Riwaya: Afisa usalama

Riwaya: Afisa usalama

RIWAYA: AFISA USALAMA
MTUNZI: EMMANUEL PHIRI
NAMBA: 0758 195 890
INSTAGRAM: immaphiri

SEHEMU: 10
ILIPOISHIA

Nesi akaweka kituo kisha akawaamuru rafiki zake Walterblanca waondoke kidogo ili mgeni apate nafasi ya kuongea na rafiki yao. Walterblanca akamkazia macho Colotilda, akafikiria kama kashawahi kumuona wapi lakini ubongo wake ukakataa kumpa taarifa hizo, hakika ilikua sura ngeni kwake.

“Eti mgeni wangu, mgeni?”

ENDELEA

Swali fupi likapita katika akili ya Walterblanca pasipo jawabu lolote. Akafungua mdomo wake akaongea pasipo kuonesha dalili yoyote ya kumjali mgeni wake

“Ni nani? Mbona simfahamu!”

“Walterblanca mdogo wangu sio kila mgeni wako lazima umfahamu, ndio maana ni mgeni kama tulivyokutambulisha…Atajielezea mwenyewe na maswali yako ya udadisi utamuhoji tu”

Nesi akakazia maelezo kisha akamtazama Colotilda akamwambia

“Unaweza kukaa hapo”

Walterblanca alimkazia macho mgeni wake kwa mara ya pili lakini mgeni yule alipuuza huku akikaa mahala alipooneshwa na nesi akae. Wakatazamana uso kwa uso na Walterblanca kisha Colotilda akaongea huku akimpa mkono wa salamu Walterblanca.

“Habari yako Walterblanca”

Macho ya makali ya Walterblanca yakaendelea kushambulia uso wa Colotilda huku akili yake ikiendelea kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu kamili. Salamu ya Colotilda ikapita pasipo majibu katoka kwa mwanafunzi yule aliyegubikwa na mawazo mazito kichwani mwake, hakika salamu ile ilipepea kama upepo mkali uvumao jangwani. Hakikua kitendo cha kiugwana machoni mwa nesi na matron kwa mgeni huyo, lakini watafanya nini wakati muhusika hataki kutoa ushirikiano?
Colotilda akawageukia nesi na matroni kisha akawaambia

“Samahanini ndugu zangu mnaweza kuniacha na Walterblanca? Nataka kuanza kazi yangu!”

Hofu ikaongezeka katika moyo wa Walterblanca baada ya kusikia mgeni anataka wabaki wenyewe, uvumilivu ukamshinda akauliza kwa jazba

“Kwanini waondoke? Unataka nini kutoka kwangu?”

“Sikiliza binti…”

Colotilda akataka kumfafanulia Walterblanca lakini hali haikuwa kama alivyofikiria na kutarajia, Walterblanca akamkatisha maelezo yake kwa sauti ya juu

“Nisikilize nini? Sitaki kusikiliza chochote kutoka kwako, Unaweza kuondoka tu”

Matroni akamtazama Walterbanca kwa jicho la hasira kisha akamwambia

“Do you love yourself and love your brother? If the answer is yes, listern to your visitor but if the answer is no, let her go”
“(Unajipenda na kumpenda kaka yako? Kama jibu ni ndio, msikilize mgeni wako lakini kama jibu ni hapana, mwacho aondoke)”

Walterblanca akamtazama matroni wake asielewe nini alichosikia kisha akamuuliza

“What do you mean?”
“(Una maana gani?)”

“What do you mean! Unamuuliza nani what do you mean? Nimekwambia na umenielewa vizuri, kazi kwako kuamua kusuka au kunyoa".

