RIWAYA: Anga ya Washenzi na Gilbert Evarist Mushi

RIWAYA: Anga ya Washenzi na Gilbert Evarist Mushi

Riwaya: Anga ya Washenzi
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
Phone: 0765824715.

Msimu wa Pili.
Sehemu ya 04

"Mkuu tupo kwenye hatari ya kukamatwa. Nasikia kwa mbali sauti za magari zikijongea, bila shaka wanatutafuta" Mmoja kati ya wanaume wale, aliyeonekana ndiye kiongozi alipiga simu na kuwasiliana na Mheshimiwa Eliud Sumbi ambaye ni makamu wa rais.
Alipatiwa maelekezo mafupi sana na kisha kukata simu ile. Aliyepiga simu anaitwa Henry, Na ndiye kiongozi wa wenzake. Yeye alikuwa ametangulia mbele kidogo na kuwaacha wenzake wawili pamoja na David hatua moja tu. Aliwasimamisha wenzake huku akiirejesha simu yake mfukoni na kuchomoa bastola yake ndogo.

"Mkuu amenipatia maelekezo ni kitu gani cha kufanya. Tunapaswa kuwa na maamuzi magumu mno ili tuweze kuondoka eneo hili tukiwa salama. Maamuzi hayo ni haya amesema,"

Mwanaume yule alizungumza huku akiikoki bastola ile baada ya kuichomoa kutoka kiunoni, haraka sana aliwapiga risasi za kichwa wenzake wawili. Alipouelekeza mkono wake kwa David, haraka sana David alimrukia kama nyani hali iliyopelekea bastola ile kudondokea chini. Walianguka wote chini na kuanza kukunjana kama mafahali wawili huku kila mmoja akijitahidi kuutetea uhai wake. Wanaume wengine wawili waliopigwa risasi za kichwa walipoteza maisha palepale bila kutoa hata sauti. Walikufa kifo cha ghafla sana, na aliyeamua iwe hivyo ni Mheshimiwa Eliud Sumbi baada ya kumtaka kijana aliyepiga simu kuwateketeza wenzake pamoja na David ili kuilinda siri. Aliona ni heri wafe ili mmoja atakayebaki iwe rahisi kwake kutoroka kuliko kutoroka eneo lile wakiwa pamoja.
David alijitahidi sana kupambana na mwanaume yule lakini hakuwa na ujanja zaidi kutokana na mikono yake kufungwa na pingu. Alichukuliwa kama mhalifu pale kambini hivyo alikuwa bado kifungoni. Mwanaume yule baada ya kumzidi nguvu David, alichomoa kisu chake na kukikita mara tatu katika tumbo la David. Akanyanyuka haraka na kumshindilia David mateke mazito ya tumbo. Baada ya kuridhika haraka sana aliisogelea miili ya wenzake na kuchomoa kila kitu ikiwemo Simu zao pamoja na waleti. Ni vitambulisho tu aliviacha pale ikiwemo na chake walivyovitumia kama utambulisho wao wakati wakiingia katika kambi ile. Baada ya kujiridhisha alianza kukimbia ili kutoka eneo lile kwani Wanajeshi walikuwa karibu sana kufika pale.

"Milio ya risasi imesikika kutoka upande huu. Twende huku." Daniel akiongozana na mwanajeshi mmoja walikuwa wakizidi kuzama katikati ya miti iliyosongamana. Nao waliisikia milio ya risasi, hivyo walikuwa wakielekea hukohuko. Ndani ya muda mfupi tu wanajeshi karibu kumi na tatu wakalizunguka eneo ambalo walilihisi ndilo eneo uliposikika mlio wa risasi. Walianza kulisogelea eneo lile na hatimaye waliona miili mitatu chini isiyokuwa na dalili ya uhai.
Daniel Mwaseba, Gilbert Mwaitika pamoja na mwanajeshi mmoja walishirikiana kuikagua miili ile na waligundua mtu mmoja kati ya wale watatu ndiye aliyewaangamiza wenzake na yeye kukimbia ili kuuficha ushahidi. Lakini pia waligundua mwili mmoja kati ya ile mitatu ulikuwa bado unapumua. Na mwili huo ulikuwa ni wa David. Kisu alichokitwa nacho David katika tumbo lake hakikuweza kuuondoa uhai wake, na hii ilimpa tabasamu la mbali Daniel kwani alijua lazima David awe na kitu cha kuwasaidia. Juu ya mwili mmoja kulikuwa na vitambulisho vitatu. Ni vile vya maofisa kutoka usalama wa taifa vilivyokuwa vikitumika kufanyia uhalifu.
Daniel Mwaseba alivichukua na kuviweka mfukoni.

"Mmoja bado yupo ndani ya msitu huu,tena hayupo mbali nasi. Ufanyike msako wa nguvu haraka sana akamatwe aletwe kambini" Mwanajeshi aliyekuwa pembeni ya Daniel aliamuru. Palepale msako hatari ulianza huku wanajeshi wawili wakisaidiana na kina Daniel kuibeba miili ile na kuipeleka kwenye gari. David naye alibebwa na kupelekwa kwenye gari ili kuwahishwa hospitalini kwa matibabu zaidi.

"Swala la David kuwa hai linahitaji usiri mkubwa sana. Akijulikana yupo hai bado watataka kumuua maana analo jambo nyeti sana kifuani pake ambalo hawataki atuambie." Daniel Mwaseba alisema kwa sauti ya chini akiwaambia wanajeshi watatu waliokuwa wakisaidiana kuipeleka ile miili isiyokuwa na uhai kwenye gari

Hatua nane kutoka pale walipokuwa kina Daniel kulikuwa na kichaka kidogo kilichozungukwa na majani mabichi. Ndani ya kichaka kile kulikuwa na macho mawili yakiwatazama kina Daniel kwa umakini mkubwa sana. Alikuwa ni Henry, mwanaume yule aliyewateketeza wenzake. Baada ya kuona ni vigumu kukimbia alifukua ardhini na kutengeneza shimo pana na kuchuchumaa kisha kujifukia na kubakisha kichwa tu. Kichwa hicho kilifunikwa na majani makavu pamoja na mabichi yaliyotengeneza mfano wa taswira ya kichaka. Na hiyo ilikuwa ni mbinu iliyomnusuru kukamatwa. Lakini kwa bahati mbaya zaidi, taarifa ya David kuwa hai, mwanaume huyu aliisikia kwa masikio yake mawili kutoka katika kinywa cha Daniel Mwaseba.
Msako ulikuwa mkali, lakini ukali huo haukufanikisha kumnasa mtu huyo. Wanajeshi wale walitafuta na hatimaye kukata tamaa baada ya kutoambulia chochote. Mtafutwaji alitumia akili kubwa sana katika namna ya kujificha kwani hakuwa ametoka pale alipojifukia. Kila kilichokuwa kikiendelea alikiona na kukisikia pia. Hivyo hadi magharibi ya jua inaanza kuingia wanajeshi walianza kurejea kambini na kumpatia mwanaume yule nafasi ya kuuacha msitu.

"Wamemsaka yule mmoja bila mafanikio yoyote. Hawajampata kabisa" Gilbert Mwaitika akamwambia Daniel Mwaseba. Hii ni baada ya Gilbert kupigiwa simu kutoka kambi ya jeshi Njiro na kuelezwa kilichojiri.
Walikuwa wakiiacha barabara ya Majengo na kuelekea maeneo ya stesheni walipoweka kambi. Na huko Majengo walipokuwa wakitoka ni nyumbani kwa Dokta Yusha baada ya ombi la kumtibu David kwa usiri bila kufahamika kama yupo hai. Dokta Yusha aliwakubalia na kuwataka wampeleke nyumbani kwake.

