Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

Ukitaka kujua kwamba bichwa lako umejaza minyoo kichwani jiulize hili swali; "Je, ni asilimia ngapi kati ya hiyo asilimia 80 wanalima mahindi?", si kila mahali panafaa kulima mahindi, ndio maana wengine hulima ndizi, kahawa na mchele, na wote tunategemeana kama taifa kiujumla. Tena kuna sehemu zingine ni kame na hazitoi mazao yabkutosha, mfano ni mikoa ya Dodoma na Singida, kwahiyo tunategemeana kama taifa, Dodoma wakilima zabibu haimaanishi kwamba hawataki mahindi, bali ni mazingira ndio yanafavour zaidi zabibu, na ni lazima wauze zabibu na wanunue mahindi, tunategemeana kama taifa. Leo serikali ikikusanya kodi itokanayo na vileo vya zabibu kisha ikatumia hizo pesa kutoa ruzuku za pembejeo kwa mfumo wa vocha it means nao wamehusika kwenye uzalishaji wa hayo mahindi, na wote tunahaki yabkuyafaidi, kila mtu na kila kitu kiko intertwined, tuache ubinafsi wa kiboya huo. Masuala ya cement nk. kupungua bei hutegemea na demand na supply, viwanda vikizalisha cement nyingi kuliko demand kama mnavyofanya nyinyi wakulima wa mahindi bei itashuka tu, maana kwa sasa TZ hai-export cement kwenda nje, sana sana ndio tunazidi kuagiza cement toka pakistan lakini bado bei iko juu, means demand ni kubwa, sasa imagine tungeanza kuagiza mahindi toka marekani, bei si itakuwa 5,000/= kwa gunia? Kilimo ni biashara, hivyo tengenezeni feasibility study ya kujua zao gani litakuwa na demand kiasi gani wapi na lini, pia muangalie sera ya serikali juu ya zao husika, ndio mtu unalima, sio mnalima tu blindly wakati mnajua kabisa before hand sera ya serikali juu yabku-export chakula, maana kama Kenya bei ni kubwa kwanini msiende mkanunue ardhi Kenya mlime? Serikali ya TZ imehakikisha ardhi za wazawa zinalindwa ndio maana mazao ni mengi, bali Kenya kumiliki ardhi kwa mkulima ni ndoto, wengi ni vibarua kwenye mashamba ya akina uhuru Kenyatta, huku mtu unajikatia lishamba unalima tu, acheni kelele na fanyeni kilimo kinacholipa kama mahindi hayalipi!
Mkuu,
Unaongea kama vile wewe si mtanzania ama umetoka dunia ya kwanza.

Hongera sana mkuu
 
Mazao yote yanatakiwa kushuka bei zaidi ili watu waweze kuishi, Usiongee kwa sababu una Mshahara ambao hata kijijini kwenu huwatumii huo Mshashara ongea ukitafakari maisha ya Watanzania waliowengi. Mungu aendelee kusaidia Yashuke zaidi na zaidi, haitakiwi kufika sehemu mtu awaze anakula nini kula ni hitaji la Muhimu eboooo
Ninatabiri upungufu mkubwa wa chakula ndani ya miaka miwili ijayo kama hili halitatafutiwa ufumbuzi.

Idadi ya ekari zilizolimwa mwaka Jana zimeshuka mwaka huu, na kama hili litaendelea watu waliojiajiri kwenye kilimo cha kibiashara ambao ndio wazalishaji wakubwa watakimbia kitu kitakachopelekea low production ambayo haiendani na demand.

Watanzania tuna akili sana ila tatizo letu hatuzitumii. Mungu atusaidie sana ili tusiendelee kujidhania kwamba tumesimama.
 
Bei ilipokuwa juu mlilalamika sasahivi imeshuka ili kuwapunguzia ugumu wa maisha watu wa kipato cha chini tena mnalalamika! Watanzania mnataka nini? Kwani bei ya gunia la mahindi kuuzwa sh. 20,000/= ndio mara ya kwanza katika historia ya Tanzania toka ipate uhuru?
Hivi unajua kazi za ghala za chakula za serikali ama?
 
Kwani unaposikia serikali inatoa vocha za ruzuku huwa unaelewa nini? Au serikali inapojenga miundombinu za barabara kwenda vijiji vyabwakulima ili kurahisisha usafiri wa mazao huwa uanelewa nini? Au serikali inapoweka vituo vya hali ya hewa ili kwashauri wakulima muda muafaka wa kulima huwa unaelewa nini? Au serikali inapotekeleza ujenzi wa mabwawa ya umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji wa mazao huwa unaelewa nini? Au serikali inapoagiza matrekta na kuyatoa kama mikopo kwa vikundi vya wakulima kwa bei nafuu huwa unaelewa nini?, au serikali inapoendesha vituo vya utafiti wa mbegu bora zinazovumilia ukama na kutoa mazao mengi kwa muda mfupi huwa unaelewa nini? Nk.nk.nk.nk.; au huwa unafikiri hivyo vitu havina gharama? Serikali huchangia moja kwa moja katika uzalishaji wa hayo mahindi, hivi wamehusika na mahindi kuwa mengi na bei kushuka, toa hayo makonokono kichwani and think straight! Tena kwa hasira naenda kununua kila 100 za unga naweka ndani, just incase mahindi yakapanda bei, shenzi kabisa!
Nitajie mbegu mojawapo ya mahindi tuliyozalisha ambayo unasema imechagiza mavuno ili tupate pa kuanzia
 
Mnakomaaaa kujadili bei za mazao ya vyakula. Yaaan mazao ya biashara hamyajui?!?
 
Kama chakuka kinapatikana na masikini wanakula wanashiba acha bei iendelee kushuka. Baadhi ya Binadamu wakipewa lift hawana shukrani wataanza kuponda hata hiyo lift waliyopewa.
 
Hii ni record mpya kuwahi kushuhudiwa Tanzania. Kwa mara ya kwanza gunia mahindi linauzwa kati ya Shilingi 20,000 hadi 27,000 kutegemea na eneo husika. Tanga gunia ni Tsh 25,000/- Mbeya 25,000/-, Sumbawanga na Rukwa 20,000.

Wachambuzi wa mambo wanasema Tanzania ilikataa kuuzia Kenya mahindi mwaka jana, Kenya wakaamua kuchukua mahindi nje ya bara la Africa hivyo soko soko la Africa Mashariki likajikuta limejaa mahindi kutoka bara la America ya kusini. Baada ya wakulima kulia sana Tanzania ikafungua mipaka lakini ikawa too late.

Wakulima wanalia, walioweka mahindi Godown wanalia kwa hasara ambayo haijawahi kushuhudiwa. Kila mtu anaisoma namba kwa wakati wake

Tujiongeze,tusizoee kuuza raw materials kwa viwanda vya wenzetu,tuuze products,pia hakuta kua na njaa kamwe
 
Sijawahi ona mkulima akiuza mahindi nje.
Wakulima wa Uganda na Zambia hawauzi mahindi yao nje. Ni nyie wafanya biashara.
Upo sahihi mkuu,wasipokuwepo hao wafanyabiashara mazao yatabaki mashambani. iwe korosho,kahawa,pamba,chai,miwa,shairi,mpunga dengu,ufuta n.k.
 
Hii ni record mpya kuwahi kushuhudiwa Tanzania. Kwa mara ya kwanza gunia mahindi linauzwa kati ya Shilingi 20,000 hadi 27,000 kutegemea na eneo husika. Tanga gunia ni Tsh 25,000/- Mbeya 25,000/-, Sumbawanga na Rukwa 20,000.

Wachambuzi wa mambo wanasema Tanzania ilikataa kuuzia Kenya mahindi mwaka jana, Kenya wakaamua kuchukua mahindi nje ya bara la Africa hivyo soko soko la Africa Mashariki likajikuta limejaa mahindi kutoka bara la America ya kusini. Baada ya wakulima kulia sana Tanzania ikafungua mipaka lakini ikawa too late.

Wakulima wanalia, walioweka mahindi Godown wanalia kwa hasara ambayo haijawahi kushuhudiwa. Kila mtu anaisoma namba kwa wakati wake
[emoji3] [emoji3] [emoji3] hapo hakuna katibu wa chama wala mwenyekiti wa kijiji wote ni mwendo wakuisoma namba tu.
 
Hii ni record mpya kuwahi kushuhudiwa Tanzania. Kwa mara ya kwanza gunia mahindi linauzwa kati ya Shilingi 20,000 hadi 27,000 kutegemea na eneo husika. Tanga gunia ni Tsh 25,000/- Mbeya 25,000/-, Sumbawanga na Rukwa 20,000.

Wachambuzi wa mambo wanasema Tanzania ilikataa kuuzia Kenya mahindi mwaka jana, Kenya wakaamua kuchukua mahindi nje ya bara la Africa hivyo soko soko la Africa Mashariki likajikuta limejaa mahindi kutoka bara la America ya kusini. Baada ya wakulima kulia sana Tanzania ikafungua mipaka lakini ikawa too late.

Wakulima wanalia, walioweka mahindi Godown wanalia kwa hasara ambayo haijawahi kushuhudiwa. Kila mtu anaisoma namba kwa wakati wake
Mungu wangu....hii ni hatari kwa uchumi wa wakulima....badae mheshimiwa atasema hao nao ni wapiga dili meee
 
Basi hawa wafanyabiashara wa reja reja wanapiga sana pesa aisee, maana juzi nimenunua kilo ya mahindi 1800/= tzs Zanzibar.
 
Bei ya unga ikipanda mnafungua thread kulalamik
Hiyo ni commerce ya form II,mambo ya demand na supply
 
Back
Top Bottom