Vodacom yaongoza Tanzania kwa idadi ya Wateja

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1698256554295.png

Kwa mujibu wa Ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inayoangazia Takwimu za Mawasiliano Nchini, Mtandao wa Vodacom umeongoza kwa idadi ya Wateja ambapo hadi mwishoni mwa Septemba 2023 wamefikia 20,555,763

Ripoti imeonesha Mitandao yote kwa ujumla ilikuwa na ongezeko la 4.7% kutoka Wateja 64,088,651 Juni 2023 hadi 67,117,449 Septemba 2023. Mtandao wa Airtel umepanda kutoka Wateja 17,505,139 hadi 18,485,232 (28%), tiGO imefikisha Wateja 18,181,259 kutoka 17,484,387 (27%)

Halotel imepoteza Wateja 143,709 na kubaki na 8,266,320 (12%), TTCL imeongeza Wateja 61,959 kutoka 1,559,090 (2%) na Smile imezidi kupoteza Wateja kutoka 13,840 waliokuwepo Juni hadi 7,826 waliobaki kufikia Septemba 2023
 
Huo mtandao wa smile sijawahi kuona ofisi zake, wakala wake, namba ya simu ilivyo siijui hata kwenye contact list sina.
 
Back
Top Bottom