Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

Mimi bado siwaelewi watanzania kwa kweli.

Anayepanga bei ya mazao kama mahindi ni nani?

Wewe mkulima unalalamika gunia 20,000 wakati mfanyabiashara anakuja kuuza gunia hilo hilo elfu 70 mpaka laki.

Huoni anayekunyonya ni mfanyabiashara na siyo serikali?

Kwanini vyama vya wakulima wasione hili na kupanga bei rasmi kulingana na wingi au uchache wa mazao badala ya kulalamikia serikali?

Maana bei ikishuka mnalalamika, bei ikipanda watumiaji wanalalamika. Mnatakiwa mshinikize vyama vya wakulima kupanga bei itakayo walinda wakulima.

Kama bei ya mafuta yanavyopangwa, bei ya mazao pia ipangwe.

Serikali ikipanga bei bado mtalalamika. WATANZANIA TUACHE KUTEGEMEA KILA KITU KUFANYWA NA SERIKALI. TUJIKOMBOE dahh...
Kaaazii kweli kweli.
 
Huko sio kushuka kwa bei bali ni kuporomoka, kilio kwa mkulima furaha kwa mlaji
 
Mimi bado siwaelewi watanzania kwa kweli.

Anayepanga bei ya mazao kama mahindi ni nani?

Wewe mkulima unalalamika gunia 20,000 wakati mfanyabiashara anakuja kuuza gunia hilo hilo elfu 70 mpaka laki.

Huoni anayekunyonya ni mfanyabiashara na siyo serikali?

Kwanini vyama vya wakulima wasione hili na kupanga bei rasmi kulingana na wingi au uchache wa mazao badala ya kulalamikia serikali?

Maana bei ikishuka mnalalamika, bei ikipanda watumiaji wanalalamika. Mnatakiwa mshinikize vyama vya wakulima kupanga bei itakayo walinda wakulima.

Kama bei ya mafuta yanavyopangwa, bei ya mazao pia ipangwe.

Serikali ikipanga bei bado mtalalamika. WATANZANIA TUACHE KUTEGEMEA KILA KITU KUFANYWA NA SERIKALI. TUJIKOMBOE dahh...
Kaaazii kweli kweli.
Mkulima hana uwezo wa kugharamia garama za usafirishaji wa mizigo yake kulifata hilo soko la elf70, ndio tatizo linapokuja hapo
 
wewe mtumiaji hutaki chakula kiwe bei chini ? kama mahindi yamepungua bei hongera rais
 
Mkulima hana uwezo wa kugharamia garama za usafirishaji wa mizigo yake kulifata hilo soko la elf70, ndio tatizo linapokuja hapo
Haijalishi, Mfanyabiashara anakodi lorry analopakia magunia mengi, kwa misingi hiyo gunia moja hali cost zaidi ya 20,000 kusafirisha, hapo inaacha kuanzia elfu 30,000 mpaka 60,000 wakati mkulima kapewa elfu 20.

Hakuna kisingizio, wafanyabiashara ndio wanao wanyonya wakulima.

Ni swali simple tu, kwanini mfanyabiashara anatajirika na siyo mkulima? Jibu nikuwa tatizo siyo soko la kuuzia mazao, tatizo ni wafanyabiashara wana waumiza wakulima.

Vyama vya wakulima wanatakiwa kuliona, kulielewe na kulifanyia kazi hili swala.
 
Uhakika wa kupata lishe kwa kumuumiza mkulima? Yani mkulima masikini wa mwisho kijijini auze mahindi kwa hasara ili wewe upate milo mitatu?
halafu 80% ya tz population ni wakulima unamaanisha hao wote (80%) wazidi kukandamizwa kwenye umasikini ili ww ununue unga 200tsh?
Kilimo ni biashara kama zilivyo biashara nyingine na kama ishu ni kumnufaisha mlaji bila kujali maslahi ya mzalishaji basi na mfuko wa cement uuzwe 5000, soda100, mafuta Lt 500tsh au ikiwezekana watuwekee bure kwenye magari,
Kama hayo hayawezekani why mkulima?? yeye pia anatumia rasilimali muda,mbolea,nguvu, madawa, usafiri nk kwenye uzalishaji.

Huu ni ubinafsi wa hali ya juu sana!!
Mkuu akili ni nyingi napendekeza uwe waziri wa uchumi
 
Haijalishi, Mfanyabiashara anakodi lorry analopakia magunia mengi, kwa misingi hiyo gunia moja hali cost zaidi ya 20,000 kusafirisha, hapo inaacha kuanzia elfu 30,000 mpaka 60,000 wakati mkulima kapewa elfu 20.

Hakuna kisingizio, wafanyabiashara ndio wanao wanyonya wakulima.

Ni swali simple tu, kwanini mfanyabiashara anatajirika na siyo mkulima? Jibu nikuwa tatizo siyo soko la kuuzia mazao, tatizo ni wafanyabiashara wana waumiza wakulima.

Vyama vya wakulima wanatakiwa kuliona, kulielewe na kulifanyia kazi hili swala.
Labda kama hvyo vyama vikiwepo vinaweza kusaidia ndio itakua mkombozi hapo sawa

Lakini mkulima kukwepa kunyonywa na mfanya biashara ni ngumu sana tena sana maana kiuhalisia soko la elfu 70 hawezi kulifikia...
 
Siyo swala la kama hivyo vyama vikiwepo, chama kipo. Ishu ni kwamba kinafanya nini?
Huko ndo sehemu yakuelekeza malalamiko ya bei ya mazao.

Na wala haihitaji mkulima kufata soko la elfu 70. Ni swala la kushare profit tu.
 
Mnaofurahia kuporomoka kushuka kwa bei kumbukeni serikali ilifanya kampeni kubwa na ilitumia fedha nyingi kuhamasisha kilimo cha mahindi nchini. Msifikiri kama hali hii ikiendelea kwa muda wa miaka mitano wakulima wataendelea kuzalisha mahindi kwa wingi, na hapo ndo tutarudi kuanza kuagiza mahindi nje. Ni kweli kwa hizi nchi kwa kiasi kikubwa mfumko wa bei unasababishwa na kupanda kwa bei ya vyakula hasa nafaka, lakini njia nzuri siyo kuzuia watu kusafirisha nje kwani baadae matokeo yake siyo mazuri. Ili kupata uhakika wa chakula nchini serikali inatakiwa kuwapa wakulima pembejeo kwa wakati na kuwatafutia masoko pale inapo bidi mfano mwaka huu.
 
Yani maamuzi ya mjinga mmoja yanasababisha hasara kwa wakulima na kuongezea watu umaskini
 
Siyo swala la kama hivyo vyama vikiwepo, chama kipo. Ishu ni kwamba kinafanya nini?
Huko ndo sehemu yakuelekeza malalamiko ya bei ya mazao.

Na wala haihitaji mkulima kufata soko la elfu 70. Ni swala la kushare profit tu.
Basi lawama zote ziende kwa hivyo vyama
 
Ila huoni kwamba masikini sasa wana uhakika wa kupata walau milo miwili kwa siku?

Bei ya unga ingepanda pia ungelaumu serikali kwamba mnakufa njaa, bei ya mahindi na unga inashuka pia mnalia, mnataka nini nyinyi kasuku?
Usisahau akina Zitto walipiga kele na takwimu kibao za ghala la hifadhi ya chakula kuwa na mzigo mdogo.
Wakapandisha bei ya unga wa mahindi (sembe na dona) ikafika 2000/-.
 
Ila huoni kwamba masikini sasa wana uhakika wa kupata walau milo miwili kwa siku?

Bei ya unga ingepanda pia ungelaumu serikali kwamba mnakufa njaa, bei ya mahindi na unga inashuka pia mnalia, mnataka nini nyinyi kasuku?
Kuna kipindi unga ulifika 2000 kwa kilo watu wakalia sana
 
Chakufanya sasa ni kuyachoma moto yote ili kutengeneza scarcity we all know wanaolima yakutosha kujilisha kwa msimu mzima ni wachache kuliko wanao nunua, otherwise tuzidi kuzisoma namba tu...

Yaani hata hatua moja haujalima...unakuja na hoja za kipuuzi kama hizi. Badala ya kufikiria tunatokaje hapa ili wakulima wasipate hasara unakuja na hoja za kishetani.
 
Ni kusoma namba kwa zamu, mwaka juzi ilikua kwa walaji ambapo nakumbuka kiloba cha unga kg 25 kilikua kinachezea elfu 40-50. Sasa ni zamu ya wakulima. I hope kipindi hicho wakulima walipiga hela sana
 
Back
Top Bottom