Ridhiwani Kikwete: Chalinze tumepata maendeleo makubwa ndani ya muda mfupi wa uongozi wa Rais Samia

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete aishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa JMT Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kazi Nzuri inayofanywa na Serikali yetu ya Awamu ya Sita Chini ya Uongozi wa Mhe. Samia Suluhu Hassan ndani ya Kipindi hiki cha Miezi Sita katika Sekunde 25 za Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete aliposhiriki kwenye mapokezi ya Rais Samia akielekea Bagamoyo Kurekodi kipindi Cha Royal Tour.

View attachment 1923250

#KaziIendelee #AsanteRaisWetu #KaziUnaipigaKweli #Chalinze tunakushukuru
Aache uongo, kama ni ujenzi wa makao makuu ya wilaya Chalinze uliachwa ukiwa hatua za mwisho, barabara za zege ameziacha mtangulizi wake, eneo la ujenzi wa kituo cha kupozea umeme wa bwawa la Nyerere limeachwa na mtangulizi wake, ujenzi wa viwanda mbalimbali umeachwa na mtangulizi wake, vituo vya afya ameacha mtangulizi wake sasa ni kipi kipya zaidi ya hapo?

Reli ya mwendo kasi kaacha mtanguli wake pia yeye anaendeleza tu

Jambo baya ambalo mbunge na wengine hawajafanya vizuri ni kuacha ujenzi wa bandari ya nchi kavu na majengo ya shirika la nyumba hapo kwenye eneo kabla hujafika Msoga kwenye makazi ya rais mstaafu JK. Kijiji cha Msoga kinatakiwa kipandishwe hadhi kuwa mji mdogo na uwekezaji ufanyike hapo maana mazingira yanaruhusu
 
Eti Ridhiwani Kikwete nae ni Mbunge. Kuna muda huwa nawatafakari Watanzania na vilivyomo Ubongoni mwao na huwa sipati Majibu ya Kuniridhisha.
Utamfananisha na watu km Kibajaji, Gwajima, Kabud.!!!
 
Hahahahah baba baba aziza umepata maendeleo makubwa sio

Ridhiwani bana hahahaha sema nn simama pekee yako mkuu
 
Back
Top Bottom