mkuu ongeza kimoja cha mwisho basiRIWAYA: AFISA USALAMA
MTUNZI: EMMANUEL PHIRI
NAMBA: 0758 195 890
INSTAGRAM: immaphiri
SEHEMU 04
ILIPOISHIA
Godfrey akaona huo ndio muda muafaka wa kwenda kupaki bajaji kwa bosi wake. Akamuaga Festo Jambo kisha akawasha bajaji yake taratibu kuelekea usawa wa baa (bar) maarufu eneo hilo iitwayo Just in Time Resort ili ashike barabara ya vumbi inayoelekea ilipo nyumba ya bosi wake. Lakini kabla hajaifikia bar ya Just in Time Resort, vijana wawili wakamsimamisha karibu na nembo ya shule ya msingi Airport. Vijana hao walikua wamevaa makoti marefu meusi toka mabegani mpaka usawa wa magoti, mmoja alivaa kofia aina ya pama iliyoficha sehemu kubwa ya kichwa chake, wa pili alikua amevaa kofia kubwa aina ya mzula yenye chapa mbele iliyosomeka “Manchester United”. Mzula ule ulificha sehemu ndogo ya kichwa chake hivyo Godfrey akafanikiwa kuiona sura ile nzuri tena yenye bashasha za upole na ukarimu. Akafikiria kama ameshawahi kuiona ile sura awali lakini jibu likawa ‘hapana’
ENDELEA
“Samahani kaka tupeleke Ujiji mtaa wa Makondeko”
Kijana mwenye sura ya ukarimu akavunja ukimya.
“Hiyo sio route yangu, samahani sana siwezi kuwapeleka”
Godfrey akajibu lakini akili yake bado ilishindwa kuwaelewa hasa ule muonekano wao usiku ule wa giza.
“Tutakupa pesa utakayohitaji, tupeleke ndugu yangu”
Kijana yule akakazia kidogo baada ya kuona Godfrey anaweka ngumu huku macho yake yakimtazama Godfrey moja kwa moja bila kupepesa.
“Hata hivyo nipo naenda kupaki, masaa ya kazi yangu yameshanitupa mkono, kama mnataka bajaji za kuelekea Makondeko nendeni mtaa wa BELLA jirani na soko la mwanga, nina imani mtazipata tu”
“Najua masaa yameenda na unatakiwa kwenda kupaki ila tunaomba basi utupeleke hapo kwa Bella zinapopatikana bajaji za kuelekea ujiji Makondeko”
Kijana mwenye kofia ya pama iliyoficha sehemu kubwa ya sura yake akavunja ukimya wake.
Godfrey akawatazama kwa macho ya udadisi akahisi wanahitaji msaada na anapaswa kuwasaidia iwezekanavyo lakini moyo wake ukapingana na wazo hilo. Hakika alikuwa njia panda. Ghafla akaropoka bila hata kuafikiana na akili yake
“Ingieni twende”
KOSA
Moyo ukapingana na kauli yake lakini atafanya nini na amesha waamuru waingie?. Vijana wale wenye muonekano usio eleweka kabisa, taratibu tena bila haraka yoyote wakaingia ndani ya bajaji. Safari ikaanza, safari isiyo na maongezi yoyote, kimya kilitawala kila mmoja akifikiria lake. Baada ya dakika chache kupita simu ya kijana aliyevaa kofia yenye chapa ya ‘Manchester United’ ikaita, Akaichomoa kutoka kwenye mfuko wa koti lake na kuipokea
“Hallo Bosi”
Sauti ya upande wa pili wa simu iliyokua ikiongea na kijana huyo haikuweza kusikika katika masikio ya Godfrey wala yule kijana mwenye kofia ya pama.
