Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

mwaka jana mahindi yaliosnda sana hadi kilo ya sembe ilikuwa 2000 tukalalamika maisha magumu leo imeshuka tunalalamika

na hii ipo popote duniani.

kwangu mimi sidhani kama ni record mpya kwani ukirudi miaka ya tisini hadi 2000 mwanzoni bado mahindi Mayalikuwa na bei ndogo chini ya hii

ninachokiona hapa kwa ni hasara ni kwa mkulima kutokana na kutumia gharama kubwa kuliko bei aliyi tegemea

nini kifanyike ni muda wa serikali kutoa ruzuku kwa wingi kupunguza hasara hii wakulima wanayopata
Mkuu unataka kutuambia 20,000tsh ya miaka ya tisini ni sawa na 20elf tsh ya sasa?

Mahindi kuuzwa 20,000 miaka ya tisini si tatizo kwasababu ni pesa nyingi kwa wakati huo.
Kwani mbolea iliuzwa 60,000 miaka hiyo?
Gharama za uzalishaji za miaka ya 90 na 2018 zinafanana?

Mimi naona mkulima alikuwa anapata faida kubwa wakati huo kuliko sasa.
 
Mie nadhani bei imeshuka ili tuweze kuishi vizuri kwa kula milo iliyokamili!!
 
Kuna rafiki yangu alinunua magunia 400 mwaka jana kwa bei kati ya 70000 na 75000. Plus kuyakusanya na kusafirisha kupeleka kwake home, gharama ya dawa, magunia tupu, labour charge ya kuchanganya dawa, hapo sijui itakuwa ngapi kwa kila gunia. Sasa hivi nikikutana naye hata sitaki kuanzisha hiyo story, labda aanze kubwabwaja mwenyewe. Mimi nimeacha kulima mahindi, navizia msimu kama huu tu nanunua gunia tatu, ova. tena simalizi kwa matumizi ya mwaka mzima kwa familia.
 
Mazao yote yanatakiwa kushuka bei zaidi ili watu waweze kuishi, Usiongee kwa sababu una Mshahara ambao hata kijijini kwenu huwatumii huo Mshashara ongea ukitafakari maisha ya Watanzania waliowengi. Mungu aendelee kusaidia Yashuke zaidi na zaidi, haitakiwi kufika sehemu mtu awaze anakula nini kula ni hitaji la Muhimu eboooo

Ukiwa mbumbumbu wa aina hii usitegemee lolote. Eti yashuke hata chini zaidi, hivi huyo mkulima anaeuza gunia sh elfu 20 mwakani atakuwa na pesa ya pembejeo ili akulimie zaidi? kuzalisha gunia moja ni Tsh 35,000, auze kwa elfu 20?
 
Maisha bora kwa kila mtanzania. Mm asbh hii nimepiga zangu ugalii safi na dagaa. Niko safi niko smart masuala ya kula chapati chai au supu mandazi akaaaaaa!! Ya nini sasa.
 
Hapa ndiyo huwa haya mambo siyaelew kabisa maana unga kiroba cha kilo 25 kwa dar es salaam kimepanda kutoka 17000 mpaka 18500
Sasa wew unakuja na hizi taarifa za kushuka kwa mahindi wakati wauza sembe wanadai yamepanda nje na matazamio yao
 
Nakumbuka debe ndo lilikuwa bei hiyo 20000~25000 sasa kama gunia kweli linauzwa 20000 mmh hatari imbombo gafugwe
 
Ukiwa mbumbumbu wa aina hii usitegemee lolote. Eti yashuke hata chini zaidi, hivi huyo mkulima anaeuza gunia sh elfu 20 mwakani atakuwa na pesa ya pembejeo ili akulimie zaidi? kuzalisha gunia moja ni Tsh 35,000, auze kwa elfu 20?
Bei ya mahindi inatakiwa kushuka gharama za kuzalisha Mahindi kwenye Ekari 1 ni hii:-

1. Kulima 20,000
2. Mbegu 30,000
3. Mbolea (2) 120,000
4. Dawa kuulia wadudu 20,000

Total 190,000

Hakuna gharama nyingine tena Kwa Mkulima kupalia na kuvuna ni kazi yake kama wewe unavyokwenda Ofisini.

Kipato Kwa Ekari 1 ni gunia 30 mnataka nini?
 
Bei ya mahindi inatakiwa kushuka gharama za kuzalisha Mahindi kwenye Ekari 1 ni hii:-

1. Kulima 20,000
2. Mbegu 30,000
3. Mbolea (2) 120,000
4. Dawa kuulia wadudu 20,000

Total 190,000

Hakuna gharama nyingine tena Kwa Mkulima kupalia na kuvuna ni kazi yake kama wewe unavyokwenda Ofisini.

Kipato Kwa Ekari 1 ni gunia 30 mnataka nini?


