gilbert35
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 247
- 474
- Thread starter
- #81
Riwaya: Anga ya Washenzi
Imeandikwa na Gilbert Evarist Mushi
Phone: 0765824715.
Msimu Wa Nne
Sehemu ya 01
Lakini mita mia moja kutoka pale ilipopaki gari ya Daniel alisimama Elton Tonny ambaye ni mpambe wa Makamu wa rais. Elton Tonny alikuwa akilitazama gari la Daniel hadi lilipotoweka mbele ya macho yake. Upesi akakamata simu yake na kupiga namba fulani..
"Kila kitu kipo sawa huku. Kaeni tayari. Anakuja" Elton Tonny alisema na kurejesha simu mfukoni.
_____________
Daniel Mwaseba akiwa ndani ya gari aliuingiza mkono mmoja mfukoni na kuitoa simu yake, ni baada ya kusikia mtetemo mfupi wa kuashiria ujumbe kuingia. Akiwa makini na kuendesha gari, alitoa nywila katika simu yake na kuufungua ujumbe ule.
"Festus amezinduka."
Ulikuwa ni ujumbe mfupi kutoka kwa Gilbert Mwaitika. Akaamua kumpigia Gilbert. Simu ikaita kwa sekunde nne na kisha kupokelewa.
"Niambie Daniel" sauti ya Gilbert ikasikika ikisema simuni.
"Usiniambie Festus ameamka" Daniel akasema.
Wakati akiongea na simu, macho yake yakauona mteremko ukiambatana na kona kali mbele. Mita mia mbele ulikatiza mto mkubwa unaotoa maji yake kutoka kilele cha Mlima Kilimanjaro. Mto huo unajulikana kama mto Isiye ndio chanzo kikuu cha maji katika mto Pangani unaopita mkoani Tanga na kumwaga maji yake katika bahari ya Hindi.
Hali ilikuwa ni ya utulivu sana barabarani, hakukuwa na gari la ziada ama mtu akikatisha eneo la karibu. Daniel Mwaseba aliutoa mguu wake wa kulia kutoka kwenye kinyonya mafuta na kuupeleka katika sehemu ya kukanyaga breki ili aweze kuendana na mteremko ule mkali. Matairi ya gari yalianza kuisugua lami kwa mwendo wa taratibu na gari ilitii na kuanza kupungua mwendo. Lakini katika kupungua mwendo ulizuka mlio wa ajabu, mlio ambao ulishabihiana kwa kiasi kikubwa na mlio wa saa. Aliifungua droo ndogo iliyopo kwenye dashbodi ya gari na kuitoa saa yake, Lakini mlio anaousikia haukuwa ukitoka katika saa ile.
"Gilbert hebu subiri nitakupigia. Kuna kitu kinanichanganya hapa" Daniel Mwaseba alisema na kukata simu. Akaiweka mfukoni na kukanyaga breki tena na kupelekea gari kutembea kwa mwendo mdogo zaidi, akaisogeza gari yake hadi kando ya barabara ili aweze kuubaini mlio ule unatokea wapi.
Baada ya kupaki gari ile, Daniel Mwaseba alitega sikio lake kwa sekunde nane ndipo alipobaini mlio ule haukuwa ukisikika ndani ya gari, bali katika uvungu wa gari. Akafungua mlango wa gari na kutoka ili kwenda kutazama nje, alipofika akainama chini kidogo na kuchungulia...
Loooh!!! Aliona bomu limetegwa pembeni ya waya wa breki. Akajua bila shaka muda ule alipoikaribia kona iliyoambatana na mteremko akaikanyaga breki basi ilipelekea kulitegua bomu hilo kwani bomu hilo lilitegwa kuendana na mfumo wa breki ya gari. Hata hivyo asingeweza kulitegua bomu lile kwa kuwa alishachelewa, wakati anagundua bomu hilo, aliona sehemu yenye namba zinazojihesabu mithili ya saa zikionyesha zilibakia sekunde tano tu kabla ya bomu kulipuka.
Sekunde Tano zilikuwa ni nyingi sana kwa Daniel Mwaseba pindi awapo katika hatari, lakini leo hii zilikuwa ni chache sana, uchache huo ulitokana na ule mshangao uliomkumba baada ya kubaini kwamba lile ni bomu. Mshangao ule ukameza sekunde mbili, sekunde tatu zilizobakia Daniel Mwaseba aligeuka kwa kasi na kuanza kuzipiga hatua ndefu kukimbia...
Hakumalizia hatua ya pili, Mlipuko mkubwa ulitokea na kulisambaratisha gari lile huku yeye akirushwa kuelekea juu na kurushiwa umbali wa hatua kama Tano kutoka pale ulipotokea mlipuko. Pembeni ya barabara ile kulikuwa na mtaro mrefu sana uliojengwa kwa kuelekezwa katika Mto Isiye. Daniel Mwaseba aliporushwa kutokana na mlipuko ule alidondokea ndani ya mtaro ule na kubiringika mithili ya tairi hadi katika kingo za mto Isiye.