"Kwa namna tulivyokuwa tumelizunguka eneo lile ilikuwa ni vigumu kwa yeye kutoka. Bila shaka alijificha kwa namna ambayo bila kuufikirisha ubongo asingeweza kuonekana. Labda juu ya miti, au alijifananisha na majani kwa kujifunika nayo." Daniel alisema huku akitoa ishara ya kuchepukia kushoto kwa kuwasha taa ya gari. Walikuwa wakiingia Moshi Mjini, maeneo ya stesheni ya treni.

"Ila bado hatujamkosa. Katika ofisi ya kanali kunayo kamera ya siri. Hivyo tunaweza kuwasiliana na Kanali kule kambini akatupatia picha" Gilbert akasema kwa uhakika. Wakati huo giza lilikuwa likiukimbiza mwangaza wa jua na walishafika kambini. Walichokuwa wakisubiri ni kufunguliwa geti baada ya kupiga honi. Muda mchache geti likafunguliwa na Elizabeth Neville, wakaingia baada ya kuhakikisha hakuna mtu yoyote aliyekuwa akiwafwatilia nyuma.
Daniel Mwaseba alipitiliza moja kwa moja hadi ndani ya chumba kidogo alichofungiwa Ochewa. Mbali na kupoteza fahamu lakini alifungwa kisawasawa kiasi kwamba ilikuwa ni ngumu kufurukuta pindi fahamu zitakapomrejea. Daniel akaufungua mlango taratibu kabisa na kwenda hadi katika kiti cha chuma alichofungiwa Ochewa kwa kukalishwa kitako. Kamba zilikuwa zimelizunguka tumbo na kifua chake na kufungwa kwa nyuma. Mikono yake miwili nayo ilipelekwa nyuma na kukutanishwa kisha kufungwa na kamba pia. Hii ni namna tu ambayo aliweza kufungwa. Daniel alijisogeza taratibu hadi karibu kabisa na pale alipofungwa Ochewa. Ndani ya chumba mwanga mkali uliangaza vyema na kufanya kila kitu kionekane vyema, ndani ya chumba hakukuwa na chochote cha ziada. Daniel alikuwa akimtazama Ochewa Owechi aliyekuwa amejiinamia kwenye kiti akiwa ametopea usingizini. Tangu ashambuliwe wakati ule hakuwa bado amerejewa na fahamu. Daniel aliupeleka mkono wake wa kulia kinywani ya kuyagusa meno yake mawili ya mbele. Yalikuwa yakimletea maumivu makali sana.

"Ulitaka kuyang'oa siyo? Pumzika kwanza ukusanye nguvu ya kuvumilia hapo baadae" Daniel alisema kwa sauti ya chini.
Aliuingiza mkono wake mfukoni na kuchomoa kalamu ya kuandikia. Taratibu akawa anaupeleka mkono wake kuelekea katika sikio la Ochewa. Lengo la Daniel kufanya vile ilikuwa ni kutaka kujihakikishia kama ni kweli Ochewa hakuwa amezinduka. Na kweli alipojaribu kumchokoza sikioni kwa ncha ya kalamu ile, Ochewa hakujigusa. Hii ilimwaminisha Daniel Mwaseba ya kuwa bado.

"Unahitaji kumzindua?" Sauti laini ya kike ilisikika nyuma ya Daniel Mwaseba. Alikuwa ni mkewe, Elizabeth Neville. Elizabeth alitembea taratibu hadi katika mgongo wake na kumkombatia kwa kuipeleka mikono katika kifua chake. Walikuwa ni mume na mke wanaopendana sana. Na uhusiano wao ulianza pindi walipokutana katika mkasa mzito uliohusisha upotevu wa nyaraka za siri ndani ya serikali.

"Come on mine." Daniel akasema kwa hisia kali. Akamgeukia Elizabeth Neville na kuzifakamia lipsi zake.

"Acha Daniel, tutaoneka" Elizabeth akasihi akijitahidi kujitoa mikononi mwa Daniel.

"Nimekuita huku kwani?" Daniel akazidi kumng'ang'ania Elizabeth, na taratibu Elizabeth akaanza kutoa ushirikiano ipasavyo.

"Hata hivyo nimekumisi sana D. Hizi kazi zinatufanya tuwe mbali mara nyingi, hadi napaliwa na kiu eti" Elizabeth akaanza kudeka. Mbali na ukomandoo aliokuwa nao lakini ni mkate mlaini kwa chai. Na chai hiyo ni mumewe kipenzi.

"Mh Mh" mara sauti ya mtu akijikohoza kuweka koho lake sawa ikasikika kutokea nyuma yao. Alikuwa ni Gilbert Mwaitika. "Samahanini kwa kuingia ghafla" alisihi.
"Daniel nimeongea na yule Kanali, ameniambia kamera imenasa tu migongo yao. Bila shaka nao walikuwa wanatambua katika ofisi ile kulikuwa na kamera" Gilbert Mwaitika akasema.

"Uuuuh! Hakuna namna. Inabidi tumlinde David kwa gharama yoyote ile hadi atakapopona. Yeye anafahamu kitu. Elizabeth waite kina Cara ukumbini tujadiliane kwanza baadhi ya mambo" Daniel akatoa pumzi ndefu na kusema.
Wote wakaelekea katika ukumbi mdogo mle ndani uliofaa kuwa sebule yao ya muda. Na baada ya dakika kadhaa waliungana wote kwa pamoja na kuzungumza.

Huu ni Msimu wa Pili. Hii ni Anga ya Washenzi. Mwandishi wako ni Gilbert. Msimu wa pili bado unapatikana kwa Tshs 1000 tu. Lipa kwenda M pesa namba 0765824715 kisha njoo whatsapp kwa namba 0621249611 nikutumie. Kama huna whatsapp nitext hata messenger hapa hapa fb nitakutumia. Wengine tukutane Alhamisi
 
Riwaya: Anga ya Washenzi
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
Phone: 0765824715.

Msimu wa Pili. Sehemu ya 05
Wote wakaelekea katika ukumbi mdogo mle ndani uliofaa kuwa sebule yao ya muda. Na baada ya dakika kadhaa waliungana wote kwa pamoja na kuzungumza.

"Hatimaye David yupo katika mikono yetu, lakini hali yake ni mbaya sana, hivyo hali yake itakapotengamaa anaweza akatuambia kila kitu anachokifahamu. Pia tunaye Ochewa Owechi kama hati yake ya kusafiria inavyoeleza. Jukumu letu ni kufahamu ni kitu gani kimemleta hapa Tanzania kutoka kwao Kenya. Haitakuwa kazi rahisi kumfanya aseme, lakini kwa kuwa nia tunayo na uwezo tunao basi atasema. Pia tunapaswa kuzifwatilia nyendo za Makamu wa rais, Mheshimiwa Eliud Sumbi kuanzia sasa, maana kwenye hili sakata nina mashaka naye sana kutokana na vitu alivyokuwa akivifanya pale ziarani. Hii kazi ni ngumu sana, lakini ni nyepesi pia kama tutashirikiana vyema." Daniel alianza kusema.

