anayemjua ama la! Je akiwa ni yeye kitatokea nini??


VAN HEIST muuza ubuyu amina mabata shabani hassani culbby sam II
 
Nashindwa hata kutafakari kitakachotokea.... maana yakutokea ni mengi ... ngoja nisubiri
 
SEHEMU YA 11
RIWAYA: CHOKORAA
MTUNZI: George Iron Mosenya


SEHEMU YA KUMI NA MOJA


Kila mtu aliamini kuwa watoto wa mitaani hawana utu! Wanauwezo wa kuua na kujeruhi bila wasiwasi.
Mahakamani hawakupata dhamana!!
Ukikosa dhamana mahakamani ukiwa umetokea rumande ya kituo cha polisi. Unahamishiwa mahabusu katika gereza!!
Frida akatupwa Segerea.
Isha makazi yake yakawa gereza la Keko!


Nani wa kuwatetea watoto hawa!! Hawakuwa na mtetezi. Hivyo mtu wa kufanya msukumo wa kesi yao kutajwa hakuwepo. Wakaendfelea kusota gerezani, kula mlo mmoja kwa siku.
Kulala kwa tabu! Yalikuwa mateso ambayo hawakuyatarajia.
Dunia ilikuwa kimya ikitazama yote haya.
Bila kutoa msaada!


******
MIEZI minne baadaye baada ya Frida na Isha kusota rumande hatimaye waliachiwa rasmi baada ya kuonekana wanajaza selo ilhali hawana kubwa linalowakabiri.
Mwanaidi aliwapokea mtaani ambapo aliwaambia kuwa ni pachungu kulio huko jela walipokuwa.
Wote wakajihisi wana laana!!!
Majira ya saa kumi na moja jioni. Mwanaidi alitoa wazo la kuvamia shrehe ambayo yatima wamealikwa kwa ajili ya chakula cha mchana na usiku. Hawakuwa na ujanja wa kupata chakula kwa siku hiyo. Njia ya kuingia katika sherehe hiyo ikawa pekee kwa ajili yao.
Wakajikongoja hadi katika viwanja vya Biafra kinondoni ambapo paliandaliwa kwa ajili ya jambo hili.
Watoto walikusanyika. Wote walitangaza jambo moja katika nyuso. Huzuni!! Hakuna aliyekuwa na furaha ya moja kwa moja.
Majira ya saa moja usiku nao wakawa kati ya kundi kubwa la watoto.
Na ulikuwa muda muafaka kwa ajili ya kupata chakula.
Utaratibu maalumu ulifuatwa bila mtafaruku, mambo yote yakaenda sahihi.
Walipomaliza kula ukafuata wakati wa vinywaji. Hapa sasa aliyeandaa sherehe hii alizungumza mengi huku akiwasihi watoto hawa yatima na machokoraa kutokata tamaa katika maisha yao.
Katika kunogesha maongezi yake aliwasimulia stori kuhusu chokoraa. Ilikuwa inasisimua sana huku ikiwatoa watu machozi.
Frida aliyekuwa amesafiri maili mia kwa mawazo aliguswa na simulizi hii. Mara akatajwa jina lake!!
Aliponyanyua uso wake. Alidondosha chupa yake ya soda!!!
Mshtuko!!!


