RIWAYA: Anga ya Washenzi na Gilbert Evarist Mushi

RIWAYA: Anga ya Washenzi na Gilbert Evarist Mushi

Riwaya: Anga ya Washenzi
Mwandishi: Gilbert Evarist Mushi
Phone: 0765824715.

Msimu Wa Tatu
Sehemu ya 01
Katika msimu wa pili tuliona Elizabeth Neville akifanikiwa kuingia ndani ya hoteli aliyopo makamu wa rais, ni katika harakati za kuwa karibu na mheshimiwa ili apate kumpeleleza. Wakati huo hali ya David bado si nzuri baada ya kunusurika kifo. Daniel na timu yake wanahitaji David awaeleze anachokifahamu kuhusu sakata la helikopta. Kwa Ochewa au Festus napo wapelelezi wanagundua jambo linalowashangaza, Mtandao wa kijasusi nchini Kenya unaonyesha Festus alishauwawa wakati bado anaishi. Hata hivyo bado hajasema ni nini kimemleta Tanzania. Gilbert Mwaitika naye amefanikiwa kumleta Henry ambaye anatumika kufanya maovu bila kupenda.

Songa nayo Sasa....
"Ninafurahi sana kukutana nawe Daniel. Jihesabieni kwamba mmepiga hatua kubwa zaidi. Nitawaeleza yote" Henry aliongea kilevi. Bado pombe ilikuwa ikiutawala ubongo wake. Hawakujali anachokisema, aliingizwa ndani na kufungiwa katika chumba cha peke yake.
Punde Daniel Mwaseba aliingia baada ya kuiingiza gari ile ndani.

"Hakukuwa na mtu anawaungia mkia?" Daniel alimuuliza Gilbert Mwaitika.

"Nilikuwa makini sana Daniel. Hakukuwa na mnyapiaji kabisa" Gilbert akasema kwa uhakika. Mara Cara akaja akikimbia,

"Daniel.... Daniel njooni. Festus yupo katika hali mbaya" Cara alisema. Wote wakaelekea katika chumba alichowekwa Festus. Mwanasheria naye aliiacha tarakishi yake bila kuizima na kuwahi kutazama. Walisahau kama wametoka kumfungia Henry ndani ya chumba cha peke yake. Hawakumfunga, bali waliufunga tu mlango huo.
Mwili wa Festus ulikuwa umetulia juu ya sakafu, kwa macho ya harakaharaka ungesema tayari Festus alishajifia, lakini baada ya Daniel kuugusa mshipa wa shingo ya Festus akagundua bado yupo hai, lakini mapigo yake ya moyo yalikuwa yakipiga kwa mbali sana.

"Dokta Yusha inabidi afike hapa mara moja. Hali yake si nzuri" Daniel akasema.

"Nipeni nafasi nitawasaidia." Mara sauti ikasikika ikisema kutoka nyuma yao. Haraka sana Gilbert Mwaitika na Mwanasheria wakazichomoa bastola zao kutoka viunoni na kugeuka kwa kasi ya ajabu. Walishangaa sana kukutana na mtu waliyetoka kumfungia muda si mrefu. Henry aliinyoosha mikono yake juu akiwatazama..

"Tafadhalini niaminini, sijatumwa na mtu. Hata huyu aliyenileta hapa asingenileta ningewatafuta tu niwaambie. Nipeni nafasi niwaeleze nayoyajua" Henry alisisitiza. Mwanasheria, Gilbert Mwaitika, Daniel Mwaseba pamoja na Cara wakatazamana kwa zamu. Macho yao yalikuwa yakizungumza kwa ishara, Gilbert Mwaitika alikuwa bado ameielekeza bastola yake aliposimama Henry.

"Hatuna haja ya kumsikiliza kwa sasa, Gilbert kamfunge hadi mambo yatakapokaa sawa. Cara njoo tusaidiane kumnyanyua tumpeleke kwenye gari." Daniel alisema. Gilbert Mwaitika akamtaka Henry ageuke na kuongoza chumba alichotoka.

"Ningekuwa na haja ya kutoroka ningeshatoroka baada ya kuufungua ule mlango. Niaminini tafadhali, Mwanangu ataenda kufa kama hatutofanya kitu nisikilizeni tafadhali" Henry alikuwa akipiga kelele wakati Gilbert Mwaitika akimpeleka ndani ya chumba kumfunga. Daniel aliyasikia maneno yale lakini mawazo yake yalikuwa kwa Festus. Alisaidiana na Cara kumnyanyua baada ya kumfungua kamba zile, wakampeleka garini.

Gilbert alihakikisha amemfunga vyema Henry kwa kamba ndipo akaelekea mlangoni ili aweze kutoka.

"Kumbe ni nyie ndio mliomteka Festus?" Gilbert Mwaitika akasita kutoka nje baada ya Henry kuuliza. Akageuka na kumtazama kwa sekunde nne bila kuzungumza chochote.

"Nipo tayari kuwasaidia, lakini kunifungia hapa ni hatari kwa maisha ya mwanangu. Nimepewa kazi ya kumtafuta mtu mnayemhitaji nyie nimwangamize, nikapatiwa siku ya leo tu hadi kesho saa sita mchana, nisipofanya hivyo mwanangu atauwawa na pia mimi nitakuwa hatarini. Mnaponifungia hapa nikashindwa kuonekana ama kuifanya kazi hiyo itakuwa ni hatari kwa familia yangu. Naomba mnisaidie nami nitawasaidia" Henry akasema akiwa ametulia akiegemea chuma kubwa iliyotumika kumfungia na kamba mikono na miguu yake.

"Unafikiri sijui kama unamtafuta David ummalize baada ya kushindwa kufanya hivyo kule Njiro? Hutaweza tena nakuhakikishia" Gilbert Mwaitika akasema kwa kujiamini. Alifundishwa kujiamini, na pia nguvu ya kumfanya ajiamini alikuwa nayo.

"Hahahaha. Eti sitaweza tena, mimi kuweza ninaweza sema tu ninahitaji kushirikiana na nyie ili tuyaondoe magugu yote katika shamba. Mbona hapa nimeshajifungua kamba za mikono? Za miguu ni tendo la sekunde tu naweza kufungua. Kama ningekuwa na dhamira mbaya nakuhakikishia ningetoroka hapa. Nakuhakikishia na sio utani. Nisaidieni niwasaidie" Henry akasema huku akiitupa chini kamba iliyokuwa imetumika kuifunga mikono yake. Na kweli Gilbert Mwaitika alipoona alistaajabu sana kwani alihakikisha amemfunga vyema Henry. Hata alipojaribu kumkagua apate kujua aliikata kamba ile kwa kutumia nini hakupata chochote.

"Kwa jinsi kamba hii ilivyo, asingeweza kuikata kwa meno. Halafu ameikata kwa uharaka mkubwa bila mimi kuona. Ametumia nini huyu?" Gilbert alikuwa akitafakari huku akimsogelea karibu zaidi Henry.
Akampa onyo.

"Kama unajipenda tulia. Awamu hii sitokufunga na chochote, nitaufunga tu mlango na ole wako ufanye ujanja wowote. Sitajali familia inakutegemea ama unaitegemea. Tulia" Gilbert Mwaitika akatoka nje na kuufunga mlango. Mlango huo haukuwa na kitasa, bali komeo.

"Uuuh. Lakini naamimi watanisaidia. Ngoja nivute subira." Akajisemea Henry, akaona bora afungue na kamba aliyofungwa miguuni. Na kumbe alikuwa akitumia kiwembe kidogo sana ambacho alikihifadhi ndani ya ukucha wa kidoleni. Kidole chake cha kwanza, maarufu kama kidole gumba katika mkono wake wa kushoto kilikuwa na ukucha mrefu uliomwezesha kukibana kiwembe hicho bila kugundulika.

"Simu yangu ikiita nileteeni, msipoileta mtaniingiza kwenye matatizo tena" Akaropoka kwa nguvu akiamini atasikiwa na waliomweka kifungoni. Sasa akaamua kujituliza sakafuni huku akitafakari baadhi ya mambo ya nyuma ambayo aliwahi kupitia nyuma. Usingizi ukamnyemelea taratibu, ukamchukua.

Zilipita Dakika tano za ukimya, zikapita tena nyingine tano, jumla zikawa kumi wakati Cara akiwa bize kwenye tarakishi mpakato yake. Daniel Mwaseba akishirikiana na Mwanasheria walishatoka kwa lengo la kumwahisha Festus kwa Dokta Yusha baada ya hali yake kubadilika.

"Hivi mtu wako yupo kweli? Kumekuwa kimya sana." Cara akasema huku akimtazama Gilbert Mwaitika, alikuwa amejiegemeza kitini kama mtu aliyelala.

"Sasa unadhani ataenda wapi? Ni lazima atulie himo chumbani" Gilbert Mwaitika akasema akiwa bado ameyafumba macho yake.
Cara akaiacha tarakishi na kwenda kuhakiki maana ukimya ule ulimshtua sana. Haikuingia akilini eti mtu afungiwe chumbani bila kufungwa na kitu chochote halafu akatulia. Nafsi yake ilikataa kuamini.
Alifika na kufungua komeo la mlango, akatazama ndani na kukutana na mtu anayekoroma. Henry alikuwa amezama katika usingizi mzito sana. Cara akaachana naye na kurejea katika tarakishi yake. Wakati huo Gilbert Mwaitika alikuwa bado ameegemeza kichwa chake katika kiti, kama mtu aliyepitiwa na usingizi. Lakini Cara hakutaka kumsumbua, alimwacha na kuendelea kuchezea tarakishi.

ITAENDELEA
 
Riwaya: Anga ya Washenzi
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
Phone: 0765824715.

Msimu Wa Tatu
Sehemu ya 02
Daniel Mwaseba na Mwanasheria walifika mbele ya nyumba ya Dokta Yusha. Yalikuwa ni majira ya saa nne na nusu usiku, na walikuwa pamoja na Festus ambaye bado hali yake haikuwa sawa, Daniel mwaseba alipiga honi mara moja tu pale getini na punde geti likafunguliwa na Dokta Yusha aliyeonekana kuvalia pensi nyeupe na tisheti ya samawati.

"Karibuni ndani" Akasema Dokta Yusha

"Yule mfanyakazi wako hayupo?" Daniel akauliza huku akiingiza gari ile ndani.

"Nimempa likizo ya ghafla baada ya wewe kumleta David mchana hapa. Si unajua tena ulitaka hii iwe siri yetu? na mimi simwamini sana maana yeye ni mtu wa mtandaoni sana" Dokta Yusha akasema. Na Daniel akafanikiwa kuingiza gari ndani ya uwanja wa nyumba hiyo, akasaidiana na Mwanasheria kumbeba Ochewa na kuingia ndani.

"Nyoosheni naye moja kwa moja hadi chumba kile" Dokta Yusha akasema huku akitoa ishara ya mkono kuonyesha ni chumba kipi walipaswa kumwingiza Jasusi yule. Nao wakafanya kama walivyoambiwa, wakakuta kitanda kifananacho na vitanda vya hospitalini, wakamlaza hapo.

"Mh! Dokta usiniambie ulijipanga kabisa, hadi vitanda vya mahospitalini vipo nyumbani kwako?" Mwanasheria akatania, na wote wakacheka.

"Unajua si kila muda nitakuwa hospitalini, halafu kuna wagonjwa wengine unakuta unahitajika kuwa nao karibu mda wote kwa ajili ya uangalizi maalum, sasa nikaona bora niwe na kitanda angalau kimoja ama viwili nyumbani kwangu ili ikitokea siku moja kama ya leo mgonjwa anahitaji uangalizi wangu na mimi nipo nyumbani basi niwe naye hapa. Hata hivyo sipo mwenyewe, nina msaidizi wangu ambaye ni nesi. Anamsafisha David katika kile chumba tulichomweka muda ule" Dokta Yusha akaeleza.

"Ohoo kumbe, sikujua hilo Dokta. David hajaamka bado?" Mwanasheria Mlevi akauliza.

"Bado. Ila anaendelea vyema. Hadi kufikia kesho anaweza kuamka. Kwa sasa amepumzika baada ya kutibu yale majeraha ya kuchomwa visu." Dokta Yusha akasema huku akimkagua Festus katika mishipa ya mikono, akatoa tochi ndogo na kumulika katika macho ya Jasusi huyu. Wakati huo Daniel alikuwa bize akizungumza na simu.

"Eeh Dokta," Daniel akasema baada ya kumaliza kuzungumza na simu.

"Daniel mmemfanya nini tena huyu? Mbona kuna sumu inatambaa kwa kasi katika mishipa yake ya damu? Ulimpa nini?" Dokta Yusha akauliza huku akimkazia macho Daniel.

"Nilikuwa kwenye harakati za kumfanya aseme Dokta" Daniel akajibu kwa ufupi.

"Ndio kumfanyaje sasa huku? Hivi si kumuua Daniel? Mhalifu akishaingiaga kwenye mikono yako khaa, ni hatari. Vipi sasa baada ya kumfanya hivi alisema?"
Daniel hakujibu, alimtazama Dokta Yusha kimaswali.

"Mtu mwenyewe mgumu balaa, na mateso yote yale wala hakuufungua mdomo wake kusema anachokijua" Mwanasheria akasema.

"Sasa hapa kama hatutawapata hao Nge mliowatumia kumtesea hatutoweza kuiondoa sumu hii kwa haraka. Tutachelewa sana kama tukitegemea njia nyingine zaidi ya ile ya asili, na anaweza akafa pia." Dokta Yusha akasema kwa kumaanisha.

"Dokta umejuaje hiyo ni sumu ya nge?" Mwanasheria Mlevi alishangaa uwezo wa ajabu wa kugundua kwa haraka ile ni sumu ya Nge.
"Unamaanisha wale Nge waliomuuma waletwe?" Daniel Mwaseba akauliza.

"Ndio hivyo. Fanya juu chini wafike hapa Nge wote waliomuuma. Dokta Yusha alisema kwa msisitizo.

"Uuuh! Kazi ipo." Daniel akasema akiachia pumzi ndefu. Alikumbuka hakuwarejesha Nge wale ndani ya kikopo alichowatoa, na bila shaka walibaki mle chumbani wakizungukazunguka. Daniel akaitoa simu yake mfukoni na kumpigia Gilbert Mwaitika
******
SURA YA NNE
Mheshimiwa Eliud Sumbi alitoka bafuni baada ya kujisafisha mwili kwa takribani dakika kumi. Elton Tonny ambaye ni mpambe wake alisimama mlangoni muda wote, na hili lilikuwa ni jukumu lake kwa nyakati zote, kuwa karibu na Mheshimiwa kwa nyakati zote hadi pale atakapoambiwa na mheshimiwa akapumzike ndipo humuacha.

"Ameshafika?" Mheshimiwa Eliud Sumbi akauliza

"Ndiyo Mheshimiwa, nimemtaka atangulie chumbani anakusubiri" Elton Tonny akajibu

"Vipi unamwonaje? Anavutia?" Mheshimiwa akauliza akiachia tabasamu. Alikuwa akiuliza kuhusu mwanamke, na alihitaji kulala na mwanamke usiku wa leo hivyo aliomba atafutiwe mwanamke mrembo.

"Amekamilika Mkuu. Hakika anakufaa wewe tu" Elton Tonny akajibu.

"Si unajua kesho Rais Mark atakutana na wadau wa kilimo cha kahawa katika ikulu ndogo ya hapa Moshi? Kesho hatokuwa kwenye ziara hivyo bado nitakuwa hapa kwa muda, ngoja niutumie usiku huu vizuri hadi kesho asubuhi kabla ya kwenda kuungana naye. Umewasiliana na Henry?"

"Bado sijawasiliana naye Mkuu, ngoja nifanye hivyo sasa hivi."

"Utafanya asubuhi umuulize amefikia wapi. David anapaswa kuuwawa kwa gharama yoyote ile kama ikithibitika bado angali hai." Mheshimiwa Eliud Sumbi akasema huku akielekea katika chumba alichoambiwa mwanamke anamsubiri.
Lakini ghafla akasita na kugeuka nyuma baada ya kukumbuka kitu, akamkazia macho Elton Tonny

"Yule Mpelelezi hakikisheni mnampata, yasizidi masaa ishirini na nne awe ameshapelekwa katika kambi yetu ya Amboni. Kesho kutwa tutaelekea Arusha kwa mwendelezo wa ziara, hivyo hadi siku ya ziara inafika awe ameshapatikana. Kama hajapatikana yeye basi awe amepatikana Ochewa." Eliud Sumbi alisema, akauendea mlango na kuufungua.

"Juu ya kitanda aliketi mwanamke mwembamba kiasi, mrefu na mwenye weupe wa mbali. Alikuwa ni mwanamke mrembo kumtazama machoni, haswa kwa mwanaume rijali. Mheshimiwa Eliud Sumbi alishindwa kuyakwepesha macho yake yaliyotua kwenye mgongo laini wa mwanamke huyu, alishindwa hata kuufunga mlango wa chumba, na mkono pia ulibaki kwenye kitasa cha mlango. Funda la mate likamteremka kisa tamaa,

"Amekamilika Mkuu. Hakika anakufaa wewe tu" Maneno haya yalipita kwenye kichwa chake. Ni Elton Tonny ndiye aliyeyasema kabla hawajaagana dakika chache zilizopita.
Mwanamke yule akaigeuza shingo yake kwa madoido huku akiachia cheko la madeko. Na kumbe mwanamke huyu ni Elizabeth Neville.

Huu ni Msimu wa Tatu wa Anga ya Washenzi. Kama ulilipia msimu wa nne nicheki whatsapp kwa namba 0621249611 nikutumie. Kama bado basi utaupata kwa Tshs 1000 tu. Lipa kwenda Halopesa namba 0621249611 au Mpesa namba 0765824715 kisha njoo whatsapp.
 
Riwaya: Anga ya Washenzi
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
Phone: 0765824715.

Msimu Wa Tatu
Sehemu ya 03

"Amekamilika Mkuu. Hakika anakufaa wewe tu" Maneno haya yalipita kwenye kichwa chake. Ni Elton Tonny ndiye aliyeyasema kabla hawajaagana dakika chache zilizopita.
Mwanamke yule akaigeuza shingo yake kwa madoido huku akiachia cheko la madeko. Na kumbe mwanamke huyu ni Elizabeth Neville.

Unakumbuka muda ule Elton Tonny akizungumza na Henry? Basi muda huo Elizabeth Neville alipita karibu yao kwa vazi kihudumu, na muda huo katika kudadisi akabahatika kukutana na changudoa ambaye alishaandaliwa kwa ajili ya kustarehe na mheshimiwa. Basi Elizabeth Neville akamchukua changudoa huyo na kwenda kuzungumza naye, na baada ya pesa kuzungumza basi wakakubaliana Elizabeth Neville aende badala ya changudoa huyo kwani alitumiwa palepale kwenye simu yake shilingi milioni mbili na Elizabeth kama posho ya kuafiki ombi lake. Changudoa yule alipotaka kujua kwanini Elizabeth alitaka kwenda kustarehe na mheshimiwa hakumweka wazi.

"Mwanamke mrembo sana huyu, lakini hii sura si ngeni kwangu. Nilimwonaga wapi?" Mheshimiwa Eliud Sumbi akajisemea huku akikiachia kitasa cha mlango na kukisogelea kitanda.

"Ndio hadi kusahau kufunga mlango?" Elizabeth Neville akasema huku akiliachia cheko la madeko.

"Unavutia sana. Hakika u mrembo. Wewe ni Mtanzania kweli?" Mheshimiwa akasema huku akizidi kusogea taratibu karibu na kitanda. Hata mlango hakuwa ameufunga, ulibaki wazi. Akamsogelea Elizabeth Neville anbaye kwa juu hakuwa amevalia nguo yoyote zaidi ya kaniki nyekundu. Hakika Elizabeth Neville alijipanga vyema katika mawindo yake. Uso wake ulipendeza sana, kichwani kwa namna alivyoziseti nywele zake isingekuwa rahisi kwa mtu kukubali kama Elizabeth Neville ni mtanzania. Lakini ni kweli Elizabeth Neville si mtanzania kwa kuzaliwa, bali kwa kuandikishwa.

"Yeah Mimi ni mtanzania ndiyo" Elizabeth Neville akajibu huku akitazama kwa macho ya aibu. Akanyanyuka kuuendea mlango lakini ghafla akavutwa na mkono wa Mheshimiwa Eliud Sumbi na kujikuta yupo kifuani pake.

"Lakini mbona kama niliwahi kukuona mahali fulani? Tena sehemu nyeti sana." Mheshimiwa Eliud akasema akimkazia macho Elizabeth Neville.

"Mmmh mimi au? Labda ulinifananisha mheshimiwa, au ni club uliniona? Maana ndio maeneo yangu hayo mara nyingi" Elizabeth Neville akasema.

"Sio klabuni hata, ni sehemu za heshima kidogo. Anyway tuachane na hayo. Unaitwa nani mrembo?"

"Naitwa Utamu mwingi" Elizabeth Neville akasema kwa masihara

"Hahahaha, eti utamu mwingi. Ndio jina ulilopewa na wazazi wako? Au hii ni moja kati ya sifa zako?" Mheshimiwa akasema huku akikiweka kiganja cha mkono wake juu ya paja laini la Elizabeth Neville. Elizabeth Neville alikuwa ni mrembo kuvutia pindi umtazamapo. Isingekuwa rahisi kuamini kama ni jasusi na mpelelezi wa siri wa serikali. Labda ungeligundua hilo kwa kutumia nguvu, tena nguvu ya kupambana naye kiakili na kinguvu.

"Jina langu mimi ni Angel, hili la utamu mwingi ni watu tu hupenda kuniita hivyo" Elizabeth Neville akasema

"Oooh My Angel. Kwa uzuri huu uliobarikiwa utakuwa my angel wa pekee. Hilo jina la utamu mwingi itabidi niwe nakuita mimi tu, na si mwingine akuite hivyo. Au unaonaje?" Mheshimiwa Eliud Sumbi akachombeza. Elizabeth Neville akabaki kucheka tu kwa namna ya kumaanisha ana aibu. Lakini hakuwa na hata lepe la aibu, ni kujifanyisha tu alijifanya. Alikuwa kazini, na kazi yake ni kumchunguza Mheshimiwa Eliud Sumbi
Atamchunguza vipi? Twende sawa tutajua zaidi..
************

Simu ya Cara iliunguruma kwa sauti ya juu kuashiria inaita. Cara akaachana na tarakishi na kuichukua simu yake iliyokuwa juu ya meza. Makelele hayo ya simu kuita yakamfanya Gilbert Mwaitika afungue macho na kunyanyuka kutoka pale alipokuwa amejipumzisha kidogo.

"Niambie Daniel, kuna habari gani huko?" Cara aliipokea simu na kusema. Ilikuwa ni simu kutoka kwa Daniel Mwaseba. Wakati huohuo Cara akiongea na simu ile, Gilbert Mwaitika alichukua simu ya Henry na kuelekea nayo katika chumba ambacho Henry alifungiwa.

"Unamaanisha nini Daniel! Tuwatafute wale nge! ... Sasa nani atawaleta?.... Mmmh haya sawa" Cara akairejesha simu mezani baada ya mazungumzo kati yake na Daniel kufikia tamati. Daniel alimtaka aende katika kile chumba alichokuwa amefungiwa Ochewa (Festus) kuwaangalia Nge wale apate kuwachukua ampelekee kwani Dokta Yusha aliwaambia hiyo ndiyo dawa pekee ambayo ingeweza kumfanya Festus apone kwa haraka.

Cara akaingia ndani ya chumba kile, na kwa bahati nzuri akapata kumwona Nge mmoja akipanda na ukuta. Akamchukua Nge huyo na kumwingiza ndani ya boksi aliloliona chumbani hapo kama alivyoelekezwa na Daniel. Kazi ikawa kwenye kumtafuta Nge wa pili, akamtafuta kwa dakika tano bila mafanikio. Akahakikisha anapiga sachi kila kona lakini hakuweza kumwona. Akachukua simu yake na kumpigia Daniel. Akamweleza

"Nimetafuta kila mahali Daniel, ni huyu mmoja tu....... Itakuwa labda, kwa hiyo nimlete huyu? Yeah kwa maelekezo nitafika hapo, ngoja nitafute bodaboda karibu anilete huko. Sawa Daniel nitakuwa makini" Cara akamaliza kuzungumza na simu, akaelekea katika chumba alichokuwa Henry na kumkuta Gilbert Mwaitika akigusisha kidole cha Henry na simu ili apate kuifungua kwani ilimhitaji nywila ama alama za vidole kuifungua simu hiyo.

"Mmmh, si ungeniambia kama unataka kuifungua? Ninayo programu katika tarakishi yangu, ingeweza kukusaidia kufungua simu hiyo." Cara akasema

"Sikufahamu hilo, ila nimefanikiwa maana jamaa aliitia simu yake ulinzi wa alama za vidole" Gilbert Mwaitika akasema

"Haya mimi natoka kidogo, kuna mzigo nampelekea Daniel fasta narudi." Cara akasema. Gilbert Mwaitika akamtakia heri aendapo na kumsihi awe makini.
Cara akipotoka tu, Gilbert Mwaitika akaanza kunyonya data zote kutoka kwenye simu ile na kuingiza kwenye tarakishi aliyokuwa akiitumia Mwanasheria Mlevi. Akaona pia ujumbe mpya ulioingia dakika chache zilizopita kutoka kwenye namba iliyohifadhiwa kwa jina la Elton Tonny.
'Ukijua ni wapi amepelekwa David usisite kuniambia, maana kuna kazi ya ziada nimepewa'
Gilbert akausoma ujumbe huo. Baada ya hapo akarudi tena ndani ya chumba kile na kumwamsha Henry

"Hey imetosha sasa, amka"
Taratibu Henry akajinyoosha na kuyafungua macho yake yaliyokuwa yameanza kuvimba kutokana na kumezwa na usingizi mzito.

"Si ungeniacha nilalelale kidogo kwanza?" Henry akahoji kichovu akisindikizwa na mihayo

"Naweza nikakuacha, lakini unapozidi kulala huoni mwanao Jerry ndio anazidi kuwa hatarini? Au usingizi ni bora kuliko mwanao?" Kauli hii ikamwamsha Hennry kutoka usingizini baada ya kusikia jina la mwanaye likitajwa. Alikuwa anampenda sana Jerry, alikuwa ni mwanaye wa pekee, na pia Jerry angezidi kuwa wa pekee katika maisha yake yote.

" Simu yako hii, kuna ujumbe uliingia sijajua ni wa Biko au Mshindo Milionea." Gilbert akasema huku anamkabidhi Henry simu ile. Akabaki akimtazama tu Henry baada ya kumpatia simu yake. Henry alichokifanya ni kwenda kuufungua ujumbe ule ambao ulitoka kwa Elton Tonny.

"Bado sijafanikiwa kujua, ila naelekea kujua" alichakata ujumbe na kuutuma kwa Elton. Akaitafuta namba ya mkewe, kabla ya kuipiga akamtazama Gilbert Mwaitika

"Naweza kuzungumza na mke wangu?"

"Waweza, ila sihitaji ujanja wa aina yoyote ile" Gilbert akageuka na kutoka nje ya chumba kile. Lakini hakwenda mbali, alibaki amejiegemeza pale mlangoni. Akamsikia Henry akiomba radhi kwa mkewe kwa kosa la kutokumtafuta tangu asubuhi, akijitetea ni ubize mwingi kazini. Isitoshe akaeleza juu ya kutokuwa na uwezekano wa kurejea tena nyumbani hadi kesho. Lakini pia hakusita kuuliza maendeleo ya Jerry mwanaye. Wakaagana kwa upendo. Na hapo Gilbert Mwaitika akagundua ya kuwa Henry na mkewe walikuwa wakipendana na kusikilizana pia.
"Nitaendelea kumtazama kwa jicho la tatu hadi kina Daniel warejee. Akizidi kuwa mstaarabu nasi tutakuwa wastaarabu kwake. Ngoja nimwache peke yake huku ndani, lakini sitamwacha abaki na simu yake" Gilbert Mwaitika akajisemea huku akiingia ndani ya chumba hicho, akaichukua simu ya Henry na kuelekea ukumbini. Lakini hakuufunga mlango wa chumba kile. Alifanya vile kwa makusudi na wala sio bahati mbaya.

"Najua ananipima kama nitafanya ujanja. Katu siwezi kufanya, nitatulia nione kama watanisaidia. Nimechoka maisha ya utumwa. Nitakuwa mpole" Henry alijisemea huku akitazama juu baada ya kuona mlango haujafungwa.

Festus atapona kweli? Nini hatma ya Henry na David? Washenzi ni wakinanani hao? Huu ni Msimu wa Tatu wa Anga ya Washenzi.
Ofa ya wekend ni ukilipia Tshs 1,500 utaupata msimu huu wa tatu na ule wa nne pia. Lipia sasa kwenda M pesa namba 0765824715 au Halopesa namba 0621249611 kisha nitext whatsapp kwa namba 0621249611 nikutumie.
 
Anga ya Washenzi.
Screenshot_20230203-155155.jpg
 
Gilbert anaandika Anga ya Washenzi
WhatsApp 0621249611

Huu ni Msimu Wa Tatu
Sehemu ya 04

"Najua ananipima kama nitafanya ujanja. Katu siwezi kufanya, nitatulia nione kama watanisaidia. Nimechoka maisha ya utumwa. Nitakuwa mpole" Henry alijisemea huku akitazama juu baada ya kuona mlango haujafungwa.
*****
Ndani ya Ghorofa ya nne katika hoteli ya KiliView shughuli ilikuwa pevu. Mheshimiwa Eliud Sumbi alikuwa akishinikiza kumwingia Elizabeth Neville huku Elizabeth Neville akizidi kumkwepa. Ilianza kama mchezo kukimbizana na kukizunguka kitanda, baadae likawa ni jambo la kutilia maanani, mheshimiwa Eliud Sumbi hasira zikamshika, damu ikazidi kumchemka, hamu ya kutaka kitoweo ikamkolea, akapaniki na kuanza kulazimisha.

"Nini maana ya kuletwa humu ndani? Haukuelezwa?" Mheshimiwa akauliza kwa kufoka.

"Taratibu mpenzi, mambo mazuri huwa hayahitaji haraka. Mbona muda bado upo mwingi? Kesho ni karibu lakini ni mbali pia tunapokuwa karibu zaidi. Wakati tulivu kama huu tupo wawili tu, inapendeza" Elizabeth Neville akanong'ona katika sikio la Eliud Sumbi huku akiizungusha mikono katika mgongo wake. Eliud Sumbi akaihisi faraja ya moyo kwani mara nyingi hupendezwa na mambo kama haya. Mara nyingi hupenda starehe. Yeye hana mke wala mtoto baada ya ajali iliyotokea miaka saba iliyopita kipindi akiwa mbunge wa viti maalum. Katika ajali hiyo walitoka matembezi yeye na mkewe pamoja na wanaye wawili, wakiwa katika mwendo mkali, kwa bahati mbaya tairi ya mbele ikapasuka na kupelekea gari kuyumba na kupinduka zaidi ya mara mbili. Ni yeye tu alipona katika ajali ile ambayo watoto wake walifariki palepale huku mkewe akifia njiani wakati akiwahishwa hospitali.
Lakini starehe hakuianza baada ya msiba huo mzito, alikuwa na tabia hiyo hata kabla ya kuwa na familia.

Hadithi za mapenzi ndio zilikuwa zikiendelea ndani ya chumba. Walizungumza na kutekenyana hadi inatimia saa sita usiki. Ilipofika saa sita ndipo Elizabeth Neville akaianza kazi yake rasmi iliyomleta pale. Kwanza alisimama mbele ya Eliud Sumbi. Alipoona mheshimiwa kasimama, haraka akamsukuma na kumlalia kwa juu. Akaanza kumchombeza kwa namna ajuayo, namna ambayo pia aliwahi kufundishwa katika mafunzo magumu ya kijasusi nchini Cuba ili kumteka mwanaume kirahisi. Alihakikisha amemgusa kila sehemu dhaifu ambayo ingeweza kumletea mheshimiwa hisia kali za mapenzi na uchovu kwa pamoja. Hili likawa rahisi sana kwake; maana kipindi yupo nchini Cuba mafunzoni aliwahi kufundishwa mbinu hii, akaielewa mbinu hii, na akaihitimu pia ndipo akaifaulu, na sasa anaitumia. Kuandaa mazingira ya kumchunguza makamu wa rais, Mheshimiwa Eliud Sumbi.

Zilipita kama dakika tano za vicheko na miguno kutoka kwa Eliud Sumbi, kukafwatiwa na sauti ya mtu akikoroma.Amini usiamini, Mheshimiwa Eliud Sumbi alishapitiwa na usingizi, tena usingizi mzito kwelikweli. Haraka Elizabeth Neville akaliendea Gauni lake fupi alilokuwa amelivua na kukitoa kifaa fulani kidogo sana. Kifaa hiki alikiingiza kwenye simu ya Mheshimiwa kwenye tundu la kuchomeka waya ya masikioni maarufu kama 'earphone'

"Si rahisi kwake kutumia earphone. Sidhani kama hupendelea. Sasa kila kitu atakachokizungumza kupitia simu yake kitaenda kusikiwa na sisi"
Elizabeth Neville akasema huku akitabasamu. Kifaa alichokiweka kilikuwa ni kifaa ambacho kingeweza kunasa mazungumzo yote ya mpigaji na mpigiwaji wa simu. Alitabasamu tena kwa furaha kwani aliona hii ni hatua kubwa watakuwa wameipiga katika kuwa karibu zaidi na mheshimiwa Eliud Sumbi. Akairejesha simu ya Mheshimiwa katika mfuko wa koti lake lililokuwa limening'inizwa katika pembe ya mguu wa kitanda. Alipohakikisha kila kitu kimekaa sawa taratibu akarejea kitandani na kumkombatia mheshimiwa. Wakaungana katika usingizi.

Majira ya Saa saba usiku simu ya Mheshimiwa Eliud ikaunguruma. Kuashiria inaita. Kumbe Elizabeth Neville hakuwa amelala, hakuwa na hata lepe la usingizi kutokana na kuwa kazini. Akajifanya kujigeuza kivivu na kumtikisa mheshimiwa.

"Mheshimiwa... Mheshimiwa"

"Naam kuna nini? Sauti ya mheshimiwa ikauliza kivivu kutokana na usingizi ulikuwa bado unamlevya.

"Ni kama simu yako inaita sijui! Au ni alarm?" Elizabeth Neville akasema

"Ina maana bado upo hapa? Mmmh" Eliud Sumbi akahamaki. Akajiinua na kupeleka mkono katika koti lake na kuchomoa simu yake. Alipotazama kioo cha simu alimtazama Elizabeth Neville na kisha kuyarejesha macho yake simuni.

"Unaweza kwenda, usiku wetu umeishia hapa. Ahsante pia kwa huduma." Mheshimiwa alisema huku macho yake yakizidi kuitazama simu ile.

"Jamani mheshimiwa.. Mbona unanifukuza lakini? Naomba uchukue hata namba zangu basi ili tuwe tunatafutana siku ukihitaji huduma yangu tena?
Mheshimiwa aliona kama anacheleweshwa. Alitoa business card na kumkabidhi Elizabeth Neville huku akimharakisha aondoke.

" Haya nenda, usinipigie, utanitumia tu ujumbe mfupi nami siku nikikuhitaji nitakuita. Hata nikiwa Dar es Salaam au Dodoma nitakuita"
Elizabeth Neville akamrukia mheshimiwa kwa furaha na kupokea karatasi ile. Akampiga busu katika shavu lake huku akimshukuru. Lakini wakati akifanya hivyo jicho lake lilifanikiwa kukitazama kioo cha simu ya mheshimiwa. Namba iliyokuwa ikipiga simu ilikuwa ni ngeni, na code ya simu ilianza na +254 ikimaanisha ilikuwa ni simu kutoka nchini Kenya. Elizabeth Neville akatumia sekunde tatu tu kuinakili namba ile katika kumbukumbu ya kichwa chake.
Wakaagana
******
"Ilikuwa ni kama bahati tu Cara. Muda ule nilipokuambia uwalete Nge wale kumbe mmoja alikuwa ndani ya gari tuliyokuja nayo, katika siti ya Nyuma tulipomlaza Festus." Daniel alisema wakati anaendesha gari. Walikuwa barabarani wakirejea kambini majira ya saa nane usiku wakitokea nyumbani kwa Dokta Yusha. Ndani ya gari alikuwa yeye na Cara.

"Basi itakuwa wakati ule tunamtoa ndani na kumpeleka garini huyo Nge alikuwa bado anatambaa juu ya mwili wake" Cara akajibu.

"Nge mwenyewe Mwanasheria alimkuta amekufa. Mwanasheria alikuwa anaifwata simu yake ndani ya gari ndipo alipomwona Nge huyo. Na Dokta Yusha alikuwa ameshasema kama hawatapatikana Nge wote basi ingekuwa ni sawa na bure. Sijui ingekuwaje" Daniel Mwaseba alisema

"Eti nge anachomwa halafu majivu yake yanatumika kama dawa. Hakika hii inavutia. Kumbe ukigongwa na nge dawa pekee ni huyohuyo Nge? Sijawahi kufahamu hili kabisa, nilikuwa nasikia tu midomoni mwa watu" Cara akasema. Wakati huo gari yao ilikuwa ikizidi kwenda kwa mwendo wa wastani.

"Si dawa pekee. Alisema ni dawa ya haraka inayoweza kuondoa sumu ile kuliko dawa za mahospitalini." Daniel Mwaseba alisema huku akichomoa simu yake baada ya kusikia mtetemo mfupi ulioashiria ujumbe mfupi kuingia. Mkono mmoja akatumia kuendesha huku mwingine ukifungua ujumbe ule.

"Kuwa makini Daniel. Hii ni barabara, wewe chati tu. Ni Elizabeth Neville huyo au?" Cara akasema na Kuuliza

'DONE'
Daniel aliusoma ujumbe ule, ulikuwa umebeba neno moja tu. Ujumbe huo ulitoka kwa mtu aliyehifadhiwa kwa jina la 'HoneyBee'. Bila shaka ulitoka kwa Elizabeth Neville .

'Uko wapi Elizabeth?' Daniel akachakata ujumbe na kuutuma.

'Nipo kambini tayari, nyie je?' uliingia tena ujumbe mwingine kutoka kwa Elizabeth Neville.

'Tunakuja' Daniel akajibu.

"Elizabeth Neville amefanikisha. Ndiyo alikuwa ananiambia hapa. Kumbe ameshafiika kambini" Daniel akasema akitabasamu.

"Mmmh, sijategemea kama kazi ingekuwa ni nyepesi hivyo. Kirahisi ameweza kukutana na mheshimiwa!" Cara akashangaa

"Huyo ndiyo Elizabeth Neville. Watu wengi hawamfahamu kabisa, anao uwezo mkubwa sana, na sikufanya makosa kumpendekeza kwa Chifu wetu aingizwe kwenye idara yetu" Daniel alisema. Cara alibaki akitabasamu. Wakati huo walikuwa wakikaribia maeneo ya stesheni ya treni.

Tukutane Jioni hapahapa.
 
Riwaya: Anga ya Washenzi
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
Phone: 0765824715.

Msimu Wa Tatu
Sehemu ya 05
"Huyo ndiyo Elizabeth Neville. Watu wengi hawamfahamu kabisa, anao uwezo mkubwa sana, na sikufanya makosa kumpendekeza kwa Chifu wetu aingizwe kwenye idara yetu" Daniel alisema. Cara alibaki akitabasamu. Wakati huo walikuwa wakikaribia maeneo ya stesheni ya treni.