"Kufwatilia nyendo za Mheshimiwa Eliud Sumbi ni jambo la hatari sana, linahitaji umakini wa hali ya juu maana kama akigundua tunamchunguza inaweza kuwa hatari kwetu. Yeye ni mtu mkubwa sana Daniel. Tufanyaje?" Gilbert akasema.
Wote wakamtazama Daniel kumsubiri atie neno

"Tunaye Elizabeth Neville, tunaye pia Cara. Mnaonaje kama mmoja wao akabeba jukumu la kumfwatilia mheshimiwa? Kuhusu namna atakayoitumia sifahamu, lakini njia pekee na rahisi kumnasa Mheshimiwa ni hii" Mwanasheria Mlevi alisema. Ukumbi mzima ukamtazama Daniel na kisha Elizabeth Neville. Ni kama vile Elizabeth alikuwa akipigiwa chapuo kuifanya kazi hiyo. Daniel naye akamtazama Elizabeth na kuachia tabasamu.

"Nitalibeba jukumu hilo mimi. " Elizabeth Neville akasema kwa uhakika. Na alisema baada ya kuona Daniel akitabasamu.

"Songelael na mimi tutadili na Ochewa, tutahakikisha anatuambia hata visivyoambilika." Daniel akasema. Mwanasheria Mlevi naye akaunga mkono.

"Vipi kuhusu sisi?" aliuliza Cara, akimaanisha yeye na Gilbert hawakuwa katika orodha ya majukumu.

"Nyie ni kama nguvu kazi yetu, mna umuhimu sana kwetu. Mtakuwa mnacheza pande zote, kwetu na kwa Elizabeth kutegemeana na hali ya wakati husika" Daniel alisema. Wote kwa pamoja wakakubaliana.
Haraka sana Cara aliwahi kwenye jokofu na kutoa mvinyo. Akautia katika glasi tano zilizokuwa juu ya jokofu lile. Akasaidiana na Elizabeth Neville kuzisambaza kwa wote. Na kila mtu alipata glasi yake iliyotiwa mvinyo tayari.

"Sisi ni ndugu" Daniel akasema akigongelesha glasi yake na ya Mwanasheria Mlevi.

"Umoja wetu ndiyo ushindi wetu siku zote" Mwanasheria akajibu huku akigongelesha glasi yake na ya Elizabeth Neville.

"Kama ni kufa tutakufa pamoja katika kazi hii" Elizabeth akasema huku akizigonganisha glasi yake na ya Gilbert Mwaitika na ya Cara kwa pamoja.
Daniel akainyanyua glasi yake juu, usawa wa kichwa chake. Nao wakazinyanyua zao kama alivyofanya Daniel. Taratibu wakazishusha na kuzipeleka vinywani mwao kwa pamoja na kuumimina mvinyo. .
Walielewana. Walikuwa tayari kwa lolote, kwa chochote.
******

Majira ya Saa Tano usiku Elton Tonny ambaye ni mpambe wa makamu wa rais, Mheshimiwa Eliud Sumbi, aliisimamisha gari yake katika viwanja vya hoteli ya Kili Night. Akaufungua mlango wa gari na kushuka. Upande wa kushoto wa dereva napo mlango ulifunguka. Akashuka Henry, mwanaume aliyewateketeza wenzake katika kambi ya jeshi Njiro. Henry alifanikiwa kutoka salama katika eneo lile na kumpigia simu Elton Tonny aende kumchukua.

"Sijui mheshimiwa atasema nini. Sikufichi Henry, ila nakuambia ukweli utakuwa umefanya uzembe mkubwa sana kama ikithibitika ni kweli David yupo hai. David atatapika kila kitu nakuambia. Ataanika yote. Twende tukamsikilize kwanza Mheshimiwa atasema nini" Elton Tonny alisema huku akipiga hatua kubwa kubwa kuingia ndani ya hoteli. Nyuma yake alikuwa ameambatana na Henry.

Henry hakuwa amejibu chochote, alikuwa akimfuata Elton Tonny nyuma yake wakizidi kuzama ndani ya hoteli. Walichukua lifti na kupanda juu kuelekea ghorofa ya tisa ambayo Makamu wa rais alikuwa humo. Henry muda wote alikuwa akiwaza ni namna gani ataeleweka mbele ya Mheshimiwa Eliud Sumbi. Alijua wazi kabisa uzembe alioufanya ulikuwa ni wa kiwango cha lami. Uzembe ambao haukustahili kuvumilika.

"Sijui atasema nini! Nitaomba nafasi ya mwisho, na nikikubaliwa naahidi kumnyonga David kwa mikono yangu ndani ya siku mbili tu, nitakuwa nishampata" Henry alikuwa akiwaza peke yake wakati lifti ikizidi kuwapandisha juu.
Mlango wa lifti ukafunguka, wakatoka na kukamata njia ndefu kuelekea katika ukumbi mdogo, mahali alipo Mheshimiwa Eliud Sumbi. Ulinzi ulikuwa ni mkubwa sana, kila kona kulikuwa na walinzi kutoka serikalini kwani Kiongozi mkubwa wa nchi, Makamu wa rais alikuwa pale.
Walifika katika mlango wa ukumbi. Pale mlangoni walisimama walinzi wawili waliovalia suti nyeusi. Kwa vile Elton Tonny pamoja na Henry walikuwa wakifahamika basi waliingia ndani bila kizuizi chochote. Mheshimiwa Eliud Sumbi alikuwa ameketi kwenye kochi huku mabinti wadogo warembo wakimsindikiza kwa kuushikashika mwili wake sehemu mbalimbali. Mkononi alishikilia glasi iliyo na mvinyo huku mbele yake kuna meza kubwa iliyobebelea chupa ya mvinyo yenye chapa ya jina 'Jim Beam Bourbon'
Mheshimiwa Eliud Sumbi alikuwa ni mpenda starehe sana. Starehe yake kubwa mbali na ulevi, wanawake pia.
Alipomwona Elton Tonny akiwa pamoja na Henry, akawapa ishara ya kuondoka mabinti wale, ili wasiweze kufahamu kinachoendelea.

"Hawajakutia machoni?" Mheshimiwa Eliud Sumbi alianza na swali akimtazama Henry, kijana pekee aliyerejea katika wanaume watatu waliokuwa wameelekea Njiro kumchukua David. Aliwateketeza wenzake kwa kutumia bastola yake mwenyewe.

"Hapana Mkuu. Hawajaniona kabisa." Henry akajibu kwa uthabiti wa kutosha.

"Umehakikisha David hapumui?" Henry alionyesha mshtuko dhahiri baada ya Kuulizwa swali hili. Mheshimiwa Eliud Sumbi aliuliza akimtazama Henry machoni. Henry aliyashusha magoti yake haraka hadi sakafuni. Kama ungemwona basi ungemwonea huruma kwa namna alivyokuwa akitetemeka.

"Mkuu nilimshambulia ipasavyo, wakati wanakuja nilikimbia kujificha na kumwacha katika hali ambayo hawezi kupona. Nilimsikia mmoja wao akiwaambia wenzake bado yupo hai. Nakuomba mkuu nipe nafasi nikammalize kama atakuwa bado yupo hai." Henry alisema kwa unyenyekevu mkubwa sana. Alisema huku akiwa amekiinamisha kichwa chake na kukitua juu ya sakafu. Akahisi mkono wa mheshimiwa ukimgusa katika mgongo wake na kumsihi anyanyuke.

"Henry tambua uhai wa mwanao upo mikononi mwangu, Sihitaji uzembe tena utokee. Hadi kesho saa sita mchana hakikisha David havuti pumzi hii ninayovuta mimi na wewe. Na kama atakuwa anavuta pumzi hii basi hakikisha wewe hauivuti mda huo." Mheshimiwa Makamu wa rais alisema kwa kumaanisha.

ITAENDELEA

Henry atafanikiwa kummaliza David aliya tayari mikononi mwa kina Daniel? Kwanini Mheshimiwa anamuambia David kwamba ameushika uhai wa mwanaye? Naam hii ni Anga ya Washenzi. Msimu wa Tatu upo tayari kwa wewe kuusoma. Lipia Tshs 1000 kwa ajili ya msimu wa 3 halafu mimi nitakupa na msimu wa pili bure uumalizie. Lipa kwenda M pesa namba 0765824715 kisha njoo whatsapp kwa namba 0621249611 nikutumie
 
[emoji91][emoji91][emoji91]
CapaEbook_1bd7c07c-b01e-461a-9c99-29550281f197_2.jpg
 
Hii kitu taam
 
Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
Riwaya: Anga ya Washenzi
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
Phone: 0765824715.

Msimu wa Pili.
Sehemu ya 06

"Henry tambua uhai wa mwanao upo mikononi mwangu, Sihitaji uzembe tena utokee. Hadi kesho saa sita mchana hakikisha David havuti pumzi hii ninayovuta mimi na wewe. Na kama atakuwa anavuta pumzi hii basi hakikisha wewe hauivuti mda huo." Mheshimiwa Makamu wa rais alisema kwa kumaanisha. Sauti yake ilikuwa ni amri tosha, amri iliyomfanya Henry kuhisi kama kuna msumari wa moto ukichoma kifuani pake.
_________________

Nje ya hoteli ya Kili Night, mita mia kutoka lango kuu la kuingilia hotelini ilipaki Harrier Hybrid nyeusi. Gari hii ilipaki jirani kabisa na mti mkubwa sana na sehemu hiyo giza lilikuwa kubwa kiasi kwamba ingemuwia mtu ugumu kugundua kama kuna gari pale. Ndani ya gari hiyo katika kiti cha dereva alikaa Gilbert Mwaitika huku pembeni yake akiwa Elizabeth Neville aliyekuwa akiangaza pale getini muda wote kwa kutumia miwani ya Shetani.
Elizabeth Neville alishaanza usiku huu kazi ya kuzifwatilia nyendo za Mheshimiwa Eliud Sumbi. Kwa vile yeye alikuwa ni askari mpelelezi basi ilikuwa ni rahisi kwake kujua mheshimiwa alikuwa wapi kwa wakati huu. Na baada tu ya kugundua Mheshimiwa alikuwa amepumzika ndani ya hoteli ya Kili Night alipanga kwenda usiku huohuo akiwa na Gilbert Mwaitika.

"Itatuchukua mda gani kuendelea kukaa hapa?" Gilbert akamuuliza Elizabeth baada ya kupita dakika mbili za ukimya tangu kufika pale.

"Lazima nijitahidi niingie ndani. Nikishaingia nitajifanya mimi ni muhudumu na nitafanya kila linalowezekana nikamhudumie mheshimiwa. Nikishakutana naye tu na akanitazama kwa macho yake mawili basi imekula kwake." Elizabeth alisema huku akimkabidhi Gilbert Mwaitika miwani ile ya kuangaza mbali.

"Hahaha, eti akikutazama tu imekula kwake. Unataka kuharibu usafi wa Daniel eti?" Gilbert akasema katika hali ya utani.

"Daniel mwenyewe anajua namsaliti. Hata hapa ambapo nipo na wewe nimeshamsaliti, na uzuri analitambua hilo" Elizabeth akajibu na kuachia tabasamu. Akajihakikishia ya kwamba yupo vyema, na kumwacha Gilbert Mwaitika ndani ya gari ile kisha kuzama ndani ya hoteli.
**********

"Daniel sogea uone." Cara aliita wakati anabofya vitufe vya tarakishi mpakato yake. Wakati huo Daniel Mwaseba akiwa na Mwanasheria Mlevi walikuwa wakiitazama saa ya Ochewa aliyovuliwa na Daniel kule hotelini.

"Ochewa Owechi. Jina lake halisi ni Festus Jabir Cosmas. Ni mzaliwa wa Kisii nchini Kenya, asili yake ni mkenya. Jamaa alikuwa ni jasusi wa kutumainiwa sana ndani ya shirika la kijasusi nchini Kenya. Tena cha kushangaza ni kwamba, mtandao wa kijasusi nchini humo ulishathibitisha kuwa Festus alishakufa." Cara alitulia kidogo na kuwatazama wenzake. Hii ilikuwa ni mpya kwa kila mtu. Daniel alishangazwa sana na maneno ya Cara.

"Alikufa kifo cha aina gani? Aliuwawa au alijifia mwenyewe?" Daniel akauliza

"Rest in peace Festus 1980-2020. Shirika la ujasusi pamoja na Serikali ya Kenya inafahamu ya kwamba Festus Jabir ni mfu tangu miaka miwili iliyopita. Kabla ya umauti kumkuta alishashiriki baadhi ya mauaji ya viongozi wakubwa nchini kenya na hata wafanya biashara wakubwa." Cara alizidi kueleza
" Unamkumbuka Tark Hajir yule mfanya biashara wa madini aliyekuwa ananunua madini ya Tanzanite kutoka Mererani na kwenda kuyauzia Kenya? Sasa ilibainika huyo aliuwawa baada ya kupigwa risasi na Ochewa. Na siku hiyohiyo Ochewa alishambuliwa na kuuwawa wakati akiyatekeleza mauaji ya mfanyabiashara huyo." Cara alisema huku akizidi kuichezea tarakishi yake.

"Umejuaje yote haya Cara?" Daniel aliuliza kwa kuhamaki.

"Hupaswi kuniuliza nimejuaje Daniel. Au mimi sistahili kuwa na uwezo kama wa Hannan?. Tunafaa tujiulize nini kimemleta nchini." Cara alijibu baada ya kumtazama Daniel Mwaseba kwa sekunde mbili machoni pake.

"Aisee wewe mwanamke noma sana. Yaani umeingia katika mtandao wa siri wa majasusi nchini kenya? Nilijua hii kazi anaweza kuifanya Hannan tu lakini kumbe nawe si haba, hongera sana" Mwanasheria akasema.

"Kwanza lazima tujue kwanini alisingiziwa kifo. Inaonekana kuna kitu nyuma yake, kifo chake kilitengenezwa kwa lengo fulani ili aendelee kutumika kwa siri. Halafu pia lazima tujue ni jambo gani limemleta hapa Tanzania na alikuwa na lengo la kumuua nani. Ngoja nikamwamshe atueleze" Daniel alisema akizipiga hatua zake kuelekea kwenye jokofu.
Basi Daniel akalifikia jokofu lile, akalifungua na kutoa chupa kubwa ya maji ya Kilimanjaro yenye ujazo wa lita moja na nusu. Na maji hayo yalikuwa na ubaridi sana kiasi kwamba yangekaa tena ndani ya jokofu angalau lisaa limoja tena yangetengeneza barafu.
Basi Daniel Mwaseba akayabeba maji yale na kuelekea nayo hadi katika chumba alichohifadhiwa Ochewa. Wakati huo meno yake mawili ya mbele yalikuwa bado yakimletea maumivu makali sana, ila tu alijikaza.

"Wakati umewadia kaka mkubwa.. Amka" Daniel alisema kwa sauti ya juu huku akimimina maji yale katika kichwa cha Ochewa Owechi. Ochewa alikurupuka kutoka katika usingizi mzito na kuanza kutetemeka. Maji yale yalikuwa ni makali sana kwa baridi. Mbaya zaidi tisheti aliyoivaa iliyafyonza maji yale na kumjengea ubaridi wa kudumu katika mwili wake

"Festus Jabir Cosmas." Daniel aliita. "Ni jambo gani limekuleta hapa Tanzania?" Mshtuko dhahiri ulionekana katika uso wa Ochewa baada ya Daniel kumwita kwa jina la Festus. Mbali na jitihada za kuuficha mshtuko ule lakini macho mawili ya Daniel Mwaseba yaliwahi kuuona.

