Sibonike
JF-Expert Member
- Dec 23, 2010
- 17,297
- 18,046
Wadada wengi wa Dsm (niliwaona nilipoendaga) hasa wale wenye miguu myembamba wanaogopa kuvaa nguo fupi.
Wengi wao hawajiamini, na wanaume eti nasikia na wenyewe wanataka wanawake wenye miguu minene, kwa ki Mongolia inaitwa "miguu ya bia". Hatari sana Sheikh.
Tena siku hizi nasikia wanaume wengi wa huko Dar wanapenda sana kulelewa.
Eti mali atafute mwanamke dume litumie tu, kule kwenye uzinduzi wa jengo la kwanza kuwa na lift wanasema "Fya deso"
Sasa jana nilikuwa naangalia michuano ya madola, kwa kweli wale wanawake wote waliobeba medali za riadha hakukuwa hata mmoja aliyekuwa na hiyo miguu ya chupa ya bia, wote mifupa yao ya miguuni haikuwa na nyama. (Kumbe miguu myembamba dili ehh)
Sasa wito kwa dada zangu wenye miguu yetu ileeeee, ya Wambulu, nawaombeni sana muanze kukimbia riadha, kwa kweli naona neema kubwa mbele yenu, ushindi utakapopatikana, ni utajiri umeingia malangoni mwako.
Hapo ndio utawaona mabitozi wakianza kukusarandia na nguo zao za kuazima
Mimi naamini Mungu hampi mtu vyote. Aliyepungukiwa hiki, kamjalia kile. Ni theory ya Compensation. Wadada wenye fito wana vitu vyao vya ziada na si kila mtu anataka mguu wa bia! Sio kila mtu anatumia alcohol!