BAADA YA SEHEMU HII, HIYO INAYOFUATA NI YA MWISHO.
NILIPOISHIA
Sikuwa naona raha ya kuishi mtaa wa Magomeni tena niliwaza kupanga nje ya mtaa huu lakini nilikamatwa na maswali kadhaa ikiwa ni pamoja na 'natoa wapi hela ya kwenda kupanga mahali'
niliwaza sana nalitatua vipi tatizo hili maana sasa naishi kama mkimbizi kwenye mkoa wangu, mwisho nikapata jibu kwamba niende kwa mwenyekiti wa mtaa ili anikutanishe na ustadhi nimtake radhi kwa kosa nililomkosea.
ENDELEA.
Nikamuibukia mwenye kiti wa mtaa na kumuelekeza shida yangu, Akaniuliza maswali mawili matatu nami nikamjibu huku nikanusha kabisa suala la mimi kuwa na mahusiano na Mwanahamisi na kusema akinikutanisha na ustadhi nitakubali kila kitu ili tu haya mambo yaishe.
Tukamaliza maongezi nikatokomea mtaani.
Baada ya kupita siku mbili nikaibuka tena kwa mwenye kiti ili kujua nini kinaendelea.
Mwenye kiti akasema ameongea na ustadhi lakini ustadhi amemuomba mwenye kiti aliache kama lilivyo hili jambo ili yeye anifundishe namna ya kuishi na watu.
Nilizidi kuvurugwa Baada ya kuambiwa maneno yale na mwenye kiti.
Mwisho alisema hili suala nimwachie yeye ndani ya wiki atalimaliza.
Baada ya kupita hiyo wiki mambo yalikuwa yale yale.
Bimkubwa mtaani habari ikamfikia juu ya kile kinacho endelea kati yangu na ustadhi, kwakuwa nilikuwa sipotei sana kwao kwa wiki zile siku moja aliniita na kuanza kunihoji, sikumficha chochote Bimkubwa nikamweleza kila kitu japo ilikuwa ni aibu lakini sasa maji yalishanifika shingoni.
Bimkubwa akaniahidi atakwenda kuongea na ustadhi Hassani ili kulimaliza hili jambo.
Baada ya Bimkubwa kukutana na ustadhi Hassani na kuongea nae bado msimamo wa ustadhi ulikuwa pale pale kwamba anataka kunifundisha adabu.
Bimkubwa akaniambia kwamba ataongea na wajomba ili wakaripoti kuhusu vitisho vya ustadhi ili likinikuta jambo lolote baya yeye ndio awe mtuhumiwa namba moja.
Wakati Bimkubwa anafanya harakati zake mimi pia nilikuwa nachora mbinu ili nipate hela ya pamoja ili nipate chumba mtaa mwingine nihame mtaa huu wa Magomeni.
Muda huo nilihamia kwa bimkubwa kwa muda japo nako nilikuwa siishi kwa kujiachia maana ni mtaa huu huu mmoja.
Siku moja mida ya saa 11 jioni nikapokea simu kutoka kwa Mama Tunu.
MIMI 'haloo dada'
YEYE 'Rajabu hujambo'
MIMI 'Sijambo habari za tangu juzi'
YEYE 'Salama tu nimepata nafasi ya kuongea na Mama Hawa (mke wa ustadhi) leo ameniambia kila kilichotokea unajuwa nimecheka!'
MIMI 'Mh ilikuwaje!'
YEYE 'Hahahaha! Yaani nyinyi watu mna vibweka, mwenzako kumbe ile siku aliambiwa atalala na hawa Chumbani kwa shehe maana ndiyo kuna vitu vingi vya kuvilinda, sasa ile siku ulivyompa karatasi kumwambia aende kulala unamsubiri ndiyo akaingia nayo kule Chumbani. Sasa wakati anazuga kusubiri Hawa alale akaanza kulala yeye.
Sasa Mama Hawa na shehe wamerudi ile alfajiri wakamuamsha akaenda Chumbani kwake, hawa walimuacha tu alale maana muda ule shehe alitoka kwenda kuwahi swala ya alfajiri.
Sasa Mama Hawa amekaa kitandani anaona kuna karatasi akaichukua akaisoma imeandikwa namba za simu na maneno JIFANYE KAMA UNAENDA KULALA MIMI NAKUSUBIRI.
Akafikiria sana ile karatasi inahusu nini upande mmoja alikuwa anawaza kama ni ujumbe kaandikiwa Mwanamisi lakini akili nyingine inakataa, akaona ngoja amsubiri mumewe amuulize. Mumewe aliporudi akampa ile karatasi, alipoisoma sasa ndiyo akaanza kubwabwaja Akaongea sana kwamba anaejifanya yeye ni mwamba kumfanyia fujo kwa familia yake atamkomesha ili iwe fundisho kwa wengine. Akamuamsha Mwanahamisi na kumuuliza akajifanya hajui chochote, palipokucha kidogo ndiyo akaenda kumwita mdogo wake yule Shaibu kuja nae kwao.
Alipofika akampa ile karatasi na kumwambia inabidi tujue hizi namba ni za nani. Shaibu akaanza kuziandika zile namba kwenye simu yake, sasa kila anavyo ziandika linatokea jina lako mpaka namba zote kumi zinaisha (Shaibu alikuwa na namba zangu)
mwisho akamuonesha ustadhi kwamba zinasoma Roja, we we we... Ustadhi hapo ndipo alipocharuka na kuzidi kufoka, ndiyo ule muda ambao alikuja nyumbani kwa spidi ile siku.
Shaibu akamwita mwana na kuanza kumuhoji, muda huo mwana alikuwa anajing'ata ng'ata tu, hahaha! Alichezea vifuti dada wa watu hadi akili ikamkaa sawa, kama unavyomjua shaibu tena kwa kupenda maungoni.
Muda ule ule Mwana akafungashiwa kila kilicho chake na kusindikizwa stendi safari ya kwao lindi.
Yaani alipo nisimulia nimecheka mpaka basi, kwanza wewe ilikukuta akili gani hadi ukaandika namba zako si ungeweka namba yoyote ile ambayo haipo hewani?'
MIMI 'Ah ndiyo ili ajali tu itimie niliwaza basi kama itakuja kutokea hivi!'
YEYE 'Hahaha! Jamani pole unajuwa kinachoendelea endelea hapa nyumbani sasa hivi'
MIMI 'Hapana'
YEYE 'Yule shaibu hapotei sana hapa mida ya mchana hasa shehe anapoenda kazini, nahisi wanahofia utakuja kuhamisha vitu vyako na kukimbia mtaa'
MIMI 'Kwahiyo wanataka wanizuie hata kama nikiamua kuhama!'
YEYE 'Ndiyo inavyosemwa na watu maana shaibu hana mazoea kuja huku mchana'
MIMI 'Ah huo itakuwa uboya sasa, kwanza ustadhi mwenyewe anajionaje, Anajiona mungu au! yeye amesha fanya uhuni kibao tu na watu hawakumuwinda kiasi hiki, ashazini na wake za watu ameawaachisha masomo watoto wa watu na mambo mengine ya ajabu mengi tu,
alishawahi kuishi na dadaangu mpaka anaolewa tena mimi nikiwa najitambua japo nilikuwa mdogo, yeye .uma ya mdogo wake ndiyo imemuuma kiasi hiki! Huu ni usen.ge sasa kesho asubuhi namjia huko huko afanye hicho anacho taka kunifanya'
YEYE 'Rajabu unajua kwamba unaongea na Dadaako lakini?'
MIMI 'Ah sore dada tatizo huyu jamaa anajikuta sana, machafu aliyoyafanya kwa watu kama ingekuwa watu wanamuhukumu kama anavyofanya yeye unadhani angekuwa hai! mimi asubuhi nakuja hukohuko halafu afanye alichopanga kunifanya.
Mama tunu alijitahidi kunisihi ili nisiende kwa ustadhi kwa maana nikienda kumwaga mbovu atazidisha hasira na tutaingiana maungoni.
Nilipinga kila hoja yake kwa kuushika ule msemo 'Jasiri anakufa mara moja tu ila muoga anakufa mara nyingi'
Msimamo wangu ulibaki pale pale kwamba asubuhi nitakwenda kukinukisha maana ndiyo risasi pekee niliyobaki nayo akilini mwangu ama inipe uhai (uhuru) ama inipe kifo (kichapo)
Nitaendelea wakuu 😂😂😂
SEHEMU INAYOFUATA NI YA MWISHO
kama nina baya semeni...