"Kama wameshagundua jina langu halisi basi nimekwisha. Watu hawa ni hatari kwangu kuliko hata neno hatari, Lakini mbali na uhatari wao kamwe sitowaambia ukweli wowote ule, nitawatazama tu kama sijui chochote hadi tone la mwisho. Nipo tayari kwa lolote, kwa chochote"
Festus ama Ochewa alijisemea kifuani pake. Alikuwa akimtazama Daniel kwa jicho baya sana bila kumsemesha. Ingekuwa labda anamtazama mtoto anayelia hovyo kwa jicho hilo basi mtoto angeacha kulia mara moja; lakini Daniel hakuwa mtoto, aliliona jicho lile ni la kawaida sana kwake. Alishazoea kutazamwa na macho kama yale.

"Festus sina muda wa kubembelezana na wewe, nachohitaji ni wewe kuyajibu maswali yangu kwa usahihi. Ni jambo gani limekuleta hapa Tanzania?" Daniel aliuliza tena kwa mara ya pili. Lakini bado Festus hakusema chochote.

Danile alimwacha mle ndani na kutoka nje. Moja kwa moja alielekea hadi ukumbini na kumkuta Cara akiwa na Mwanasheria Mlevi wakiikagua ile saa aliyokuwa nayo Festus Jabir ama Ochewa Owechi.

"Cara kisanduku changu ulifanikiwa kuja nacho?" Daniel akauliza.

"Yeah, nilimpatia Elizabeth muda ule mlipoitwa na Chifu. Halafu Daniel kuna kitu nimekigundua kupitia hii saa. Tangu umvue jamaa mchana hadi sasa umeshabofya mahali popote kwenye hii saa? Alisema Cara na kisha kuachia swali. Mwanasheria Mlevi yeye alikuwa bize akiibofya ile tarakishi, alikiwa katika mtandao wa amazon akijaribu kutafuta saa kama ile.

"Hapana kwa kweli. Kwanini umeuliza hivyo Cara?"

"Unajua nini Daniel! Hii saa imewekewa GPS track, na ili huu mfumo ufanye kazi ni lazima kwanza batani yoyote iwe imebonyezwa. Festus alikuwa akiitumia saa hii katika mawasiliano na pia ilikuwa ni kama ishara kwake ya kuonyesha mahali alipo" Cara akaeleza

"Lakini tulimkuta pia na Chip ndogo katika kiatu chake. Ina maana kulikuwa na vitu viwili vinavyoonyesha mahali alipo?" Daniel akauliza

"Nahisi kuna watu wawili nyuma yake. Labda hii saa ni kutoka kwa mtu anayemmiliki, na ile chipu mliyoiharibu ni kwa aliyemleta nchini. Ila sina uhakika, ni mawazo yangu tu" Cara alisema

"Ooooh! Hadi kichwa kinauma. Unajua muda ule tumekuja naye, wewe na Elizabeth mkatangulia ndani jamaa alitaka kuning'oa meno. Yaani meno yamelegea yananipa maumivu makali sana hadi nahisi homa. Ona yalivyolegea." Daniel akasema huku akiyagusa meno mawili ya mbele katika taya la juu.

"Mamaaa. Haki ya Mungu Daniel unaenda kuitwa Mapengo. Kwa nini na wewe usimtoe angalau meno saba? Lakini kama hutaki kuwa mapengo nasikia eti kuna dawa ya kienyeji ukiitafuna ukaiweka kwenye hayo meno ndani ya muda mchache yanakuwa imara kama mwanzo." Mwanasheria alisema huku akiacha kuichezea tarakishi ile.

"Hata mimi nilisikia hicho kitu siku moja. Tena uzuri ni kwamba upo huku Moshi unaweza kuitafuta kwa kuwauliza wenyeji maana nasikia dawa hiyo inamea sana katika mikoa yenye baridi." Cara akasema.
"Vipi Mwanasheria umepata chochote?" Cara akasema na kumgeukia Mwanasheria Mlevi kama wengi wapendavyo kumwita.

"Hii saa mzalishaji wake mkuu ni Amazon, na saa hii humilikiwa sana na majasusi katika kazi zao. Saa hizi zina sifa ya kupiga picha, kurekodi tukio na pia kupokea taarifa ya ujumbe mfupi, japo kutuma ujumbe haiwezi. Hizi ndizo sifa za saa hii ambayo imepewa jina na kuitwa 'Dark Watch'." Mwanasheria alisema.

"Mengine atatuambia yeye mwenyewe, Ngoja nikachukue kisanduku changu" Daniel Mwaseba alisema huku akielekea katika chumba alichohifadhi lile briefcase alilokutwa nalo Festus. Na huko kwa bahati nzuri alikiona pia kisanduku chake ambacho kilisheheni dhana mbalimbali za kuwafanya wasiosema wapate kusema.

Naam. Hii ni Anga ya Washenzi, mwandishi wako ni Gilbert Evarist Mushi. Sehemu ijayo si ya kukosa[emoji3062][emoji91]

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
Riwaya: Anga ya Washenzi
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
Phone: 0765824715.

Msimu wa Pili. Sehemu ya 07

"Mengine atatuambia yeye mwenyewe, Ngoja nikachukue kisanduku changu" Daniel Mwaseba alisema huku akielekea katika chumba alichohifadhi lile briefcase alilokutwa nalo Festus. Na huko kwa bahati nzuri alikiona pia kisanduku chake ambacho kilisheheni dhana mbalimbali za kuwafanya wasiosema wapate kusema.

Mlango ulifunguliwa tena. Awamu hii Daniel Mwaseba hakumsemesha tena Festus, badala yake akakifungua kisanduku chake na kutoa boksi dogo ndani yake. Ndani ya boksi hilo dogo kulikuwa na Nge wawili wakubwa.
Daniel alimtazama Festus kwa Sekunde tano, taratibu akamsogelea, alipomfikia akamsukuma kwa teke la kifua, alipohakikisha Festus ameanguka chini alimsogelea hadi karibu. Akainama kidogo na kuifungua zipu ya suruali ya Festus huku akitabasamu.

"Unataka kunifanya nini wewe?" Festus alivunja ukimya baada ya kuona tayari zipu ya suruali ya jinsi aliyovalia ipo wazi. Alianza kuingiwa na woga.
Daniel alijifanya kutokusikia chochote, yeye aliendelea na zoezi lake na wakati huu alianza kuichana suruali ile badala ya kuivua. Aliona njia rahisi ya kuiondoa katika mwili wa Festus ni kuichana. Sasa Festus ama Ochewa Owechi alibakiwa na Bukta nyeusi iliyombana vyema na kuyasitiri maungo yake. Juu alisitiriwa na tisheti yake baada ya koti lake kuvuliwa tangu akiwa KCMC hospitali.

"Usithubutu kunifanyia chochote wewe mwanaume, hakika mnachokitafuta hamtakipata nakuapia. Katu usijaribu kufanya unachotaka kufanya, utajutia hapo baadae." Festus Jabir ama Ochewa aling'aka. Daniel wala hakujali, sasa alichukua waya mwembamba ulio mfano wa banio kama la kubebea mkaa wenye moto. Waya huu akautumia kumbebea Nge mmoja na kumsogelea Ochewa pale chini.

"Muda wa kubembelezana umeisha, sasa ni muda wa mwalimu kumpa adhabu mtoto mtukutu asiyetaka kujibu anachoulizwa. Wewe utakuwa ni mtoto huyo, ambaye ni mwanafunzi, nami nitakuwa mwalimu mwongoza kipindi. Haya sasa, tuanze kipindi chetu." Daniel Mwaseba alisema huku akiivuta bukta ya Ochewa na kufanya maungo yake yawe wazi. Hapohapo bila kuchelewa akafanya kumwachia Nge yule na kuirejesha mahala pake bukta ile. Kitendo cha Daniel kuirejesha mahala pake bukta ile kikapelekea Nge yule kubanwa kwa ndani. Festus hakuwa na namna yoyote ile ya kujisaidia, kila kona ya mwili wake ilipita kamba ngumu iliyomfanya ashindwe kujisaidia. Na kadiri alivyokuwa akijitingisha kwa woga ndivyo Nge yule alikuwa akizidi kuchokozwa.

"Nitoe please. Nitoeeee" Festus alisema kwa sauti ya juu ishara iliyoonyesha wazi Nge yule alishaanza kufanya yake. Na kadiri alivyokuwa akijitingisha ndivyo Nge huyo alivyozidi kumchoma na kumwachia sumu iliyoambatana na maumivu makali. Ni nani basi asiyeyajua maumivu ya kuumwa na Nge? Tena katika sehemu nyeti? Ochewa alikuwa ni jasusi aliyekidhi viwango vya kuwa jasusi, lakini hapa alishindwa kuvumilia. Alikuwa akilia kama mtoto mdogo, alimwita Daniel na kumpa hadi cheo cha uheshimiwa, lakini Daniel hakujali, akajifanya asikii chochote. Badala yake alimchukua tena nge wa pili na kumsogelea Ochewa.

"Mheshimiwa naombaaaa. Aaaaagh" Festus alikuwa akipiga kelele zilizoambatana na maumivu.
Daniel alijua namna sahihi ya kucheza na kila aina ya watu. Katu hakuishiwa namna sahihi ya kumfanya mtu azungumze, hivyo hata kwa Ochewa Owechi alishajua ni namna gani ya kufanya aweze kuufungua mdomo wake. Alishatambua Festus ama Ochewa alikuwa ni sugu, hivyo aliona amzawadie dawa ya usugu. Kwa mara nyingine Daniel akakamata tena waya ule ulio mfano wa koleo Akaifunua tisheti yake na kumwachilia Nge wa pili katikati ya tumbo la Festus. Akamfunika na kuanza kumkandamiza kwa juu pale tumboni. Ili apate kumchokoza vyema Nge yule.
Nge naye bila hiyana akakubali kuchokozeka. Akamwachia Festus Dhahma.

"Ni nani amekutuma Festus?" Daniel aliuliza huku akisogeza sikio lake karibu na mdomo wa Festus.

"Nitoe hawa Nge tafadhali, nitakueleza kila kitu Kaka yangu" Festus akasema kwa huruma huku akigugumia kwa maumivu makali. Sumu ya Nge ilianza kumtambaa taratibu katika mishipa ya damu.

"Sasa hivi waniita Kaka, lakini tunapoelekea utaniita Babu. Ninahitaji jibu la swali langu. Ni nani amekutuma kutoka Nchini Kenya na kuja hapa Tanzania? Nijibu kwanza hilo tu, mengine yataendelea." Daniel Mwaseba akasema huku akinyanyuka, akakisogelea kisanduku chake na kupeleka mkono wa kulia ili kuchukua kitu fulani.

"Hutojua lolote Mbwa mtoto. Mimi na wewe hatuna tofauti yoyote ile, unatumiwa nami natumiwa. Unaambiwa bweka pale nawe unabweka. Nakuapia kama nikitoka hapa nitakuua kwa mikono yangu hii. Ni bora uniue kuliko kunipa mateso makali hivi, maana sitosema chochote... Aaaaaaagh" Festus alisema kwa uchungu mzito huku akizidi kulalamika kutokana na maumivu ya kuumwa na Nge. Taratibu mwili wake ulianza kuyazoea maumivu yale na kumfanya Daniel kuwaza njia nyingine mbadala.
__________________

Elizabeth Neville alikuwa ndani ya chumba cha kubadilishia nguo wahudumu, katika hoteli ya KiliView. Alifanikiwa kuingia ndani na kumwacha Gilbert Mwaitika akiwa nje. Elizabeth Neville akiwa ndani alishafanikiwa kumteka mhudumu mmoja na kuyavaa mavazi yake. Elizabeth Neville alimfunga na kamba mhudumu yule na kumshindilia nguo mdomoni, akamfungia ndani ya bafu katika chumba kile.

"Utanisamehe mrembo, sifanyi kwa ubaya. Nitakuja kukufungulia baadae na utaendelea na kazi zako" Elizabeth Neville alisema huku akiufunga mlango ule kwa nje. Akatumia dakika mbili kujikagua, na baada ya kujihakikisha yuko sawa alitoka mle chumbani. Kilikuwa ni chumba namba kumi na tisa, katika sakafu ya pili ya ghorofa ndani ya hoteli ya Kiliview.

"Gilbert! Tegemea majibu mazuri usiku huu" Elizabeth Neville alisema kwa sauti ndogo huku akigusa kisikilizio alichokiweka katika sikio lake la kushoto.

"Nice to hear it. Kuwa makini jasusi mrembo" Sauti ya Gilbert Mwaitika ilisikika ikijibu.
Kukawa kimya.
________________

Ulinzi katika sakafu ya nne ya ghorofa ulikuwa ni wa hali ya juu. Vyumba vyote katika sakafu ya nne ya ghorofa havikuwa na wateja, hii ni kutokana na kitendo cha Mheshimiwa Eliud Sumbi kupumzika katika hoteli hii. Kila mtu alikuwa bize na majukumu yake. Mlangoni walisimama walinzi wawili wakiwa makini kutazama mbele, upande wa ndani Mheshimiwa Eliud Sumbi alikuwa bado anakandwa mwili wake na wale wadada wawili huku pembeni yake alisimama Elton Tonny ambaye ni mpambe wake wa karibu.
Mheshimiwa Eliud Sumbi alisimama ghafla na kumfuata Elton Tonny pale aliposimama.
"Fanya hima chunguzeni kama David yupo hai. Pia andaa watu kuhakikisha yule mpelelezi wa kujiita Daniel anapelekwa kambini. Tena akiwa hai maana anapoelekea sasa anazidi, ataifanya kazi yangu kwa mikono yake" alisema huku akimtazama Elton.

"Agizo lako kwangu ni amri kwangu Mheshimiwa" Elton Tonny akasema huku akipiga hatua mbili kinyumenyume na kisha kugeuka
Elton akaufungua mlango na kutoka nje. Pale mlangoni alinong'onezana na mlinzi mmoja miongoni mwa wale waliokuwa wamesimama kuimarisha ulinzi.
Wakati wakinong'onezana pale, binti mmoja mrefu alikuwa akikatiza karibu yao kwa mwendo wa madaha. Binti huyo alibebelea sinia kubwa lililofunikwa kwa juu. Na Binti huyo alikuwa ni Elizabeth Neville akiwa katika vazi la kihudumu.
____________

Henry alikuwa ameketi peke yake akijipatia mvinyo ndani ya Hugos Hotel.
Hugos Hotel ilikuwa ni ukumbi maarufu mjini Moshi wenye shamrashamra za vinywaji vya kila aina na nyama choma, pamoja na vyakula vya asili kama vile mtori na kibulu. Ukumbi huu huvutia sana watu wengi ndani ya Mji ya Moshi kutokana na huduma za pale zinazotolewa huku zikisindikizwa na mziki laini wa kiasili wa kitanzania.
Henry alikuwa ameketi peke yake. Alikuwa kwenye mawazo mazito huku akizidi kujimiminia kileo aina ya Hansons Choice. Japokuwa kileo hiki kilikuwa ni kikali lakini alikuwa akikimimina mdomoni kama maji. Juu ya meza kulikuwa na chupa mbili za Hansons Choice, mojawapo ikiwa nusu huku nyingine ikiwa tupu. Alikuwa na hasira

"Mimi ni mbwa.... mimi ni mbwa tu. Mbwa asiye na makazi. Naendeshwa anavyotaka, kwani nitafanyaje? Nikimbie?nitakimbilia wapi sasa? Nafanya haya kwa ajili ya uhai wako mwanangu. Jerry mwanangu hii dunia ni ya wenye nguvu, si yetu. Si yetu kamwe..... Ina wenyewe. Wenyewe hao ni wenye nguvu. Na wenye nguvu ndiyo wanaoishi. Wazungu wanasema 'The strong to survive' na ndivyo ilivyo" Henry alikuwa akiropoka.
Watu walikuwa wakimchukulia kama mlevi tu, lakini alichokuwa akikisema kilikuwa na ukweli ndani yake. Hii dunia si ya wanadamu wote kama unavyodhani. Wapo wenye nguvu wanaotamani kuiendesha watakavyo, ndiyo maana Henry analaumu. Ulishawahi kuusikia ule usemi ya kwamba mwenye nguvu ndiye anayeishi? Hawakumaanisha asiye na nguvu atakufa, bali ataishia kuwa mtumwa wa mwenye nguvu hadi pale umauti utakapomkuta.
Henry anaye mke na mtoto mmoja. Mara zote amekuwa akimtumikia mheshimiwa Eliud Sumbi si kwa kupenda, ni shinikizo tu. Mwanaye alikuwa amepandikizwa kifaa maalum cha kuuondoa uhai wake kiitwacho 'kill chip'. Kifaa hichi hutumika kufanyia mauaji, kwa aliyepandikizwa kifaa hichi huwa katika hatari ya kuuwawa kutoka kwa mtu aliyempandikiza kwani hutumia mtandao kufanya hivyo. Hivyo mwanaye aitwaye Jerry alipandikizwa mienzi mitatu iliyopita baada ya Henry kutoroshwa magereza katika gereza kuu la Karanga mjini Moshi ambapo alikuwa akitumikia kifungo chake. Henry kabla ya kutiwa magereza alikuwa ni jambazi sugu wa kutumia silaha. Hadi anatoroshwa gerezani alihakikishiwa kupatiwa maisha bora kwake na familia yake kwa sharti moja. Sharti la kufanya kila atakachoagizwa. Alipokuja kugundua analopaswa kulifanya ni jambo la hatari alianza kuleta ubishi, ndipo mpango wa kumwekea mwanaye kifaa hicho ukafanyika ili kumfanya Henry kukubali kufanya kwa lazima.

"Liwalo na liwe, sitokubali niwe chini ya sheria. Lazima nimwage mboga. Nikimpata David itakuwa ni njia ya kuwapata waliomchukua, haswa yule mpelelezi aitwaye Daniel lazima nimweleze anisaidie. Mwanangu Jerry atarudi kwenye hali yale ya mwanzoni na maisha yataenda kuwa mazuri mimi na mke wangu kama zamani" Henry alijishauri. Pombe ilikuwa ikimwendesha, pia alishayachoka maisha ya kuendeshwa na watu. Ni heri angekuwa anafanya yaliyo ya haki, lakini haikuwa hivyo.
Alimaliza kunywa, akaacha bili aliyokuwa akidaiwa juu ya meza na kuelekea katika gari yake. Aliufungua mlango na kuzama ndani, akaitekenya gari kwa funguo na kuondoa hand breki. Ndipo aliposhtushwa na sauti nzito nyuma yake.

"Tulia hivyohivyo, endesha gari na fwata maelekezo yangu"

Ubaridi wa bastola aliouhisi katika shingo yake ulitosha kumwaminisha alikuwa chini ya ulinzi. Alitazama kupitia kioo cha mbele na kufanikiwa kuiona sura ngeni machoni pake. Sura hii hakuwahi kuiona hapo kabla.

Ni nani huyu amemweka Henry chini ya ulinzi? Elizabeth Neville atafanikiwa? Nini hatima ya Festus aliye mikononi mwa kina Daniel? Usikose sehemu ijayo hapahapa Gilbert akusimulie [emoji3526]
 
Riwaya: Anga ya Washenzi
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
Phone: 0765824715.

Msimu wa Pili. Sehemu ya 08

Henry alimaliza kunywa, akaacha bili aliyokuwa akidaiwa juu ya meza na kuelekea katika gari yake. Aliufungua mlango na kuzama ndani, akaitekenya gari kwa funguo na kuondoa hand breki. Ndipo aliposhtushwa na sauti nzito nyuma yake.

"Tulia hivyohivyo, endesha gari na fwata maelekezo yangu"

Ubaridi wa bastola aliouhisi katika shingo yake ulitosha kumwaminisha alikuwa chini ya ulinzi. Alitazama kupitia kioo cha mbele na kufanikiwa kuiona sura ngeni machoni pake. Sura hii hakuwahi kuiona hapo kabla.

"Wewe ni nani na unataka nini kwangu?" Henry aliuliza kwa sauti ya kilevi iliyojaa woga.

"Fuata maelekezo yangu. Sihitaji maswali" Gilbert Mwaitika aliamrisha. Alikuwa ni yeye.

Wakati ule Gilbert Mwaitika akiwa nje ya hoteli ya KiliView baada ya kutengana na Elizabeth Neville, Gilbert Mwaitika alifanikiwa kumwona Henry akitoka nje ya hoteli ile kwa miguu. Ndipo kumbukumbu ikamjia katika tukio lile la Njiro, kunako kambi ya jeshi. Baada ya kuambiwa na Koplo Mugiro kwamba kamera ziliwanasa wanaume watatu waliokuja kumchukua David, Gilbert Mwaitika aliomba apatiwe picha zile japokuwa kamera haikufanikiwa kuzinasa sura zao, bali maumbo yao kwa nyuma. Na kupitia picha zile alikariri maumbo ya wanaume wale. Henry alikuwa amenyoa upara, umbo lake lilikuwa ni la wastani, si mnene sana. Alikuwa ni mweusi pia. Hivyo wakati Gilbert Mwaitika alipomwona Henry basi aliyathibitisha macho yake kwamba sifa hizo zilikuwa ni za Henry. Na hapo ndipo alipoanza kumfwatilia hadi kufikia Hugos Hotel. Alipofika Hugos akazama ndani ya gari ya Henry baada ya kuchokonoa mlango wa buti kwa sekunde kadhaa akitumia waya mgumu na hatimaye kuzama ndani.

"Fwata barabara hii, sihitaji maelezo wala maswali" Gilbert Mwaitika alizidi kumwamrisha Henry. Alipanga kumpeleka katika kambi yao usiku ule. Akiwa njiani akamtaka Henry asimamishe gari na kuizima. Akamtaka akae kiti cha pembeni ya Dereva, akampiga na kiwiko cha bastola na kumfanya apoteze fahamu. Alipoona amepoteza fahamu haraka akahamia siti ya dereva, akamvalisha Henry kitambaa cheusi kichwani na kuhakikisha macho yake yamefunikwa. Akawasha gari ile, safari ya kuelekea kambini ikaendelea.
**********

"Sijui nitumie njia gani azungumze. Amegoma kabisa kusema, na mwili wake ni rahisi kuyazoea mateso" Daniel Mwaseba alisema aliporudi ukumbini. Alimkuta Cara na Mwanasheria wakiwa bize na tarakishi zao. Pale ukumbini kulikuwa na tarakishi mpakato mbili. Moja aliitumia Cara na nyingine alikuwa akiitumia Mwanasheria Mlevi.

"Kuna njia pekee imenijia Daniel. Hiyo ikishindikana ndio basi. Njia hii itamfanya aseme. Mwanasheria Mlevi alisema huku akiacha kubofya tarakishi yake.
Cara yeye hakusema kitu, alikuwa akifuatilia taarifa moja iliyowekwa katika mtandao wa Jamii Forum. Taarifa ile ilikuwa imewekwa masaa mawili tu nyuma huku ikielezea hifadhi ya taifa ya Mikumi kukumbwa na ukame wa ghafla na kupelekea wanyama wengi kupoteza maisha huku wengine kukimbilia makazi ya watu. Cara katika kufuatilia maoni ya watu aligundua ukame huo haukusababishwa na hali ya hewa, hii ni kutokana na mvua zilizokuwa zikizidi kunyesha katika mkoa wa Morogoro. Ilikuwa ni mwenzi wa nne, mwenzi ambao mvua zilikuwa ni nyingi sana katika Mkoa wa Morogoro na mikoa ya pwani ya bahari ya Hindi kwa ujumla. Wengi walishangazwa na ukame huo kutokana na mvua zilizokuwa zikiendelea.
'Ni lazima serikali ifanye uchunguzi wa kina. Mimi nipo karibu kabisa na hifadhi hii na mvua ni kubwa sana tangu mwenzi uliopita. Huo ukame ni wa aina gani'
Yalikuwa ni moja kati ya maoni yaliyotolewa na baadhi ya wadau wakichangia kuhusiana na taarifa hiyo.

"Daniel! Ona hii taarifa, imenishangaza sana" Cara alisema

"Ni taarifa gani hiyo?" Daniel aliuliza huku akisogea karibu kutazama. Cara akamsogezea tarakishi ile apate kuisoma. Mwanasheria mlevi naye akasogea apate kuisoma.

"Duh, taarifa kama hii niliwahi kuiona nchini Cuba miaka minne iliyopita. Ilikuwa ni kama hii kabisa yaani. Kulikuwa na mbuga moja kubwa sana iliyokuwa ni kivutio kikubwa cha utalii ndani ya nchi ile. Sasa katika mbuga ile kulikuwa na twiga wengi sana, kiongozi mmoja wa juu serikalini akawa anashirikiana na majangili kumwaga sumu hatarishi mbugani na kudai ni vyema serikali iwahamishe wale twiga wasife kwa ukame kumbe ilikuwa ni namna ya yeye na wenzake kuwasafirisha twiga na kwenda kuwauza huko Canada na Marekani. Wananchi wakawa wanajua twiga wanahamishwa ili kuwanusuru lakini kumbe nyuma ya pazia kuna kikundi kinanufaika. Ni twiga wachache sana walihamishiwa kwenda mbuga za karibu, lakini wengi waliuzwa kwenda nchi hizo. Hii taarifa naifananisha na hiyo tena baada ya kujua na mvua zinanyesha. Lakini tuwaachie wanaohusika watafanya uchunguzi wenyewe." Daniel Mwaseba alieleza kwa kirefu juu ya taarifa ile.

"Mimi kinachonipa mashaka na kuhisi yamkini kuna kitu nyuma ya pazia ni kutokana na waziri wa Utalii ni rafiki mkubwa sana na makamu wa rais. Wote ni wafipa, wametoka mkoa mmoja pia. Yamkini kuna jambo nyuma ya pazia hatulifahamu." Mwanasheria akasema

"Wakati sahihi wa kujua kuhusiana na makamu wa rais ukifika tutayajua mengi. Maana pia nina mashaka naye sana kutokana na tukio lile la mchana. Alikuwa akichati na kutazama eneo lile alilopo Festus kila mara. Nahisi anahusika" Daniel alisema. Mara wakasikia honi kali ya gari huko nje.

"Atakuwa ni nani? Elizabeth hawezi kurejea huku leo. Hakuna anayejua tumeweka kambi yetu wapi zaidi yake na Gilbert." Cara aliuliza huku akiwatazama wenzake.

"Kuweni makini, ngoja nikachungulie" Daniel alisema akitoka nje. Aliupeleka mkono kiunoni kuichungulia bastola yake kama ipo sawa. Ilikuwa ikimsubiri yeye tu. Kwa tahadhari alizipiga hatua kuelekea getini.
Daniel baada ya kuchungulia alifanikiwa kumwona Gilbert Mwaitika akiwa amemnyooshea mtu bastola. Alifungua mlango mdogo wa geti.

"Kumbe ni wewe Gilbert, huyu ni nani tena?" Daniel aliuliza huku akitazama huku na kule kuangalia kama kuna mtu alikuwa anawachungulia.

"Ni kama bahati Daniel. Wale watu watatu waliokwenda katika kambi ya jeshi kule njiro basi mmoja wao ni huyu hapa" Gilbert akasema.

"Hongera sana Gilbert, hii ni hatua kubwa sana tumeipiga. Ulijuaje lakini kama ni yeye?" Daniel aliuliza.

"Ni wakati ule nikiwa na Elizabeth Neville pale KiliView, nilimwona huyu akitoka. Nilipomwona tu nikaikumbuka ile picha niliyotumiwa na kanali wa jeshi kule Njiro." Gilbert Mwaitika alijigamba.

"Unastahili sifa Gilbert. Mpeleke ndani ngoja mimi niiingize hii gari isigundulike na wambea kama ipo hapa. Bila shaka funguo yake ipo ndani" Daniel Mwaseba alisema huku akifungua geti ili apate kuingiza gari ile.
Gilbert Mwaitika akavua kitambaa kile alichomwekea Henry kichwani baada ya kumwingiza ndani ya geti. Henry akapata kuona nuru machoni pake baada ya muda mfupi wa kiza.

"Ninafurahi sana kukutana nawe Daniel. Jihesabieni kwamba mmepiga hatua kubwa zaidi. Nitawaeleza yote" Henry aliongea kwa sauti ya kilevi. Bado pombe ilikuwa ikikitawala kichwa chake.
________________
Elizabeth Neville amefanikiwa kuingia ndani ya hoteli aliyopo makamu wa rais, ni katika harakati za kuwa karibu na mheshimiwa ili kumpeleleza. Wakati huo hali ya David bado si nzuri baada ya kunusurika kifo. Daniel na timu yake wanahitaji David awaeleze anachokifahamu kuhusu sakata la helikopta. Kwa Ochewa au Festus napo tayari imebainika anaishi lakini ripoti kutoka nchini Kenya zinaonyesha alishafariki dunia baada ya kuuwawa. Isitoshe pia bado hajasema ni nini kimemleta nchini Tanzania. Gilbert Mwaitika naye amefanikiwa kumleta Henry ambaye anatumika kufanya maovu bila kupenda. Nini hatima ya mambo haya yote? Usikose msimu wa tatu katika riwaya hii ya aina yake. Njoo Gilbert Evarist Mushi akusimulie.
 
Back
Top Bottom