Richmond + TANESCO: The complete deal

we nyani.. kwanini umekuja na figure ya 5' 2 inawezekana ni 6'4 so inakuwa shida kidogo kupata mtu wa kucheza naye.. robot iendayo kama upepo imefanya kazi vizuri zaidi na ninatumaini kuna mengine yako jikoni yanapikwa.. sijui kama meza itatosha..!
 
we nyani.. kwanini umekuja na figure ya 5' 2 inawezekana ni 6'4 so inakuwa shida kidogo kupata mtu wa kucheza naye.. robot iendayo kama upepo imefanya kazi vizuri zaidi na ninatumaini kuna mengine yako jikoni yanapikwa.. sijui kama meza itatosha..!

Yakhe mbona umekuwa defensive hivyo....?Lol
Kama ni 6'4 basi sidhani kama utapata shida. Maana hapa kijijini visura wengi huvaa stilleto...so hata kama yeye ni 5'4 akivaa za inchi 4 au 5 tayari anakuwa anakukaribia. Hutaki yule atakayekuzidi urefu....ila kama uko 5'2...loh! basi sijui hata nikusaidieje....
 
Hii ni hatari. Inakuwaje watumishi wa serikali kuvujisha siri za serikali. Kama kuna jambo namuomba Rais wetu afanye ni kurudisha nidhamu serikalini, vinginevyo kuna siri nyingine ambazo hazitakiwi kutoka. Wakati umefika kwa serikali kuwaonya watumishi wake wanaovujisha siri za serikali na siyo kutishia tu bali pia kuwachukulia hatua kali.

Serikali haiwezi kuendeshwa namna hii.

Asanteni.
 
Hii ni hatari. Inakuwaje watumishi wa serikali kuvujisha siri za serikali. Kama kuna jambo namuomba Rais wetu afanye ni kurudisha nidhamu serikalini, vinginevyo kuna siri nyingine ambazo hazitakiwi kutoka. Wakati umefika kwa serikali kuwaonya watumishi wake wanaovujisha siri za serikali na siyo kutishia tu bali pia kuwachukulia hatua kali.

Serikali haiwezi kuendeshwa namna hii.

Asanteni.

Kwani na kuvuja kwa huu mkataba kunahatarisha usalama wa nchi?.
 
Mbona imeshavuja mingi tu na karibu yote tunayo? Akianza leo atakuwa ameshachelewa. Mimi ningemshauri Kikwete atumie hizo safari zake nje ya nchi kutafuta nchi ya kukimbilia mambo yatakapomfika shingoni.

Yanayokuja na tuliyokwishapata so far yanatisha. Wana JF kaeni tu mkao wa kula. Mwaka huu kila kitu kitawekwa wazi. Watasaigni mikataba ufaransa tena usiku wa manane lakini JF itaiweka hapa mchana kweupeeeeeeeee
 
JK ameyakanyaga ya moto, machozi ya furaha aliyolia kule chimwaga atayajutia kwa kasi kama hii ya wananchi kumchoka vile mapema

Angalieni sahihi za mashahidi na jinsi walivyoandika majina yao kisanii kweli; hahahaaa mmeumia wote mliotia sahihi ktk mkataba huu, Hiyo % itawatokea puani kwa kula pesa sa wavuja jasho wa milima udzungwa, usambala na urukuru bila kusahau kijiwe cha maroni pale Mwz.

Tanzania kumekucha jamani amkeniiiiiiii''''
Ikifika saa nne asubuhi vigogo wote tutahakikisha wamekimbia familia zao

Invisible kazi nzuri keep it up
 
Mkombozi you are right on this!,
Mi nilisha sema kumbe hata alkaeda siyo vichaa! Inafikia mahali maudhi yakikuzidi yanakupelekea kuwaza ndivyo sivyo!

..ndo maana naipenda jf!

..watu wanaelimisha vizuri sana!

..btw,inatia hasira sana hata mtu unaanza kufikiria mabaya
 
Hii ni hatari. Inakuwaje watumishi wa serikali kuvujisha siri za serikali. Kama kuna jambo namuomba Rais wetu afanye ni kurudisha nidhamu serikalini, vinginevyo kuna siri nyingine ambazo hazitakiwi kutoka. Wakati umefika kwa serikali kuwaonya watumishi wake wanaovujisha siri za serikali na siyo kutishia tu bali pia kuwachukulia hatua kali.

Serikali haiwezi kuendeshwa namna hii.

Asanteni.

..cha kujiuliza ni kwanini imevuja?

..aliyevujisha ananufaika na nini?

..na kama hiyo serikali haiwezi endeshwa hivyo,iendeshwaje?

..ukipata majibu ya hayo!utaelewa!
 
Haya wandugu. Mkataba umetufikia. Una matatizo gani?
So far naona watu wanazunguka kichaka.
 
:) Kwanza pongezi nyingi kwa kuweka hadharani mkataba huu. Pili, ningependa kusisitiza umuhimu wa Freedom of Information Act, ambapo kama Marekani, hata minutes za mkutano huko White House huwekwa hadharani baada ya miaka kadhaa (hakuna cha usalama wa taifa au nini)Sometimes wanajaribu kuzamisha ili ifunguliwe after 50 years, lakini miaka ikipita, ukweli unajulikana! Kama Tanzania tungekuwa wazi hivyo mikataba kama hii ingekuwa inatayarishwa kwa makini. Tatu, zaidi ya watu waliosaini mkataba ni muhimu kujua nani aliandaa mkataba (which party - Richmond au serikali?) Na hizo sahihi mbona hivyo hata sehemu ya jina nashindwa kusoma! So the people behind this should be held accountable.
Kuna swali what is wrong with it... well, let me also finish reading all details then let us start a separate thread.
Again thank you Invisible!
 
Sorry, nilisahau another question: who is Mohamed Gire, can we google him or find other source of info? That's where the interesting stuff is, I think....
 
....too much kwa mtu wa kawaida kusoma na kuelewa kila kitu,ila kwa mtu mwenye akili huwezi kutumia zaidi ya dola milioni 120 kwa rent ya umeme wa miaka miwili,hiyo ni kanyaboya ya hali ya juu...why not build your own power plant kwa hiyo pesa ambayo itakupa power at least for 25 yrs...what i know the average of brand new gas powered plant (100MW) kutoka GM haizidi milioni 100...sasa hawa wametuletea rental & used one ...ni deal chafu tuu and very expensive!
 
People, you need to have this copy! I have nothing to add.

Enjoy the contents in the deal.

Invisible


Thanks for the tune.


invisible na wengine ( najua kuna wengi wamefanikisha huu muziki kuwepo) hongereni kuuweka hapa. kilichobaki tu-udigest huku tukisubiri vibao vingine vikali zaidi.

Shukrani kwa wote waliofanya iwezekane kwani hakuna siri kwenye mali ya wananchi.

mkataba kwa niaba ya serikali ulisainiwa nwa
Mr. Singi R. Madata
Assistant Commissioner
Debt Management Department
Ministry of Finance.

sheria inasemaje?

Jamani sheria inasemaje? Waliyo na sheria mnalijua hili? Unaweza kufungwa goli mtu hapahapa.

mie nina mikataba yote..namba yangu ni 0754 77 77 77,waambie hata usalama,
am tired with this bullshit kabisaaaaa,bora kuwa Mungiki tu

Mzee naona unahasira sana na mali ya walipa kodi, usijali tutafika tu.

Haya baada ya pongezi zote, tunaomba uchambuzi!!! kifungu kwa kifungu!!!
Tanzania sio ya mtu moja au watu fulani kwa nini wewe usianze na huo uchambuzi kifungu kwa kifungu na wengine waendelee. Au unafurahia ufedhuli wa mafisadi?

Hii ni hatari. Inakuwaje watumishi wa serikali kuvujisha siri za serikali. Kama kuna jambo namuomba Rais wetu afanye ni kurudisha nidhamu serikalini, vinginevyo kuna siri nyingine ambazo hazitakiwi kutoka. Wakati umefika kwa serikali kuwaonya watumishi wake wanaovujisha siri za serikali na siyo kutishia tu bali pia kuwachukulia hatua kali.

Serikali haiwezi kuendeshwa namna hii.

Asanteni.

Hatari gani hiyo? Serikali haina siri, mafisadi ndio wenye siri. Heshima ya serikali yoyote duniani ni kuwatumikia wananchi ambao wanaiwezesha kuwepo. Wananchi ambao ndio walipa kodi hawawezi kuburuzwa na mafisadi kwa siri, naona viongozi wetu na ngedere wanapenda kufanya vitu vya kawaida kuwa siri. Serikali hata siku moja isijaribu kuwa na siri, siri ni ya kwako moyoni ukishaitoa moyoni sio siri tena.
 
