Riwaya: Banguzi

Riwaya: Banguzi

RIWAYA: BANGUZI
NA: HASSAN O MAMBOSASA


_____SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA________


"Sapraaaiziiiiiiii! Happy birthday", Sauti za mabinti wengi zilisikika wakiwa wapo mlangoni huku wameshika sahani yenye keki ndogo yiliyobeba mshumaa unaowaka.


____________TIRIRIKA NAYO


Loh! Kwa jinsi alivyopatwa na kihoro alimanusura haja ndogo imtoke, alitamani hata kuwapiga wenzake kwa kumshtua huko. Siku hiyo alijihisi ameingia kwenye himaya asiyoitambua kwa jinsi matukio ya hapo awali yalivyokuwa yakijitokeza. Lakini kwa kujitokeza wenzake mahala hapo alijua wazi huo ni sehemu ya mchezo waliyokuwa wakimfanyia.

Tangu kuanze kwa siku mpya ambayo daima hungi saa sita kamili usiku wa manane, hakujua kama kuwaambia wenzake siku inayofuata ni siku yake ya kuzaliwa kungeweza kupelekea hayo. Alidhani wangeweza kumfanyia kituko muda ambao kumeshakucha, kumbe wanamngoja majira hayo

Alikumbuka jinsi Heriety alivyomwaga anatoka kwenda chumbani kwa Alice mara moja, mdua huo akiwa yupo kitandnai akijiandaa kulala. Hakujua kama hakurudi na usingizi ndipo ulipompitia, hadi wamefikia hatua ya kumfanyia kioja kama hicho.

"Happy birthday to you! Happy birthday to you! Happy bithday! Happy birthday! Happy birthday to youuuu!", Walimwimbia huku wakimsogeza sahani yenye keki pamoja na mshumaa, alitakiwa kuuzima naye alitimiza jambo hilo bila hiyana.

Baada ya hapo alianza kuwalisha keki mmoja baada ya mwingine miongoni mwa watoto hao wa kike, muda mchache baadaye alishamaliza kuwapa wote na sehemu ya chakula kile kwa jili ya siku hii maalum kikabaki. Gina alichukua kipande kingine akiwa amekiweka kwenye kijiti akiwa amejiandaa kumlisha anayefuata, hakujua kama miongoni mwa mabinti hao tayari walishamalizika. Alibaki akiangaza kuona atakayekuja mbele ila hakukuonekana aliyesogea mbele kulishwa. Akiwa yupo namna hiyohiyo, umeme ukazimika tena kwa mara nyingine na kuwafanya watu waachie miguno ya fadhaa.

"Aaaah! Jeta unazingua sasa hebu kwanza njoo toka huko kwenye korido, kupewa main swichi naona ushaingiza mengine", Grace alisema huku akitazama upande ambao kuna ngazi kwenye hosteli hiyo zinazoenda ghorofa ya juu. Umeme uliwashwa kwa mara nyingine lakini muitwaji, hakujitokeza.

"Jeta please njoo basi", Heriety alihimiza.

Gina aliposikia anayehitajika mahala hapo, alipeleka shingo ngazini. Akiwa na hamu haswa ya kumwona kwenye siku yake muhimu, wakisubiri afike yeye aliona kama kijana huyo ni mwenye kukawia mno kusogea hapo na kupelekea hata atamani asogee eneo alipo amlete kwa nguvu.

Ukimya uliganda na wote wakitazama huko, muda huo kukaanza kuonekana kivuli cha mvulana ambacho kimetokana na kumulikwa na taa ya ghorofa ya juu yenye mwanga mkali kuliko ya eneo walilopo. Hatimaye alijitokeza Jamal akiwa amevaa nguo ya mazoezi chini, juu akiwa na fulana iliyokatwa mikono yake na kufanya mkono wake wote uwe wazi. Nywele zake majira hayo alizichna kimtindo ambao uliweka uwazi sehemu ya pembeni ya utosi.

Binti aliyeshtukizwa alipomwona, alijikuta akimwoneshea ishara ya kumpelekea keki kuonesha kipande hiko ni muhimu kwa ajili yake. Jamal alipoona ishara hiyo, alijikuta akiganda hapo kwa muda mfupi kisha akapiga hatua kwa mwendo wa taratibu kwenda kupokea kipande hicho cha keki.

Hatimaye alifika na kulishwa, baada ya kumalizika hiyo alikumbatiwa kwa namna ambayo haikuwa kutokea tangu ajuane na binti huyo. Hakufanya ajizi hata kama aliwahi kumfanyia mengi kipindi cha nyuma, alimpokea na kupelekea waliyopo hapo wapige makofi. Muda huo ikitokea hilo, tayari baadhi ya wanafunzi wa chuo wanaoishi jengo hilo, ambapo hawakualikwa wajitokeza nje na kushuhudia tukio hilo.

Gina ilikuwa ni faraja kubwa kwake, jambo ambalo lilikuwa likiutesa moyo wake kwa muda mrefu. Alihisi limeanza kupunguza uzito, kwa kumalizika kwa tukio hilo alijiona ni kiumbe wa pekee. Hata walipoingia chumbani mwao, wote kwa pamojana kuanza kuongea kwa furaha. Siku hii alijiona ni wa pekee kwani Jamal alijibu na kuongea naye kwa furaha. Haikuwahi kkutokea jambo kama hilo kabla ya hapo, alijiona yupo huru zaidi fuadini mwake.

Maongezi yaliponoga, aliona ni muda mwafaka wa kusahihisha kile ambacho aliwahi kukiharibu kipindi kilichopita. Aliamua kuinuka alipoketi kitandani kisha akajongea hadi mbele ya Jamal, alipofika alimwonesha ishara ya kumpa mkono. Kijana naye bila ajizi aliupokea ambapo alivutwa hadi akasimama wima huku wengine wakishuhudia. Alimvuta kuelekea nje ya chumba hicho, Jamal naye alifuata tu mithili ya Kondoo anapelekwa machinjioni.
"Lui mbona namna hiyo? Jeta mna nini nyinyi mbona sirisiri tu?", Grace aliuliza kimzaha.

"Ushasema kisirisiri, toka lini siri ikaelezwa?", Jamal alirejesha jibu la swali kwa mtindo huo akiwa amefika mlangoni na Gina tayari yupo nje.

Alipojibu anavyojua yeye, aliurudishia mlango kisha akamtazama Gina ambaye amesimama takribani mita moja kutoka hapo alipo. Mikono akiwa ameifumbata kifuani mwake, na kufanya sehemu ya mwili wake ziilizokuwa zimefichikana zijichora kwa juu ya fulana kubwaaliyovaa.

"What?", Jamal aliuliza akimaanisha anahitaji kujua alichomwitia hapo.

"Iam sorry", Gina aliomba radhi.

"Sorry for what? Au bado unakumbuka ile past hostility?"

"Ni kosa nililifanya na sikuomba msahama, kukaa nalo hadi hivi sasa nikiwa nimekufanyia mengi makubwa. Jeta nilirisk maisha yako kwa kukupush mtoni, bado nikapelekea pia ulazwe kwa kukuambia maneno mabovu wakati wewe ni mtu mzuri. Nisipoomba msamaha nitakuwa kiumbe wa aina gani mimi?", Gina alipoongea hayo, Jamali alipiga hatua hafifu kumsogelea kisha akaweka viganja vya mikono yake mabegani mwake.
"Upendo huishi milele, ila chuki ni jambo la muda mfupi na baadaye hutoweka lenyewe. Usitegemee mimi kukwambia nakuchukia siku ile, nitaweza kubakia namna hiyohiyo milele. Chuki kwangu ni sawa na neno ambalo naweza kuliongea miaka mingi iliyopita na nikalisahau, hayo yote nilishayafuta akilini mwangu ndiyo manaa nilipoitwa na Heryn leo nilikuja bila hiyana. Nina moyoni wa dhahabu daima hung'aa, hata ukiingiwa na uchafu basi huondoka. Sahau kuhusu hilo"

Maneno hayo yalimtoa kijana huyo akiwa na uso wenye umakini, alipomaliza kuyaongea mwenyewe binti alijikuta akijikuta akimkumbatia kwa nguvu huku akitokwa na matokwa na machozi. Alijuta haswa kwa aliyowahi kumfanyia, hata kuambiwa amesamehewa uchungu ulibaki bado mtimani mwake.

Jamal alipoona kilio kilio hicho alimtoa kifuani mwake na kusema,"No! No! Usifie huko, nitaondoka sasa hivi kama unalia. Hebu tabasamu basi, ukishindwa tu sibaki hapa naondoka na hutoniona ng'oo!". Maneno hayo yalimfanya Gina atabasamu mwenyewe, namna ilivyotolewa na jinsi uso wa kijana alivyouweka hakuna ambaye angeweza kununa.

"Good girl, twende ndani", Jamal alimshika mkono na kugeuka nyuma kisha akashika kitasa cha mlango, aliufungua na kuingia naye ndani ambapo alikuta mabinti wenye kuongea ila walipomwona tu walikaa kimya ghafla.

"Waoneni nyinyi hamna haya hata, mlikuwa mnatusema tu", Aliwaambia.

"Sasa kuondoka huko kisiri ulitegemea nini, unajua girls ndiyo tulivyoumbwa", Heriety alisema.

"Kama ni mpango wa kuwateka nyinyi nyote au kuwalipua, napo tuwaambie kama tunaenda kujadili namna gani tutawateka au kuwalipua. Sasa huko tutakuwa tunafanya ujuha", Kauli hii mabinti walicheka wenyewe.

"Basi mshindi wewe, ila ulipolia kama Paka huko dirishani umemuweza sana huyo", Grace alisema.

"Inamaana sauti ya paka huko nje wakipigana kumbe ni huyu Jeta?,", Gina aliuliza.

"Huyohuyo tena hakuwa nje wala nini, alipita chumba cha kina Fetty akatokea dirishani. Akifanya ujinga huo alikuwa amejibanza kwenye zege ya dirisha", Heriety alisema.

"Mnajua huyu anajitafutia majanga huyu, sasa Jeta ungeanguka je?", Gin alisema.

"Mwenzangu mimi nilijiuliza hilo, ila kwa utundu wa huyu ilibidi tukae kimya", Nasra alinena.

"Sasa si mpaka nikianguka, sijaanguka sasa utajuaje ilikuwaje?"
"Haya mshindi wewe", Heriety alisema
"Girls nafikiri ni time ya kuondoka, ngoja niwaache mpige umbea tutaonana asubuhi. See you"

"See you!", Mabinti wote kwa pamoja waliitikia, Jamal aliatoka nje huku akiwa na bashasha usoni mwake kutokana na yaliyojiri siku hiyo.

_____________

Majira hayo Kevi ambaye ni mwanafunzi wa chuo hichohicho, alikuwa yupo kifuani mwa binti mnyange aliyeweza kumnasa ndani ya siku hiyo. Aliachiwa chumba mwenyewe kutokana na kuingia na mwandani, hakujali ni wangapi waliyokuwa wakiteseka kwa kuwatumia huko. Alichojua ni kuendelea kuonja tu ladha ya kila binti mpya, kufikia mwaka wa kwanza wa masomo alishamaliza wanafunzi wengi na hata akawa ni mwenye kujijengea jina kwa tabia yake mbovu hiyo.

Akiwa yu mchezoni, daima huonesha ni namna gani anaujua ufundi huo usiyohitajika ujuzi wa kalamu zaidi ya uzoefu wa kuijua miili tofauti ya mabinti. Msichana aliyekuwa yupo kitandani majira hayo alimpelekesha haswa na hadi alipokuja kumaliza naye mchezo akawa hajiwezi kwa uchovu. Yeye wala hakuonekana kuchoka, ndiyo kwanza alikaa kitako kitanda cha chini cha chumbani humo kilichotumika kubeba mazito hayo.

Binti alipitiwa na usingizi, yeye akabaki akimtazama tu umbile lake lilivyo huku akianza kumwona hafai majira hayo ambayo alimtumia vya kutosha. Kevi alianza kujiuliza kichwani alimfuatia nini haswa binti huyo, ilihali hakuona kigeni kwake. Msichana wa aina hiyo alishawatumia wengi mno, alibaki akiona haikuwa hata na haja ya kuja kumwita na kumchombeza hadi kufikia hatua ya kumchomoa kufuli. Hii ndiyo tabia ya wavulana wengi waliyo nayo, ubaya wa msichana huuona pale anapokuwa tayari amemjua ndani yupoje. Ila kabla ya hapo hutamani , huhamasika haswa kujua ladha ya tunda jingine. Loh! Yaani hata hujisahau kama tufaa daima huwa na ladha moja, labda itofautiane kutokana na asili. Haikuwa na ulazima wa kufanya hivyo, ujana tu ndiyo hupelekea watu wakajipelekesha namna hiyo.

Kevi akiwa amekaa kitao hapo, simu yake ya mkononi iliita kwa kutetemeka kwani aliitoa mlio. Hali hiyo ilifanya amtazame mrembo aliyejilaza mahala hapo, kisha akaitwa na kuipokea alipoona haina madhara kuongea hapo.

"Ndiyo Roja si unajua nimesizi na bibie sasa hivi, mbona simu usiku huu?........Unasema kweli wewe acha utani ndugu utaniua..............poapoa yupo wapi sasa hivi?!...........haya ngoja nifanye manuva fasta nitimbe huko", Kevi alikata simu kwa haraka kisha akamgeukia binti ambaye alipitiwa na usingizi, alimwamsha haraka kwa kumtikisa ila binti alikuwa mzito kutokana na uchovu aliyo nao.

"Sara! Sara! Mpenzi amka basi unisikilize?", Kevi alihimiza akionekana ni mwenye la umuhimu kumweleza binti huyo na kupelekea agutuke usingizini huku akifinya macho kwa uchovu.

"Nini Kevi, hujui kama nimechoka"

"Si unakumbuka nilikwambia Vice wa chuo ni mjomba wangu"

"Yap nakumbuka mtu wangu beibi, kwani kuna nini?"

"Kapewa taarifa huko sijui na mbea gani kama humu ndani nipo na mwanamke, yaani ninavyokwambia alikuwa anatoka kwenye sherehe badala ya kuuunganisha nyumbani kwake. Anakuja huku hosteli, Roja ndiyo kanipa taarifa sasa hivi"

"Unasema!", Binti alitamka hayo usingizi wote hata haukujulikana umepotelea wapi, alikaa kitako akiwa hana nguo hata moja"

"Yaani akikukuta huku jua ni msala huu, si unasikia alivyowahi kumfanyia Enoki alipomkuta na Gilda?", Kevi alisema huku akimrushia nguo zake yule binti akionekana amechachawa. Sara naye kwa upesi alivaa nguo hizo kwa pupa, alijikuta akiasahau kuvaa nguo ya ndani. Brazia nayo ilibaki kidogo aiache, Kevi tu ndiyo alimkumbusha akaiweka mwilini. Alipomaliza kuvaa kabisa, ndipo akakumbuka kuwa hakuvaa kufuli.

"Kevi sijavaa chupi nimesahau", Sara alianza kusema huku akainza kuvua suruali ya kubana aliyovaa. Kevi alipoona hali hiyo akaona ni kupoteza muda, kwa haraka aliiitwa nguo ile na kumuwekea mfukoni akaishindilia vilivyo.

"Sara kimbia fasta room kwako utaenda kuvaa hukohuko, huoni anaweza kufika na usiku huu foleni hamna", Alimwambia huku akimpatia viatu vyake visivyo na kisigino, Sara alipokea kisha akachukua simu yake iliyokuwa mezani na kutoka humo ndani kwa kasi akimwacha Kevi akimtazama tu.

"Ma**e ukisikia kufumaniwa ingekuwa leo hii yaani, ngoja nikapige maji fasta", Kevi alijisemea huku akichukua taulo na kutoka humo ndani.

______________

Muda ambao Kevi anatoka kwenda kuoga, eneo la takribani kilometa moja kutoka hosteli zilipo. Kulikuwa na kituo cha madereva teksi, hawa wengi wao hawakuwa na ratiba maalum ya kulala kutokana na utafutaji wao fedha uliyovuka kiwango. Walikaa wakisubiri wateja kwani asilimia kubwa ya wanafunzi hurejea usiku sana, au hutoka majira isiyofaa kwa ajili ya kwenda sehemu za starehe. Wengi walikaa nje ya magari yao kusubiri abiria, huku wakipiga domo pamoja na kunywa kahawa waweze kuondoa usingizi.

Mida hiyo ndipo ilipokuja kusimama gari binafasi karibu yao, milango ilifunguliwa na walishuka wasichana watatu pamoja na wavulana wawili kwa pamoja. Watu hawa watano walipoteremka waliongea maneno machache na waliyomo ndani ya gari ile kisha wakaagana nao na kusogea jirani na teksi hizo.

Maderva waliwachangamkia mno, kila mmoja akihitaji awapokee waingie kwenye ofisi zao. Wakigombea hivyo alichaguliwa mmojawapo ambapo waliingia wote kwa pamoja, msichana mmoja akakaa mbele na wengine wakatulia nyuma.

"Suka tuwahishe hosteli, si unapapata pale ninapostei", Mojawapo wa vijana aliyepo nyuma alisema.

"Roja nisipajue tena bloki unayoishi, mchanganuo uwepo tu", Derva alisema.

"Poa we twende"


*JAMAL ASAMEHE ALIYOWAHI KUFANYIWA NA GINA, JE NI RAHISI HII? ANAAMISHA MSAMAHA KWELI?

*KEVI AKURUPUSHWA CHUMBANI NA ROJA, KUNA NINI?




ITAENDELEA!!!
 
RIWAYA: BANGUZI
NA: HASSAN O MAMBOSASA


_______SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI_____


"Roja nisipajue tena bloki unayoishi, mchanganuo uwepo tu", Derva alisema.

"Poa we twende


_________TIRIRIKA NAYO

Dakika takribani kumi baadaye, waliwasili chini ya ghorofa ambalo Roja anaishi. Wote kwa pamoja walishuka na kumlipa dereva, gari ilipondoka walianza kutembEa huku wakipiga domo na kuzifikia ngazi ya eneo hilo na kuzipandisha kwa maringo hadi walipofika ghorofa ya kwanza ambapo ndipo kituo chao.

Roja akiwa mbele aliwaongoza wenzake hadi mlangoni mwa chumba kimojawapo, alinyonga kitasa lakini akakuta umefungwa na kupelekea agonge.
"Aaargh! Huyu kevi si bure atakuwa amelala leo kapiga msuli sana", Aliwaambia wenzake.

"He! Mnajua kuna watu wabaya dunia hii, na wale wambea walivyomwambia ana mwanamke humo ndani. Ona sasa Radhia ungekuja kujitia presha bure, nilikwambia usisikilize ya watu shosti", Mmoja wa wasichan alimwambia yule abinti aliyekaa mbele walipopanda teksi.

Banati yule naye alijikuta akikosa la kusema, ingawa bado alionekana ni mwenye shaka. Mlango ulipofunguliwa na kumwona Kevi akiwa amekunja uso kuashiria akionekana ametoka kulala, kidogo alionekana ni mwenye ahueni na aliachia tabasmau kisha akamsogelea na kumkumbatia kwa nguvu.
"Jamaa yaani huko ilikuwa ni tifu mno alikuwa haniamini huyu, haya huyo hapo. Shem tatizo wewe una wivu kupitiliza", Roja alisema.

"Akaa! Babu wee! Abiria huchunga chake, wivu sunna", Radhia alisema na kupelekea wengine wacheke.

"Haya jamani karibuni ndani", Kevi aliwakaribisha ndani huku akimtazama Roja halafu akampa ishara.

"Yaani mtu wangu tuache tu, kuna magashi hapa wanajua kumsemea mtu kam vile wanamwona", Mvulana mwingine aliyeongozana nao alisema.

"Jofu unajua kabisa, nina maadui wengi hapa chuoni fikiria wamemjua hadi Radhia anayesoma IFM huko. Jiulize hatujawahi kumwambia mtu, walimjua vipi?"

"Ndiyo hapo mtu wangu, Radhia leo alimpa kampani shosti wake tukiwa klabu, sasa kuja kutuona tu ndiyo wakaleta sumu zao hawajui watakuja kumuua mtu wale maboya", Jofu alisema.

"Sasa hivi roho yangu nyeupee!", Radhia alisema.

"Shosti nawe una wivu kupitiliza, unaweza kumtoa masikio dada yake huyu ukimwona naye", Binti mmoja alisema.

"Khaaa! Tabu jamani yashaisha basi" Radhia alisema kisha akamgukia Kevi na kumshika kidevu halafu akaendelea, "Eti baby kuna mapenzi bila wivu? Wivu si ndiyo mapenzi ati, au wewe hunioni wivu?"

"Haki ya Mungu natamani hata kushika bunduki nikikuona umesimama tu na ndugu yako kwa jinsi nilivyokuwa na wivu. Sasa fikiri nikikukuta na mwingine", Kevi alisema na kupelekea wengine wacheke.

"Kumbe bilabila hapa", Tabu alisema.

"Unafikiria ni mchezo nini kupenda sikieni, oyaa Kevi kile kitasa mbona hujakiweka freshi mwanangu?", Roja alisema kisha akaongezea kwa kumuuliza swali Kevi.

"Halafu unajua sikukusoma jamaa ulitaka kiwe namna gani maana ninakiona kipo sawa", Kevi alinena

"Hebu ngoja nikakuoneshe jamaa", Roja alisema huku akiinuka halafu akawaambia wengine, "Jamani tunarudi sasa hivi tunaenda kucheki kitasa, kuna ishu nilimpa akiweke sawa nikasahau kumpa maelekezo"

"Poa", Jofu ndiyo akawa wa kwanza kuitikia na kuwafanya hata wengine waone inatosha si lazima wainue wao midomo.

Wavulana hawa waliongozana hadi mlangoni na waliufungua, kisha wakatoka nje na kuufunga. Baada ya kufanya hivyo Roja alikichezesha kitasa karibia mara nne, halafu akamgeukia Kevi. Walipotazama kila mmoja aliweka mkono mdomoni na kuanza kucheka kimyakimya, kuhofia wangeweza kusikiwa ndani.

"Ma**na wewe ungefumwa leo yaani ushukuru nilivyompanga mimi na Jofu", Roja alisema kwa sauti ya chini.

"Mam*e yaani leo nilikuwa naadhirika mtu wangu, hivi ulipata wapi huo muda wa kunipigia simu jamaa maana ulikuwa na Tabu"

"Mtu wangu ilibidi nichomoke fasta na kwenda chooni kule klabu, huko ndiyo nikakupa data zote anataka kuja huku ajihakikishe.Yaani hatujakaa hata hilo tifu lake, imebidi turudi tu. Hivi Sara umemtoa vipi hapa ulikuwa ushapiga show"

"Mtu wangu tayari mchezo na kalala pono, nilitaka niliamshe dude asubuhi ila uliponipigia simu nikamwambia Mgaya katonywa nimeingiza demu ndani anakuja huku yaani kafura kwa hasira", Kevi aliposema hayo Roja alicheka nusura atoe sauti, tena huku akiendelea kukichezesha kitasa ili wa ndani wajue wanaelekezana.

"Dadeki wewe mtu mbaya sana, yaani mademu wanavyomwogopa yule, umemuweza. Tuzame ndani jamaa yangu, stori zingine kesho si unajua huyo mtu wako leo hatoki leo", Jofu alisema huku akifungua mlango, aliingia ndani huku akitembea kwa taratibu na kwenda kuketi jirani na Tabu.

Kevi naye aliingia huku akisikitika halafu akasema, "Jamaa siku nyingine uache ubishi, kitasa chenyewe kumbe cha kufunguliwa kabisa maana hakifai kufix bila kufungua kile kimeshalegea chuma cha ndani"

"Beibi utamuweza basi huyu Roja, yaani ubishi wake kama Tatu hapa. Naona Mungu hakukosea kuwaweka pamoja", Radhia alidakia pasipo kujua hiyo ni sehemu ya kuzuga tu.

"Si unajua tena ndege wafafanao hukaa pamoja, huwezi kukuta Kipanga akakaa na Kuku", Jofu alisema na kupelekea waliyomo humo ndani wacheke mno.

"Sawa leo mmetuweza", Roja alisema huku akiinamisha uso chini.

_______________

Sarah akijua kule anakuja mjomba wa Kevi mule ndani, alifika jengo analoishi na mwenzake akiwa na hofu kubwa. Aliwasili chumba chake na kukuta tayari taa imezimwa na mlango umefungwa, aliugonga mlango kwa nguvu. Hakujibiwa jambo llilomfanya aendelee kufanya hivyo, ukimya ulipozidi alijikuta akichukua simu huku bado mapigo ya moyo yakimwenda mbio. Mawazoni aliona kama vile ndiyo anafuatwa na kaimu mkuu wa chuo hicho, hofu ilimtawala haswa.

Aliipiga simu ya mwenzake anayeishi naye humo ndani, lakini iliita haikpokelewa. Hali hiyo alijikuta akipigapiga nyayo zake zilizo ndani ya viatu alivyovivaa njiani hapo sakafuni. Alijaribu kwa mara ya nyingine, ila haikujiiwa mambo yakawa ni yaleyale. Alijikuta akikata tamaa ila nafsi ikamsihi apige tena, safari hii simu ilijibiwa. Alianza kuongea kwa pupa, "Atu! Ni.......nipo mlangoni nifungulie haraka..... usiniulize nifungulie niingie ndiyo nitakujibu....haya".

Simu ilikatwa na alijikuta akitazama kushoto na kulia kwa eneo hilo, hakuona mtu yeyote na alishusha pumzi za ahueni. Mlango ulifunguliwa na aliingia ndani kwa papara kuu, kisha akaufunga mwenyewe akabaki akihema kwa nguvu.

"Sara vipi mbona tunatishana? Kwani huko kwa shem kumetokea nini?", Atu aliuliza huku akifikicha macho.

"Atu acha tu, yule mzee mnoko si kaambiwa yupo na mwanamke hosteli. Yaani alikuwa yupo njiani anawahi kuja huko, asingepigiwa simu na rafiki yake aliyesikia hiyo habari sijui ingekuwaje?", Sara alisema.

"He! Nani?"

"Mjomba wake Kevi, Professa Mgaya"

"(Huku akiweka mikono kichwani) Mungu wangu yaani ingekula kwako leo, cha moto ungekiona, sijasahau alichomfanyia mwanae wa kumzaa na demu wake"

"Shosti mwenzangu yaani nimetoka mbio hata sijui nimepata wapi spidi ile. Chupi yenyewe sijavaa nimewekewa mfukoni kama leso", Atu aliposikia maneno hayo ya Sara, alijikuta akicheka kwa nguvu mno.

"Unacheka unaona mazuri siyo?" Sara aliuliza kwa sauti ya kulalamika.

"Yaani ulivyotoka huko wacha nicheke tu shosti, mbio unazijua kumbe siku zote unajifanya umechoka tu ukitembea umbali mrefu tu"

" Nyoo ingekuwa ni wewe ungefanyaje sasa?"

"Hebu tuache hayo, jitazame huko usije ukawa umejichafua kama kaenda bila ganda"

"Ngoja nivue tu nguo nikaoge usiku huuhuu", Sara aliongea huku akainza kutoa nguo ya juu.

Hakujua kama aliyoambiwa ni uongo uliyopangwa kikamilifu, kutokana na jinsi Kevi alivyoonekana kuwa na hofu kubwa alijua wazi siku hiyo ni sawa na kiama. Kumbe alichoelezwa hakijatokea, aliingia himaya ya waongo waliyotaka kumwepusha mwenzio asigonganishe magari.

_________

Asubuhi ya siku iliyofuata Jamal aliamka kwa kuchelewa kutokana na kulala muda mbaya, alikuta anayeishi naye chumba kimoja akiwa hayupo ndani. Alijiinua kwa uchovu mkubwa kisha akaketi kitako, hapo alijikuta akitokwa na tabasamu usoni mwake na alibaki ni mwenye kutafakari jambo fulani kichwani mwake.

Alipoteza muda kitandani na hatimaye alishuka kisha akachukua taulo na mswaki wake, alitoka nje ambapo alitumia robo saa akawa amerejea akiwa ameoga. Jamal alibadili nguo akatoka chumbani anapoishi na kufika hadi nje akaanza kutembea kwa taratibu akikata mitaa ya mahali hapo. Jamal hakuwa na hili wala lile majira hayo akitembea, alishtuka tu akipigiwa honi ya gari. Alishtuka na kusoge kando ya njia kabla hajaangalia nyuma, ila alipogeuka alijikuta akiachia tabasamua baada ya kuona msafara wa baba yake ukisimama.

Walinzi walishuka na kufungua mlango wa gari alilopanda bosi wao, JD alishuka akiwa na uso wenye furaha. Alifika na kumkumbatia mwanae, huku walinzi wakiwa wamesimama imara kuhakikisha usalama unakuwepo.

"Baba mbona ghafla hivyo?", Jamal aliuliza.

"Yote ni kuhakikisha tu kama upo ok, nilikuja muda mrefu mno nikatuma mtu aje kuangalia nikaambiwa umelala. Nimengoja umeamka hadi umetoka nje, ndiyo nikaja mahala hapa", JD alisema.

"Sasa baba kwanini usingekuja tu ndani, ulipaswa uniamshe mimi mtoto hukupaswa kunisubiri namna hiyo. Mimi ndiyo ninatakiwa kukusubiri hivyo nikikukuta umepumzika"

"Hapana nipo sahihi kufanya hivi nifanyavyo, nikuache upumzike kijana wangu sijajua umelala saa ngapi hadi nije nifikie kukumsha tu"

"Sawa, ila kuna kitu kimoja kama mwanao huwa sikipendi sana"

"Uko huru kusema"

"Sipendi mno kuongozana na walinzi wengi hivi baba, napenda uwe mwenyewe kama nilivyo mie", Jamal aliposema hivyo, JD aliuzungusha mkono shingoni mwake na kuanza kutembea kuelekea lilipo gari aliloshuka.

"Nimetokea familia yenye uhasama mno, Baba yangu alikuwa akiendesha mipango yake kibabe na kunipelekea mimi niingie kundi hilo. Hivyo nina maadui wengi mno, ukiachana na hilo ukumbuke nimetoroka Argentina. Sipaswi kujiamini muda wowote"

"Ok nimekuelewa, nahitaji uwe salama siku zote"

"Nimekufuata hapa tuwahi nyumbani kwa Bi Agatha si unajua kuna nini leo, ingia garini twende. Kwanza nafikiri tupitie ukaptae chai, nina uhakika hapo ulipo bado hujatia kitu tumboni"

"Hujakosea hata", Waliingia kwa pamoja garini, msafara huo uliondoka mahali hapo huku baadhi ya wanafunzi wakiwa wameona kile kinachoendelea na walibaki wakitazama tu kwa mbali.

____________


"Mwanangu Kevi we mbaya sijapata kuona yaani, una mbinu hatari", Jofu alisema huku akicheka, muda huo ni tayari mabinti wale waliyokuja nao usiku walishaondoka. Walibaki wenyewe tu, ndipo wakaanza kuijadili mada ya jana jinsi mwenzao alivyoweza kuepuka kikwazo kikubwa kwenye mahusiano yake.

"Yaani hizi harakati kama mjeda, vita nyingi ndiyo ujuzi unazidi. Ulitegemea ningefanyaje nimtoe gashi mule. Radhia naye si alikomalia aje huku", Kevi alisema.

"Ila we boya umezidi yaani sisi tunaenda klabu ukaona ni njia nzuri tu kujipiga mwenyewe humu. Ulitaka ukeshe kabisaa", Roja alisema.

"Sasa ulisema hurudi unachukua chumba kwa juu ujisevie, ulitegemea nifanye nini na mtoto kaingia kumi na nane yule. Sikuwa na mpango wa kupiga jana ila kaja humu mwenyewe eti kupiga stori, nikaona usinitanie wewe. Uingie pango la mamba utoke mzima wewe"

'Ukajipigia tu kumbe huko tulipo moto umewaka hata kuchukua vyumba tuliacha tuje tumwoneshe kadanganywa", Roja alisema.

"Wana tuacheni utani mimi ni mwongo wa kupanga mbinu za kila namna, ila gredi ya huyu boya sijafikia aisee. Una mbinu za ajabu", Jofu alisema.

"Mtu wangu ukizoea kudanganya akili inakuwa fasta tu kutunga uongo mwingine, nimepiga dabo sasa. Sara nikimwona namlia boksi kama simjui, yaani nakuwa nimepoteza kumbukumbu zake kabisaa"

"Namna hiyohiyo si kajileta, ufanyaje?", Jofu alisema.

"Dah! Akiniona atajua nina tintedi simwoni, yaani mikausho tu ninaangalia mwingine nani atajileta"

"Sema nini yule happy mnene fulani hivi kaingia saiti tayari, inabidi uniachie chinjio hili usiku wa leo namaliza mchezo humu", Roja alisema.

"Kupigia asteaste kwa Tabu umeona uje kutulizia kwa yule yote", Jofu alisema.

"Sasa kumbe je nifanyeje mimi, Mungu atupe nini sisi yaani watoto wenyewe wanakuja. Wacha nijipigie mwenyewe", Roja alisema.

"Sawasawa balozi wa shirika la wakataa mimba, Katibu mkuu wa wizara ya wasiyotumia ndomu"

"Sawa Spika wa Bunge la wavua chupi, mbunge wa jimbo la uzinzi", Roja alisema na kupelekea wote wacheke huku wakigonganisha mikono yao.


*LOH! HAWA WAHUNI HAWA WAMEZIDI
*DUH! KUNA WATU UONGO KAMA WALIINGIA CHUONI KUUSOMEA
*SARA KAINGIA ORODHA YA KEVI
*JE NINI HATMA YAO HAWA WAHUNI?




ITAENDELEA!!!
 
Safi sana...

Kevi na company yake washenzi sana...

Nahisi Jamal na Gina will end up together...


Cc: mahondaw
 
RIWAYA: BANGUZI
NA: HASSAN O MAMBOSASA


______SEHEMU YA THELATHINI NA TATU______


"Sawasawa balozi wa shirika la wakataa mimba, Katibu mkuu wa wizara ya wasiyotumia ndomu"

"Sawa Spika wa Bunge la wavua chupi, mbunge wa jimbo la uzinzi", Roja alisema na kupelekea wote wacheke huku wakigonganisha mikono yao.


_____________TIRIRIKA NAYO

Furaha yao na ushindi wao ni kuona maungo ya watoto wa kike tu, kwao ni mithili ya mwanajeshi apatapo ushindi kwenye uwanja wa vita. Huwa hajali namna gani mpinzani wake atakavyosononeka kwa kushindwa kwake, na hawa walikuwa ni hivyo kwa mabinti. Hawakujali hayo wayafanyao yangweza kuwa ni matatizo huko siku za mbeleni, walichojali ni kufanya kile nafsi yao inapenda.

________

Majira hayo kina Gina pamoja na marafiki kadhaa wa chuo chao, walikuwa wapo kwenye maduka ya kununua nguo na vitu mbalimbali vya kike. Siku waliazimia kuifanya iwe ya kipekee ndiyo maan wakawa wanafanya manunuzi makubwa kuliko kawaida. Kundi lote la watoto wa kike ambao daima huwa pamoja, walimaliza kutumia kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kujipendezesha tu na hatimaye walielekea nyumbani kwa akina Lui ambapo walikuwa wakisubiriwa kwa hamu kubwa ili waweze kufanya maandalizi ya sherehe ya kuzaliwa kwa binti huyo.

Walifika na kukuta baadhi ya vitu vikiwa vimeanza kuandaliwa ikiwemo eneo lakufanyia shughuli, baadhi ya ndugu ikiwemo wadogo zake Gina na hata Mama yake waliwapokea kwa furaha kutokana na kutarajia ujio. Mabinti hawa kwa pamoja walikaa sebuleni wakiongea machache na hatimaye wakahamia chumbani ambapo walikuwa huru zaidi.

Wote kwa pamoja walifikia kitandani huku wengine wakijiweka kwenye makochi, ilimradi kila mtu alipata mahali pa kuketi humo ndani. Muda huo ikiwa inaelekea majira ya kupata chakula cha mchana, wao waliamua kuupoteza kwa kupiga domo huku baadhi wakiangalia picha za mwenzao za miaka kadhaa iliyopita humo ndani.
"Gina halafu unajua usiku hukutupa mkanda kilichokufanya umwite Jetaa nje", Grace alisema akiwa amejilaza kitandani.

"Nanyi bado mna hayo tu, not a big deal just somethng special", Gina alisema.

"Bibi wewe ndo hatutakiwi tujue basi, toka ukaanza siri na sisi jamani", Heriety naye alidakia.

"Ndiyo hapo hata mimi namshangaa, wakati tupo wote for the long time", Nasra alisema.

"Jamani au nilifanya vibaya kumwita nje?"

"Nop, ila huo usiri wako huo nina wasiwasi kuna namna", Nasra alisema.

"Ni about the past girls, I want to clear my mistakes. Mnajua wazi nilikuwa namchukuliaje tukiwa Tambaza, kumbe he is a good guy kuwahi kutokea kwenye maisha yangu. Without saying sorry i will not be in peace"

"Nashukuru umeona kama ulikuwa ukikosea sana umfikiria vibaya Jeta, najua amekusamehe maana huwa haweki vitu moyoni yule", Nasra alisema.

"He is so strange, kumbe alishasahau tangu kipindi kile"

"That's why I love him, yaani yupo msafi moyoni haweki kitu", Heriety alisema.

"Oooh! No Heryn una boyfriend wewe na bado unampenda yule, hivi mfano ikitokea ndiyo kaja na kukupa maneno itakuwaje?", Grace aliuliza.

"Nitakuwa tayari kuvunja uhusiano na Moka ila si kumkosa huyu, najua haitowezekana maana He is in love too with another girl", Heriety alisema.

"Weeee! Inamaana Jeta ana girlfriend na unajua? Ni nani huyo?", Gina aliuliza.

"Simjui hata jina nasiki tu kwa jina la Angel aliniambia Alice, na hayupo bongo kwa sasa ndiyo maana unamwona yupo vile hana time na yeyote", Heriety alisema.

"Thats gurl is so lucky", Nasra alisema"

"Yeah! She won his heart", Grace alisema.

____________

Pamoja na kumsahau Jamal na kuendelea na maisha mengine, hadi akafikie kuweza kupata tulizo jingine la moyo wake. Bado kijana yule alibaki ni wa pekee moyoni mwake, alitamani ndani ya siku moja tu aweze kumpata kwenye maisha yake ila ndiyo hivyo aliona uwezekano ni mdogo.

Kuambiwa jina la msichana anayemiliki moyo wa kijana yule, kusikia yupo nje ya nchi na hakuwahi kurejea hata siku moja na kuweza kumtia machoni walau hata siku moja na kumwona ni ana kitu gani cha ziada cha kuweza kumpata kijana kama yule na wengine wote wamkose. Alijikuta akiishi na mawazo hayo kila siku, ingawa alishaingia kwenye mahusiano mapya akiwa chuoni.

Alice kipindi hiki yupo mapenzini na kijana mwenye kuitwa Tony, huyu alikutana naye hapo katika siku ya kwanza kufika chumbani kwa Jamal. Kijana alijikuta akimtazama kwa kitambo kirefu, binti hakustahimili hilo kutokana na kuingiwa na iabu machoni mwake.

Tangu kukutana hapo walianza kuwa marfiki kwa kipindi kirefu, hatiamaye wakaja kuangukia kwenye mapenzi. Huo ndiyo ukawa mwanzo wa kumpata huyo, ambaye hata Jamal alimfahamu vyema na alikuwa rafiki yake mkubwa tena ndiye aliyefanya binti akampenda.

Alice na Tony kwa siku hii walitoka kwa pamoja, walielekea hadi Mji mwema na kuishia kwenye ufukwe wa South beach. Wandani hawa walifikia kwenye kibanda kimojawapo cha eneo hilo, waliketi huku wakipata vinywaji kufurahia siku hiyo. Jinsi walivyokaa kila aliyekatiza, aliweza kumaizi wawili hao wana zaidi ya urafiki mioyoni mwao.
"Alice pamoja na kuongea mengi ila hujaniambia jambo moja tu",Tony alisema majira hayo akiwa amepakatwa kichwa chake mapajani mwa binti.

"Nini hicho mpenzi?", Alice aliuliza.

"Leo ni siku nzuri kwa Luigina yule shoga yake Heryn, nashangaa umeamua kuja kutoka kivyako"

"Tony, Heryn is my best friend but not Gina. Simpendi yule mdada hata sielewi kwasababu gani"

"Unamchukia mtu bila sababu kweli?"

"Hivi ushawahi kukutana na mtu, ukajikuta tu ni ghafla humpendi?"

"Yap ishawahi kunitokea hiyo ila nilipigana na hali hiyo"

"Ndiyo ipo kwangu na kupigana nayo siwezi, hata yeye mwenyewe ni hivyohivyo. Kiufupi hatupendani kabisa, hata Jeta nahisi yupo hivyohivyo kwa Gina"

"Jeta ni mtu mweupe yule, hakai na doa. Hawezi kuchukia mtu, ni mwanaume mwenye tabia za kiume"

"Kwani kukaa na chuki ni tabia za kike?"

"Sasa kumbe je? Chuki bila ya sababu haipo kwa wa kiume mwenye kujitambua"

"Haya mshindi wewe bwana, ila leo inabidi nitafute sababu ya kudanganya tu kwa kutoenda kwenye sherehe ya huyo Gina"

"Kwanini?"

"Sis Doreen na Shem Shehoza watakuwepo huko, unafikiri nisipoonekana mimi itakuwaje?"

"Alice, nakuomba usiact namna hiyo, go to her birthday"

"Tony!"

"If you love me, yu will go. Fikiria wewe kila mtu yupo pale halafu wewe taarifa unayo usionekane. Nakushauri ungana na dada yako uende leo tukitoka hapa", Tony alisema hivyo Alice alimtazama kwa kitambo kifupi, alikaza macho akitarajia mvulana huyo anaweza kuongea jingine na walau kulegeza uzi uliyokaza.

"Sipendi ujiingize kwenye chuki zisizo na sababu, wewe nenda kwenye party yake. Kama yeye anakuchukia akikuona mahali hapo, umekuja kumpongeza nadhani atageuka moyo wake. Nadhani ni muda wa kuishi na watu vizuri, hiki ndiyo kitu nilichojifunza baada ya kukaa na Jeta kwa muda mrefu kama roommate wake. Nimebadili mfumo wa maisha for my best friend Jeta na wewe naomba ubadili kwa ajili yake. Usipofanya hivyo nitakuona haupo upande wake", Tony alitilia mkazo
.
"Ok, I will"

"(Huku akijiinua kichwa chake na kumbusu mdomoni) Thats why I love you"

_______________



UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU NYERERE

Ndege ya shirika la ndege la Uswisi ilifika kwenye anga la uwanja huo, ilifanya mawasiliano na ofisi za uwanjani hapo na baada ya kila kitu kuwa sawa taratibu ilianza kushuka kwenye njia ya kutua. Magurudumu yote yakiwa yamechomoza, ililalia upande wa nyuma wa nyuma ambao kuna gia ya kutua(Landing gear/magurumu ya nyuma). Ikiwa namna hiyo ilienda mwendo wa kasi na hatimaye ikagusa ardhi, ilitembea namna hiyo na kisha magurudumu ya mbele nayo yakafuatia kwa kugusa eneo la hapo uwanjani.

Ilikimbia kwa kasi kubwa na hatimaye ilifika eneo ikapunguza mwendokasi, huku rubani wa chombo kile akifuata maelekezo ya mtu maalum anayemwonesha mahala pa kuegesha. Muda mchache baadaye ilisimama eneo la maegesho, ilitulia namna hiyo na hatimaye mlango ulifunguliwa kwa watu kuanza kushuka.

Watu wenye asili mbalimbali walionekana wakiteremka kwenye ngazi maalum iliyowekwa na gari. Mwishoni kabisa walishuka watu wawili wenye asili ya uafrika, ambao waliteremka ngazi hizo wakiwa wameshika mikono. Wakiwa na mizigo yao, walitoka mahali hapo kwa mwendo wa taratibu na kuelekea kwenye ofisi za uwanja huo kwa ajili ya kufanya taratibu na kuingia nchini.

Baada ya kukamilisha taratibu zote, walitoka kuelekea lango ambalo huwepo wenyeji wanaosubiri wageni. Watu hao wakiwa namna hiyo, walitembea na kufikia eneo hilo ambapo walikutana na Mwanamke mtu mzima akiwa amesimama na vijana wenye miili mikubwa. Kumwona huyo mahala hapo, walijikuta kwa pamoja wakimkimbilia na kumkumbatia huku wakitoa mayowe pasipo kujali wapo eneo lenye umati miubwa wa watu.

"Rocky, umekuwa jibaba mwanangu", Mwanamke yule alisema huku akimtazama mvulana aliyefika na msichana yule. Alimgeukia binti yule na kumwambia," Angel yaani usingewahi kunikumbatia ningekusahau kabisa ingawa nimekuwa nikiona picha zako ulizonitumia. Wanangu mmerejea, za masomoni?"

"Safi tu tunamshukuru Mungu tumemaliza salama", Rocky alisema.

"Kwanza anti niambie besti yangu yupo huko, yaani nimemisi kupitiliza sijui anafananaje sasa hivi?", Angel alisema.

"Nani? Mchumba wako Kimweri?"

"Antiiiii", Angel alilalamika.

"Na anavyompenda Msomali wake, kufika na kufika kamuulizia yeye", Rocky alisema.

"Rocky nitakudunda nyau wee!", Angel alisema.

"Kimweri yupo kama ulivyomwacha, siku hizi anatumia jina la Jamal"

"Aliniambia hilo nilipomtafuta kwa Skype tukawa tukiongea, nataka nimwone live alivyo tu maana nimeishia kumwona kwenye picha tu nataka laivu laivu", Angel alisema.

"Haya jamani twendeni kwanza mkapumzike, Kimweri wako utamwona kesho", Mwanamke huyo aliwaambia huku wapmbe aliyofika nao mahala hapo wakichukua mzigo yao halafu wakaanza kutembea kwa pamoja kutoka uwanjani hapo.

_______________

Majira ya mchana Jamal na baba yake walishafika nyumbani kwa akina Gina wakiwa wamependeza kupitiliza. Siku hii baba na mwana walivaa nguo zenye kufanana huku kila mmoja akiwa na mikufu kadhaa shingoni mwake ya fedha. Mikononi walivaa pete zinazofanana, majira hayo walifikia eneo maalum ambalo kulikua na viti na baadhi ya watu wakiwa wameketi kusubiri sherehe ianze.

Jamal alikaa eneo hilo akibadilishana mawazo na baba yake, lakini alihitaji pia kukaa na vijana wenzake. Aliomba ruhusa ya kufanya hivyo na aliruhusiwa, aliinuka na kwenda moja kwa moja mahali ambapo kuna baadhi ya vijana wakiongea. Alijiunga nao na kupiga domo kusogeza muda, alikaa hapo kwa dakika kadhaa napo hakudumu alikuja kuinuliwa na Grace aliyefika mahala hapo mara moja. Alivutwa mono kuingia ndani, alijikuta kenda tu kama kondoo hakuwa na pingamizi lolote lile hadi akafika kwenye sebule ya nyumba hiyo.

Mahali hapo alikutana na mabinti na wadogo zake Gina, hao walimkimbilia na kumkumbatia kwani tayari alishakuwa kama kaka yao. Kwa jinsi wanavyopenda kuchekeshwa. Walijikuta wakimwomba Grace amwache kwanza ambapo aliongea nao kwa muda mfupi. Mabinti hawa walicheka haswa, na muda anawaaga tayari Grace alishapanda chumbani kwa Gina. Ilimbidi naye aende huko, alitoka mahala hapo na kwenda moja kwa moja alipoelekezwa, akiwa na mwendo wa taratibu aliufikia mlango wa chumba ambapo aligonga mara moja kisha akatulia.

Mlango ulifunguliwa na Grace ambaye bila ya kusema kitu alimvuta mkono na kuingia naye ndani. Kijana huyu alijikuta akiwa ametokea eneo ambalo kuna mabinti watupu na kila mmoja akiwa amevaa tayari na ilionesha wazi walikuwa wakipiga domo na hakuna kingine wanachokifanya.

"Mmmh! Nimeingia chumba sicho kabisa", Jamal alisema huku akigeuka nyuma, Grace aliwahi kufunga mlango na kuuegemea.

"Ushaanza kujitoa akili wewe", Grace alisema.

"Haki vile naona nimeingia chumba cha midoli humu ndani, hivi Gina yupo na wengine wapo chumba gani?", Jamal alisema akijifanya hawaoni kina Gina.

"Kwani wale waliyokaa pale ni kina nani?", Grace aliuliza.

"Midoli naiona tu hakuna kingine"

"Huyu nyau anatutania make up zetu", Heriety alisema

"Kama hapo yaani Gina akitoka hadi kwa akina Spora watamuuliza hujambo maana wanamwona mtoto kuliko wao, sasa aamke asubuhi uone kama hajapokea shikamoo zisizo na idadi kufidia za jana kwa kutomtambua", Kauli hiyo ilifanya mabinti walicheka Gina mwenyewe ilikuwa ni hivyohivyo ila alijikuta akiinuka na kuanza kumkimbiza Jamal.

"Mmeona ukweli unauma, anataka kuniua", Jamal alisema huku akizunguka chumbani humo kumkwepa Gina, mwishowe alifikia kuketi kwenye kochi baada ya Gina kuanza kumkimbiza.

"Jeta naona leo micheni mingi mno, ukidondoka nahisi utatoa mlio wa kengele", Heriety alisema na kupelekea wengine wacheke.

"Haya mjanja wewe umeniweza kweli, mshua kanikomalia nivae kwa leo tu ningefanyaje sasa"


*TONY AMSHAWISHI ALICE KWENDA NYUMBANI AKINA GINA, JE ITAMALIZA CHUKI YAKE?
*VIPI GINA ATAMWONAJE ALICE ILIHALI HAWALANDANI?





ITAENDELEA!!!
 
