Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

Cha msingi ukisha lima anzisha kiwanda cha kuchakata mahindi kuwa unga uuze unga siyo mshindi.Lakini ni watz wangapi wenye uwezo huo wa mtaji usiopungua mil 80?
Utamuuzia nani unga endapo kila mtu kujijini ana mahindi yake? Wanunuzi wa unga wa mahindi hawafiki 5% ya walaji wote!
 
Hii ni record mpya kuwahi kushuhudiwa Tanzania. Kwa mara ya kwanza gunia mahindi linauzwa kati ya Shilingi 20,000 hadi 27,000 kutegemea na eneo husika. Tanga gunia ni Tsh 25,000/- Mbeya 25,000/-, Sumbawanga na Rukwa 20,000.

Wachambuzi wa mambo wanasema Tanzania ilikataa kuuzia Kenya mahindi mwaka jana, Kenya wakaamua kuchukua mahindi nje ya bara la Africa hivyo soko soko la Africa Mashariki likajikuta limejaa mahindi kutoka bara la America ya kusini. Baada ya wakulima kulia sana Tanzania ikafungua mipaka lakini ikawa too late.

Wakulima wanalia, walioweka mahindi Godown wanalia kwa hasara ambayo haijawahi kushuhudiwa. Kila mtu anaisoma namba kwa wakati wake

deleted
 
Mkuu, hapa tunaongea uhalisia ww unaleta theories, labda nikuulize swali
Ni ndugu zako wangapi vijijini wana uwezo wa kusafirisha mahindi kwenda Arusha Mwanza na Dar kwa gharama zao?
Kama wanategemea madalali na madalali hawanunui wafanyeje?

Binafsi nimefika Songea, wakulima hali ni mbaya mno, gunia la mahindi ni 20,000 na hata hiyo bei hayanunuliwi.

Ukumbuke kaya nyingi masikini vijijini hawana store za kuhifadhia, hawana pesa za kununua dawa za kuzuia wadudu waharibifu hivyo mahindi yanaharibika pia hawana fedha kwaajili ya msimu huu kilimo hivyo wengine hawakuweza kulima tena, hii ndio ajira inayotegemewa na 70-80% ya watanzania ambao ni wakulima vijijini
hapo sijaongelea mbaazi...mnajua imefika 150tsh/kg
Sijaweka wavuvi na (wana hasira hawa sasaiv wananyanyaswa sana na policcm)
Sijawagusa waliofungiwa maduka na TRA.. Mtaji 450,000, EFD mashine 650,000 si uonezi huu?
Sijaweka magazeti yanayofungiwa kwa ubabe

Serikali haitoi ajita fine, tuachieni basi hata hizi tuloanzisha kwa jasho letu Wanapoteza ajira ngapi? Haya ndio maendeleo?

NAKUPENDA TANZANIA.

Hapa kazi tu!!


Magufuli anaua uchumi
 
Hizi taarifa hazina uhalisia! Kwenye mitandao kila mtu anasema lake. Juzi nimenunua dona 25kg Dar kwa 19,000. Sasa unataka kuniambia gunia la kilo 100 liuzwe bei sawa na kilo 25?? Unamdanganya nani?
Mzee, changanyika kidogovhuku kwetu uswekeni ujionee pesa inavyoheshimika sasa hivi, acha kung'ang'ania tu mjini ukaishi kwa kukariri.
 
Ila huoni kwamba masikini sasa wana uhakika wa kupata walau milo miwili kwa siku?

Bei ya unga ingepanda pia ungelaumu serikali kwamba mnakufa njaa, bei ya mahindi na unga inashuka pia mnalia, mnataka nini nyinyi kasuku?
mahindi yameshuka bei unajua maharage bei ngapi kilo? ,mchele nao?? sukari na mafuta yakula.
nimeshangaa kuambiwa nyanya moja mia4 yaani bei ya nyanya ni sawa na pakiti ya chumvi
 
Songea pia ni 20,000 kwa gunia,
Serikari iangalie namna ya kuwasaidia wakulima.
Kama kuna uwezekano wa kufungua masoko ya nje basi ifanye hivyo, ili hata sisi tunaozurula mjini tuvutike kwenda kulima.
Nchii hii ina ardhi kubwa yenye rutuba na maji tele na hii ni fulsa nzuri ya kuinua kipato cha wananchi.
Hivi kweli hapa Tz, kuna wakulima wengi wanaotumia mahindi kama zao la biashara?
Ninavyojua, mazao ya biashara yapo, lakini siyo mahindi.
 
Hiyo sio hoja.Kununua kwako bei imanishi mahindi yana bei.Umenunua wapi?.Labda wamekufunika ndugu. Njoo uku uchukue dona 25 kwa sh 10,000/=
Sawasawa hii ndio bei yake.
 
mahindi yameshuka bei unajua maharage bei ngapi kilo? ,mchele nao?? sukari na mafuta yakula.
nimeshangaa kuambiwa nyanya moja mia4 yaani bei ya nyanya ni sawa na pakiti ya chumvi
Sasa kwanini mnalima mahindi badala ya nyanya? Demand vs supply ndio hupanga bei, sio serikali
 
Tunatoa maoni, tunabadilishana mawazo mwisho tunatukanana. Kuna walioko Mbeya, kuna walioko Sumbawanga, kuna walioko Tarime, Kahama, DSM na kila mtu ana mtazamo wake kulingana na mahali alipo. Kuna mlaji na mkulima. Mlanguzi yuko pembeni.

Kwa maoni yangu na mimi ni kuwa kilimo chetu hakina tija. Tunatumia gharama kubwa kuzalisha kidogo. Biashara ya sasa hivi zalisha kwa wingi ili uuze kwa bei ndogo kuwezesha ushindani na kupata faida. Kuzalisha zaidi ni kwa kutumia mbinu bora. Kiasi hicho hicho cha pembejeo kinachotumika kwa eka moja kinaweza kuzalisha magunia 25 ya mahindi lakini mkulima wetu amejitahidi sana sana anapata gunia 15. Silaumu sana maana hata mkulima mwenyewe hajui atumie mbolea aina gani, kinachotumika ni mazoea tu nina maanisha hakuna utafiti wa kutosha wa udongo kuwezesha kujua ni aina gani ya mbolea inahitajika mahali gani. Sampling inakuwa katika eneo kubwa, mfano unaambiwa utumie DAP kiwilaya wakati ilitakiwa aina za mbolea angalau kikata, ndio maana unakuta watu wawili ktk wilaya moja wametumia pembejeo aina moja lakini kila mmoja ana uzalishaji wake. Swala la ruzuku kwenye pembejeo pia lisibaki nyuma.

Kwa upande mwingine serikali ilitakiwa istabilize bei ya mahindi nchi nzima kwa kuwa mnunuzi mkubwa hata kama inadai serikali haifanyi biashara (ina taasisi zake zinaweza kufanya hivyo km SGR). Kwa mfano inunue mahindi kule Ruvuma, Iringa, Rukwa kwa bei ya Sh. 500 kwa kilo ina maana gunia litakuwa sh.50,000, iprocess na kuuza unga mfano kwa sh. 600/= hapa mlanguzi ataondoka. Pia ziada ya mahindi itakayokuwepo inaweza kuuzwa nje ya nchi kwani majirani zetu (Kenya, Somalia na Sudan pamoja na nchi zilizo vitani/mashirika ya kimataifa ya misaada) wanayahitaji.
Kwa hapa nchini bei ikipanda wana ya release mlaji anafaidika bei ikishuka wanayanunua toka kwa mkulima naye anafaidika. Lengo ni kumtoa nje mlanguzi maana ndiye anayeharibu masoko.
Mkuu,kila kitu ni mpango na uwe shirikishi na kwa weledi siyo hasira na ubaguzi.
Mwl. Nyerere aliliona hilo mapema ndo maana alianzisha NMC
. Sasa nikuulize,aliyeuwa na kuuza NMC kwa kina Bakhresa aliwaza nini,na alishirikisha nani?
Pili, kwa nini serikali huita mnunuzi wa mazao ni mlanguzi?ia Mf. Mwaka juzi,NFRA ilinunua mahindi 50,000 kwa gunia la kilo mmoja,huku wafanyabiashara wanaoitwa walanguzi wakinunua hadi 100,000/= kwa gunia. Je,hapo mlanguzi ni nani?
Tatu, kwa mawazo ya kawaida,mkulima wa mahindi pale Namanyere Rukwa,anaweza kujenga kiwanda cha kuprocess unga na kushindana soko la unga na Bakhresa? huku ukijua pia Rukwa yote karibia wotee wana mahindi ndani?
Nne, Je,kuna uwezeshaji wowote wakulima hawa wamefanyiwa kuhusu usindikaji,namna ya kupenetrate soko nk ?
Mkuu, najua tuko pamoja na serikali kuona mkulima anapata stahiki yake kwa jasho na nguvu anazopoteza,lakini tuwe na sera bayana kufikia malengo.
 
wakati serikali inafanya jitihada wananchi wake wale washibe watu wamekaa kuwakashifu hivi ni mkulima gani alikuwa na uwezo wa kuuza mahindi Kenya kama sio watu wa kati serikali hii iko makini kwa mambo muhimu kama njaa bila hivyo sasa hivi tungesikia vilio kila sehemu kuna uhaba wa chakula
 
Mahindi ni zao la chakula halihusiani na biashara japo wakulima wetu hulitumia kama la biashara..

Kikubwa cha kwanza Serikali ilicholenga ni kutaka kuuza product nikimaanisha Kuuza Unga na sio Mahindi ili kikuza ukuaji Wa viwanda na kuwaongezea Pesa wakulima wetu..

2. Kupunza mfumko Wa bei, ikimaanisha tubakishe kingi ndani kitakachotutosheleza kwanza ndipo tuanze kuuza nje, sio imetokea dharura tunaanza kuomba misaada ya chakula nje..
 
Kiukweli kwa nchi ambayo Kilimo ni uti wa mgongo hii ni aibu ya kuvunja record. Tutambue mkulima anategemea kuuza mazao yake ili hela hiyo aingize shambani lakini ndo hivyo tena.

Nchi ya viwanda very shame na hakika Tanzania naona tunazama kwenye umaskini wa kupindukia. Huwezi kusema unajali wanyonge wakati hata masoko ya mazao huna na bado unazuia mazao kuuzwa nje.


Hivi Tanzania tulilogwa na nani mbona uwezo wa viongozi wetu kufikilia ipo chini sana.

Natamani kumwambia mamangu aache kulima hadi pale mazao ya Kilimo yapande bei, mwaka uliopita gunia za mahindi 40 zinaonzea ndani hakuna soko, alafu usimame jukwaani useme inchi ya viwanda na 85% ya watanzania ni wakulima na kuonyesha kuwa Kilimo ndo kimeajiri watu wengi zaidi lakini bado hutambui maumivu yao. Sijui hii serikali inazungumzia wanyonge wa nchi gani maana sio Tanzania
 
Mkuu kama hujui chochote ni bora ukae kimya.. Mimi mwenyewe nimeamua kuyauza mahindi yangu niliyonunua sh 50,000/ kwa @ gunia. Now nimekubali kuyauza 30,000@ gunia ili pesa niifanyie mambo mengine.. Nakuhakikishia km unahela njoo nikupeleke upate mahindi hata tani 200 kwa 27,000 hadi 25,000 kwa gunia huku UNYAMWANGA RUKWA
Mkuu 25000 ni nyingi sana aende Songea gunia 20000 tena kwa mkopo, Cash 18000/bag
 
Back
Top Bottom