Wewe kweli ni standard VII ukilima heka mia utapalilia mwenyewe? Hiyoo garama 20,000 kulima ni ya wapi.


Ukishamaliza kusoma ukaingia mtaani ndo utaelewa tunachojadili.
 
Bei ya mahindi inatakiwa kushuka gharama za kuzalisha Mahindi kwenye Ekari 1 ni hii:-

1. Kulima 20,000
2. Mbegu 30,000
3. Mbolea (2) 120,000
4. Dawa kuulia wadudu 20,000

Total 190,000

Hakuna gharama nyingine tena Kwa Mkulima kupalia na kuvuna ni kazi yake kama wewe unavyokwenda Ofisini.

Kipato Kwa Ekari 1 ni gunia 30 mnataka nini?

Uko sahihi kabisa
 
Hii ni record mpya kuwahi kushuhudiwa Tanzania. Kwa mara ya kwanza gunia mahindi linauzwa kati ya Shilingi 20,000 hadi 27,000 kutegemea na eneo husika. Tanga gunia ni Tsh 25,000/- Mbeya 25,000/-, Sumbawanga na Rukwa 20,000.

Wachambuzi wa mambo wanasema Tanzania ilikataa kuuzia Kenya mahindi mwaka jana, Kenya wakaamua kuchukua mahindi nje ya bara la Africa hivyo soko soko la Africa Mashariki likajikuta limejaa mahindi kutoka bara la America ya kusini. Baada ya wakulima kulia sana Tanzania ikafungua mipaka lakini ikawa too late.

Wakulima wanalia, walioweka mahindi Godown wanalia kwa hasara ambayo haijawahi kushuhudiwa. Kila mtu anaisoma namba kwa wakati wake

Niliona mahali gunia la mahindi linauzwa mpaka sh.15,000...lakini wachumi watueleze kama hili ni jambo jema au baya...
 
Ukitaka kujua kwamba bichwa lako umejaza minyoo kichwani jiulize hili swali; "Je, ni asilimia ngapi kati ya hiyo asilimia 80 wanalima mahindi?", si kila mahali panafaa kulima mahindi, ndio maana wengine hulima ndizi, kahawa na mchele, na wote tunategemeana kama taifa kiujumla. Tena kuna sehemu zingine ni kame na hazitoi mazao yabkutosha, mfano ni mikoa ya Dodoma na Singida, kwahiyo tunategemeana kama taifa, Dodoma wakilima zabibu haimaanishi kwamba hawataki mahindi, bali ni mazingira ndio yanafavour zaidi zabibu, na ni lazima wauze zabibu na wanunue mahindi, tunategemeana kama taifa. Leo serikali ikikusanya kodi itokanayo na vileo vya zabibu kisha ikatumia hizo pesa kutoa ruzuku za pembejeo kwa mfumo wa vocha it means nao wamehusika kwenye uzalishaji wa hayo mahindi, na wote tunahaki yabkuyafaidi, kila mtu na kila kitu kiko intertwined, tuache ubinafsi wa kiboya huo. Masuala ya cement nk. kupungua bei hutegemea na demand na supply, viwanda vikizalisha cement nyingi kuliko demand kama mnavyofanya nyinyi wakulima wa mahindi bei itashuka tu, maana kwa sasa TZ hai-export cement kwenda nje, sana sana ndio tunazidi kuagiza cement toka pakistan lakini bado bei iko juu, means demand ni kubwa, sasa imagine tungeanza kuagiza mahindi toka marekani, bei si itakuwa 5,000/= kwa gunia? Kilimo ni biashara, hivyo tengenezeni feasibility study ya kujua zao gani litakuwa na demand kiasi gani wapi na lini, pia muangalie sera ya serikali juu ya zao husika, ndio mtu unalima, sio mnalima tu blindly wakati mnajua kabisa before hand sera ya serikali juu yabku-export chakula, maana kama Kenya bei ni kubwa kwanini msiende mkanunue ardhi Kenya mlime? Serikali ya TZ imehakikisha ardhi za wazawa zinalindwa ndio maana mazao ni mengi, bali Kenya kumiliki ardhi kwa mkulima ni ndoto, wengi ni vibarua kwenye mashamba ya akina uhuru Kenyatta, huku mtu unajikatia lishamba unalima tu, acheni kelele na fanyeni kilimo kinacholipa kama mahindi hayalipi!
Toka mwanzo nilikuwa na mashaka sana na uwezo wako wa kufikiri Sijaona sababu ya matusi hapo mkuu, toa hoja!

Ni kofia tu ya kijani mnapewa au sikuiz wanatoa full suit kama gharama za kumnadi "malaika" wenu??

Wenyewe (serikali) wameshakiri kwa matendo kwamba walikosea na wakafungua mipaka ila it was too late, sioni sababu ya ww kupingana na waliokutuma.
 
Back
Top Bottom