Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

Rekodi mpya: Gunia la mahindi lafika 20,000/-

Walio chukua mikopo nanwanaopanga kichukua mikopo subirini kwanza
Si kwa uchumi huu usiotabirika.
WAULIZE WAZANZIBARI NA KIWANDA CHAO CHA SUKARI AMBAPO KUFUMBA NA KUFUMBUA SUKARI IMEPIGWA MARUFUKU KUJA BARA
WAUZE HAPO HAPO ZENJI
KWISHAAAAAAAAAAAAA
SASA WE CHUKUA MKOPO UWEKEZE KWENYE KILIMO NYUKI HUKO TABORA ILI UUZE MBEYA NA DSM THEN UMEKAA SEBULENI UNAONA NEWS JUST IN

WAZIRI KAPIGA MARUDUKU UUZAJI WA ASARI KUANZIA LEO HADI KILA MWANANCHI WA TABORA ATAKAPO PATA ASATI KABATINI MWAKE NDO KIBALI CHA KUTOA ASARI NJE YA TABORA KITOLEWE"

KWISHAAAAAAAA
 
Hii ni aibu ya taifa maana tumelima jmn ata kuuza tunafail ay bhna nchi ya viwanda mungu anawaona lkn.
 
Kwa fedheha kama hii basi tusitarajie wawekezaji wa kilimo biashara.
Cha msingi ukisha lima anzisha kiwanda cha kuchakata mahindi kuwa unga uuze unga siyo mshindi.Lakini ni watz wangapi wenye uwezo huo wa mtaji usiopungua mil 80?
 
Hii ni record mpya kuwahi kushuhudiwa Tanzania. Kwa mara ya kwanza gunia mahindi linauzwa kati ya Shilingi 20,000 hadi 27,000 kutegemea na eneo husika. Tanga gunia ni Tsh 25,000/- Mbeya 25,000/-, Sumbawanga na Rukwa 20,000.

Wachambuzi wa mambo wanasema Tanzania ilikataa kuuzia Kenya mahindi mwaka jana, Kenya wakaamua kuchukua mahindi nje ya bara la Africa hivyo soko soko la Africa Mashariki likajikuta limejaa mahindi kutoka bara la America ya kusini. Baada ya wakulima kulia sana Tanzania ikafungua mipaka lakini ikawa too late.

Wakulima wanalia, walioweka mahindi Godown wanalia kwa hasara ambayo haijawahi kushuhudiwa. Kila mtu anaisoma namba kwa wakati wake
lifike hata 5,000 watu wale ugali na mboga mboga za majani waachane na chips zege.😀😀😀😀😀😀😀😀
 
tupaze sauti zetu huku nako wakulima tunaumia bei ya gunia ni chini sana wafungue mipaka tuuze nje.

bei ya mbolea ni kubwa kupitiliza tufanyaje kilimo kwa hali hii.
Serikali ingeuza mbolea hata 3500/=per mfuko hata tungeuza mshindi 2500/= kwa gunia faida tungepata
 
Kumbe mahindi ni kilimo cha biashara!! Sio chakula!!
Biashara ni korosho;pamba Kahawa, hii mtama na mahindi ni vyakula vikipanda bei watu inafaa waandamane
[emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji85]
 
Hii ni record mpya kuwahi kushuhudiwa Tanzania. Kwa mara ya kwanza gunia mahindi linauzwa kati ya Shilingi 20,000 hadi 27,000 kutegemea na eneo husika. Tanga gunia ni Tsh 25,000/- Mbeya 25,000/-, Sumbawanga na Rukwa 20,000.

Wachambuzi wa mambo wanasema Tanzania ilikataa kuuzia Kenya mahindi mwaka jana, Kenya wakaamua kuchukua mahindi nje ya bara la Africa hivyo soko soko la Africa Mashariki likajikuta limejaa mahindi kutoka bara la America ya kusini. Baada ya wakulima kulia sana Tanzania ikafungua mipaka lakini ikawa too late.

Wakulima wanalia, walioweka mahindi Godown wanalia kwa hasara ambayo haijawahi kushuhudiwa. Kila mtu anaisoma namba kwa wakati wake
MBOZI sh18000,lakini bado tunalalamika bei kubwa.
 
Ila huoni kwamba masikini sasa wana uhakika wa kupata walau milo miwili kwa siku?

Bei ya unga ingepanda pia ungelaumu serikali kwamba mnakufa njaa, bei ya mahindi na unga inashuka pia mnalia, mnataka nini nyinyi kasuku?
maana yake kuna hatar ya watu kutolima msimu unaofuata na kuleta njaa ya hatar!beiitakuwa mara elfu
 
Uhakika wa kupata lishe kwa kumuumiza mkulima? Yani mkulima masikini wa mwisho kijijini auze mahindi kwa hasara ili wewe upate milo mitatu?
halafu 80% ya tz population ni wakulima unamaanisha hao wote (80%) wazidi kukandamizwa kwenye umasikini ili ww ununue unga 200tsh?
Kilimo ni biashara kama zilivyo biashara nyingine na kama ishu ni kumnufaisha mlaji bila kujali maslahi ya mzalishaji basi na mfuko wa cement uuzwe 5000, soda100, mafuta Lt 500tsh au ikiwezekana watuwekee bure kwenye magari,
Kama hayo hayawezekani why mkulima?? yeye pia anatumia rasilimali muda,mbolea,nguvu, madawa, usafiri nk kwenye uzalishaji.


Huu ni ubinafsi wa hali ya juu sana!!
best reply !
 
Tunatoa maoni, tunabadilishana mawazo mwisho tunatukanana. Kuna walioko Mbeya, kuna walioko Sumbawanga, kuna walioko Tarime, Kahama, DSM na kila mtu ana mtazamo wake kulingana na mahali alipo. Kuna mlaji na mkulima. Mlanguzi yuko pembeni.

Kwa maoni yangu na mimi ni kuwa kilimo chetu hakina tija. Tunatumia gharama kubwa kuzalisha kidogo. Biashara ya sasa hivi zalisha kwa wingi ili uuze kwa bei ndogo kuwezesha ushindani na kupata faida. Kuzalisha zaidi ni kwa kutumia mbinu bora. Kiasi hicho hicho cha pembejeo kinachotumika kwa eka moja kinaweza kuzalisha magunia 25 ya mahindi lakini mkulima wetu amejitahidi sana sana anapata gunia 15. Silaumu sana maana hata mkulima mwenyewe hajui atumie mbolea aina gani, kinachotumika ni mazoea tu nina maanisha hakuna utafiti wa kutosha wa udongo kuwezesha kujua ni aina gani ya mbolea inahitajika mahali gani. Sampling inakuwa katika eneo kubwa, mfano unaambiwa utumie DAP kiwilaya wakati ilitakiwa aina za mbolea angalau kikata, ndio maana unakuta watu wawili ktk wilaya moja wametumia pembejeo aina moja lakini kila mmoja ana uzalishaji wake. Swala la ruzuku kwenye pembejeo pia lisibaki nyuma.

Kwa upande mwingine serikali ilitakiwa istabilize bei ya mahindi nchi nzima kwa kuwa mnunuzi mkubwa hata kama inadai serikali haifanyi biashara (ina taasisi zake zinaweza kufanya hivyo km SGR). Kwa mfano inunue mahindi kule Ruvuma, Iringa, Rukwa kwa bei ya Sh. 500 kwa kilo ina maana gunia litakuwa sh.50,000, iprocess na kuuza unga mfano kwa sh. 600/= hapa mlanguzi ataondoka. Pia ziada ya mahindi itakayokuwepo inaweza kuuzwa nje ya nchi kwani majirani zetu (Kenya, Somalia na Sudan pamoja na nchi zilizo vitani/mashirika ya kimataifa ya misaada) wanayahitaji.
Kwa hapa nchini bei ikipanda wana ya release mlaji anafaidika bei ikishuka wanayanunua toka kwa mkulima naye anafaidika. Lengo ni kumtoa nje mlanguzi maana ndiye anayeharibu masoko.
 
Halafu UREA mfuko mmoja 60,000/= .Maskini Tz
Wajua UREA mfuko wa Kg 50 uzalishaji wake ni Kg ngapi? Wajua bei elekezi ya mbolea ni kiasi gani? Endelea na maaandamano Mkuuu mi nauliza tu wakati ukiendelea kuandama uwe unamuuliza mtunisha misur mwenzio kwenye haya maaandamano. Pia kama kweli mahindi ni bei hiyo huko kwingneko HIYO NI FURSA ITUMIENI maaana kwingneko Eg. Kahama, Dar nk bei ni 70,000/= tuache kulalamika.
 
Wajua UREA mfuko wa Kg 50 uzalishaji wake ni Kg ngapi? Wajua bei elekezi ya mbolea ni kiasi gani? Endelea na maaandamano Mkuuu mi nauliza tu wakati ukiendelea kuandama uwe unamuuliza mtunisha misur mwenzio kwenye haya maaandamano. Pia kama kweli mahindi ni bei hiyo huko kwingneko HIYO NI FURSA ITUMIENI maaana kwingneko Eg. Kahama, Dar nk bei ni 70,000/= tuache kulalamika.
Unga wa ndele ni kitu kibaya sana kwa ustawi wa akili.
 
Yanini kuosha Vyombo vya jirani wakati vyombo vyako bado vichafu??

Hapa nchini uhitaji wa mahindi bado mkubwa na ndo maana hata beo ya unga ipo juu.

Market forces za demand and supply zinaweza thibitisha hili sasa kwanini tusisupply kwenye soko la ndan kwanza vyema.

Mbona hutaji bei za dar,Arusha,Mwanza na mikoa mingine
Mkuu, hapa tunaongea uhalisia ww unaleta theories, labda nikuulize swali
Ni ndugu zako wangapi vijijini wana uwezo wa kusafirisha mahindi kwenda Arusha Mwanza na Dar kwa gharama zao?
Kama wanategemea madalali na madalali hawanunui wafanyeje?

Binafsi nimefika Songea, wakulima hali ni mbaya mno, gunia la mahindi ni 20,000 na hata hiyo bei hayanunuliwi.

Ukumbuke kaya nyingi masikini vijijini hawana store za kuhifadhia, hawana pesa za kununua dawa za kuzuia wadudu waharibifu hivyo mahindi yanaharibika pia hawana fedha kwaajili ya msimu huu kilimo hivyo wengine hawakuweza kulima tena, hii ndio ajira inayotegemewa na 70-80% ya watanzania ambao ni wakulima vijijini
hapo sijaongelea mbaazi...mnajua imefika 150tsh/kg
Sijaweka wavuvi na (wana hasira hawa sasaiv wananyanyaswa sana na policcm)
Sijawagusa waliofungiwa maduka na TRA.. Mtaji 450,000, EFD mashine 650,000 si uonezi huu?
Sijaweka magazeti yanayofungiwa kwa ubabe

Serikali haitoi ajita fine, tuachieni basi hata hizi tuloanzisha kwa jasho letu Wanapoteza ajira ngapi? Haya ndio maendeleo?

NAKUPENDA TANZANIA.

Hapa kazi tu!!
 
Back
Top Bottom