Risasi yangu ya mwisho

Risasi yangu ya mwisho

NILIPOISHIA

MIMI 'Ah sore dada tatizo huyu jamaa anajikuta sana, machafu aliyoyafanya kwa watu kama ingekuwa watu wanamuhukumu kama anavyofanya yeye unadhani angekuwa hai! mimi asubuhi nakuja hukohuko halafu afanye alichopanga kunifanya.

Mama tunu alijitahidi kunisihi ili nisiende kwa ustadhi kwa maana nikienda kumwaga mbovu atazidisha hasira na tutaingiana maungoni.
Nilipinga kila hoja yake kwa kuushika ule msemo 'Jasiri anakufa mara moja tu ila muoga anakufa mara nyingi'

Msimamo wangu ulibaki pale pale kwamba asubuhi nitakwenda kukinukisha maana ndiyo risasi pekee niliyobaki nayo akilini mwangu ama inipe uhai (uhuru) ama inipe kifo (kichapo)


ENDELEA

Siku hii ilipita nikiwa na amani kabisa kwani roho yangu ilishachagua kujitoa muhanga kwa jitu lenye umbo kubwa na ubandidu mwingi (ustadhi)
Japo mimi ni mrefu lakini nilikuwa mwembamba tu kipindi hiko, si mnajuwa tena sikuwa na hela kama sasa🤣🤣

Kumbuka muda huu nilikuwa nisharudisha majeshi kwa bimkubwa.
Asubuhi mapema tu niliamka na nikiwa na furaha kabisa nilifanya shughuli ndogo ndogo za nyumbani huku nikisubiri kupambazuke kidogo (ili nikienda kujilipua kuwe na watu ambao watakuwa ni kama mashahidi wa kitakacho tokea) wamakonde tunasema chilume na oga.

Saa 1:30 asubuhi baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa Ochu kwamba ustadhi yupo nikajitia njiani.

Nilijitahidi kuvuta picha la kila ninachokihisi ni uonevu kwangu ili kuiita hasira, nilifanya hivyo hadi nikapata hasira ambayo iliniongezea ujasiri wa kuongeza mwendo huku nikitembea kikakamavu mno.

Nikatembea hadi kuanza kuiona nyumba yetu (niliyohama kwa muda) na nyumba ya Ustadhi.
Ochu na Mama Tunu walikuwa nje kwenye nyumba yetu, huku kwenye nyumba ya ustadhi hapakuwa na mtu nje.
Sikutaka kuwatazama sana akina Ochu kwani nilijua wangenitoa mchezoni na oparesheni yangu hii kuharibika.

Nilitembea hadi kwenye nyumba ya Ustadhi na kubisha hodi, hodi yangu iliitikiwa na mke wa ustadhi akaja nje. nikamuomba aniitie mumewe bila hata ya kumsalimia.
Muda huo kwenye paji la uso nimezibandika 111 mzee sina habari.

Mke wa ustadhi akaingia ndani na kumwita mumewe.

Ustadhi akatoka nje huku akionesha hali ya kunishangaa, muda huo nilikuwa nimemkazia macho nikiwa na usirias wa hali ya juu kama wale majambazi wa bongo muvi😠

MIMI "nimesikia unanitafuta kwa sababu nimeishi na mdogo wako numekuja sasa nifanye unachotaka kufanya"

Ustadhi alibaki kimya huku akiniangalia kama vile hanijuwi.

MIMI "Nimesikia unanitafuta unifundishe adabu kwa sababu nimetembea na mdogo wako nifundishe sasa hiyo adabu nataka kwenda"

Hapa Niliongea kwa kupayuka, nikamwona mke wa ustadhi akitoka ndani na kusimama mlangoni.

USTADHI "Kwahiyo ndiyo umekuja kuonesha ushababi wako hadi barazani kwangu si ndiyo"

"Ndiyo nimekuja kukuonesha kwamba mimi ni mwanaume nimeishi na mdogo wako na huna cha kunifanya, huna cha kunifa narudia. Wewe umeishi na wanawake wangapi ambao ni ndugu za watu, wewe umekamatwa ugoni mara ngapi na wake za watu walikufanya nini, eee walikufanya ninii? Wewe hukuwa unaiba vitu vya watu, walikufanya nini! walikufanya nini? Wewe hukuwa unam.omba dadaangu wewe na unafika hadi nyumbani kwetu mimi nilikufa nini? Nilikufanya ninii eee! Si nakuuliza mimi nilikufanya nini! Au ndiyo kwamba .uma ya mdogo wako inauma sana kuliko ya dadaangu! K.maamak. sasa nimukuja unipige, nipigee nipigee mse.ge wewee'

Nilipayuka huku machozi yakinilenga lenga hadi nikashindwa kuizuia hasira yangu na kumrukia shingoni ustadhi na kumkaba singland aliyoivaa.

Sikujua walimwengu walitokea wapi maana muda huo huo walinidaka na kunitenganisha na ustadhi, nilikuwa nalia kwa hasira huku nikijitahidi kujitoa maungoni mwa watu walionizingira kwa lengo la kunizuia. nilikuwa nalia huku nasema 'niacheni aniue si ananitafuta nimekuja sasa niacheni anipige aniue niacheniii'

Watu walionizingira akiwepo Mama Tunu na Ochu walinibeba juu juu hadi barazani kwetu, walinishusha na kutaka kuniingiza ndani lakini nilidinda, Ochu alikuwa akiniita kwa Nguvu huku akinisihi niwe muelewa lakini sikutaka kumsikiliza.

Hatimae wakafanikiwa kuniingiza ndani kimabavu na kunikalisha chini sebuleni, Mama Tunu aliongea sana ili kuninyamazisha matusi niliyokuwa nayatoa huku watu wamenishikilia bado. mwisho nilitulia na kulala chini huku nikiwa nalia kwa kulalama kwa kile nilichokiona ni uonevu dhidi yangu.

Macho yangu nilikuwa nimeyafumba, nilikuwa nasikia sauti tu za watu dirishani ambao nilijuwa ni wengi kutokana na mvumo wa zile sauti.

Baada ya muda kidogo ile hali ya hasira nikahisi kama imepungua, niliinuka na kuwaomba kina Ochu waniache maana bado walikuwa wamenishikilia, Mlango ulikuwa umefungwa nilipogeukia dirishani kulikuwa na watu wengi mno hasa wamama.

"Ochu niko sawa niacheni niende chumbani"

Niliongea kwa sauti ya kawaida sana kiasi cha kuwaaminisha kwamba kweli nipo sawa.

Waliniacha huku bado wakiwa wananichunga kwa macho.

Nikaanza kutembea kuelekea ulipo Mlango wa chumba changu.

Wakati nafika Mlangoni ndiyo nikakumbuka kwamba sina funguo.

Nikamwomba Ochu funguo ambayo anayo wakati anaenda kunipa nikasikia sauti ya bimkubwa akiomba afunguliwe Mlango aingie ndani.

Mama Tunu akafungua bimkubwa akaingia kisha Mama Tunu akawashukuru watu wengine ambao walinishika na kuwaomba wakaendelee na mambo mengine.

Nilimsalimia bimkubwa na kumuaminisha kwamba niko sawa na kumuomba aniache kwa muda maana sikuwa najisikia kuongea na mtu yoyote.
Bimkubwa akanitaka tuondoke kwenda kwake maana hatujui Ustadhi atakuwa na maamuzi baada ya kilichotokea.
Nilimwambia bimkubwa kwamba nimeshakimbia sana sasa nataka kupumzika kama ataamua kufanya lolote acha anifanye tu.

Bimkubwa japo hakupendezwa na uamuzi wangu wa kubaki nyumbani lakini hakuwa na namna ya kunishawishi kunitoa mwisho akaondoka na kuniacha.

Nifungua chumba changu ambacho nilikiasi kwa masiku ya kuhesabika nikaingia na kukitazama kwa muda kidogo kisha nikatabasamu na kuanza kuweka vitu kwenye mpangilio.

Baadae nikahisi njaa inaniuma nikamwomba Ochu buku ili nikapige chai mgahawani, Ochu akasema haitakuwa fresh kutembea mtaani kwa sasa maana watu watanitazama kama kideo. Akatoka yeye na kwenda kuninunulia mazaga, nikashindilia na nikaenda kuoga na kujitupa kitandani kuubonda usingizi ambao niliumisi kwa muda mrefu.

Siku hii ilipita salama kabisa japo nilikuwa na hofu sana kwamba labda jamaa angeniibukia kishari usiku.

Baasi bwana... ikawa mchana ikawa usiku, ikawa mchana ikawa usiku.
Japo hofu haikukata mara moja lakini hakukuwa na jipya lolote tena kutoka kwa ustadhi.

Hofu yangu ilikuja kuisha siku moja ambayo tulikutana uso kwa uso mimi nikitoka mtaani yeye akiingia, aseee moyo ulinipiga nikaona leo ndiyo siku ya huyu jamaa kunivamia.
Nilitamani hata kubadilisha njia lakini hapakuwa na uchochoro mwingine labda kurudi nyuma jambo ambalo ingekuwa ni kumpa jamaa point 3 za mezani.

Nikauandaa mwili kwa ajili ya mapambano kisha nikaanza kutembea kikakamavu hadi tunakutana, nikamsalimia 'habari mjomba' akaitikia 'Salama' kisha tukapishana.

Na huo ndiyo ikawa mwisho wa hofu yangu kwake na halikotokea tukio lolote tena la kutatanisha baina yetu hadi leo hii.

Kwa sasa naishi mtaa wa pembeni kidogo na kina Ustadhi.
------------------------------------

Yule Dada ambae tumemtambua humu kama Mwanahamisi aliwahi kuja tena wakati mimi naishi pale ni kama mwaka hivi tangu lile tukio kupita. nikamtupia tena ndoano yenye chambo lakini wapi! Aliruka mita mia akisema siwezi kumuingiza tena kwenye aibu kama ile ya mwanzo.
Lakini raundi hii ile hali yake ya usikivu hafifu ilikuwa imezidi, na hata alipoondoka na kurudi tena kuwatembelea kina Ustadhi ile hali iliendelea kukomaa.

Hadi mara ya mwisho Yule dada alikuwa hasikii kabisa, yaani kama unataka kumwambia kitu kwa kutumia maneno utapayuka hadi nyumba ya saba watasikia.

Mara ya mwisho nilisikia yupo kwenye ndoa sijui kwa sasa.


MWIIIIIIIIiiiiiiiiiiiiiSHOOOoooooooooo

Kama una swali lolote ndani na nje ya kisa hiki karibu nitakujibu.

kama nina baya semeni...
 
Back
Top Bottom