Benki ya Dunia Yaipa Tanzania Trilioni 2.8

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Bodi ya Wakurugenzi ya Watendaji wa Benki ya Dunia kupitia ufadhili wa Sera yake ya Maendeleo (DPF) imeidhinishia Tanzania Dola za Marekani milioni 750 (Sh trilioni 1.9) kwa ajili ya kusaidia sekta binafsi.

Pia imeiidhinishia Tanzania Dola za Marekani milioni 385 (Sh bilioni 964.3) kwa ajili ya awamu ya pili ya Mradi wa Mandeleo ya jiji la Dar es Salaam (DMDP) ili kuboresha huduma za mijini, uwezo wa kitaasisi na kuhimili mabadiliko ya tabianchi Dar es Salaam ambazo kwa ujumla wake, ni sawa na Sh trilioni 2.8.

Taarifa ya benki hiyo kwa vyombo vya habari jana ilisema kuwa uidhinishaji huo ulifanyika juzi jijini Washington, Marekani.

Benki hiyo ilisema kuwa mpango wa pili wa ufadhili wa Sera ya Maendeleo ya kukuza uchumi wa Tanzania ambao msingi wake ni awamu ya kwanza ya DPF iliyoidhinishwa Desemba, mwaka jana utasaidia kuushawishi Mfuko wa Maendeleo ya Kimataifa (IDA) wa Benki ya Dunia katika kutatua changamoto za muda mrefu za kimuundo zilizokwamisha ukuaji wa uchumi na sekta binafsi, kutoa msukumo wa mageuzi yanayolenga kuboresha mazingira ya biashara, usimamizi wa mashirika ya serikali (SOEs), kuimarisha uwazi na kuimarisha uchumi.

"Tunaipongeza Serikali ya Tanzania kwa kusimamia mageuzi ya ukuaji jumuishi, sekta binafsi na ukuaji himilivu huku ikikabiliana na changamoto zinazosababishwa na matukio ya dunia yasiyotabirika. Tumedhamiria kuiunga mkono Tanzania katika kuimarisha mageuzi yatakayowezesha ufufuaji wa haraka na kuimarisha misingi ya ukuaji endelevu wa uchumi jumuishi na himilivu," alisema Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Victoria Kwakwa.

Benki hiyo ilibainisha kuwa ufadhili mpya na awamu ya pili ya DMDP utazingatia miundombinu ya kipaumbele ya hali ya hewa, miundombinu ya taka ngumu na kuimarisha taasisi za mijini. Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Nathan Belete alisema Tanzania bado iko katika. hatari ya kukabiliwa na mabadiliko ya tabianchi na ina uwezo mdogo wa kukabiliana na athari mbaya, hivyo awamu hiyo ya pili inalenga kuimarisha zaidi Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa benki hiyo, awamu ya kwanza ya DMDP ilisaidia usafiri kwa watu milioni 4.1 kutokana na ujenzi wà barabara zenye urefu wa kilomita 207.8 husu-sani katika maeneo ya watu wenye kipato cha chini. Pia ilisema imedhibiti maturiko kwa hekta 406 za ardhi ya mijini na kuboresha makazi yasiyo rasmi 152 na kuboresha hali ya maisha kwa maelfu ya wakazi ambao wanapata huduma bora na za msingi.​
 
Bado tunakopesheka, Kopa Mama, uzuri Waziri alishatuambia hakuna mtanzania atagongewa mlango kuombwa kulipa deni la taifa.
 
Back
Top Bottom