Dakika moja baada ya kutokea mlipuko ule ilifika Lori la kubebea mchanga na kupaki jirani kabisa na pale ulipotokea mlipuko. Punde vijana wapatao saba waliovalia tisheti nyeusi zenye nembo ya Fuvu la Kichwa wakateremka wakiwa na madumu makubwa yenye maji pamoja na mtungi mkubwa wa kuzima moto (Fire Extinguisher) na kuusogelea moto ule, mmoja wao alianza kuuzima moto kwa kutumia mtungi ule, baada ya moto kuzima wanaume wale walioshikilia madumu yenye maji walianza kumwaga maji sehemu ile na kukusanya vipande vya mabaki ya gari ya Daniel Mwaseba na kuvipakia ndani ya Lori. Baada ya kuhakikisha hakuna baki lolote lililosalia vijana watano walipanda lori lile na kuondoka. Vijana wawili waliobakia waliteremka na mtaro ule taratibu wakijisogeza mahali alipodondokea Daniel Mwaseba. Na mmoja kati ya wanaume hao alikuwa ni Henry.
Henry baada ya kuuona mwili ule alishtuka sana.
"Vipi, unamfahamu? Naona umeshtuka baada ya kumwona" mwanaume aliyeambatana nae akamuuliza Henry
"Aa.. amna, hata simfahamu ndio kwanza namwona leo. Kwani vipi?" Henry akajitetea akijaribu kujiweka sawa.
"Kumbe tuliyetumwa kumchukua ni Daniel Mwaseba! Daaah! Kama ningejua ni yeye ningemtaarifu mapema. Sijui nifanyaje hapa na wanaweza kunigundua kama nafahamiana nae" Henry alikuwa anawaza peke yake. Alikumbuka usiku wa jana kabla Daniel Mwaseba na wenzake hawajaachana naye alipatiwa karatasi yenye namba ya simu
"Chukua namba zangu. Ukipata chochote tutafahamishana." aliyakumbuka maneno haya, aliambiwa na Daniel usiku kabla ya kurudishwa na gari.
"Unawaza nini? Hebu tumwinue tunasubiriwa juu" Henry alishtuliwa na mwenzake kutoka kwenye dimbwi la mawazo. Bila kuchelewa wakashirikiana kuunyanyua mwili huo na kurejea nao barabarani, walipofika barabarani walikuta Noah Nyeusi imepaki pembezoni mwa barabara ikiwasubiri. Bila kuchelewa wakauingiza mwili wa Daniel Mwaseba ndani ya buti, wakaingia ndani ya Noah ile na kuondoka nayo.
-----------------------
Gilbert Mwaitika, Elizabeth Neville, Mwanasheria Mlevi pamoja na mwanadada aitwaye Cara walikuwa wakimsubiri Daniel Mwaseba kwa hamu kubwa. Hii ilikuwa ni baada ya David kuufungua mdomo wake punde tu baada ya kuzinduka. Wote walihamia nyumbani kwa Dokta Yusha baada ya kuitwa na Gilbert Mwaitika.
David hakuficha kitu, aliwaeleza jinsi alivyoitwa na mpambe wa Mheshimiwa Eliud Sumbi siku moja kabla ya ziara ya rais kufanyika. David aliwaeleza jinsi alivyokutanishwa na mheshimiwa Eliud Sumbi na kupatiwa mpango wa kubadili helikopta.
Siku ile ilikuwa hivi...
Baada ya David kuonana na mheshimiwa Eliud Sumbi, Siku hiyo walizungumza kwa takribani nusu saa na baada ya kuukubali mpango wa mheshimiwa Eliud, David alipatiwa dawa ya usingizi na Elton Tonny.
"Dawa hii utaipulizia kesho ndani ya Helikopta yenu nusu saa kabla ya kuingia. Baada ya hapo, muda ukifika wa kuirusha helikopta angani hakikisha wenzako ndio wanaanza kuingia ndani. Wakishaingia na kuvuta pumzi haitawachukua muda, watadondoka chini kama maembe machanga yaliyozidiwa na upepo" Elton Tonny alisema
"Watakufa?" David aliuliza baada ya kupatiwa dawa hiyo
"Hapana. Watapata usingizi mzito ambao hauamshiki hadi masaa thelathini na sita yapite. Wewe usiingie ndani hadi zipite tena dakika kumi na tano. Baada ya hapo utaingia, nawe utasinzia lakini ni kwa masaa manne tu ndipo utarejewa na fahamu. Ukisharejewa na fahamu utajifanya kutoa ripoti huelewi ni kitu gani kinaendelea. Na wakati huo sisi tutakuwa tumeshaimaliza kazi yetu. Kuhusu Helikopta ondoa shaka maana wakati huo tutairusha helikopta ya kufanana na yenu ili iwe rahisi kwa kazi yetu kukamilika"
David alipotaka kujua ni kazi gani aliambiwa atulie hadi itakapokamilika ndipo atajuzwa.
Na hivyo ndivyo ilivyokuwa, wote wakaridhika na maelezo ya David, japokuwa walimwonea sana huruma kwani tayari alikuwa ni msaliti.
TUKUTANE TENA KESHO SAA 12 JIONI.
NOTE: Kama utauhitaji msimu huu wa nne utaupata jwa gharama ndogo tu ya Tshs 1000 tu. Lipia kwenda M pesa namba 0765824715 au TigoPesa namba 0678824073 kisha njoo whatsapp kwa namba 0621249611 nikutumie. Wale wengine tutaendelea kuisoma hapahapa kila ninapopata nafasi ya kuiweka.
Msimu wa Tano ndio msimu wa mwisho wa Riwaya hii, utaanza kupatikana kesho mchana kwa Tshs 700 tu