Matroni akamshika mkono nesi na kisha akamtazama Colotilda, akamwambia. Matroni Manase alikuwa ameshafura hasira

“Sisi tunakuacha uongee nae akiwa mbishi achana nae”

Baada ya maneno hayo mazito matroni na nesi wakaondoka ndani ya chumba kile cha kupumzikia wagonjwa, na kuwaacha mtu na mgeni wake. Colotilda akarudisha macho kwa Walterblanca aliyechanganywa na maneno aliyoambiwa na matroni wa shule kisha akamwambia

“Naitwa Colotlida Kamanzi, nimekuja hapa kuongea na wewe vitu vichache kama utaamua kunipa ushirikiano”

Walterblanca akamtazama Colotilda kwa jicho lenye chuki dhahiri kisha akauliza swali lenye kutaka maelezo ya kina

“Jina lako sio muhimu sana kwangu, nachotaka kujua shida yako ni nini na una uhusiano gani na kaka yangu?”

Colotilda akamtazama binti yule kisha akatoa tabasamu hafifu lenye kukinzana na hali halisi aliyojisikia moyoni baada ya kujibiwa kijeuri na mwanafunzi. Akachukua mkoba wake aliokuwa ameuweka pembeni kisha akafungua zipu na kutoa bahasha ndogo, akamkabizi Walterblanca, akamwambia

“Tazama kilicho ndani ya bahasha kisha tutaendelea na maongezi”

Walterblanca akaipokea bahasha kwa shauku kubwa ya kutaka kujua kusudio la mgeni wake kisha akaifungua, akatoa picha na kipande kidogo cha karatasi chenye maandishi machache yaliyosomeka

“I love you, Colotilda”
“(Nakupenda, Colotilda)”

Akarudisha macho kwa Colotilda kisha akamuuliza

“Nini maana yake? Mapenzi ya watu unaniletea mimi!”

Colotilda akatabasamu kisha akaongea

“Tazama hiyo picha kwanza ndiyo utajua nini maana ya hayo maandishi na kwanini nimekuletea wewe”

Walterblanca akarudisha macho yake katika picha ile, mshangao ukaiteka sura yake akahisi mapigo ya moyo yakiongezea kasi huku kijasho chembamba kikitambaa katika ngozi yake laini. Akauliza maswali mfululizo bila kutoa nafasi ya kujibiwa

“Umeitoa wapi hii picha? Wewe ni nani haswa? Kwanini unayo hii picha?”

Colotilda akamtazama Walterblanca kisha akamwambia

“Kama nilivyokwambia naitwa Colotlida Kamanzi nimekuja hapa ili niongee na wewe maswala ya kaka yako”

Colotilda akaingiza mkono katika pochi yake akatoa kitambulisho alichokitumia kuingia katika shule hiyo akamkabidhi Walterblanca kisha akaongea

“Kitambulisho kina jina langu na picha yangu lakini hakina kazi yangu halisi, sifanyi kazi katika shirika lolote la haki za binadamu…nimekwambia hivyo kwa sababu isije kutokea ukaja kunitafuta katika ofisi zao. Huwezi kunipata habadani”

Akakohoa kidogo kisha akaendelea

“Najua nazidi kukuchanganya, naelewa hilo ila ipo siku utajua mimi ni nani haswa na nina shughuli gani. Cha msingi hapa ni kumsaidia kaka yako tu na sio vinginevyo"

Hasira za Walterblanca zikaanza kutoweka taratibu, sasa aliamini kuna msaada ndani ya mgeni wake. Kwa umakini wa hali ya juu akauliza

“Bado unanichanganya zaidi! Eti hufanyi kazi shirika la haki za binadamu! Sasa kwanini umewadanganya walimu na walezi wangu?...Na mbona hujibu swali langu kuhusu ulipoitoa hii picha?”

