RITA yapiga marufuku NIKAB

Status
Not open for further replies.
Sasa tutajuwaje hilo ni dume au la? Na hiyo picha kweli utaitumia kwenye vitu official kama passport etc?

attachment.php

Hii Kali.....unamhudumia vipi binadamu huyu... Kesho na keshokutwa likitokea jambo halafu ukaambiwa umtambue mahakamani kuwa ndiye uliyemhudumia unajibuje???
 
Ile ya NINJA kusema kweli imepita mpaka ni utamaduni wa Watu wa Iran, Yemen na AfghanStan kuzia vumbi la mchanga uendao kasi jangwani lakini bongo imekuwa fashion.. hao waislaam watakao andamana wangefanya hivyo kupinga uvaaji nguo za uchi (zilizokatazwa kidini) na sii kulilia utamaduni wa watu wengine..
mmmh! If u want to criticiz othrz, ctrciz the way u want them to crtcz you, the word "uchizi" n la kuudhi kdogo
 
Hivi kwa kuandamana Waislamu watakuwa wanatetea dini yao au utamaduni wa kiarabu maana hivi vitu viwili ni mkanganyiko mtupu.
Isitoshe si ustaarabu wala utaratibu wa Kitanzania kwa mtu kutembea amejifunika utadhani kavaa sanda; binadamu tunatambuana kwa kutazamana usoni, hii michezo ya kuziba nyuso ni mazoea yasiyo ya kistaarabu; ni vizuri RITA wameliona hilo.
Hivi hao wavaa niqab picha zao za passport huwa zikoje?
Ni lazima watu tujifunze kuacha tamaduni zilizopitwa na wakati.

Mbona hatuoni mtu kutetea utamaduni wa Kiafrika wa kuvaa kipabde cha ngozi mbele na nyuma kuwacha makalio wazi.
 
Hii Kali.....unamhudumia vipi binadamu huyu... Kesho na keshokutwa likitokea jambo halafu ukaambiwa umtambue mahakamani kuwa ndiye uliyemhudumia unajibuje???

Ahudumiwe na mwanamke mawenzie, kwani lazima amuoneshe kila mtu sura yake?
 
awe MKRISTO au MUISLAM kinachotakiwa ni kuvaa mavazi ya heshma kuusitiri mwili wake, sasa hayo ya kuvaa NINJA yanahatarisha usalama wa raia wengine
 
Hivi kwa kuandamana Waislamu watakuwa wanatetea dini yao au utamaduni wa kiarabu maana hivi vitu viwili ni mkanganyiko mtupu.
Isitoshe si ustaarabu wala utaratibu wa Kitanzania kwa mtu kutembea amejifunika utadhani kavaa sanda; binadamu tunatambuana kwa kutazamana usoni, hii michezo ya kuziba nyuso ni mazoea yasiyo ya kistaarabu; ni vizuri RITA wameliona hilo.
Hivi hao wavaa niqab picha zao za passport huwa zikoje?
Ni lazima watu tujifunze kuacha tamaduni zilizopitwa na wakati.

huijui dini ya kiislam, bora unyamaze kuliko kuongea utumbo....
 
Hivi jamani tumeridhika kwa ofisi ya serikali kuwa na tangazo rasmi lililovunja maadili ya uandishi namna hiyo?

Nadhani hilo ni tatizo kubwa mno kuliko hata hayo maudhui
 
Ile ya NINJA kusema kweli imepita mpaka ni utamaduni wa Watu wa Iran, Yemen na AfghanStan kuzia vumbi la mchanga uendao kasi jangwani lakini bongo imekuwa fashion.. hao waislaam watakao andamana wangefanya hivyo kupinga uvaaji nguo za uchi (zilizokatazwa kidini) na sii kulilia utamaduni wa watu wengine..

Si kweli.

Na kuvaa suruali na koti na tai na jinsi za kubana makalio na kuweka chupi nje (KK) ni utamaduni wa Kiafrika?
 
Nikab inapinga maadili ya utambuliko wa mtu pia yale ya kitanzania kwa kuleta ya kiiran. Are we together dude? Maadili mengine inayopinga ni ile hali ya kuwa vazi la kudhalilisha sawa na yale ya kuonyesha uchi. Too much of anything is always poisonous.

Inaitwa NIKAB/NIQAB au HIJAB?
 
Ngoja wakumbane na wanawake wanaojuwa haki zao waende pale uone kazi itavyokuwa kazi.
 
Hivi jamani tumeridhika kwa ofisi ya serikali kuwa na tangazo rasmi lililovunja maadili ya uandishi namna hiyo?

Nadhani hilo ni tatizo kubwa mno kuliko hata hayo maudhui

kwa hiyo unatushauri kuandamana!? Lakini mi siandamani.
 
Mbona miaka yote mnaandamana mnapata nini,tumewazoea kwani hamna kazi ya kufanya ndo maana mnaishia vijiweni na watoto wenu ndo maana mnafeli sana vidato.

wewe na makalio yako ndio mna kazi ya kufanya
 
Ile ya NINJA kusema kweli imepita mpaka ni utamaduni wa Watu wa Iran, Yemen na AfghanStan kuzia vumbi la mchanga uendao kasi jangwani lakini bongo imekuwa fashion.. hao waislaam watakao andamana ni machizi tu maana kama kuandamana wangefanya hivyo kupinga uvaaji nguo za uchi (zilizokatazwa kidini) na sii kulilia utamaduni wa watu wengine..

Chizi ni wewe na family yako na ukoo wako,kama huna chakuchangia kaa kimya sio kudharau imani za wengine
 
Hapa kinachoandamwa ni ushamba wa kufakamia mila za watu. Kwanini hawatetei kaptula hawa wanaodhani wanachokozwa waislam? Mbona kabla ya kufanyika mapinduzi ya Iran mwaka 1978 hatukuwahi kuona ninja? Kwani uislam umeanza jana au ni ujuha na ushamba wa wanaovaa ninja wakidhani wanajisitiri wakati ni kujidhalilisha. Kwanini kumfunika mkeo kama maiti kwenye hiyo sanda bila kungoja afe?
hujui usemalo, unaongea kama umefungiwa ndani ya mtungi kilaza wewe
 
..Na wanaposema "mavazi yasiyofaa au yasiyo na heshima" wanakusudia kusemaje kuhusu vazi hilo wakati msingi wa hoja yao ni kuwa taasisi inawndeshwa kimaadili?

Gaijin, "umechakachua" kidogo walichokisema kwenye hilo tangazo...wamesema "mavazi yasiofaa na yasio na heshima". Sina hakika hiyo nikab inaangukia upande upi...inawezakana ni ule wa "mavazi yasiofaa".

Lakini kwa vyovyote vile hakukuwa na umakini wa kutosha katika kuandaa tangazo hilo. Sioni hata nembo za hao RITA, isijekuwa tunajadili kitu ambacho hakipo!
 
Ile ya NINJA kusema kweli imepita mpaka ni utamaduni wa Watu wa Iran, Yemen na AfghanStan kuzia vumbi la mchanga uendao kasi jangwani lakini bongo imekuwa fashion.. hao waislaam watakao andamana wangefanya hivyo kupinga uvaaji nguo za uchi (zilizokatazwa kidini) na sii kulilia utamaduni wa watu wengine..

uhuru wa kuabudu uko wapi??? serikali gani inayoingilia uhuru wa kuabudu wa raia wake??? kama RITA ni taasisi ya serikali kwa nini iingilie uhuru wa kuabudu??? maana kumzuia mtu kuvaa mavazi kama imani yake inavyo mwambia ni sawa na kuingilia uhuru wake wa kuabudu.... hapo kikubwa ni kupinga NIQAB hayo mengine ni kuzuga tu..... Takbirrrrrrrrrrr
tutapambana mpaka tone la mwisho la damu
 
Gaijin, "umechakachua" kidogo walichokisema kwenye hilo tangazo...wamesema "mavazi yasiofaa na yasio na heshima". Sina hakika hiyo nikab inaangukia upande upi...inawezakana ni ule wa "mavazi yasiofaa".

Lakini kwa vyovyote vile hakukuwa na umakini wa kutosha katika kuandaa tangazo hilo. Sioni hata nembo za hao RITA, isijekuwa tunajadili kitu ambacho hakipo!

Sijachakachua mkuu

Premise yao ni "kwa vile taasisi inawndeshwa kimaadili", ikimaanisha kuwa chochote kitchofuata kita-base hapo. Kwa hiyo "mavazi yasiyofaa na yasiyo heshima" yote hayo ni kwa mujibu wa premise-maadili

Kwa hiyo ni sawa na kusema "nikab haifai kimaadili" au "nikab si vazi la heshima kimaadili"

Hakuna lenye afuweni hapo

Tangazo limekosa umakini, na kuonyesha dharau
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Tatizo letu sisi tuna Matatizo ya Kuamini kuwa kila kitu kuhusu Maadili ni kuoneana hasa hili la Mavazi. Je? Umewahi kuona Nywele na Masikio vya Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani - Hajjat Mwantumu Bakari Mahiza siku zote toka awe Mwislam! Na Je? Umewahi kuona pia vya Mheshimiwa Waziri wa Nchi ofisi
ya Rais Utawala Bora - Hawa Ghasia!

Hii ni mifano tosha kwetu kuhusu waislamu wenye kuonwa kila siku, hawa niliowataja hapa ni Musilm tena Siku wamejipambanua hivyo! Ndugu zangu watanzania Hebu tujadili mambo ya Msingi katika Taifa letu! Hili swala la Mavazi tena Kufunga au kufungua Uso mbona halina Mashiko!

Nchii hii bado hatujafanikiwa kuwakabili Serikali na Gharama za Kupanda kwa Bei ya Umeme! Mafisadi bado wanatamba! Bunge kujiongezea Posho! Na Mengine Mengi.

Hivi yote haya hatujayaona na kuuamua Kundamana kwa Dhati au ndo Kidato kinasumbua ndugu zangu! Watanzania tuache unafiki wa kujifanya tunathamini sana Dini na Mavazi yake wakati ni Wezi na Dhuluma imetujaa! Mimi nilidhani Waislam tunaandama
kudai kupitisha Michango kwa Kila Msikiti ili tujenge Hospital Kubwa na Kisasa au tunaandama Waislam wenzetu hasa walioko madarakani sasa hivi wajesahau sana katika kuchochea Maendeleo katika Taasisi zetu!

Mimi nadhani hata leo Rais Kikwete na Makamu wa Rais Bilal tukiwaita na baadhi ya Waislamu wengine Serikalini bado Swali linarudi kwetu! Tunanini Mkononi ?.

Wakati sisi tunataka Misikiti Mikubwa na ya Kifahari wenzetu wanajenga Maabara za Kisasa ndani ya Hospitali zao!

Wakati sisi tunawaza maandamano ya Niqab wenzetu wanaandama ndani ya Makanisa yao
na kuongeza idadi ya Seminari zenye uwezo wa Kutoa Form Four - A- ya Kila Mchepuo sisi ni Mashaidi Shule gani Zinaongoza kwa Kila Mwaka!

Wakati sisi tunazidi kupoteza Muda na Swali la Kwanini wenzetu wanapoteza Muda na kuongeza pale Palipopungua!

Ndugu zangu waislamu ni lazima tufike Mahali tujiulize kwanini wao isiwe sisi ? Kasumba ya kufoka kutunisha misuli bado haijatusaidia mimi naamini tunaweza kusonga endapo tutakaa chini na kuamua kusonga mbele!

Wako wengi tu ambao ni ndugu zetu watatusaidia katika mikakati yetu! Mfano, Wafanyabiasha - Bakharesa, Jitu Patel, Yusuph Manji,Zakaria. Maofisini - Dr Ramadhan Dau,Idd Azzan, na Wengine Wengi
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom