BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 328
- 414
Kumekucha Chalinze!!
Ni Jumatano hii ya Oktoba 11, 2023 ambapo Jimbo la Chalinze chini ya Mbunge wake ambaye pia ni Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete litafanya Mkutano mkubwa wa Jimbo la Chalinze. Mkutano huo utatumika kueleza mambo makubwa yaliyofanyika katika Jimbo la Chalinze katika kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kutekeleza Ilani ya CCM ya 2020-2025, kusukuma maendeleo ya wananchi na kutatua kero zao katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, maji, kilimo, miundombinu, nishati n.k.
Mkutano huu Mkuu pia utatumika kueleza mikakati na mipango ya Jimbo kuwawezesha vijana, kupambana na changamoto ya ajira, kutangaza fursa za uwekezaji na maendeleo zinazopatikana Chalinze na mengine mengi. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dotto Biteko.
KaziInaendeleaChalinze.