“Ndio Bosi, Kazi uliyotupa tumetekeleza ipasavyo. Utasikia habari muda sio mrefu…na yule binti anayejifanya mjanja hah hah hah! Kwisha habari yake”
Maneno hayo yakapenya vizuri katika masikio ya Godfrey japokuwa alikua makini sana na usukani wa bajaji yake lakini akili yake iliweza kutafasiri hali ya hatari. Kijana mwenye kofia ya pama akachukua simu kwa mwenzake kisha akaongea
“Sisi ni vijana wa kazi”
Akakaa kimya kusikiliza maelekezo toka upande wa pili wa simu (upande wa Bosi). Akatigisha kichwa kumaanisha kaafikiana na maelekezo hayo, japokuwa kitendo hicho cha ishara hakikua na maana yoyote mbele ya Bosi. Akatoa simu sikioni kumaanisha mazungumzo yameisha na simu imeshakatwa kisha akamwambia mwenzake
“Hakika mafahari wawili hawawezi kukaa zizi moja…Hah hah hah! Hamis Ernest”
Godfrey akashindwa kuelewa nini maana ya maongezi ya wale vijana ila mwisho wa uwezo wake wa kufikiria uliamini vijana wale sio wema kabisa, hofu ikajaa kwenye moyo wake akihofia usalama wake. Akaongeza kasi ya bajaji yake huku akiwatazama vijana wale kupitia site/ side mirror (koo cha upande), upande wa kulia wa bajaji yake, hakufanikiwa kuwaona ipasavyo kutokana na giza lililofukuza mwanga masaa kadhaa yaliyopita. Ukimya ukatawala huku amani nayo ikiendelea kukimbia kusikojulikana.
“Mungu wangu naomba unilinde na chochote kinachoweza kunidhuru maana naona dalili za kutokua salama…balaa gani hili!”
Godfrey alimkumbuka muumba wake kwa sauti iliyosikika ndani ya moyo wake. Mungu si Athumani bajaji ya Godfrey ikafanikiwa kufika kwa kituo cha Bella salama salimini bila tatizo lolote.
“Nafikiri nimewafikisha tulipokubaliana”
Kauli isiyo na hofu yoyote ikatoka ndani ya kinywa cha Godfrey akiamini mawazo aliyokuwa akiwawazia vijana wale yalikua potofu maana wamepita sehemu nyingi zilizokuwa kimya na hatari lakini hawakumdhuru kwa lolote. Sasa wapo katika kituo maarufu, kituo kinachofurika watu muda wote wanaopanda na kushuka katika vyombo vya usafiri hasa daladala, bajaji na pikipiki. Godfrey akajihakikishia usalama wake.
“Bila shaka tumefika”
Kijana mwenye kofia aina ya mzula yenye chapa ya ‘Manchester United’ akajibu kauli ya Godfrey huku akiingiza mkono wake wa kulia katika mfuko wa koti lake ndefu lililomfunika mpaka sehemu za magoti. Akachomoa noti ya shilingi elfu kumi na kumpatia Godfrey, kisha akamwambia
“Keep chenji…Tumekusumbua sana, hayo ni malipo ya fadhila ya uungwana wako”
Godfrey akabaki ameishikiria noti ile huku akishuhudia vijana wale wakishuka katika bajaji yake kisha wakakodisha Taxi na kuelekea uelekeo wa Ujiji. Alishangaa kuachiwa noti ya shilingi elfu kumi wakati alistahili kulipwa elfu moja. Godfrey akafikiria tukio zima tangu alipowapakia vijana wale wenye makoti marefu mpaka alipoachana nao muda mfupi uliopita kisha akajisemea moyoni.
“Usilolijua ni kama usiku wa giza na umzaniae ndie kumbe sie…yaani umbali naotakiwa kulipwa mia tano kwa kichwa kimoja wamenilipa elfu kumi!”
Laiti angejua, asingekubali kuwabeba wale vijana. Hakika asingekubali abadani.
Taratibu akageuza bajaji yake moja kwa moja mpaka kwa Bosi wake mzee Ramadhani Simba, baada ya kuipaki akaenda katika chumba chake alichopanga na kujiegesha katika godoro lake lenye kunguni. Kichwa kikarudisha mawazo ya vijana wa kutisha aliokutana nao akawafikiria sana pasipo majibu. Kama ilivyo kawaida tendo lisilo la hiyari likachukua nafasi yake, usingizi mzito ukamchukua taratibu pasipo mwenyewe kuelewa. Ndotoni akaona taswira za vijana wale wakiwa wamevaa suti nzuri nyeusi zilizowakaa vizuri kama maafisa wa serikali, kilichomshangaza walikuwa wakimtazama kwa macho ya chuki na hasira kali.
#### #### ####
Sauti kali ya jogoo lenye hadhi ya kuitwa dume lilikoroma kwa fujo katika masikio ya Godfrey, akajitahidi kupambana na sauti hiyo ili isiweze kuathiri usingizi wake lakini alikua kama anatwanga maji kwenye kinu. Usingizi ukamruka kabisa, akalani vikali kelele za jogoo yule, akaamua kuinuka alipolala akaifuata suruali yake chakavu aliyoivaa siku iliyopita kisha akaingiza mkono katika mfuko wa kulia wa suruali hiyo na kuchomoa saa. Akaitazama saa ile ikamuonesha kuwa ni saa kumi na mbili kasoro robo saa. Akajisemea moyoni
“Ngoja nilazimishe usingizi hii robo saa iliyobaki”
Akarudi katika godoro lake na kujilaza kivivu akisubiria usingizi uchukue nafasi yake. Haikua kama alivyotarajia, kabla hata hajafaidi kilichompeleka pale kwenye godoro ghafla akajipiga kibao kikali mgongoni baada ya kusikia maumivu makali sehemu hiyo. Akasikia harufu kali ya kunguni aliyekua akimshambulia bila huruma. Akahisi maumivu yakizidi, hapo ndipo alipokumbuka ule usemi usemao
“Heri nusu shari kuliko shari kamili”
Akajiinua kinyonge pale alipolala, akapatazama kwa hasira kisha akatamka taratibu kama mtu aliyenong`oneza
“Kwanini niendelee kusumbuliwa na hawa wadudu wakati pameshakucha?"
Akaitazama tena saa yake ikamuonesha kuwa ni saa kumi na mbili kasoro dakika nane. Wazo la kujiandaa na shughuli yake ya bajaji likachukua nafasi yake. Mwanga ukaendelea kulifukuza giza taratibu lililodumu usiku mzima, nguvu ya mwanga ikafanikiwa kupambana na giza kwa sababu kila baada ya dakika chake nuru iliongezeka katika sura ya dunia. Miale ya jua ikapenya kichokozi mpaka kwenye chumba kisichopendwa na anayekimiliki, ikaangaza na kuonesha vitu visivyo na thamani vilivyotapakaa ovyo ndani ya chumba hicho. Godfrey akahesabu pesa aliyobaki nayo baada ya kumkabizi mtoto wa Bosi wake pesa aliyotakiwa kukabizi kila siku. Ilimbidi amkabizi kijana huyo baada ya kukuta mzee mwenye bajaji ameshalala, vilevile alikumbuka alivyoambiwa na mtoto wa bosi wake kuwa anatakiwa awe anapaki mapema kwa usalama wake na usalama wa chombo hicho cha moto.
“Yaani siku moja nimeingiza elfu thelathini na sita ya ziada! Duuuh! Mungu mkubwa kwa kweli”
Mawazo yakarudi nyuma akawakumbuka wale vijana wenye makoti makubwa waliompa noti ya elfu kumi bila kuhitaji pesa yao iliyobaki
“Mungu awabariki maana wameniongezea akiba yangu, leo nikifanya kazi vizuri kama jana nina uhakika wa kumlipa mama mwenye nyumba pesa yake ili aniachie kelele zake”
Akaitazama saa yake kwa mara ya tatu, ikamuonesha kuwa ni saa kumi na mbili na robo. Akaona muda wa kufanya kazi umefika, akatupa macho katika bahasha yake iliyochakaa akachomoa karatasi lake lenye maneno yaliyokua yakimpa faraja, akapiga ishara ya msalaba kumkumbuka Muumba wake kisha akasoma sentensi moja taratibu
“Life is hard, Its harder if your stupid” – John Wayne
Akarudia kuisoma kwa mara ya pili sentensi hiyo kisha akajisemea moyoni
“Hakika maisha ni magumu lakini alichokiongea John Wayne kina ukweli ndani yake? Lazima jasho langu lipate mafanikio”
Tabasamu hafifu likachomoza katika sura ya Godfrey lakini bila ya kutarajia tabasamu hilo likafukuzwa haraka baada ya kuona taswira ya baba yake ikimjia akilini, akakumbuka maneno aliyoambiwa siku aliyofukuzwa nyumbani kwao. Furaha yote ya moyoni ikaondoka na hali ya huzuni ikashambulia sura na moyo wa Godfrey pasipo huruma yoyote. Akajipa moyo
“Potelea mbali, kila kitu kinatokea kwa sababu”
Akapanga kila kitu mahala pake kisha akafunga mlango. Safari ya kwenda kwa bosi kuchukua bajaji ikaanza. Hakika kila siku mpya ina matatizo yake haswa kwa watu wa hali ya chini. Godfrey alitembea kichwa chini mikono nyuma huku akitafakari maisha yake, hasira ikamjaa moyoni na akajikuta akiongea peke yake kama chizi
“Sikutarajia kama kuna siku nitakuja kuishi maisha magumu kama haya, kweli usicheke mamba kabla hujavuka mto…Hujafa hujaumbika”
Alitembea kama bubu asiyeona umuhimu wa kusalimia wala kuitikia salamu za watu, aliwapita watu kama vijisanamu hata waliomsalimia alihisi walikua wakimsumbua kufungua mdomo wake ili aitikie salamu zao. Raia wenye hasira walitoa maneno machafu dhidi yake lakini wengine wakampuuza huku wakimsindikiza kwa maneno ya kuudhi
“Hakika ameanza kuwa chizi, atakua amerogwa sababu amezidi kudhurumu wenzake”
Godfrey hakujali maneno wala matusi ya watu, yeye kichwa chake kilikua chini kama kobe au kondoo jike. Hakina hakuna marefu yasiyo na mwisho, mwisho wa safari ikafika, akanyanyua kichwa chake na kusoma maandishi
KUNA MBWA MKALI
Akasogelea zaidi geti la bosi wake kwa lengo la kugonga na kufunguliwa kama afanyavyo siku zote lakini siku hiyo akahisi kitu tofauti sana na siku zote alizofika eneo hilo. Alisikia sauti za watu wengi wakiongea ndani ya geti hilo, alishindwa kuelewa maongezi yao yalikua yakimaanisha nini. Godfrey akasita kugonga mlango lakini akachungulia ndani huku akiongeza umakini katika sikio lake ili aweze kushuhudia na kuzibitisha alichokisikia. Akawaona wanaume tisa akiwemo mwenyekiti wa mtaa, katibu wa mtaa, mwenye nyumba pamoja na wengine wakiwa bize na maongezi mazito aliyohisi kama hadithi za bunuasi. Vilevile aliona idadi kubwa ya akina mama na watoto wa makamo yanayokaribia ujana aliyoshindwa kupata idadi yao kamili, lakini kilichomshangaza zaidi aliona bajaji anayoitumia kwenye shughuli zake ikipigwa picha ovyo na watu wale. Sauti kali na nzito ya mwenyekiti ikasababisha Godfrey ahisi dunia sio sehemu nzuri na salama kwake labda azikwe au ardhi ipasuke ajifiche.
ITAENDELEA
NB * Vijana wenye makoti marefu wana nini?
- Yupo wapi God Mother?
- Familia ya Godfrey vipi?

Unataka Kimoja cha Mwisho eemkuu ongeza kimoja cha mwisho basi
Nzuri sanaRIWAYA: AFISA USALAMA
MTUNZI: EMMANUEL PHIRI
NAMBA: 0758 195 890
INSTAGRAM: immaphiri
SEHEMU 05
ILIPOISHIA
Hakina hakuna marefu yasiyo na mwisho, mwisho wa safari ikafika, akanyanyua kichwa chake na kusoma maandishi
“KUNA MBWA MKALI”.
Akasogelea zaidi geti la bosi wake kwa lengo la kugonga na kufunguliwa kama ilivyokua siku zote lakini akahisi kitu tofauti sana na siku zote alizofika eneo hilo. Alisikia sauti za watu wengi wakiongea ndani ya geti hilo, alishindwa kuelewa maongezi yao yalikua yakimaanisha nini. Godfrey akasita kugonga mlango lakini akachungulia ndani huku akiongeza umakini katika sikio lake ili aweze kushuhudia na kuzibitisha alichokisikia. Akawaona wanaume tisa akiwemo mwenyekiti wa mtaa, katibu wa mtaa, mwenye nyumba pamoja na wengine wakiwa bize na maongezi mazito aliyohisi kama hadithi za bunuasi. Vilevile aliona idadi kubwa ya akina mama na watoto aliyoshindwa kupata idadi yake kamili lakini kilichomshangaza zaidi aliona bajaji anayoitumia kwenye shughuli zake ikipigwa picha ovyo na watu wale. Sauti kali na nzito ya mwenyekiti ikasababisha Godfrey ahisi dunia sio sehemu nzuri na salama kwake labda azikwe au ardhi ipasuke ajifiche.
ENDELEA
“Wiki haijaisha Colotlida alikuja ofisini kwangu kulalamika suala la Godfrey kuwa anamsumbua…kashamwambia kuwa hamtaki wala hataki mazoea nae lakini Godfrey hasikii na amekua king`ang`anizi kama kupe”
Mwenyekiti akavuta pumzi ndani kisha akaitoa taratibu kama mtu aliyechoka na safari ndefu ya muda mrefu, akaendelea
“Nasikia juzi pia Colotlida alimtukana Godfrey mbele ya halaiki ya watu, akimwita tapeli, mwizi na matusi mengine yasiyo elezeka mbele ya watu…Akamwambia akiendelea kumsumbua atampigia kelele za kutaka kumbaka. Hakika Colotilda alichukizwa na tabia ya Godfrey”
Mwenyekiti akameza funda dogo la mate kisha akakohoa kidogo ili kurekebisha sauti yake, akaendelea
“Mashuhuda wa tukio hilo wanadai Godfrey aliumia sana,mpaka akajikuta anatoa chozi mbele ya watu…hakika alipenda asipopendwa”.
Mwenyekiti akaweka nukta kisha akawatazama waliokua wakimsikiliza kwa umakini wa hali ya juu, akamuuliza mzee mwenye nyumba
“Hujawahi sikia mambo haya?”
Mzee Ramadhani Simba akajibu swali la mwenyekiti huku macho yake yakiendelea kukagua bajaji yake
“Sijawahi sikia taarifa hizo…Kinachonishangaza na kushindwa kuelewa kabisa ni hii picha ya Colotlida ilivyotapakaa damu. Tazama bajaji yangu ilivyochakazwa kwa damu katika siti za wateja…hali hii inaongeza mashaka na udadisi”
Akapumua sekunde kadhaa kisha akaendelea
“Yaani picha ya Colotlida ikutwe ndani ya bajaji anayoendesha Godfrey? Tena ikiwa na damu!, nina mashaka na usalama wa Colotlida kwa sababu hakuna uhusiano mzuri kati yao”
Akapumzika kama sekunde tatu kupisha maoni ya wengine alivyoona ukimya umetawala akaendelea na ufafanuzi wake
“Nahisi Godfrey atakua kamdhuru au kumuua kabisa Colotilda baada ya kuaibishwa na kutukanwa mbele ya watu, na kama sio hivyo damu na picha ya Colotilda vimefikaje kwenye usafiri huu?”
Mama mmoja wa makamo akachangia mada.
“Nasikia jana alichelewa kupaki bajaji tofauti na siku zingine za nyuma labda kuna uhusiano wowote na suala hili…Lakini tunapaswa kutoa taarifa mapema polisi ili wafanye uchunguzi haraka inavyowezekana”
Mzee Ramadhani Simba akapumzika kidogo kisha akaendelea na maneno yaliyoendelea kurarua moyo wa Godfrey
“Haya ndio masaa yake ya kuja kuchukua bajaji, nafikiri yupo njiani”
Akachukua simu yake ya mkononi kisha akatafuta namba aliyoijua mwenyewe kisha akaipigia. Kundi zima likamshangaa mzee Ramadhani Simba lisijue alikua akimpigia nani, ukimya ukatawala kila mtu akisikilizia mzee yule wa makamo ataongea nini haswa na anayempigia.
“Hallo! Afande Emmanuel Ngogo”
Upande wa pili wa simu ukaitikia
“Ndio mzee wangu, nakusikiliza”
Afande Emmanuel Ngogo aliitikia upande wa pili wa simu. Afande Emmanuel Ngogo alikua polisi maarufu mitaa hiyo kwa sababu ya uchapakazi wake anapoongozana na kikosi chake alichokiongoza kilichopachikwa jina la
‘Young Gifted Black’,
kikosi ambacho hakikua na sifa ya kuharibu kazi. Afande Emmanuel Ngogo alipendwa sana mtaani kwa sababu huwasaidia sana wakazi hao katika mambo mbalimbali yaliyohusu usalama wao na mali zao. Hakika alikua mtetezi wa wanyonge kama alivyoitwa na wengi.
“Hapa nyumbani kwangu kuna tatizo”
Mzee Ramadhani Simba akaweka nukta kisha akamtazama mwenyekiti, mwenyekiti akamuonesha ishara ya dole gumba akiwa na maana aendelea kuongea na afande huyo ili uchunguze yakinifu uanze mapema. Mzee Ramadhani Simba akamueleza kila kitu afande Emmanuel Ngogo kuhusu damu iliyotapakaa kwenye bajaji yake, suala la picha ya Colotilda pamoja na ugomvi wa Colotilda na Godfrey. Upande wa pili wa geti hali ilizidi kuwa mbaya kwa Godfrey, joto likazidi kupanda mwilini mwake, akahisi kuanguka kwa kizunguzungu cha hofu, nguvu zikamwisha. Mawazo tofauti yakaigombania akili yake mpaka akahisi kuchanganyikiwa, akashindwa kuelewa achukue maamuzi gani, aingie au aondoke haraka mahali hapo. Hata akiondoka aelekee wapi?.
“Nini tena hiki muumba wangu?”
Akajiuliza mwenyewe moyoni mwake. Wazo la ghafla likamjia, akakumbuka kituo cha polisi hakipo mbali na eneo hilo hivyo akizubaa watamkuta hapo hapo getini alafu akamatwe kizembe kama kondoo. Akaangalia kushoto kisha kulia akageka taratibu na kuanza kurudi alipotoka huku kichwa chake kikimuelemea kwa uzito wa mawazo.
“Sasa nakimbia nini? Hata sijui nahusika vipi… Colotlida kafanywa nini jamani?”
Godfrey akaongeza kasi japokua alikua hajui anaelekea wapi. Akahisi akienda katika chumba alipopanga itakua rahisi kukamatwa maana polisi lazima waanzie kule. Alitembea mpaka ilipo barabara kubwa inayoelekea ilipo baa ya Just in Time – Resort, akili ikawaza aeleke huko au laaah! Kipindi akiendelea kubishana na mawazo yake ghafla akasikia vilio vya ving`ora vya gari za polisi vikija kwa kasi eneo hilo. Hofu ikamjaa moyoni mwake. Sasa akahisi yupo mikonini mwa polisi. Akatazama kulia kisha kushoto akaliona jengo kubwa ambalo bado halijamalizwa kukarabatiwa, wazo likamjia ajifiche mapema ndani ya jengo hilo kabla hajakutwa na polisi hao aliohisi walikua wakielekea kwa mzee Ramadhani Simba baada ya kupigiwa simu na mzee huyo. Kwa mwendo wa haraka sana akaondoka barabarani kisha akaingia ndani ya jengo lile.
Baada ya kama sekunde kadhaa kupita, difenda mbili zilizojaa polisi vijana wenye hamu na hali ya kuchapa kazi kwa usahihi unaohitajika lilipita katika upeo wa macho. Godfrey alizishindikiza kwa macho difenda zile mpaka zilipokata kona kuelekea kwa bosi wake, Mzee Ramadhani Simba. Tukio lote hilo alilishuhudia kupitia dirisha la nyumba hiyo huku akiwa makini sana asije kuonwa na aliokua akiwatazama au raia wanaopita katika eneo hilo. Baada ya kujilizisha kuwa polisi wameshatokomea alipotoka, wazo la kuondoka eneo hilo likamjia. Akachungulia nje kwa mara nyingine, akajihakikishia usalama upo
“Hakuna cha kusubiri hapa ni kuchapa lapa tu”
Akili yake ikayapitisha mawazo hayo haraka sana kama mwanga wa kurunzi kwenye giza totoro, akasogea mpaka ulipo mlango alioingilia akachungulia nje, hali sio shwari. Akaona vijana pamoja na akina mama wakitembea kimakundi makundi
“Au wanajadili suala langu? Mungu wangu nimekwisha mimi…baba alinikataa, jamii nayo inaniandama kila siku duuuh! Leo hii sheria nao inachuki dhidi yangu…Hiyo picha yenye damu imefikaje kwenye bajaji yangu?”
Akaona mlango ule alioingilia haufai tena, akarudi ndani na kuelekea ulipo mlango mwingine upande wa uwani ili autumie kutoka. Akafuata korido ndefu kuelekea upande wa uwani ulipo mlango wa kutokea, kabla hajaufikia mlango huo ghafla akasikia sauti za watu wakiongea upande ule anaoelekea. Hofu ikamtanda moyoni, pasipo kutarajia akakata kona kulia na kuingia katika chumba kilicho karibu zaidi na mlango huo kwa lengo la kujificha asije kuonwa na watu hao.
Akili yake yote ikatazama mlango wa chumba kile alichoingia ili kuona kama wale watu watapita au kuingia katika chumba alichomo. Akazisikia sauti zile zikiendelea kuongea nje ya jengo lile lakini baada ya kama dakika kumi ukimya ukatawala eneo lile, akasubiri zaidi kama dakika tano akaona hali ya ukimya imetawala kama awali. Hali ya amani ikarudi katika moyo wa Godfrey na akaona huo ndio muda muafaka wa kuondoka lakini kabda hajapiga hatua hata moja ya kuuruhusu mwili wake kuondoka eneo hilo, pasipo kutarajia akasikia sauti asizozielewa ndani ya chumba hicho, katika kona ya upande wa kulia nyuma yake, hofu ikamjaa upya tena zaidi ya alivyokua awali. Nguvu zikamuisha na akahisi kuanguka lakini akajikaza kiume
“Hakika mbio za sakafuni huishia ukingoni”
Hiyo ndio sentensi iliyotawala akili ya Godfrey kipindi hicho. Taratibu akageuka na kuangalia upande aliposikia sauti zile, macho yake yakatua katika taswira alizoshindwa kuzielewa wala kuzielezea. Hofu ikazidi kuushambulia moyo wake bila kuupumzisha hata dakika moja. Aliona mabegi mawili makubwa ya rangi ya blue yakiwa yametelekezwa ndani ya chumba hicho, begi moja likiwa limetulia lakini begi la pili lilikua likicheza cheza taratibu kama vile limehifadhi kiumbe hai ndani yake. Hakika ndio lililotoa sauti zile alizozisikia awali. Akarudisha macho kutazama mlango alioingilia akaona upo shwari kabisa, akarudisha macho na kuyatazama yale mabegi, akili yake ikamsukuma kujua yale mabegi yana nini, hasa lile begi lililokua likicheza cheza.
KOSA
Akasogea taratibu tena kwa uangalifu wa hali ya juu mpaka yalipo mabegi yale, akayatazama vizuri ndipo alipohisi dunia sio mahala salama kabisa. Mabegi yote yalikua yametapakaa damu tena damu mbichi kabisa iliyokua ikiendelea kutengeneza mifereji mirefu. Godfrey alishindwa kuelewa nini kilichotokea na alipaswa kufanya nini ili kukwepa hatari aliyoona ipo mbele yake. Wazo jipya likamjia kichwani
“Hapa ni kuondoka tu, sipo mahala salama kabisa”
Akayatazama vizuri yale mabegi ndipo alipogundua kuna kitambaa cheupe katikati ya mabegi hayo, kipande kikubwa cha kitambaa hicho kilikua kimefichwa na mabegi hayo lakini kipande kilichokua kikionekana kilimuongezea udadisi Godfrey. Kitambaa kile kilikua kina maandishi ya damu lakini Godfrey alishindwa kuyasoma maandishi yote kwa sababu sehemu kubwa ya kitambaa hicho ilikua imejificha chini ya mabegi hayo. Akili yake ikamsukuma ainame na kukichomoa kile kitambaa ili agundue ujumbe uliokusudiwa kwenye kitambaa hicho. Akafanya kama akili yake ilivyohitaji, moyo wa Godfrey ukapiga Paaah!!! baada ya kuchomoa kitambaa kile na kuusoma ujumbe ulioandikwa. Maandishi mazito yaliyoandikwa kwa damu ya binadamu yalisomeka
'Very sorry marehemu’
Maandishi yale hayakua mageni hata kidogo kwa Godfrey, yamesharipotiwa sana kwenye vyombo vya habari. Mara nyingi hukutwa yameambatanishwa kwa watu waliouliwa kikatili. Kitambaa chenye maandishi yale kilikua gumzo nchini kwa sababu kilikua hakipiti kipindi kirefu bila kukutwa maiti iliyoambatanishiwa maandishi hayo. Miaka zaidi ya kumi na sita sasa serikali hailali usiku na mchana ikihangaika kuwatafuta wahusika wa mauaji hayo yanayoendelea kila siku iitwayo leo. Kilichowapa hofu zaidi serikali pamoja na raia wake ni watu waliokua wakiuliwa kikatili, walikua watu maarufu nchini yaani viongozi wakubwa wa nchi, mikoa, wilaya, wafanyabiashara wakubwa, matajiri na watu maarufu wa kada zingine kama sanaa, mitindo na wengineo. Mara chache sana kukuta mlala hoi asiye na mbele wala nyuma akiwa kauliwa alafu kaambatanishiwa kitambaa chenye maandishi ya damu kilichobeba ujumbe unaosomeka
'Very sorry marehemu’
ITAENDELEA
NB: * Mabegi yana nini?
- Yupo wapi God Mother?
- Nini hatima ya Godfrey?
- Colotilda ndio nani?
* Utunzi zaidi Instagram: immaphiri
Poor godfreyRIWAYA: AFISA USALAMA