Ripoti ya Kifo cha Mwangosi

Ripoti ya Kifo cha Mwangosi

watanzania wote tumekuwa vichwa vya waenda wazimu...! matumizi mabaya ya kodi zetu na haya matume yasiyoleta ukweli
 
Hii ni janja nyingine ya kuthibiti vyama vya siasa vya upinzani, eti sheria ya vyama iangaliwe ili kuwezesha siasa zihamie bungeni baada ya uchaguzi. Hapa CCM wanajaribu kuhifadhi ngome zao za vijijini. Lakini kuiosha polisi kuwa hawahusiki na mauwaji ya Mwangosi ni kujichanganya maana kila kitu kipo wazi.
 
kwa hili, nchimbi kapotea zaidi, pamoja na kujitetea kote, lakini sicho tulichotazamia katika report hii
 
Nzuri...ila imewananga CDM...imeuma imepuliza...all in all imesema watuhumiwa wachukuliwe hatua
 
Hiyo ya kamati ya nchibi bora hata isingeundwa. Naona imeleta report ya kuwasafisha PoliCCM kiaina!!!!

Mkuu ukiona hivyo ujue lawama zinapelekwa kwa lile libunduki...tear gas cannister launcher
Tutaambiwa lile libunduki lilikuwa libovu, au marehemu alilikamata akalivuta wakati askari akiwa ameweka kidole kwenye triger....


STUKA.....
 
Nashukuru mdau kwa report lkn mm naona kwamba kwanza ingekuwa kwa lugha yetu kwakua hili swala lilitendeka ndani ya Tanzania ili kuleta tija na uelewa kwa kila mtanzania. Hivi ndg zangu hasa wale waliodhuhudia tukio zima wataielewa hii report kweli??
Na swala la wao kusema kua"....hayakupangwa si tayari wameingilia uhuru wa mahakama??" kwani hiki ndicho walichotumwa?
 
hakuna jipya hapo yaleyale ya kulisafisha jeshi la police na kuwakandamiza chadema
 
Hivi na Pili Mtambalike si mwandishi wa habari?

Anawezaje kutia sahihi ripoti ya hovyo kama hii??


Kama hii nchi ingekuwa na watu majasiri, hakika hawa jamaa walitakiwa waturudishie gharama walizotumia kufanya huu uchunguzi feki...!!
 
Yaaaaani hiii nchi sijui sisi ni VIPOFU au tumelishwa dawa gani tusione kilichotokea.
Je nani anahusika kwenye mauaji au alifyatua mwenyewe

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Hii ni repot au taarifa jamani? Sikutegemea zaidi ya Haya. Je CDM wanampango gani dhidi ya mapendekezo Yao waliotoa juu ya polisi? I mean baada ya tariifa hii ya kamati nini msimamo wa CDM?
 
Mie bado sijaelewa hii report source yake ni wapi? MCT na Nchimbi yupi ndio mwenye report hii!!
 
Nchi hii vituko vitaisha lini jamani, labda Vasco akianguka na ndege.

Haki ya nani damu ya Mwangosi haitawaacha kuanzia amiri jeshi mkuu, waziri wa hao maafande, maafande wote na hiyo kamati ya waziri wa maafande.
 
Nguruvi3, I don't know what is more painful, kuangalia picha ya mabaki ya Daudi Mwangosi au kusoma hii report ya Nchimbi? Report inaonesha ni jinsi gani Jaji Ihema na wapambe wake wanavyoona watanzania ni mazuzu! Na inaelekea walichokifuata Iringa ni eneo la kukaa na kuandika mambo ambayo walishakubaliana.

Nimesoma kwa kurukaruka sehemu maana report imejaa upuuzi wa viwango vya juu sana. Inaharibu kabisa taswira ya majaji wetu pamoja na mwandishi wa habari Theophil. Yaani pamoja na vielelezo vyote (stilll and moving pictures) bado wanaleta habari za kutunga? Kama sio madharau kwa watanzania ni nini?

Kama huyu Jaji na wenzake walikuwa na nia njema wangeanza kwa kuuliza amri ya vyama vya siasa kutofanya mikutano wakati wa sensa ilihusu chama kimoja au vyote? Na amri hiyo ilihusu mikutano ya hadhara au mikutano ya ndani? Na CHADEMA walikuwa na mkutano wa hadhara au wa ndani?

Pili, maaskari waliokuwa kwenye eneo la tukio wote ni wa mahali hapo? kama jibu ni hapana, walikuja lini, na kwa sababu zipi?

Lakini kuna mambo kwenye hii report yanatia kichefuchefu. Jaji Ihema anaonekana ku-suggest kuwa Daudi Mwangosi aliuwawa na mtu/watu wengine mbali na polisi! Na anaenda mbele zaidi na kutoa maoni kuwa vikundi vya ulinzi kama Green guards, blue, guards and red guards viangaliwe upya. Moja kwa moja utaona kuwa anachosema jaji ni kwamba Daudi Mwangosi aliuliwa na moja ya hivyo vikundi?

Yote tisa, kumi Jaji anatoa mapendekezo ya kufuta shughuli za siasa nje ya bunge!

Kwa maoni yangu, hii tume ilikuwa na kazi maalum, kazi ya kuungaunga habari ili wapate nafasi ya kuchomekeza mapendekezo 'maalum' kama kuweka sheria ya kukandamiza vyama 'vya msimu' na kumpa msajili wa vyama vya siasa nguvu ya kuburuza vyama vinavyosumbuwa wakubwa.

Kwa zama tunazoishi sasa, ni kituko tena kituko kweli kweli kuandaa report chafu kama hiyo. Watanzania wengi wanajua mkanda mzima wa mauaji ya Daudi Mwangosi. Kamati ingejiwekea heshma kwa kuleta report inayoeleka na sio hizo ngonjera za mwaka 47. Yaani wameingiza mpaka points za Shibuda?!
 
Last edited by a moderator:
navyofahamu kamati iliundwa kuchunguza waliomuua sasa si waje na jibu moja kama wenzao.. waseme ni nani waliomuua. sio ripot ndeeefu ka hotuba ya mwisho wa mwez ukiipitia jibu hamna..
 
Kuna watu wana ubongo kama wa sisimizi halafu tumewapa jukumu kuwa viongozi wa nchi hii...UGenge mtupu(toa G kubwa weka s)..ipo siku tutaamka wamegeuka machizi na kuiweka nchi rehani!!
 
Hiki ni kinyesi na wala sio report. Inaleta hasira sana pale ukweli unapopindishwa ila kulinda maslahi fulani...
 
Nonsense! Imejaa siasa na almost kila kitu kilikua kinajulikana hakuna jipya! Wamepoteza hela tu hawa! Kwanza ripoti imejaa woga na kujipendekeza kwa serikali! Ukweli haina jipya nimepoteza muda wangu kuisoma! Wamejaza quotes za watu badala ya kutoa conclusive opinion basing on those quotes! Yaani utadhani ripoti ya mwanafunzi wa kidato cha nne. Hopeless kabisa
 
nimewatukana tusi kubwa kuliko yote hapa duniani na ahera,nchimbi na kamati yako wote!
 
Back
Top Bottom