Tusibabaishane huu utawala wa CCM na vikaragosi vyake umemaliza muda wa kuwepo madarakani, walichonacho hivi sasa ni kununua muda na kujaribu kujipanga upya,kwa kweli wasipewe muda huo wa kujipanga upya waondolewe tu,hakuna kutazama kipengele wa kikengele,muda na wakati wao umekwisha,wafunge funge na kukaa pembeni.
Watawala wanaokaribia nusu karne na hawajaweza kuiendeleza Nchi yao watawala hao hawafai ni lazima waondoke tu.Waondolewe kwa kura wakiiba waondolewe kwa nguvu
Muda wote huo Tanzania iliyojaa mito kila kona wameshindwa kumpatia mwananchi maji safi na ya uhakika, Tanzania iliyojaa uranium wameshindwa kuwapatia umeme wa uhakika tunabaki kusulubiana kwa mitambo ya watu wengine ambao wameshatuibia na kuyoyomea mbele sisi tumebaki nani aliruhusu nani alibania nani alipokea ! Yatatufikisha wapi ? Zaidi ya CCM kubadilisha na kutia rizavu mwengine.
Utawala wa CCM unatuharibia muda wetu wa kupiga hatua mbele ,hapa tulipokwama nao hatuendi mbele zaidi ya kuporomoka kwani hawana hata jipya moja watakalo kuja nalo zaidi ya ubabaishaji ,mawazo yao yamejifunga katika wizi ni vipi watafanikiwa kuanza kuiba tena ,ni vipi wavuke hewa hii inayowachafulia mirija yao.
Hivyo muda wa kujadiliana nao utafikiwa wakishaondoka kwenye madaraka ,huku wanakong'ang;ania ni kununua muda ili tusiwakurupushe katika mambo mengine ,mambo ambayo ni muhimu katika kujikwamua na shida zao.
Mambo ya kudai Katiba mpya ,mambo ya kudai tume mpya ya uchaguzi,mambo ya mahakama huru ,haya ndio mambo ambayo utawala wa CCM unajaribu kuyakwepa ni mambo ambayo yanahitaji kushughulikiwa kwa nguvu zetu zote na baadae ndio tutaweza kupambana na CCM katika ufisadi wao,lakini kuyarukia wanayoyafanya nyuma ya pazia ni kujihangaisha.
Vyama vya Upinzani havina budi kwanza kuyadai mambo makuu hayo na yakishakupatikana ndio tuwageukie wahujumu uchumi njia yao ya kutubabaisha itakuwa ndogo sana na pengine isiwepo kabsaa ,hapo ndipo patakapokuwa patamu.