RIWAYA: BANGUZI
NA: HASSAN O MAMBOSASA


_______SEHEMU YA THELATHINI NA NNE____

"Jeta naona leo micheni mingi mno, ukidondoka nahisi utatoa mlio wa kengele", Heriety alisema na kupelekea wengine wacheke.

"Haya mjanja wewe umeniweza kweli, mshua kanikomalia nivae kwa leo tu ningefanyaje sasa"


____________TIRIRIKA NAYO

"Safi sana huyo ndiyo baba sasa, anataka wanae wagombewe na si kingine", Heriety alisema.

"Baba yako anakupenda ndiyo maana anpenda upendeze Jeta", Nasra alisema.

"Kupendeza ndiyo na hii micheni kama kuonekana Dog wa kizungu", Jamal alisema.

"Hujioni tu ni jinsi gani leo unayoonekana HB, baba yako mtu wa kisasa sana kajua kukupa vitu vya kupendeza", Grace alisema.

"Mngejua kwanini sipendi kuvaa hizi cheni wala msingesema hivyo"

"Sasa kama una sababu zako unazificha sisi tutajuaje, ila umependeza kwakweli.

"Mmeona hiki kidani cha bawa kwenye cheni ambacho kipo hadi kwenye pete na hata cheni ile niliyompa Bi mkubwa wake Gina. Hii ni alama ya ukoo wetu ambayo inatumika tangu enzi na enzi, wakoloni hawajaja hii alama ipo. Yaani akitokea mtu yeyote ambaye anajua historia yetu basi atanijua mimi ni wa Barahain", Jamal alisema huku akishika mikufu aliyovaa.

"Jeta sijakupata hata kidogo", Gina alisema.

"Kiufupi ni hivi, Baharain ni ukoo uliyoanzia wa Abdulwahid bin Furhan Albaharain. Huyu ni mmoja watu wa zamani mno katika himaya ya Habaishi ambayo leo hii inajulikana kama Ethiopia. Alibahatika kuoa na kuacha mara nyingi na kupelekea ifike idadi ya wake ishirini aliyowahi kuwaoa kwenye maisha yake. Alipata watoto sitini kutoka kwenye uzao huo na wote wakiwa wa kiume watupu, hawa nao walioa na kuwa na familia zao ila waliishi kwenye viunga vya Mzee Abdulwahid. Kipindi kile familia huwa kama himaya na hivyo hutambulika kuwa na nembo maalum, alama ile ya bawa la ndege ndiyo ikawa ni alama ya familia ile. Miaka mingiabaadaye walienea sehemu mbalimbali za Afrika, ndugu wa ukoo huu wakawa ni wengi mno na wenye asili moja kama ya baba yangu. Wote walipokutana mahali popote duniani walitambuana kwa alama hiyo tu, ukoo huu ndiyo babu yangu Daud Dolan Albaharain yeye alizaliwa Somalia na mama wa kisomali. Yeye alihamia hapa nchini akiwa na mke wake na shemeji yake miaka iliyopita, alimzaa baba yangu hapa nchini. Jamani huwa sipendi mno kuwaeleza watu kuhusu hili jambo ila inapaswa mlijue ili msipende kuiongelea kwa watu. Alama hii kuivaa manufaa yake nikija kuvamiwa na wasomali wa sehemu yeyote ile, kama ni jamaa zangu huweza kunitambua ila kama ni maadui wa ukoo weu napo huweza kunimaliza kwa haraka", Jamal alisimulia.

"He! Jeta ndiyo sasa hapo utafanyaje? Kuvaa ni balaa na kuvua ni balaa", Heriety alisema.

"Nyinyi acheni tu yaani, ndiyo maana cheni sivai huwa naifunga mkononi si rahisi adui kunijua. Pia nikishikwa nitatumia kuwaonesha tu kama ni jamaa zangu wanitambue"

"Kumbe mna historia pana namna hiyo, sasa kwa kukadiria hivi ukoo wenu mnafika wangapi", Nasra aliuliza.

"Siwezi hata kutamka kwa mdomo hivihivi maana sina hata idadi hiyo ya kukadiria. Ila tambua tupo wengi na tumesambaa dunia nzima. Hebu fikiria toka karne zilizopita kuanzia kizazi cha mwasisi wa ukoo huu, unajua tumezaliwa wangapi?"

"Hapo ngumu kujua kwakweli, ila nasikia nyinyi ni watu ambao makatili kupitiliza yaani", Nasra aliongeza

"Makatili ni wengi ila siyo wote, hapa Bongo nadhani habari ya mzee wangu zinavuma sana. Ni kutokana na kutokea ukoo huo, pia babu yangu alikuwa ni mafia nadhani historia yake mlishawahi kuisikia"

"Kwahiyo hadi wewe nawe ni katili?", Heriety aliuliza na kumfanya Jamal atabasamu.

"Nilikwambia si kila mtu ana roho ya namna hiyo, wengi wamekuwa hivyo kutokana na kuwa na vita na familia zingine na kushuhudia ukatili mwingi. ikiria mtu akiwa toka mtoto anashuhudia hayo akikua itakuwaje"

"Loh! Mwenzangu ningekujua toka mwanzo ningekuwa mpole na si mtata kama kipindi kile", Gina alisema.

"Sipati picha nahisi mkojo ungekutoka kila unaponiona, au tumbo la kuhara lingekudaka", Kauli hiyo ilifanya wacheke mno, Jamal alinyanyuka kutoka kwenye kochi aliposimama na kusema, "Girls wacha nikapige domo na masela kule chini, niwape nafasi ya kuendelea kupiga umbea".

___________

Yakijiri hayo nyumbani kwa kina Gina, upande mwinmgine wa jijini ndani ya nyumba ya Leo ambayo haipo mbali kutoka ulipo ufukwe wa bahari. Mwenye nyumba hii alibaki akiumiza kichwa juu ya nyendo za kaka yake, alishazoea kuona akiua kwa mfululizo ila kwa kipindi hicho hakuwa amesababisha mauaji mengine tangu alipommaliza Dokta Yunus. Haikuwa kawaida hiyo, ndiyo maana majira hayo alibaki akifikiria juu yake.

Akili yake ilimwambia kuwa huenda una mpango mpya anausuka wka ajili ya kazi yake, au ameweza kukimbia nchi na kwena kwingine ilimradi tu aendelea na kufuru yake ileile ya kuangamiza watu. Alifikiri awezavyo na hadi kufikia siku hiyo, ilishatimia miezi akimuwazia yeye ila hakupata jibu lolote juu yake. Hata alipojaribu kuuliza nchi nyingine kama kumetokea mauaji ya madaktari, na hapo hakusikia kitu kama hicho ndipo akazidi kuwa shaka zaidi hadi mpambe wake akaona ayupo sawa.
"Leo si kawaida, siku za hivikaribuni nakuona haupo sawa kabisa", Mpambe wake aliulizaza.

"Tangu auawe Dokta Yunus hivi sasa nyendo za Jus sizijui zipo wapi kabisa yaani sisikii chochote kuhusu yeye. Huyu kaka yangu sielewi anajipanga na nini huko, ukimya wake huu wakati siyo kawaida inabidi nibaki na maswali tu. Asije akaja na mbinu nyingine na kuzidi kupoteza madaktari wasiyo na hatia"

"Hata mimi nimekuwa nikijiuliza hivyo, pengine huyu mtu amepooza tayari na dawa ile aliyopatiwa na Fernando"

"Thubutu, anatumia dozi kila siku ya kujizuia asifikie hatua hiyo. Huyu bado yupo hai anadunda mjini ila kabadilika tu"

"Tusidhanie tu, huyu jamaa tunamjua keshaondoka kwenye ulimwengu wanaotembea kwa miguu miwili"

"Hebu nawe jaribu kuifikirisha akili yako vizuri, dawa zile ambazo anatumia kujidanga ziliingia hapa Tanzania miezi miwili iliyopita. Yaani tani moja ya dawa zile imenunuliwa na mtu mmoja, kama si yeye ni nani na ukumbuke ananunua mzigo mkubwa mno"

"Sidhani kama ni yeye maana kununua kiasi hicho kungeweza kuwashtua watu wa Fernando kuwa yupo nchini. Wangekuja kumaliza kazi tu na wewe ukaondoka"

"Patro amka wewe naona umelala usingizini, ukiona kaachiwa hadi kaweza kuondoka nchini mule na kufikia huku basi jua hiyo ndiyo adhabu pekee aliyompatia hana haja naye tena. Kama shida ni kumuua basi asingemwacha akafika huku"
"Hapo umeniamsha akili yangu, hawatomtafuta. Ila nadhani Justus ni mtu hatari kupitiliza atakuja kuwasaka wao siku yeyote"

"Ataanzia wapi unafikiri, uhatari wa kaka yangu nataka nimmalize tu ili wengine wawe huru kama yupo radhi kumuua aliyemletea matatizo its ok. Maana bila yeye asingefikia huku na wala asingeasi jeshini"

"Hapo sawa, vipi na kuhusu mtoto wake tukishamuua yeye inakuwaje?"

"Mtoto wa kaka yangu ni mtoto wangu, nitamchukua na kuishi. Patro unajua ninampenda sana kaka yangu ila kwa njia aliyoichukua wacha nimchhukie tu"

__________________

Majira ya jioni shughuli iliyopangwa ilianza, waalikwa tayri walisiafika kuweza kutimiza wito wa wao kuja mahala hapo. Kukiwa na viti vimepambwa vilivyo, huku upande wa mbele akiwepo Gina pamoja na Herety wamekaa kwenye kochi moja kulifana shughuli hii na kupelekea watu wavutike nayo na kuwa makini kufuatilia kila kinachoendelea.

Upande wa meza mojawapo, Bi Mwanahawa, JD, Shehoza, Doreen, Jamal, Alice walikaa pamoja huku wakifuatilia kila kinachoendelea. Ukimya ulitawala kwa muda ambaqo mshereheshaji wa sherehe hiyo anaongea, hata minong'ono iliyokuwa ikiendelea kwa baadhi ya watu iliisha.

Ilipoanza kuletwa keki mahali hapo muziki maalum ulipigwa huku wageni wakinyanyuka na kucheza sambamba nao hadi uliposimama muda ambao watu maalum wa jikoni waliposogeza meza yenye keki mbele. Baada ya hapo ulifuata muda wa kuzima mishumaa ambapo walimwimbia Gina akitimiza jukumu hilo, lilipotimia hilo kukafuata tendo la kulishwa keki. Watu mbalimbali walifika hapo kuendana na majina yao kuitwa, hadi walipomalizika kwa pamoja.

Yakijiri hayo kwa mujibu wa ratiba, Gina aliweza kumwona Alice akiwa amekaa sambamba na Jamal kule kutokana na kukaa eneo la jukwaani huku waalikwa wakiwa chini. Hakumwita binti huyo kumlisha keki hata, ingawa ni sehemu ya mmoja wa rafiki wa Heriety. Moyo wake ulikuwa mzito kufanya hivyo, kumwona mahala hapo alitamani hata amtimue kwenye sherehe yake. Ila angeanzia wapi yupo karibu na familia ya Jamal, si ingekuwa mwanzo wa maelewano baina ya familia ya JD na familia yao kuondoka. Alisita tu kila akifikiria hayo, ila kiukweli hakutaka hata kuiona sura ya binti huyo mahala hapo kwa jinsi asivyopenda.

Muda wa kupewa zawadi ulipofika, alimwona akija kutoa zawadi iliyovika kwenye kasha maalum lenye kufunikwa na makaratasi laini ya zawadi. Alijikuta akikunja sura hata Heriety alijua hilo, ila alikaa kimya hakutia neno. Kutokuwa na maelewano mazuri yeye na Alice alifahamu vilivyo, kuiona hali ya kukunjika sura alishatambua chanzo ni Alice kuwepo hapo. Msichana asiyempenda aliweka zawadi mahali hapo akiwa na tabasmau pana usoni mwake, alimkumbatia na yeye akakubali kinafiki kumpatia kumbatio.

Alice aliporejea kitini alimsindikiza kwa jicho la pembeni, hadi rafiki yake mkubwa aliyeketi naye kochi moja alishika begani na kupelekea amtazame.

"Gina siyo namna hiyo shosti", Heriety alisema.

"Yaani ungejua Heryn we acha tu", Gina alisema.

"Hajawahi kukukosea na wewe hujawahi kumkosea, why muwe namna hiyo. Kaja kukusupport akiwa na familia yake, pia kabeba zawadi hii kakuleta hapa. Change your mind pal"

"Its difficult, na sijui kwanini nipo hivi yaani"

"Kuna msemo mmoja ambao Jeta anapenda sana kuusema ambao ni kwamba chuki haiwezi kumwongoza mtu ikiwa hatoruhusu imwongoze vilevile upendo hauwezi kumtoka mtu ikiwa hatoruhusu umtoke. Wake up"

"(huku akitabasamu) Yaani wewe na umemuweka Jeta misemo yake kichwani mithili ya falsafa za Plato kwenye GS"

"(Akitoa tabasamu hafifu) I love him hata kama I'm in love, yaani unajua yule ana wisdom mno kuna muda unaongea naye yupo kwenye masihara na kuna muda yupo serious mfano tulivyokuwa naye room mida ile"

"Ujue hata mimi nimemshangaa sana, alikuwa serious ingawa alianza na matani kidogo"

"Sasa akiwa vile ndiyo utaona yule ana uwezo kubwa wa kufikiria, ndiyo maana wengi wanampenda mno"

"Even me"

"(Muda huo Gina akitamka hilo Heriety alikuwa akinywa mvinyo usiyo na kilevi, alijikuta akipaliwa na kukohoa halafu akamtazama mwenzake) Gina ni wewe kweli ninayekujua au mwingine?"

"Yuleyule Gina, tukiwa A level nilikuwa wrong juu yake. Ila Heryn hukuwahi kuniambia kitu chochote kuhusu kule hospitali ya jeshi mlipompeleka", Gina alisema huku akiinuka kusogea eneo la chakula, majira hayo yalifika ilikuwa ni kwa ajili ya kupata chakula siku hiyo.

Heriety alimfuata nyuma huku akisema, "ningeanza vipi Gina kukueleza wakati kipindi kile hutakia hata kusikia stori yeyote kuhusu yeye na pia niliporudi wenzetu nao hawakuwepo hivyo sikuwahi kumweleza yeyote yule kuhusu hilo suala hadi leo"

Gina akiwa ameshafika eneo la chakula ananawishwa mikono alisema, "Thats was another mistake i made". Heriery naye alimwambia, "ngoja tuchukue msosi nitakwambia".

Walikabidhiwa sahani na walizunguka kwenye meza kubwa ambayo kuna wasichana wanaopakua chakula. Hapo walitiliwa kile wakitakacho, walipotoka hapo walielekea mezani ambapo ni tofauti na pale walipokuwa awali ambapo aliketi. Gina alimtazama Heriety akiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua, mwenzake aliamua asimfiche itu anachokifahamu.

"Jeta ana presha mbaya mno, yaani kama hatakiwi kuwa na hasira wala hatakiwi kuwa na msongo wa mawazo wowote ule. Ndiyo maana siku ile akawa namna vile, yaani alikata network kabisa", Heriety alisema.

"Jesus!" , Gina alisema kwa mshtuko mkubwa.

"Huo ndiyo ukweli Gina, hata siku ile alivyoanguka uwanjani ilikuwa ni hiyohiyo. Hatakiwi kufanya kazi nzito pia nasikia"

"Sasa hizo stress si risk kwenye maisha yake jamani"

"Thats the truth, yaani ndiyo maana muda wote unamwona ni mtu wa kucheka tu na kutabasamu na si kununa. Amechagua aishi namna ile ili awe salama, so Gina my friend kama uliwahi kujaribu kumkera don't try again"

"So sad, thats smile hide many things kumbe. I like him"

"(Huku akimtazama kwa jicho la pembeni) Kama akija kukupiga mistari je?"

"Yaani wewe nyau wewe, kila muda unawaza hiko tu. Love love love all time"

"Tumezaliwa tupende na tunaishi ili tupende, hivyo tupendane. One of his quote"

"He! Nawe yaani umekremu misemo yake, hebu kula huko"

"They call it, we call it, you call it, and I call it love", Heriety alijibukwa kutia mistari ya nyimbo ya msanii Lionel Richie kutoka Marekani.



*HAYA MAPENZI KWA JAMAL, UPI MIWHSO WAKE?
*JE ZAWADI ALIYOPEWA GINA ITAWEZA KUMBADLISHA?






ITAENDELEA!!!
 
Msione kimya jamani, wizi umekithiri mtu anafungua hadi blog na kuhamisha riwaya zangu kama anajua nilipata tabu gani kuandika.

Humu riwaya ikikamilika inabebwa, ndo maana nikaamua nisitishe. Nimeshuhudia riwaya zangu mbili ns ya The Bold moja imechukuliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom