RITA yapiga marufuku NIKAB

Status
Not open for further replies.

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
rita.jpg

Kuna taarifa kuwa kuna maandamano na matamko makali yanaandaliwa na waislam kupinga wanawake ambao ni wateja na wahitaji huduma wa kiislam kupigwa marufuku kwenda kwenye ofisi za idara hii ya serikali.

Hivi kweli waislam wakilalamika wataambiwa wakorofi na wanaendekeza udini?
 
Ile ya NINJA kusema kweli imepita mpaka ni utamaduni wa Watu wa Iran, Yemen na AfghanStan kuzia vumbi la mchanga uendao kasi jangwani lakini bongo imekuwa fashion.. hao waislaam watakao andamana wangefanya hivyo kupinga uvaaji nguo za uchi (zilizokatazwa kidini) na sii kulilia utamaduni wa watu wengine..
 
Kuna watu huwa wanafurahia sana kuwachokoza waislamu? juzi ndanda wamefukuza wanafunzi 20 leo mjinga moja anataka kuleta dress code mbuzi..tutafika tu..

Mke wangu angekuwa anafanya kazi hapo ningemwambia avae hilo vazi, halafu mimi mwenyewe wala sihitaji waislam wengine ningemthibiti atakayemfukuza kazi..
 
Hivi kwa kuandamana Waislamu watakuwa wanatetea dini yao au utamaduni wa kiarabu maana hivi vitu viwili ni mkanganyiko mtupu.
Isitoshe si ustaarabu wala utaratibu wa Kitanzania kwa mtu kutembea amejifunika utadhani kavaa sanda; binadamu tunatambuana kwa kutazamana usoni, hii michezo ya kuziba nyuso ni mazoea yasiyo ya kistaarabu; ni vizuri RITA wameliona hilo.
Hivi hao wavaa niqab picha zao za passport huwa zikoje?
Ni lazima watu tujifunze kuacha tamaduni zilizopitwa na wakati.
 
Hivi kwa nini kila mara waislamu wanafikiri wanaonewa? kama swala ni kufunika uso hata masister hufunika lakini sijawahi sikia wakisema wataandamana. Sometimes nafikiri na elimu inasaidia kuepusha ukorofi wa mambo madogo madogo ya kiubinadamu kama haya.
 
Licha ya kuwa RITA ina hoja ya msingi juu ya utaratibu wake wa kutohudumia watu wasiowaona nyuso zao lakini tangazo lao halijakaa kiheshima

Kininja ndio nini?

Kwa nini neno nikab lina alama ya nukuu?

Na wanaposema "mavazi yasiyofaa au yasiyo na heshima" wanakusudia kusemaje kuhusu vazi hilo wakati msingi wa hoja yao ni kuwa taasisi inawndeshwa kimaadili?
 
Kuna watu huwa wanafurahia sana kuwachokoza waislamu? juzi ndanda wamefukuza wanafunzi 20 leo mjinga moja anataka kuleta dress code mbuzi..tutafika tu..

Mke wangu angekuwa anafanya kazi hapo ningemwambia avae hilo vazi, halafu mimi mwenyewe wala sihitaji waislam wengine ningemthibiti atakayemfukuza kazi..

Kikwete na Bilal wamelala nini? au wataamka baada ya 2015?
 
Licha ya kuwa RITA ina hoja ya msingi juu ya utaratibu wake wa kutohudumia watu wasiowaona nyuso zao ...
Na wanaposema "mavazi yasiyofaa au yasiyo na heshima" wanakusudia kusemaje kuhusu vazi hilo wakati msingi wa hoja yao ni kuwa taasisi inawndeshwa kimaadili?
Hueleweki!

Umeshasema RITA wana hoja ya msingi kukataa kuhudumia mtu wasiemwona usoni, hiyo ni kauli yako wewe. Sasa unakosoa nini tena kuhusu "msingi wa hoja yao"? Watanzania tuna matatizo makubwa sana ya kuwasiliana, ndio maana wakati mwingine sishangai nikisoma tangazo liliondikwa ovyo ovyo kama hilo, kwa sababu wasomaji wenyewe nao ndio wale wale.
 
Hapa kinachoandamwa ni ushamba wa kufakamia mila za watu. Kwanini hawatetei kaptula hawa wanaodhani wanachokozwa waislam? Mbona kabla ya kufanyika mapinduzi ya Iran mwaka 1978 hatukuwahi kuona ninja? Kwani uislam umeanza jana au ni ujuha na ushamba wa wanaovaa ninja wakidhani wanajisitiri wakati ni kujidhalilisha. Kwanini kumfunika mkeo kama maiti kwenye hiyo sanda bila kungoja afe?
 
Hueleweki!

Umeshasema RITA wana hoja ya msingi kukataa kuhudumia mtu wasiemwona usoni, hiyo ni kauli yako wewe. Sasa unakosoa nini tena kuhusu "msingi wa hoja yao"? Watanzania tuna matatizo makubwa sana ya kuwasiliana, ndio maana wakati mwingine sishangai nikisoma tangazo liliondikwa ovyo ovyo kama hilo, kwa sababu wasomaji wenyewe nao ndio wale wale.

Premise waliyoweka ni kuwa wanapinga baadhi ya mavazi kwa sababu taasisi yao inaendeshwa kimaadili.

Sasa wanaposema niqab hairuhusiwi ni kwa sababu inakiuka maadili? Gani?

*Hoja ya msingi ni kutohudumia watu wasiowaona nyuso zao, kinachonitatiza ni premise ya hoja hiyo.
 
Nikab inapinga maadili ya utambuliko wa mtu pia yale ya kitanzania kwa kuleta ya kiiran. Are we together dude? Maadili mengine inayopinga ni ile hali ya kuwa vazi la kudhalilisha sawa na yale ya kuonyesha uchi. Too much of anything is always poisonous.
 
Hivi maadili ya Kitanzania ndo yepi hasa? Manake kila mara nasikiaga maadili ya Kitanzania...mara sijui maadili ya Kiafrika....ndo yepi hayo?
 
Mbona miaka yote mnaandamana mnapata nini,tumewazoea kwani hamna kazi ya kufanya ndo maana mnaishia vijiweni na watoto wenu ndo maana mnafeli sana vidato.
 
ile ya ninja kusema kweli imepita mpaka ni utamaduni wa watu wa iran, yemen na afghanstan kuzia vumbi la mchanga uendao kasi jangwani lakini bongo imekuwa fashion.. Hao waislaam watakao andamana wangefanya hivyo kupinga uvaaji nguo za uchi (zilizokatazwa kidini) na sii kulilia utamaduni wa watu wengine..

huu ni wehu na wendawazimu_huko yemen na afghanistan kuna wanaume wanaovaa niqab kuthibitisha madai yako_au hilo vumbi ni kwa w/wake 2?
 
Ile ya NINJA kusema kweli imepita mpaka ni utamaduni wa Watu wa Iran, Yemen na AfghanStan kuzia vumbi la mchanga uendao kasi jangwani lakini bongo imekuwa fashion.. hao waislaam watakao andamana wangefanya hivyo kupinga uvaaji nguo za uchi (zilizokatazwa kidini) na sii kulilia utamaduni wa watu wengine..

vimini ruksa?,kanzu?
 
nikab inapinga maadili ya utambuliko wa mtu pia yale ya kitanzania kwa kuleta ya kiiran. Are we together dude? Maadili mengine inayopinga ni ile hali ya kuwa vazi la kudhalilisha sawa na yale ya kuonyesha uchi. Too much of anything is always poisonous.

utambuliko upi unaopingwa na nikabu? Kwa nani? Vimini na vitop hayo ni maadili ya wapi? America, uk, france ama vatican? Labda mwanamke mkatoliki akivaa nikabu kwake ni udhalili, kwa muislamu ni ibada yenye kumletea heshima
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom