NILIPOISHIA
Nilipofika nikamwita akaitika nikamwambia "Mama faizi (wanasoma wote madrasa) amenipa hii namba amesema umpigie"
Akapokea karatasi mimi nikasepa na kurudi kwenye mtego wangu kuona kinachoendelea.
Nikamwona akiielekeza ile karatasi upande wenye mwanga ili aone vizuri.
Moyo ukapasuka kwa furaha baada ya kuona wote wanainuka kwenye mkeka na kuukunja.
Wakazama ndani huku mimi nikibaki nje kwani niliogopa kwenda ndani pengine usingizi ungeniharibia mpango wangu katika usiku ule.
ENDELEA...
Nilicheza karata zangu kifundi sana ili kuhakikisha Ochu na Mama Tunu hawaelewi kinacho endelea.
Nilikomaa hadi inaingia saa nne lakini mwana hakutokea, nikaona acha niendelee kukomaa pengine anasubiri mji uzidi kuwa kimya nikatulia zangu hadi inagonga saa 5 bado hakutokea, nikawaza nifanyeje ila akili ikaniambia pengine anaibuka punde.
Nilikaa hadi inagonga saa 6 hapa sasa nikaanza kujiambia pengine itakuwa amezingua ila hakutaka tu kunichana ukweli, lakini moyo wa matumaini bado haukufa moja kwa moja.
Kwa kuwa ni usiku sana nikaingia ndani na kwenda chumbani kwangu, nikafungua dirisha na kusimama kuona pengine mwana anaweza kutokea (chumba changu kilikuwa upande wenye nyumba yao)
Wakuu nilikesha nikiwa nimesimama hii siku, kama utani tu nilisika "swala.. swala.. swala.." kwenye vipaza sauti vya misikiti ikihashiria ni alfajiri, nikacheki muda kwenye simu ni saa 10 nikatega Alarm ya saa mbili kamili.
Nikajitupa kitandani na kulala fofofo.
Ilipofika saa 2:00 asubuhi Alarm ikaanza kunipigia makelele, nikaamka huku nimechukia sana maana usingizi ilikuwa haujanitosha kabisa.
Nilipokumbuka jana sijaenda kazini nikapata nguvu za ajabu nikaamka na kuanza harakati za kuingia kazini mara moja.
Nilipofanya kila kitu nikatoka nje ili kuanza safari ya kuelekea kazini, nikamwona mke wa ustadhi pale nje nikamsalimia na kumpita huku nikitupa jicho la upande upande pengine naweza kumwona mwana ndani lakini haikuwa hivyo.
Nikaendelea na safari yangu hadi mnadani, nikanunua sambusa na juisi na kuanza kula huku nikisubiri mnada kufunguliwa.
Mawazo ya kile kilicho tokea jana yakaanza kuja kichwani, swali kubwa ikiwa ni kwanini Mwanahamisi hakutokea kama tulivopanga, kama hakuwa akihitaji kuonana na mimi si angesema tu?
Baasi bwana... wanasema kwenye wengi hapaharibiki jambo, harakati za ma pointer na wauza bidhaa zikayasomba mawazo yangu na kuyarejesha kwenye mabishano yao ya simba na yanga ambayo wanaendelea nayo.
Mwisho mnada ukafunguliwa na harakati zikaanza rasmi.
Baada ya mnada kufungwa mida ya saa 7 kasoro nikapanga vizuri nguo zangu na kuingia mtaani kukimbiza.
Wakati nipo mtaani kichwa kishapata moto nishapiga vinguo viwili vitatu nikapokea simu ya Mama Tunu mama ambae naishi nae kama sista.
MIMI 'Naam dada'
YEYE 'Rajabu uko wapi sasa hivi?'
MIMI 'Nipo Soko kubwa huku sasa natembeza nguo'
YEYE 'Ahaa sawa kwani umemkosea nini ustadhi Hassani'
MIMI 'Ustadhi Hassani!!!'
YEYE 'Ndiyo ameongea sana asubuhi kabla wewe hujaamka, baadae akatoka akaongoza njia ya Chuno. amerudi wakati wewe umeondoka, amerudi na mdogo wake yule shaibu Wakaingia ndani kwake, sijuwi wamefanya nini huko ndani ametoka kwa kasi kuja huku kwetu muda huo mimi najiandaa kutoka, Akaniuliza Rajabu yupo? Mimi nikamwambia Hapana ametoka, akarudi kwake na mimi nikatoka kuja huku kazini'
Maneno ya Mama Tunu nikama yaliingia katika mfumo wangu wa ubongo na kuvuruga kila kitu kiasi cha kunifanya nione kama dunia inazunguka.
Niliwaza ni nini nimetokea hadi ustadhi anitafute huku ni kiwa na dhana ya kwamba asilimia 999.9 jambo hilo ni kuhusu Mwanahamisi.
Nilipouwaza mtanange wa ustadhi ndiyo nilizidi kuishiwa nguvu, Ustadhi anaogopeka kwa sababu ni mtata sana, zamani alikuwa muhuni ila akibadilika ukubwani tu na kumrudia mungu, kwahiyo ni mtu ambae ukimletea usela ama uhuni wa namna yoyote yeye hapeleki kesi sirikali ya mtaa bali anakutafuta mnamalizana kihuni, kama ni Mali yake umemzingua utairejesha kwa namna yoyote na kama ni ishu inayomshawishi kukudunda anakudunda haswa.
'Haloo Rajabu unanisikia?'
MIMI 'eee nakusikia Dada'
YEYE ' Nimekuuliza kuna kitu umemkosea?'
MIMI 'Hapana sijajuwa itakuwa ana ishu gani'
MIMI 'Ahaa sawa ila kuwa makini utakaporudi nyumbani uelewe kinaendelea nini kabla hamjaonana, maana mtu mwenyewe hachelewagi kufanya vitu vya hovyo yule'
MIMI 'Sawa nitafanya hivyo'
Akakata simu.
Nguvu zote ziliniishia nikashusha pumzi kubwa huku nikisogea kwenye kibaraza cha fremu ambayo imefungwa.
Nikavua begi mgongoni nikaliweka kwenye kibaraza, nikakaa chini kwa kujitupa huku nikiwaza umbo la Ustadhi na kulinganisha umbo langu na kuwaza itakuwaje akinitia mkononi😢. Nikaweka nguo zangu juu ya begi kuanza kutafakuri maneno ya Mama tunu huku nikijaribu kuikwepesha akili isihusianishe tukio la kuuliziwa na ustadhi na tukio la mahusiano yangu na Mwanahamisi.
Niliwaza sana hapo mwisho nikaona bora niendelee na harakati majibu sahihi nitayapata jioni.
Nikaendelea na kukuru kakara hadi inafika jioni.
Nikaanza safari ya kurudi home kama ilivo kawaida huku kichwani nikichora ni namna gani nitaingia home.
Hiyo ilikuwa ni saa 12 jioni.
Wakati nipo njiani nikapokea meseji ya Ochu.
'Oya home kuna msala huku. kumbe mzee ulikuwa unatafuna yule kuku kimya kimya tu, ku.amaake wewe jamaa nyoko'
Nilishindwa kujua nicheke au nifanyeje baada ya kuisoma meseji hii ambayo Ochu ameiandika kama kichekesho lakini imebeba ujumbe ulionitia ganzi mwilini.
MIMI 'Kuna msala gani kaka na Kuku gani huyo unamsema?'
YEYE 'Huyu wakienyeji hapa kwa Ustadhi, hapa ustadhi kachanganyikiwa kama ng'ombe aliyempoteza mwanae, kila baada ya dakika 5, 6 amekuja kuuliza kama umerudi hahaha! Mjomba umemchapa shehe kwenye mshono'
MIMI 'Duh mbona mimi sijala kwa yule dogo, kimetokea nini kwani?'
YEYE 'Hahahaha! Eti kimetokea nini! Mimi sijuwi lakini hapa tunapoongea dogo usingizi wa leo atauchapa kwao lindi maana ashafurushwa na virago vyake tangu asubuhi, sasa kama wewe unasema hujuwi kitu sawa ila ukiumana na ustadhi ndiyo tutajua upi mchele na zipi ni pumba hahahahaha...'
Nikachati na Ochu kwa muda huku akinipanga kila kinachoendelea home huku Mama Tunu nae akinipa Update kama nafatilia boli kupitia uzi wa Jf.
Nilipoona hadi saa moja na nusu inaingia na bado nyumbani kwangu kuna kisanga nikainuka mahali nilipokuwa nimekaa na kuanza safari ya kuelekea kwa bimkubwa ambapo ni mtaa huu huu wa Magomeni.
Nikafika kwa bimkubwa na kujifanya nimepita tu kumjulia hali na kuongea nae kidogo maana nilimmis sana siku ya leo.
Tuligonga sana stori na bimkubwa na sista hiyo siku.
Nilikaa hapo hadi saa nne, nikawaaga na kuondoka kuelekea home huku nikiwaambia begi nitalijia asubuhi.
Nikafika home na kukuta mtaa umepoa kabisa, Nikaingia magetoni baada ya kufunguliwa na Ochu.
Sikuwasha taa chumbani nilifanya harakati zite kwa kutumia mwanga wa screen ya simu tu hata tochi ya simu sikuthubutu kuwasha😂
Nilipoweka sawa kila kitu nikampanga Ochu mbinu ambayo tutaitumia kama ustadhi atakuja kugonga usiku.
japo nilikuwa na uchovu wa kukesha jana lakini usingizi ulijitenga na mimi kabisa huku hofu ikifungua mgahawa kabisa kwenye moyo wangu.
Mwisho usingizi uliichukua nafasi yake na kunifanya nisijuwe nini kinaendelea.
Kwenye mida ya saa tisa nilikurupuka na kuvaa nguo haraka haraka kisha nikatoka home na kutokomea mtaani.
Nili jilaani sana na kumlaani Ustadhi, mbwa anaenifanya nashindwa kupata usingizi wa kueleweka.
Niliwaza mshkaji gani naweza kwenda kumuamsha ili nipate hifadhi lakini nilighaili maana niliona sio freshi kwenda kwa mtu usiku vile.
Hapo kwa bimkubwa ndiyo sikutaka kwenda kabisa maana nilihofia kumpa maswali mengi na mwisho kujua kinachoendelea.
Niliishi kwenye maisha hayo kama wiki na masiku kadhaa hivi, swali la kwamba nini kilitokea bado lilikuwa ni mkate mgumu ambao chai ni Ustadhi, watu wake wa ndani na Mwanahamisi mwenyewe ambae siku anakunja mkeka kuingia ndani ndiyo ilikuwa siku yangu ya mwisho kumuona.
Nikamuomba Mama Tunu anifanyie ujasusi kwa mke wa ustadhi ili nijuwe nini kilifanyika hadi mimi napewa hizi tuhuma (muda huo mama Tunu na Ochu nishawapanga kila kitu)
Sikuwa naona raha ya kuishi mtaa wa Magomeni tena niliwaza kupanga nje ya mtaa huu lakini nilikamatwa na maswali kadhaa ikiwa ni pamoja na 'natoa wapi hela ya kwenda kupanga mahali'
niliwaza sana nalitatua vipi tatizo hili maana sasa naishi kama mkimbizi kwenye mkoa wangu, mwisho nikapata jibu kwamba niende kwa mwenyekiti wa mtaa ili anikutanishe na ustadhi nimtake radhi kwa kosa ambalo nimelitenda.
Nitaendelea wajumbe 😂😂😂