...good observation Mkuu, it makes sense, ukizingatia ni Wa-pot wa marehemu...
...Kimsingi nadhani mauaji yamefanywa na yule kijana mwembamba aliyeelekeza bunduki ya kulipulia mabomu ya machozi akiwa takribani mita 0.5 kutoka kwenye tumbo la marehemu, ifahamike kuwa bomu la machozi linapaswa kupigwa kwenye umbali wa takriban mita
100 ili lisiwe na madhara na shurti lisielekezwe direct kwenye mwili wa binadamu...
...Kosa la huyo dogo,kama hakutumwa basi ni kichwa cha bangi, alilenga mwili na alikuwa karibu mno kinyume na utaratibu wa matumizi ya mabomu haya, na mbaya zaidi nadhani badala ya kutumia bomu la machozi lenye kizibo cha njano yeye alitumia bomu la mlipuko ambalo lina kizibo chekundu japo yote yana rangi ya jungle green,kosa kubwa...
...Bomu la mlipuko likipigwa na kugonga kitu kigumu(kama uti wa mgongo kwenye kesi hii) linalipuka na kutoa kishindo kizito, naamini ndicho kilichotokea na kuusambaratisha mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi...