Ndebile
JF-Expert Member
- Sep 14, 2011
- 7,237
- 9,871
Wanasubiri Habari Mbaya tu dhidi ya nchi yao!KundiB wanataka nini
Wanasubiri Habari Mbaya tu dhidi ya nchi yao!KundiB wanataka nini
Hata hizo habari za uchumi wa Kati no kwa mujibu wa takwimu za beberuSisi tuko uchumi wa kati, hayo matakwimu yao ya kibeberu wabaki nayo huko, sisi tuko vizuri wanatuobea wivu tu.
Au nasema uongo ndugu zangu
Wachukue kiti wakae maana watasubiri sanaWanasubiri Habari Mbaya tu dhidi ya nchi yao!
Nilivyoona comments zimekuwa chache hapa nikajua Uchumi umepanda....ambayo ni habari mbaya kwa kundi B!
Naona kama swali la kama Tanzania kufikia uchumi wa kati je tumefikia malengo ya dira ya maendeleo ya 2025 limepotezewa.
Kwan ripoti ya WHO au WORD BANK?Serikali ingeanza kutoa taarifa za maambukizi na vifo vitokanavyo na COVID 19 hii ingesaidia kujua hali halisi ya athari zitokanzo na janga hili.
Pia kutoa taarifa sahihi kuhusu hali halisi ya kiuchumi kuliko kuwaambia wananchi kuwa uchumi wetu umekua kwa kasi huku hali ya maisha ya mwananchi ikizidi kuporomoka.
Naona ipo haja ya serikali kupitia upya baadhi ya misimamo yake na kuibadili ili kisaidia wananchi kuepukana na janga la Corona na pia kuisaidia nchi iimarike kiuchumi.
Mkuu kama sijakosea lengo letu ni dola 3000 naomba mchango wakokiufupi amejibu technically ili kuliepuka ila nakumbuka Kikwete aliliongelea katika speech yake kwenye msiba wa Mzee Mkapa .
Makadirio ya pato la mtu mmoja mmoja kulinganisha na pato la taifa (Per capital income) kama kigezo kikubwa, tayari lilikuwa limefikia pazuri kwa nchi kupewa status ya "lower middle income nation" toka mzee Kikwete alipoliacha..
Hivyo, ili kupima kama tupo vizuri kufikia malengo ya 2025 chini ya utawala huu, haitoangaliwa "status" ya nchi tuliyopewa bali kiwango cha Per capital Income kilichoongezeka toka 2015 v/s Target yetu v/s Ukuaji wa tawala zilizopita.
Hii ndio njia sahihi ya kupima peformance ya sasa, zilizobaki ni kelele ambazo sidhani kama zitaendana na uhalisia
Mkuu kama sijakosea lengo letu ni dola 3000 naomba mchango wako
Hapa hautawaona wachangiaji wengi. Karanga nakuomba utoe neno hapa. Waalike na wengineSekta zilizochangia katika ukuaji wa uchumi.
1. Madini
2.Uwekezaji katika miundombinu
3. Huduma za fedha na mawasiliano.
4. Usafirishaji wa bidhaa.
Sekta hizi zinatumia mitaji mikubwa na idadi ya rasilimali watu katika sekta hizo ni ndogo kwasababu ya kutumia teknolojia ya mitambo zaidi.
Utalii umeshuka kwa mujibu wa ripoti. Kilimo kinachangia sehemu ndogo sana ukilinganisha na idadi ya watu walio katika sekta hiyo.
Mada fikirishi sana hii. Nangoja wadau waje tujadili.
Hivi uchumi ni kama nini labda
Kundi B umemaanisha upande wa pili?Nilivyoona comments zimekuwa chache hapa nikajua Uchumi umepanda....ambayo ni habari mbaya kwa kundi B!