Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

Bei ya mahindi inatakiwa kushuka gharama za kuzalisha Mahindi kwenye Ekari 1 ni hii:-

1. Kulima 20,000
2. Mbegu 30,000
3. Mbolea (2) 120,000
4. Dawa kuulia wadudu 20,000

Total 190,000

Hakuna gharama nyingine tena Kwa Mkulima kupalia na kuvuna ni kazi yake kama wewe unavyokwenda Ofisini.

Kipato Kwa Ekari 1 ni gunia 30 mnataka nini?
Kosa kubwa unafanya kumwambia mkulima asihesabie nguvu yake anapoenda shambani.Nauli ya kwenda shambani mbona hujasema?
 
Na yangeuzwa yote halafu waanze tena kulia kwa kuilaumu serikali kwa kuruhusu mahindi kuuzwa nje.Mbongo kubadilisha agenda ni dk moja.

Tatizo uelewa wako mdogo. Gharama za kuzalisha kilo moja ya mahindi inakaribia sh 500 . Sasa unapozuia mkulima asiuze kwenye soko linaweza kumpa faida unadhani kesho ataweza vp kulima. Huwezi zuia bei ya kilo ya unga isipande kwa kumuonea mkulima. Athari yake watu haswa wakulima wakubwa watashindwa au wataacha kulima matokeo yake ugali utakosekana.
 
Naomba mahindi kwa bei hiyo mimi nipo Dar , kama naweza kupewa kwa bei hiyo hapa Dar niunganishe ninunue gunia zangu nne za kula nyumbani.
 
No yangu 0716282670
Nataka gunia nne nipo Dar na ntakuja kuchukua mwenyewe.
 
Kwa staili hii ya kuwatesa na kuwakwamisha wakulima, Hata hivyo viwanda sidhani kama vitafanikiwa.
Viwanda bila malighafi havifanyi kazi.
M/mungu ibariki serikali iwaangalie wakulima kwa jicho la tatu.
 
Kama chakuka kinapatikana na masikini wanakula wanashiba acha bei iendelee kushuka. Baadhi ya Binadamu wakipewa lift hawana shukrani wataanza kuponda hata hiyo lift waliyopewa.
Mkuu tatizo ni kuwa gharama za kulima hazijashuka matokeo yake hii hasara anabeba mkulima, mwisho ataacha kulima.
 
Halafu wapuuzi hawa wanaleta propaganda ya kukuza kilimo ..........pumbavu kabisa watu wamekeza mamilioni kwenye hii biashara ........ masilahi ya wakulima yanahitaji kuzingatiwa sio kuwa biased upande mmoja tu
 
Ila nakumbuka mkulu wetu alishawahi kusema mkulima asipangiwe bei ya kuuza,huyo anayekupangia mwambie na yeye akalime yake
 
Mkuu tatizo ni kuwa gharama za kulima hazijashuka matokeo yake hii hasara anabeba mkulima, mwisho ataacha kulima.
Ila nakumbuka mkulu wetu alishawahi kusema mkulima asipangiwe bei ya kuuza,huyo anayekupangia mwambie na yeye akalime yake
Mhh,mkuu,mkulima hana ujanja huo, hii ni misemo tuuu. Kusini mwa Tz mwaka huu kuna mahindi ya kufa mtu! Ya mwaka jana mengi bado yapo maghalani,gunia ni Tsh 15,000/= na hakuna mnunuzi. Je, kwa halihiyo,hiyo bei atapangia wapi na nani ampangie?
 
Back
Top Bottom