Maswali hayo yanatokana na Kamati kushindwa kuweka hadharani ripoti ya kiini cha mauaji hayo ya kinyama yaliyofanywa na baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi kutokana na kesi hiyo ya Mahakamani ingawa ripoti tumeelezwa hiyo ipo.Siku tatu baada ya Mwangosi kuuawa kikatili, Waziri wa Mambo ya Ndani, Nchimbi aliwaeleza Waandishi wa habari kuwa atalishughulikia suala hilo kwa haraka na kuhakikisha wale wote waliohusika wanafikishwa mahakamani.Siku mbili kabla ya maandamo ya Waandishi wa Habari kulaani mauaji hayo, Nchimbi aliwatia moyo waandishi wa habari na tayari alikuwa amekwishaunda Kamati ya kuchunguza mauaji hayo. Tunahoji kama Nchimbi alifahamu kwamba matokeo ya ripoti ya Kamati kuhusu kiini cha kifo cha Mwangosi haiwezi kuwekwa hadharani, alikuwa na haja gani ya kuunda kamati hiyo?Kama kweli pia alikuwa na dhamira ya dhati katika kulishughulikia jambo hilo, kwa nini mtu anayedaiwa kumuua Mwangosi alifikishwa mahakamani na kisha siku chache baadae akaunda kamati?