Riwaya - Balaa

Riwaya - Balaa

naona unarefusha story tu... mtu mmoja tu atasumbuaje ngome hvo...!!! maliza story tufanye mambo mengine
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
Simu; 0757 633010

SEHEMU YA MIA NA TISA

Bosi wa Six killers, Don Genge alikuwa anayaangalia yote hayo kwa umakini mkubwa sana, huku akitabasamu. Aliuhusudu sana uwezo uliokuwa unaoneshwa na vijana wake.

Mbili alivyotua chini alijipanga imara, huku akimkuta Daniel Mwaseba akiwa imara zaidi yake. Wanaume wawili walikuwa tayari kwa kazi! Mmoja kutetea kazi haramu, mwengine kupinga kazi haramu.

Mbili alirusha teke la nguvu kwa mguu wake wa kulia, teke lililokuwa linaenda katika sura ya Daniel Mwaseba, lakini Daniel aliliona. Alifanya mambo mawili kwa kasi ya haraka sana. Daniel alibonyea kwa chini kidogo huku akiufyatua ule mguu wa kushoto wa Mbili uliobaki chini. Kwa mara ya kwanza tangu waanze kupambana Daniel Mwaseba alikuwa amemuweza Mbili. Jamaa alidondoka chini vibaya sana. Ilikuwa mithili ya gunia la viazi limerushwa toka kwenye fuso. Daniel Mwaseba hakutaka kabisa kushangaa, aliruka juu kiasi na kutua kwa nguvu tena kwa miguu yake yote miwili katika tumbo la Mbili wa six killers.
Mbili aliipatapata!
Mkanyago ule ulimwingia barabara Mbili. Alitema majimaji mekundu mdomoni bila kupenda, Ilikuwa ni damu!. Daniel Mwaseba hakuzubaa, aliruka tena juu huku goti lake la mguu wa kulia likielekea shingoni kwa Mbili. Hili sasa lilikuwa pigo la kifo!
Lakini cha ajabu goti lile la Daniel Mwaseba halikufika katika shingo ya Mbili. Ndio halikufika kabisa!
Tano wa six killers aliingilia kati kumuokoa jamaa yake, maana bila hivyo, Daniel Mwaseba alikuwa ameshageuka mbogo!

Tano aliruka juu nae na kumvaa Daniel Mwaseba hukohuko angani.... .

Nini mwisho wa Daniel Mwaseba katika kambi hatari...Je kina Mwanasheria na Dokta Yusha watafanyaje ili kutimiza lengo lao?

ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU! 0757 633010

SEHEMU YA MIA NA KUMI

Tano na Daniel Mwaseba walivaana kulekule angani na kudondoka chini kwa pamoja mithili ya mizigo. Katika watu wote walikuwa mahali pale, Daniel Mwaseba hakuna mtu aliyekuwa hampendi kama Tano wa Six killers. Tano alikuwa sugu, Tano alikuwa jeuri, na kwa bahati mbaya kabisa ni Tano wa Six killers ndiye aliyemfata Daniel Mwaseba kule angani. Walipotua tu chini Tano hakujiuliza mara mbili, alimuwahi kwa kumbinya Daniel Mwaseba katika koromeo. Alimbinya hasa!
Daniel alisikia maumivu makali sana, alitoa mkoromo usioeleweka, lakini yule jamaa aliendelea kumbinya. Akiongeza nguvu kila mshale wa saa wa sekunde ulivyokuwa unasogea kuelekea kulia.

Balaa!

Daniel Mwaseba alianza kuona watu wakiwa wamevaa mavazi meupe wakieleaelea hewani, kisha walitoweka ghafla. Mara likaja giza kubwa sana, kitu kimoja tu kikapita katika akili ya Daniel Mwaseba kwamba alikuwa nd'o anaelekea kufa. Baada ya kama dakika moja ya giza lile la ajabu, Daniel hakuelewa tena kilichokuwa kinaendelea duniani. Daniel Mwaseba nae alitoka duniani na kulifata lile giza la kutisha. Daniel Mwaseba aliwafata wale malaika weupe wakioelea hewani..

ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA
 
SIMULIZI; BALAA
Mwandishi: HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA MIA NA KUMI NA MOJA

Kule upande.... katika nyumba ya kulala wageni ya Mjaka hali ilikuwa ngumu sana kwa Dokta Kilumba. Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi walikuwa wamembana vizuri sana daktari yule Mwanaharam.
Pamoja na upole wake wote lakini cha ajabu Dokta Yusha sasa aligeuka mbogo. Jasho lilikuwa linamtoka huku akimnyanyasa daktari mwenzake. Tena alikuwa Bosi wake, kumbuka Dokta Kilumba alikuwa ndiye daktari mkuu wa wilaya ya Kilwa. Pamoja na hasira zake zote Dokta Yusha lakini mara kwa mara hakusita kuzishangaa mbinu za mateso akizotumia Mwanasheria mlevi. Mwanasheria alikuwa anatoa mateso ya hali ya juu kwa Dokta Kilumba, tena kwa mbinu zinazotumiwa na majasusi wa kimataifa. Dokta Kilumba alijitahidi sana kuvumilia mateso ya watu wale wawili....

Dokta yusha na Mwanasheria mlevi lengo lao kuu la kumtesa lilikuwa ni Dokta Kikumba awatajie mahali kambi ya watu wale hatari ilipo, na Dokta Kilumba alikuwa anaonesha utukutu. Hakutaka kabisa kuwatajia.

Dokta Yusha akahisi yule jamaa labda amekula kiapo cha kutotoa siri.

"Hata kama amekula kiapo atasema leo" Dokta Yusha alijisemea kimoyomoyo.

Dokta Yusha alijisachi mfukoni na kutoa mashine ya kukatia kucha. Aliishusha suruali ya Dokta Kilumba mpaka magotini. Mwanasheria mlevi alikuwa makini akiangalia kitu alichotaka kufanya Dokta Yusha. Dokta Yusha aliichukua ile mashine ya kukatia kucha na kuanza kunyofoa vipande vidogovidogo kutoka katika paja la dokta Kilumba. Alikuwa ananyofoa na kuweka sakafuni vile vipande.
Balaa!
Maumivu makali aliyokuwa anayapata Dokta Kilumba yalimfanya alie kama mtoto mdogo, aliona paja na mwili wake wote kwa ujumla unawaka moto!
Bila kupenda huku akipitia katika mateso makali Dokta Kilumba aliwatajia Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi mahali kambi ya Six killers ilipo.

Baada ya kutajiwa hawakumuacha Dokta Kilumba pale, walitoka nae kama rafiki, Mhudumu wa nyumba ile ya kulala wageni hakuelewa chochote kilichokuwa kinaendelea, hakujua kabisa kama mteja wake alikuwa ametekwa. Walitoka nae na kwenda nae hadi katika nyumba ya kulala wageni alikopanga Dokta Yusha na kumfungia kwa ndani katika chumba chake katika nyumba ile ya wageni aliyopanga.

Usiku uleule safari ya kuelekea porini ngome ilianza, kambini kwa kundi hatari la Six killers. Pamoja na kupoteapotea sana kule porini lakini wazalendo hawa wawili wenye nia ya dhati ya kuokoa raia wema walifika katika eneo ambako kulikuwa na kambi ya kundi hatari la Six killers...

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
Asantee lakini hii ndo ntolee, tucount a number of days to go
 
story tamu sana....ila kuna kitu kama umekosea...story inaelezea matukio yaliyotokea mwaka 1989 lakini naona kuna matumizi ya simu za mkonon kwa wahusika.
 
story tamu sana....ila kuna kitu kama umekosea...story inaelezea matukio yaliyotokea mwaka 1989 lakini naona kuna matumizi ya simu za mkonon kwa wahusika.

Potezea n makosa ya kiufund
Mfano; Dr.yusha ikabidi achukue bodaboda baada ya kumuona mwanasheria yupo mbele kapora pikpik na kumfukuzia...! ENZ HZO HAKUNA BODABODA,CJUI HUKO KILWA.
Juu ya yote,hadith ni tamu lete uhondo.
 
Potezea n makosa ya kiufund
Mfano; Dr.yusha ikabidi achukue bodaboda baada ya kumuona mwanasheria yupo mbele kapora pikpik na kumfukuzia...! ENZ HZO HAKUNA BODABODA,CJUI HUKO KILWA.
Juu ya yote,hadith ni tamu lete uhondo.

Tena piki piki aina ya boxer!! bora ingekuwa suzuki, honda au yamaha.
 
SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU; 0757 633010

SEHEMU YA MIA NA KUMI NA MBILI

Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi walitumia saa zaidi ya mbili wakizitumia wakiwa nje wakitafuta namna ya kuingia mle katika kambi ile hatari. Lakini hawakupata namna yoyote ya kuingia kambini kwa kambi ile hatari. Hadi jua la asubuhi linachomoza Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi walibaki wakiwa nje, bado wakihaha kutafuta njia ya kuwawezesha kujipenyeza mle kambini.

Mle ndani ya kambi Daniel Mwaseba alikuwa katika hali ngumu sana. Ilikuwa ni hali mbaya zaidi kuwahi kukutana nayo mpelelezi huyu mahiri nchini Tanzania. Baada ya ule mbinyo wa nguvu shingoni, mbinyo aliopewa na jambazi katili, Tano wa Six killers Daniel Mwaseba alipoteza fahamu. Sasa mwili wake usio na pumzi ulikuwa katika chumba cha mateso cha watu wale makatili. Chumba kilekile alichowahi kuingizwa Dokta Yusha baada ya kutekwa kule hospitali Kivinje.
Naam..... Chumba cha kifo kama walivyokuwa wanakiita wenyewe Six killers. Mwili wa mpelelezi Daniel Mwaseba ukiwa haujitambui ulilazwa katika sakafu ukisubiri muda wa kuja kutolewa uhai tu.

Tangu saa tisa usiku mwili ule uliowekwa katika chumba kile cha kifo. Masaa matatu baadae Daniel Mwaseba alifumbua macho taratibu. Ni kudra za Mwenyezi Mungu tu zilimusha. Na kitu cha kwanza kukiona japo kwa shida katika chumba kile cha kifo kilikuwa ni kiti, kiti cha kifo! Kiti hatari sana kisichofaa kukaliwa na binadamu....

Daniel kaamka..kitu cha kwanza kukiona ni kiti cha kifo..Je ataenda kukaa au?

ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA
 
Back
Top Bottom