Colotilda akamtazama Walterblanca kwa umakini zaidi, akasogeza kiti karibu yake zaidi kisha akamwambia

“Kuhusu utambulisho wangu bado hutakiwi kujua wewe wala uongozi wako wa shule, na sababu ya kukwambia nilichokwambia ni kutaka usije nitafuta katika ofisi za haki za binadamu maana najua utakua na uchu wa kuniona kila wakati baada ya kumaliza maongezi ya leo….Kuhusu picha hiyo niliipata wapi? Niliipata siku aliyohukumiwa kaka yako. Kwa bahati mbaya kwako au nzuri kwangu kipindi unatolewa na polisi ndani ya jumba la mahakama ulinipamia ukaiangusha hiyo picha, nilikuwa sikujui lakini nilivyoitazama hiyo picha nikahusianisha na baadhi ya matukio niliyowahi kuyasikia na kuyaona kuhusu kaka yako, nikapata taswira fulani na ndio maana nipo hapa leo kujua zaidi”

Akapiga chafya kisha akaendelea

“Kuhusu nina uhusiano gani na kaka yako! Simple answer ni kwamba, kama hicho kipande cha karatasi nilichokupa kinavyojieleza. Kaka yako alikua akihitaji niwe mpenzi wake lakini hilo halikufanikiwa”

Akavuta pumzi ndefu ndani kisha akaitoa taratibu, akaendelea

“Kesi iliyompeleka ndani kaka yako inanihusu mimi kwa asilimia kubwa kwa sababu inasemekana alituteka mimi na marehemu Mr Hamisi Ernest, maarufu kwa jina la Kidua lakini kwa muujiza wa Mungu lengo lake la kuniua halikufanikiwa”.

Colotilda akarekebisha miwani yake iliyomuongezea urembo mrembo yule, kisha akaendela

“Najua kaka yako hausiki kwa lolote na nina uhakika na kauli yangu lakini kinachonishangaza zaidi kwanini alikubali kesi? Alafu kwanini hakuna ndugu anayemsaidia katika janga lake hili zaidi yako?. Ndio maana nimekufuata ili unipe maelezo ya kutosha kuhusu maisha ya kaka yako, nijue naanzia wapi juu ya mambo yake japokuwa ameshahukumiwa kifungo cha maisha”

Walterblanca akainamisha kichwa chini kama sekunde kama kumi akatafakari aliyoyasikia kisha akainua kichwa chake akauliza

“Nilisikia kesi ya kaka ina uhusiano na masuala ya mapenzi, jambo hilo nililikataa moja kwa moja. Mapenzi hayawezi kumtesa kaka kiasi hicho mpaka aue mtu au watu …nina mfahamu vizuri kaka yangu”

Walterblanca akachukua chupa ya maji akanywa kurekebisha koo lake kisha akaendelea

“Mapenzi yalivyomtesa kaka hawezi fanya upuuzi huo tena kizembe zembe”

Colotilda akamkazia macho Walterblanca huku akiandika baadhi ya mambo aliyohisi ni muhimu kwake

“Msichana aliyekua kwenye akili ya kaka ni binti mmoja wa Arusha anayeitwa Janeth Dominic Kimaro…sasa unavyoniambia mapenzi yamempeleka jela kaka tena binti mwenyewe ni wewe na sio Janeth hapo ndipo ninapopata utata”.

Walterblanca akasubiri kauli ya Colotilda lakini Colotilda alikua kimya akiendelea kuandika alichosikia toka kwa mwanafunzi yule. Walterblanca akaongeza neno lenye swali la mshangao ndani yake, lilikua swali kama aliloulizwa awali, swali lenye mshangao mkubwa ndani yake

“Kama unavyosema una uhakika kaka ahusiki na kesi hiyo sasa kwanini alikubali?”

Colotilda akamshika bega Walterblanca kisha akamwambia

“Kuna tukio lililonitokea kipindi nikiwa mdogo ndilo haswa linalonipa ukakasi juu ya tuhuma ya kaka yako, najua unataka kuuliza ni tukio gani lakini sasa sio wakati wake wakati wa sasa ni kupambana na nshu ya kaka yako tu. Nimejaribu kuchunguza na kuhusianisha baadhi ya mambo bado naona kaka yako yupo salama…mikono ya kaka yako haina damu ya mtu”

Akaendelea

“Naomba unielezee vizuri historia ya kaka yako kuanzia maisha ya nyumbani, mtaani na chochote unachohisi kitanisaidia katika uchunguzi wangu”

Walterblanca aliona huo unaweza kuwa msaada kwa kaka yake, japokuwa alikuwa hajaambiwa utambulisho halisi wa mtu huyo lakini alichoamini huo ni msaada. Akakohoa kidogo kurekebisha sauti yake kabla hajaanza kuelezea anachojua kuhusu kaka yake, lakini kipindi akijiweka sawa mara wakaingia nesi na matroni. Nesi akaongea

“Madam, nadhani dakika ulizopewa zimeisha”

Walterblanca akamtazama nesi kwa macho ya huruma yaliyoomba wapewe muda zaidi lakini msimamo wa nesi ukawa palepale.

“Kama ni maelezo machache kama alivyosema atakua ameyapata, yatupasa tuheshimu sheria na utaratibu wa shule na sio vinginevyo”

Colotilda hakuwa mbishi kwa maelezo hayo akachukua mkoba wake akainuka kisha akaingiza mkono katika mkoba huo akatoka kadi yenye namba zake za simu akamkabidhi Walterblanca kisha akaongea

“Upatapo nafasi twaweza kuwasiliana kupitia namba hii”

Walterblanca akataka kuipokea lakini matroni akaingilia kati akasema

“Hawaruhusiwi kumiliki namba ya mtu yeyote hivyo basi hutakiwi kumpa namba yako please. Utaratibu ulioufata leo ndio unaotakiwa kuufata siku zote”

Colotilda akajibu

“OK! Sijui tunafanyaje maana taarifa ninazohitaji bado hazijakamilika na muda umeisha kama mnavyosema?…”

Kabla nesi au matroni ajajibu, Walterblanca akamjibu Colotilda kwa sauti ya upole.

“Sikiliza dada yangu, taarifa hiyo nitaiandaa vizuri kwenye kitabu changu cha kumbukumbu (Diary) then nitawasiliana na uongozi wa shule ili utaratibu ufatwe na taarifa zikufikie”

Wote wakaafikiana na jibu alilolitoa Walterblanca, wakaagana kisha Colotilda akaondoka zake. Nuru ya matumaini ikaingia katika moyo wa Walterblanca. Sasa akaamini kaka yake lazima apate haki zake stahili. Swali moja likabaki likimsumbua

“Atapataje haki zake wakati ameshaihakikishia mahakama kama aliua?”

Kitendawili.

## ## ##
Hali ya hewa ilikuwa shwari huku miale ya jua ikiringa na kuchekelea juu ya uso wa dunia, Upepo mwanana toka ziwa Tanganyika ukaendelea kuwaburudisha na kuwafurahisha wakazi wa maeneo ya Burega pamoja na maeneo ya jirani. Watu walikua bize na shughuli zao za kila siku, lakini ndani ya jumba la kifahari la mkuu wa jeshi la polisi mkoani Kigoma (RPC) wafungwa saba walikuwa wakivuja jasho kwa kazi ngumu waliyokuwa wakiifanya. Sululu zilikuwa mikononi huku kila mfungwa akiwa ameinama katika msingi aliokuwa akiuchimba, polisi walikuwa makini wakidumisha ulinzi eneo hilo huku siraha zao za moto zikiwa barabara mikononi mwao.

Godfrey Mdemu hakuwa na muda wa kutazama kushoto wala kulia katika eneo hilo, akili yake yote ilikuwa katika kazi aliyokuwa akiifanya ili asije adhibiwa na polisi waliokuwa wakiwashurutisha kila walipohisi mfungwa akitegea kazi. Wafungwa wengi hupendelea sana kufanya kazi nje ya maeneo ya magereza kwa sababu huko hufanikiwa kuona mazingira ya uraiani na wakati mwingine hupewa chakula kizuri na watu waliowafanyia kazi. Godfrey ni mmoja wa wafungwa ambao mara nyingi hupata bahati ya kufanya kazi nje ya jengo la magereza kwa sababu ya nidhamu yake aliyokuw akiionesha ndani ya gereza. Mara nyingi wafungwa huchukuliwa na kupelekwa kufanya kazi za kijamii mfano kusafisha na kufyeka maeneo ya hospitali, shule, soko na mara chache hupelekwa kufanya kazi nyumbani kwa wakuu wa jeshi la polisi.

Siku hiyo wafungwa saba walikuw bize wakifanya kazi kwa RPC wa mkoa wa Kigoma, Mr Phidelis Edward aliyeamrisha wafungwa hao waende kufanya kazi nyumbani kwake. Kipindi kazi ikiendelea na ulinzi ukiendelea kudumishwa, nje ya geti la jumba hilo gari dogo la kifahari Bugatti Chiron linalokadiriwa kuwa na gharama ya Dola 2.7 sawa na shilingi Bilioni 6.48 za kitanzania likapiga breki kisha wasichana warembo watatu waliovaa suti za kaki na miwani zikiwa zinaboresha urembo wao, wakashuka taratibu kwa madaha huku pochi zenye rangi sana na suti zao zikining`inia katika mabega yao. Polisi waliokua getini wakaamka na kulifuata gari hilo la kifahari lililopaki jirani kabisa na geti hilo kisha wakawaamuru mabinti wale wasimame kwa mahojiano kabla hawajawakaribia zaidi, lakini hali ilikua tofauti kwa mabinti wale. Hakika walizamilia kilichokua kichwani kwao. Hawakutii sharti wala amri ya polisi, wakaendelea kuwafuata polisi walipo bila hofu yoyote.

“Mnakaidi amri ya jeshi la polisi eeeh!”

Polisi mmoja kati ya wawili waliokua wakilinda geti akaropoka kwa sauti ya ukali na gadhabu baada ya kuona warembo wanakaidi amri yao, lakini warembo wale hawakujibu chochote zaidi ya kuwasogelea zaidi polisi. Warembo wale wakashusha pochi zao toka mabegani wakazishika mkononi tayari kutimiza walichopanga, sasa walikua hatua nne toka walipo polisi wa getini. Kitendo kile cha kushusha pochi kwa pamoja tena haraka namna ile, kilisababisha polisi waingiwe na hofu na hali ya hatari mioyoni mwao. Polisi aliyetoa amri kwa mabinti wale wasimame akanyoosha siraha yake ya moto kisha akawaelekezea mabinti wale kwa lengo la kuwashurutisha wasimame kwa nguvu.

KOSA.

Mrembo aliyekuwa katikati ya warembo wenzake aliruka teke kali lililompeleka afande yule chini kama mzigo wa chumvi, polisi mwenzake akahamaki kwa jazba akataka apulize filimbi yenye kuashiria hali ya hatari lakini kabla hajatimiza lengo akapigwa buti la kifua na mrembo yule machachari, akapepesuka mpaka chini. Muda wa kama sekunde kumi polisi wote wawili walikuwa wamedhibitiwa ipasavyo. Hakuna aliyekuwa kidume mbele ya warembo wale. Wakafungwa kamba kwenye mikono na miguu yao kisha wakalazwa chini kama magunia ya mbolea. Binti mmoja akachukua silaha zao za moto kisha akawaamuru wasijigeuze wala kutoa sauti yoyote inayoweza kuwapa taarifa polisi walio ndani. Binti aliyeruka mateke dakika tano zilizopita akachungulia ndani kupitia sehemu ya kutazamia katika geti lile, akaona jinsi polisi wawili walivyo bize kuwashurutisha wafungwa wafanye kazi bila kupumzika. Akawatazama vizuri wale wafungwa ndipo akagundua hawajafanya kosa lolote bali wapo sahihi kama walivyopewa taarifa, akawageukia wenzake kisha akawaambia

“Godfrey yupo…Hatuna muda wa kupoteza”

ITAENDELEA

* Riwaya imeanza rasmi sasa
Kazi nzuri
 
Shukrani
 
Back
Top Bottom