Kazi nzuri.Sasa next target ni TANGOLD NA MEREMETA Zikipatikana nyaraka zimwagwe humu maana jamaa mpaka sasa wanapayuka eti TANGOLD ni kampuni ya sirikali kwa asilimia 100 wakati nyaraka zinawapinga kwa wale ambao wanazo watushirikishe hapa ili tuzione LIVE!
 
Kwanza, kampuni iliyosajiliaw kwenye anuani iliyowekwa kwenye mkataba haihusiani na mambo ya nishati! Kabla ya kuingia kwenye mkataba huo kampuni ya RDC ilikuwa haijawahi kufanya ugavi wa umeme mahali popote!


pili,

maneno kuwa:

The supplier has the equipment, and the financial and technical capability to construct, install, commission, operate and maintain, such a a plant as required by TANESCO

yalikuwa hayana ukweli wowote. RDC haikuwa na uwezo, haikuwa na vifaa, na haikuwa na fedha za kuendesha mradi huo! Ni kwa sababu hiyo mabenki ya Marekani yalikataa kuwapa fedha kwani hawakuwa na Credit history ya kutosha kuomba mamilioni ya dola!

kwenye mkataba wenyewe, kipengele 15:14 ndicho kinaleta shida hasa baada ya kuruhusu mkataba "kuuzwa" kwa Dowans na hakuna anayesema uliuzwa kwa kiasi gani na kama kwa kufanya hivyo siyo kuvunja mkataba! Kipengele kinasema: (msisitizo wangu)

"This agreement is intended solely for the benefit of the Parties and nothing in this Agreement shall be CONSTRUED to create any duty to, standard of care with reference to, or any liability to, or confer any right of suit or action on any Person NOT a part to this Agreement other than to the extent it has been granted specific rights or benefits in the Agreement"

Kipengele hicho hakiachi nafasi kwa Dowans kununua mkataba huo kwani hakuna mahali popote ambapo aidha panaonesha kuwa RDC na Dowans ni kampuni zinazohusiana au mahali ambapo RDC ilikufa na nafasi yake kuchukuliwa na Dowans.

Kwa vile lugha ya sheria huwa inanisumbua, kipengele hiki kina maana gani:

15:16

No review and approval by TANESCO of any agreement, document, instrument or specification proposed by the Supplier (RDC) shall relieve the Supplier from any liabitity that it would otherise have had for its negligence in the preparation of such agreement, document, instrument or specification or failure to comply with the applicable Laws of Tanzania with respect thereto, or to satisfy the Supplier's obligations under this Agreemeent, nor shall TANESCO be liable to the Supplier or any other person by reason of its review, acquiescence or approval of an agreement, document, instrument or specification"

Kwa maneno mengine, endapo TANESCO baada ya kupitia nyaraka au hati mbalimbali baada ya kuingia mkataba huo na wakagundua kuwa RDC imefanya makosa ya aina fulani basi TANESCO isiishikilie RDC kwa makosa hayo. Na wao RDC wanaahidi vivyo hivyo. (apply that to selling the contract to Dowans!)

Sasa kipengele cha kushangaza zaidi ni masuala ya fedha. Wakati mwanzoni kabisa mkataba unasema kuwa:

The supplier has the equipment, and the financial and technical capability to construct, install, commission, operate and maintain, such a a plant as required by TANESCO

inakuwaje basi watake serikali ya Tanzania kuwadhamini ili wapate mkopo wa kufanyia biashara?

Haya nimewaanzia hapo...
 
Watu wanauliza huyu Gire ni nani? Hebu cheki hapa kwenye mtandao wa RDC: http://www.rdevco.com/principals.html

Mohamed A. Gire: Mr. Gire is a prominent businessman and an active private investor in emerging high-tech companies and offshore real estate and Infrastructure sectors.Mr. Gire brings a unique blend of talent and over 20 years of business acumen into growing strategic companies. Mr. Gire serves on numerous boards and commissions including a Houston's Mayoral Advisory Board for International Affairs and Development. Energy/Refinary companies that are interested in forming business alliance with us, are welcomed.

----
Nina swali, hivi huyu Julius Sarota kwenye huu mkataba ni nani huyu? Unajua nahangaika na mawazo, isijekuwa ndiyo yule jamaa aliyehawi kuchemsha vibaya vidato vya juu Mzumbe Sekondari miaka kadhaa iliyopita. Kama ndiye, kafikaje hapa?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom