Ripoti ya Kifo cha Mwangosi

Ripoti ya Kifo cha Mwangosi

Kumbuka huyu jaji ni mmojawapo wa wale ................ Tazama taarifa ya Lisu. Naona Nchimbi alikuwa anataka kupigia mstari utetezi wa Lisu.
 
Kumbuka huyu jaji ni mmojawapo wa wale ................ Tazama taarifa ya Lisu. Naona Nchimbi alikuwa anataka kupigia mstari utetezi wa Lisu.

Jambo ambalo nimenishangaza ni kuchukua maoni ya Mukama kama yalivyo na kuyaingiza kwenye mapendekezo yao, na sijaona maoni yo yote kutoka Chadema. Hapa mizani inakosekana kwani ni pande mmoja unaoonekana kutendewa haki na upande mmoja kutotendewa haki stahiki ingawa ndio waadhirika wa matukio haya.
 
Ndiyo maana awali niliposoma ripoti ya Baraza la Habari Tanzania na Jukwaa la Wahariri Tanzania nilisema:

This leaves me to wonder kama ripoti ya Baraza la Habari Tanzania na Jukwaa la Wahariri Tanzania ndiyo hii, tutegemee nini kwenye hizo ripoti za Polisi na Nchimbi?
 
Tazama Ukurasa wa 29, ripoti inasema hivi "Hata hivyo uchunguzi hauwezi kuthibitisha kama mauaji hayo ya
Mwangosi yalipangwa
". Hii sio kazi yao. Hii ingeachwa mikononi mwa makachero waliobobea, wangeweza
kubaini hili.

Mkuu mazingira ya tukio lenyewe haliitaji uwe umebobea saana kitaaluma kutambua muuaji.Ni wale wale polisi waliokuwa wamemzunguka wakimpiga.
 
Mimi bado sijasoma ila lazima sitakubaliana na majibu ya uchunguzi sababu sikukubaliana na wachunguzi tanngu mwanzo
 
hawa jamaa bwana eti Just Kidding (JK) alitangaza kuwepo kwa zoezi la sense tarehe 26 August mpaka tarehe 8 September, na wakati inafahamika sensa ilikuwa ni wiki moja kabla ya kuongezwa siku saba na Mkurugenzi wa sensa tarehe 1 Sep.!! Hivi kulikuwa hakuna watu wa kuedit hiyo report kujaribu kufukia vitu vidogo kama hivi!!!
 
"Kwa misingi hiyo Kamati imeona kwamba nguvu iliyotumika mwanzo hadi kumaliza Operesheni haikuwa kubwa. Kuhusu tukio la kuuawa Bw. Daud Mwangosi na kuumizwa baadhi ya Askari Polisi halikustahili kabisa."

Hii sentence sijaielewa. Imeandikwa na Jaji, Wahariri (Editors) wawili na Kanali Dr mmoja!!!
 
Hawa akina Mukama wasituzingue, tangu lini siasa zikaamia kwenye miongozo ya spika kibao. Halafu spika mwenyewe kada pamoja na naibu wake wenyeviti na wabunge wa CCM ambao ni mavuvuzela tu. Siasa ziko mtaani kwa mikutano, maandamano, hamasa, nyimbo, ngoma nk.
CCM wanatafuta kila njia Watanzania wasielewe unafiki na udhaifu wao. Sekondari za kata zimeshawamaliza.
 
Naomba nisichangie chochote, kule facebook Mzee Mwanakijiji kila siku anatuhamasisha kila raia mmoja mmoja kuchukuwa hatuwa za kuibadili nchi yetu, mimi tayari najuwa ni nini cha kuwafanya hawa Polisi na mamluki wote. endeleeni tu kupoteza muda wenu hapa. mimi nafanya kwa vitendo.
 
Hawa akina Mukama wasituzingue, tangu lini siasa zikaamia kwenye miongozo ya spika kibao. Halafu spika mwenyewe kada pamoja na naibu wake wenyeviti na wabunge wa CCM ambao ni mavuvuzela tu. Siasa ziko mtaani kwa mikutano, maandamano, hamasa, nyimbo, ngoma nk.
CCM wanatafuta kila njia Watanzania wasielewe unafiki na udhaifu wao. Sekondari za kata zimeshawamaliza.

Bunge ni mhimili mmojawapo wa serikali, sasa inapopendekezwa kwamba itungwe sheria ya vyama vya siasa kuhamishai shughuli za siasa bungeni, ina maana bunge ligeuzwe kuwa kijiwe cha siasa hata mwenye ubongo mbovu hawezi kuelewa nini tumelogwa watanzania.

Si vyama vyote vyenye wawakilishi bungeni, kama mpango huo usio na dhana hata ya kufikirika kiakili kuhamishia vijiwe vya kisiasa bungeni, je vyama vya siasa ambavyo havina wawakilishi bungeni vinapewa nafasi gani?

Bungeni si mahala pa kufanya siasa, bungeni si mhimili wa siasa, bungeni si sehemu ya mipasho ya siasa, Bunge ni mhimili wa serikali wenye jukumu la kutunga sheria nchini na kuisimamia serikali. Mukama kazeeka vibaya kwa kauli yake, kamati ya Nchimbi iliyoidhia kauli ya Mukama hawakutuliza kichwa kabla ya kurudhia pendekezo hilo, tena ndani kukiwamo mwanasheria.
 
Ripoti ya kiingereza ya timu ya MCT inaelezea hali halisi ni nzuri sio kama hii ingine ya kiswahili,hii ya kiswahili bado sana tena sana ipo kisiasa zaidi zaidi kwa sana.
 
Wizi mtupu:

  • Ripoti inamakosa ya kiuandishi kibao kama vile wamekurupushwa kuitoa au haikuandaliwa na wataalamu
  • Ripoti haijazingatia miiko na maadili ya kumlinda mtoa taarifa. Majina ya watu walosaidia kueleza uovu mbalimbali yametajwa waziwazi kinyume na maadili ya utafiti(imelenga kuongeza uhasama)
  • Upelelezi umefanyika kwa kuangalia picha mnato ili iwe nini wakati kunapicha za video?
  • Bomu lilipingwa baada ya watu kutawanyika, Kwa hiyo ni kweli ilikuwa makusudi
  • Polisi mkubwa wao alishawahi kutoa taarifa ya uongo mara baada ya tukio akilenga kupotosha umma, akaaibishwa na picha na vielelezo mbalimbali vilivyoweka wazi ukweli. Kama alianza kwa kudanganya kwanini tusiamini kwamba ameendeleza kusema uongo kama jadi yake? eti anashauriwa afanye uchunguzi kabla ya kutoa taarifa, achunguze nini hali na yeye alikuwepo kwenye tukio na bado akasema uongo!
SIJAKUBALIANA NA SIASA ZILIZOJILI KWENYE REPOTI YA KAMATI HII
 
"Kwa misingi hiyo Kamati imeona kwamba nguvu iliyotumika mwanzo hadi kumaliza Operesheni haikuwa kubwa. Kuhusu tukio la kuuawa Bw. Daud Mwangosi na kuumizwa baadhi ya Askari Polisi halikustahili kabisa."


Hii sentence sijaielewa. Imeandikwa na Jaji, Wahariri (Editors) wawili na Kanali Dr mmoja!!!

Mkuu hii habari inatia mashaka sana yaani hawa jamaa ni wasomi kweli maake imekaa nyepesi sana kama imeandikwa na kijana wa form 2 wa shule za kata.Sasa ndio naamini kuwa Mh Tundu Lissu alisema huyu Jaji Ihema hana lolote yaani kama kweli hivi ndio hiyo tume ya Nchimbi Lol kweli hatuna viongozi maake aliyeunda tume ni kilaza na Jaji huyu nae kama Mh Tundu Lissu alivyosema hawezi hata kuandika hukumu si mmeona hii habari ilivyo nyepesi.
Mkuu pata muda soma uchunguzi wa ukweli uliotolewa na MCT ule ulioandikwa kwa Kiingereza then utaona hii ya nchimbi ni mbofumbofu kweli Bongo hakuna viongozi hawa jamaa walipata bahati sana ya ulaji huu wa pesa za walipa kodi.Wanacheza kitaeleweka tu!!
 
The dirty dozen hawa hapa;


View attachment 67749

Mods, naomba kwa mara ya kwanza toka nijiunge na JF nitukane mtu. Walioandika hii ripoti ingefaa wakamatwe mara moja na kufikishwa wanakostahili kwa uwongo na wizi wa kujipatia hela kwa njia ya udanganyifu bila kuifanyia kazi. Hawana tofauti na mlevi aliyeshiba pombe ya pingu na kama ilivyo kawaida kalowa na bila akili anajipitisha pitisha mbele za watu bila kujitambua kuwa anatoa harufu kali ya kunuka hadi hata nzi wanamkwepa. Naapa na nasema wazi kuwa kama moja wa hawa watu angekuwa ndugu yangu, nisingeongea naye tena katika maisha yangu...ni aibu, ni aibu na ni aibu. Halafu moja wao anajiita Jaji na mwingine anajiita Mwandishi, what? Hivi tumemkosea nini Mungu? Naomba niishie hapa!

Kama hukufunzwa kutukana huta kaa utukane. Umeomba kibali cha kutukana kisha umeshindwa kufanya hivyo.
 
Mimi najiuliza, KWA NINI TUNAFUJA PESA NA MALI ZA UMMA KWA UJINGA KAMA HUU? hebu tujiulize maswali haya
  • Kama usalama wa taifa wapo na walishindwa kukusanya na kuwasilisha taarifa za tukio la kupangwa na la wazi kama hili, je wanalipwa kwa kazi gani? Nilitegemea wangetuma ripoti zao za ukweli usiku uleule.
  • Usalama wameajiliwa kwa ajili ya kuchunguza au kubaini majambo ya sirini yanayolihusu taifa na mali zake wakiwemo watu, wanalipwa kwa kazi hiyo. iweje leo kupata ukweli wa kile tunachodhani kimefichika tunaunda tume/kamati wkati tayari kuna usalama?
  • Usalama, hamuwezi kutoa taarifa ya haya yaliyo uchi namna hii, je itakuwaje kwa yale ya sirini kama kutorosha faru? Kazi ipo.
  • Hili niliwazalo, ni ujinga wangu au ujinga wao? sipati jibu
 
Wameshatafuna mamilioni yao kama posho na kuandika ripoti ambayo imejaa *****!!! Kulikuwa hakuna sababu ya kuundwa tume ili ifanye kazi ya kisanii.
 
Hizi ripoti mbili tuzisome kwa uangalifu halafu tujadili. Moja imeandaliwa na baraza la habari Tanzania na nyingine imeandaliwa na kamati ya Nchimbi. Haya The Great thinkers your brain is needed now than ever.


Chief Mkwawa wa Kalenga
pale fedha zetu zinapotumika kumaka mkaa badala ya rangi inauma sana.
 

Attachments

Hii Serikali ilishapoteza credibility yake siku nyingi sana. Na haitaki kujifunza kutokana na makosa ya nyuma bado inaendelea kufanya madudu tu kila kukicha. Kinachosikitisha ni kwamba Serikali hii bado itakuwepo madarakani kwa miaka mitatu mingine, muda ambao ndio watazidi kuiangamiza nchi kwa madudu yao mbali mbali.
 
Ahsante mkuu...nimeisoma.... lakini nadhani jina la Kamati ya kusafisha jeshi la polisi ndio lingewafaa sana
 
Back
Top Bottom