Hassan Mambosasa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2014
- 3,747
- 5,266
- Thread starter
- #21
RIWAYA: BANGUZI
NA: HASSAN O MAMBOSASA
________SEHEMU YA KUMI NA MOJA_________
"Ni ngumu mno ujue"
"Kama unampenda basi uwe tayari kutimiza hilo", Doreen aliposema hayo simu ya mkononi iliita. Aliinuka kutoka hapo kitini alipoketi akiongea na mdogo wake, akaenda kupokea simu hiyo.
_______________TIRIRIKA NAYO
Kwake ni wimbo ambao hakuhitaji kuusikia masikioni mwake, ni sauti ambaye aliiona ni sehemu ya utani kwa kuambiwa vile. Haikuwahi kujitokeza hata siku moja dada yake akawa ni sehemu ya kikwazo kwenye maisha yake, ila hiyo ikawa ni mara ya kwanza kwa kufanyiwa hivyo. Aliona wazi kuna namna yote ni mapenzi juu ya Jamal, yalielekea kumpofua. Hakujali hilo alichojali ni kuweza kumpata kijana yule, hakuelewa kabisa imekuwaje hadi aambiwe vile ilihali si mwenye nia mbaya naye. Yaani ajibiwe kama vile ni adui yake wakati haikuwa hivyo, ni maajabu kabisa.
Upande mwingine Doreen aliona ni amelimaliza suala lile, kwa jinsi alivyokuwa akiheshimiwa na mdogo wake. Hakutaraji kama angeweza kwenda kinyume na maneno yale, hakuwahi kufanyiwa hivyo na wala hakuwa na shaka ya hilo. mkubwa ni wa kusikilizwa na haki yake sharti apatiwe na mdogo, na hiyo ndiyo kaipata kutoka kwa ndugu yake huyo wa damu.
Hayo ni mawazo ya afisa huyu wa jeshi lakini huweza kuwa si sahihi, mwanadamu si mwenye kuwaza usahihi kwa kila kitu. Kutokana na kutojua ya mbeleni, huu ni udhaifu ambao anao kila kitu. Pia kutojua lililopo kifuani mwa mtu ni sehemu ya upungufu mwingine, hivyo haiwezi kufikiriwa usahihi wa mawazo yake.
Pamoja na hayo, waswahili huwa na msemo mmoja maridadi mno miongoni mwa misemo mingi waliyowahi kuitunga kuenda na hali halisi ya jamii. Husema ya kwamba, ukimkataza mtu basi ndiyo utakuwa umempa hamasa ya kujua kile ulichomkataza kina nini ndani yake. Makatazo pasipo kutoa sababu, ni sawa na kumwambia mtu afanye kile ulichomzuia. Hili hakulijua kabisa Doreen, alichojali yeye ni kusikilizwa tu. Laiti angelifikiria, basi angemfuatilia kwa karibu mno Alice.
_____________
Kundi la wengi ambao asili yao si ujasiri, haimaanishi kuwa hakutotatokea ambaye ni jasiri. Itakuja kuzaliwa kiumbe mpya ambaye atakuja kuwa tofauti na wale wa mwanzo, au kutokea ambaye atabadilika na kuweza kushangaza wengine katika eneo fulani ambalo watu huwa pamoja.
Kitendo cha Jamal kuwa kipenzi cha waliyo wengi shuleni Tambaza, ilipelekea akawa ni mwenye kuhitajika kimapenzi. Ila hulka ya kike na kushindwa kuongea, ndiyo ikawa ni kikwazo kikubwa cha kuweza kufanikiwa walau mmojawapo kutoa la moyoni. Walijaribu hata kuonesha ishara ila kutokana na jinsi ambavyo wengi wao hutaniwa mno wakawa wanaonekana ni sehemu ya utani kwake. Kukosekana kwa jasiri mmoja, mwenye kuweza kujitoa mhanga. Haikuwa chanzo cha wote kuwa hivyo, hapo ndipo akaibuka binti mmoja.
Hadija, binti wa kimakonde mwenye rangi ng'avu kwenye ngozi yake. Mwembamba akiwa na umbile lililojitenga kiurembo kiasi kwamba hata nguo ya shule ndefu na nusu kanzu aivaayo sambamba na shungi lake. Kushindwa kuuficha mtindo wa mwili wake ambao Muumba alimjalia. Binti huyu ndiye uvumilivu ulimshinda na kuja, alitafuta muda akamkuta kijana yule akiwa ni mwenyewe na kuamua kukaa akiomba kuzungumza naye. Hapo ndipo alipopasua jipu ili lisiweze kufikia hatua ya utambazi.
Maneno yaliyojaa hisia kali, alimfunulia kijana huyu ambaye ni mwingi wa masihara mno kiasi kwamba hajawahi kuoneka akiwa amekunja sura hata kwa sekunde moja tu. Binti aliamua kupangilia maneno na kuelezea hisia zake huku machozi yakimlenga, alitaka kuonesha ni kiasi gani mno amefika kwake. Matamko ambayo hata Jamal yalimfanya amtazame kwa huruma na akaingiwa na moyo wa imani, ila kitu kilichopo nafsini mwake kikamzuia kuweza kumtoa binti huyo kwenye mateso makali ambayo yupo ndani yake.
"Hadija........msichana mrembo, mwembamba mwenye urefu wa wastani na mwenye kila sifa ya kuhitajika kuwa na mvulana mzuri zaidi yangu, nafikiria haswa naona hukupaswa kabisa kunitamkia mimi nisiyestahiki kuwa na binti mrembo kama wewe", Jamal alisema baada ya kusikiliza maneno ya mtimni kwa binti huyo.
"Hapana Jamal usiseme hivyo, wewe kila msichana shuleni hapa anatamani haswa kuweza kuwa nawe hujiulizi wewe ni wa hadhi gani hadi kila mmoja atamani hilo. Wewe ni wa hadhi ya juu hata kuweza kuweza kumteka mlimbwende mwenye umaarufu duniani kimapenzi, ndiyo maana tunakupenda. Naomba sana usijishushe hadhi ni kuzidi kuniumiza mimi tu kwani wewe pendezo la moyo wangu, haikufaa nisikie unajitaja namna hiyo. Nipe mwamvuli wa huba, nondokane na jua kali mno la kusaka tulizo", Hadija aliongea akiwa ameweka kando kabisa aibu ya kike. Waswahili husema mficha uchi hazai, sasa kaona ni bora kuanika.
"Unajua ninakupenda mno na sipendi kabisa kukuumiza, nakupenda kama ninavyowapenda kila mwanadamu ndani ya dunia hii. Nimeumbwa na moyo wa kupenda na sijaumbwa na moyo wa kuchukia. Sipo radhi kabisa binadamu mwenzangu aweze kunyong'onea na kuungua moyo kwa ajili yangu. Hata wewe kukupa jibu lenye kuumiza sipo tayari kabisa, ila Hadija nitafanyaje unafikiri"
"No Jamal usiseme hivyo, nionee huruma mimi hadi machozi yanafikia kunitoka ili tu niweze kuweza hisia zangu kwako. Nateseka"
"Naelewa hilo, tatizo moyo wangu ni sawa na gari ya mashindano kwenye barabara ndefu ya huba. Yenye uwezo wa kubeba abiria mmoja tu wa pembeni, ambaye naweza kumwita ni msoma ramani wangu huku mimi nikiwa dereva kwenye njia hiyo ya kushindana kuweza kushinda vikwazo mbalimbali vya kimaisha. Vipi nitaweza kuongeza wa pili, nafasi iko wapi Hadija. Huoni naweza kukuweka juu ya paa ya gari hilo, tena nipo kwenye mwendokasi wa kushinda majaribu ya kimaisha. Ukianguka na kuumia mimi nitakuwa ni binadamu mwenye hatia, pia kumbuka nimekueleza moyo wangu ni wa kupenda tu na si kuumiza. Ili kuepuka hatia hiyo, sitokuwa na budi Hadija"
"Jamal please(huku akipiga magoti lakini Jamal anawahi kumzuia, ili asiweze kuwapa hisia mbaya watu)"
"Hadija hivi kukuumiza, na kukuacha bila ya maumivu kipi ni afadhali?"
"Ni bora kutoniumiza, ila si kuniacha Jamal"
"Sasa nitaweza vipi hayo, nafikiri lugha hiyo niliyoitumia kwako imekuwa ujumbe mzuri kabisa. Nimependwa na wa kwanza ambaye ameweza kuwahi wengine wote, na kuipata nafasi pekee ya kwenye moyo wangu kwanini kwanini nikudanganye"
"I don't care Jamal, nachohitaji ni kukupata wewe tu na si kingine"
"Ujue.....(Jamal alisita kuongea baada ya kuonekana kundi la wasichana wakifika mahali hapo)
Ujio wao mahali hapo, binti aliyekuwa akihitaji tulizo. Aliulaani kwa nguvu zote kwani waliingia na kuanza kucheka, kutokana na kumzoea kijana huyo ni mwingi mno wa kuchekesha. Jamal aliamua kufanya vituko na hata kumfanya Hadija naye acheke, alidumu namna hiyo kwa muda mfupi kisha akainuka na kuwaaaga anaelekea msalani. Alielekea moja kwa moja kwenye vyoo vya wavulana, kawaida vyoo vya shule hii vipo upande wa chini kabisa kwenye pembe ya jengo. Kutoka pale alipokuwa hadi chooni alitumia umbali kidogo hadi akafika, akaingia kwenye ukumbi wa mlangoni. Halafu akaufuata eneo ambalo hutumiwa na watu wa vituo vifupi, hapo hakukuta mtu.
Jamal kufika hapo aliamua kutazama kila upande na akahakikisha yupo mwenyewe, kilichofuata baada ya hapo alivuta pumzi kwa nguvu mno na kisha akaiachia kwa ghafla. Kitendo hicho kiliambatana na machozi kumtoka, mikono aliiweka kiunoni huku kichwa akiwa ameinamisha chini. Alivuta tena hewa na kuachia kwa mara nyingine na kupelekea machozi yamtoke zaidi, aliamua kuinua uso juu kutazama kwenye sehemu ya zege ambayo imewekwa ili kuhimili ghorofa ya juu ya jengo hilo.
Huku akinyoosha kidole cha shahada juu alisema, "na..najua ni vibaya kusemea humu ila sina pa kulalamikia wacha nilalamikie humu. Umenipa upendo kiasi kwamba sichukii mtu zaidi ya kuwapa furaha, pia umenifanya nisiweze kukosea mtu ndiyo maana sichukiwi. Nimekuwa ni mtendaji wa wema kwa kila mtu, lakini mbona unanipa mateso ya namna hii. Sistahiki kupenda mimi, kiumbe gani mwenye huruma anayemwona mwingine akiumia yupo radhi asimsaidie".
Alipoweka kituo cha maneno yake alifuta machozi yanayomtoka, kisha akavuta kamasi ambazo tayari zilianza kumnyemelea kutokana na kilio chake cha kimyakimya. Sauti aliyokuwa anaitoa haikuwa ya nguvu kiasi cha kuweza kusikika na wa nje, ila moyoni aliamini anayemlalamikia ni mwenye kumsikia.
"Maisha yangu ni bahati nasibu, sijui hata hatima yangu itakuwa ni lini. Pamoja na hayo lakini sikustahiki haya mimi, mateso juu ya mateso. Nawapa watu furaha lakini bado inabidi niwaumize, kutokana na hili ulilonijaalia. Kama lipo nililokukosea basi naomba nipatie adhabu nyingiine ila si hii kabisa, sipendi wengine waumie kwa ajili yangu ukumbuke", Jamal alizidi kulalamika huku akitoa kilio cha chini kwa chini, muda huo kukasikika sauti za viatu kuashiria kuna mtu ni mwenye kuja mahala hapo.
Aliamua kujifuta machozi kwa haraka, halafu akafungua suruali yake ya shule na kuzuga ni mwenye kuchomekea. Akifanya hivyo alimwona mvulana mmoja wa kidato cha sita akifika mahali hapo, huyo alipomwona aliachia tabasamu.
"Ayaaa! Sukari ya warembo mwenyewe Jay, usiye na makeke ya kutupia viwalo ila wananata tu juu yako", Kijana huyo alisema na kumfanya Jamal atabasamu huku akitikisa kichwa chake.
"Yaani nilivyo ni chumvi yao si unajua kituko tu muda wote ndiyo kinachekwa, sasa fikiri kipendawacho kitachekwaje na wanaokipenda na uelewe mimi ni kituko tu"
"Acha zako wewe, tembezea toto hizo zimeelewa ramani jamaa. Ngoja nipunguze oil hafu kidogo mara moja", Kijana huyo alipomalzia kuongea hayo alianza kujisaidia haja ndogo, muda huo Jamal akamwaga na kuondoka mahali hapo.
______________
_Jioni_
Alisikia akitikiswa kwa nguvu huku jina lake likiitwa, muda huo ambao ni mwenye kujilaza kutokana na uhovu wa kutwa nzima na usiku alihitaji mno kuamka akasome. Aliona ni karaha kwa jinsi alivyokuwa bado analihitaji godoro kwa usingizi wa majira ya jioni, ambao husindikizwa na kiubaridi kwa mbali kilichotokana na feni lililopo kwenye chumba hicho. Kevi alijikuta akiamka akiwa hana budi, alikutana uso kwa uso na rafiki yake ambaye wanaishi naye chumba kimoja katika hosteli zao.
"Jofu kuna nini jamaa huoni mida ya kulala hii mtu wangu, jioni ni kupiga msuli jamaa", Aliongea kichovu kwa kutoa lawama kwa rafiki yake.
"Mtu wangu kuna shori yupo nje hapo anakuulizia wewe, man sikujua kama yule demu ni kisu vile. Dadeki", Jofu alisema.
"We fala na ulivyo fisi ushamezea mate tayari, kwanza ni nani huyo?"
"Si Gina huyo, mtoto kala umini huo. Yaani mguu ni chopsi kabisa:"
"Ma**e huyo mtoto shida yake ni upini tu, utaupata. Ngoja nikamcheki kwanza, safisha rungu ile", Kevi alisema huku akiinuka kitandani.
Alitoka nje akiwa amevaa bukta, alijongea hadi kwenye henga na kuchukua suruali akaivaa kisha akatoka nje. Akiwa na mwendo wa kichovu alipofika eneo ambalo kuna mpira wa gurudumu la nje la gari ulichimbiwa ardhini, alijikuta akitoa macho kwa kutoamini kile alichokiona. Gin akiwa amevaa gauni fupi jeupe, amekaa kwenye mpira huo huku akibana miguu kutokana na urefu wa nguvu aliyovaa kutomsitiri vyema.
Kevi alijikuta akiachia tabasamu la haraka kisha akaliondoa kuepusha binti hivyo asizidi kumtupia jicho usoni. Kwani alipotokeza aliona ni mwenye uso wenye shauku ya kusubiria jambo, aliamua atoe tabasamu kisha auavae umakini juu yake.
"Hi Kevi"
"Hi Gina, upo poa mrembo?'
"Hofu kwako tu, nipo poa mie"
"Mimi mzima wa afya, naona si kawaida"
"Kawaida tu jamani, au kuja huku ndiyo unaona hivyo"
"Yap naona hivyo, niambie"
"(Akiuma midomo yake huku akilegeza macho kidogo) Kuna kitu nahitaji unielekeze hope utanisaidia maana unakielewa vizuri"
"Ni fizo au kemia?"
"Pure"
"Mh! Mbona huo ni uwanja wa Jay huo, mimi huko si mjuzi sana"
"Jamaniii si ulimwelekeza Fidawa mchana mimi nilikuwa na ishu nyingine ndiyo maana sikuwajoin"
"Ohooo! Kama ni hiyo basi nitakushukia tu usihofu mrembo, jinsi ulivyokuja namna hii unafikiri atachomoa nani. Hata kama hajui atajifanya kushika daftari tu"
"(Akicheka kiaibu) Stop please Kevi"
"Ok, saa ngapi"
"Nafikiri muda wa kujisomea usiku itakuwa poa zaidi, we unasomea wapi"
Kevi aliposikia hivyo, akabaki akifikiria juu ya hilo. Kwa jinsi alivyo mpenda mabinti, aliona hiyo ni nafasi pekee haswa baada ya kuliona umbile la Gina. Alimtamani, na binti ndiyo alizidi kuweka mikogo mbalimbali kuzidi kumchanganya kabisa.
"Pindi na dawa huyu ngoja nivutie machinjioni kabisa" Aljisema moyoni kisha akasema, "Mimi leo ninasomea geto humu maana sitoki kwenda Azania wala Muhimbili kusoma. Vipi unaweza kuwepo".
Maneno hayo yalimfanya Gina ajifikiria kwa sekunde kadhaa huku akipeleka mboni yake ya jicho pembeni, Kevi aliganda ni mwenye shauku kubwa mno ya kutaka kujua kama atakubali jambo hilo.
"Mh!", Gina aliguna.
"Mh! What Gina, hautokuwa na nafasi muda huo. Basi tufanye muda mwingine au?'
"Nop siyo hivyo, Iam ready nitakuja muda huo"
"Good girl, same as your beauty"
"Mmmmmh! Jamani"
*MMMH! HUYU KELVIN HUYU
*GINA KUBAGUA WA KUMFUNDISHA NAYE
*JAMAL NI MWENYE VITA KUBWA YA KINAFSI, JE ATAISHINDA?
*VIPI HADIJA ATAWEZA KUKUBALIANA NA HALI HALISI KAMA ALIVYOELEZWA NA JAMAL?
ITAENDELEA!!!