RITA yapiga marufuku NIKAB

Status
Not open for further replies.
Tutalumbana na kutoleana lugha za ajabu ajabu sana hapa, lakini kusema ukweli hichoo kipengele No1 cha hilo tangazo hakifai katika jamii ya watu wenye imani tofauti...

Ni aibu kwa taasisi ya serikali kuweka tangazo ambalo liko biased, na lisilo na hekima namna hiyo...!
Suala la 'Maadili' linaingiaje hapo, especially kwenye hiyo namba moja?
Kwanini isitumike lugha mbadala ya aina ya ushauri kwa wale wanaovaa mavazi ya hivyo, ili aidha siku wakienda hapo wajiandae na option nyingine, kama ni lazima kabisa kutovaa hayo mavazi?

Anyway, miaka fulani nilisoma somo linaitwa Organizational Behavior, nikajifunza kuwa unapoingia kwenye ofisi za taasisi fulani kwa mara ya kwanza, kuna viashiria fulani utakavyoviona ambavyo vitakupa picha ya taasisi hiyo!...na hivyo hutapata shida sana kujifunza namna ya kuenenda pindi uwapo hapo!

I think that office announcement says something about the workers, and their behaviors in there!
 
Sijachakachua mkuu

Premise yao ni "kwa vile taasisi inawndeshwa kimaadili", ikimaanisha kuwa chochote kitchofuata kita-base hapo. Kwa hiyo "mavazi yasiyofaa na yasiyo heshima" yote hayo ni kwa mujibu wa premise-maadili

Kwa hiyo ni sawa na kusema "nikab haifai kimaadili" au "nikab si vazi la heshima kimaadili"

Hakuna lenye afuweni hapo

Tangazo limekosa umakini, na kuonyesha dharau
Nadhani tatizo hapa ni definition ya hayo "maadili"...najua ni vigumu kupata concesus kwenye hili kwa sababu zaidi ni suala la opinion na sio hoja.

Labda tukibaki hapo kwenye "nikab" (vazi linalofunika uso wote...kuna mtu ameweka hapo juu picha lakini katika hiyo macho bado yanaonekana....zile zenyewe huwa na kitambaa chepesi hata macho hayaonekani!). Je uvaaji huu unafaa kwa "maadili" ya kitanzania? Labda mimi na wewe tujiulize tunajisikiaje tukikutana na mtu kajifunika uso wote namna hiyo? Je 'tunamtizama' mtu huyo kama mwenye maadili? Watanzania wengine (sijui wapo wengi kiasi gani!) wanasema uvaaji huo unatisha!

Kama nilivyosema mwanzo, nakubaliana nawe kuwa tangazo halikuandikwa vizuri. Tunaweza kwenda mbali zaidi kwa kusema tungetaka hilo tangazo liandikwe/lisomeke vipi ili kufikisha ujumbe wao vizuri zaidi badala ya kuishia kuwalaumu tu (Bahati nzuri wametaja mavazi wasioyapenda na pia premise yao).
 
ii
Licha ya kuwa RITA ina hoja ya msingi juu ya utaratibu wake wa kutohudumia watu wasiowaona nyuso zao lakini tangazo lao halijakaa kiheshima

Kininja ndio nini?

Kwa nini neno nikab lina alama ya nukuu?

Na wanaposema "mavazi yasiyofaa au yasiyo na heshima" wanakusudia kusemaje kuhusu vazi hilo wakati msingi wa hoja yao ni kuwa taasisi inawndeshwa kimaadili?
Mkuu Gaijin kwenye hili mimi niko na wewe, Rita wamekosea kwenye drafting ya tangazo lao. Ni kosa kuitaja Nikab kwenye kundi la mavazi yasiyofaa na yasiyo na heshima. Wangebainisha kuhusu umuhinu wa kuonekana uso kwenye issues za Rita halafu hayo mavazi yasifaa ndipo wangeingiza vimini na vitop. Kitendo cha kuichanganya nikab na vimini na vitop sio kuwatendea haki wenzetu Waislamu ingawa does not warrant maandamano!.
 
Hivi kwa kuandamana Waislamu watakuwa wanatetea dini yao au utamaduni wa kiarabu maana hivi vitu viwili ni mkanganyiko mtupu.
Isitoshe si ustaarabu wala utaratibu wa Kitanzania kwa mtu kutembea amejifunika utadhani kavaa sanda; binadamu tunatambuana kwa kutazamana usoni, hii michezo ya kuziba nyuso ni mazoea yasiyo ya kistaarabu; ni vizuri RITA wameliona hilo.
Hivi hao wavaa niqab picha zao za passport huwa zikoje?
Ni lazima watu tujifunze kuacha tamaduni zilizopitwa na wakati.

Sema yote lakini haki ya mtu lazima ieshimike.Ukisema ni utamaduni wa waarabu tu unakose coz culture is dynamic. Je dini na mavazi ya kikristo ni utamaduni wa watanzania?
 
Ndo tabu ya taasisi ikiwa na kiongozi mlokole yaani anasahau kuwa kuna watu wa mataifa!
Izo dress codes zingine sielewi why wanakata dsm joto kaptula ni jambo la kawaida!Ilo la kininja no comment!
Ni kama taasisi ya kidini au shule jamani KHAA.
 
.....
Mke wangu angekuwa anafanya kazi hapo ningemwambia avae hilo vazi, halafu mimi mwenyewe wala sihitaji waislam wengine ningemthibiti atakayemfukuza kazi..

Topical. polepole.
Vazi la Nikab haliruhusiwi pia katika ofisi za serikali Tanzania visiwani, hasa Pemba, sembuse Dar?
Ukifika katika ofisi za idara ya barabara kisiwani Pemba (Deprtment of Roads), jirani na jengo la Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), kuna matangazo kwenye ofisi hizo kwamba vazi la Kininja 'Nikab' haliruhusiwi mahali hapo, na watu wanaheshimu tangazo hilo na kupata huduma zao kama kawaida. Mbona mnakomalia tangazo la RITA tu? Kwenye ofisi zinazotoa pasi za kusafiria pia wamepiga marufuku vazi hilo. Kama kuna mtu yuko Pemba, afike mahali hapo nilipotaja na kupiga picha tangazo hilo. Tusiwe na double standard.

 
Nadhani tatizo hapa ni definition ya hayo "maadili"...najua ni vigumu kupata concesus kwenye hili kwa sababu zaidi ni suala la opinion na sio hoja.

Labda tukibaki hapo kwenye "nikab" (vazi linalofunika uso wote...kuna mtu ameweka hapo juu picha lakini katika hiyo macho bado yanaonekana....zile zenyewe huwa na kitambaa chepesi hata macho hayaonekani!). Je uvaaji huu unafaa kwa "maadili" ya kitanzania? Labda mimi na wewe tujiulize tunajisikiaje tukikutana na mtu kajifunika uso wote namna hiyo? Je 'tunamtizama' mtu huyo kama mwenye maadili? Watanzania wengine (sijui wapo wengi kiasi gani!) wanasema uvaaji huo unatisha!

Mimi sioni tatizo lolote la mtu kuvaa hivyo. Nikimkuta amevaa hivyo, nitamheshimu tu kama atakavyoniheshimu mimi. Kama kutishika, natishika zaidi na mtu anaepaka mkorogo kwa mfano, lakini hatuwezi kutarajia tangazo la RITA kusema "hatutamuhudumia yoyote atakaepaka mkorogo kwa sababu ni kinyume na maadili"

Huduma ya serikali haitakiwi ku-base kwenye maadili, kwa sababu uvunjifu wa maadili si kosa kisheria. Serikali inaponyima watu huduma kwa misingi ya kuvunja maadili ni kwenda kinyume na katiba ya nchi. Tukumbuke hilo kwanza kabla hatuja chambua maadili yenyewe ni nini.

Pili, hao wanaovaa hivyo wanarejelea kifungu cha katiba kinachompa mtu uhuru wa kuabudu. Kwa hiyo serikali haiwezi kuvunja kifungu cha wazi cha katiba kwa kufuata tu maadili ambayo wameya define kwa opinion tu za watu fulani fulani

* Zile zenyewe kwa mujibu wa nani?


ii Mkuu Gaijin kwenye hili mimi niko na wewe, Rita wamekosea kwenye drafting ya tangazo lao. Ni kosa kuitaja Nikab kwenye kundi la mavazi yasiyofaa na yasiyo na heshima. Wangebainisha kuhusu umuhinu wa kuonekana uso kwenye issues za Rita halafu hayo mavazi yasifaa ndipo wangeingiza vimini na vitop. Kitendo cha kuichanganya nikab na vimini na vitop sio kuwatendea haki wenzetu Waislamu ingawa does not warrant maandamano!.

Hili hali warant maandamano lakini lina warant kukemewa vikali na Watanzania wote. Hiyo ni ofisi ya serikali na inapaswa kuwa na mtazamo neutral kwa wananchi wote, na sio kuonyesha unfounded dharau kwa baadhi ya watu. Kwa sababu ofisi hiyo ikiulizwa Maadili ya Mtanzania ni yepi, haiwezi kujibu hilo kamwe

Pia inafaa kukemewa kwa kutudhalilisha Watanzania kwa kuandika utumbo kama huo usokosa mantiki kinadharia na hata kiuandishi. Ofisi ya serikali inaandika hivi, inatoa picha gani kwetu Watanzania?
 
Tatizo letu sisi tuna Matatizo ya Kuamini kuwa kila kitu kuhusu Maadili ni kuoneana hasa hili la Mavazi. Je? Umewahi kuona Nywele na Masikio vya Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani - Hajjat Mwantumu Bakari Mahiza siku zote toka awe Mwislam! Na Je? Umewahi kuona pia vya Mheshimiwa Waziri wa Nchi ofisi
ya Rais Utawala Bora - Hawa Ghasia!

Hii ni mifano tosha kwetu kuhusu waislamu wenye kuonwa kila siku, hawa niliowataja hapa ni Musilm tena Siku wamejipambanua hivyo! Ndugu zangu watanzania Hebu tujadili mambo ya Msingi katika Taifa letu! Hili swala la Mavazi tena Kufunga au kufungua Uso mbona halina Mashiko!

Nchii hii bado hatujafanikiwa kuwakabili Serikali na Gharama za Kupanda kwa Bei ya Umeme! Mafisadi bado wanatamba! Bunge kujiongezea Posho! Na Mengine Mengi.

Hivi yote haya hatujayaona na kuuamua Kundamana kwa Dhati au ndo Kidato kinasumbua ndugu zangu! Watanzania tuache unafiki wa kujifanya tunathamini sana Dini na Mavazi yake wakati ni Wezi na Dhuluma imetujaa! Mimi nilidhani Waislam tunaandama
kudai kupitisha Michango kwa Kila Msikiti ili tujenge Hospital Kubwa na Kisasa au tunaandama Waislam wenzetu hasa walioko madarakani sasa hivi wajesahau sana katika kuchochea Maendeleo katika Taasisi zetu!

Mimi nadhani hata leo Rais Kikwete na Makamu wa Rais Bilal tukiwaita na baadhi ya Waislamu wengine Serikalini bado Swali linarudi kwetu! Tunanini Mkononi ?.

Wakati sisi tunataka Misikiti Mikubwa na ya Kifahari wenzetu wanajenga Maabara za Kisasa ndani ya Hospitali zao!

Wakati sisi tunawaza maandamano ya Niqab wenzetu wanaandama ndani ya Makanisa yao
na kuongeza idadi ya Seminari zenye uwezo wa Kutoa Form Four - A- ya Kila Mchepuo sisi ni Mashaidi Shule gani Zinaongoza kwa Kila Mwaka!

Wakati sisi tunazidi kupoteza Muda na Swali la Kwanini wenzetu wanapoteza Muda na kuongeza pale Palipopungua!

Ndugu zangu waislamu ni lazima tufike Mahali tujiulize kwanini wao isiwe sisi ? Kasumba ya kufoka kutunisha misuli bado haijatusaidia mimi naamini tunaweza kusonga endapo tutakaa chini na kuamua kusonga mbele!

Wako wengi tu ambao ni ndugu zetu watatusaidia katika mikakati yetu! Mfano, Wafanyabiasha - Bakharesa, Jitu Patel, Yusuph Manji,Zakaria. Maofisini - Dr Ramadhan Dau,Idd Azzan, na Wengine Wengi


Asante sana! Umeeleza kile kinachotakiwa kufuata, ifike wakati juhudi zielekezwe kwenye mambo yenye tija
 
Labda ni kwa usalama zaidi.
RITA wataweza lakini kupambana na hiyo vita yake.
 
Huu ni ubaguzi wa kidini yaani Nikab inafananishwa na Vitop na Sketi fupi. hii nidharau kupita kiasi, yaani mwanamke anatakiwa ajistili wao wanataka avae vipi hata ni ofisi ya serikali. hapo hata masista hawataruhusiwa?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom