Hassan Mambosasa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2014
- 3,387
- 4,609
- Thread starter
- #41
RIWAYA: BANGUZI
NA: HASSAN O MAMBOSASA
______SEHEMU YA KUMI NA TISA______
Wenzake wakicheka, aliona ni karaha mno sauti zao. Alitamani hata nao wapatwe na hali kama yake, ndiyo hivyo halikuwezekana. Hakika jinsia ya kike ikijua kuchukia, basi hilo ni balaa kubwa lisilo na kipimo. Jinsi anavyopewa kipaumbele na mhusika mwenye siku yake, na namna ambavyo watu wanavyokongwa nyoyo na vituko vyake ndiyo kulizidi kumfanya aungue nafsini mwake.
_________TIRIRIKA NAYO
Hali hii aliyo nayo Gina, laiti kama Jamal angeliitambua mapema basi asingeruhusu itokee kwake. Lakini ndiyo hivyo hakuwa na walau umaizi juu ya suala hilo, yeye aliona sehemu hiyo mambo yote yalikuwa yakienda sawa. Tabia yake ya kupuuzia mambo, ilimfanya wala asiwe na fikra juu ya binti zaidi ya kumwona ni asiyejitambua ingawa amefika kwenye ngazi kubwa ya elimu ya sekondari.
Hatimaye Jamal alishuka chini akiwa hana hili wala lile, akakumbatiana na Heriety kwa furaha. Alipoketi kitini tu, mabinti wengi walimfuata na kila mmoja akiwa anamwongelesha na kuhitaji ajibiwe. Wapo waliyotaka kupiga naye picha na wala hakuzuia hilo alikubali bila hiyana. Kijana aligeuka kuwa nyota wa sherehe hiyo kuliko hata mwenye kuhusika nayo, muda huo hata Heriety mwenye alikuja kuketi naye karibu kutokana na kumuhusudu mno.
Aliongea naye kwani ni faraja tosha kwake kutokea jambo kama hilo, binti alipenda kumwona kijana kila muda. Alihitaji haswa walau kuliona tabasamu lake kila saa, ni mwenye kutaka kusikia sauti yake yenye kumletea bashasha kila aitoapo. Hakika alifika mno kwake, ila hakuwahi kuonesha ishara yeyote ile kwake. Jamal hakuwahi kufikiri jambo kama hilo kama litakuwepo kwa Heriety, alimwona ni rafiki tu na wala hakuwahi kumwonesha ishara yeyote ya kumpenda.
Ndiyo maana hakuwa na shaka yeyote akiwa yupo karibu yake, laiti kama angelikuwa na tatizo naye basi asingeliweza kuwa naye namna hiyo. Gina aliitwa kujumuika nao mahala walipo ambapo walikuwa na baadhi ya marafiki wengine, hakuweza kupinga hilo ingawa moyoni alilaani mno jinsi utaratibu unayoenda hapo. Walikula kwa pmoja chakula huku Jamal akiendelea kuwafurahisha, hadi wanamaliza.
Hatimaye muda wa kucheza muziki ukafika, Heriety akaomba kuufungua muziki na kijana anayemhusudu. Shoga yake ndiyo akawa anaungua moyoni kabisa kwa kuona anapewa kipaumbele, alitaka kuona hata awe kafukuzwa kwenye sherehe hiyo lakini ndiyo jambo hilo halikuwezekana hata kidogo.
Muziki ulichezeka hadi ilipofika usiku mnene zaidi, ambapo watu walianza kupungua mmoja baada ya mwingine na kusoge eneo la jirani ambapo kuna mahema. Wachache walielekea zilipo hoteli eneo hilo wapumzike. Wengine waliendelea kuburudika hadi ilipokaribia alfajiri ndipo kila mmoja alikwenda kulala, muda huo Jamal aliongozana na watu wake aliyokuja nao hadi kwenye hoteli iliyopo jirani na hapo akaenda kupumzika.
______________
Watu wakiuchapa usingizi upande wa Bagamoyo, ndani ya jiji la Dar es salaam kwenye uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere. Watu maalum waliyovaa suti nyeusi walionekana wakiwa wamesimama eneo la kusubiri wageni. Hawa walijipanga vyema huku kukiwa na mtu mzima mwenye asili ya usomali akiwa amesimama mbele yao.
Haikuchukua muda mrefu wa kujipanga hivyo, aliingia mwanaume wa kisomali mwenye suti nyeupe akiwa na mikufu kadha ya rangi ya fedha shingoni ambayo kila mmoja ulikuwa na kidani chenye kung'aa. Huyu alipoonekana mbele ya mwanaume wa kisomali alionesha tabasamu usoni mwake, halafu akamkumbatia kwa nguvu mno huku akionekana ni mwenye kumkumbuka mno.
"JD ni miaka sasa hujarejea nchini, nimekukumbuka mno mdogo wangu", Mwanaume mpokezi alisema.
"Anko Husa kazi kwa Fernando ni nyingi mno, yaani sasa hivi nimeamua kustaafu kabisa huko na kuja kuendesha miradi yangu. Vipi mwanangu hajambo? Katibiwa?"
"Hajambo ila mambo ni yaleyale hakuna jipya, ila nikupe pongezi kwa kuwa na mtoto mwanafalsafa namna ile", Husa alisema kisha akamwongoza JD hadi nje ambapo kulikuwa na magari kadhaa ya kifahari yenye kuwasubiri. Aliingia gari moja naye, huku mizigo yake ikiwekwa nyuma na safari ya kuondoka mahala hapo ikaanza msafara ukiwa mrefu.
"Hebu nipe mpya yote yaliyojiri kipindi chote ambacho mimi sipo, nitahitaji muhtasari tu lakini mkanda mzima tukifika nyumbani uniambie"
"Ni mengi mno yaliyojiri ila kikubwa ni kwamba, Mwanahawa ni kanuna mno kwa kutorejea kwako miaka zaidi ya kumi hadi mtoto kawa mkubwa. Yaani anamlea yeye na mimi nikitoa msaada ila anaona kama umemtelekeza"
"Nitaanzaje kuitelekeza damu yangu mimi, kwanza yupo wapi huyo mwanamke hivi sasa? Nahitaji sana kumwona kijana wangu Kimweri"
"Karejea kwao sasa hivi, ila Kimweri yupo ukimwona nadhani utamsahau kabisa"
"Huyo sihitaji nionane naye sasa hivi, najua kwa jinsi mama yake alivyokasirika basi kwake hakutokuwa na afadhali. Ngoja niweke mambo sawa kwa Mwanahawa"
______________
"Jus JD yule kaingia mjini leo hii, kwanza nahitaji kuonana naye anaweza kuwa msaada kwangu", Jus alisema akiwa ameketi ndani ya gari akimwona JD akitoka na wafuasi wake, pembeni yake aliketi Avi.
"Utaanzia wapi au hujui yule jamaa ni kibaraka wa Fernando kwanza unajua yupo kwa kazi gani huku nchini, kama kaja kukuua wewe je?", Avi alimwambia
"Ukiona nimeachiwa hadi nikakimbia ujue hana shida na mimi, tena yeye ndiye aliyenishauri nitoroke Fernando hana nia nzuri ila sikumsikiliza hata hadi yananikuta haya. Nahitaji niongee naye kama kuna ufumbuzi mwingine zaidi juu ya jambo hili, nimechoka kuwa mtumwa wa dawa"
"Kumbe hadi jamaa alikupa ushauri wa kutoroka usiwe mtumwa wa Fernando. Mzee yule huwa hana muda wa kumlipa fadhila mtu mwenye asili ya weusi moja kwa moja. JD asili si yako yule ndiyo maana kadumu"
"Najuta haswa, ok hebu washa gari twondoke naona msafara wake unapotea ule"
Muda huo wakijadili hayo, walimwona msomali yule akipita na kundi kubwa na wafuasi wake sambamba na Mjomba wake. Msafara ulipoanza kutoweka kwa kasi ndipo nao wakaanza kuufuatilia kwa kisiri mno huku wakihakikisha hawawezi kugunduliwa. Walifika hadi maeneo ya Ilala ambapo magari hayo kwa pamoja yaliingia eneo ambalo kuna nyumba ya kifahari yenye ghorofa mbili.
Vijana hao waliipita nyumba hiyo na kuja kusimama baada ya kuivuka mitaa mwili hivi, hapo ndipo kwa pamoja walitazamana baada ya kujua eneo ambalo mtu wao waliyokuwa wakitamtafuta ndiyoalifikia.
Walifika eneo ambalo kuna makutano ya barabara na wakahitaji kugeuka na kurejea kule walipotoka. Hapo ilimbidi Avi akanyage breki akiwa hana hili wala lile, kitendo cha kufanya hivyo kilisikika kishindo cha ajabu kisha wakaona gari lao likipelekwa upande wa pili wa barabara huku vioo vikiruka. Haikuhitaji elimu ya ziada kuweza kubaini kuwa wamegomgwa sehemu ya ubavuni jirani kabisa na magurudumu ya nyuma.
Kujiri tukio hilo hakuna ambaye alitaka kulaza damu humo garini, Avi alifungua mkanda upesi na akajirusha nje. Jus naye akafuatia ambapo waliangukia pande tofauti. Mmoja akiwa kulia na mwingine kushoto, upande wa kulia ndipo lilionekana lori lenye mtungi wa kuchanganya zege likiwa limeegeshwa.
Upande huo ndiyo alipoangukia Jus, na kitendo cha kutua chini tu. Alibimbirika kiufundi kisha akasimama wima kwa mara nyingine, akiwa namna hiyo alihisi mvumo ukimjia upande wa shavu la kushoto. Alibonyea chini kwa haraka baada ya kubaini hiyo ilikuwa ni ngumi, akiwa huko kabla hajainuka alitupa konde zito la tumboni ambalo lilimpata sawia mrushaji ngumi aliyekuwepo gizani. Aliinuka na ngumi nyingine ya kidevu na kumfanya mtu huyo aende chini, hukohuko alimuwahi kwa kumkanyaga kifuani mara mbili na kumfanya ateme damu mdomoni.
Upande wa Avi ulikuwa na afadhali hakukutana na kikwazo chochote ila aliona kile kilichokuwa kikimkumba Jus. Mwenzake alipoweza kumwangusha yule mvamizi, alishuhudia akijiwa na mwingine katika muda ambao anamshambulia kwa kukanyaga yule aliyejaribu kumdhibiti. Avi hakutaka yamkute makubwa , alitoka kwa kasi upande huo aliyokuwepo.
Alipokanyaga barabarani alikimbia kwa hatua mbili kubwa kisha akajirusha juu, alipokuja kutua alitua mabegani kwa yule mwingine aliyekuwa nyuma ya Jus. Hata mwenzake alipogeuka nyuma hakujishughulisha alijua tayari kamalizwa. Mhindi huyu bila ya kuchelewa akiwa ameketi mabegani kwa adui, alimpiga viwiko kadhaa vya utosi . Alihakikisha hadi anayumba na kuelekea chini, ndipo akajifanya kama vile anatoka mabegani mwake. Ila yule mtu alipofika chini, miguu ya Avi ilimbana shingoni na huku akawa anauvuta mkono mmoja. Mtu yule alijaribu kujinasua ila hakuweza hata, alibaki akizungusha miguu kutoka upande mmoja kuelekea mwingine.
"Kakutuma nani?', Jus aliuliza huku akimtazama adui yao aliyepigwa kabari. "Husemi siyo, Avi ongeza nguvu hizo hadi ataje mwenyewe".
"Mkuu Husa ndiyo katuagiza bada ya kupewa taarifa na vibaraka wake waliyopo kwenye maegesho kuwa mnawafuatilia", Hatimaye alisema mwenyewe na hapo Jus alijikuta akitoa tusi zito la nguoni kisha akamtukania Husa mama yake.
"Yule msomali sijui ana dawa, yaani pamoja na mbinu zote zile kumwingia na kuufuata msafara wake bado katushtukia", Jus alisema kisha akamwambia Avi, "Oyaa mzimishe huyo usimuue tu ukifanya hivyo jua JD atajua sisi tunataka vita na yeye". Alipotoa mari hiyo aligeuza uso kwa yule adui akamweleza, "Mwambie Husa J.Stone anahitaji kuonana na JD, hatuhitaji uadui wowote naye"
Ulipotolewa ujumbe huo kwa haraka Avi alibana yule mtu hadi alipoona kaishiwa nguvu ndiyo akamwachia, wote kwa pamoja waliingia kwenye gari lao ambalo limharibika upande wa nyuma. Avi akiwa ni dereva walitokomea eneo hilo kuelekea upande wa kusini wa eneo hilo, hawakutaka wakutwe eneo hilo ambalo halikuwa mbali sana kutoka yalipo makazi ya JD.
___________________
Muda mchache baadaye vijana wengine wa JD walidhani kuwa kazi waliyoenda kuifanya wenzao imekamilika. Walikubaliana waje baada ya dakika kumi na tano tangu wagonge gari hiyo ili wasafishe na ktuoacha ushahidi, walipofika muda mwafaka waliwakuta wenzao wakiwa wamelala chini hawajiwezi na ile gari iliyolengwa haikuwepo. Walichokifanya kwa haraka ni kuwachukua kisha wakarejea hadi yalipo makao yao, walifikishwa hadi mbele ya JD na Husa ambao walipowaona tu ilijulikana wazi huo ni ujumbe ndiyo maana hawakuawa.
Walipewa huduma ya kwanza hadi walipopata nafuu, JD aliamuru waletwe hadi eneo ambalo yupo na mjomba wake wakiongea. Amri ilitimziwa na walifikishwa wakawekwa chini huku wakiwa na hali ileile, walipoinua macho walitazamana na sura ya wakubwa zao wasiyo na mzaha hata kidogo.
"Mmeachiwa mmeambiwa mtuletee ujumbe mnaweza kutupatia", JD alisema na hapo hao vijana wakaeleza kila kitu juu ya walichoachiwa.
"Huyo mtu ni nani huyu", Husa aliuliza.
"Jus kum*****e kumbe yupo nchini, aisee basi hapa nahisi kuna vifo vya madaktari vimetokea jamaa kuua kwake ni kama mchezo tu", JD alisema.
"Ni kweli na hadi sasa hivi kuna madaktari wawili wa moyo wameuawa hapa nchini"
"ni huyu aliyewapa kichapo hiki, ni muuaji hatari mno ila kuwaacha wazima hawa maana yake hana vita na mimi zaidi ya mazungumzo tu. Anko bora ulivyoweka vibaraka kule airport"
"Una uhakika hana hatari yeyote ile huyu mtu?"
"Nakuhakikishia asilimia mia moja, ila hawa vijana waache yule mtu si kiwango chao ndiyo maana wapo hivi. Ulikosea kutuma mtu wa kumdhibiti, hawafai adhabu"
"Hilo halina shaka, ila huyu mtu imekuwaje hadi akajua unafika leo?'
"Akija ndiyo tutajua yote, nafikiri namba zangu za simu anazo hadi kufikia awe anajua ratiba yangu ya leo. Tusubiri simu yake tu"
_____________________
Mapambazuko ya siku mpya yalimkuta Jamal akiwa yu usingizini kutokana na uchovu wa usiku uliyopita. Majira ya saa nne asubuhi ndipo alipoweza kuamka, alishuka kitandani akiwa na uchovu mkubwa na alielekea moja kwa moja hadi maliwatoni ambapo alisafisha meno pamoja na mwili wake ndipo akarejeana kuvaa nguo nyingine.
Kifungua kinywa nacho aliletewa humo ndani muda mrefu, aliamua kupata ndipo alipotaka nje na kutazama kule ambapo baadhi ya watu walilala kwenye mahema. Aliona baadhi ya vijumba hivyo vya nguo ngumu vikiwepo huku vingine vikikunjwa, alikaa eneo la mbele ya hotelini hapo huku akitazama mandhari nzuri ya ufukwe wa bahari ambapo jana tu ametoka kukutana na kioja cha mwaka. Alijiuta akitabasamu kila akikumbuka kile alichojionea jana, hakununa hata ingawa alikiri hapo awali ameingiwa na chuki moyoni mwake.
Majira ya saa tano akiwa mahali hapo, simu yake ya mkononi iliita. Alipotazama mpigaji aliona ni Heriety, aliipokea kwa uchangamfu na kuongea maneno machache kisha akaonekana akikubaliana naye kitu halafu akaanza kushuka kwenye ngazi za hotelini.
"Dogo unaenda wapi bila kutupa sisi taarifa, unajua upo ugenini huku", Sauti ya Paki ilisikika na kumfanya ageuke nyuma na kumtazama kisha akasema, "nashuka kule beach mwenye party kanishtua sasa hivi kuna beach party imeanza ndiyo naelekea"
"Sasa sikia dogo, inabidi tuongozane na wewe ila tutakuwa nyuma yako zaidi ya kuwepo karibu muda wote ni ugenini huku", Oze ambaye alikuwepo karibu alisema, Jamal hakuwa na hiyana na alifuatana na watu hao kuelekea huko.
Walitembea mwendo wa dakika mbili wakatokea upande mwingine wa ufukwe huu ambao ulikuwa umesheheni watu wakiwa na mavazi ya kuogelea. Madanga kwa mabanti wote waliweka sehemu kubwa ya miili yao nje eneo hili, hata kina Paki walijikuta wakipiga uruzi kuonesha wamepagawa mno kuwaona mabinti namna hiyo. Jamal aliposikia alijikuta akiwatania na hapo wakacheka wote kwa pamoja, walifika hadi katikati ya kundi la watu ambapo Paki alisimama upande mwingine tofauti na Oze huku Jamal akasogea eneo alilopo Heriety ambayo mwili wake upo kwenye vazi la kuogelea jambo ambalo lilimfanya Jamal aduwae hata pale alipokumbatiwa alitumia sekunde kadhaa ndipo akapokea kumbatio hilo kwa kumfumbatana na mikono.
*VIPI CHUKI YA GINA ITAMWACHA SALAMA?
*VIPI CHUKI YA JAMAL ATAINGIWA NA MAWAZO YA KULIPA UBAYA?
ITAENDELEA!!!