Wadau tuipitie ripoti yote kuhusu kifo cha Daudi mwangosi iliyowasilishwa hapo jana na timu maalumu ya uchunguzi kwa Baraza la Habari Tanzana na kisha tuilinganishe na ripoti ya kamati ya Nchimbi. wana JF mwenye ripoti kamili ya Kamati ya Nchimbi anaombwa aiwakilishe tuijadili.
Sijapata muda wa kufanya analysis lakini report ya Nchimbi iko biased na lengo lake ni kuwasafisha polisi, serikali na ccm.
Nimesikia ITV akibabaika.
Report ya Wanahabari nayo inaubinafsi mbaya. Tangu kuuawa kwa Mwangosi wamekuwa wakionyesha kuwalaumu polisi kwa kuua mwandishi wa habari akiwa kazini.
Swali ni kwamba, kwa nini polisi wanauwa watu ovyo na kusingizia eti chanzo chadema. Chadema wasingefanya mkutano polisi wasingeua.
INALETA MAANA YOYOTE KWELI KWA POLISI KUUA MTU HATA KAMA NI MHALIFU AMBAYE HANA SILAHA, TAYARI YUKO CHINI YA UDHIBITI WAKE NA HANA UHATARISHI WOWOTE KWA USALAMA WA HAO WAKAMATAJI HATA KAMA SI MWANDISHI WA HABARI?
KWA NINI WASIMKAMATE MWANGOSI NA WOTE WANAOSHIRIKI MIKUTANO YA CHADEMA KISHA WAWAPELEKE MAHAKAMANI BADALA YA KUWAHUKUMU KIFO?
Report ya Nchimbi haijagusia mikusanyiko mingine iliyofanyika wakati huo hapa nchini ambayo si ya CHADEMA.
MAONI YA kamati yamelaumu CHADEMA ETI WAFUNDISHWE SIJUI N INI NINI hakuna hata kukemea wala kulaani mauaji ya raia wasiyo hatia katika nchi yao!.
NILIJUA TU NCHIMBI ALIPOKIMBILIA KUUNDA TUME NA KUMPELEKA YULE KIJANA POLISI MAHAKAMANI ILIKUWA NI MKAKATI WA KUTUMIA UJINGA WA WA TANZANIA KUUA SOO NA KUWALINDA WAHUSIKA WAKUU.
SERIKALI SHAME ON YOU!