gilbert35
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 247
- 474
Riwaya: Anga ya Washenzi
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
Phone: 0765824715.
Msimu wa Kwanza, Sehemu ya 01
SURA YA KWANZA
Jumatatu Tar 07/04/2022, Saa 04:00 Asubuhi.
Hali ya hewa ilikuwa ni ya baridi sana katika mji wa Moshi, maelfu ya watu walikusanyika katika uwanja wa chuo kikuu cha ushirika Moshi, kila mmoja alikuwa ndani ya makoti pamoja na masweta mazito kutokana na baridi kuwa kali. Kila mtu alikuwa makini kusikiliza Rais Mark anawaambia nini. Rais Mark alikuwa katika ziara yake ya kwanza kabisa tangu mwaka mpya wa 2022 uanze, na katika ziara hiyo mji wa Moshi ulibahatika kuanza mwaka na rais Mark. Maelfu ya watu waliokusanyika katika kiwanja hicho walikuwa bize kusikiliza maneno ya rais wao kipenzi, vyombo vya ulinzi na usalama navyo havikuwa nyuma, vilikuwa vikifuatilia kwa karibu kila tukio, huku helikopta ya jeshi la polisi nayo ikizidi kupiga ruti angani kuhakikisha usalama unakuwepo kwa asilimia zote.
Daniel Mwaseba alikuwa ni mmoja kati ya watu waliokuwa bize kufuatilia kwa karibu kila tukio lililokuwa likiendelea. Yeye ni mpelelezi nambari moja Nchini Tanzania na kipenzi cha wengi ndani na nje ya nchi hii. Yeye pamoja na timu mahususi kutoka idara ya usalama wa taifa walikuwa ndani na nje ya uwanja wa Ushirika, na jukumu lao kubwa lilikuwa ni kuhakikisha Rais wa nchi anamaliza ziara yake salama katika mji huu wa Wachaga. Muda wote macho ya Daniel hayakutulia sehemu moja, alikuwa akiyazungusha macho yake kila kona, aliyapeleka kaskazini, sekunde hiyohiyo akayapeleka kusini, akayatupia magharibi na hata mashariki aliyapeleka macho yake ilimradi tu kuhakikisha usalama unakuwepo katika viwanja hivi vya chuo kikuu cha ushirika Moshi. Katika sikio lake la kushoto Daniel alipachika kifaa maalumu ambacho kilimsaidia kuwasiliana na wenzake wakati wowote, katika mkono wake wa kulia alikuwa ameshikilia vyema miwani ya shetani iliyokuwa na uwezo wa kuona tukio lolote la mbali. Daniel Mwaseba alikuwa amesimama pembeni kidogo ya jukwaa walilokalia viongozi wa kidini.
Daniel Mwaseba aliyapepesa macho yake kwa sekunde tano tu kila kona, lakini hakuona tukio lolote la ajabu linaloweza kuathiri usalama wa ziara ile, sekunde ya sita akayahamishia macho yake hadi mbele kabisa aliposimama mheshimiwa rais Mark. Rais alikuwa bado anawahutubia wananchi.
Sekunde ya saba Daniel akayapeleka macho yake upande wa mkono wa kushoto wa rais Mark, upande huo waliketi viongozi mbalimbali wa serikali.
Macho ya Daniel yalitua katika mikono ya makamu wa rais, mh Eliud Sumbi ambaye muda huo vidole vyake vilikuwa bize vikichezea simu yake. Vidole vyake vilikuwa vikibonyeza simu kwa kasi ya ajabu, kasi ambayo ilimshtua Daniel ambaye umakini uliongezeka zaidi ya awali, akili yake ilimtuma aendelee kutazama kunani hadi makamu wa rais aonekane kubonyeza simu kwa kasi ile tena wakati ambao yupo kwenye ziara, akaona hii si kawaida kwa viongozi wa serikali kufanya vile wakati kama huu. Daniel aliamua kuyaegesha macho yake palepale alipoketi mheshimiwa Eliud Sumbi. Alifundishwa kutopuuzia jambo lolote akiwa mafunzoni miaka kadhaa iliyopita. Alifahamu fika kwenye ulimwengu wa kipelelezi hakupaswa kupuuzia jambo lolote ambalo linaweza kuwa la kijinga au dogo kwa mtu wa kawaida, na kila atakaloliona katika ulimwengu huu basi ni lazima liwe na matokeo chanya ama hasi.
Mheshimiwa Eliud Sumbi ambaye ni Makamu wa rais wa Tanzania alikuwa akiuchakata ujumbe katika simu yake. Kwa namna alivyokuwa akiuchakata ujumbe ule ilionekana wazi alikuwa na lengo la kuufikisha ujumbe huo haraka sehemu husika. Alipomaliza kubofya simu yake alipepesa macho yake kulia na kushoto, kulia kwake aliketi Waziri wa ulinzi Dk Edward Bavu, na upande wake wa kushoto aliketi waziri wa michezo Dk Janeth Julius. Aliwaona mawaziri hawa wapo bize kusikiliza mheshimiwa Rais anasema nini. Alipepesa tena macho yake mbele na nyuma yake, na hapo akayahamisha macho yake hadi juu ya jengo moja la ghorofa lililopo karibu mita Mia Tano kutoka alipo. Ghorofa ile ilikuwa ni hoteli maarufu inayoitwa Five star Hotel. Macho ya Eliud Sumbi yalitazama juu ya hoteli ile kwa sekunde tatu ndipo akaiweka simu yake katika mfuko wake wa koti la suti.