****


Burudani pekee iliyosalia katika maisha yake ilikuwa kuandika hadithi na mashairi ya muziki baada ya kile alichokoipenda maishani kuingia doa. Fani yake ya kucheza mpira iliingiliwa kati na matatizo ya moyo. Moyo wake ulikuwa umetanuka.
Majibu ya daktari yalimuweka katika kipindi kigumu cha maisha yake!! Hakutakiwa kucheza mpira wala kufanya kazi zozote ngumu!!
Haya akayaweza, mara nyingine figo yake ikajaa michanga. Aligundua matatizo haya baada ya kuwa anaumia kila akinywa maji ya kunywa. Tatizo lilikuwa limefikia pabaya sana wakati linagundulika.
Laiti kama walezi wake wasingekuwa na pesa na kazi nzuri pia kuishi vizuri na majirani huenda angekuwa amegeuka chakula cha funza zamani sana. Lakini hadi sasa anaishi baada ya kupelekwa nchini India ambapo alifanyiwa upasuaji na kuondolewa michanga hiyo. Akarejea Tanzania akiwa mzima wa afya.
Walezi wake walimpenda sana. Licha ya kwamba walimuokota akiwa ametupwa jalalani na mama yake wa kumzaa. Walimtunza kama mtoto wao.
Familia nzima ilimpenda na alikua na kukomaa akiwa mtoto wa familia ile ya watoto sita na yeye akihesabiwa kuwa damu ya mzee Emmanuel Magembe na mkewe Emelensiana .
Na haikustaajabisha alipopewa jina lenye ubini wa familia hiyo.
Akakua hadi kufikia utu uzima akiitwa George Emmanuel.
Wazazi hawa walimueleza juu ya uhusiano wake katika familia hiyo. Alimlaumu sana mama yake na baba yake wa kumzaa kwa kitendo hicho cha kikatili. Lakini lawama zikaishia hewani wazazi wake hawakuwa wakimtambua na yeye hakuwahi kuwatambua tena.
Mapendo makubwa kutoka katika familia hii yalimfanya ajisikie amani kila mara. Alipoingia shuleni ndipo alianza kukutana na watoto wasiokuwa na wazazi na wanaishi katika mazingira magumu. Huu ukawa mwanzo wa George kujiuliza ni kipi afanye kwa ajili ya yatima wenzake.
Alipoanza kuandika. Akagundua si tu kipaji cha kucheza mpira kilichokuwa ndani ya damu yake bali pia kipaji cha utunzi na uandishi wa simulizi mbalimbali.
Alianza na simulizi za mapenzi, mara za kichawi. Zote hazikudumu sana. Ni hapo alipoanza kuandika maisha halisi ya yatima anaopata kukutana nao.
Alikuwa chuo mwaka wa tatu wakati anakutana na Frida.
Alijifunza vitu kadhaa kwa Frida lakini hakupata muda wa kumuhoji zaidi akapatwa na maswahibu ya kuitwa mwizi kisha kupokea kipigo kikuu.
Akiwa hospitali ya wilaya ya Temeke, familia yake inamuhamisha na kumkimbiza nje ya nchi.
Pesa iliongea!!!
Matibabu yalipokamilika na yeye kupata nafuu. Walirejea tena Tanzania.
George alikuwa anapendwa sana. Na kupitia familia hii alijifunza mambo mengi sana. Kubwa zaidi likiwa kumcha Mungu!!!
Upendo maradufu aliopewa alitamani sana siku moja atoe zawadi kwa familia hii. Mwanzoni alitegemea kutoa zawadi kipindi atakapokuwa mchezaji katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania. Ndoto zikakatishwa na upana wa moyo wake.
Alipoanza kuandika, akapata zawadi nyingine kubwa ya kuizawadia familia yake.
Kitabu cha simulizi za kweli kuhusu watoto wa mitaani!! Na yatima. Alikiandika kimyakimya bila kumshirikisha mtu yeyote!!
Alipokutana na Frida akazidi kutanuka kimawazo. Na kuamini kuwa ataandika kazi nzuri mno.
Kumpoteza Frida lilikuwa pengo kubwa kwake. Baada ya kumkosa kule alipokuwa anaishi zamani. Aliungoja muujiza wa Mungu kumkutanisha tena na chokoraa huyu wa kike.
Alingoja sana lakini bado hakukutanishwa na Frida.


Alipomaliza elimu yake ya chuo kikuu miezi kadhaa baadaye, badala ya kuwazawadia wazazi wake kitabu kisichokuwa kamilifu aliamua kuandaa sherehe ili aweze kula kunywa na kufurahi na yatima wenzake.
Alizungumza nao mambo mengi sana. Sasa ukafika ule wakati wa kugonga chupa na watoto wote waliofika katika mualiko ule.
Ilikuwa shughuli pevu kuwafikia watoto wote. Hivyo wale wa karibu walipata nafasi hiyo.
Baada ya pale wakafanya sala ya pamoja kisha wakaagana huku George akilia. Alilia sana kwa kuwa wenzake walikuwa wanarejea mitaani kuhangaika na mbu wakali wasiokuwa na huruma.
Misukosuko ya vijana wakorofi na mengine mengi!! Yeye alikuwa anarejea kulala katika kitanda cha futi sita kwa sita huku ndani pakiwa na kila kitu.
Mawazo yake yaliyomtoa machozi yalikatishwa na sauti kali iliyomuita!!
Ni kweli alijitambulisha jina lake hapo kabla. Lakini hii sauti ilimkaa vyema masikioni. Akasita kupanda katika gari akageuka. Akakutana na mikono mingi ikimpungia.
Akasita kuondoka lakini akawa anajiuliza huyo anayepunga ni yupi?? Hakupata jawabu.
Alitaka kuendelea mbele ile sauti ikaita tena!! Sasa zilikuwa nyingi zikisaidiana. Akatazama kwa makini akawaona wasichana watatu wakipenya kundi kubwa. Akawasubiri huku akijifanya hazisikii sauti za walezi waliokuwa wakimsihi apande garini.