Baada ya dakika mbili kukatika wawili hao walifika kambini na kupaki gari. Wakakaribishwa ndani na harufu nzuri ya chakula. Elizabeth Neville alipika ndizi nyama punde tu baada ya kufika na kumkuta Gilbert Mwaitika.

"Bora hata tumefika wakati sahihi, maana njaa ambayo niko nayo si ya kitoto" Daniel Mwaseba alisema baada ya kuingia. Wakaungana mezani kula pamoja huku hadithi za hapa na pale zikiendelea.

"Hizi kazi ni za kipekee sana. Imagine tunakula saa nane usiku eti" Cara akasema wakati wanakaribia kumaliza kula. Na walipomaliza kula wakaketi pamoja na kuendelea na kile kilichopo mbele yao.

"Nimefanikiwa kuipachika ile voice tracer kwenye simu yake, hivyo kila atakachokizungumza tutakisikia" Elizabeth alianza kuelezea alivyofanikisha zoezi la kumsogeza karibu na wao makamu wa rais, Mheshimiwa Eliud Sumbi.

"Kazi nzuri Elizabeth. Tumefanikiwa pia kumtia mikononi mwetu mtu aliyemtorosha David katika kambi ya jeshi na kuwaangamiza wenzake, Gilbert alikuja naye hapa. Kuhusu David habari njema ni kwamba anaendelea vizuri, na Festus pia Dokta Yusha ameniambia hadi kesho atakuwa sawa. Mwanasheria amebaki kule kwa ajili ya kuhakikisha usalama. Kazi iliyopo mbele yetu kwa sasa ni kujua kwanini taarifa zinaonyesha Festus aliuwawa siku anafanya mauaji ya mfanyabiashara aitwaye Tark Hajir? Kwanini waseme aliuwawa wakati yupo hai? Sote tunahisi tu mtu aliye nyuma yake ni makamu wa rais Mheshimiwa Eliud Sumbi lakini hisia ni kitu kimoja na uthibitisho ni kitu kingine. Lazima tuthibitishe hili" Daniel alisema.

"Halafu kuna kitu nimekumbuka. Muda ule nipo hotelini na mheshimiwa simu yake iliita, akaonyesha wazi simu ile haikupaswa kupokewa mbele yangu hivyo alinitaka niende. Nilibahatika kuziona namba zilizokuwa juu ya kioo, zilibeba code ya Kenya. Hii ikanifanya nihusianishe juu ya uraia wa Festus na mpigaji wa simu ile." Elizabeth Neville alisema

"Ulifanikiwa kuiona namba hiyo hadi mwisho? Cara akauliza

"Si kuiona tu, na kuikariri kichwani pia" Elizabeth alisema kiutani.

"Hebu sema ukweli Elizabeth, umeikariri kweli? Cara aliuliza huku akiivuta tarakishi yake.
Daniel na Gilbert walikuwa wakishangaa tu. Kama utani vile Elizabeth akaitaja namba ile hadi mwisho.

"Hii namba nhoja niitege nipate kujua sehemu ilipo kwa sasa, nipeni dakika tano tu ngojeni muone. Sasa hapa suala la Mheshimiwa Eliud Sumbi limekwisha, twende lingine Daniel"
Cara akawa bize kubonyeza tarakishi yake na kuwaacha kina Daniel wakiendelea kuongea.

Zikapita dakika tano bila ya Cara kusema kitu. Kina Daniel walizidi kuzungumza, hatimaye dakika kumi zikakata, wote wakamgeukia Cara

"Vipi umefanikiwa?"
Cara akavuta pumzi ndefu akiwatazama wenzake.

"Imewekewa ukuta mgumu mno, yaani si rahisi kuidukua maana ina ulinzi imara sana. Nafikiri angetafutwa mtaalamu zaidi yangu. Cara alisema kwa sauti isiyo na matumaini.

"Hannan ndiye pekee anaweza kutusaidia. Sahivi kule Marekani bado mchana, unaweza kumtumia ujumbe mfupi kwenye email ili kama akiingia akauona atusaidie?" Daniel alitoa wazo.
Cara aliitikia kwa ishara ya kupandisha na kushusha kichwa chake, haraka akauchakata ujumbe mfupi na kuutuma kwa Hannan kwa njia ya barua pepe. Katika ujumbe huo aliambatanisha na namba ile.

"Halafu kuna kitu nilisahau kabisa kuwaambia. Dokta Yusha amenielekeza mahali napoweza kupata dawa ya kienyeji ya haya meno yangu yaliyolegea. Mwanzoni alinishauri meno yangu inabidi yang'olewe maana yamelegea sana, lakini binafsi sikuwa tayari kuyang'oa, ndipo akanielekeza dawa hiyo. Muda ukiniruhusu kesho nitakwenda huko kuitafuta" Daniel Mwaseba aliwaeleza wenzake.

"Hadi sauti yako imeanza kubadilika kisa homa. Pole sana Daniel. Ni wapi huko amekuelekeza?" Elizabeth Neville akasema.

"Kuna kijiji kimoja kinaitwa Uri ndipo aliponiambia, ni mwendo wa dakika 50 hivi kutoka hapa Moshi mjini hadi kufika huko. Daniel alisema, mara Tarakishi ambayo Cara anaitumia ikatoa mlio mdogo wa kuashiria kuna ujumbe mpya umeingia. Alipotazama alikuta ni Barua Pepe kutoka kwa Hannan.

"Hannan amejibu ujumbe" Cara alisema kwa furaha. Mara wakasikia ukelele wa mlango kufunguka, wote wakageuza shingo zao kutazama. Alikuwa ni Henry.

"Nimebanwa na haja ndogo, tafadhalini nionyesheni choo kilipo" Henry akasema baada ya kugundua wote walikuwa wakimtazama yeye. Kama utakumbuka kipindi anaingizwa ndani ya chumba na Gilbert Mwaitika, hakufungwa kamba wala mlango haukufungwa. Gilbert Mwaitika akamwendea na kuongozana nae chooni.

"Anapiga, Daniel zungumza naye wewe" Cara akasema huku akimsogezea Daniel Mwaseba tarakishi.
Hannan alikuwa akipiga kwa njia ya video.

"Aaah Kaka Daniel Shkamoo, habari za majuma kadhaa yaliyopita?" Hannan alizungumza baada ya kumwona Daniel.

"Marahaba Hannan, hujambo? Likizo yako inaendaje huko Marekani?" Daniel aliuliza.

"Nimekumisi sana Kaka Daniel, nimemisi pia purukushani za jiji la Dar. Wiki ijayo natarajia kurejea, nitaikatisha likizo yangu" Hannan alisema. Wakati huo Henry alikuwa akirejea na Gilbert Mwaitika kutoka chooni alipopelekwa.
Daniel akayapeleka macho yake kwa Henry, akamtazama, wakatazamana.

"Hata hivyo tupo Kilimanjaro kwa sasa, tulikuja na mheshimiwa Rais, yupo ziarani huku." Daniel alisema.

"Kabla hata hujaniambia mpo wapi nilishajua. Mpo katika mji wa Moshi, ni karibu tu na ste....." Haraka sana Daniel akabonyeza tarakishi na kuzuia sauti ya Hannan kusikiwa.

"Hannan hujaachaga tu huo ujinga? Vipi umeiona hiyo namba niliyokutumia?" Daniel aliuliza baada ya kuchomeka waya wa masikioni ili kuzuia mtu mwingine kusikia.

"Kumbe haupo peke yako kaka Daniel! Sikujua hilo, nisamehe kaka Daniel" Hannan aliomba Msamaha. Ukapita ukimya wa dakika moja,

"Hii ni namba ya nani Daniel? Imewekewa ulinzi wa hali ya juu, bila shaka mmiliki wa nambari hii si mtu wa mzaha. Ila kuna programu nitakutumia muda si mrefu kwenye akaunti yako ya telegram. Hiyo programu itakusaidia kudukua nambari hiyo, unapoingia ndani ya hiyo programu hakikisha unatumia Vpn ili iweze kuficha taarifa zako" Hannan alitoa maelekezo kwa Daniel.

"Haya Hannan. Jitahidi sana maana ni muhimu. Nakutegemea"
Daniel akaagana na Hannan. Na punde Hannan alimtumia programu ile katika simu yake kwa njia ya telegram, na ndani ya dakika tano Cara akafanikiwa kuidukua simu ile.

"Henry ana kitu cha kutuambia, anaweza kutusaidia pia. Anaomba pia msaada wetu, naombeni tuungane kumsikiliza tuone kama anaweza kutusaidia nasi tukamsaidia." Gilbert Mwaitika akasema huku akimtazama Daniel Mwaseba
Ukumbini wote walikuwa wakimtazama Henry. Licha ya kuwa bado ni usiku mnene lakini kwao ni kama ilikuwa mchana kutokana na usingizi kuwa mbali nao.

"Habari Henry. Naitwa Daniel Mwaseba, huyu anaitwa Cara. Na huyu ni Elizabeth Neville na huyu aliyekuleta hapa ni Gilbert Mwaitika. Kwa namna ulivyoletwa hapa ukaonyesha utulivu ni wazi kwamba unahitaji pia msaada wetu. Nafahamu kwamba wewe unatumika tu na mheshimiwa Eliud lakini hebu Kwanza tueleze vile vitambulisho vitatu mlivyovitumia kwenda kumchukua David kule njiro mlivipataje?" Daniel alimkazia macho na kumtaka aseme.

Henry yupo tayari kweli kusema ukweli? Usikose sehemu ijayo hapahapa Gilbert akusimulie.

Ofa ya leo ni hii hapa.... Lipia Tshs 1000 ya msimu wa nne kisha uzawadiwe bure vipande vyote vya msimu wa tatu vilivyosalia. Yaani utausoma msimu wa tatu na wa nne kwa buku lako tu. Cha kufanya sasa ni kulipia kwenda M pesa namba 0765824715 au Halopesa namba 0621249611 kisha nitext whatsapp kwa namba 0621249611 nikutumie.
 
Riwaya: Anga ya Washenzi
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
Phone: 0765824715.

Msimu Wa Tatu
Sehemu ya 06

Ukumbini wote walikuwa wakimtazama Henry. Licha ya kuwa bado ni usiku mnene lakini kwao ni kama ulikuwa mchana kutokana na usingizi kuwa mbali nao.

"Karibu kiti Henry. Naitwa Daniel Mwaseba, mwenzangu huyu anaitwa Cara. Na huyu hapa ni Elizabeth Neville. Pia huyu aliyekuleta hapa anaitwa Gilbert Mwaitika. Kwa namna ulivyoletwa hapa ukaonyesha utulivu ni wazi kwamba unahitaji pia msaada kutoka kwetu. Nafahamu kwamba wewe unatumikishwa tu na mheshimiwa Eliud. Hebu kwanza tueleze vile vitambulisho vitatu mlivyovitumia kwenda kumchukua David kule njiro mlivipataje?" Daniel alimkazia macho na kumtaka aseme.

"Daniel, mimi ni Henry Joseph, mzaliwa wa mtwara lakini makazi yangu ni Dar es Salaam. Nina mke na mtoto mmoja aitwaye Jerry. Jerry ana umri wa miaka sita" Henry akawatazama kina Daniel kwa zamu. Akagundua kila mtu alikuwa bize kumsikiliza. Cara alikuwa akimrekodi kwa kutumia tarakishi yake.

"Mienzi miwili iliyopita nilifwatwa na mwanaume mmoja aitwaye Elton Tonny, mwanaume huyu nilikuja kugundua baadae kuwa yeye ni mpambe wa makamu wa rais. Siku hiyo alinieleza kwamba amenifwatilia na kugundua niliwahi kuwa mwanajeshi kabla ya kuwa jambazi sugu ndani ya jiji la Dar. Nikiwa jeshini miaka mitano iliyopita kuna makosa yalifanyika nikafukuzwa jeshini hivyo aliniambia kama nikiungana naye tukafanya kazi pamoja anao uwezo wa kunirejesha tena jeshini, tena kwa cheo kikubwa tu. Kutokana na maisha yalikuwa ni magumu sana kwangu niliona njia ya kurejea tena jeshini kwani binafsi nilitamani sana kurejeshwa ili kulipambania taifa langu. Nikataka kujua yeye ni nani hadi awe na uwezo wa kunirejesha jeshini. Ndipo kesho yake akanikutanisha na Makamu wa rais na kunithibitishia mbele yake. Ilikuwa ni kama ndoto kukutana na makamu wa rais siku hiyo. Kweli nikakubali kufanya nao kazi bila kuhoji ni kazi gani hiyo. Lakini kwa kuwa makamu wa rais mheshimiwa Eliud Sumbi alikuwa karibu na mwanaume yule nikajiaminisha kwamba haikuwa kazi mbaya. Daniel kumbe ilikuwa ni kazi haramu eti. Nilipokuja kugundua hilo nilishachelewa, mwanangu Jerry aliwekewa kill plug katika ubongo wake. Kifaa hicho walimwekea baada ya kuona kama siridhishwi na kazi waliyonipatia, na kama ningekaidi basi wangeanza kumuua mwanangu kisha mimi na mke wangu. Nikafanya kazi yao kwa shuruti bila kupenda" Henry alizidi kueleza huku machozi yakimtoka.

"Pole sana Henry" Daniel alimwonea huruma.
"Ni kazi gani hiyo ulipewa?" Daniel akamuuliza Henry

"Daniel nawaeleza haya kwa kuwa ilikuwa ni dhamira yangu kuwaeleza. Nilishayachoka haya maisha ya kupelekeshwa eti. Mienzi miwili tu niliyofanya nao kazi ilishanigeuza kuwa mnyama. Naombeni napowaeleza haya mjitahidi kumsaidia mwanangu ili atolewe kile kifaa. Nawaahidi nitakuwa upande wenu hata kwa kuzidi kumtumikia mheshimiwa ilimradi tu muendelee kupata siri nyingi kutoka kwake"
Wote wakatazamana.

"Tupo tayari kukusaidia Henry, ni wewe tu kutueleza kila kitu unachokijua" Daniel alisema.

"Kwanza kabisa lile tukio la waandishi watano wa habari kuteketea kwa moto ndani ya kituo chao majira ya usiku lilipangwa. Haikuwa hitilafu ya umeme kama vyombo vya kiuchunguzi vilivyosema, ni mimi na wenzangu tulitumwa kwenda kuifanya kazi hiyo" Kila mtu alishtuka kusikia vile. Walikumbuka ni mwenzi sasa tangu waandishi wa habari wapate msiba mzito wa kuondokewa na waandishi wenzao watano ambao walikuwa wakisifika kwa kupekua na kunusa habari nyeti.

"Nilimwambia kabisa Songelael ile siku, nilimwambia kabisa siamini kama ni kweli moto kama ule unaweza kutokana na hitilafu ya umeme. Mungu azilaze roho zao mahala pema" Daniel alisema kwa masikitiko.

"Mmmh! Kwa hiyo na moto ambao huwa unatokea kwenye masoko makubwa huwa ni nyie pia?" Gilbert Mwaitika akauliza.

"Yote ninayowaeleza hapa haikuwa dhamira yangu Daniel, sikuwa na namna ya kukwepa kufanya." Henry alikuwa anatokwa na machozi kama mtoto mdogo
"Tulitumwa pia kuwasha moto katika masoko makubwa, kama soko la chakula la Kibaigwa kule Dodoma ni sisi tulihusika, pia lile la Manyema hapa mjini Moshi ni sisi pia, lakini ilikuwa ni maagizo kutoka kwa Mheshimiwa Eliud Sumbi kupitia kwa Elton Tonny" Henry alizidi kudondosha machozi huku akieleza. Elizabeth Neville alimwonea huruma sana, akampatia chupa ya maji ya Kilimanjaro na kumtaka anywe kwanza.

Henry akaikamata chupa ile ya maji na kumiminia kinywani hadi alipotosheka. Baada ya kuyanywa maji yale akaendelea.

"Kuna masoko ambayo hatukuhusika nayo kabisa, kama masoko mawili ya Dar es Salaam, lile la Mwanza na Arusha sijajua chanzo cha kuteketea kwa moto ni kipi, japo mheshimiwa anaweza akawa anahusika moja kwa moja maana anao vijana wengi, wanajeshi walioasi jeshini, pia huwa anawatorosha magereza majambazi sugu walio kifungoni. Sijajua nini malengo yake kwa kweli." Henry alizidi Kueleza.

"Ni hivyo tu Henry au kuna mengine?" Gilbert akauliza

"Wiki mbili zilizopita mimi na Kijana mmoja tulipewa kazi tukaifanye katika hifadhi ya taifa ya Mkomazi, tulipewa kimiminika kiasi cha lita tano na kuambiwa tukamimine kimiminika hicho ndani ya hifadhi. Tulipewa helikopta ya kutumia katika hiyo kazi, kijana niliyeongozana nae alikuwa ndiye rubani, na mimi nilikuwa na kazi ya kunyunyuza kimiminika kile, na tulipatiwa vitambulisho vilivyokuwa vikitutambulisha kama wafanyakazi wa TANAPA. Na katika hifadhi hiyo ndani ya siku mbili tu ulizuka ukame wa ajabu, kumbe kile kimiminika kilikuwa ni sumu hatarishi kwa wanyama na mimea. Japo sikujua dhamira ya kupewa kazi ile ilikuwa ni ipi lakini nahisi kina Elton wanahusika na ujangili pia maana huwa tunapeleka meno ya tembo pamoja na pembe za faru na nyati katika bandari ya Tanga" Henry aliendelea kuwaeleza kina Daniel.
Na hili likawakumbusha kina Cara majira ya alasiri waliona taarifa kama hii pia katika mtandao wa Facebook inayohusu hifadhi ya taifa ya mikumi kukumbwa na ukame wa ghafla.
"Daniel unaikumbuka ile taarifa tuliyoiona mchana kupitia mtandao wa Facebook kwenye ukurasa wa Jamii Forum? Halafu ona hii picha Daniel, bila shaka hawa ni marafiki wakubwa. Na wanayafanya haya kwa kushirikiana" Cara alisema huku akimwonyesha Daniel Mwaseba picha ya pamoja inayomwonyesha makamu wa rais, Mheshimiwa Eliud Sumbi akiwa pamoja na waziri wa utalii, maliasili na misitu, bwana Nicolaus Ndechilincho. Picha hiyo ilionyesha kuwekwa siku tatu zilizopita katika ukurasa wa Facebook wa mheshimiwa Eliud Sumbi.

"Hata waziri wa utalii anapaswa kuingizwa kwenye anga yetu ya kiuchunguzi, hili jambo ni kubwa sana. Pakikucha inabidi nikaonane na Chifu kumshirikisha haya yote" Daniel Mwaseba aliwaza.
____________
Sauti ya jogoo akiwika ilisikika kwa mbali, na wote wakagundua ilikuwa ni karibu kupambazuka kwani ilikuwa yapata saa kumi kasoro usiku. Walikubaliana na Henry arejee kwa Mheshimiwa Eliud Sumbi akaeleze kuwa David amefariki akiwa hospitalini baada ya madaktari kushindwa kuokoa uhai wake. Henry akaafiki huku akizidi kusisitiza sana mwanaye asaidiwe.

"Usijali Henry, Jerry atapona na wewe utakuwa huru na familia yako. Jina lako litasafishika pia, ila tu utuahidi kushirikiana nasi" Daniel alisema. Unapaswa kwenda kuripoti ukaeleze yote tuliyokuelekeza, waambie umekuta David ameshafariki. Sisi tutakuwa tunatafuta njia ya kumsaidia mwanao. Halafu hivi kule Njiro ilikuwaje hadi wale uliokuwa nao wakauwawa? Na vile vitambulisho hukunieleza" Daniel Mwaseba akasema

"Wale wenzangu wawili ni mimi niliwateketeza kule, niliambiwa nifanye hivyo. Kwa kupitia Elton nilipewa oda kutoka kwa Mheshimiwa Eliud Sumbi. Vile vitambulisho vitatu mimi pia sijui maana nakumbuka masaa machache baada ya kutamatika kwa ziara ya rais tulipewa kazi ya kwenda hoteli ya Five Star kumtafuta mgeni wake Mheshimiwa aliyekuwa ametoweka ghafla tu, ndipo tulipopatiwa vitambulisho hivyo tuvitumie ili kazi yetu iwe nyepesi" Henry alieleza. Wakajua bila shaka mgeni anayezungumziwa hapo ni Festus ama Ochewa aliyekamatwa na Daniel Mwaseba huko.
Kwa kuwa bado hawakuwa na imani na Henry, wakakubaliana wampeleke mbali na kambi wakiwa wamemfunika kama alivyoletwa mwanzoni. Gilbert Mwaitika akamvalisha Henry tena kitambaa cheusi kichwani ili aweze kumtoa pale kambini. Akashirikiana na Daniel hadi walipofika nje ya ukumbi wa Hugos mjini moshi. Wakamwacha hapo na kuondoka. Muda huo ilikuwa yapata saa kumi na moja alfajiri

Nini kitaendelea? Maneno ya Henry yanatosha? Usikose sehemu ijayo hapahapa katika riwaya hii yenye visa vya ajabu.

Ofa ya leo ni kwamba ukilipia Tshs 1000 utasoma vipande vilivyobakia vya msimu wa tatu na utatumiwa pia vipande vyote vya msimu wa nne. Lipa sasa kwenda M pesa namba 0765824715 au Halopesa namba 0621249611 kisha nitext whatsapp kwa namba 0621249611 nikutumie. Wahi tuwahi sasa.
 
Riwaya: Anga ya Washenzi
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
Phone: 0765824715.

Msimu Wa Tatu
Sehemu ya 07
Dakika kumi baadae Gilbert Mwaitika na Daniel Mwaseba wakarejea. Cara akaandaa chai akishirikiana na Elizabeth Neville. Wakati wakipata chai, simu ya Daniel alipata uhai, Mwanasheria Mlevi alikuwa akipiga. Na habari njema ilikuwa ni kwamba David amefungua macho yake. Hii ikawa habari njema kwao kwani kuamka kwa David kungeweza kumaliza utata juu ya kubadilishwa kwa Helikopta katika ziara ya Rais Mark. Festus hakuwa bado amerejewa na fahamu, lakini kwa mujibu wa Dokta Yusha ilikuwa ni swala la muda tu Festus azinduke. Wakapanga ratiba ya siku mpya katika kazi yao ya kiupelelezi, mwishowe wakakubaliana kupumzika kwa dakika arobaini kabla ya kukutana tena kuendelea na mambo mengine ikiwemo kusikiliza maongezi ya Mheshimiwa Eliud Sumbi akizungumza na simu kutokana na kifaa kile alichoweka Elizabeth Neville.
SURA YA TANO
Ilikuwa ni siku nyingine tena, asubuhi nyingine katika uso wa dunia na kwa wakazi wa Moshi. Baridi ilikuwa bado imetawala ikiwafanya waume kwa wake kuvalia nguo nzito na masweta. Licha ya baridi kuwa kali lakini haikuzuia shughuli za kiuchumi, kijamii na nyinginezo kuendelea. Wafanya biashara, watoto mashuleni, vyombo vya usafiri na kila shughuli kwa namna yake ziliendelea kwa kasi.
Asubuhi hiyo Rais Mark alikuwa akijiandaa kwa ajili ya kikao na wadau wa kilimo cha Kahawa mkoani kilimanjaro. Katika kikao hicho ilitarajiwa uwepo wa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro bwana Nicholaus Ndakidemi, Waziri wa kilimo na umwagiliaji, Bwana Isaack Jonathan, maofisa wa kilimo hicho pamoja na Makamu wa Rais, Mheshimiwa Eliud Sumbi.
Ulinzi uliimarishwa zaidi ya kawaida kutokana na kile kilichotaka kutokea jana ziarani. Hakuna mtu aliyekuwa akijua kilichotokea hapo jana kule ziarani zaidi ya maofisa wa siri kutoka idara ya usalama pamoja na wale walinzi wa karibu na rais. Hii ilikuwa bado ni siri kwani hata Rais Mark hakufahamishwa. IGP Kilazi, Mkurugenzi wa usalama wa taifa pamoja na Jenerali Evance walikubaliana kumweleza rais pindi ukweli utakapobainika ama hali ikianza kuwa mbaya upande wao.

Katika kikao kilichopaswa kufanyika, Daniel Mwaseba alikuwa ni mmojawapo kati ya askari kutoka kutoka usalama wa taifa waliokuwa wakiimarisha usalama. Daniel hakuwa kwenye utimamu wa mwili kutokana na Maumivu ya meno mwawili yanayomsumbua. Kama utakumbuka vyema ni lile teke alilopigwa na Festus jana jioni wakati anaufungua mlango wa buti ya gari, teke lile lilipelekea meno yake mawili kulegea kiasi cha kumpa shida haswa wakati wa kula. Homa na maumivu ya kichwa vilimsumbua kwa pamoja, ukichanganya na kwamba usiku mzima ulipita bila yeye kuupumzisha mwili wake hivyo hakuwa katika utimamu wake.

Makamu wa rais, Mheshimiwa Eliud Sumbi alifanikiwa kumwona Daniel Mwaseba wakati anawasili kabla ya kikao kuanza. Alimwona akiwa anazungumza na Mkurugenzi wa usalama wa Taifa, Chifu Abdallah Ntenga. Bila kuchelewa Mheshimiwa Eliud Sumbi akavuta simu yake na kumpigia Elton Tonny ambaye hakuwa mbali na maeneo yale.

"Elton upo wapi?..... Yule mpelelezi yupo hapa namwona. Hakikisheni leo mnamtia mikononi mwenu na apelekwe kambini" Mheshimiwa Eliud Sumbi akarejesha simu yake mfukoni baada ya kumaliza kuongea na Elton Tonny ambaye ni mpambe wake.
Elton Tonny alikuwa upande wa nje, haikuwa ngumu kuingia ndani ya viwanja vya ikulu kutokana na kutambulika kuwa ni mpambe wa makamu wa rais na isitoshe pia makamu alikuwa pale. Akiwa katika kupepesa macho yake alifanikiwa kumwona Daniel Mwaseba akiwa anazungumza na mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa. Akasubiri hadi alipoona Daniel anaelekea upande wa pili naye akamfuata kwa nyuma.

Daniel akizidi kusonga mbele alikuwa kwenye mawazo. Mawazo ya kuipata dawa aliyoelezwa na Dokta Yusha hapo jana. Alipanga aelekee katika kijiji hicho alichoelezwa baada ya kikao kinachomhusisha mheshimiwa Rais na wadau wa kilimo cha kahawa kutamatika. Akiwaza hayo ghafla alipamiana na mtu. Hii ikamfanya aanguke kwani hakuwa imara wakati akitembea.

"Oooh pole, samahani sana kaka mkubwa." Mwanaume aliyegongana na Daniel alisema huku akimpa Daniel mkono apate kujiinua.
Ndipo Daniel akainua uso wake juu kumtazama mwanaume huyu. Alikutana uso kwa uso na sura ya Elton Tonny. Alikumbuka majira ya usiku kabla hakujakucha jinsi alivyoelezwa na Henry kumuhusu mtu huyu. Mapigo yake ya moyo yalikita kwa kasi mno. Alihisi uwepo wa Elton Tonny unaweza kuwa na sababu, lakini pia akaona labda kwa vile Mheshimiwa Eliud Sumbi pia yupo pale ndio maana. Lakini hii haikumfanya Daniel Mwaseba kuacha kumtilia mashaka Elton.

"Ahsante, usijali niko sawa" Daniel alisema na kujiinua mwenyewe bila kuupokea mkono ule wa Elton Tonny. Elton akatabasamu na kuondoka zake kuelekea upande ambao vyoo vipo.
Laiti angejua lengo la mtu huyu kumparamia hadi kumwangusha! Maskini Daniel, hakujua..
Hakujua

Elton Tonny hakuambulia patupu baada ya kupamiana na Daniel, wakati anapishana na Daniel alijipeleka kwa makusudi mbele yake na kumfanya Daniel ayumbe kiasi na kuanguka. Wakati Daniel akielekea chini, haraka sana Elton Tonny akagusa soli ya kiatu cha Danieli upande wa kukanyagia na kuchomeka chipu ndogo iliyo mfano wa mwiba, baada ya kufanya vile akazuga kwa kumtaka Daniel radhi. Kitendo hiki kilifanyika kwa wepesi mno bila kumwachia maswali mtu yeyote.

"Kazi kwisha. Vimebaki vitendo tu" Elton Tonny alijisemea baada ya kuingia maliwatoni. Akajisafisha uso na kujitazama katika kioo.
Alikuwa anatabasamu, na hili lilikuwa ni tabasamu la ushindi. Lakini hapaswi kujipongeza mapema hivi, anapaswa kujua kwamba huyu ni Daniel Mwaseba, mpelelezi nambari moja nchini Tanzania.
---------------------

Wakati Mheshimiwa Eliud Sumbi akizungumza na simu ile, Elizabeth Neville pamoja na Cara wakiwa kule walipoweka kambi walikuwa wakiyasikia maongezi yale kupitia kifaa kilicho mfano wa simu. Haraka sana wakampigia Daniel na kumweleza kuhusiana na kile walichokisikia. Wakamsihi Daniel kuwa makini kwani mpelelezi aliyekuwa anazungumziwa si mwingine, bali ni yeye.

"Usijali Elizabeth, hawatoweza. Hapo baadae nitakwenda katika kijiji kile nilichoelezwa na Dokta Yusha kutafuta ile dawa ya kienyeji. Meno yameniletea homa mbaya sana, kichwa nacho kinauma pia. Hii imenifanya hadi mwili kuwa dhaifu." Daniel alikuwa anaongea na simu. Alikuwa akiongea na Elizabeth Neville.

"Tutakwenda wote Daniel. Nitakuendesha mume wangu, hupaswi kuzidi kujipa mateso ingali nipo hai Daniel" Elizabeth Neville alisema kwa hisia.

"Elizabeth" Daniel aliita

"Abee Daniel"

"Nimezungumza na Chifu muda si mrefu, nimemweleza tulipofikia na nimemwahidi kufikia kesho kabla mheshimiwa Rais hajaelekea mkoani Arusha kwa mwendelezo wa ziara. Nadhani tutakuwa tumeshafika mbali katika uchunguzi wetu., hivyo naomba mwendelee kuutumia muda huu katika kuchunguza taarifa za simu ya Mheshimiwa Eliud Sumbi na ile ya yule mtu wa Kenya. Wacha mimi niende peke yangu nyie muendelee kufanya kazi." Daniel alisema

"Haya Daniel, kwa sasa Mwanasheria na Cara wanawasiliana na idara ya upelelezi kutoka nchini Kenya kuhusiana na ule utata wa Festus kuwa hai wakati taarifa zinaonyesha aliuwawa. Gilbert Mwaitika ameenda nyumbani kwa Dokta Yusha tayari ili kuwaangalia kina Festus. Pia David amesema yupo tayari kuongea kila kitu bila kuficha. Tunakusubiri Daniel" Elizabeth Neville alisema

"Hatua kubwa sana Elizabeth, najivunia nyinyi, mnaupiga mwingi sana kiasi kwamba hata nikiwa sipo mnaweza kufanya kazi. Pindi nitakaporudi tutaenda tukiwa pamoja na Chifu na Jenerali Evance pia ili wakasikie kila kitu atakachoongea David." Daniel alisema.

Wakati Daniel akiongea, Elton Tonny alishatoka maliwatoni na sasa alikuwa akitoka nje ya Ikulu tayari kwa kumsubiri. Ilikuwa ni lazima ampate kabla siku haijaisha kama mheshimiwa Eliud Sumbi alivyosema. Kwa vile alishamwekea kifaa cha kutambua kila aendapo, hakuwa na shaka ya kumpoteza.

ITAENDELEA

Jipatie msimu wa nne wa Riwaya hii pamoja na ofa ya vipande vilivyobakia vya msimu huu wa tatu kwa malipo ya Tshs 1000 tu. Lipa kwenda Halopesa namba 0621249611 au Mpesa namba 0765824715 kisha njoo whatsapp kwa namba 0621249611 nikutumie.
 
Riwaya: Anga ya Washenzi
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
Phone: 0765824715.

Msimu Wa Tatu
Sehemu ya 08
Daniel akiongea, Elton Tonny alishatoka maliwatoni na sasa alikuwa akitoka nje ya Ikulu tayari kwa kumsubiri Daniel. Ilikuwa ni lazima ampate kabla siku haijaisha kama mheshimiwa Eliud Sumbi alivyosema. Kwa vile alishamwekea kifaa cha kutambua kila aendapo, hakuwa na shaka ya kumpoteza.
--------------------

Kikao kinachohusisha wadau wa kilimo cha kahawa na Rais Mark ulianza kama ilivyopangwa. Rais Mark pamoja na makamu wake walikuwa wakisikiliza changamoto zinazowakabili wakulima wa zao hilo ambalo limekuwa ni zao pekee linalozidi kutokomea kila kukicha. Hoja zikachangiwa na kukusanywa na mwisho kuahidiwa kutafutiwa ufumbuzi kwa changamoto zote, mzigo ukabebeshwa kwa wizara ya kilimo na umwagiliaji chini ya Waziri Isaack Jonathan. Mwishowe kikao kikatamatikana.
Saa tano kamili asubuhi ilipotimia taarifa kutoka kwa msemaji wa serikali ikasema Rais angeelekea kesho yake Jijini Arusha kwa mwendelezo wa ziara. Hivyo maandalizi yakaanza mapema huku idara ya usalama wa taifa ikishirikiana na Jeshi la wananchi na lile la Polisi chini ya IGP Kilazi zikapanga mipango yao ya kiulinzi ili kusiwepo na tukio lolote tena linaloweza kutishia usalama kama lile la Ushirika Moshi.
*********
Ilikuwa ni saa saba mchana ambayo ilimkutia Dwaniel Mwaseba katika kijiji cha Uchau, mahali ambapo alielekezwa angepata dawa ya kienyeji kwa ajili ya meno mawili yanayozidi kumuuma na kumletea homa. Japokuwa alishauriwa na Dokta Yusha ang'olewe meno yale lakini hakuwa tayari kuwa na mapengo, tena mapengo ya meno ya mbele. Kwa kuwa alipata uhakika wa dawa ya kienyeji inayoweza kumtibu basi aliiendea katika kijiji hichi. Baada ya kuwasili katika kijiji hichi aliamua kupaki gari yake nje ya baa moja aliyoiona inayouza pombe za kienyeji. Baada ya kushuka garini akahakikisha amefunga mlango wa gari kwa funguo ndipo alipozipiga hatua zake kuelekea upande wa ndani kwani baa hii ilizungushiwa mabati pamoja na miti kama uzio. Baada ya kuingia ndani ya uzio, akaelekea moja kwa moja hadi katika meza moja iliyokaliwa bibi kikongwe ambaye alionekana akinywa pombe maarufu kwa wachaga ijulikanayo kama Mbege.
Alipoifikia meza ile akasalimiana na bibi huyu.

"Samahani Mama yangu, mimi si mwenyeji hapa, nimeelekezwa katika kijiji hiki kwamba inapatikana dawa ya jino. Naomba unisaidie inapatikana wapi dawa hii" alieleza Daniel

"Wewe ndio unayeumwa na jino!, fo.. mai tataa mbee... maumivu ya jino nayajua, ni makali sana. Pole sana kijana wangu; kipindi nina umri kama wako nilianguka na kung'oka jino moja, mengine yakalegea na kunipa maumivu makali sana, lakini baada ya kutumia hiyo dawa nilipona kabisa. Kijana wangu hiyo dawa imeota pale kwa mama kimboka, ni mama kimboka tu anayo hapa mtaani kwetu, wewe mpelekee tu ugoro mkebe mmoja anakuruhusu uichume" Bibi yule alisema akionyesha mbege ilishaanza kumlevya. Alikuwa akijibu kilevi huku akichanganya na lugha ya kichaga.
Daniel aliposikia dawa hiyo inapatikana kwa mama Kimboka alimshukuru bibi yule na kisha kutoa noti ya shilingi elfu Tano na kumkabidhi kama ahsante. Bibi yule alishukuru sana huku akimsifia mwanamke aliyemzaa kijana huyu. Nadhani kama angejua huyu aliyempatia maelekezo haya anaitwa Daniel Mwaseba ambaye kila kukicha sifa zake huimbwa kwenye mitandao ya kijamii na majarida kutokana na kazi zake za kipelelezi basi angeipongeza hadi ardhi inayokanyagwa na miguu yake.
Daniel Mwaseba alinyanyuka na kuelekea katika uchochoro mmoja alioelekezwa kama njia ya kumfikisha kwa Mama Kimboka.
Akiwa katika uchochoro ule alikutana na mtoto mmoja akiwa na sare za shule akicheza

"Hujambo Mtoto mzuri!," Daniel alimsabahi mtoto yule kwa tabasamu la upendo.

"Sijambo shkamoo" alijibu mtoto yule baada ya kusimama na kugeuka

"Marahabaa mtoto mzuri, unaitwa nani?"

"Naitwa Fat-Hiya"

"Wow, jina zuri kweli, umetoka shule?"

"Ndiyo"

Ohoo, mama anaitwa nani?" Daniel Mwaseba alimuuuliza mtoto yule,

"Mama yangu anaitwa Mama Kimboka"
Moyo wa Daniel ulimlipuka kwa shangwe baada ya kusikia jina lile, akajua bila shaka ndiye mama huyohuyo aliyeelekezwa na bibi yule ndipo inapopatikana dawa ya jino.

"Haya nipeleke kwa mama nikamsalimie, sawa mtoto mzurie," alimwambi mtoto yule, taratibu wakaelekea nyumbani anapokaa mtoto Fat-Hiya.
Baada ya dakika mbili walifika. Mama Fat-Hiya alikuwa ni mama wa makamo kidogo, alipomwona mwanaye akija na mgeni haraka aliingia jikoni na kutoka na Kigoda. Kigoda ni kiti cha miguu mitatu kinachotumiwa sana na wachaga haswa maeneo ya jikoni. Labda kutokana na uchache wa viti ilipelekea Daniel kupewa kigoda akalie. Alikaribishwa kwenye Kigoda kile. Bila kusita Daniel akaupokea ukaribisho huo

"Ahsante sana mama, nashukuru kwa ukaribisho huu" Daniel alushukuru huku akiketi.

"Wewe ni mtoto wa nani kijana wangu?" Mama yule alimuuliza Daniel Mwaseba huku akijitahidi kuketi chini

"Mimi si mwenyeji wa mtaa huu mama, nimetoka mbali kidogo. Ninasumbuliwa sana na jino hivyo nikaelekezwa dawa ya jino inapatikana katika kijiji hiki."

"Sasa umekuja na nini kijana wangu?" Mama yule aliuliza huku akiitazama mikono ya Daniel. Daniel alielewa nini anapaswa kufanya. Hakuwa na ugoro kama bibi yule alivyomueleza katika baa ile iuzayo pombe za kienyeji, alichofanya akauingiza mkono wake mfukoni na kutoa noti mbili za shilingi Elfu kumi. Mama Fat-Hiya akaunyoosha mkono wake kwa haraka kuzipokea noti zile, na akazikwapua kabla hata Daniel Mwaseba hajairuhusu mikono yake kuziachia.

"Mbona unanipa hela nyingi hivi mwanangu?, Mungu akubariki sana kijana wangu. Ahsante sana........ Wewe Fat-Hiya hebu let kisu haraka nikamchumie mgeni dawa" Mama yule alisema huku akizihifadhi noti zile ndani ya bikini iliyoyahifadhi matiti yake.
Punde Fat-Hiya alitoka nje akiwa na kisu mkononi, akamkabidhi mama yake na kisha kurejea tena ndani.

"Twende huku" Mama Fat-Hiya alisema huku akinyanyuka, Daniel Mwaseba akanyanyuka na kuongozana na mama yule hadi nyuma ya kijumba chake kilichoezekwa kwa makuti. Mama yule alisimama mbele ya mti mmoja mdogo ulio mfano wa ua. Mti huo wenye majani ya kijani kibichi chenye kung'ara sana, majani yake yalikuwa ni dawa tosha kwa mtu anayesumbuliwa na jino. Pindi unapolitafuna jani hili na kuliweka katika fizi za jino legevu basi jino hilo huwa imara na kurejea katika hali yake ya mwanzo.
Mama Fat-Hiya aliyachuma majani matano kwa kutumia kisu na kumkabidhi Daniel.

"Tunayachuma na kisu ili kuepusha mti wake kunyauka. Huwa unanyauka kama ukiyachuma vibaya majani yake, ndiyo maana mti huu ni adimu sana." Alisema mama Fat-Hiya.
Ilichukua karibu dakika kumi na tano kwa Daniel Mwaseba kuzungumza mengi na mama yule, akaelekezwa pia njia sahihi ya kuyatumia majani yale ili aweze kupona kwa wakati. Daniel Mwaseba alishukuru sana kwa mama yule huku akiahidi kurejea na zawadi pindi aponapo. Baada ya maongezi hayo Daniel aliaga na kurejea katika baa ile.
Akiwa njiani kuelekea katika ile baa alipoiacha gari yake alitoa simu yake na kumpigia Dokta Yusha.

"Hatimaye nimeipata dawa" Daniel Mwaseba alisema kwa furaha baada ya simu kupokelewa.

"Jani lake ni la mviringo na ni kijani kibichi king'aacho?" Dokta Yusha aliuliza simuni

"Ndiyo ni yenyewe, hatimaye jino langu linaenda kukaa sawa. Naahidi yule mwanaharamu atalipa meno saba zaidi ya haya mawili aliyotaka kuning'oa, nina hasira naye sana mshenzi huyu. Kwanza ameshazinduka?"

"Hahaha, acha hasira Daniel, nimemwacha Gilbert Mwaitika nyumbani, nadhani Festus atakuwa ameshazinduka maana nilimwacha akiwa anaendelea vyema. Kwa sasa mimi naingia katika chumba cha upasuaji, nadhani tutawasiliana baadae Daniel" Dokta Yusha alisema na kisha kukata simu.
Daniel akairejesha simu yake mfukoni. Akatoa jani moja mfukoni katika yale matano aliyopatiwa, akaliweka mdomoni na kulitafuna. Baada ya kusagika akaliegesha katika meno ya mbele huku akizidi kuzipiga hatua kuelekea katika baa ile. Na alipokuwa akienda alianza kuwaza ni kwa namna gani angeshangilia pindi ikithibitika Makamu wa rais ndiye mhusika wa mambo yote aliyoelezwa na Henry hapo jana usiku. Aliamini hadi walipofikia ilibaki tu David aseme kuhusiana na Helikopta tu ndipo ukweli ubainike.
Baada ya dakika tano Daniel Mwaseba aliweza kufika pale alipoiacha gari yake. Alitazama katika meza ile aliyomwacha bibi yule aliyemwambia inapopatikana Dawa ya Jino. Lakini hakukuwa na mtu katika meza ile. Akatoka na kuelekea garini, akautoa ufunguo wake na kuufungua mlango wa gari, akaingia na kuwasha gari na hatimaye kuondoka, safari ya kurudi Moshi Mjini ikaanza.
Lakini mita mia moja kutoka pale ilipopaki gari ya Daniel alisimama Elton Tonny. Alilitama gari la Daniel hadi lilipotoweka mbele ya macho yake. Akakamata simu yake na kupiga.

"Kila kitu kipo sawa huku. Kaeni tayari. Anakuja" Elton Tonny alisema na kurejesha simu mfukoni. Uso wake ulinakshiwa kwa tabasamu.

Huu ni Mwisho wa Msimu wa Tatu wa Anga ya Washenzi. Msimu wa nne upo tayari, ni moto utawaka. Usikose[emoji3059]

Msimu wa nne unapatikana kwa Tshs 1000 tu. Utatumiwa whatsapp au hapahapa Fb. Lipia kwenda Halopesa namba 0621249611 au Mpesa namba 0765824715 kisha nitext inbox hapa fb au whatsapp kwa namba 0621249611 nikutumie
Hii ni Anga ya Washenzi.
 
#AngaYaWashenzi

Ilianza kama tukio la kigaidi pale viwanja vya Chuo kikuu cha Ushirika Moshi. Bahati nzuri Daniel Mwaseba na wenzake wakafanikiwa kulidhibiti tukio hilo mapema kabla halijatokea. Ndani ya tukio hilo wanakutana na mambo makubwa, yenye kushangaza. Lakini katika harakati za kukamilisha uchunguzi yanaibuka mazito huku Daniel Mwaseba akionekana kuwekewa mtego wa kukamatwa na Elton Tonny kwa amri ya Mheshimiwa Eliud Sumbi. Hakika Daniel Mwaseba atakwenda kukamatika. Atakamatika vipi? Wenzake watamwokoa mapema? Atapitia yapi kifungoni?
Msimu wa nne utatupa mwangaza, kisha msimu wa tano utatukamilishia riwaya hii.
Jipatie leo Msimu wote wa nne kwa Malipo kidogo ya Tshs 1000 tu kupitia WhatsApp namba 0621249611 au hapa facebook inbox. Lipa kwenda Halopesa namba 0621249611 au Mpesa namba 0765824715.

gilbert Evarist Mushi
 
Riwaya: Anga ya Washenzi
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
Phone: 0765824715.

Msimu Wa Nne
Sehemu ya 01
Lakini mita mia moja kutoka pale ilipopaki gari ya Daniel alisimama Elton Tonny ambaye ni mpambe wa Makamu wa rais. Elton Tonny alikuwa akilitazama gari la Daniel hadi lilipotoweka mbele ya macho yake. Upesi akakamata simu yake na kupiga namba fulani..

"Kila kitu kipo sawa huku. Kaeni tayari. Anakuja" Elton Tonny alisema na kurejesha simu mfukoni.
_____________
Daniel Mwaseba akiwa ndani ya gari aliuingiza mkono mmoja mfukoni na kuitoa simu yake, ni baada ya kusikia mtetemo mfupi wa kuashiria ujumbe kuingia. Akiwa makini na kuendesha gari, alitoa nywila katika simu yake na kuufungua ujumbe ule.

"Festus amezinduka."
Ulikuwa ni ujumbe mfupi kutoka kwa Gilbert Mwaitika. Akaamua kumpigia Gilbert. Simu ikaita kwa sekunde nne na kisha kupokelewa.

"Niambie Daniel" sauti ya Gilbert ikasikika ikisema simuni.

"Usiniambie Festus ameamka" Daniel akasema.
Wakati akiongea na simu, macho yake yakauona mteremko ukiambatana na kona kali mbele. Mita mia mbele ulikatiza mto mkubwa unaotoa maji yake kutoka kilele cha Mlima Kilimanjaro. Mto huo unajulikana kama mto Isiye ndio chanzo kikuu cha maji katika mto Pangani unaopita mkoani Tanga na kumwaga maji yake katika bahari ya Hindi.
Hali ilikuwa ni ya utulivu sana barabarani, hakukuwa na gari la ziada ama mtu akikatisha eneo la karibu. Daniel Mwaseba aliutoa mguu wake wa kulia kutoka kwenye kinyonya mafuta na kuupeleka katika sehemu ya kukanyaga breki ili aweze kuendana na mteremko ule mkali. Matairi ya gari yalianza kuisugua lami kwa mwendo wa taratibu na gari ilitii na kuanza kupungua mwendo. Lakini katika kupungua mwendo ulizuka mlio wa ajabu, mlio ambao ulishabihiana kwa kiasi kikubwa na mlio wa saa. Aliifungua droo ndogo iliyopo kwenye dashbodi ya gari na kuitoa saa yake, Lakini mlio anaousikia haukuwa ukitoka katika saa ile.

"Gilbert hebu subiri nitakupigia. Kuna kitu kinanichanganya hapa" Daniel Mwaseba alisema na kukata simu. Akaiweka mfukoni na kukanyaga breki tena na kupelekea gari kutembea kwa mwendo mdogo zaidi, akaisogeza gari yake hadi kando ya barabara ili aweze kuubaini mlio ule unatokea wapi.
Baada ya kupaki gari ile, Daniel Mwaseba alitega sikio lake kwa sekunde nane ndipo alipobaini mlio ule haukuwa ukisikika ndani ya gari, bali katika uvungu wa gari. Akafungua mlango wa gari na kutoka ili kwenda kutazama nje, alipofika akainama chini kidogo na kuchungulia...
Loooh!!! Aliona bomu limetegwa pembeni ya waya wa breki. Akajua bila shaka muda ule alipoikaribia kona iliyoambatana na mteremko akaikanyaga breki basi ilipelekea kulitegua bomu hilo kwani bomu hilo lilitegwa kuendana na mfumo wa breki ya gari. Hata hivyo asingeweza kulitegua bomu lile kwa kuwa alishachelewa, wakati anagundua bomu hilo, aliona sehemu yenye namba zinazojihesabu mithili ya saa zikionyesha zilibakia sekunde tano tu kabla ya bomu kulipuka.
Sekunde Tano zilikuwa ni nyingi sana kwa Daniel Mwaseba pindi awapo katika hatari, lakini leo hii zilikuwa ni chache sana, uchache huo ulitokana na ule mshangao uliomkumba baada ya kubaini kwamba lile ni bomu. Mshangao ule ukameza sekunde mbili, sekunde tatu zilizobakia Daniel Mwaseba aligeuka kwa kasi na kuanza kuzipiga hatua ndefu kukimbia...
Hakumalizia hatua ya pili, Mlipuko mkubwa ulitokea na kulisambaratisha gari lile huku yeye akirushwa kuelekea juu na kurushiwa umbali wa hatua kama Tano kutoka pale ulipotokea mlipuko. Pembeni ya barabara ile kulikuwa na mtaro mrefu sana uliojengwa kwa kuelekezwa katika Mto Isiye. Daniel Mwaseba aliporushwa kutokana na mlipuko ule alidondokea ndani ya mtaro ule na kubiringika mithili ya tairi hadi katika kingo za mto Isiye.

Dakika moja baada ya kutokea mlipuko ule ilifika Lori la kubebea mchanga na kupaki jirani kabisa na pale ulipotokea mlipuko. Punde vijana wapatao saba waliovalia tisheti nyeusi zenye nembo ya Fuvu la Kichwa wakateremka wakiwa na madumu makubwa yenye maji pamoja na mtungi mkubwa wa kuzima moto (Fire Extinguisher) na kuusogelea moto ule, mmoja wao alianza kuuzima moto kwa kutumia mtungi ule, baada ya moto kuzima wanaume wale walioshikilia madumu yenye maji walianza kumwaga maji sehemu ile na kukusanya vipande vya mabaki ya gari ya Daniel Mwaseba na kuvipakia ndani ya Lori. Baada ya kuhakikisha hakuna baki lolote lililosalia vijana watano walipanda lori lile na kuondoka. Vijana wawili waliobakia waliteremka na mtaro ule taratibu wakijisogeza mahali alipodondokea Daniel Mwaseba. Na mmoja kati ya wanaume hao alikuwa ni Henry.
Henry baada ya kuuona mwili ule alishtuka sana.

"Vipi, unamfahamu? Naona umeshtuka baada ya kumwona" mwanaume aliyeambatana nae akamuuliza Henry

"Aa.. amna, hata simfahamu ndio kwanza namwona leo. Kwani vipi?" Henry akajitetea akijaribu kujiweka sawa.

"Kumbe tuliyetumwa kumchukua ni Daniel Mwaseba! Daaah! Kama ningejua ni yeye ningemtaarifu mapema. Sijui nifanyaje hapa na wanaweza kunigundua kama nafahamiana nae" Henry alikuwa anawaza peke yake. Alikumbuka usiku wa jana kabla Daniel Mwaseba na wenzake hawajaachana naye alipatiwa karatasi yenye namba ya simu

"Chukua namba zangu. Ukipata chochote tutafahamishana." aliyakumbuka maneno haya, aliambiwa na Daniel usiku kabla ya kurudishwa na gari.

"Unawaza nini? Hebu tumwinue tunasubiriwa juu" Henry alishtuliwa na mwenzake kutoka kwenye dimbwi la mawazo. Bila kuchelewa wakashirikiana kuunyanyua mwili huo na kurejea nao barabarani, walipofika barabarani walikuta Noah Nyeusi imepaki pembezoni mwa barabara ikiwasubiri. Bila kuchelewa wakauingiza mwili wa Daniel Mwaseba ndani ya buti, wakaingia ndani ya Noah ile na kuondoka nayo.
-----------------------

Gilbert Mwaitika, Elizabeth Neville, Mwanasheria Mlevi pamoja na mwanadada aitwaye Cara walikuwa wakimsubiri Daniel Mwaseba kwa hamu kubwa. Hii ilikuwa ni baada ya David kuufungua mdomo wake punde tu baada ya kuzinduka. Wote walihamia nyumbani kwa Dokta Yusha baada ya kuitwa na Gilbert Mwaitika.
David hakuficha kitu, aliwaeleza jinsi alivyoitwa na mpambe wa Mheshimiwa Eliud Sumbi siku moja kabla ya ziara ya rais kufanyika. David aliwaeleza jinsi alivyokutanishwa na mheshimiwa Eliud Sumbi na kupatiwa mpango wa kubadili helikopta.

Siku ile ilikuwa hivi...
Baada ya David kuonana na mheshimiwa Eliud Sumbi, Siku hiyo walizungumza kwa takribani nusu saa na baada ya kuukubali mpango wa mheshimiwa Eliud, David alipatiwa dawa ya usingizi na Elton Tonny.

"Dawa hii utaipulizia kesho ndani ya Helikopta yenu nusu saa kabla ya kuingia. Baada ya hapo, muda ukifika wa kuirusha helikopta angani hakikisha wenzako ndio wanaanza kuingia ndani. Wakishaingia na kuvuta pumzi haitawachukua muda, watadondoka chini kama maembe machanga yaliyozidiwa na upepo" Elton Tonny alisema

"Watakufa?" David aliuliza baada ya kupatiwa dawa hiyo

"Hapana. Watapata usingizi mzito ambao hauamshiki hadi masaa thelathini na sita yapite. Wewe usiingie ndani hadi zipite tena dakika kumi na tano. Baada ya hapo utaingia, nawe utasinzia lakini ni kwa masaa manne tu ndipo utarejewa na fahamu. Ukisharejewa na fahamu utajifanya kutoa ripoti huelewi ni kitu gani kinaendelea. Na wakati huo sisi tutakuwa tumeshaimaliza kazi yetu. Kuhusu Helikopta ondoa shaka maana wakati huo tutairusha helikopta ya kufanana na yenu ili iwe rahisi kwa kazi yetu kukamilika"
David alipotaka kujua ni kazi gani aliambiwa atulie hadi itakapokamilika ndipo atajuzwa.

Na hivyo ndivyo ilivyokuwa, wote wakaridhika na maelezo ya David, japokuwa walimwonea sana huruma kwani tayari alikuwa ni msaliti.

TUKUTANE TENA KESHO SAA 12 JIONI.

NOTE: Kama utauhitaji msimu huu wa nne utaupata jwa gharama ndogo tu ya Tshs 1000 tu. Lipia kwenda M pesa namba 0765824715 au TigoPesa namba 0678824073 kisha njoo whatsapp kwa namba 0621249611 nikutumie. Wale wengine tutaendelea kuisoma hapahapa kila ninapopata nafasi ya kuiweka.
Msimu wa Tano ndio msimu wa mwisho wa Riwaya hii, utaanza kupatikana kesho mchana kwa Tshs 700 tu
 
Riwaya: Anga ya Washenzi
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
Phone: 0765824715.

Msimu Wa Nne
Sehemu ya 01
Lakini mita mia moja kutoka pale ilipopaki gari ya Daniel alisimama Elton Tonny ambaye ni mpambe wa Makamu wa rais. Elton Tonny alikuwa akilitazama gari la Daniel hadi lilipotoweka mbele ya macho yake. Upesi akakamata simu yake na kupiga namba fulani..

"Kila kitu kipo sawa huku. Kaeni tayari. Anakuja" Elton Tonny alisema na kurejesha simu mfukoni.
_____________
Daniel Mwaseba akiwa ndani ya gari aliuingiza mkono mmoja mfukoni na kuitoa simu yake, ni baada ya kusikia mtetemo mfupi wa kuashiria ujumbe kuingia. Akiwa makini na kuendesha gari, alitoa nywila katika simu yake na kuufungua ujumbe ule.

"Festus amezinduka."
Ulikuwa ni ujumbe mfupi kutoka kwa Gilbert Mwaitika. Akaamua kumpigia Gilbert. Simu ikaita kwa sekunde nne na kisha kupokelewa.

"Niambie Daniel" sauti ya Gilbert ikasikika ikisema simuni.

"Usiniambie Festus ameamka" Daniel akasema.
Wakati akiongea na simu, macho yake yakauona mteremko ukiambatana na kona kali mbele. Mita mia mbele ulikatiza mto mkubwa unaotoa maji yake kutoka kilele cha Mlima Kilimanjaro. Mto huo unajulikana kama mto Isiye ndio chanzo kikuu cha maji katika mto Pangani unaopita mkoani Tanga na kumwaga maji yake katika bahari ya Hindi.
Hali ilikuwa ni ya utulivu sana barabarani, hakukuwa na gari la ziada ama mtu akikatisha eneo la karibu. Daniel Mwaseba aliutoa mguu wake wa kulia kutoka kwenye kinyonya mafuta na kuupeleka katika sehemu ya kukanyaga breki ili aweze kuendana na mteremko ule mkali. Matairi ya gari yalianza kuisugua lami kwa mwendo wa taratibu na gari ilitii na kuanza kupungua mwendo. Lakini katika kupungua mwendo ulizuka mlio wa ajabu, mlio ambao ulishabihiana kwa kiasi kikubwa na mlio wa saa. Aliifungua droo ndogo iliyopo kwenye dashbodi ya gari na kuitoa saa yake, Lakini mlio anaousikia haukuwa ukitoka katika saa ile.

"Gilbert hebu subiri nitakupigia. Kuna kitu kinanichanganya hapa" Daniel Mwaseba alisema na kukata simu. Akaiweka mfukoni na kukanyaga breki tena na kupelekea gari kutembea kwa mwendo mdogo zaidi, akaisogeza gari yake hadi kando ya barabara ili aweze kuubaini mlio ule unatokea wapi.
Baada ya kupaki gari ile, Daniel Mwaseba alitega sikio lake kwa sekunde nane ndipo alipobaini mlio ule haukuwa ukisikika ndani ya gari, bali katika uvungu wa gari. Akafungua mlango wa gari na kutoka ili kwenda kutazama nje, alipofika akainama chini kidogo na kuchungulia...
Loooh!!! Aliona bomu limetegwa pembeni ya waya wa breki. Akajua bila shaka muda ule alipoikaribia kona iliyoambatana na mteremko akaikanyaga breki basi ilipelekea kulitegua bomu hilo kwani bomu hilo lilitegwa kuendana na mfumo wa breki ya gari. Hata hivyo asingeweza kulitegua bomu lile kwa kuwa alishachelewa, wakati anagundua bomu hilo, aliona sehemu yenye namba zinazojihesabu mithili ya saa zikionyesha zilibakia sekunde tano tu kabla ya bomu kulipuka.
Sekunde Tano zilikuwa ni nyingi sana kwa Daniel Mwaseba pindi awapo katika hatari, lakini leo hii zilikuwa ni chache sana, uchache huo ulitokana na ule mshangao uliomkumba baada ya kubaini kwamba lile ni bomu. Mshangao ule ukameza sekunde mbili, sekunde tatu zilizobakia Daniel Mwaseba aligeuka kwa kasi na kuanza kuzipiga hatua ndefu kukimbia...
Hakumalizia hatua ya pili, Mlipuko mkubwa ulitokea na kulisambaratisha gari lile huku yeye akirushwa kuelekea juu na kurushiwa umbali wa hatua kama Tano kutoka pale ulipotokea mlipuko. Pembeni ya barabara ile kulikuwa na mtaro mrefu sana uliojengwa kwa kuelekezwa katika Mto Isiye. Daniel Mwaseba aliporushwa kutokana na mlipuko ule alidondokea ndani ya mtaro ule na kubiringika mithili ya tairi hadi katika kingo za mto Isiye.

Dakika moja baada ya kutokea mlipuko ule ilifika Lori la kubebea mchanga na kupaki jirani kabisa na pale ulipotokea mlipuko. Punde vijana wapatao saba waliovalia tisheti nyeusi zenye nembo ya Fuvu la Kichwa wakateremka wakiwa na madumu makubwa yenye maji pamoja na mtungi mkubwa wa kuzima moto (Fire Extinguisher) na kuusogelea moto ule, mmoja wao alianza kuuzima moto kwa kutumia mtungi ule, baada ya moto kuzima wanaume wale walioshikilia madumu yenye maji walianza kumwaga maji sehemu ile na kukusanya vipande vya mabaki ya gari ya Daniel Mwaseba na kuvipakia ndani ya Lori. Baada ya kuhakikisha hakuna baki lolote lililosalia vijana watano walipanda lori lile na kuondoka. Vijana wawili waliobakia waliteremka na mtaro ule taratibu wakijisogeza mahali alipodondokea Daniel Mwaseba. Na mmoja kati ya wanaume hao alikuwa ni Henry.
Henry baada ya kuuona mwili ule alishtuka sana.

"Vipi, unamfahamu? Naona umeshtuka baada ya kumwona" mwanaume aliyeambatana nae akamuuliza Henry

"Aa.. amna, hata simfahamu ndio kwanza namwona leo. Kwani vipi?" Henry akajitetea akijaribu kujiweka sawa.

"Kumbe tuliyetumwa kumchukua ni Daniel Mwaseba! Daaah! Kama ningejua ni yeye ningemtaarifu mapema. Sijui nifanyaje hapa na wanaweza kunigundua kama nafahamiana nae" Henry alikuwa anawaza peke yake. Alikumbuka usiku wa jana kabla Daniel Mwaseba na wenzake hawajaachana naye alipatiwa karatasi yenye namba ya simu

"Chukua namba zangu. Ukipata chochote tutafahamishana." aliyakumbuka maneno haya, aliambiwa na Daniel usiku kabla ya kurudishwa na gari.

"Unawaza nini? Hebu tumwinue tunasubiriwa juu" Henry alishtuliwa na mwenzake kutoka kwenye dimbwi la mawazo. Bila kuchelewa wakashirikiana kuunyanyua mwili huo na kurejea nao barabarani, walipofika barabarani walikuta Noah Nyeusi imepaki pembezoni mwa barabara ikiwasubiri. Bila kuchelewa wakauingiza mwili wa Daniel Mwaseba ndani ya buti, wakaingia ndani ya Noah ile na kuondoka nayo.
-----------------------

Gilbert Mwaitika, Elizabeth Neville, Mwanasheria Mlevi pamoja na mwanadada aitwaye Cara walikuwa wakimsubiri Daniel Mwaseba kwa hamu kubwa. Hii ilikuwa ni baada ya David kuufungua mdomo wake punde tu baada ya kuzinduka. Wote walihamia nyumbani kwa Dokta Yusha baada ya kuitwa na Gilbert Mwaitika.
David hakuficha kitu, aliwaeleza jinsi alivyoitwa na mpambe wa Mheshimiwa Eliud Sumbi siku moja kabla ya ziara ya rais kufanyika. David aliwaeleza jinsi alivyokutanishwa na mheshimiwa Eliud Sumbi na kupatiwa mpango wa kubadili helikopta.

Siku ile ilikuwa hivi...
Baada ya David kuonana na mheshimiwa Eliud Sumbi, Siku hiyo walizungumza kwa takribani nusu saa na baada ya kuukubali mpango wa mheshimiwa Eliud, David alipatiwa dawa ya usingizi na Elton Tonny.

"Dawa hii utaipulizia kesho ndani ya Helikopta yenu nusu saa kabla ya kuingia. Baada ya hapo, muda ukifika wa kuirusha helikopta angani hakikisha wenzako ndio wanaanza kuingia ndani. Wakishaingia na kuvuta pumzi haitawachukua muda, watadondoka chini kama maembe machanga yaliyozidiwa na upepo" Elton Tonny alisema

"Watakufa?" David aliuliza baada ya kupatiwa dawa hiyo

"Hapana. Watapata usingizi mzito ambao hauamshiki hadi masaa thelathini na sita yapite. Wewe usiingie ndani hadi zipite tena dakika kumi na tano. Baada ya hapo utaingia, nawe utasinzia lakini ni kwa masaa manne tu ndipo utarejewa na fahamu. Ukisharejewa na fahamu utajifanya kutoa ripoti huelewi ni kitu gani kinaendelea. Na wakati huo sisi tutakuwa tumeshaimaliza kazi yetu. Kuhusu Helikopta ondoa shaka maana wakati huo tutairusha helikopta ya kufanana na yenu ili iwe rahisi kwa kazi yetu kukamilika"
David alipotaka kujua ni kazi gani aliambiwa atulie hadi itakapokamilika ndipo atajuzwa.

Na hivyo ndivyo ilivyokuwa, wote wakaridhika na maelezo ya David, japokuwa walimwonea sana huruma kwani tayari alikuwa ni msaliti.

TUKUTANE TENA KESHO SAA 12 JIONI.

NOTE: Kama utauhitaji msimu huu wa nne utaupata jwa gharama ndogo tu ya Tshs 1000 tu. Lipia kwenda M pesa namba 0765824715 au TigoPesa namba 0678824073 kisha njoo whatsapp kwa namba 0621249611 nikutumie. Wale wengine tutaendelea kuisoma hapahapa kila ninapopata nafasi ya kuiweka.
Msimu wa Tano ndio msimu wa mwisho wa Riwaya hii, utaanza kupatikana kesho mchana kwa Tshs 700 tu
 
Back
Top Bottom