Daniel Mwaseba hakuwa nyuma, alikuwa bize akiyafuatilia macho ya Makamu wa rais kila yanapotazama, alimwona mheshimiwa makamu wa Rais akitazama upande wake wa kushoto, akamwona pia akitazama kulia, Daniel naye akatazama hukohuko alipotazama mheshimiwa Eliud Sumbi. Alipoyapeleka macho yake katika kilele cha hoteli ya Five Star, Daniel naye aliyapeleka macho yake huko pia, na hapo ndipo hisia zake zilizaa matunda, Hisia mbaya za kumtilia shaka mheshimiwa Eliud Sumbi kutokana na ubonyezaji wake wa simu wenye kutia wasiwasi, tena wakati ambao ziara ya Mkuu wa nchi ikiendelea.
Juu kabisa ya Ghorofa, Five Star Hotel Daniel Mwaseba alifanikiwa kuona kivuli kikijisogeza taratibu, Ilihitaji macho ya mwewe kugundua juu ya ghorofa kuna kivuli, lakini macho ya Daniel yaliweza kugundua juu ya ghorofa kuna kivuli kikijisogeza karibu, na yalifanikiwa pia kuuona mkono wa binadamu ukijichomoza taratibu.
"Daniel kama unanipata, angalia kwa makini angani, itazame ile helikopta inayoimarisha ulinzi angani. Mbona kama si ile iliyopangiwa? Hii kama rangi yake ya kijani imepoa sana" Sauti ilisikika kutoka kisikilizio kilichopachikwa katika sikio la Daniel
"Nam Elizabeth Neville, upo upande gani kwani?" Daniel aliachia swali huku mkono mmoja ukigusa kisikilizio kile, macho yake yalikuwa bado yakitazama palepale juu ya jengo la Five Star hotel. Kwa haraka aliyarudisha macho yake pale alipoketi Makamu wa Rais, alimwona mheshimiwa Eliud Sumbi akitazama saa yake ya mkononi. Daniel Mwaseba aliyarudisha tena macho yake kwa kasi hadi juu ya jengo la hoteli ya Five star. Sasa alimshuhudia mdunguaji aliyelala mithili ya nyoka akiiseti bunduki ya masafa marefu.
"Nipo hema la kusini Daniel, jaribu kuwasiliana na Chifu ameketi na jenerali Evance, amuulize Jenerali ili nasi tuweze kufahamu kama ana taarifa yoyote ya kubadilishwa kwa helikopta maana hii inashangaza, kiusalama si kawaida. Najiuliza kwanini wameweza kuibadilisha bila sisi kujulishwa, nina uhakika wamebadilisha helikopta maana hii ni tofauti na ile ya kwanza tuliyoiona" Sauti ya kike ilisikika ikieleza kupitia kisikilizio alichopachika Daniel katika sikio lake.
"Elizabeth Neville! Kumekucha" Aliropoka Daniel. Aliiona hatari inayokwenda kutokea.
"Kama juu ya hoteli ile kuna mdunguaji na angani kuna helikopta ambayo si ile tuliyofahamishwa jana, ina maana walio ndani ya helikopta hawamwoni mdunguaji? Hapa kuna mchezo unaendelea, Rais Mark ana maadui wengi kwa sasa na nisipokuwa makini atauwawa" alijisemea Daniel huku akipiga hatua za haraka haraka kuelekea alipoketi Chifu Abdallah Ntenga ambaye ni Mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa
"Daniel kuna nini? Nifahamishe Daniel kama nakupata" Sauti ya Elizabeth Neville ilipenya kupitia kisikilizio kile na kutua katika sikio la Daniel Mwaseba
"Kuna tatizo Elizabeth, nadhani kuna tukio limepangwa kutokea hapa, siwezi kukuambia moja kwa moja ni nini lakini tambua hii ziara ipo kwenye hatari. Sasa hivi ninaelekea alipo chifu, niambie upo wapi Elizabeth" alisema Daniel huku akizipiga hatua zake kuelekea alipo chifu Abdallah Ntenga.
"Daniel mimi nipo huku nje ya uwanja kabisa, nakuja huko ndani sasa hivi" alisema Elizabeth Neville, wakati huo Daniel Mwaseba alishafika karibu na sehemu alipoketi chifu Abdallah Ntenga. Chifu alikuwa ameketi pamoja na mkuu wa majeshi ya Tanzania, jenerali Evance, pamoja pia na mkuu wa jeshi la polisi, IGP Kilazi. Alipokaribia alimpa ishara Chifu na palepale alinyanyuka na kumfuata.
"Kuna jambo halipo sawa Chifu, helikopta inayoranda juu ni tofauti na ile tuliyoiona mwanzoni, ulipewa taarifa juu ya kubadilishwa kwake?" aliuliza Daniel. Chifu alionekana kushtuka sana
"Unasemaje Daniel! Wamebadili helikopta? Kivipi wabadili helikopta bila kutufahamisha? Ile nyingine tuliyoiona jana ikifanyiwa majaribio imepata dharura gani?" aliuliza Chifu katika hali ya kushangaa kwani haikuwa kawaida kubadilishwa baadhi ya mambo ya kiusalama bila wao kujulishwa kwanza. Wakiwa bado wamesimama palepale mlio wa helikopta ulisikika kwa mbali, wote kwa pamoja wakainua vichwa vyao angani kuitazama helikopta ile. Chifu alipeleka mkono wake mdomoni, Daniel naye alionekana kushika kichwa chake.
"Mungu wangu...! Si yenyewe hii" alisema Chifu
Kuna nini nyuma ya pazia?
Tuwe wote kesho tena panapo uhai