Uso wake ulikuwa umechakaa sana lakini sauti yake yenye mikwaruzo bado ilikuwa inasikika vyema.
"Frida!!" alishangaa George, kisha akachomoka kwa nguvu akamkumbatia Frida!! Mwanaidi na Isha wakawa watazamaji.
George alimvuta Frida pembeni kidogo. Mshtuko alioupata hakujua hata aulize kipi na kipi asiulize.
Frida alijilazimisha kutabasamu.
"George, nipo na rafiki zangu. Tumetokea rumande..bila kosa tumefungiwa miezi mingi. Najihisi naumwa sana, naumwa. Imekuwa kama bahati kukutana nawe. Iwapo ni vyema tafadhali tusaidie chochote kitu. Kesho niweze kwenda hospitali na walau leo niweze kulala mahali penye unafuu. Nahisi mgongo wangu umeoza..najua naumwa vingi lakini kama I sahihi kwako naomba unisaidie nateseka!!!" alijieleza Frida. George akapepesa macho na kujizuia machozi yasimdondoke. Jicho la kuume likakosa subira likakubali kulia, na la kushoto likapatwa na tamaa likaiga maisha ya jicho la kuume likalia. Koo likajibana, kwikwi ikatoka mfululizo.
Hatimaye George akawa analia kama mtoto huku akimtazama binti aliyechujika ngozi yake, nywele chafu kama kichaa, macho yaliyobonyea kuingia ndani na mabega yaliyopanda juu. Sahau kuhusu mavazi yasiyostahili kuitwa mavazi.
Frida alijisikia vibaya. Kila jicho lilikuwa linamuangalia yeye!!!


George alitumia dakika tatu akaingia garini. Akarejea na bahasha, akamnong'oneza kitu Frida kisha akampatia. Wakaagana akarejea garini na kutoweka.
Mwanaidi na Isha wakamwekea ulinzi Frida. Wakatoweka eneo lile.
Shilingi laki moja za kitanzania na simu ya mkononi!!
Hivyo ndo vitu walivyovikuta katika bahasha. Frida akalia sana kilio cha furaha huku akimwombea George kwa Mungu amjalie Baraka zaidi. Isha na Mwanaid wakaitikia ‘Amen'. Kisha wakajicheka maana hata kanisa wala msikiti hawakujua vilipo!!
"Amesema kesho nimtafute!!" hatimaye Frida aliwaambia wenzake!! Huku akichukua namba ya simu iliyoambatanishwa katika simu iliyopo ndani ya bahasha.
Siku hii walilala nyumba ya kulala wageni na siku iiyofuata asubuhi. Frida na Isha walimtembelea daktari kwa ajili ya matibabu!!


****


Frida na Isha walisikilizwa na daktari, wakafanyiwa vipimo kisha wakapatiwa dawa za bei ya kawaida. Wakatoweka.
Wakati wanatoka hospitali walipishana na mtu ambaye alisababisha Frida na Mwanaidi wote watazamane na kugundua kuwa wameona kitu cha kufanana. Mwanaidi aliukunja uso wake kwa hasira.
"Mungu atatulipia.." Alisema Frida. Mwanaidi hakutaka kukubaliana na hilo ombi.
Roho mbaya ikamuingia. Roho isiyokuwa na uoga.
Akaitamani tena roho ya mwanadamu!!
Hyu alikuwa ni mkuu wa kituo cha kulea yatima kule Mbagala. Aliyemnyanyasa Frida kisha akamtelekeza akiwa na mimba.
Sasa anaingizwa hospitali. Wawili hawa wanamuona.
Frida anaweka ubinadamu mbele.
Mwanaidi anauvaa unyama!!!
Hawashirikishi lolote akina Isha na Frida lakini anawaza juu ya kumuadabisha yule mwanaume asiyekuwa na utu.


***GEORGE atafanya nini ili kuwasaidia chokoraa hawa!!!
**MWANAIDI atafikia hatua gani!!


VAN HEIST muuza ubuyu amina mabata shabani hassani culbby sam II
 
Casuist asante sana mkuu, nilikuwa kijijini mawasiliano ni mpaka upande ule mti wa mission kwa padri. Imenigusa sana.
 
Last edited by a moderator:
Casuist, Asante sana kwa simulizi ya chokoraaa, baadhi ya sehemu zimenitoa machozi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom